Ramadhan Special Thread
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب حق الجار والوصية بِهِ

039-Mlango Wa Haki Ya Jirani na Kumtendea Wema



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:

وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَبِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَالْجَارِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَالْجَارِ الْجُنُبِ وَالصَّاحِبِ بِالْجَنبِ وَابْنِ السَّبِيلِ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۗ ﴿٣٦﴾

Na mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni ihsaan wazazi wawili na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini na jirani mwenye ujamaa na jirani asiye na ujamaa na rafiki wa karibu, na msafiri aliyeishiwa masurufu, na wale iliyowamiliki mikono yenu ya kulia. [An-Nisaa: 36]





Hadiyth – 1

وعن ابن عمر وعائشة رضي الله عنهما ، قالا : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( مَا زَالَ جِبْريلُ يُوصِيني بِالجَارِ حَتَّى ظَنَنْتُ أنَّهُ سَيُورِّثُهُ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Kutoka kwa ibn 'Umar na 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhummaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuwacha Jibriyl kuniusia kuhusu jirani mpaka nikadhania kuwa atamrithisha (mali)." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 2

وعن أَبي ذر رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( يَا أَبَا ذَرٍّ ، إِذَا طَبَخْتَ مَرَقَةً ، فَأكثِرْ مَاءهَا ، وَتَعَاهَدْ جيرَانَكَ )) رواه مسلم .

وفي رواية لَهُ عن أَبي ذررضي الله عنه، قَالَ : إنّ خليلي صلى الله عليه وسلم أوْصَاني : (( إِذَا طَبَخْتَ مَرَقَاً فَأكْثِرْ مَاءها ، ثُمَّ انْظُرْ أهْلَ بَيْتٍ مِنْ جِيرَانِكَ ، فَأصِبْهُمْ مِنْهَا بِمعرُوفٍ )) .

Na imepokewa na Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ee Abu Dharr! Unapopika supu, ongeza maji, kisha utizame kama jirani yako (anahitajia)." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na katika riwaayah ya Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Hakika rafiki yangu, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameniusia: "Unapotengeneza supu ongeza maji, kisha tizama kama baadhi ya jirani zako (wanahitajia), kisha wapelekee sehemu yake kwa wema."





Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( واللهِ لاَ يُؤْمِنُ ، وَاللهِ لاَ يُؤْمِنُ ، وَاللهِ لاَ يُؤْمِنُ ! )) قِيلَ : مَنْ يَا رَسُول الله ؟ قَالَ : (( الَّذِي لاَ يَأمَنُ جَارُهُ بَوَائِقَهُ ! )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية لمسلم : (( لا يَدْخُلُ الجَنَّةَ مَنْ لاَ يَأمَنُ جَارُهُ بَوَائِقَهُ )) .

Imepokewa kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Wa-Allaahi haamini! Wa-Allaahi haamini!Akaulizwa: "Nani Ee Rasuli wa Allaah?" Akasema: "Ambaye jirani yake hasalimiki na shari zake." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na katika riwaayah ya Muslim: "Hataingia Peponi ambaye jirani yake hasalimiki na shari zake."





Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( يَا نِسَاء المُسْلِمَاتِ ، لاَ تَحْقِرَنَّ جَارةٌ لِجَارَتِهَا وَلَوْ فِرْسِنَ شَاة )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Na imepokewa kutoka kwake Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Enyi wanawake wa Kiislamu! Jirani asimdharau jirani yake hata kama amepika kwato za mbuzi." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( لاَ يَمْنَعْ جَارٌ جَارَهُ أنْ يَغْرِزَ خَشَبَةً في جِدَارِهِ )) ، ثُمَّ يقُولُ أَبُو هريرة : مَا لِي أرَاكُمْ عَنْهَا مُعْرِضينَ ! وَاللهِ لأرْمِيَنَّ بِهَا بَيْنَ أكْتَافِكُمْ . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Na imepokewa kutoka kwake Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Jirani asimkataze jirani kukita mbao katika ukuta wake." Abuu Hurayrah alikuwa akisema: "Mbona nawaona mumeipa mgongo Sunnah hii! Wa-Allaahi nitawaambia (hata mkichukia)." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 6

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بالله وَاليَومِ الآخرِ ، فَلاَ يُؤْذِ جَارَهُ ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ باللهِ وَاليَومِ الآخِرِ ، فَلْيُكْرِمْ ضَيْفَهُ ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ باللهِ وَاليَومِ الآخِرِ ، فَلْيَقُلْ خَيْراً أَوْ لِيَسْكُتْ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Na imepokewa kutoka kwake Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho asimuudhi jirani yake. Na mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho amkirimu mgeni wake. Na mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho aseme maneno ya kheri (mazuri) au anyamaze." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud na At-Tirmidhiy]





Hadiyth – 7

وعن أَبي شُرَيْح الخُزَاعيِّ رضي الله عنه: أن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( مَنْ كَانَ يُؤمِنُ بِاللهِ وَاليَومِ الآخِرِ ، فَلْيُحْسِنْ إِلَى جَارِهِ ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ باللهِ وَاليَومِ الآخِرِ ، فَلْيُكْرِمْ ضَيْفَهُ ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللهِ وَاليَومِ الآخِرِ ، فَلْيَقُلْ خَيْراً أَوْ لِيَسْكُتْ )) رواه مسلم بهذا اللفظ ، وروى البخاري بعضه .

Imepokewa kutoka kwa Abu Shuraykh Al-Khuzaa'iyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuwa anamuamini Allaah na Siku ya Mwisho, amfanyie hisani jirani yake. Na mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho amkirimu mgeni wake. Na mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho asema maneno ya kheri (mazuri) au anyamaze." [Muslim kwa lafdhi hii, na Al-Bukhaariy baadhi yake]





Hadiyth – 8

وعن عائشة رضي الله عنها ، قَالَت : قُلْتُ : يَا رَسُول الله ، إنَّ لِي جارَيْنِ ، فإلى أيِّهِمَا أُهْدِي ؟ قَالَ : (( إِلَى أقْرَبِهِمَا مِنكِ بَاباً )) رواه البخاري .

Kutoka kwa 'Aa'ishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) Amesema: Nilisema: "Ee Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), hakika mimi nina majirani wawili, ni yupi kati yao nimpelekee zawadi?" Akasema: "Ambaye mlango wake uko karibu zaidi nawe." [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 9

وعن عبدِ الله بن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( خَيْرُ الأَصْحَابِ عِنْدَ الله تَعَالَى خَيْرُهُمْ لِصَاحِبِهِ ، وَخَيرُ الجِيرَانِ عِنْدَ الله تَعَالَى خَيْرُهُمْ لِجَارِهِ )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwake 'Abdillaahi bin 'Amr bin Al-'Aasw (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mbora kabisa wa sahibu mbele ya Allaah Aliyetukuka ni aliye bora kwa sahibu yake. Na mbora mno wa jirani mbele ya Allaah Aliyetukuka ni aliye bora kwa jirani yake." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب بر الوالدين وصلة الأرحام

040-Mlango Wa Kuwafanyia Wema Wazazi na Kuunga Kizazi (Ujamaa)



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:

وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَبِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَالْجَارِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَالْجَارِ الْجُنُبِ وَالصَّاحِبِ بِالْجَنبِ وَابْنِ السَّبِيلِ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۗ ﴿٣٦﴾

Na mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni ihsaan wazazi wawili na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini na jirani mwenye ujamaa na jirani asiye na ujamaa na rafiki wa karibu, na msafiri aliyeishiwa masurufu, na wale iliyowamiliki mikono yenu ya kulia. [An-Nisaa: 36]

وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحَامَ ۚ ﴿١﴾

Na mcheni Allaah Ambaye Kwake mnaombana (haki zenu kwa kuunga) undugu. [An-Nisaa:1]

وَالَّذِينَ يَصِلُونَ مَا أَمَرَ اللَّـهُ بِهِ أَن يُوصَلَ ﴿٢١﴾

Na ambao wanaunga yale Aliyoamrisha Allaah kuungwa. [Ar-Ra'd: 21]

وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ حُسْنًا ۖ ﴿٨﴾

Na Tumemuusia insani kuwafanyia wema wazazi wake wawili. [Al-'Ankabuwt: 8]

وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۚ إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا ﴿٢٣﴾ وَاخْفِضْ لَهُمَا جَنَاحَ الذُّلِّ مِنَ الرَّحْمَةِ وَقُل رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا ﴿٢٤﴾

Na Rabb wako Amehukumu kwamba: Msiabudu isipokuwa Yeye Pekee na (Ameamrisha) kuwafanyia ihsaan wazazi wawili. Kama mmoja wao akifikia uzee naye yuko pamoja nawe, au wote wawili basi usiwaambie, Uff! Na wala usiwakemee; na waambie maneno ya heshima.Na wainamishie bawa la unyenyekevu kwa huruma, na useme: Rabb wangu! Warehemu kama walivyonilea udogoni. [Al-Israa: 23-24]

وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ وَهْنًا عَلَىٰ وَهْنٍ وَفِصَالُهُ فِي عَامَيْنِ أَنِ اشْكُرْ لِي وَلِوَالِدَيْكَ ﴿١٤﴾

Na Tumemuusia insani kwa wazazi wake wawili. Mama yake ameibeba mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumwachisha ziwa katika miaka mwili; ya kwamba, unishukuru Mimi, na wazazi wako; [Luqmaan: 14]







Hadiyth – 1

وعن أَبي عبد الرحمان عبد الله بن مسعود رضي الله عنه، قَالَ : سألت النبي صلى الله عليه وسلم: أيُّ العَمَلِ أحَبُّ إِلَى اللهِ تَعَالَى ؟ قَالَ : (( الصَّلاةُ عَلَى وَقْتِهَا )) ، قُلْتُ : ثُمَّ أي ؟ قَالَ : (( بِرُّ الوَالِدَيْنِ )) ، قُلْتُ : ثُمَّ أيٌّ ؟ قَالَ : (( الجِهَادُ في سبيلِ الله )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu 'Abdur-Rahman 'Abdillaah bin bin Mas'uud (Radhwiya Allaahu 'anhu) alimuuliza Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ni amali gani inayompendeza zaidi Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)? Akajibu: "Swalaah kwa wakati wake." Nikasema: "Kisha ipi?" Akasema: "Wema kwa wazazi wawili." Nikasema: "Kisha ipi?" Akasema: "Jihaad katika Njia ya Allaah." [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( لا يَجْزِي وَلَدٌ وَالِداً إلاَّ أنْ يَجِدَهُ مَمْلُوكاً ، فَيَشْتَرِيهُ فَيُعْتِقَهُ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtoto hawezi kumlipa mzazi isipokuwa kama atamkuta amemilikiwa (mtumwa), akamnunua kisha akamuacha huru." [Muslim]







Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ باللهِ وَاليَومِ الآخِرِ ، فَلْيُكْرِمْ ضَيْفَهُ ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ باللهِ وَاليَومِ الآخِرِ ، فَلْيَصِلْ رَحِمَهُ ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللهِ وَاليَومِ الآخِرِ ، فَلْيَقُلْ خَيْراً أَوْ لِيَصْمُتْ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho amkirimu mgeni wake. Na mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho aunge kizazi. Na mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho aseme maneno ya kheri (mazuri) au anyamaze." [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( إنَّ اللهَ تَعَالَى خَلَقَ الخَلْقَ حَتَّى إِذَا فَرَغَ مِنْهُمْ قَامَتِ الرَّحِمُ ، فَقَالَتْ : هَذَا مُقَامُ العَائِذِ بِكَ مِنَ القَطِيعةِ ، قَالَ : نَعَمْ ، أمَا تَرْضَيْنَ أنْ أصِلَ مَنْ وَصَلَكِ ، وَأقْطَعَ مَنْ قَطَعَكِ ؟ قَالَتْ : بَلَى ، قَالَ : فَذَلِكَ لَكِ ، ثُمَّ قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( اقْرَؤُوا إنْ شِئْتمْ : ( فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِنْ تَوَلَّيْتُمْ أَنْ تُفْسِدُوا فِي الأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا أَرْحَامَكُمْ أُولَئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَى أَبْصَارَهُمْ ) [ محمد : 22 - 23 ] مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية للبخاري : فَقَالَ الله تَعَالَى : (( مَنْ وَصَلَكِ ، وَصَلْتُهُ ، وَمَنْ قَطَعَكِ ، قَطَعْتُهُ )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) baada ya kuumba viumbe vyote, mpaka Alipomaliza (kukamilisha), yalisimama matumbo (kizazi) na kusema: "Hii ni nafasi ya mtu anayetaka ulinzi na kinga kutoka Kwako kwa mwemye kukata (kizazi, na kihitaji ulinzi)." Akasema: "Ndio je huridhiki Kwangu kumuunga anayekuunga, na kumkata mwenye kukukata?" Kikasema: "Ndio (naridhika)." Akaambiwa: "Hilo ni lako." Kisha akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Someni mkitaka: "Basi huenda nyinyi mkigeuka ndio mfanye ufisadi katika ardhi na kukata jamaa zenu wa uhusiano wa damu? Hao ndio ambao Allaah Amewalaani; Akawafanya viziwi na Akawapofua macho yao." [Muhammad: 22-23] [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na katika riwaayah ya Al-Bukhaariy: Akasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa): "Anayekuunga, Nitamuunga na anayekukata Nitamkata."







Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ: جاء رجل إِلَى رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، فَقَالَ: يَا رَسُول الله ، مَنْ أحَقُّ النَّاسِ بِحُسْنِ صَحَابَتِي ؟ قَالَ : (( أُمُّكَ )) قَالَ : ثُمَّ مَنْ ؟ قَالَ : (( أُمُّكَ )) ، قَالَ : ثُمَّ مَنْ ؟ قَالَ : (( أُمُّكَ )) ، قَالَ : ثُمَّ مَنْ ؟ قَالَ : (( أبُوكَ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية : يَا رَسُول الله ، مَنْ أَحَقُّ بحُسْنِ الصُّحْبَةِ ؟ قَالَ : (( أُمُّكَ ، ثُمَّ أُمُّكَ ، ثُمَّ أُمُّكَ ، ثُمَّ أَبَاكَ ، ثُمَّ أدْنَاكَ أدْنَاكَ )) .

Na kutoka kwake Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Alikuja mtu kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza: "Ee Rasli wa Allaah! Nani mwenye haki zaidi miongoni mwa watu wa kuwa naye na ushirikiano mzuri (na mwema)?" na Akasema: "Mama yako." Akauliza tena: "Kisha nani?" Akasema: "Mama yako." Akauliza: "Kisha nani?" Akasema: "Mama yako." Akauliza tena: "Kisha nani?" Akasema: "Baba yako." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Katika riwaayah nyengine: "Ee Rasuli wa Allaah! Nani mwenye haki zaidi ya kusuhubiana naye kwa mema?" Akasema: "Mamako, kisha mamako, kisha mamako, kisha babako, kisha wale alio chini yao."









Hadiyth – 6

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( رغِم أنفُ ، ثُمَّ رَغِمَ أنْفُ ، ثُمَّ رَغِمَ أنْفُ مَنْ أدْرَكَ أبَويهِ عِنْدَ الكِبَرِ ، أَحَدهُما أَوْ كِليهمَا فَلَمْ يَدْخُلِ الجَنَّةَ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Raghima anf, kisha raghima anf, kisha raghima anf (kudhalilishwa), mtu aliyewakuta wazazi wake katika uzee; mmoja wao au wote wawili na asiingie Peponi." [Muslim]









Hadiyth – 7

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أن رجلاً قَالَ : يَا رَسُول الله ، إنّ لِي قَرابةً أصِلُهُمْ وَيَقْطَعُوني ، وَأُحْسِنُ إلَيْهِمْ وَيُسِيئُونَ إلَيَّ ، وَأحْلَمُ عَنْهُمْ وَيَجْهَلُونَ عَلَيَّ ، فَقَالَ 🙁( لَئِنْ كُنْتَ كَمَا قُلْتَ ، فَكأنَّمَا تُسِفُّهُمْ الْمَلَّ ، وَلاَ يَزَالُ مَعَكَ مِنَ اللهِ ظَهِيرٌ عَلَيْهِمْ مَا دُمْتَ عَلَى ذلِكَ )) رواه مسلم .

Na kutoka kwake Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu): "Kuna mtu alisema: "Ee Rasuli wa Allaah! Hakika mimi nina jamaa zangu, ninaowaunga, nao wananikata. Nawafanyia wema wananifanyia mabaya; nawasamehe wananitukana." Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): " Ikiwa uko kama unavyosema, itakuwa ni kama unawalisha jivu la moto; na muda huachi kuwa hivyo ila Allaah atakusaidia dhidi yao." [Muslim]









Hadiyth – 8

وعن أنسٍ رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( من أحَبَّ أنْ يُبْسَطَ لَهُ في رِزْقِهِ ، ويُنْسأَ لَهُ في أثَرِهِ ، فَلْيَصِلْ رَحِمَهُ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa na Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anayependa akunjuliwe riziki yake, na arefushiwe maisha yake basi aunge kizazi chake." [Al-Bukhaariy, Muslim na Abu Daawuud]







Hadiyth – 9

وعن أنسٍ رضي الله عنه، قَالَ : كَانَ أَبُو طَلْحَةَ أكْثَرَ الأنْصَارِ بالمَدينَةِ مَالاً مِنْ نَخل ، وَكَانَ أحَبُّ أمْوَاله إِلَيْهِ بَيْرَحاء ، وَكَانَتْ مسْتَقْبَلَةَ المَسْجِدِ ، وَكَانَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يَدْخُلُهَا ، وَيَشْرَبُ مِنْ مَاءٍ فِيهَا طَيِّب ، فَلَمَّا نَزَلَتْ هذِهِ الآيةُ : ( لَنْ تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّى تُنْفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ) [ آل عمران : 92 ] قَامَ أَبُو طَلْحَةَ إِلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم، فَقَالَ : يَا رَسُول الله ، إنَّ الله تبارك وتَعَالَى ، يقول : ( لَنْ تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّى تُنْفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ) وَإنَّ أَحَبَّ مَالِي إِلَيَّ بَيْرَحَاءُ ، وَإنَّهَا صَدَقَةٌ للهِ تَعَالَى ، أرْجُو بِرَّهَا وَذُخْرَهَا عِنْدَ الله تَعَالَى ، فَضَعْهَا يَا رَسُول الله ، حَيْثُ أرَاكَ الله . فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( بَخ ! ذلِكَ مَالٌ رَابحٌ ، ذلِكَ مَالٌ رَابحٌ ! وقَدْ سَمِعْتُ مَا قُلْتَ ، وَإنِّي أرَى أنْ تَجْعَلَهَا في الأقْرَبينَ )) ، فَقَالَ أَبُو طَلْحَةَ : أفْعَلُ يَا رَسُول الله ، فَقَسَّمَهَا أَبُو طَلْحَةَ في أقَارِبِهِ وبَنِي عَمِّهِ . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Toka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: 'Abu Twalhah alikuwa na mitende mingi kuliko Answariwote. Mali iliyompendeza zaidi ni shamba lililokuwa Bayrahaa', lililokuwa limeelekeana na Msikiti wa Nabiy. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiingia humo na kunywa maji yake tamu. Amesema Anas: Ilipoteremka ayah hii (Hamtoweza kuufikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda) [Aal-'Imraan: 92] Abu Twalhah alimwendea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Allaah ( Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amekuteremshia: '(Hamtoweza kuufikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda)'. Kwa hakika mali niipendayo sana ni shamba la Bayrahaa', nimelitoa sadaka kwa ajili ya Allaah nikitaraji kheri na ujira kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Ee Rasuli wa Allaah, nakuomba uliweke Atakavyokuonyesha Allaah. Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Bakhin, Hiyo ni mali yenye faida, hiyo ni mali yenye faida. Bila shaka nimesikia uliyosema. Mimi naona uwape jamaa zako wa karibu." Abu Twalhah akasema: "Nitafanya, Ee Rasuli wa Allaah! Abu Twalhah akaligawa kwa jamaa zake na binamu zake." [Al-Bukhaariy na Muslim]









Hadiyth – 10

وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما ، قَالَ : أقبلَ رَجُلٌ إِلَى نَبيِّ الله صلى الله عليه وسلم، فَقَالَ : أُبَايِعُكَ عَلَى الهِجْرَةِ وَالجِهَادِ أَبْتَغي الأجْرَ مِنَ الله تَعَالَى . قَالَ : (( فَهَلْ لَكَ مِنْ وَالِدَيْكَ أحَدٌ حَيٌّ ؟ )) قَالَ : نَعَمْ ، بَلْ كِلاهُمَا . قَالَ : (( فَتَبْتَغي الأجْرَ مِنَ الله تَعَالَى ؟ )) قَالَ : نَعَمْ . قَالَ : (( فارْجِعْ إِلَى وَالِدَيْكَ ، فَأحْسِنْ صُحْبَتَهُمَا )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ ، وهذا لَفْظُ مسلِم .

وفي رواية لَهُمَا : جَاءَ رَجُلٌ فَاسْتَأذَنَهُ في الجِهَادِ ، فقَالَ : (( أحَيٌّ وَالِداكَ ؟ ))
قَالَ : نَعَمْ ، قَالَ : (( فَفيهِمَا فَجَاهِدْ )) .

Na amesema 'Abdillaahi bin 'Amr bin al-'Aasw (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa): Mtu mmoja alimkabili Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: "Nitakubai juu ya Hijra na Jihaad nikitafuta ujira kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)." Akasema: "Je, katika wazazi wako yuko aliye hai?" Akajibu: "Ndio, bali wote wawili." Akamuuliza: "je, unataka ujira kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)?" Akasema: "Ndio." Akamwambia: "Rudi kwa wazazi wako na usuhubiane nao kwa wema (wafanyie wema)." [Al-Bukhaariy na Muslim], na hii ni lafdhi ya Muslim. pia imenukuliwa na Abu Daawuud na An-Nasaa'iy.

Riwaayah ya wao wawili: Alikuja mtu akataka ruhusa ya Jihaad. Akaulizwa: "Je wazazi wako wako hai?" Akasema: "Ndio." Akaambiwa: "Kwao wao, pigana Jihaad."









Hadiyth – 11

وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( لَيْسَ الوَاصِلُ بِالمُكَافِىء ، وَلكِنَّ الوَاصِلَ الَّذِي إِذَا قَطَعَتْ رَحِمُهُ وَصَلَهَا )) رواه البخاري .

Na kutoka kwake Ibn 'Amr bin al-'Aasw (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa): Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anayeunga si yule anayetoa anapopewa, lakini anayeunga jamaa ni ambaye jamaa zake wanapomkata, yeye huwaunga." [Al-Bukhaariy, Abu Daawuud na At-Tirmidhiy]









Hadiyth – 12

وعن عائشة ، قَالَتْ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( الرَّحِمُ مُعَلَّقَةٌ بِالعَرْشِ تَقُولُ : مَنْ وَصَلَنِي ، وَصَلَهُ اللهُ ، وَمَنْ قَطَعَنِي ، قَطَعَهُ اللهُ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Aa'ishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kizazi kimetundikwa katika 'Arshi, kinasema: "Anayeniunga, Allaah atamuunga, na anayenikata, Allaah Atamkata." [Al-Bukhaariy na Muslim]









Hadiyth – 13

وعن أم المؤمنين ميمونة بنتِ الحارث رضي الله عنها : أنَّهَا أعْتَقَتْ وَليدَةً وَلَمْ تَستَأذِنِ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم، فَلَمَّا كَانَ يَوْمُهَا الَّذِي يَدُورُ عَلَيْهَا فِيهِ ، قَالَتْ : أشَعَرْتَ يَا رَسُول الله ، أنِّي أعتَقْتُ وَليدَتِي ؟ قَالَ : (( أَوَ فَعَلْتِ ؟ )) قَالَتْ : نَعَمْ . قَالَ : (( أما إنَّكِ لَوْ أعْطَيْتِهَا أخْوَالَكِ كَانَ أعْظَمَ لأجْرِكِ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Mama wa Waumini Maymuunah bint Al-Haarith (Radhwiya Allaahu 'Anhaa) kuwa alimwacha huru kijakazi bila kumuomba idhini Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alipomtembelea (Maymuunah) siku yake, alimuuliza: "Je umejua, Ee Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa nimemwacha huru kijakazi wangu?" Akamuuliza: "Je, umefanya hivyo?" Akajibu: "Ndio." Akasema: "Lau ungewapatia (kijakazi huyo) wajomba zako ungepata ujira mkubwa zaidi." [Al-Bukhaariy, Muslim na Abu Daawuud]









Hadiyth – 14

وعن أسماءَ بنتِ أَبي بكر الصديق رضي الله عنهما ، قَالَتْ : قَدِمَتْ عَلَيَّ أُمِّي وَهِيَ مُشركةٌ في عَهْدِ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم، فاسْتَفْتَيْتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قُلْتُ : قَدِمَتْ عَلَيَّ أُمِّي وَهِيَ رَاغِبَةٌ ، أفَأصِلُ أُمِّي ؟ قَالَ : (( نَعَمْ ، صِلِي أُمَّكِ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Na amesema Asmaa' bint Abu Bakr Asw-Swiddiyq (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa): Alikuja kwangu mamangu, akiwa ni mushrik katika zama za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akitaka usaidizi kutoka kwangu. Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Mamangu amekuja kwangu akitaka usaidizi, je nimuunge mamngu (kwa kumfanyia wema) mamako." [Al-Bukhaariy, Muslim na Abu Daawuud]









Hadiyth – 15

وعن زينب الثقفيةِ امرأةِ عبدِ الله بن مسعود رضي الله عَنْهُ وعنها ، قَالَتْ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( تَصَدَّقْنَ يَا مَعْشَرَ النِّسَاءِ وَلَوْ مِنْ حُلِيِّكُنَّ ))، قَالَتْ : فَرَجَعْتُ إِلَى عبد الله بنِ مسعود ، فقلتُ لَهُ : إنَّكَ رَجُلٌ خَفِيفُ ذَاتِ اليَدِ ، وَإنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَدْ أمَرَنَا بِالصَّدَقَةِ فَأْتِهِ ، فَاسألهُ ، فإنْ كَانَ ذلِكَ يْجُزِىءُ عَنِّي وَإلاَّ صَرَفْتُهَا إِلَى غَيْرِكُمْ . فَقَالَ عبدُ اللهِ : بَلِ ائْتِيهِ أنتِ ، فانْطَلَقتُ ، فَإذا امْرأةٌ مِنَ الأنْصارِ بِبَابِ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم حَاجَتي حَاجَتُها ، وَكَانَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَدْ أُلْقِيَتْ عَلَيهِ المَهَابَةُ ، فَخَرجَ عَلَيْنَا بِلاَلٌ ، فَقُلْنَا لَهُ : ائْتِ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، فَأخْبرْهُ أنَّ امْرَأتَيْنِ بالبَابِ تَسألانِكَ : أُتُجْزِىءُ الصَّدَقَةُ عَنْهُمَا عَلَى أزْواجِهمَا وَعَلَى أيْتَامٍ في حُجُورِهِما ؟ ، وَلاَ تُخْبِرْهُ مَنْ نَحْنُ ، فَدَخلَ بِلاَلٌ عَلَى رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، فسأله ، فَقَالَ لَهُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( مَنْ هُمَا ؟ )) قَالَ : امْرَأةٌ مِنَ الأنْصَارِ وَزَيْنَبُ . فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم : (( أيُّ الزَّيَانِبِ هِيَ ؟ )) ، قَالَ : امْرَأةُ عبدِ الله ، فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( لَهُمَا أجْرَانِ : أجْرُ القَرَابَةِ وَأجْرُ الصَّدَقَةِ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Na imepokewa kwa Zaynab Ath-Thaqafiyyah (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) mke wa 'Abdillaahi bin Mas'uud kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Enyi kongamano la wanawake, toeni sadaqah japokuwa ni mapambo ya vito." Akasema: Nilirudi kwa 'Abdillaahi bin Mas'uud nikamwambia: "Hakika wewe ni mtu mwenye mali kidogo na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuamuru tutoe sadaqah, nenda ukamuulize ikiwa inanitosheleza kukupa wewe, ikiwa si hinyo nimpatie mwengine." Akasema 'Abdillaahi: "Bali nenda mwenyewe." Nikatoka kuelekea (kwa Rasuli), hapo nikakutana na mwanamke miongoni mwa Answaar mlangoni mwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), haja yake ni kama yangu. Na tulikuwa tunamstahi sana Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Hivyo, pindi alipotutokea Bilaal (Radhwiyah Allaahu 'anhu) tulimwambia: "Nenda kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) umpashe habari kuwa wapo wanawake wawili mlangoni wanakuuliza: "Je, inatosha kwa wao wanawake kuwapatia waume zao swadaqah (zakaah) na pia mayatima majumbani mwao wala usimwambie sisi ni nani." Bilaal akaingia kumuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akauliza: "Wao ni nani?" Akajibu: "Mwanamke wa Ki-Answaar na Zaynab." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ni Zaynab gani huyo?" Akajibu: "Ni mkewe 'Abdillaahi." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Watapata thawabu mara mbili: Ujira wa ujamaa na ujira wa swadaqah." [Al-Bukhaariy na Muslim]









Hadiyth – 16

وعن أَبي سفيان صخر بنِ حرب رضي الله عَنْهُ في حديثِهِ الطويل في قِصَّةِ هِرَقْلَ : أنَّ هرقْلَ قَالَ لأبي سُفْيَانَ : فَمَاذَا يَأمُرُكُمْ بِهِ ؟ يَعْنِي النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : قُلْتُ : يقول : (( اعْبُدُوا اللهَ وَحْدَهُ ، وَلاَ تُشْرِكُوا بِهِ شَيئاً ، واتْرُكُوا مَا يَقُولُ آبَاؤُكُمْ ، وَيَأمُرُنَا بِالصَّلاةِ ، وَالصّدْقِ ، والعَفَافِ ، والصِّلَةِ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Sufyaan Swakhr bin Harb (Radhwiyah Allaahu 'anhu) katika hadiyth yake ndefu kuhusiana na kisa cha Hiraql. Hiraqal alimuuliza Abu Sufyaan: "Je, anawaamuru nini, Yani: Nabiy?" Akasema: Nikamwambia kuwa anasema: Muabuduni Allaah Peke Yake wala usimshirikishe Yeye na chochote, na acheni wanayosema baba zenu, anatuamuru kuswali, kusema ukweli, kuwa safi (kutozini) na kuunga uzazi." [Al-Bukhaariy na Muslim]









Hadiyth – 17

وعن أَبي ذرّ رضي الله عَنْهُ، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( إنَّكُمْ سَتَفْتَحُونَ أرْضاً يُذْكَرُ فِيهَا القِيرَاطُ )) . وفي رواية : (( سَتَفْتَحونَ مِصْرَ وَهِيَ أرْضٌ يُسَمَّى فِيهَا القِيراطُ ، فَاسْتَوْصُوا بأهْلِهَا خَيْراً ؛ فَإنَّ لَهُمْ ذِمَّةً وَرَحِماً )) وفي رواية : (( فإذا افتتحتموها ، فأحسنوا إلى أهلها ؛ فإن لهم ذمة ورحماً )) ، أَوْ قَالَ : (( ذِمَّةً وصِهْراً )) رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika nyinyi mtaifungua ardhi inayoitwa Qiyraatw." Na katika riwaayah nyengine: Mtaifungua Misri na hiyo ni ardhi inayoitwa Qiyraatw, wafanyieni wema watu wake; kwani wana uhusiano nanyi, katika haki ya ulinzi na kizazi", Katika riwaayah : Mapoifungua, wafanyieni wema watu wake; kwani tuna uhusiano naowa ulinzi na kizazi" au amesema: "haki na ukwe." [Muslim]







Hadiyth – 18

وعن أَبي هريرة رضي الله عَنْهُ، قَالَ : لما نزلت هذِهِ الآية : ( وَأَنْذِرْ عَشِيرَتَكَ الأَقْرَبِينَ ) [ الشعراء : 214] دَعَا رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قُرَيْشاً ، فَاجْتَمَعُوا فَعَمَّ وَخَصَّ ، وَقالَ : (( يَا بَنِي عَبْدِ شَمْسٍ ، يا بَنِي كَعْبِ بْنِ لُؤيٍّ ، أنقِذُوا أنْفُسَكُمْ مِنَ النَّارِ ، يَا بَنِي مُرَّةَ بن كَعْبٍ ، أنْقِذُوا أنْفُسَكُمْ مِنَ النَّارِ ، يَا بَنِي عَبْدِ مَنَاف ، أنْقِذُوا أنْفُسَكُمْ مِنَ النَّارِ ، يَا بَنِي هاشم ، أنقذوا أنفسكم من النار ، يَا بني عبد المطلب ، انقذوا أنفسكم من النار ، يَا فَاطِمَةُ ، أنْقِذي نَفْسَكِ مِنَ النَّارِ . فَإنِّي لا أمْلِكُ لَكُمْ مِنَ اللهِ شَيئاً ، غَيْرَ أنَّ لَكُمْ رَحِماً سَأبُلُّهَا بِبِلالِهَا )) رواه مسلم .

Imepokewa na Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: Ilipoteremka aayah hii: "Na onya (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) jamaa zako wa karibu." [Ash-Shu'araa: 214]. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaita Maquraysh katika makundi yao na watu binafsi, akasema: "Enyi Bani 'Abdi Shams, enyi Bani Ka'b bin Lu'ayy, ziokoeni nafsi zenu na Moto. Enyi Bani Murrah bin Ka'b, ziokoeni nafsi zenu na Moto; enyi Bani 'Abdi Manaaf, ziokoeni nafsi zenu na Moto, enyi Bani Haashim, ziokoeni nafsi zenu na Moto; enyi Bani 'Abdil Mutwtwalib, ziokoeni nafsi zenu na Moto; Ee Faatwimah, okoa nafsi yako na Moto, kwani siwezi kuwafanyia lolote mbele ya Allaah. Hata hivyo, baina yetu kuna unasaba, nami nitaulinda. (na kuuhifadhi)." [Muslim]





Hadiyth – 19

وعن أَبي عبد الله عمرو بن العاص رضي الله عنهما ، قَالَ : سمعت رَسُول الله صلى الله عليه وسلم جِهَاراً غَيْرَ سِرٍّ ، يَقُولُ : (( إنَّ آل بَني فُلاَن لَيْسُوا بِأولِيَائِي ، إِنَّمَاوَلِيِّيَ اللهُ وَصَالِحُ المُؤْمِنينَ ، وَلَكِنْ لَهُمْ رَحِمٌ أبُلُّهَا بِبلاَلِهَا )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ ، واللفظ للبخاري .

Kutoka kwa Abu Abdillaahi 'Amr bin Al-'Aasw (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema waziwazi bila kuficha: "Hakika jamaa wa Bani fulani si rafiki zangu. Hakika rafiki yangu ni Allaah na walio wema katika Waumini, lakini wana ujamaa, nitauunga." [Al-Bukhaariy na Muslim, na lafdhi ni ya Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 20

وعن أَبي أيوب خالد بن زيد الأنصاري رضي الله عَنْهُ: أنَّ رجلاً قَالَ : يَا رَسُول الله ، أخْبِرْني بِعَمَلٍ يُدْخِلُني الجَنَّةَ ، وَيُبَاعِدُني مِنَ النَّارِ . فَقَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم: (( تَعْبُدُ الله ، وَلاَ تُشْرِكُ بِهِ شَيئاً ، وَتُقِيمُ الصَّلاةَ ، وتُؤتِي الزَّكَاةَ ، وتَصِلُ الرَّحمَ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Ayyuub Khaalid bin Zayd Al-Answaariy (Radhwiyah Allaahu 'anhumma) kuwa mtu mmoja alisema: "Ee Rasuli wa Allaah! Nipe habari ya amali itakayo niingiza Peponi na kuniepusha na Moto?" Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Muabuduni Allaah wala usimshirikishe kwa chochote, usimamishe Swalaah, utoe Zakaah na uunge kizazi (ujamaa)." [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 21

وعن سلمان بن عامر رضي الله عَنْهُ ، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( إِذَا أفْطَرَ أحَدُكُمْ ، فَلْيُفْطرْ عَلَى تَمْرٍ ؛ فَإنَّهُ بَرَكةٌ ، فَإنْ لَمْ يَجِدْ تَمْراً ، فالمَاءُ ؛ فَإنَّهُ طَهُورٌ )) ، وَقالَ : (( الصَّدَقَةُ عَلَى المِسكينِ صَدَقةٌ ، وعَلَى ذِي الرَّحِمِ ثِنْتَانِ : صَدَقَةٌ وَصِلَةٌ )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن )) .

Na imepokewa kutoka kwa Salmaan bin 'Aamir (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapofuturu mmoja wenu afuturu kwa tende, kwani ina baraka. Asiopata tende, basi afungue kwa maji; kwani yanatwahirisha." Na akasema: "Sadaqah kwa maskini ni sadaqah na kumpa jamaa ina ujira mara mbili: ni sadaqah na kuunga ujamaa." [At-Tirmidhiy, na akasema Hadiyth Hasan]





Hadiyth – 22

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : كَانَتْ تَحْتِي امْرَأةٌ ، وَكُنْتُ أحِبُّهَا ، وَكَانَ عُمَرُ يَكْرَهُهَا ، فَقَالَ لي : طَلِّقْهَا ، فَأبَيْتُ ، فَأتَى عُمَرُ رضي الله عَنْهُ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، فَذَكَرَ ذلِكَ لَهُ ، فَقَالَ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم: (( طَلِّقْهَا )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن صحيح )) .

Amesema Ibn 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa): Nilimuoa mke niliyekuwa nampenda; lakini 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhu) alikuwa anamchukia. Akaniambia: "Mpatie talaka", Nikakataa. 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhu) alikwenda kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumtajia jambo hilo. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Mtaliki." [Abu Daawuud na At-Tirmidhiy, naye akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]







Hadiyth – 23

وعن أَبي الدرداءِ رضي الله عَنْهُ: أن رجلاً أتاه ، قَالَ : إنّ لي امرأةً وإنّ أُمِّي تَأمُرُنِي بِطَلاقِهَا ؟ فَقَالَ : سَمِعْتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( الوَالِدُ أوْسَطُ أبْوَابِ الجَنَّةِ ، فَإنْ شِئْتَ ، فَأضِعْ ذلِكَ البَابَ ، أَو احْفَظْهُ )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن صحيح )) .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Dardaa (Radhwiyah Allaah 'anhu) kuwa mtu mmoja alikuja kwake, akamuuliza: "Hakika mimi nina mke, ambaye mamangu anataka nimuache?" Akamwambia: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mzazi ndiye mlango bora miongoni mwa milango ya Peponi, ukitaka upoteze huo mlango au uhifadhi." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]







Hadiyth – 24

وعن البراءِ بن عازب رضي اللهُ عنهما ، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( الخَالةُ بِمَنْزِلَةِ الأُمِّ )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن صحيح )) .

Na imepokewa kutoka kwa Al-Baraa' bin 'Aazib (Radhiwyah Allaahu 'anhummaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Halati (mama mdogo) yu katika daraja ya mama." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
 
Baadhi ya post za zamani.....


Ningependa Leo nizungumzie maswala ya kiroho na walengwa ambao Nataka niwakumbushe neno la Mungu ni Wale wanao mwamini Mwenyezi Mungu. Kama wewe humwamini Mwenyezi Mungu au unaamini Mungu hayupo basi huu Uzi haukufai.

Mwenyezi Mungu anasema katika Kitabu chake katika Suratul Ibrahim Aya ya 31:
''Waambie waja wangu walio amini, washike Sala, na watoe katika tulivyo waruzuku, kwa siri na dhaahiri, kabla haijafika Siku isiyo kuwa na biashara wala urafiki.''

Mwenyezi Mungu katika Kitabu chake amekuwa na kawaida ya kuongea na watu Kwa daraja zao, ndio maana kuna Aya anazungumza Kwa kusema Enyi watu na Aya nyingine anasema Enyi mlioamini. Anapozungumzia Enyi watu mara nyingi huzungumza na viumbe wake wote wanao mwamini yeye na wasio mwamini yeye na wanaomini Mungu zaidi ya mmoja. Na mara nyingi huwapa hoja mbali mbali za kufikirisha akili zao na bongo zao juu ya kuumbwa Kwa ulimwengu na viumbe wake pamoja na yaliyomo ndani yake, je hayo wanayo yaona hayatoshi kuwafanya wao kutafakari na kuona kuwa hayo hayakutokea bure Tu Ila kuna Mwenyezi Mungu aliyeumba mambo yote hayo? Huo ni mfano mmoja Tu nilio ugusa hapo.

Na anapo ongea na walioamini, anaongea na watu ambao tayar wamemwamini Mungu Mmoja na hawa ndio wamesalimika,kwasababu Mwenyezi Mungu hana ushirika wala usaidizi toka Kwa kiumbe kingine chochote kile, yeye ndio mkuu na ndiye aliye juu, sifa zake amezieleza vizuri katika Suratul Bakara Aya ya 255:

''Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu.''

Baada ya kuona sifa zake..turudi kwenye lengo kuu la Aya ambayo nimeshaitaja awali. Kwanza Mwenyezi Mungu anasema Waambie waja wangu walioamini wasimamishe Sala, ndugu zangu katika Imani, Sala au Swala ndio amali au kitendo cha Kwanza kuhesabiwa siku ya hukumu,hapo unaona ni jinsi gani Swala ilivyo na umuhimu mkubwa mbele ya Allah, na katika nguzo tano ambazo Uislamu umejengwa juu yake basi Swala ndio Nguzo ya pili kusimikwa mara baada Tu ya kukiri kuwa Hapana Mola apasae KUABUDIWA Kwa haki isipokuwa Allah/Mwenyezi Mungu. Na anayesimamisha au anayedumu na ibada hii basi hakika amesimamisha Dini,na ikasemwa pia tofauti ya walioamini na waliokufuru ni Swala.

Na Mtume (rehma na Amani iwe juu yake) akasema '' mfano wa swala tano ni kama mtu ambaye nyumba yake ipo karibu na mto, na anaoga mara tano Kwa siku. Je, mtu kama huyo atakuwa na uchafu mwilini mwake?'' Hapo inaonyesha hakika kila kipindi kimoja cha swala kinafuta madhambi ya mja wa Allah,hakika amali hii ni muhimu hivyo hatuna budi kujitahidi kuifanya kwa uwezo wetu wote Mjumbe wa Allah alisema ukimuona mtu anapenda kwenda msikitini basi yatosha kusema huyu mtu ana Imani.

Pili Mwenyezi Mungu anasema tutoe katika vile alivyoturuzuku Kwa Siri na dhahiri...ni mtu asiye mwamini Mwenyezi Mungu Tu ndio anaamini kuwa mafanikio aliyonayo kayapata Kwa ujanja wake au Kwa maarifa yake,lakini mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu hakika anajua vyote alivyonavyo amepewa na Mola wake mlezi,na hivyo Hana budi kutoa sadaka,zaka na kuwasaidia wenye uhitaji kwakuwa anajua ndani ya nafsi yake kuwa IPO siku ataulizwa juu ya neema aliyopewa.

Na sadaka waeza Toa Kwa Siri au Kwa dhahiri lakini kitu kibaya ni kutoa Kwa kutaka Sifa mbele za watu uonekane kuwa wewe ni mtoaji mzuri,hapo hautapata malipo toka Kwa Mwenyezi Mungu kwakuwa ulikusudia ktk moyo wako usifiwe na watu,lkn kama ulitoa mbele za watu Kwa Nia ya kutaka radhi za Mwenyezi Mungu basi hakika utapata malipo toka Kwa Mola wako.

Lakini tunaambiwa kutoa sadaka Kwa Siri ndio Bora zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu,na hapo unakuja ule msemo kuwa ukitoa sadaka Kwa mkono wa Kulia basi mkono WA kushoto usijue,maana halisi ndiyo utoe Kwa Siri sadaka yako...ingawa baadhi ya watu unakuta wakitoa hela zao msikitini basi daah wanazikunja hizo hela mpaka zinakosa hewa! Yaani kama zingekuwa zinapumua basi zingekosa pumzi na kufa hahah! Kutokutoa Kwa Siri ni kama vile unatoa huku unatangaza Kwa watu,Mimi bwana nimetoa shilingi kadhaa au unamuona Fulani alikuwa hana hela ya kula ujue Mimi ndio nimemsaidia,hakika sadaka za namna hiyo hazina malipo mbele ya Mwenyezi Mungu hata kidogo.

Mwisho Mwenyezi Mungu anawaonya waumini kuwa washike sala na kutoa katika vile walivyoruzukiwa kabla haijaja siku isiyo na biashara wala Urafiki, tunajua hapa duniani huwa tunanufaishana na kusaidiana Kwa kuwa ni marafiki,kuna watu hawafungwi jela kwasababu ya Urafiki,hawalipi Kodi stahiki kwasababu ya Urafiki, wanafanya dhuluma mbali mbali kisa Tu Wana Urafiki na polisi hivyo huwezi kuwagusa,yote hayo siku ya hukumu hakuna habari hizo....

Ukija upande WA biashara nako hivyo hivyo,hapa duniani ndio sehemu nzur ya kufanya biashara na Mwenyezi Mungu,ukitenda mema utalipwa mema zaidi ya hayo uliyotenda,ni sehemu ya kuchuma thawabu zitakazo kufaa huko mbele ya safari,lakini kama hakufanya biashara hiyo wakati huko hai basi siku hiyo ya hukumu hakutakuwa na nafasi nyingine ya kuchuma mema.

Namalizia na dua ya Nabii Ibrahim pale alipo muomba Mola wake Mlezi amsaidie kusimamisha Sala pamoja na familia yake:

"Mola wangu Mlezi! Nijaalie niwe mwenye kushika Sala, na katika dhuriya zangu pia. Ewe Mola wetu Mlezi, na ipokee dua yangu."
Surah Ibrahim :40
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com







41-Je, Inajuzu kupinduka mipaka kumsifu Nabiy kwa kumpandisha cheo kama cha Allaah?



Hapana! Haijuzu kupinduka mipaka kumsifu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mpaka kumfikisha cheo cha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).



قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi ni mtu kama nyinyi, nafunuliwa Wahy kwamba: Hakika Muabudiwa wa haki wenu ni Ilaah Mmoja Pekee [Al-Kahf: 111]



((لا تُطْرُونِي كَمَا أَطْرَتْ النَّصَارَى ابْنَ مَرْيَمَ فَإِنَّمَا أَنَا عَبْدُهُ فَقُولُوا عَبْدُ اللَّهِ وَرَسُولُهُ)) متفق عليه

((Msinitukuze kama Manaswara walivyomtukuza Masiyh mwana wa Maryam, hakika mimi ni mja kwa hiyo semeni mja wa Allaah na Rasuli Wake)) [Al-Bukhaariy, Muslim]
 
42-Nani kiumbe cha mwanzo na kipi kilichoumbwa mwanzo?



Kiumbe cha mwanzo kabisa ni Aadam ('Alayhis-Salaam) na kitu cha mwanzo kuumbwa ni kalamu.

إِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي خَالِقٌ بَشَرًا مِّن طِينٍ ﴿٧١﴾

Pale Rabb wako Alipowaambia Malaika: “Hakika Mimi Namuumba mtu kutokana na udongo. [Swaad: 71]



((إنّ أوّلَ مَا خَلَقَ اللهُ الْقَلَم)) رواه أبو داود والترمذي، وقال: حسن صحيح

((Kitu cha kwanza Alichoumba Allaah ni kalamu)) [Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy amesema Hasan Swahiyh]
 
43-Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameumbwa kutokana na nini?



Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameumbwa kutokana na manii (kwa sababu yeye ni mwana Aadam kama sisi).



هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ

Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbeni kutokana na mchanga, kisha kutokana na tone la manii. [Ghaafir: 67]



((إنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ في بَطْنِ أُمِّه فِي أرْبعينَ يوْماً نُطْفَةً)) متفق عليه

((Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake siku arubaini akiwa ni mkusanyiko wa manii)) [Al-Bukhaariy, Muslim]



Manii ni mbegu za uzazi za mama na baba
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com







44-Nini hukumu ya jihaad kwa Muislamu?



Kufanya jihaad ni waajib kwa Muislamu kwa kutumia mali, nafsi, na ulimi.



انفِرُوا خِفَافًا وَثِقَالًا وَجَاهِدُوا بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ

Tokeni mwende (vitani) mkiwa wepesi na (mkiwa) wazito, na fanyeni jihaad kwa mali zenu na nafsi zenu katika njia ya Allaah. [At-Tawbah: 41]



((جَاهِدُوا الْمُشْرِكِينَ بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنْفُسِكُمْ وَأَلْسِنَتِكُمْ)) صحيح أبي داود

((Piganeni Jihaad na washirikina kwa mali zenu, nafsi zenu na ndimi zenu)) [Swahiyh Abiy Daawuwd: (2186)]
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com









45-Vipi kuwafanyia urafiki Waumini?



Kuwafanyia urafiki Waumini ni kuwaandama kwa mapenzi na kuwanusuru Waumini walioshikamana na Tawhiyd.

وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ

71. Na Waumini wanaume na Waumini wanawake ni marafiki wandani wao kwa wao, [At-Twabah: 71]





((الْمُؤْمِنُ لِلْمُؤْمِنِ كَالْبُنْيَانِ يَشُدُّ بَعْضُهُ بَعْضًا)) متفق عليه.

((Muumini kwa Muumini mwenzake ni kama mfano wa jengo (matofali) hushikamana pamoja. [Al-Bukhaariy, Muslim]
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com









46-Je, Inafaa kufanya urafiki na makafiri na kuwasaidia?



Hapana! Haifai kufanya urafiki na kuwaandama makafiri na kuwasaidia.



وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ

Na yeyote atakayewafanya marafiki wao wandani; basi hakika yeye ni miongoni mwao. [Al-Maaidah: 51]



((إنَّ آلَ أَبِي فُلَانٍ لَيْسُوا لِي بأولياء)) متّفق عَلَيهِ

لأنّهم من الكفّار

((Hakika watu wa kabila fulani si vipenzi vyangu))[Al-Bukhaariy, Muslim]



Kwa sababu wao ni makafiri.
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com









47-Nani Waliyy wa Allaah?



Waliyy wa Allaah ni Muumini mwenye taqwa mno na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).



أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّـهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴿٦٢﴾

Tanabahi! Hakika vipenzi wa Allaah hawana khofu juu yao, na wala hawatohuzunika



الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ﴿٦٣﴾

Ambao wameamini na wakawa wana taqwa. [Yuwnus: 63]



((إِنَّمَا وَلِيِّيَ اللهُ وَصَالِحُ الْمُؤْمِنِينَ)) متّفق عَلَيهِ

((Bali yeye ni kipenzi cha Allaah na Muumini mwema)) [Al-Bukhaariy, Muslim]
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com









48-Kwanini Allaah Ameteremsha Qur-aan?



Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ameteremsha Qur-aan ili tufuate yaliyomo.



اتَّبِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلَا تَتَّبِعُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ ۗ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ ﴿٣﴾

Fuateni yale mliyoteremshiwa kutoka kwa Rabb wenu na wala msifuate badala Yake walinzi. Ni machache mnayoyakumbuka. [Al-A’raaf: 3]



((اقْرَءُوا الْقُرْآنَ وَاعْمَلُوا بِهِ وَلَا تَغْلُوا فِيه وَلَا تَجْفُوا عَنْهُ وَلَا تَأْكُلُوا بِهِ وَلَا تَسْتَكْثِرُوا بِهِ)) رواه أحمد

((Someni Qur-aan na muifanyie kazi, na wala msipokee ujira kwa kuisoma)) [Ahmad]
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com









49-Je, tutosheke na Qur-aan bila Hadiyth?





Hapana! Tunapaswa tuifuate Qur-aan na pia Hadiyth bila kutosheka na Qur-aan pekee.



وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ

(Tumewatuma) Kwa hoja bayana na vitabu. Na Tumekuteremshia Ukumbusho (Qur-aan) ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao. [An-Nahl: 44]



((أَلَا إِنِّي أُوتِيتُ الْقُرْآنَ وَمِثْلَهُ مَعَهُ)) صحيح رواه أبو داود

((Hakika mimi nimepewa Qur-aan na mfano wake)) [Hadiyth Swahiyh, Abuu Daawuwd]
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com









50-Je? Tunaweza kutanguliza maneno yetu mbele ya kauli ya Allaah Na Rasuli Wake?





Hapana! Haifai kutanguliza maneno yetu mbele ya kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)



Yaani: Msilete rai zenu wala msifanye kinyume na Aliyoamrisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيِ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿١﴾

Enyi walioamini! Msikadimishe (lolote) mbele ya Allaah na Rasuli Wake [Al-Hujuraat: 1]



((لَا طَاعَة لأحدَ فِي مَعْصِيَةِ اللَّهِ إِنَّمَا الطَّاعَةُ فِي الْمَعْرُوفِ)) متّفق عَلَيهِ

((Hakuna kumtii mtu yeyote katika kumuasi Allaah, Bali Utiifu ni katika mambo mema)) [Al-Bukhaariy, Muslim]
 
Amefariki Hana Wazazi Wala Watoto
Maswali: Mirathi
SWALI

ASSALAM ALAYKUM,

AMEFARIKI MTU (MWANAUME) HAKUACHA WAZAZI WALA MTOTO BALI WARITHI WAKE NI;

(A) NDUGU (WAWILI) WA KIKE MMOJA NA WAKIUME MMOJA. ALIOZALIWA NAO BABA MMOJA NA MAMA MMOJA (SHAQIIQ)

(B) NDUGU (WANANE) WA KIKE WATANO NA WAKIUME WATATU. ALIOZALIWA NAO BABA MMOJA MAMA MBALIMBALI.

JE WANAORITHI NI (A) TU, AU (A) NA (B) PAMOJA?







JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.





Shukran kwa swali lako hilo kuhusu urithi wa wafiwa. Samahani kwa kuchelewa kukujibu. Hapa chini tumeweka mgawo wa mali ya aliyefariki baada ya kutoa matumizi ya mazishi na madeni yake.



Mrithi



Uhusiano

Haki yake

Hukumu

1

Kaka shaqiqi

66.66%



Huyu anapata thuluthi mbili (2/3)

2

Dada shaqiqi

33.33%



Nasibu yake ni thuluthi (1/3)

3

Kaka wa baba1

0

Anazuiliwa kurithi kwa kuwepo ndugu wa kiume aliye shaqiqi wa aliyefariki.

4

Kaka wa baba2

0

Anazuiliwa kurithi kwa kuwepo ndugu wa kiume aliye shaqiqi wa aliyefariki.

5

Kaka wa baba3

0

Anazuiliwa kurithi kwa kuwepo ndugu wa kiume aliye shaqiqi wa aliyefariki.

6

Dada wa baba1

0

Anazuiliwa kurithi kwa kuwepo ndugu wa kiume aliye shaqiqi wa aliyefariki.



Dada wa baba2

0

Anazuiliwa kurithi kwa kuwepo ndugu wa kiume aliye shaqiqi wa aliyefariki.



Dada wa baba3

0

Anazuiliwa kurithi kwa kuwepo ndugu wa kiume aliye shaqiqi wa aliyefariki.



Dada wa baba4

0

Anazuiliwa kurithi kwa kuwepo ndugu wa kiume aliye shaqiqi wa aliyefariki.



Dada wa baba5

0

Anazuiliwa kurithi kwa kuwepo ndugu wa kiume aliye shaqiqi wa aliyefariki.



Jumla

100%







Na Allaah Anajua zaidi
 
Aliyefariki Ameacha Kaka, Dada Na Mjukuu
Maswali: Mirathi
SWALI:

Aliyefariki amewachja kaka mmoja wa mama mmoja, kaka mmoja wa baba mmoja, madada wawili wa mama mmoja na mjukuu kwa mtoto wake wa kiume {aliyefariki kabla}. Ahsante.





JIBU:

AlhamduliLlaah - Himdi Na Sifa Zote Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho



Hakika swali hili haliko moja kwa moja kwani kuna mengi ambayo hayakuelezwa lakini ikiwa muulizaji ana hakika hao ndio warithi au jamaa wa karibu kabisa kwa aliyefariki basi watarithi kama ifuatavyo:

1) Mjukuu akiwa ni wa kiume atapata wirathi wote na hao wengine, kaka wa kwa mama, madada wa kwa mama na kaka wa kwa baba hawatapa chochote.

2) Ikiwa mjukuu ni msichana basi atapata nusu (1/2) ya wirathi, kaka wa kwa mama na madada wa kwa mama hawatapata chochote na kilichobaki yaani nusu (1/2) atapewa kaka wa kwa baba.

Lau huyu aliyefariki alikuwa na mzazi au wazazi walio hai na pia alikuwa na mke au mume mgawo wa wirathi utabadilika.



Tanbihi kwa wenye kuuliza Maswali ya Mirathi:



Ili maswali yenu yajibike haraka inatakiwa kuwa wale watu wote ambao wana ukaribu wa kidamu wa aliyefariki wawe ni wenye kuandikwa ili iwe hapana utata wowote. Na katika hayo tungependa watu wafuatao watiliwe maanani sana:

1. Kijana mwanamume.

2. Kijana mwanaume wa kijana mwanaume (mjukuu).

3. Baba.

4. Babu wa kwa baba.

5. Ndugu mume wa kwa baba na mama (khalisa).

6. Ndugu wa kwa baba.

7. Ndugu mume wa kwa mama.

8. Kijana mwanaume wa ndugu mume khalisa.

9. Kijana mwanaume wa ndugu mume wa kwa baba.

10. Ami wa kwa baba na mama.

11. Ami wa kwa baba.

12. Kijana mwanaume wa ami wa kwa baba na mama.

13. Kijana mwanaume wa ami wa kwa baba.

14. Mume.

15. Binti.

16. Binti wa kijana mwanaume.

17. Mama.

18. Dada khalisa.

19. Dada wa kwa baba.

20. Dada wa kwa mama.

21. Bibi mzaa baba.

22. Bibi mzaa mama.

23. Mke.

Hii itatusaidia sana katika kujibu maswali yenu ya mirathi. Shukran.



Na Allaah Anajua zaidi.
 
Ameacha Mke, Watoto Wa Kike Wawili, Ndugu Wa Kike Watatu
Maswali: Mirathi
SWALI:



ASALAM ALEYKUM. Aliyefariki ameacha watoto wa kike wawili, mjane, ndugu wa kiume mmoja, na ndugu wa kike wa tatu. Je, asilimia ngapi kila mtu atapata?





JIBU:





Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukran zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mirathi ya baba aliyeaga. Muulizaji hakututajia kama aliyefariki aliacha wazazi wote wawili au mmoja hivyo tunachukulia kuwa hakuacha.



Katika hilo hakika ni kuwa mjane aliyebaki anapata fungu lake maalumu, nalo ni thumuni (1/8) kwa sababu ya aliyefariki kuwa na watoto. Allaah Aliyetukuka Anasema:

“Na wake zenu watapata robo mlichokiacha, ikiwa hamna mtoto. Mkiwa mna mtoto basi sehemu yao ni thumuni ya mlichokiacha, baada ya wasia mliousia au kulipa deni” (4: 12).

Na mabinti kwa kuwa wao ni wawili watapata kila mmoja thuluthi (1/3).



Ama ndugu wa aliyefariki watarithi kwa sababu ya kutowepo watoto waaliyefariki wa kiume.





Jadwali ya wirathi itakuwa kama ifuatavyo:





Namba

Uhusiano na Aliyefariki

Kiwango

Asilimia

1

Mjane

Thumuni (1/8)

12.5

2

Binti 1

Thuluthi (1/3)

33.33

3

Binti 2

Thuluthi (1/3)

33.33

4

Kaka



8.34

5

Dada 1



4.17

6

Dada 2



4.17

7

Dada 3



4.17



Jumla



100.01





Na Allaah Anajua zaidi
 
Ameacha Wake Wawili Watoto Watano Wakiume, Mke Aliyemtaliki Ana Watoto Watatu
Maswali: Mirathi
SWALI:



Baba yetu amefariki karibu mwezi wa pili sasa na mirathi imepangwa kuzungumzwa baada ya kuisha eda za wake zake wawili. Ameacha watoto watano wakiume (watu wazima wenye familia zao) kutoka mke wa kwanza. Pia ameacha mtoto mmoja wa kiume (umri miaka 2) kutoka mke wa pili. halafu kuna mke alimtariki kitambo kabla ya kumuoa huyu mke wa pili, huko alizaa naye watoto watatu wa kiume (wote -umri chini ya miaka 10) vilevile baba alikuwa akiwalea wajuu zake wanne-3 wa kike, 1 wa kiume, watoto wa aliyefariki dada yetu (kutoka mke wa kwanza) SWALI NI KWAMBA NANI NI WARITHI HALALI WA HUYU ALIYEFARIKI NA NINI UWIANO WA MGAO WA MALI ZA ALIYEFARIKI KWA HAO WARITHI?







JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mirathi ya warithi waliofiliwa na mume/ au baba yao. Wale ambao wanamrithi aliyefariki akiwa ni mwanamme kama ilivyo kwenu ni wazazi wakiwa hai, mke au wake zake na watoto wake kama alivyopanga Allaah Aliyetukuka katika Qur-aan.



Kwa kuwa hamukutaja kama wazazi wa aliyefariki wapo kumaanisha kuwa wameshaaga, yaani hawapo tena duniani. Ikiwa si hivyo mtatueleza. Baada ya kueleza hayo ni kuwa wale watakaomrithi kulingana na ulivyoeleza ni:



Wake zake wawili ambao wanamkalia eda, ama yule aliyetalikiwa hatapata chochote. Hawa wake wawili watagawa thumuni (1/8) ya mali ya mzee. Hii inamaanisha kila mke atapata nusu ya thumuni (1/16). Hii ni kulingana na kauli Ya Allaah Aliyetukuka: “Na wake zenu watapata robo mlicho kiacha, ikiwa hamna mtoto. Mkiwa mna mtoto basi sehemu yao ni thumuni ya mlicho kiacha, baada ya wasia mlio usia au kulipa deni” (an-Nisaa’ [4]: 12).


Ama watoto kwa kuwa wote ni wanaume watarithi sawasawa kilichobaki. Na watoto watakaorithi ni watoto wakiume watano kwa mke wa kwanza. Mtoto wa kiume wa miaka miwili wa mke wa pili na pia watoto wa tatu kwa mtalaka wake. Ama wajukuu hawatapa chochote kwa kuwepo watoto wake.


Na Allaah Anajua zaidi.
 
Ameacha Watoto Wa Kiume Na Wakike Wakiwa Matumbo Mawili Tofauti – Mke Mkubwa Alimuacha Kabla Ya Kifo – Je Watoto Wake Wanahaki?
Maswali: Mirathi
SWALI:



ASS-ALAM ALAIKUM?

Mtu amefariki ameacha watoto wa KIUUME/WAKIKE, wakiwa wamezaliwa ktk matumbo mawili tofauti, Mke mkubwa alisha muacha kabla ya kifo chake. Jee hawa watoto wa mke mkubwa wanawajibu wa kisheria wa kumtimizia mahitajio kizuka huyu? Naomba jibu kwa Qurani na Khadithi. WABILAHI TAWFIQI.









JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mirathi baada ya kufa baba mzazi. Katika Uislamu, watoto wa aliyefariki ni watoto, wawe ni wakike au wa kiume, wawe ni kutoka tumbo moja au kwa mama tofauti. Kila mmoja amepatiwa haki yake ya kurithi ya Allaah Aliyetukuka.



Baba anapofariki akiwa mke wake wa kwanza aliyemtaliki yu hai, mke huyo hatapata chochote katika mirathi. Mke mwenye kupata mirathi ni yule ambaye ni mke wa aliyefariki. Aliyefariki akiwa na watoto kama ilivyo katika swali lako, mke wa aliyefariki anapata thumuni (1/8). Hii ni kwa ajili ya maneno ya Aliyetukuka: “Na wake zenu watapata robo mlicho kiacha, ikiwa hamna mtoto. Mkiwa mna mtoto basi sehemu yao ni thumni ya mlicho kiacha, baada ya wasia mlio usia au kulipa deni” (an-Nisaa’ [4]: 12).



Na watoto wake wanapata kwa kiwango kifuatacho, kijana wa kiume sehemu mbili kwa msichana sehemu moja. Allaah Aliyetukuka Anasema: “Allaah Anakuusieni juu ya watoto wenu: Fungu la mwanamume ni kama fungu la wanawake wawili” (an-Nisaa’ [4]: 11). Wale ambao hawatarithi ni watoto wa mke mkubwa aliyetalikiwa aliowapata kwa mume mwingine au watoto wa mke wa pili alionao kutoka kwa mume mwingine labda kabla hajaolewa na aliyefariki hata kama amewalea yeye, aliyefariki.



Ikiwa tutapata idadi ya watoto wa aliyefariki, wa kike na wa kiume tunaweza kuwajulisha kila mmoja atarithi ngapi.



Na Allaah Anajua zaidi.
 
Amefariki Hana Wazazi Wala Mke Wala Watoto Anao Ndugu
Maswali: Mirathi
SWALI:



ASSALAAM ALAYKUM



AMEFARIKI HANA WAZAZI WALA MKE WALA WATOTO A-WALIO CHANGIA NA ALIYEFARIKI BABA NA MAMA NI WANAWAKE WATATU TU B-WALIO CHANGIA BABA TU NA ALIYEFARIKI NI MWANAUME MMOJA NA WANAWAKE WATATU.



JAZAAKUMULLAAH KHAIR - WABILLAAH TAWFIQ



Assalaam alaykum,


Nashukuru sana kwa kulitilia hima suala langu. Ningependa kujua jinsi ya kuigawa mali ya aliyefariki kwa wanandugu wanaostahiki kisheria kurithi mali ya kaka yao. Ikiwa ni fedha taslim pamoja na nyumba. Kama nilivyoelezea kuwa aliyefariki AMEACHA NDUGU WALIOCHANGIA MAMA NA BABA WATATU AMBAO NI WANAWAKE TU. Na amewacha NDUGU WA BABA MMOJA WANNE, KATI YAO MMOJA NI MWANAUME NA WATATU NI WANAWAKE. Natumai swali langu liko wazi.


Jazaakumullah khair wabillaah tawfiq



JIBU:





Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.





Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu Mirathi iliyoachwa na kaka aliyeaga dunia. Na hili swali tayari tutumelijibu hapo mbeleni na sijui kama jibu halikueleweka au vipi lakini naona ni kama vile awali isipokuwa limefafanua kuwa aliyefariki hana wazazi, mke wala watoto. Swali lako ni kuwa jamaa wa aliyaefariki waliobaki ni kama wafuatao:



1. Dada watatu shaqiqi (kwa baba na mama).

2. Dada watatu kwa baba, na

3. Kaka kwa baba tu.



Urithi wa jamaa wa aliyefariki ni kama katika jadwali ifuatayo:





Namba

Uhusiano na Aliyefariki

Mgao

1

Dada Shaqiqi 1

2/9 (22.222)

2

Dada Shaqiqi 2

2/9 (22.222)

3

Dada Shaqiqi 3

2/9 (22.222)

4

Dada kwa Baba 1

1/15 (6.667)

5

Dada kwa Baba 2

1/15 (6.667)

6

Dada kwa Baba 3

1/15 (6.667)

7

Kaka kwa Baba

2/15 (13.333)



JUMLA

1 (100)



Kwa vitu vilivyobaki vya kurithiwa ni nyumba na fedha taslimu alizoacha aliyefariki. Fedha taslimu zitagawanywa kulingana na mgao ulio hapo juu, ama nyumba itategemea wanavyoona warithi. Inaweza kuajirishwa, na ijara inayopatikana igawa kwa mgao kila mmoja haki yake, au inaweza kuuzwa na pesa kupatiwa kila mmoja anachostahiki au mwenye uwezo akainunua miongoni mwa ndugu kisha hizo fedha zilizopatikana kwa njia hiyo kuweza kugawiwa kila mmoja.



Ikiwa ni nyumba kubwa ambayo inaweza kugawiwa kila mmoja bila matatizo na kila mmoja akapata haki yake anayostahiki kutakuwa hakuna matatizo.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Amewaandikia Nyumba Watoto Wa Mke Wa Mwisho, Watoto Wa Mke Wa Mwanzo, Wanadai Mirathi Baada Ya Miaka 12
Maswali: Mirathi
SWALI:



A'aleykum. Mzee alikua na wake watatu. Mzee aliwaandikia nyumba watoto wa mke mwisho kwa sababu hawa watoto walikua wadogo na yeye mzee sana. Huu mwaka wa 12 wamekuja watoto wa mzee kudai haki yao kwenye hii nyumba. Je wanayo haki?

Tunaomba ushauri nini kifanyike ili amani ipatikane?







JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu Mirathi ya watoto kutoka kwa baba yao aliyeaga dunia.

Hakika ni makosa kwa mzazi kuacha wasiya nani arithi nini wakati anaaga dunia au kabla ya hapo. Mirathi kawaida kishari’ah haandikiwi chochote bali anapata kile kilichopangwa na Allaah Aliyetukuka. Wasiya mtu anaweza kumuandikia asiyerithi na haifai kuzidi thuluthi moja.



Ama katika kadhiya hii, inatakiwa mali iliyoachwa na mzee yatiwe thamani kisha yagawiwe kulingana na shari’ah ya Kiislamu. Mgao wa kila mmoja utategemea kama mzee huyo alikuwa na wazazi au la? Na wakati anaaga dunia alikuwa na wake wote watatu au wengine walikuwa wamekufa? Kulingana na uzee wa aliyefariki inaonekana kama hakuacha mzazi nyuma hata mmoja. Ikiwa wazazi wake watakuwa wapo hai mtatueleza. Ikiwa ni kama hivyo, basi mgao utakuwa kama ifuatavyo:



1. Mke au wake atapata au watapata thumuni (1/8). Ikiwa aliyebaki hai ni mmoja atapata thumuni na ikiwa wapo wote watatu watagawa hiyo thumuni.

2. Watoto watapata kilichobaki, mtoto wa kiume akipata sehemu mbili ilhali msichana akipata moja. Sasa inategemea aliacha watoto wangapi.



Inatakiwa kwa sasa waliobaki wafanye haki kwa kuigawa inavyotakiwa na Uislamu. Na wenye kufanya uadilifu huo watapata thawabu nyingi kutoka kwa Mola wao Mlezi. Ikiwa baadhi ya wake wameaga dunia au watoto wengine wamefariki, sehemu zao watagawiwa warithi wao.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Back
Top Bottom