Ramadhan Special Thread
Inafaa Kusoma Qur-aan Kwa Kutazama Musw-haf Katika Swalaah Za Sunnah?
Maswali: Qur-aan


Inafaa Kusoma Qur-aan Kwa Kutazama Musw-haf Katika Swalaah Za Sunnah?



Alhidaaya.com





SWALI:



Assalaam alaykum. My dear brothers.



My question is it possible to my Sunnah prayers, while reading the suwrah by holding the holly Qur'aan in my hand? I did not memorize those suwrah, I would like to know if it is possible.





Asslm alekum.

Niliuliza suali, kusoma Qur-aani katika swala kwa kushika kitabu mkononi kusoma suwrah,je inakubalika hilo, naomba jibu. Tafadhali, kwani mimi sijajua kusoma kwa moyo bado.

asanteni.









JIBU:





AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Hakika ni kuwa inajuzu kwa Muislamu kushika msahafu na kusoma kwayo akiwa anaswali Swalah za Sunnah bila ya tatizo lolote na hasa ikiwa ni Swalah ya usiku (kama Tahajjud) ambayo inahitajika kuwa ndefu kiasi.







Na Allaah Anajua zaidi
 
Ipi Bora Kuhifadhi Qur-aan Yote Bila Ya Kujua Maana Au Kuhifadhi Kidogo Kwa Maana?
Maswali: Qur-aan


Ipi Bora Kuhifadhi Qur-aan Yote Bila Ya Kujua Maana Au Kuhifadhi Kidogo Kwa Maana?



Alhidaaya.com







SWALI:



Assalam alaykum warahmatuLLaahi wabarakatuhu. Nataka nipate ufumbuzi kuhufadhi Quran ni kusoma zwahiri, au nikuhifadhi bila ya kujuwa maana yake au ni kuhifadhi na maana yake? Kwa sababu nilisikia kama mtu akihifadhi Quran hataingiya motoni.



Na nani kahifadhi kati ya yule anasoma Quran yote bila kuifaham maana yake na yule anae juwa sura kumi na maana yake? Barakallahu fikum wasalam alaykum warhamatullahi wa Barakatuhu





JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Hakika ambayo haipingiki na yeyote mwenye akili timamu ni kuwa Qur-aan imeteremshwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kutimiza malengo fulani kwa wana Aadam. Lengo kubwa zaidi ni kuwaongoza watu wote katika njia nyoofu na ya sawa kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ

Mwezi wa Ramadhwaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na pambanuo (la haki na batili). [Al-Baqarah: 184]





na hivyo hivyo kwa wenye taqwa kama Anavyosema pia Allaah ('Azza wa Jalla):



ذَٰلِكَ الْكِتَابُ لَا رَيْبَ ۛ فِيهِ ۛ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٢﴾

Hiki ni Kitabu kisicho na shaka ndani yake, ni mwongozo kwa wenye taqwa [Al-Baqarah: 2]





Kwa minajili hiyo ni bora na muhimu zaidi kwa Muislamu kuisoma Qur-aan kwa kuizingatia maana yake pamoja na kufuata kimatendo yaliyomo ndani. Hivyo ndivyo walivyokuwa wakifanya Wema waliotangulia. Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhuma) alikuwa akisoma Aayah kumi, anazihifadhi na kutekeleza kimatendo maagizo yaliyomo ndani yake. Kwa njia hiyo alichukua miaka kumi kuihifadhi Suwratul-Baqarah [Maalik].





Maswahaba nao ndivyo walivyokuwa wakifanya walikuwa hawachukui Aayah nyengine hata kama zimeteremka siku hiyo mpaka zile walizokuwa nazo kuzihifadhi pamoja na kutwabikisha amri zilizomo ndani.



Japokuwa kuhifadhi Qur-aan kuna fadhila zake, na kila unaposoma herufi utapata thawabu kumi, lakini henda mtu akawa anasoma Qur-aan na huku inamlaani lakini hajui wala hatambui hilo.



Pia sisi hatutakiwi tuwe na ile sifa ya Mayahudi kama Anavyosema Allaah ('Azza wa Jalla):





مَثَلُ الَّذِينَ حُمِّلُوا التَّوْرَاةَ ثُمَّ لَمْ يَحْمِلُوهَا كَمَثَلِ الْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًا ۚ بِئْسَ مَثَلُ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴿٥﴾

Mfano wa wale waliobebeshwa Tawraat, kisha wasiibebe ni kama mfano wa punda abebaye mijalada ya vitabu. Ubaya ulioje mfano wa watu waliokadhibisha Aayaat za Allaah, na Allaah Haongoi watu madhalimu. [Al-Jumu’ah: 5]





Udhalimu unakuwa mkubwa ikiwa tutaibeba Qur-aan vifuani mwetu lakini hatuitilii maanani. Ndipo Allaah ('Azza wa Jalla) Anasema:



أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآنَ أَمْ عَلَىٰ قُلُوبٍ أَقْفَالُهَا﴿٢٤﴾

Je, hawaizingatii Qur-aan; au nyoyoni (mwao) mna kufuli? [Muhammad: 24]



Nasiha zetu za dhati kwa ndugu zetu ni kuwa mtu asome juzuu au hizbu au hata ukurasa mmoja wa Qur-aan kila siku bila kuacha pamoja na kufanya bidii kuhifadhi Suwrah au baadhi za Aayah anazoweza. Hivyo hivyo atenge wakati wa kusoma Tafsiyr kuanzia mwanzo wa Suwratul-Faatihah kidogo kidogo na kufanya juhudi kutekeleza hayo kimatendo.



Na Allah Anajua zaidi
 
Je, بسم الله (BismiLLaah) Inahesabika Kuwa Ni Aayah Katika Suwratul Faatihah?
Maswali: Qur-aan


Je, بسم الله (BismiLLaah) Inahesabika Kuwa Ni Aayah Katika Suwratul Faatihah?



Alhidaaya.com



SWALI:



Assalamu Aleykum Warahmatullahi Wabarakatu, Swali Langu Ni Hili Katika Suwrah Nyingine Zote Tunapata Kuwa Bismillahi Rahmani Rahim Ndio Utangulizi Au Ndio Ufunguzi Wa Suwrah Lakini Katika Suwrah Faatihah 'bismillahi Rahmani Rahim' Imekuwa Kama Aayah Ya Kwanza Ya Suwrah 'Faatihah' Naomba Ufafanuzi Kutoka Kwenu, Jee Bismillahi Rahmani Rahim Ile Katika Suwrah 'Al-Faatihah' Na Zile Bismillahi Rahmani Rahim Nyingine Katika Zile Suwrah Nyingine Tafauti Yake Ni Nini? Shukran Wa Jazakallah Kher.









JIBU:





AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu Bismillaahi ar-Rahmanir Rahiym katika Suwrah Faatihah na Suwrah nyinginezo. Kuhusu suala hilo kuna tofauti baina ya wanachuoni na kila mmoja ana dalili zake kuhusu hilo:



Mwanzo ni kuwa wanazuoni wamekubaliana kuwa al-basmalah (BismiLlaahir Rahmaanir Rahiym) iliyopo katika Surawh Naml (27) kuwa ni sehemu ya Aayah katika kauli Yake Aliyetukuka:



إِنَّهُ مِن سُلَيْمَانَ وَإِنَّهُ بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ ﴿٣٠﴾

30. Hakika hiyo ni kutoka kwa Sulaymaan, na hakika hiyo (imeanza) Kwa Jina la Allaah, Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu. [An-Naml: 30]



Na haihesabiwi kuwa ni mwanzo wa Aayah ya Suwrah hiyo, na kuisoma mwanzo wa Suwrah hiyo ni Makruuh.



Hata hivyo, wanachuoni wametofautiana kama al-basmalah ni Aayah katika Suwrah Faatihah na katika mwanzo wa kila Suwrah au la? Kauli za wanachuoni katika hilo ni kama zifuatazo:



1. Hiyo ni Aayah katika Suwrah Al-Faatihah na kila Suwrah katika kila Surah isipokuwa Bara’ah (Suwrah Tawbah). Na hiyo Madh-hab ya Imaam Ash-Shaafi'iy, Ath-Thawriy, Ibnul Mubaarak na kundi la wanachuoni.



2. Si Aayah katika Suratul Faatihah wala Surah nyingine yoyote katika Qur-aan. Na hiyo ni kauli ya Imaam Maalik, Al-Awzaa’iy na moja ya riwaya kutoka kwa Imaam Ahmad (Ingawa kuna mashaka kuhusu usahihi wa hiyo riwaya kutoka kwa Imaam Ahmad kama ilivyotajwa katika Al-Muhadhab).





3. Hiyo ni Aayah kamili katika Suwrah Al-Faatihah na si katika Suwrah zingine. Hii ni kauli ya Is-haaq, Abu ‘Ubayd na riwaya moja kutoka kwa Imaam Ahmad.





4. Si Aayah katika Suwrah Al- Faatihah wala mwanzo wa Suwrah nyinginezo, bali ni Aayah kitenganishi baina ya Suwrah. Na hiyo ni kauli ya Madh-hab ya Imaam Abu Haniyfah na ndio kauli sahihi katika madh-hab ya Imaam Ahmad.



Rai hii ya nne, ameielezea Shaykhul Islaam Ibn Taymiyah kuwa ni rai au maelezo yaliyo ya kati kwa kati katika maelezo yote yaliyotangulia.



Na inayoonekana ni kuwa kauli ya Abu Haniyfah ina nguvu zaidi.



Ama kusoma al-basmalah katika Swalah, wanachuoni pia wametofautiana kwa kauli zifuatazo:





1. Imaam Maalik amekataza kusoma al-basmallah katika Swalah za Faradhi, kwa sauti au kawa siri. Hilo halifai kufanywa katika ufunguzi wa Suwrah Al-Faatihah wala Suwrah nyingine. Na amejuzisha kusomwa katika Swalah za Sunnah.



2. Imaam Abu Haniyfah naye amejuzisha kuisoma kwa siri pamoja na al-Faatihah katika kila Rak'ah ya Swalah, na ikiwa ataisoma pamoja na kila Suwrah itakuwa vyema.





3. Ama Imaam ash-Shaafi'iy, ni wajibu kwa mwenye kuswali kuisoma, ikiwa kwa sauti aisome kwa sauti na ikiwa ni Swalah ya siri basi kwa siri.





4. Na Imaam Ahmad bin Hanbal naye amesema, anafaa mwenye kuisoma aisome kwa siri na haifai kuijihirisha kabisa.



Hakika ni kuwa Suwrah Al-Faatihah ina Aayah saba peke yake na katika hilo wametofautiana wanachuoni kuhusu ni ipi Aayah ya mwanzo. Wengine wamesema bismiLLaah ni Aayah na wengine wameona sio.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Kuandika Aayah Za Qur-aan Katika Ukuta
Maswali: Qur-aan




Kuandika Aayah Za Qur-aan Katika Ukuta



Alhidaaya.com







SWALI:



Assalama alaekum wa Rahmatu llahi wa barakatu.



Swali jee inafaa kuandika aya za Quraan katika ukuta wa nyumba compound wall.



JIBU:





AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Hebu tulitazame swali hili kwa makini. Je, hizi Aayah ambazo zitaandikwa kwenye ukuta wa nyumba zimeandikwa kwa lengo gani? Ikiwa lengo ni kuondoa hasadi, au urogi, au kuwa kama kinga kutokana na mashaytwaan hilo litakuwa halifai kwani kuondoa hayo yote Aayah zinatakiwa zisomwe sio kuandikwa. Na kufanya hivyo kutampelekea mtu katika ushirikina.



Inatakiwa tuelewe na kufahamu kuwa Qur-aan haikuletwa kutundikwa nyumbani au kuandikwa ukutani bali kusomwa na kuongoza wanaadamu. Hivyo, inatakiwa iwe katika vifua vya watu pamoja na kutiwa katika matendo ya wanaadamu ili wapate ufanisi hapa duniani na Kesho Aakhirah. Allaah ('Azza wa Jalla) Anasema:



ذَٰلِكَ الْكِتَابُ لَا رَيْبَ ۛ فِيهِ ۛ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٢﴾

Hiki ni Kitabu kisicho na shaka ndani yake, ni mwongozo kwa wenye taqwa [Al-Baqarah: 2]





Na Anasema pia Allaah ('Azza wa Jalla):



شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ

Mwezi wa Ramadhwaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na pambanuo (la haki na batili). [Al-Baqarah: 185]





Kwa hiyo, Qur-aan inatakiwa iwapatie uongofu Waumini na hilo halitopatikana kwa kuandika Aayah kwenye kuta bali kusomwa, kuifahamu na kufuata maagizo yake pamoja na kuacha makatazo yaliyo ndani. Na kwa wanaadamu wengine pia ni lazima waisome ndio wapate uongofu, Aayah ambazo ni chache zilizoandikwa katika ukuta hazitowafaidisha bali itakuwa ni kuzifanyia Aayah hizo mzaha na hilo halifai.





Wengine utakuta wanatoa hoja dhaifu kuwa kuwekwa Aayah ukutani kunamkumbusha mtu Qur-aan! Lakini je, kumkumbusha huko kuisoma Qur-aan ni kwa kwa pale tu anapoiona na akirudi kwake au akienda kwengine husahaulika. Muumin, mwenye imani ya kweli huisoma Qur-aan kila siku na haihitajii kukumbushwa na Qur-aan za kutani.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Kuhusu Zabuwr, Tawraat, Injiyl Na Qur-aan

Alhidaaya.com







SWALI:



Assalam Aleikum,



1- Kitabu cha mwisho kushuka ni Qur´ani cha kwanza kilikuwa Biblia au vipi?



2- Nifahamisheni maana ya Taurati, Injili na Zaburi na kazi zake?



3- Nini maana ya Agano la kale na Agano Jipya?









JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Tufahamu kuwa Biblia si kitabu kitakatifu kama wanavyofahamu wengi miongoni mwa Waislamu wa kawaida. Biblia imetokana na neno Biblos, ambalo ni neno la Kigirki lemye maana ya mkusanyiko wa Vitabu. Katika Biblia utapata maneno ya Allaah Aliyetukuka yaliyobaki katika usahihi wake, kauli za Rusuli (‘Alayhim-Salaam) na maneno ya watu wasiojulikana. Na yapo maneno mengi yaliyozuliwa ambayo hayawezi kuwa maneno ya Allaah wala Mitume.



Kitabu cha kwanza kuteremshwa ni kile alichopewa Nabii Ibraahiym (‘Alayhis Salaam). Allaah Aliyetukuka Anasema:

صُحُفِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ ﴿١٩﴾

Maandiko tukufu ya Ibraahiym na Muwsaa. [Al-A'laa: 19]



Tawraat ni kitabu alichoteremshiwa Nabiy Muwsaa (‘Alayhis-salaam) kilichokuwa na amri kumi. Ama Injiyl ni habari njema, nacho ni kitabu alichoteremshiwa na Allaah Aliyetukuka Nabiy ‘Iysa (‘Alayhis-salaam) ama maana ya Zabuwr ni nyimbo na maombi. Hicho ni kitabu alichoteremshiwa Nabii Daawuud (‘Alayhis-salaam). Kazi za vitabu vyote ambavyo kwa sasa vimepotea katika mfumo wake wa kiasili ni kuwaongoza Bani Israili katika kumjua na kufuata maamrisho ya Allaah Aliyetukuka pamoja na kuwa na maadili mema hapa duniani ili kupata ufanisi Kesho Aakhirah.



Ama maana ya Agano la kale kwa Wakristo ina maana vile vitabu vya kale kabla ya kuja kwa ‘Iysa mwana wa Maryam katika Biblia. Vitabu vyenyewe vinaanza kitabu cha Mwanzo hadi Malaki. Ilhali Agano Jipya ni vitabu vinavyosimulia kuhusu Yesu pamoja na barua ambazo wafuasi Wakristo waliokuwa wakiandikiana. Hivi ni vitabu ambavyo vipo katika Biblia inayofuatwa na Wakristo, hata hivyo Mayahudi hawaiamini Agano hiyo mpya. Vitabu vyenyewe vinaanza kuanzia Injili kama ilivyoandikwa na Mathayo hadi Ufunuo.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Kujifunza Tajwiyd Kwa Kufuatilia Wasomaji
Maswali: Qur-aan





Kujifunza Tajwiyd Kwa Kufuatilia Wasomaji



Alhidaaya.com





SWALI:



Nawashukuru sana kwa kuweza kutusaidia kujibu majibu yetu na inshaAllaah jaza yenu iko kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Mimi ni miongoni wa wanafunzi niliosoma Quraan zamani sana. Na wakati ule tulikuwa tunasomeshwa tu, hatujui wapi katika harufu, kunavutwa, wapi kuna kikomo, n.k. Sikama sasa ambapo wanafunzi wanafundishwa sawa sawa.

Si mlaumu mtu kwa hili na namshukuru mwalimu wangu wa mwanzo kunifundisha mimi Quraan na jaza yake iko kwa Allaah na Mungu amrehemu na amuweke penye wema (Amin) Sasa mimi hujaribu kusikiza na kufuata quran inaposomwa na masheikh kwenye CDS, ili nipate kujua wapi kunavutwa, shadda n.k na alhamdullillah nime improve sana. Je ninafanya sawa kufanya hivi ama mutanipa ushauri gani?

Jakaza Allaah







JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.







Bila shaka unafaa upongezwe kwa juhudi nasi tunakuombea ufanikiwe na uwe ni mwenye kuisoma Qur-aan kwa njia iliyo bora zaidi.



Hakika zipo njia na mbinu nyingi za kujifunza Qur-aan. Mojawapo ni hiyo ambayo unaitumia kwa kufuatanisha msomi.



Hata hivyo, tungekunasihi upate mtu ambaye ni mjuzi wa Tajwiyd na kusoma Qur-aan awe anakusikiliza kadiri itakavyowezekana. Hiyo ni kuwa katika kufuatanisha inakuwa ni rahisi na yenye ufanisi zaidi kuliko mtu kusoma Qur-aan peke yake kwani si rahisi kuyajua makosa yake anapokosea.



Kujifunza Qur-aan ni muhimu sana na hata ikikubidi kuigharamia basi fanya hivyo. Na elimu hiyo yahitaji mazoezi sana na marudio ya kila mara, hivyo usiache kufanya hivyo unapojifunza.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Kujikinga Na Shaytwaani Katikati Ya Surah Unaposoma Qur-aan
Maswali: Qur-aan



Kujikinga Na Shaytwaan Katikati Ya Suwrah Unaposoma Qur-aan



Alhidaaya.com







SWALI:



Je, ikiwa unasoma Qur-aan na umeanza katikati ya sura inafaa kusema A'udhu BiLLaahi mina-shaytaanir-rajiym







JIBU



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.







Ni sawa kabisa kuanza kusoma Qur-aan kwa



أَعـوذُ بِاللهِ مِنَ الشَّيْـطانِ الرَّجيـم





Ikiwa ni katikati ya Suwrah kwani tumeamrishwa kufanya hivyo mtu anapoanza kusoma Qur-aan kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



فَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ﴿٩٨﴾

Unaposoma Qur-aan basi (kwanza) omba kinga kwa Allaah dhidi ya shaytwaan aliyetokomezwa mbali na kulaaniwa. [An-Nahl: 98]





Unaweza pia kuongezea na

بِسْمِ اَللَّهِ اَلرَّحْمَنِ اَلرَّحِيمِ



BismiLLaahir-Rahmaanir-Rahiym



hata kama ni katikati ya Suwrah. Na kama ni mwanzo wa Suwrah basi uanze na



أَعـوذُ بِاللهِ مِنَ الشَّيْـطانِ الرَّجيـم . بِسْمِ اَللَّهِ اَلرَّحْمَنِ اَلرَّحِيمِ



Isipokuwa Suwrah At-Tawbah ambayo inaanzwa kwa

أَعـوذُ بِاللهِ مِنَ الشَّيْـطانِ الرَّجيـم



bila ya kusema

بِسْمِ اَللَّهِ اَلرَّحْمَنِ اَلرَّحِيمِ







Na Allaah Anajua zaidi
 
Kulia Wakati Wa Kusoma Qur-aan Kunamaanisha Nini?
Maswali: Qur-aan



Kulia Wakati Wa Kusoma Qur-aan Kunamaanisha Nini



Alhidaaya.com



SWALI:



Ningependa kuuliza swali kuhusu quran,unaposoma na ukawa unalia je nini?maana yake ni nini?







JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Unaposoma Qur-aan ukalia, bila shaka ni nyongeza ya iymaan katika moyo wa msomaji, kwani hayo ni maneno ya Allaah ('Azza wa Jalla), maneno ambayo nafsi zilimtambua kabla ya kuumbwa duniani na kumuitikia kuwa zitamtii. Dalili ya kuwa ni iymaani ni kutoka katika Qur-aan na Sunnah.



Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّـهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ﴿٢﴾

Hakika Waumini ni wale ambao Anapotajwa Allaah, nyoyo zao zinajaa khofu na wanaposomewa Aayaat Zake huwazidishia iymaan, na kwa Rabb wao wanatawakali. [Al-Anfaal:4]





Vile vile Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَإِذَا مَا أُنزِلَتْ سُورَةٌ فَمِنْهُم مَّن يَقُولُ أَيُّكُمْ زَادَتْهُ هَـٰذِهِ إِيمَانًا ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا فَزَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَهُمْ يَسْتَبْشِرُونَ﴿١٢٤﴾

Na inapoteremshwa Suwrah, basi miongoni mwao wako wanaosema: Nani kati yenu imemzidishia (Suwrah) hii iymaan? Ama wale walioamini huwazidishia iymaan nao wanafurahia. [At-Tawbah:124]



Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwamba kuzidishiwa Iymaan hiyo ni Hidaaya kutoka Kwake.



اللَّـهُ نَزَّلَ أَحْسَنَ الْحَدِيثِ كِتَابًا مُّتَشَابِهًا مَّثَانِيَ تَقْشَعِرُّ مِنْهُ جُلُودُ الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُمْ ثُمَّ تَلِينُ جُلُودُهُمْ وَقُلُوبُهُمْ إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ هُدَى اللَّـهِ يَهْدِي بِهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِنْ هَادٍ ﴿٢٣﴾

Allaah Ameteremsha kauli nzuri kabisa, Kitabu; zinazoshabihiana ibara zake, zenye kukaririwa kila mara, zinasisimua kwazo ngozi za wale wanaomkhofu Rabb wao, kisha zinalainisha ngozi zao na nyoyo zao katika kumdhukuru Allaah. Huo ndio mwongozo wa Allaah Humwongoza kwao Amtakaye. Na ambaye Allaah Amempotoa basi hana wa kumuongoa. [Az-Zumar: 23]





Kama tunavyoona katika Aayah hiyo tukufu, kwamba kusoma Qur-aan husisimua ngozi na kutia khofu nyoyo na kuulainisha hadi imsababishe mja kutokwa machozi. Na aghalabu humtokea mja mwema khaswa mwenye elimu ya Qur-aan anapofahamu na kutadabari (kuzingatia).



Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amewasifia waja hao wanaotokwa machozi pindi wanaposoma au kusikiliza Aayah Zake, huzidishiwa iymaan, khofu, unyenyekevu na hulia na huporomoka kuliakumsujudia Allaah :



قُلْ آمِنُوا بِهِ أَوْ لَا تُؤْمِنُوا ۚ إِنَّ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ مِن قَبْلِهِ إِذَا يُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ يَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ سُجَّدًا ﴿١٠٧﴾

Sema: Iaminini au msiamini. Hakika wale waliopewa elimu kabla yake wanaposomewa (Qur-aan) wanaporomoka kifudifudi wanasujudu.



وَيَقُولُونَ سُبْحَانَ رَبِّنَا إِن كَانَ وَعْدُ رَبِّنَا لَمَفْعُولًا ﴿١٠٨﴾

Na wanasema: Utakasifu ni wa Rabb wetu; hakika ahadi ya Rabb wetu lazima itimizwe.



وَيَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ يَبْكُونَ وَيَزِيدُهُمْ خُشُوعًا ۩﴿١٠٩﴾

Na wanaporomoka kifudifudi huku wanalia na inawazidishia unyenyekevu. [Al-Israa: 107-109]



Ndio maana vile vile Anatuambia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) inaposomwa Qur-aan tuwe tunaisikiliza ili tuifahamu na tupate Rahma Yake:



وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٢٠٤﴾

Na inaposomwa Qur-aan, basi isikilizeni kwa makini na bakieni kimya (mzingatie) ili mpate kurehemewa. [Al-A'raaf:204]



Na Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipomuomba Swahaba 'Abdullaah bin Mas'uwd (Radhwiya-Allaahu ‘anhu) amsomee Qur-aan, akamsomea hadi alipofika Aayah fulani, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akatokwa na machozi:





عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه قال: قال لي النبي صلى الله عليه وسلم ((اقرأ علي)) قلت: يا رسول الله، أقرأ عليك وعليك أُنزلَ؟ قال: ((نعم، إني أحب أن أسمعه من غيري)) فقرأت سورة النساء، حتى أتيت إلى هذه الآية: (( فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِنْ كُلِّ أُمَّةٍ بِشَهِيدٍ وَجِئْنَا بِكَ عَلَى هَؤُلاءِ شَهِيدًا )) قال: ((حسبك الآن)) فإذا عيناه تَذْرِفَان.


Amesimulia ‘Abdullaah bin Mas‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ) aliniambia: “Nisomee!”. Nikamwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Nikusomee na hali (Qur-aan) imeteremshwa kwako? Akasema: “Naam! Lakini mimi napenda kusikia wengine wakiisoma.” Nikasoma Suwratun-Nisaa mpaka nilipofikia Aayah:



فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِن كُلِّ أُمَّةٍ بِشَهِيدٍ وَجِئْنَا بِكَ عَلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ شَهِيدًا ﴿٤١﴾

“Basi itakuwaje Tutakapoleta kutoka kila ummah shahidi, na Tukakuleta (ee Muhammad صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ) kuwa shahidi juu ya hawa?”



Akasema: “Hasbuka! (Inatosha, simama hapo).” Nikaona machozi yamejaa machoni mwake. [Al-Bukhaariy]





Muumini anapolia pindi anaposoma Qur-aan akiwa peke yake na akatokwa na machozi, pia ni bishara ya kwamba yeye atakuwa miongoni mwa watu saba waliotajwa kuwa watakuwa katika kivuli cha Allaah Siku ya Qiyaamah, siku ambayo hakutakuweko kivuli ila kivuli cha Allaah kama alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):





عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ ((سَبْعَةٌ يُظِلُّهُمْ اللَّهُ فِي ظِلِّهِ يَوْمَ لا ظِلَّ إِلا ظِلُّهُ: الإِمَامُ الْعَادِلُ، وَشَابٌّ نَشَأ فِي عِبَادَةِ رَبِّهِ، وَرَجُلٌ قَلْبُهُ مُعَلَّقٌ فِي الْمَسَاجِدِ، وَرَجُلَانِ تَحَابَّا فِي اللَّهِ اجْتَمَعَا عَلَيْهِ وَتَفَرَّقَا عَلَيْهِ، وَرَجُلٌ طَلَبَتْهُ امْرَأَةٌ ذَاتُ مَنْصِبٍ وَجَمَالٍ فَقَالَ إِنِّي أَخَافُ اللَّهَ، وَرَجُلٌ تَصَدَّقَ بِصَدَقَةٍ فَأَخْفَاهَا حَتَّى لا تَعْلَمَ شِمَالُهُ مَا تُنْفِقُ يَمِينُهُ، وَرَجُلٌ ذَكَرَ اللَّهَ خَالِيًا فَفَاضَتْ عَيْنَاهُ)) متفق عليه



Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Watu saba Allaah Atawafunika katika kivuli Chake, Siku ambayo hakutokuwa na kivuli ila kivuli Chake: (i) Imaam (kiongozi) muadilifu. (ii) Kijana ambaye amekulia katika ibaada ya Rabb wake. (iii) Mtu ambaye moyo wake umeambatana na Misikiti (iv) Watu wawili wanaopendana kwa ajili ya Allaah; wanakutana kwa ajili Yake na wanafarikiana kwa ajili Yake. (v) Mwanamme aliyetakwa na mwanamke mwenye hadhi na mrembo wa kuvutia akasema: Mimi namkhofu Allaah! (vi) Mtu aliyetoa swadaqa yake akaificha hadi kwamba mkono wake wa kushoto usijue nini ulichotoa mkono wake wa kulia. (vii) Mtu aliyemdhukuru Allaah kwa siri macho yake yakatokwa machozi.” [Al-Bukhaariy, Muslim]









Kwa hivyo ndugu yetu tunakupa bishara njema na tunakuombea Allaah Akuzidishie iymaan na taqwa.



Na Allah Anajua zaidi
 
Hikmah Ya Kuteremshwa Qur-aan Kidogo Kidogo Wakati Mbali Mbali



Alhidaaya.com







Qur-aan ni kitabu cha mwisho kilichoteremshwa na Allaah (سبحانه وتعالى), ni Mwongozo kamili kwa walimwengu wote duniani, kwa hiyo Qur-aan ni tofauti na vitabu vinginevyo ambavyo viliteremshwa kwa kaumu fulani au mataifa fulani kama mfano Tawraat imeteremshwa kwa Nabiy Muwsaa na watu wake Bani Israaiyl na Injiyl kwa Nabiy 'Iysaa na wafuasi wake.





Tofauti nyingine baina ya vitabu hivyo na Qur-aan ni kwamba Vitabu vilotangulia, vimeteremshwa kwa mteremsho mmoja. Ama Qur-aan haikuteremshwa mara moja ikawa kamilifu, bali imeteremshwa kidogo kidogo kwa wakati mbali mbali ima bila ya kutokea tukio au kwa kutokea matukio. Imeteremshwa kama ni Wahy (ufunuo) katika moyo wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).



Hikma za kuteremshwa Qur-aan ni nyingi miongoni mwazo ni zifuatazo:





Hikma Ya Kwanza: Kuwasahilishia Swahaba Hukmu Za Makatazo Ya Maasi Waliyokuwa Nayo Katika Ujaahiliyyah:





Moja ya hikma ni kwamba kwa sababu ya kuwavutia watu kuingia katika Dini kwa kufuata maamrisho yake na makatazo yake polepole, na hii ni njia itumikayo na yenye matunda katika da'wah. Kwani ingelikuwa ni kufuata makatazo yote na kufuata maamrisho yote kwa pamoja, basi ingelikuwa ni vigumu sana watu kufuata, na ndio maana kwa muda wa miaka kumi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuwa Makkah hakukuwa na zaidi ya kuwaita watu kuingia katika Dini, neno la ‘Laa ilaah illa Allaah’, ndilo lililokuwa lengo, hakukuwa na amri za fardhi yoyote wala hukmu zozote.



Mfano, makatazo ya ulevi, kwa vile ulevi ulikuwa ni moja ya maasi makuu na hata baada ya kuja Uislamu, baadhi ya Swahaba walikuwa bado wakilewa. Hii ni kwa sababu ilikuwa ni ada na desturi zao walizozirithi katika ujaahiliyyah kama zilivyo desturi nyinginezo walizokuwanazo mfano kuwaua watoto wa kike, kuwanyima urithi wanawake n.k. Ukaja Uislamu na kuondosha dhulma zote hizo. Hivyo jambo kama ulevi lilihitajika hikma ya kuukataza kwa polepole na ndio maana tunaona kwamba kuna Aayah tatu zinazohusiana na makatazo ya ulevi ilianza kwanza kwa kutaja madhara yake na manufaa yake, kisha polepole hadi kukataza kabisa.



Hadiyth ifuatayo imethibiti hayo:



حَدَّثَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ مُوسَى، أَخْبَرَنَا هِشَامُ بْنُ يُوسُفَ، أَنَّ ابْنَ جُرَيْجٍ، أَخْبَرَهُمْ قَالَ وَأَخْبَرَنِي يُوسُفُ بْنُ مَاهَكَ، قَالَ إِنِّي عِنْدَ عَائِشَةَ أُمِّ الْمُؤْمِنِينَ ـ رضى الله عنها ـ إِذْ جَاءَهَا عِرَاقِيٌّ فَقَالَ أَىُّ الْكَفَنِ خَيْرٌ قَالَتْ وَيْحَكَ وَمَا يَضُرُّكَ قَالَ يَا أُمَّ الْمُؤْمِنِينَ أَرِينِي مُصْحَفَكِ‏.‏ قَالَتْ لِمَ قَالَ لَعَلِّي أُوَلِّفُ الْقُرْآنَ عَلَيْهِ فَإِنَّهُ يُقْرَأُ غَيْرَ مُؤَلَّفٍ‏.‏ قَالَتْ وَمَا يَضُرُّكَ أَيَّهُ قَرَأْتَ قَبْلُ، إِنَّمَا نَزَلَ أَوَّلَ مَا نَزَلَ مِنْهُ سُورَةٌ مِنَ الْمُفَصَّلِ فِيهَا ذِكْرُ الْجَنَّةِ وَالنَّارِ حَتَّى إِذَا ثَابَ النَّاسُ إِلَى الإِسْلاَمِ نَزَلَ الْحَلاَلُ وَالْحَرَامُ، وَلَوْ نَزَلَ أَوَّلَ شَىْءٍ لاَ تَشْرَبُوا الْخَمْرَ‏.‏ لَقَالُوا لاَ نَدَعُ الْخَمْرَ أَبَدًا‏.‏ وَلَوْ نَزَلَ‏.‏ لاَ تَزْنُوا‏.‏ لَقَالُوا لاَ نَدَعُ الزِّنَا أَبَدًا‏.‏


Ametuhadithia Ibraahiym bin Muwsaa, ametujulisha Hishaam bin Yuwsuf, kwamba Ibn Jurayj amewajulisha amesema: Amesema au amenijulisha Yuwsuf bin Maahak kuwa alipokuwa pamoja na ‘Aaishah Mama wa Waumini (رضي الله عنها), mara akaja kwake mtu kutoka Iraaq, akamuuliza: Ni kafani (sanda) gani iliyo bora zaidi? Akasema (رضي الله عنها): Allaah Akurehemu! Itakusaidia nini kujua hilo (ukiwa maiti sanda yoyote utakafiniwa nayo)?! Akasema: Ee Mama wa Waumini, nionyeshe Mswahafu wako. Akasema (رضي الله عنها): Kwa nini? Akasema: Huenda nikaukusanya na kuipanga Qur-aan kulingana nayo, kwani watu wanaisoma pamoja na Suwrah zake sio kwa mpangilio wa sawasawa. Akasema (رضي الله عنها): Haijalishi ni sehemu gani unayosoma mwanzo. (Fahamu kuwa) kitu cha kwanza kuteremshwa kwayo ni Suwrah za al-Mufaswswal (fupi fupi) ambazo kumetajwa ndani yake Jannah na Moto. Na watu wanapokuwa wamekomaa na nafsi zao kutulia juu ya hilo, Aayah kuhusiana na halali na haramu ziliteremshwa. Na lau ingeteremshwa mwanzo (kwa mfano): “Msinywe pombe (mvinyo)”, watu wangesema: “Hatutaacha kunywa (pombe)”. Na lau kungeteremshwa: “Msizini”, watu wangesema: “Hatutaacha kuzini”. [Al-Bukhaariy]



'Umar ibn Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه) ambaye alikuwa mmoja wa Swahaba aliyekuwa akilewa, aliomba hukmu kuhusu pombe alisema: “Ee Allaah tubainishie kuhusu pombe bainisho la kuridhisha.” Ikateremshwa:



سْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَا أَكْبَرُ مِن نَّفْعِهِمَا ۗ

Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema: “Katika viwili hivyo mna dhambi kubwa na (baadhi ya) manufaa kwa watu. Na dhambi yake viwili hivyo ni kubwa kuliko manufaa yake.” [Al-Baqarah: 219]



Wakaendelea kunywa pombe hadi siku moja katika Swalaah, Swahaba mmoja alikosea kusoma Suwratul-Kaafiruwn basi hapo ikateremshwa Aayah:



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنتُمْ سُكَارَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا مَا تَقُولُونَ

Enyi walioamini! Msikaribie Swalaah na hali mmelewa mpaka mjue mnayoyasema, [An-Nisaa: 43]



Wakaacha kulewa nyakati za Swalaah na wakaendelea nyakati nyingine hadi kukatokea maovu mengine ndipo 'Umar (رضي الله عنه) akasema tena: “Ee Allaah! Tupe Aayah iliyo wazi kabisa kuhusu Al-Khamr (pombe). Ndipo Aayah ya mwisho kuhusu makatazo ya ulevi ikateremshwa [Tafsiyr ibn Kathiyr] ambayo ni:



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٩٠﴾ إِنَّمَا يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُوقِعَ بَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ فِي الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ وَعَنِ الصَّلَاةِ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّنتَهُونَ ﴿٩١﴾

Enyi walioamini! Hakika pombe na kamari na masanamu na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli; ni najisi na chukizo kutokana na kitendo cha shaytwaan; basi jiepusheni navyo, mpate kufaulu. Hakika shaytwaan anataka kukutilieni baina yenu uadui na bughudha katika pombe na kamari na akuzuieni na kumdhukuru Allaah na (akuzuieni pia) Swalaah; basi je mtakoma? [Al-Maaidah: 90 – 91]



Basi ‘Umar (رضي الله عنه) akasema: “Tumekoma.”



Maelezo ya Hadiyth kama ilivyothibiti:



عَنْ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ، قَالَ لَمَّا نَزَلَ تَحْرِيمُ الْخَمْرِ قَالَ عُمَرُ: اللَّهُمَّ بَيِّنْ لَنَا فِي الْخَمْرِ بَيَانًا شِفَاءً ، فَنَزَلَتِ الآيَةُ الَّتِي فِي الْبَقَرَةِ: ((‏يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ)) الآيَةَ قَالَ: فَدُعِيَ عُمَرُ فَقُرِئَتْ عَلَيْهِ، قَالَ: اللَّهُمَّ بَيِّنْ لَنَا فِي الْخَمْرِ بَيَانًا شِفَاءً، فَنَزَلَتِ الآيَةُ الَّتِي فِي النِّسَاءِ: ((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لاَ تَقْرَبُوا الصَّلاَةَ وَأَنْتُمْ سُكَارَى))‏ فَكَانَ مُنَادِي رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا أُقِيمَتِ الصَّلاَةُ يُنَادِي: أَلاَ لاَ يَقْرَبَنَّ الصَّلاَةَ سَكْرَانُ، فَدُعِيَ عُمَرُ فَقُرِئَتْ عَلَيْهِ فَقَالَ: اللَّهُمَّ بَيِّنْ لَنَا فِي الْخَمْرِ بَيَانًا شِفَاءً فَنَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ: ((‏فَهَلْ أَنْتُمْ مُنْتَهُونَ))‏ قَالَ عُمَرُ: انْتَهَيْنَا.‏

Imepokelewa kutoka kwa ‘Umar bin Al-Khattwaab (رضي الله عنه) kwamba ilipoharamishwa pombe alisema ‘Umar: Ee Allaah tubainishie kuhusu pombe bainisho la kuridhisha.” Hapo ikateremshwa Aayah katika Suwratul-Baqarah:

‏يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ

Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema: “Katika viwili hivyo mna dhambi kubwa.



[Al-Baqarah 2: 219] Akaitwa ‘Umar akasomewa. Kisha akasema: “Ee Allaah tubainishie kuhusu pombe bainisho la kuridhisha.” Kisha ikateremshwa Aayah katika Suwratun-Nisaa:



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لاَ تَقْرَبُوا الصَّلاَةَ وَأَنْتُمْ سُكَارَى

“Enyi waloamini! Msikaribie Swalaah na hali mmelewa...” [An-Nisaa 4: 43]



Kisha muitaji wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akitangaza pale inapokimiwa Swalaah: “Tahadharini! Aliyelewa asikaribie Swalaah!” ‘Umar akaitwa tena na akasomewa akasema: “Ee Allaah tubainishie kuhusu pombe bainisho la kuridhisha.” Ikateremka Aayah:

‏فَهَلْ أَنْتُمْ مُنْتَهُونَ

“...basi je, mtakoma?” [Al-Maaidah 5: 90-91] ‘Umar akasema: “Tumekoma.” [Imaam Al-Albaaniy ameisahihisha katika Swahiyh Abiy Daawuwd (3670)]







Hikma Ya Pili: Kuthibitisha Qur-aan Katika Kifua Cha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):



Hikma nyingine ya kuteremshwa kidogokidogo ni kwa sababu ya kuithibisha Qur-aan katika kifua cha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwani ingelikuwa vigumu kwake kuipokea yote mara moja. Hii ni kwa sababu Qur-aan ni maneno mazito ya Allaah (عز وجل) kama Anavyosema Mwenyewe Allaah (سبحانه وتعالى):



وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلًا﴿٤﴾ إِنَّا سَنُلْقِي عَلَيْكَ قَوْلًا ثَقِيلًا﴿٥﴾

Na soma Qur-aan kwa kisomo cha utaratibu upasao, kuitamka vizuri na kutaamali. Hakika Sisi Tutakuteremshia juu yako kauli nzito. [Al-Muzzammil: 4 – 5]





Na pia, kumwezesha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhifadhi na kuifahamu kwani alikuwa ana pupa na hamu kubwa ya kuipokea, kuisoma, kuihifadhi na kuifahamu, Allaah (سبحانه وتعالى) Akamwambia:



وَلَا تَعْجَلْ بِالْقُرْآنِ مِن قَبْلِ أَن يُقْضَىٰ إِلَيْكَ وَحْيُهُ ۖ وَقُل رَّبِّ زِدْنِي عِلْمًا ﴿١١٤﴾

wala usiiharakize Qur-aan (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kabla haikumalizwa kufunuliwa Wahy kwako. Na sema: Rabb wangu! Nizidishie elimu. [Twaahaa: 114]



Allaah (سبحانه وتعالى) Akamtuliza na kumthibitishia kuisoma kwake, kuhifadhi na kuifahamu kwa kumwambia:



لَا تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ﴿١٦﴾ إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَهُ وَقُرْآنَهُ﴿١٧﴾ فَإِذَا قَرَأْنَاهُ فَاتَّبِعْ قُرْآنَهُ﴿١٨﴾ ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُ﴿١٩﴾




Usiutikisie (huu Wahy) ulimi wako ili kuiharakiza (Qur-aan ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Hakika ni juu Yetu kuikusanya na kukuwezesha kuisoma kwake. Basi Tunapoisoma (kupitia Jibriyl), fuata kusomwa kwake. Kisha ni juu Yetu kuibainisha (kwako). [Al-Qiyaamah: 16 – 19]


Na pia, kuthibitisha moyo wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kukariri kumteremshia Wahyi kidogokidogo kwani hivyo ilimsaidia Nabiy kuihifadhi kwa wepesi na kufahamu hukmu na shariy’ah zake na hivi ndivyo ilivyowezekana kuthibitisha moyo wake na kuimarisha azimio lake. Allaah (سبحانه وتعالى) Akamwambia:



وَكُلًّا نَّقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنبَاءِ الرُّسُلِ مَا نُثَبِّتُ بِهِ فُؤَادَكَ ۚ وَجَاءَكَ فِي هَـٰذِهِ الْحَقُّ وَمَوْعِظَةٌ وَذِكْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ﴿١٢٠﴾

Na yote Tunayokusimulia katika khabari muhimuu za Rusuli, Tunathibitisha kwazo moyo wako. Na imekujia katika hii haki na mawaidha na ukumbusho kwa Waumini. [Huwd: 120]







Hikma Ya Tatu: Kuithibitisha Qur-aan Kwa Swahaba Katika Kujifunza Kuisoma Na Kuifanyia Kazi.





Anasema Allaah (سبحانه وتعالى)



وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلًا﴿٤﴾

Na soma Qur-aan kwa kisomo cha utaratibu upasao, kuitamka vizuri na kutaamali. [Al-Muzzammil: 4]



Kwa Tartiyl (Usomaji wa taratibu wa kutaamali) hiyo, Allaah (سبحانه وتعالى) Akamfundisha Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) polepole na kidogokidogo naye awasomee Waumini hivyo hivyo. Ingelikuwa Qur-aan imeteremshwa kwa mteremsho mmoja, asingeweza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuisoma hivyo kwa Tartiyl na kuwafundisha Swahaba, jambo ambalo nao wasingeweza kuwafikishia Ummah wakaweza kuisioma na kuihifdhai kiwepesi.



Ndio maana Anasema Allaah (سبحانه وتعالى)



وَقُرْآنًا فَرَقْنَاهُ لِتَقْرَأَهُ عَلَى النَّاسِ عَلَىٰ مُكْثٍ وَنَزَّلْنَاهُ تَنزِيلًا ﴿١٠٦﴾

Na Qur-aan Tumeigawanya sehemu mbali mbali ili uwasomee watu kwa vipindi mbali mbali; na Tumeiteremsha mteremsho wa kidogokidogo. [Al-Israa:106]



Basi Aayah zilipokuwa zinateremshwa, Swahaba walikuwa wakizisoma na kuzihifadhi na kuzifanyia kazi. Hawakuwa wakihifadhi Aayah nyingine hadi wahakikishe wamezifahamu vizuri hizo chache, na kutekeleza maamrisho na makatazo yake. Imaam Atw-Twabariy (رحمه الله) amesema katika Tafsiyr yake: [Atw-Twabariy (1/80)]



Abu ‘Abdirrahmaan As-Salamiy amesema "Wametuhadithia wale ambao walikuwa wakitusomea Qur-aan, kwamba walikuwa wakitafuta kujifunza kuisoma Qur-aan kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), wakawa wanajifunza Aayah kumi kisha hawaendelei mpaka wazifanyie kazi, basi na hivyo hivyo nasi tukajifunza Qur-aan na kuifanyia kazi pamoja kwa wakati mmoja.” [Tafsiyr Atw-Twabariy (1/80)]



Lakini makafiri katika kejeli na ukaidi wao wa kukanusha Qur-aan walileta swali hili, "Kwa nini Qur-aan isiteremshwe mara moja?” Basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akawajibu kwamba Ameteremsha kwa kutaka kuthibitisha Quraan katika kifua cha Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم):



وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْلَا نُزِّلَ عَلَيْهِ الْقُرْآنُ جُمْلَةً وَاحِدَةً ۚ كَذَٰلِكَ لِنُثَبِّتَ بِهِ فُؤَادَكَ ۖ وَرَتَّلْنَاهُ تَرْتِيلًا ﴿٣٢﴾

Na wakasema wale waliokufuru: Kwa nini hakuteremshiwa Qur-aan kwa ujumla mara moja tu? Hivyo hivyo, ili Tukithibitishe kifua chako; na Tumeifunulia Wahyi punde kwa punde kwa kuratibu. [Al-Furqaan:32]



Imaam As-Sa’diy (رحمه الله) katika Tafsiyr yake amesema kuhusu Kauli hiyo ya Allaah (سبحانه وتعالى):



وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْلَا نُزِّلَ عَلَيْهِ الْقُرْآنُ جُمْلَةً وَاحِدَةً كَذَلِكَ لِنُثَبِّتَ بِهِ فُؤَادَكَ



“Kwa sababu kila alipoteremshiwa Qur-aan (صلى الله عليه وآله وسلم), alizidishiwa utulivu na thabaat (kuthibitika moyoni), khaswa wakati kulikuwa na sababu ya khofu, wasiwasi na dhiki, kwani Qur-aan ilipoteremshwa wakati wa sababu ya tukio fulani (Sabab Nuzuwl), basi huwa ina hadhi kubwa na uthibitisho wake ni wa nguvu na mkubwa zaidi kuliko kama ingeteremshwa kabla ya hapo. Na hivyo hukumbukwa zaidi inapotatuliwa jambo la tukio (kwa sababu ya kuteremshwa Qur-aan).”



Na kuhusu Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى)



وَرَتَّلْنَاهُ تَرْتِيلًا


Yaani, Tuliichelewesha polepole na tukakuambatanisha nayo, na yote haya yanaonyesha utunzaji wa Allaah (سبحانه وتعالى) juu ya Kitabu Chake na Rasuli Wake Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kwani Alifanya kuteremshwa Kitabu Chake kwa mtiririko wa polepole kulingana na hali ya Rasuli na masilahi yake ya Dini.



Na kuhusu kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

وَقُرْآنًا فَرَقْنَاهُ لِتَقْرَأَهُ عَلَى النَّاسِ عَلَىٰ مُكْثٍ وَنَزَّلْنَاهُ تَنزِيلًا ﴿١٠٦﴾

Na Qur-aan Tumeigawanya sehemu mbali mbali ili uwasomee watu kwa vipindi mbali mbali; na Tumeiteremsha mteremsho wa kidogokidogo. [Al-Israa:106]



عَلَى مُكْثٍ

kwa vipindi mbali mbali



Yaani: Polepole ili waizingatie na watafakari maana zake na watoe humo maarifa kuhusu Sayansi yake.



وَنَزَّلْنَاهُ تَنْزيلاً

na Tumeiteremsha mteremsho wa kidogokidogo:



Yaani: Kidogokidogo kwa kutengwa katika miaka ishirini na tatu.







Hikma Ya Nne: Baadhi ya maswali aliyokuwa akiulizwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) yalihitaji asubiri ateremshiwe Wahyi:





Changamoto pindi makafiri walipokuwa wakimjaribu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kumuuliza maswali ya kimiujiza. Ikawa ni ngumu kwake kuwajibu bila ya kuweko tayari Wahyi. Mfano kama vile kumuuliza juu ya Saa (Qiyaamah kitatokea lini), na wakati wowote washirikina walipomuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) swali kama hilo, Allaah (سبحانه وتعالى) Aliteremsha Qur-aan kujibu swali lao, juu ya kuwa Wahyi uliteremshwa kidogokidogo kwa wakati tofauti na mbalimbali, lakini hawakuweza wao kuleta kitu kama Qur-aan juu ya kuwa walijaribu kutunga maneno yao yakawa batili, Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):



قُل لَّئِنِ اجْتَمَعَتِ الْإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَىٰ أَن يَأْتُوا بِمِثْلِ هَـٰذَا الْقُرْآنِ لَا يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا ﴿٨٨﴾

Sema: Ikiwa watajumuika wana Aadam na majini ili walete mfano wa hii Qur-aan; hawatoweza kuleta mfano wake na japokuwa watasaidiana wao kwa wao. [Al-Israa: 88]





Qur-aan ikaendelea kuteremshwa katika hali za kuhitajika kwa dharura pia kama kuhusu swali la washirikina kuungana na Mayahudi kutaka kumjaribu Unabii wake Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) wakamuuliza kuhusu roho, Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:



وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الرُّوحِ ۖ قُلِ الرُّوحُ مِنْ أَمْرِ رَبِّي وَمَا أُوتِيتُم مِّنَ الْعِلْمِ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٨٥﴾

Na wanakuuliza kuhusu roho. Sema: Roho ni katika amri ya Rabb wangu. Na hamkupewa ujuzi isipokuwa kidogo tu. [Al-Israa: 85]





Au kuhusu swali la Waumini waliomuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu hukmu ya pombe, na kuhusu kutoa mali zao, na kuhusu Yatima, Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha Aayah mbili zinazofuatana kujibu yote hayo:





يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَا أَكْبَرُ مِن نَّفْعِهِمَا ۗ وَيَسْأَلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَ قُلِ الْعَفْوَ ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ ﴿٢١٩﴾ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۗ وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْيَتَامَىٰ ۖ قُلْ إِصْلَاحٌ لَّهُمْ خَيْرٌ ۖ وَإِن تُخَالِطُوهُمْ فَإِخْوَانُكُمْ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ الْمُفْسِدَ مِنَ الْمُصْلِحِ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَأَعْنَتَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٢٠﴾



Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema: Katika viwili hivyo mna dhambi kubwa na (baadhi ya) manufaa kwa watu. Na dhambi yake viwili hivyo ni kubwa kuliko manufaa yake. Na wanakuuliza nini watoe. Sema: Yaliyokuzidieni. Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat (na shariy’ah) ili mpate kutafakari. Katika dunia na Aakhirah. Na wanakuuliza kuhusu mayatima. Sema: Kuwatengeneza ni khayr. Na mkichanganya mambo yenu na yao basi hao ni ndugu zenu. Na Allaah Anamjua fisadi na mtengenezaji. Na lau Angetaka Allaah Angelikutieni katika shida. Hakika Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Al-Baqarah: 219 – 220]





Na maswali mengi mengineyo alikuwa akiulizwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ima na washirikina au Waumini na akawa anasubiri Wahyi uteremshwe kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى) ili awajibu. Na hii ndio hikma mojawapo iliyohitajika kuteremshwa Qur-aan kidogokidogo kwa sababu ilithibitisha zaidi Unabii wake kwa kuwa alitegemea na kusubiri Wahyi uteremshwe kutoka kwa Rabb wake.







Hikma Ya Tano: Kuteremshwa Kutokana Na Matukio Mbalimbali Kipindi Tofauti.



Kwa vile baadhi ya Aayah za Qur-aan zilikuwa zikiteremshwa kutokana na sababu ya matukio mbali mbali mfano; Kisa cha Watu watatu waliokhalifu katika vita vya Tabuk au kisa cha Ifk (kusingiziwa kashfah Mama Wa Waumini) n.k. hivyo kulihitaji kuweko na hukmu zake, ndio maana Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):



وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ تِبْيَانًا لِّكُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً وَبُشْرَىٰ لِلْمُسْلِمِينَ﴿٨٩﴾

Na Tumekuteremshia Kitabu kikiwa ni kielezo bayana cha kila kitu na ni mwongozo na rahmah na bishara kwa Waislamu. [An-Nahl: 89]



Matukio mengine yalimhitaji Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) asubiri Wahy kutoka kwa Allaah, mfano mmoja mzuri kabisa ni kisa cha Swahaabiyyah Khawlah bint Khuwaylid pindi mumewe alipomtajia idhwhaar (tamko la talaka la zama za kijaahiliyyah) basi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alishindwa kumpa hukmu. Baada ya muda si mrefu Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha hukmu. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ



قَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّتِي تُجَادِلُكَ فِي زَوْجِهَا وَتَشْتَكِي إِلَى اللَّـهِ وَاللَّـهُ يَسْمَعُ تَحَاوُرَكُمَا ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ﴿١﴾ الَّذِينَ يُظَاهِرُونَ مِنكُم مِّن نِّسَائِهِم مَّا هُنَّ أُمَّهَاتِهِمْ ۖ إِنْ أُمَّهَاتُهُمْ إِلَّا اللَّائِي وَلَدْنَهُمْ ۚ وَإِنَّهُمْ لَيَقُولُونَ مُنكَرًا مِّنَ الْقَوْلِ وَزُورًا ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ لَعَفُوٌّ غَفُورٌ﴿٢﴾ وَالَّذِينَ يُظَاهِرُونَ مِن نِّسَائِهِمْ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا قَالُوا فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مِّن قَبْلِ أَن يَتَمَاسَّا ۚ ذَٰلِكُمْ تُوعَظُونَ بِهِ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ﴿٣﴾ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ مِن قَبْلِ أَن يَتَمَاسَّا ۖ فَمَن لَّمْ يَسْتَطِعْ فَإِطْعَامُ سِتِّينَ مِسْكِينًا ۚ ذَٰلِكَ لِتُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۚ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ ۗ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٤﴾



Allaah Amekwishasikia kauli ya yule mwanamke anayejadiliana nawe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu mumewe, na anamshitakia Allaah; na Allaah Anayasikia majibizano yenu. Hakika Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote. Wale miongoni mwenu wanaowatamkia wake zao dhwihaar: Nyinyi kwetu kama migongo ya mama zetu. Hao wake zao si mama zao. Hawakuwa mama zao isipokuwa wale waliowazaa. Na hakika wao bila shaka wanasema yasiyokubalika na kauli ya kuchukiza na uongo. Na hakika Allaah bila shaka ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kughufuria. Na wale wanaowatamkia wake zao dhwihaar, kisha wakarudi katika waliyoyasema (kuitengua dhwihaar), basi ni kuacha huru mtumwa kabla ya kugusana. Hayo mnawaidhiwa kwayo. Na Allaah kwa yale myatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. Na yule asiyepata uwezo, basi afunge Swiyaam miezi miwili mfululuzo kabla ya kugusana. Na yule asiyeweza, basi alishe chakula masikini sitini. Hivyo ili mumuamini Allaah na Rasuli Wake. Na hiyo ni mipaka ya Allaah. Na makafiri watapata adhabu iumizayo. [Al-Mujaadalah: 1- 4].



Tukio kama hili na mengineyo, ni hikma ya kuteremshwa Qur-aan kidogokidogo pamoja na hukumu yake ili watu wafahamu pia hizo hukmu zake polepole. Mfano pia tukio lilosababisha kuteremshwa Aayah za Tayammu kama ifuatavyo:



عَنْ عَائِشَةَ، زَوْجِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَتْ خَرَجْنَا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي بَعْضِ أَسْفَارِهِ، حَتَّى إِذَا كُنَّا بِالْبَيْدَاءِ ـ أَوْ بِذَاتِ الْجَيْشِ ـ انْقَطَعَ عِقْدٌ لِي، فَأَقَامَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَلَى الْتِمَاسِهِ، وَأَقَامَ النَّاسُ مَعَهُ، وَلَيْسُوا عَلَى مَاءٍ، فَأَتَى النَّاسُ إِلَى أَبِي بَكْرٍ الصِّدِّيقِ فَقَالُوا أَلاَ تَرَى مَا صَنَعَتْ عَائِشَةُ أَقَامَتْ بِرَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَالنَّاسِ، وَلَيْسُوا عَلَى مَاءٍ، وَلَيْسَ مَعَهُمْ مَاءٌ‏.‏ فَجَاءَ أَبُو بَكْرٍ وَرَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَاضِعٌ رَأْسَهُ عَلَى فَخِذِي قَدْ نَامَ فَقَالَ حَبَسْتِ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَالنَّاسَ، وَلَيْسُوا عَلَى مَاءٍ، وَلَيْسَ مَعَهُمْ مَاءٌ‏.‏ فَقَالَتْ عَائِشَةُ فَعَاتَبَنِي أَبُو بَكْرٍ، وَقَالَ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَقُولَ، وَجَعَلَ يَطْعُنُنِي بِيَدِهِ فِي خَاصِرَتِي، فَلاَ يَمْنَعُنِي مِنَ التَّحَرُّكِ إِلاَّ مَكَانُ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَلَى فَخِذِي، فَقَامَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم حِينَ أَصْبَحَ عَلَى غَيْرِ مَاءٍ، فَأَنْزَلَ اللَّهُ آيَةَ التَّيَمُّمِ فَتَيَمَّمُوا‏.‏ فَقَالَ أُسَيْدُ بْنُ الْحُضَيْرِ مَا هِيَ بِأَوَّلِ بَرَكَتِكُمْ يَا آلَ أَبِي بَكْرٍ‏.‏ قَالَتْ فَبَعَثْنَا الْبَعِيرَ الَّذِي كُنْتُ عَلَيْهِ، فَأَصَبْنَا الْعِقْدَ تَحْتَهُ‏.‏

Mama wa ‘Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) amehadithia: “Tulikwenda katika moja ya safari tukafika Al-Baydaa au Dhaatul-Jaysh ambako kidani changu kilivunjika (na kikapotea). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawa anakitafuta, kisha pia watu wengineo wakainuka kukitafuta. Hapakuweko na maji sehemu hiyo, basi watu wakamwendea Abuu Bakr Asw-Swiddiyq na kusema: Huoni alivyofanya ‘Aaishah? Kamfanya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) pamoja na watu wakae sehemu ambayo hakuna maji! Abuu Bakr akaja wakati Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa amelaa akiwa amelaza kichwa chake mapajani mwangu. Akaniambia: Umemzuia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na watu sehemu ambako hakuna maji na wala hawana (akiba ya) maji. Basi akanigombesha na akasema Aliyomjaalia (Allaah) kusema kuhusu mimi na akanipiga ubavuni kwa mkono wake. Hakuna kilichonizuia kusogea (kutokana na maumivu) isipokuwa kwa vile Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alilala mapajani mwangu. Hapo Allaah Akateremsha Aayah ya tayammum, basi wakatayammam. ‘Usayd bin Al-Hudhwayr akasema: Ee ahli ya Abuu Bakr! Hii si baraka ya kwanza kwenu. Kisha akaendeshwa ngamia ambaye nilikuwa nimempanda na tukakipata kidani chini yake.” [Al-Bukhaariy].



Kadhaalika matukio mengineo ambayo pia yametokea kisha zikateremshwa Aayah pamoja na hukmu zake na ndipo ikawa wepesi Swahaba kuisoma, kuihifadhi na kuifanyia kazi maamrisho na makatazo yake yote.





Hikma Ya Sita: Kuthibitisha Nyoyo Za Waumini Kwa Subira Katika Mitihani:





Waumini pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) walihitaji kuthibitishwa katika iymaan zao kwa sababu walisibiwa na mitihani mbali mbali kwa kuingia kwao katika Uislaam, ikawa ni jaribio la iymaan zao, Allaah (سبحانه وتعالى) Akawateremshia Kauli Zake mbali mbali zikiwemo:





أَحَسِبَ النَّاسُ أَن يُتْرَكُوا أَن يَقُولُوا آمَنَّا وَهُمْ لَا يُفْتَنُونَ ﴿٢﴾ وَلَقَدْ فَتَنَّا الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۖ فَلَيَعْلَمَنَّ اللَّـهُ الَّذِينَ صَدَقُوا وَلَيَعْلَمَنَّ الْكَاذِبِينَ ﴿٣﴾

Je, wanadhani watu kwamba wataachwa kwa kuwa wanasema: Tumeamini. Nao ndio wasijaribiwe? Kwa yakini Tuliwajaribu wale wa kabla yao, ili Allaah Awatambulishe wale walio wakweli na ili Awatambulishe walio waongo. [Al-‘Ankabuwt: 2 – 3]



Na pia,



أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَعْلَمِ اللَّـهُ الَّذِينَ جَاهَدُوا مِنكُمْ وَيَعْلَمَ الصَّابِرِينَ ﴿١٤٢﴾

Je, Mnadhani kwamba mtaingia Jannah na hali Allaah Hakudhihirisha wale waliofanya jihaad miongoni mwenu na Akadhihirisha wenye kusubiri? [Aal-‘Imraan: 142]



Na pia,



أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَأْتِكُم مَّثَلُ الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلِكُم ۖ مَّسَّتْهُمُ الْبَأْسَاءُ وَالضَّرَّاءُ وَزُلْزِلُوا حَتَّىٰ يَقُولَ الرَّسُولُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ مَتَىٰ نَصْرُ اللَّـهِ ۗ أَلَا إِنَّ نَصْرَ اللَّـهِ قَرِيبٌ ﴿٢١٤﴾

Je, mnadhani kwamba mtaingia Jannah na hali bado haijakufikieni (mitihani) kama ya wale waliopita kabla yenu? Iliwagusa dhiki za umasikini na maafa ya magonjwa na njaa na wakatetemeshwa mpaka Rasuli na wale walioamini pamoja naye wanasema: Lini itafika nusura ya Allaah? Tanabahi! Hakika nusura ya Allaah iko karibu. [Al-Baqarah: 214]



Kwa hiyo Allaah (سبحانه وتعالى) Alipowateremshiwa Kauli Zake, ziliwasaidia kuendeleza subira zao na kuwafunza kubakia katika subra.





Na pia Suwrah na Aayah mbali mbali ziliteremshwa kusimulia visa vya Manabii waliotangulia ili wapate funzo kuwa si pekee yao waliosibiwa na mitihani.





Na pia Waumini walipohajiri kutoka Makkah kwenda Madiynah wakaacha masikani zao, mali zao na hata familia zao, baada ya kudhikishwa na makafiri wa Makkah, Allaah (سبحانه وتعالى) Akawateremshia Aayah za kuwabashiria Nusra kutoka Kwake na kuwaahidi malipo mema ya Jannah kutokana na subira zao na kuthibitika kwao na kubakia katika taqwa zao. Allaah (سبحانه وتعالى) Akawabashiria:



أُذِنَ لِلَّذِينَ يُقَاتَلُونَ بِأَنَّهُمْ ظُلِمُوا ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ نَصْرِهِمْ لَقَدِيرٌ ﴿٣٩﴾ الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِم بِغَيْرِ حَقٍّ إِلَّا أَن يَقُولُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ۗ وَلَوْلَا دَفْعُ اللَّـهِ النَّاسَ بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لَّهُدِّمَتْ صَوَامِعُ وَبِيَعٌ وَصَلَوَاتٌ وَمَسَاجِدُ يُذْكَرُ فِيهَا اسْمُ اللَّـهِ كَثِيرًا ۗ وَلَيَنصُرَنَّ اللَّـهُ مَن يَنصُرُهُ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ ﴿٤٠﴾



Wameruhusiwa (kupigana) kwa wale wanaopigwa kwa kuwa wamedhulumiwa. Na kwamba Allaah bila shaka ni Muweza wa kuwanusuru. Ambao wametolewa majumbani mwao bila ya haki isipokuwa kwa kuwa wanasema: Rabb wetu ni Allaah. Na lau ingelikuwa Allaah Hawakingi watu baadhi yao kwa wengine, bila shaka yangelivunjwa mahekalu na makanisa, na masinagogi na Misikiti inayotajwa humo Jina la Allaah kwa wingi. Na bila shaka Allaah Atamnusuru yeyote yule anayenusuru Dini Yake. Hakika Allaah bila shaka ni Mwenye nguvu zote, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika. [Al-Hajj: 39 – 40]



Hivyo ndio ikawa hikma mojawapo ya kuteremshwa Qur-aan kidogokidogo na kwa wakati mbalimbali khasa wakati wa matukio.







.
 
TUZINGATIE SANA HILI SWALA.....


Ipi Bora Kuhifadhi Qur-aan Yote Bila Ya Kujua Maana Au Kuhifadhi Kidogo Kwa Maana?
Maswali: Qur-aan


Ipi Bora Kuhifadhi Qur-aan Yote Bila Ya Kujua Maana Au Kuhifadhi Kidogo Kwa Maana?



Alhidaaya.com







SWALI:



Assalam alaykum warahmatuLLaahi wabarakatuhu. Nataka nipate ufumbuzi kuhufadhi Quran ni kusoma zwahiri, au nikuhifadhi bila ya kujuwa maana yake au ni kuhifadhi na maana yake? Kwa sababu nilisikia kama mtu akihifadhi Quran hataingiya motoni.



Na nani kahifadhi kati ya yule anasoma Quran yote bila kuifaham maana yake na yule anae juwa sura kumi na maana yake? Barakallahu fikum wasalam alaykum warhamatullahi wa Barakatuhu





JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Hakika ambayo haipingiki na yeyote mwenye akili timamu ni kuwa Qur-aan imeteremshwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kutimiza malengo fulani kwa wana Aadam. Lengo kubwa zaidi ni kuwaongoza watu wote katika njia nyoofu na ya sawa kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ

Mwezi wa Ramadhwaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na pambanuo (la haki na batili). [Al-Baqarah: 184]





na hivyo hivyo kwa wenye taqwa kama Anavyosema pia Allaah ('Azza wa Jalla):



ذَٰلِكَ الْكِتَابُ لَا رَيْبَ ۛ فِيهِ ۛ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٢﴾

Hiki ni Kitabu kisicho na shaka ndani yake, ni mwongozo kwa wenye taqwa [Al-Baqarah: 2]





Kwa minajili hiyo ni bora na muhimu zaidi kwa Muislamu kuisoma Qur-aan kwa kuizingatia maana yake pamoja na kufuata kimatendo yaliyomo ndani. Hivyo ndivyo walivyokuwa wakifanya Wema waliotangulia. Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhuma) alikuwa akisoma Aayah kumi, anazihifadhi na kutekeleza kimatendo maagizo yaliyomo ndani yake. Kwa njia hiyo alichukua miaka kumi kuihifadhi Suwratul-Baqarah [Maalik].





Maswahaba nao ndivyo walivyokuwa wakifanya walikuwa hawachukui Aayah nyengine hata kama zimeteremka siku hiyo mpaka zile walizokuwa nazo kuzihifadhi pamoja na kutwabikisha amri zilizomo ndani.



Japokuwa kuhifadhi Qur-aan kuna fadhila zake, na kila unaposoma herufi utapata thawabu kumi, lakini henda mtu akawa anasoma Qur-aan na huku inamlaani lakini hajui wala hatambui hilo.



Pia sisi hatutakiwi tuwe na ile sifa ya Mayahudi kama Anavyosema Allaah ('Azza wa Jalla):





مَثَلُ الَّذِينَ حُمِّلُوا التَّوْرَاةَ ثُمَّ لَمْ يَحْمِلُوهَا كَمَثَلِ الْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًا ۚ بِئْسَ مَثَلُ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴿٥﴾

Mfano wa wale waliobebeshwa Tawraat, kisha wasiibebe ni kama mfano wa punda abebaye mijalada ya vitabu. Ubaya ulioje mfano wa watu waliokadhibisha Aayaat za Allaah, na Allaah Haongoi watu madhalimu. [Al-Jumu’ah: 5]





Udhalimu unakuwa mkubwa ikiwa tutaibeba Qur-aan vifuani mwetu lakini hatuitilii maanani. Ndipo Allaah ('Azza wa Jalla) Anasema:



أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآنَ أَمْ عَلَىٰ قُلُوبٍ أَقْفَالُهَا﴿٢٤﴾

Je, hawaizingatii Qur-aan; au nyoyoni (mwao) mna kufuli? [Muhammad: 24]



Nasiha zetu za dhati kwa ndugu zetu ni kuwa mtu asome juzuu au hizbu au hata ukurasa mmoja wa Qur-aan kila siku bila kuacha pamoja na kufanya bidii kuhifadhi Suwrah au baadhi za Aayah anazoweza. Hivyo hivyo atenge wakati wa kusoma Tafsiyr kuanzia mwanzo wa Suwratul-Faatihah kidogo kidogo na kufanya juhudi kutekeleza hayo kimatendo.



Na Allah Anajua zaidi
 
Screenshot_20250511_215546_WhatsApp.jpg
 
UJUMBE WA SIKU:

Nabii Swalla Aallahu alaihy wasallam anasema

" Muumini hawezi kuwa na sifa ya UBAKHILI na TABIA MBAYA"

Ndugu zangu katika imani ni hakika yule aliyemwamini Allah na siku ya mwisho katu hawezi kuwa mbakhili,siku zote atapenda kutoa katika njia ya Allah

Kwakuwa anajua kutoa ni ibada kubwa sana aliyotuamrisha Allah subhaanahu wa Taala,daima atatoa sadaka pamoja na kuwasaidia wenye uhitaji

Siku moja bibi Aisha (Radhiallahu anha) aliendewa na Swahaba mmoja aliyekuwa na uhitaji wa fedha,basi mama Aisha akamwambia mtu yule lau ningekuwa na hela ningekupa dinari elfu kumi,basi yule mtu akaondoka zake

Mda si mrefu mtu mmoja akaja kumletea mama Aisha dinari elfu kumi,basi mama Aisha (radhiallahu anha) akasema huu nimepewa mtihani na Allah,maana nilimuahidi mtu mmoja nitampa dinari elfu kumi,nami nimeletwa hizo hizo,hapo hapo mama Aisha akazitoa dinar zote hizo na angali yeye hakubakia na kitu chochote

Watu walipouliza ni zipi zilikuwa tabia za Nabii Swalla Aallahu alaihy wa aalih wasallam,waakambiwa na mama Aisha,hakika tabia za Nabii Muhammad Swalla Aallahu alayhi wasallam ni Qu'an

Kwa maana alifuata yote yaliyo amrishwa kwenye qu'ran na kuacha yote yaliyo katazwa katika qu'ran

Kwa kifupi alikuwa na tabia njema

Basi nasi tujipambe na Tabia njema
 
031-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kusuluhisha Baini Ya Watu


Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب الإصلاح بَيْنَ الناس

031-Mlango Wa Kusuluhisha Baini Ya Watu



Alhidaaya.com



:قَالَ الله تَعَالَى



وَإِنِ امْرَأَةٌ خَافَتْ مِن بَعْلِهَا نُشُوزًا أَوْ إِعْرَاضًا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يُصْلِحَا بَيْنَهُمَا صُلْحًا ۚ وَالصُّلْحُ خَيْرٌ ۗ وَأُحْضِرَتِ الْأَنفُسُ الشُّحَّ ۚ وَإِن تُحْسِنُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿١٢٨﴾

Na ikiwa mke atakhofia kutoka kwa mumewe uonevu wa ndoa au kutengwa, basi si vibaya juu yake wakisikilizana baina yao kwa suluhu Na suluhu ni bora. Na nafsi zimewekewa uchoyo. Na mkifanya ihsaan na mkawa na taqwa, basi hakika Allaah kwa yale myatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [An-Nisaa 128]





لَّ خَيْرَ فِي كَثِيرٍ مِّن نَّجْوَاهُمْ إِلَّا مَنْ أَمَرَ بِصَدَقَةٍ أَوْ مَعْرُوفٍ أَوْ إِصْلَاحٍ بَيْنَ النَّاسِ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿١١٤﴾

Hakuna khayr katika minong’ono yao mingi isipokuwa anayeamrisha swadaqah, au mema, au kusuluhisha baina ya watu. Na atakayefanya hivyo kutaka radhi za Allaah, basi Tutampa ujira adhimu. [An-Nisaa: 114]





يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَنفَالِ ۖ قُلِ الْأَنفَالُ لِلَّـهِ وَالرَّسُولِ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَصْلِحُوا ذَاتَ بَيْنِكُمْ ۖ وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿١﴾

Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu ngawira; sema: Ngawira ni ya Allaah na Rasuli. Basi mcheni Allaah na tengenezeni yaliyo baina yenu. Na mtiini Allaah na Rasuli Wake mkiwa ni Waumini. [Al-Anfaal:1]





إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ﴿١٠﴾

Hakika Waumini ni ndugu, basi suluhisheni baina ya ndugu zenu. Na mcheni Allaah ili mpate kurehemewa. [Al-Hujuraat:10]





Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( كُلُّ سُلاَمَى مِنَ النَّاسِ عَلَيهِ صَدَقَةٌ ، كُلَّ يَوْمٍ تَطْلُعُ فِيهِ الشَّمْسُ : تَعْدِلُ بَيْنَ الاثْنَينِ صَدَقَةٌ ، وَتُعينُ الرَّجُلَ في دَابَّتِهِ فَتَحْمِلُهُ عَلَيْهَا، أَوْ تَرْفَعُ لَهُ عَلَيْهَا مَتَاعَهُ صَدَقَةٌ ، وَالكَلِمَةُ الطَّيِّبَةُ صَدَقةٌ ، وَبِكُلِّ خَطْوَةٍ تَمشِيهَا إِلَى الصَّلاةِ صَدَقَةٌ ، وَتُميطُ الأَذى عَنِ الطَّريقِ صَدَقَةٌ )). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kila kiungo cha mwanadamu kinafanya sadaka kila siku linapochomoza jua: Kusuluhisha kwa uadilifu baina ya watu wawili ni sadaka, kumsaidia mtu juu ya mnyama wake ukampandisha au ukamnyanyulia mzigo wake ni sadaka, kusema neno jema/zuri ni sadaka, kila hatua unayopiga kwenda kwenye Swalaah ni sadaka na kuondoa taka (uchafu) njiani ni sadaka. [Al-Bukhaariy na Muslim].





Hadiyth – 2

وعن أمِّ كُلْثُوم بنت عُقْبَة بن أَبي مُعَيط رضي الله عنها ، قَالَتْ : سمِعتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يَقُولُ : (( لَيْسَ الكَذَّابُ الَّذِي يُصْلِحُ بَيْنَ النَّاسِ فَيَنْمِي خَيراً ، أَوْ يقُولُ خَيْراً )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ. وفي رواية مسلم زيادة ، قَالَتْ : "وَلَمْ أسْمَعْهُ يُرْخِّصُ في شَيْءٍ مِمَّا يَقُولُهُ النَّاسُ إلاَّ في ثَلاثٍ ، تَعْنِي : الحَرْبَ ، وَالإِصْلاَحَ بَيْنَ النَّاسِ ، وَحَدِيثَ الرَّجُلِ امْرَأَتَهُ ، وَحَدِيثَ المَرْأةِ زَوْجَهَا".

Na imepokewa kutoka kwa Umm Kulthuum bint 'Uqbah bin Abuu Mu'aytw (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Si muongo yule anayesuluhisha baina ya watu akawa anasambaza habari za kheri, au anasema kheri." [Al-Bukhaariy na Muslim].

Na katika riwaayah ya Muslim ipo ziada inayosema: "Akasema: ' Wala sijamsikia akiruhusu chochote katika uwongo kwa wanayosema watu ila katika mambo matatu, yaani katika vita, kusuluhisha baina ya watu na mazungumzo ya mwaname kwa mkewe na mke kuzungumza na mumewe."





Hadiyth – 3

وعن عائشة رضي الله عنها ، قَالَتْ : سَمِعَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم صَوْتَ خُصُومٍ بِالبَابِ عَاليةً أصْوَاتُهُمَا ، وَإِذَا أحَدُهُمَا يَسْتَوْضِعُ الآخَر وَيَسْتَرْفِقُهُ في شَيءٍ ، وَهُوَ يَقُولُ : والله لا أفْعَلُ، فَخَرجَ عَلَيْهِمَا رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : (( أيْنَ المُتَأَلِّي عَلَى اللهِ لاَ يَفْعَلُ المَعْرُوفَ ؟ )) ، فَقَالَ : أَنَا يَارسولَ اللهِ ، فَلَهُ أيُّ ذلِكَ أحَبَّ . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa na ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisikia sauti ya watu wakiteta mlangoni wakiwa wamenyanyua sauti zao. Mmoja wapo alikuwa akimwomba mwenziwe ampunguzie deni na adai kwa upole, na yule mwingine akisema:"Wa -Allaahi sikubali?" Akawatokea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akauliza: "NI yupi aliyeapa kwa Allaah kuwa hatafanya wema?" Akasema: "Ni mimi, Ee Rasuli wa Allaah, nimempa khiyari afanye analopenda. [Al-Bukhaariy na Muslim].





Hadiyth – 4

وعن أَبي العباس سهل بن سَعد الساعِدِيّ رضي الله عنه : أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم بَلَغَهُ أنَّ َني عَمرو بن عَوْفٍ كَانَ بَيْنَهُمْ شَرٌّ ، فَخَرَجَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يُصْلِحُ بَينَهُمْ في أُنَاس مَعَهُ ، فَحُبِسَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم وَحَانَتِ الصَّلاة ، فَجَاءَ بِلالٌ إِلَى أَبي بكر رضي الله عنهما ، فَقَالَ: يَا أَبا بَكْر ، إنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَدْ حُبِسَ وَحَانَتِ الصَّلاةُ فَهَلْ لَكَ أنْ تَؤُمَّ النَّاس ؟ قَالَ : نَعَمْ ، إنْ شِئْتَ ، فَأقَامَ بِلالٌ الصَّلاةَ ، وتَقَدَّمَ أَبُو بَكْرٍ فَكَبَّرَ وَكَبَّرَ النَّاسُ ، وَجَاءَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يَمشي في الصُّفُوفِ حَتَّى قَامَ في الصَّفِّ ، فَأَخَذَ النَّاسُ في التَّصْفيقِ ، وَكَانَ أَبُو بكرٍ رضي الله عنه لا يَلْتَفِتُ في الصَّلاةِ ، فَلَمَّا أكْثَرَ النَّاسُ في التَّصْفيقِ الْتَفَتَ ، فإِذَا رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، فَأَشَارَإِِلَيْه رسولُ الله صلى الله عليه وسلم فَرَفَعَ أَبُو بَكْر رضي الله عنه يَدَهُ فَحَمِدَ اللهَ ، وَرَجَعَ القَهْقَرَى وَرَاءهُ حَتَّى قَامَ في الصَّفِّ ، فَتَقَدَّمَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، فَصَلَّى للنَّاسِ ، فَلَمَّا فَرَغَ أقْبَلَ عَلَى النَّاسِ ، فَقَالَ : (( أيُّهَا النَّاسُ ، مَا لَكُمْ حِينَ نَابَكُمْ شَيْءٌ في الصَّلاةِ أخَذْتُمْ في التَّصفيق ؟! إِنَّمَا التَّصفيق للنِّساء . مَنْ نَابَهُ شَيْءٌ في صَلاتِهِ فَلْيَقُلْ : سُبْحَانَ الله ، فَإِنَّهُ لاَ يَسْمَعُهُ أحدٌ حِينَ يقُولُ : سُبْحَانَ الله ، إلاَّ الْتَفَتَ . يَا أَبا بَكْر : مَا مَنَعَكَ أنْ تُصَلِّي بالنَّاسِ حِينَ أشَرْتُ إلَيْكَ ؟ )) ، فَقَالَ أَبُو بَكْرٍ : مَا كَانَ يَنْبَغي لابْنِ أَبي قُحَافَةَ أنْ يُصَلِّي بالنَّاسِ بَيْنَ يَدَيْ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Abil 'Abbaas Sahl bin Sa'ad As-Saa'idiyy (Radhwiya Allaahu 'Anhu) kuwa ilimfikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa kuna mzozano baina ya vikundi vya Bani 'Amru bin 'Awf. Akatoka Rasuli wa Allaah kwenda kuwasuluhisha pamoja na kundi la maswahaba wake. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akawa ni mwenye kuzuiliwa (baada ya hiyo sulhu kwa kualikwa karamu) na wakati wa swalaah ukafika akiwa katika hali hiyo. Bilaal alikuja kwa Abuu Bakr (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) akamwambia: " Ee Abuu Bakr, hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amezuiliwa na wakati wa swalaah umefika, utaswalisha watu?" Akasema: "Ndio ukitaka." Kwa hiyo, Bilaal akakimu swalaah, naye Abuu Bakr akajongea na kufunga swalaah, nao watu wakamfuata (kwa kupiga takbiyr ya kufungia swalaah) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuja akiwa anapita katika safu mpaka akasimama katika safu. Watu wakaanza kupiga makofi, Naye Abuu Bakr (Radhwiya Allaahu 'anhu) alikuwa hana tabia ya kugeuka katika Swalaah yake. watu walipokithirisha kupiga makofi (Abuu Bakr) aligeuka na kumuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwashiria aendelee, Abuu Bakr (Radhwiya Allaahu 'anhu) alinyanyua mikono na kumuhimidi Allaah, kisha akarudi kinyumenyume nyuma yake mpaka akasimama kwenye safu. Hapo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alijongea mbele na kuwaswalisha watu. Alipomaliza kuswalisha aliwaelekea watu, akasema: "Enyi watu! Mna nini nyinyi linapotendeka jambo mnaanza kupiga makofi? Hakika kupiga makofi ni kwa wanawake. Linapotendeka jambo katika Swalaah (nawe unataka kumkumbusha Imaam) basi aseme mmoja wenu: Subhaana Allaah( Ametakasika Allaah, yaani hana mapungufu yoyote yale). Hiyo ni kuwa hatasikia yeyote pindi unaposema: Subhaana Allaah ila atatizama. Ee Abuu bakr! Ni lipi liliokukataza kuwaswalisha watu nilipokuashiria?" Akasema Abuu Bakr (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Haifalii kwa mtoto wa Abuu Quwhaafah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwaswalisha watu mbele ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)." [Al-Bukhaariy na Muslim].
 
032-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila Za Waislamu Wanyonge, Mafakiri Wasiojulikana


Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب فضل ضعفة المسلمين والفقراء والخاملين

032-Mlango Wa Fadhila Za Waislamu Wanyonge,Mafakiri Wasiojulikana



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:

وَاصْبِرْ نَفْسَكَ مَعَ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ وَلَا تَعْدُ عَيْنَاكَ عَنْهُمْ تُرِيدُ زِينَةَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَلَا تُطِعْ مَنْ أَغْفَلْنَا قَلْبَهُ عَن ذِكْرِنَا وَاتَّبَعَ هَوَاهُ وَكَانَ أَمْرُهُ فُرُطًا ﴿٢٨﴾

Na isubirishe nafsi yako pamoja na wale wanaomuomba Rabb wao asubuhi kabla jua kucha na jioni, wanataka Wajihi Wake. Na wala macho yako yasiwavuke kwa kutaka pambo la uhai wa dunia. Na wala usimtii Tuliyemghafilisha moyo wake na Ukumbusho Wetu akafuata hawaa zake, na jambo lake limekuwa la kuzidi kuvuka mipaka. [Al-Kahf: 28]





Hadiyth – 1

وعن حارثة بن وهْبٍ رضي الله عنه ، قَالَ : سمعت رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، يقولُ 🙁( ألاَ أُخْبِرُكُمْ بِأهْلِ الجَنَّةِ ؟ كُلُّ ضَعِيف مُتَضَعَّف، لَوْ أقْسَمَ عَلَى اللهِ لأَبَرَّهُ ، أَلاَ أُخْبِرُكُمْ بِأهْلِ النَّارِ ؟ كُلُّ عُتُلٍّ جَوّاظٍ مُسْتَكْبِرٍ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwake Haarithah bin Wahb (Radhwiya Allaahu 'anhu) aliyesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: " Je, niwajulishe nyinyi watu wa peponi? Kila mnyonge na mwenye kunyongeshwa, lau atakula yamini kwa Allaah basi atakubaliwa. Je, niwapashe habari ya watu wa motoni? Kila msusuwavu, mgumu na mwenye kiburi katika kutembea kwake." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 2

وعن أَبي عباس سهل بن سعد الساعِدِيِّ رضي الله عنه، قَالَ : مَرَّ رَجُلٌ عَلَى النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، فَقَالَ لرَجُلٍ عِنْدَهُ جَالِسٌ : (( مَا رَأيُكَ في هَذَا ؟ )) ، فَقَالَ : رَجُلٌ مِنْ أشْرَافِ النَّاسِ ، هَذَا واللهِ حَرِيٌّ إنْ خَطَبَ أنْ يُنْكَحَ ، وَإنْ شَفَعَ أنْ يُشَفَّعَ . فَسَكَتَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم، ثُمَّ مَرَّ رَجُلٌ آخَرُ ، فَقَالَ لَهُ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: (( مَا رَأيُكَ في هَذَا ؟ )) فَقَالَ : يَا رَسُولَ الله ، هَذَا رَجُلٌ مِنْ فُقَراءِ المُسْلِمِينَ ، هَذَا حَرِيٌّ إنْ خَطَبَ أنْ لا يُنْكَحَ ، وَإنْ شَفَعَ أنْ لا يُشَفَّعَ ، وَإنْ قَالَ أنْ لاَ يُسْمَعَ لِقَولِهِ . فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( هَذَا خَيْرٌ مِنْ مِلءِ الأرْضِ مِثْلَ هَذَا )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abil 'Abbaas Sahl bin Sa'ad As-Saa'idiyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa mtu mmoja alipita mbele ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) naye akamuuliza mtu aliyekuwa ameketi pamoja naye: "Ni Yepi maoni yako kuhusu mtu huyu?" Akasema: "Mtu huyu ni miongoni mwa watu watukufu. Wa-Allaahi, huyu anastahiki akienda kuposa aozeshwe na akiombea akubaliwe ombi lake. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akanyamaza, halafu akapita mtu mwingine, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza tena: "Ni Yepi maoni yako kuhusu mtu huyu?" Akasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Huyu mtu ni miongoni mwa mafakiri wa Waislamu, naye anafaa akienda kuposa asiozeshwe na akiombea asikubaliwe ombi lake na akizungumza asisikilizwe." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Huyu (fakiri) ni bora kuliko kuijaza ardhi na watu mfano wake (mtu wa kwanza). [Al-Bukhaariy na Muslim]



Hadiyth – 3

وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( احْتَجَّتِ الجَنَّةُ والنَّارُ ، فقالتِ النَّارُ : فِيَّ الجَبَّارُونَ وَالمُتَكَبِّرُونَ . وَقَالتِ الجَنَّةُ : فِيَّ ضُعَفَاءُ النَّاسِ وَمَسَاكِينُهُمْ ، فَقَضَى اللهُ بَيْنَهُمَا : إنَّكِ الجَنَّةُ رَحْمَتِي أرْحَمُ بِكِ مَنْ أشَاءُ ، وَإنَّكِ النَّارُ عَذَابِي أُعَذِّبُ بِكِ مَنْ أشَاءُ ، وَلِكلَيْكُمَا عَلَيَّ مِلْؤُهَا )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Pepo na Moto zilizozana. Moto ukasema: 'kwangu ni majabari na wenye kiburi'. Na ikasema Pepo: 'Kwangu ni wanyonge na maskini wao'. Allaah Akahukumu baina yao: "Hakika wewe pepo ni rehma Yangu, kwako Ninamrehemu Nimtakaye. Na hakika wewe Moto ni adhabu Yangu, kwako Ninamuadhibu nimtakaye, na nyote Nitawajaza." [Muslim]





Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( إنَّهُ لَيَأتِي الرَّجُلُ السَّمِينُ العَظِيمُ يَوْمَ القِيَامَةِ لاَ يَزِنُ عِنْدَ اللهِ جَناحَ بَعُوضَةٍ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika atakuja mtu mkubwa na mnene siku ya Qiyaamah, hatakuwa na uzito mbele ya Allaah siku hiyo (japo uzito wa) ubawa wa mbu." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ امْرَأَةً سَوْدَاءَ كَانَتْ تَقُمُّ المَسْجِدَ ، أَوْ شَابّاً ، فَفَقَدَهَا ، أَوْ فَقَدَهُ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم، فَسَأَلَ عَنْهَا ، أو عنه ، فقالوا : مَاتَ . قَالَ : (( أَفَلا كُنْتُمْ آذَنْتُمُونِي )) فَكَأنَّهُمْ صَغَّرُوا أمْرَهَا ، أَوْ أمْرهُ ، فَقَالَ : (( دُلُّونِي عَلَى قَبْرِهِ )) فَدَلُّوهُ فَصَلَّى عَلَيْهَا ، ثُمَّ قَالَ : (( إنَّ هذِهِ القُبُورَ مَمْلُوءةٌ ظُلْمَةً عَلَى أهْلِهَا ، وَإنَّ اللهَ تعالى . يُنَوِّرُهَا لَهُمْ بِصَلاتِي عَلَيْهِمْ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Kutoka kwake Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa kulikuwa na mwanamke mweusi au kijana aliyekuwa akisafisha Msikiti. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamkosa, akamuulizia. Wakasema: "Amefariki." Akasema: "Kwanini hamukunieleza?" Hiyo ni kama kwamba jambo lake waliliona dogo. Akasema: "Nionyesheni kaburi yake." Wakamuonyesha, naye (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaswali hapo kaburini. Kisha akasema: "Hakika haya makaburi yamejaa kiza kwa watu wake na kuwa Allaah Aliyetukuka Anayatia mwangaza kwa mimi kuwaswalia." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 6

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( رُبَّ أشْعَثَ أغبرَ مَدْفُوعٍ بالأبْوابِ لَوْ أقْسَمَ عَلَى اللهِ لأَبَرَّهُ )) رواه مسلم .

Abuu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: "Huenda mwenye nywele timtim, aliyejaa vumbi anayefukuzwa milangoni, lau atamuapia Allaah (amfanyie jambo lolote lile) Angemfanyia." [Muslim]





Hadiyth – 7

وعن أسامة رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( قُمْتُ عَلَى بَابِ الجَنَّةِ ، فَإِذَا عَامَّةُ مَنْ دَخَلَهَا المَسَاكِينُ ، وَأصْحَابُ الجَدِّ مَحْبُوسُونَ ، غَيْرَ أنَّ أصْحَابَ النَّارِ قَدْ أُمِرَ بِهِمْ إِلَى النَّارِ . وَقُمْتُ عَلَى بَابِ النَّارِ فَإِذَا عَامَّةُ مَنْ دَخَلَهَا النِّسَاءُ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Usaamah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "NIlisimama katika mlango wa Peponi, wengi waliokuwa wakiingia ni maskini, matajiri wamefungwa, ila watu wa Motoni wameamriwa motoni. Na nikasimama kwenye mlango wa Motoni; wengi waliokuwa wakiingia humo ni wanawake." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 8

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( لَمْ يَتَكَلَّمْ في المَهْدِ إلاَّ ثَلاثَةٌ : عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ ، وَصَاحِبُ جُرَيْجٍ ، وَكَانَ جُرَيْجٌ رَجُلاً عَابِداً ، فَاتَّخَذَ صَوْمَعَةً فَكَانَ فِيهَا ، فَأَتَتْهُ أُمُّهُ وَهُوَ يُصَلِّي ، فَقَالَتْ : يَا جُرَيْجُ ، فَقَالَ : يَا رَبِّ أُمِّي وَصَلاتِي فَأَقْبَلَ عَلَى صَلاتِهِ فَانْصَرَفَتْ . فَلَمَّا كَانَ مِنَ الغَدِ أتَتْهُ وَهُوَ يُصَلِّي ، فَقَالَتْ : يَا جُرَيْجُ ، فَقَالَ : أيْ رَبِّ أمِّي وَصَلاتِي ، فَأقْبَلَ عَلَى صَلاتِهِ ، فَلَمَّا كَانَ مِنْ الغَدِ أتَتْهُ وَهُوَ يُصَلِّي ، فَقَالَتْ : يَا جُرَيْجُ ، فَقَالَ : أيْ رَبِّ أمِّي وَصَلاتِي ، فَأقْبَلَ عَلَى صَلاَتِهِ ، فَقَالَتْ : اللَّهُمَّ لاَ تُمِتْهُ حَتَّى يَنْظُرَ إِلَى وُجُوهِ المُومِسَاتِ . فَتَذَاكَرَ بَنُو إسْرائِيل جُرَيْجاً وَعِبَادَتَهُ ، وَكَانَتِ امْرَأةٌ بَغِيٌّ يُتَمَثَّلُ بحُسْنِهَا ، فَقَالَتْ : إنْ شِئْتُمْ لأَفْتِنَنَّهُ ، فَتَعَرَّضَتْ لَهُ ، فَلَمْ يَلْتَفِتْ إِلَيْهَا ، فَأتَتْ رَاعِياً كَانَ يَأوِي إِلَى صَوْمَعَتِهِ ، فَأَمْكَنَتْهُ مِنْ نَفْسِهَا فَوقَعَ عَلَيْهَا ، فَحَمَلَتْ ، فَلَمَّا وَلَدَتْ ، قَالَتْ : هُوَ مِنْ جُريج ، فَأتَوْهُ فَاسْتَنْزَلُوهُ وَهَدَمُوا صَوْمَعَتَهُ ، وَجَعَلُوا يَضْرِبُونَهُ ، فَقَالَ : مَا شَأنُكُمْ ؟ قَالُوا : زَنَيْتَ بهذِهِ البَغِيِّ فَوَلَدَتْ مِنْكَ . قَالَ : أيْنَ الصَّبيُّ ؟ فَجَاؤُوا بِهِ فَقَالَ : دَعُوني حَتَّى أصَلِّي ، فَصَلَّى فَلَمَّا انْصَرفَ أتَى الصَّبيَّ فَطَعنَ في بَطْنِهِ ، وَقالَ : يَا غُلامُ مَنْ أبُوكَ ؟ قَالَ : فُلانٌ الرَّاعِي ، فَأَقْبَلُوا عَلَى جُرَيْجٍ يُقَبِّلُونَهُ وَيَتَمَسَّحُونَ بِهِ ، وَقَالُوا : نَبْنِي لَكَ صَوْمَعَتَكَ مِنْ ذَهَب . قَالَ : لاَ ، أعِيدُوهَا مِنْ طِينٍ كَمَا كَانَتْ ، فَفَعلُوا . وبَينَا صَبِيٌّ يَرْضَعُ منْ أُمِّهِ فَمَرَّ رَجُلٌ رَاكِبٌ عَلَى دَابَّةٍ فَارِهَةٍ وَشَارَةٍ حَسَنَةٍ ، فَقَالَتْ أُمُّهُ : اللَّهُمَّ اجْعَل ابْنِي مِثْلَ هَذَا ، فَتَرَكَ الثَّدْيَ وَأقْبَلَ إِلَيْهِ فَنَظَرَ إِلَيْهِ ، فَقَالَ : اللَّهُمَّ لاَ تَجْعَلْنِي مِثْلَهُ ، ثُمَّ أقْبَلَ عَلَى ثَدْيه فَجَعَلَ يَرتَضِعُ )) ، فَكَأنِّي أنْظُرُ إِلَى رَسُول الله r وَهُوَ يَحْكِي ارْتضَاعَهُ بِأصْبَعِهِ السَّبَّابَةِ في فِيه ، فَجَعَلَ يَمُصُّهَا ، قَالَ : (( وَمَرُّوا بِجَارِيَةٍ وَهُم يَضْرِبُونَهَا ، ويَقُولُونَ : زَنَيْتِ سَرَقْتِ ، وَهِيَ تَقُولُ : حَسْبِيَ اللهُ ونِعْمَ الوَكِيلُ . فَقَالَتْ أمُّهُ : اللَّهُمَّ لاَ تَجْعَل ابْنِي مِثْلَهَا ، فَتَركَ الرَّضَاعَ ونَظَرَ إِلَيْهَا ، فَقَالَ : اللَّهُمَّ اجْعَلْنِي مثْلَهَا ، فَهُنَالِكَ تَرَاجَعَا الحَديثَ، فَقَالَتْ : مَرَّ رَجُلٌ حَسَنُ الهَيْئَةِ ، فَقُلْتُ : اللَّهُمَّ اجْعَلْ ابْنِي مِثْلَهُ ، فَقُلْتَ : اللَّهُمَّ لاَ تَجْعَلْنِي مِثْلَهُ ، وَمَرُّوا بهذِهِ الأمَةِ وَهُمْ يَضْرِبُونَهَا وَيَقُولُونَ : زَنَيْتِ سَرَقْتِ ، فقلتُ : اللَّهُمَّ لاَ تَجْعَلِ ابْنِي مِثْلَهَا ، فَقُلْتَ : اللَّهُمَّ اجْعَلْنِي مِثْلَهَا ؟! قَالَ : إنَّ ذلك الرَّجُل كَانَ جَبَّاراً ، فَقُلْتُ : اللَّهُمَّ لا تَجْعَلْنِي مِثْلَهُ ، وَإنَّ هذِهِ يَقُولُونَ : زَنَيْتِ ، وَلَمْ تَزْنِ وَسَرقْتِ ، وَلَمْ تَسْرِقْ ، فَقُلْتُ : اللَّهُمَّ اجْعَلْنِي مِثْلَهَا )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hawakuzungumza ulezini (uchangani) ila watatu: 'Iysa bin Maryam, Saahibu wa Jurayj. Jurayj alikuwa mtu mwenye kuabudu, naye akajenga kihekalumchake, akakaa humo, Alipokuja mamake akiwa anaswali Akamwuita: "Ee Jurayj." Akasema: "Ee Mola wangu! Mamangu na Swalaah yangu." Hivyo, akaendelea kuswali, basi akaondoka. Kesho yake alikuja akiwa anaswali. Akamuita: "Ee Jurayj." Akasema: "Ee Mola wangu! Mamangu na Swalaah yangu." Akaendelea kuswali, Akaondoka. Kesho yake akaja akiwa anaswali. Akamuita: "Ee Jurayj." Akasema: "Ee Mola wangu! Mamangu na Swalaah yangu." Akasema (mama): Ee Allaah, usimfishe mpaka aone nyuso za kahaba." Banu Israaiyli wakazungumza habari ya Jurayj na Ibada zake, Kulikuwa na mwanamke kahaba aliyepigiwa mfano kwa uzuri wake, akasema: "Mkitaka nitamfitini. Akamjia, hakumtazama. Akaja kwa mchungaji aliyekuwa akilala kwenye kihekalu chake, akammakinisha katika nafsi yake, akajamiiana naye. Akabeba mimba, Alipozaa, alisema: "Huyu ni mtoto wa Jurayj." Watu wakaja kwake, wakamteremsha na kuvunja kihekalu chake huku wanampiga. Akawauliza: "Mna nini nyinyi?" Wakasema: "Umezini na huyu malaya, naye kakuzalia mtoto." Akasema: "Mtoto yuko wapi?" Wakamleta akawaambia:"Niacheni ni swali." Akaswali,alipomaliza Swalaah yake akaja kwa mtoto na kumchua kwenye tumbo lake, akamuuliza:"Ee kijana! Nani baba yako?" Akasema: "Fulani mchungaji." Watu wakamkabili Jurayj kumbusu na kumwuomba msamaha. Wakasema: "Tunakujengea kihekalu chako kwa dhahabu." Akasema: "Hapana, irudisheni kama ilivyokuwa ya udongo." (Wa tatu); Mtoto akiwa ananyonya kwa mamake, akapita mtu mwenye kupanda mnyama, umbile na hali yake nzuri, na vazi lake zuri. Mamake akasema: "Ee Allaah , mjaalie mwnangu mfano wa huyu.: Mtoto akaacha kunyonya, akamtazama yule mtu, akasema: "Ee Allaah, usinijaalie kama huyu." Kisha akaelekea kwenye nyonyo na akaendelea kunyonya. Ni kana kwamba mimi namtazama Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiingiza kunyonya kwake (mtoto huyo) kwa kidole chake cha shahada mdomoni mwake. Akasema mara wakapita kwa kijakazi huku wanampiga,
wakisema: "Umezini, umeiba," naye anasema: "Allaah Ananitosha Naye ni Mbora wa kutegemewa." Mamake akasema: "Ee Allaah, usimjaalie mwanangu mfano wake." Akaacha kunyonya, akatazama, kisha akasema: "Ee Allaah , nijaalie mfano wake." Hapo mazungumzo yakajiri; Mama akasema: "Alipita mtu mwenye umbo zuri, nikasema: Ee Allaah, mjaalie mwanangu kama huyu, ukasema: 'Allaah usinifanye hivyo.' Akapita huyu kijakazi, nao wanampiga huku wakisema: Umezini, umeiba. Nikasema: 'Ee Allaah, usimjaalie mwanangu kama huyu.' Ukasema: 'Ee Allaah, nijaalie kama yeye.' Akasema mtoto: "Hakika yule mtu alikuwa jabari, hivyo nikasema: 'Ee Allaah usinijaalie kama yeye.' Na hakika huyu (kijakazi), wanamwambia: Umezidi, hajazini, Umeiba, hajaiba Nikasema: 'Ee Allaah, nijaalie kama yeye." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب ملاطفة اليتيم والبنات وسائر الضعفة والمساكين

والمنكسرين والإحسان إليهم والشفقة عليهم

والتواضع معهم وخفض الجناح لهم

033- Mlango Wa Kuwafanyia Upole Mayatima, Mabinti, Wanyonge wote, Maskini, Waliofilisika Pamoja na Kuwafanyia Hisani, Kuwahurumia, Kuwanyenyekea na kuwainamishia Bawa



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:

لَا تَمُدَّنَّ عَيْنَيْكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعْنَا بِهِ أَزْوَاجًا مِّنْهُمْ وَلَا تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَاخْفِضْ جَنَاحَكَ لِلْمُؤْمِنِينَ﴿٨٨﴾

Usikodoe kabisa macho yako katika Tuliyowasterehesha makundi fulani miongoni mwao, na wala usihuzunike juu yao. Na inamisha bawa lako kwa Waumini (kuwahurumia). [Al-Hijr: 88]



وَاصْبِرْ نَفْسَكَ مَعَ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ وَلَا تَعْدُ عَيْنَاكَ عَنْهُمْ تُرِيدُ زِينَةَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَلَا تُطِعْ مَنْ أَغْفَلْنَا قَلْبَهُ عَن ذِكْرِنَا وَاتَّبَعَ هَوَاهُ وَكَانَ أَمْرُهُ فُرُطًا ﴿٢٨﴾

Na isubirishe nafsi yako pamoja na wale wanaomuomba Rabb wao asubuhi kabla jua kucha na jioni, wanataka Wajihi Wake. Na wala macho yako yasiwavuke kwa kutaka pambo la uhai wa dunia. Na wala usimtii Tuliyemghafilisha moyo wake na Ukumbusho Wetu akafuata hawaa zake, na jambo lake limekuwa la kuzidi kuvuka mipaka. [Al-Kahf: 28]



فَأَمَّا الْيَتِيمَ فَلَا تَقْهَرْ ﴿٩﴾ وَأَمَّا السَّائِلَ فَلَا تَنْهَرْ ﴿١٠﴾

Kwa hivyo basi yatima usimuonee. Na mwombaji usimkaripie. [Adhw-Dhwuhaa: 9-10]

أَرَأَيْتَ الَّذِي يُكَذِّبُ بِالدِّينِ ﴿١﴾ فَذَٰلِكَ الَّذِي يَدُعُّ الْيَتِيمَ ﴿٢﴾ وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ الْمِسْكِينِ ﴿٣﴾

Je, umemuona yule anayekadhibisha malipo? Basi huyo ndiye anayemsukuma yatima. Na wala hahamasishi kulisha maskini. [Al-Maa'uwn: 1-3]





Hadiyth – 1

وعن سعد بن أَبي وَقَّاص رضي الله عنه، قَالَ : كُنَّا مَعَ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم سِتَّةَ نَفَرٍ ، فَقَالَ المُشْرِكُونَ للنَّبيِّ صلى الله عليه وسلم: اطْرُدْ هؤلاء لا يَجْتَرِئُونَ عَلَيْنَا ، وَكُنْتُ أنَا وَابْنُ مَسْعُودٍ . وَرَجُلٌ مِنْ هُذَيْلٍ وَبِلالٌ وَرَجُلاَنِ لَسْتُ أُسَمِّيهِمَا ، فَوَقَعَ في نفس رَسُول الله صلى الله عليه وسلم مَا شَاءَ اللهُ أنْ يَقَعَ فَحَدَّثَ نَفسَهُ ، فَأنْزَلَ اللهُ تعالى : ( وَلا تَطْرُدِ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ) [ الأنعام : 52 ] رواه مسلم .

Amesema Sa'ad bin Abu Waqqaasw (Radhwiya Allaahu 'anhu) Tulikuwa watu sita pamija na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), na washirikina wakamwambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Wafukuze hawa (watu sita) ili wasiwe na ujasiri wa kutukabili sisi." Watu sita hao walikuwa ni mimi, Ibn Mas'uud, mtu katika ukoo wa Hudhayl, Bilaal na watu wawili ambao sikuyajua majina yao. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akahisi alivyopenda Allaah ahisi, hivyo kuanza kuihadithia nafsi yake kuhusu hilo. Hapo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akateremsha: (Na wala usiwafukuze wale wanaomwomba Rabb wao asubuhi na jioni wanataka Wajihi Wake). [Al-An'aam:52] Muslim





Hadiyth – 2

وعن أَبي هُبَيرَة عائِذ بن عمرو المزنِي وَهُوَ مِنْ أهْل بيعة الرضوان رضي الله عنه: أنَّ أبا سُفْيَانَ أتَى عَلَى سَلْمَانَ وَصُهَيْبٍ وَبلاَلٍ في نَفَرٍ ، فقالوا : مَا أخَذَتْ سُيُوفُ اللهِ مِنْ عَدُوِّ الله مَأْخَذَهَا ، فَقَالَ أَبُو بَكْرٍرضي الله عنه: أتَقُولُون هَذَا لِشَيْخِ قُرَيْشٍ وَسَيدِهِمْ ؟ فَأتَى النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم، فَأخْبَرهُ ، فَقَالَ : (( يَا أَبَا بَكْرٍ ، لَعلَّكَ أغْضَبتَهُمْ ؟ لَئِنْ كُنْتَ أغْضَبْتَهُمْ لَقَدْ أغْضَبتَ رَبَّكَ )) فَأَتَاهُمْ فَقَالَ : يَا إخْوَتَاهُ ، أغْضَبْتُكُمْ ؟ قالوا : لاَ ، يَغْفِرُ اللهُ لَكَ يَا أُخَيَّ . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah 'Aa'idh bin 'Amr Al Muzaniy. katika maswahaba wa Bay'ah ya Ridhwaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Abu Sufyaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) alipita kwenye kikundi cha watu akiwemo Salman, Suhayb na Bilaal (Radhwiya Allaahu 'anhu) wakasema: "Panga za Allaah hazijatekeleza haki yake kwa adui wa Allaah." Abu Bakr akasema: "Mnasema haya kwa mzee na bwana wa Maquraysh?" Wakaja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakampa habari. Akasema: "Ee Abu Bakr! Nimekuudhini? ikiwa umewaudhi umemkasirisha Mola wako." Akaenda kwao akawaambia: "Ndugu zangu, je nimewaudhi?" Wakasema: "Hapana, Ee ndugu yetu Allaah Akughufirie." [Muslim]





Hadiyth – 3

وعن سهل بن سعد رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( أَنَا وَكَافلُ اليَتِيمِ في الجَنَّةِ هَكَذا )) وَأَشارَ بالسَّبَّابَةِ وَالوُسْطَى ، وَفَرَّجَ بَيْنَهُمَا . رواه البخاري .

Na imepokewa kutoka kwa Sa'ad bin Sahl (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mimi na mwenye kumsimamia yatima tuko Peponi kama hivi." Akaashiria kwa kidole cha shahada na cha kati na kupambanua baina yake." [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( كَافلُ اليَتيِم لَهُ أَوْ لِغَيْرِهِ أَنَا وَهُوَ كَهَاتَيْنِ في الجَنَّةِ )) وَأَشَارَ الرَّ‌اوِي وَهُوَ مَالِكُ بْنُ أنَس بالسَّبَّابَةِ وَالوُسْطَى . رواه مسلم .

Na imepokewa na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mimi na mwenye kumsimamia yatima wake au mwengineo, mimi na yeye tutakuwa hivi Peponi." Maalik bin Anas ambaye ndie mpokezi akaashiria kwa kidole cha shahada na cha kati. [Muslim]





Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( لَيْسَ المِسْكينُ الَّذِي تَرُدُّهُ التَّمْرَةُ وَالتَّمْرَتَانِ ، وَلا اللُّقْمَةُ وَاللُّقْمَتَانِ إِنَّمَا المِسكِينُ الَّذِي يَتَعَفَّفُ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية في الصحيحين : (( لَيْسَ المِسكِينُ الَّذِي يَطُوفُ عَلَى النَّاسِ تَرُدُّهُ اللُّقْمَةُ واللُّقْمَتانِ ، وَالتَّمْرَةُ والتَّمْرَتَانِ ، وَلَكِنَّ المِسْكِينَ الَّذِي لاَ يَجِدُ غنىً يُغْنِيه ، وَلاَ يُفْطَنُ بِهِ فَيُتَصَدَّقَ عَلَيهِ ، وَلاَ يَقُومُ فَيَسْأَلُ النَّاسَ )) .

Na imepokewa na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Si maskini mwenye kurudisha kwa ajili ya tende moja au mbili. hakika maskini ni yule anayeacha kuomba pamoja na ufakiri wake." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Katika riwaayah iliyo katika Sahihi Mbili: "Sio maskini mwenye kuwazungukia watu akapewa tonge moja au mbili na tende moja au mbili lakini maskini ni yule asiyepata cha kumtosheleza wala hajulikani ili akapewa sadaka wala haombi."





Hadiyth – 6

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ: عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( السَّاعِي عَلَى الأَرْمَلَةِ وَالمِسْكِينِ ، كَالمُجَاهِدِ في سَبيلِ اللهِ )) وَأحسَبُهُ قَالَ : (( وَكالقَائِمِ الَّذِي لاَ يَفْتُرُ ، وَكَالصَّائِمِ الَّذِي لاَ يُفْطِرُ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Na imepokewa na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kumsimamia mjane na maskini (kwa matumizi) ni kama Mujaahid katika Njia ya Allaah." Na nadhani alisema: "Na ni kama anayeswali usiku pasi na kupumzika na mafungaji asiyekula." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 7

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ: عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( شَرُّ الطَّعَامِ طَعَامُ الوَلِيمَةِ ، يُمْنَعُهَا مَنْ يَأتِيهَا ، وَيُدْعَى إِلَيْهَا مَنْ يَأْبَاهَا ، وَمَنْ لَمْ يُجِبِ الدَّعْوَةَ فَقَدْ عَصَى اللهَ وَرَسُولَهُ )) رواه مسلم .

وفي رواية في الصحيحين ، عن أَبي هريرة من قوله : (( بئْسَ الطَّعَامُ طَعَامُ الوَلِيمَةِ يُدْعَى إِلَيْهَا الأغْنِيَاءُ ويُتْرَكُ الفُقَراءُ )) .

Na imepokewa na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Chakula kibaya kabisa ni chakula cha walima, kinanyimwa anayekiendea na hualikwa anayekikataa. Na asiyejibu mwaliko basi amemuasi Allaah na Rasuli wake." [Muslim]

Katika riwaayah iliyo katika Sahihi Mbili: Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwa kauli yake chakula kibaya ni cha walima. wanaalikwa kwayo matajiri na kuachwa mafakiri."





Hadiyth – 8

وعن أنس رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( مَنْ عَالَ جَارِيَتَيْن حَتَّى تَبْلُغَا جَاءَ يَوْمَ القِيَامَةِ أنَا وَهُوَ كَهَاتَيْنِ )) وضَمَّ أصَابِعَهُ . رواه مسلم .

Na imepokewa na Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Atakaye wasimamia mabinti wawili mpaka akabaleghe, atakuja siku ya Qiyaamah mimi na yeye ni kama hivi." Akavishikanisha vidole vyake viwili. [Muslim]





Hadiyth – 9

وعن عائشة رضي الله عنها ، قَالَتْ : دَخَلَتْ عَلَيَّ امْرَأةٌ وَمَعَهَا ابنتان لَهَا ، تَسْأَلُ فَلَمْ تَجِدْ عِنْدِي شَيئاً غَيْرَ تَمْرَةٍ وَاحدَةٍ ، فَأعْطَيْتُهَا إيَّاهَا فَقَسَمَتْهَا بَيْنَ ابْنَتَيْها ولَمْ تَأكُلْ مِنْهَا ، ثُمَّ قَامَتْ فَخَرجَتْ ، فَدَخَلَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم عَلَينَا ، فَأخْبَرْتُهُ فَقَالَ : (( مَنِ ابْتُليَ مِنْ هذِهِ البَنَاتِ بِشَيءٍ فَأحْسَنَ إلَيْهِنَّ ، كُنَّ لَهُ سِتراً مِنَ النَّارِ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwake 'Aa'ishah (Radhwiya Allaahu 'anha) amesema: "Aliingia kwangu mwanamke akiwa na binti zake wawili kuomba. sikuwa na chochote ila tende moja, ambayo nilimpatia, naye akaigawa mara mbili ili kuwapatia binti zake, naye hakula chochote. Kisha akasimama, akatoka. hapo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia, nami nikampasha habari kuhusu tukio hilo, akasema: "Mwenye kutahaniwa na mabinti hawa kwa chochote, naye akawafanyia ihsani, watakuwa ni kinga kwake na Moto." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 10

وعن عائشة رضي الله عنها ، قَالَتْ : جَاءتني مِسْكينةٌ تَحْمِلُ ابْنَتَيْنِ لَهَا ، فَأطْعَمْتُها ثَلاثَ تَمرَات ، فَأعْطَتْ كُلَّ وَاحِدَة مِنْهُمَا تَمْرَةً وَرَفَعتْ إِلَى فِيها تَمْرَةً لِتَأكُلها ، فَاسْتَطعَمَتهَا ابْنَتَاهَا ، فَشَقَّتِ التَّمْرَةَ الَّتي كَانَتْ تُريدُ أنْ تَأكُلَهَا بَيْنَهُما ، فَأعجَبَنِي شَأنُهَا ، فَذَكَرْتُ الَّذِي صَنَعَتْ لرسولِ الله صلى الله عليه وسلم، فَقَالَ : (( إنَّ الله قَدْ أوْجَبَ لَهَا بها الجَنَّةَ ، أَوْ أعتَقَهَا بِهَا مِنَ النَّارِ )) رواه مسلم .

Imepokewa kwa 'Aa'ishah (Radhwiya Allaahu 'anha) amesema: "Maskini alikuja kwangu na mabinti wawili. Nikampa tende tatu, naye akampatia kila mmoja wao tende, akanyanyua moja mdomoni mwake ili aile. Mabinti zake wakaitaka, akagawa baina yao tende aliotaka kuila. Bikapendezwa na aliochofanya, nikamtajia jambo hilo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "hakika Allaah Amewajibisha kuingia kwake Peponi kwa kitendo hicho au kumwacha nacho na Moto." [Muslim]





Hadiyth – 11

وعن أَبي شُرَيحٍ خُوَيْلِدِ بن عمرو الخزاعِيِّ رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم: (( اللَّهُمَّ إنِّي أُحَرِّجُ حَقَّ الضَّعِيفَينِ : اليَتِيم وَالمَرْأةِ )) حديث حسن رواه النسائي بإسناد جيد .

Imepokewa kutoka kwa Abu Shurayh Khuwaylid bin 'Ammr Al-Khuzaa'iyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ee Allaah! Hakika nimemtangaza kuwa mwenye dhambi yeyote anayepoteza haki ya wanyonge wawili: Yatima na mwanamke." [Hadiyth hasan iliyonukuliwa na An-Nasaa'iy kwa isnad nzuri].





Hadiyth – 12

وعن مصعب بن سعد بن أَبي وقَّاص رضي الله عنهما ، قَالَ : رَأى سعد أنَّ لَهُ فَضْلاً عَلَى مَنْ دُونَهُ ، فَقَالَ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم: (( هَلْ تُنْصرُونَ وتُرْزَقُونَ إلاَّ بِضُعَفَائِكُمْ )) رواه البخاري هكذا مُرسلاً ، فإن مصعب بن سعد تابعيٌّ ، ورواه الحافظ أَبُو بكر البرقاني في صحيحه متصلاً عن مصعب ، عن أبيه رضي الله عنه.

Amesema Musw'ab bin Sa'ad bin waqqaasw (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Sa'ad aliona yeye ni mwenye fadhila kuliko wengine. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akasema: "Hamnusuriwi na kuruzikiwa ila kwa wanyonge wenu." [Al-Bukhaariy ameipokea hivi Mursal, kwani Musw'ab bin sa'ad ni Taabi'iyy, na ameipokea Haafidh Abuu Bakr Al-Barqaaniy katika sahihi yake toka kwa Musw'ab kwa baba yake Radhwiya Allaahu 'anhu]





Hadiyth – 13

وعن أَبي الدَّرداءِ عُويمر رضي الله عنه، قَالَ : سمعتُ رَسُولَ الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( ابْغُوني الضُّعَفَاء ، فَإنَّمَا تُنْصَرُونَ وتُرْزَقُونَ ، بِضُعَفَائِكُمْ )) رواه أَبُو داود بإسناد جيد .

Kutoka kwake Abu Dardaa' 'Uwaymir Amesema: "Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Nisaidieni (kwa kuwasaidia) wanyonge, hakika mnanusuriwa na kuruzukiwa kwa sababu ya wanyonge wenu." [Abuu Daawuud kwa Isnaad nzuri]
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب الوصية بالنساء

034-Mlango Wa Wasia Kwa Wanawake



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:

وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ﴿١٩﴾

Na kaeni nao kwa wema. [An-Nisaa: 19]



وَلَن تَسْتَطِيعُوا أَن تَعْدِلُوا بَيْنَ النِّسَاءِ وَلَوْ حَرَصْتُمْ ۖ فَلَا تَمِيلُوا كُلَّ الْمَيْلِ فَتَذَرُوهَا كَالْمُعَلَّقَةِ ۚ وَإِن تُصْلِحُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٢٩﴾

Na wala hamtoweza kuadilisha baina ya wake japokuwa mkipania. Basi msimili muelemeo wote (kwa mke mmoja) mkamuacha (mwengine) kama kining’inio. Na mkisuluhisha na mkawa na taqwa, basi hakika Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [An-Nisaa: 129]





Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( اسْتَوْصُوا بالنِّساءِ خَيْراً ؛ فَإِنَّ المَرْأَةَ خُلِقَتْ مِنْ ضِلعٍ ، وَإنَّ أعْوَجَ مَا في الضِّلَعِ أعْلاهُ ، فَإنْ ذَهَبتَ تُقيمُهُ كَسَرْتَهُ ، وَإنْ تَرَكْتَهُ ، لَمْ يَزَلْ أعْوجَ ، فَاسْتَوصُوا بالنِّساءِ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية في الصحيحين : (( المَرأةُ كالضِّلَعِ إنْ أقَمْتَهَا كَسَرْتَهَا ، وَإن اسْتَمتَعْتَ بِهَا ، اسْتَمتَعْتَ وفِيهَا عوَجٌ )) .

وفي رواية لمسلم : (( إنَّ المَرأةَ خُلِقَت مِنْ ضِلَع ، لَنْ تَسْتَقِيمَ لَكَ عَلَى طَريقة ، فإن اسْتَمْتَعْتَ بِهَا اسْتَمْتَعْتَ بِهَا وَفيهَا عوَجٌ ، وإنْ ذَهَبْتَ تُقِيمُهَا كَسَرْتَها ، وَكَسْرُهَا طَلاَقُهَا )) .

Na imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nawausieni kuwafanyia wema wanawake, kwani mwanamke ameumbwa kutokana na ubavu, na sehemu laini na yenye matatizo katika ubavu ni sehemu ya juu. Ukijaribu kuinyoosha, utaivunja; na ukiiacha, itabaki kombo. Nawausieni kuwatendea wema wanawake. [Al-Bukhaariy na Muslim]

Katika riwaayah iliyo katika Sahihi Mbili: ((Mwanamke ni kama mbavu, ukuiunyoosha utauvunja. Na ukitaka kupata faida kwayo, itabidi upate faida na ujongo wake)).

Katika riwaayah ya Muslim: ((Hakika mwanamke ameumbwa kutokana na ubavu. Hakuna njia ya kuunyoosha. Ukitaka kupata faida kwayo, itabidi upate faida na ujongo wake. Na ukitaka kuunyoosha, utauvunja na kuuvunja kwako ni kumpatia talaka)).





Hadiyth – 2

وعن عبد الله بن زَمْعَةَ رضي الله عنه: أنَّهُ سَمِعَ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم يَخْطُبُ ، وَذَكَرَ النَّاقَةَ وَالَّذِي عَقَرَهَا ، فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( إِذ انْبَعَثَ أشْقَاهَا انْبَعَثَ لَهَا رَجُلٌ عَزيزٌ ، عَارِمٌ مَنيعٌ في رَهْطِهِ )) ، ثُمَّ ذَكَرَ النِّسَاءَ ، فَوعَظَ فِيهنَّ ، فَقَالَ : (( يَعْمِدُ أحَدُكُمْ فَيَجْلِدُ امْرَأتَهُ جَلْدَ العَبْدِ فَلَعَلَّهُ يُضَاجِعُهَا مِنْ آخِرِ يَومِهِ )) ثُمَّ وَعَظَهُمْ في ضَحِكِهمْ مِنَ الضَّرْطَةِ ، وَقالَ : (( لِمَ يَضْحَكُ أَحَدُكُمْ مِمَّا يَفْعَلُ ؟! )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwake 'Abdillaahi bin Zam'ah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akihhutubu, akamtaja ngamia, na yule aliyemchinja. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akasema: "Pale alipochomoka haraka muovu wao mkuu. [Ash-Shams: 12]. Alimrukia muovu wao mwenye nguvu, mfisadi, mwenye kinga ya watu wake (akamchinja)." Kisha akataja wanawake, akawa waadhi kuhusu wao, akasema: "Mmoja wenu anampiga mkewe kipigo cha mtumwa, na huenda mwisho wa siku akamwingilia." Kisha akawadhia juu ya kucheka kwao kwa sababu ya kutokwa na upepo, akasema: "kwa nini mmoja wenu anacheka analolifanya?" [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( لاَ يَفْرَكْ مُؤْمِنٌ مُؤْمِنَةً إنْ كَرِهَ مِنْهَا خُلُقاً رَضِيَ مِنْهَا آخَرَ )) ، أَوْ قَالَ : (( غَيْرَهُ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Muumini mwanamume asimchukie Muumini mwanamke. Akichukizwa na tabia yake moja, ataridhika naye kwa tabia nyengine." [Muslim]





Hadiyth – 4

وعن عمرو بن الأحوصِ الجُشَمي رضي الله عنه: أنَّهُ سَمِعَ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم في حَجَّةِ الوَدَاعِ يَقُولُ بَعْدَ أنْ حَمِدَ الله تَعَالَى ، وَأثْنَى عَلَيهِ وَذَكَّرَ وَوَعظَ ، ثُمَّ قَالَ : (( ألا وَاسْتَوصُوا بالنِّساءِ خَيْراً ، فَإِنَّمَا هُنَّ عَوَانٍ عِنْدَكُمْ لَيْسَ تَمْلِكُونَ مِنْهُنَّ شَيْئاً غَيْرَ ذلِكَ إلاَّ أنْ يَأتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُبَيِّنَةٍ ، فَإنْ فَعَلْنَ فَاهْجُرُوهُنَّ في المَضَاجِع ، وَاضْرِبُوهُنَّ ضَرباً غَيْرَ مُبَرِّحٍ ، فإنْ أطَعْنَكُمْ فَلا تَبْغُوا عَلَيهنَّ سَبيلاً ؛ ألاَ إنَّ لَكُمْ عَلَى نِسَائِكُمْ حَقّاً ، وَلِنِسَائِكُمْ عَلَيْكُمْ حَقّاً ؛ فَحَقُّكُمْ عَلَيهِنَّ أنْ لا يُوطِئْنَ فُرُشَكُمْ مَنْ تَكْرَهُونَ ، وَلا يَأْذَنَّ في بُيُوتِكُمْ لِمَنْ تَكْرَهُونَ ؛ ألاَ وَحَقُّهُنَّ عَلَيْكُمْ أنْ تُحْسِنُوا إِلَيْهِنَّ في كِسْوَتِهنَّ وَطَعَامِهنَّ )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن صحيح )) .

Na 'Ammr bin Al-Ahwasw Al- Jushamiyy' (Radhwiya Allaahu 'anhu) amemsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema katiak Hajjatil Wadaa' baada ya kumhimidi na kumsifu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), akakumbusha na kuwaidhinkisha akasema: "Jueni! nawausieni kuwatendea wema wanawake, kwani wao ni wasaidizi wenu, hamna mnachomiliki kwao isipokuwa hicho kustarehe nao isipokuwa wanapotenda uovu wa wazi. Wakifanya hivyo wahameni katika malazi, na wapigeni pigo lisiloumiza. Wakiwatii msiwatafutie njia (ya kuwaudhi). Jueni! Hakika nyinyi mna haki juu ya wake zenu, na wake zenu wana haki juu yenu. Haki yenu juu yao ni kutomruhusu mnayemchukia kulala katika vitanda vyenu, wala wasiwaruhusu kuingia majumbani mwenu mnayemchukia. Fahamuni! Na haki zao juu yenu ni kuwafanyia hisani katika mavazi na chakula chao." [At- Tirmidhiy, na akasema: Hadiyth Swahiyh]





Hadiyth – 5

وعن معاوية بن حيدة رضي الله عنه، قَالَ : قُلْتُ : يَا رَسُول الله ، مَا حق زَوجَةِ أَحَدِنَا عَلَيهِ ؟ قَالَ : (( أنْ تُطْعِمَهَا إِذَا طعِمْتَ ، وَتَكْسُوهَا إِذَا اكْتَسَيْتَ ، وَلاَ تَضْرِبِ الوَجْهَ ، وَلا تُقَبِّحْ ، وَلا تَهْجُرْ إلاَّ في البَيْتِ )) حديثٌ حسنٌ رواه أَبُو داود.

imepokewa kutoka kwake Mu'aawiyyah bin Haydah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ni ipi haki ya mke wa mmoja wetu kwa mumewe?" Akajibu: "Ni kumlisha anapokula, kumvisha anapovaa wala usimpige uso wala usimkaripie wala usimhame ila nyumbani tu." [ Hadiyth Hasan iliyonukuliwa na Abu Daawuud]





Hadiyth – 6

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( أكْمَلُ المُؤمِنِينَ إيمَاناً أحْسَنُهُمْ خُلُقاً ، وخِيَارُكُمْ خياركم لِنِسَائِهِمْ )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن صحيح )) .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Muumini mkamilifu wa Iymaani ni mzuri wa tabia, na wabora wenu ni wabora wenu kwa wake zao." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hahiyth Hasan Swahiyh]





Hadiyth – 7

وعن إياس بن عبد الله بن أَبي ذباب رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( لاَ تَضْرِبُوا إمَاء الله )) فجاء عُمَرُ رضي الله عنه إِلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم، فَقَالَ :ذَئِرْنَ النِّسَاءُ عَلَى أزْوَاجِهِنَّ ، فَرَخَّصَ في ضَرْبِهِنَّ ، فَأطَافَ بآلِ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم نِسَاءٌ كَثيرٌ يَشْكُونَ أزْواجَهُنَّ ، فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( لَقَدْ أطَافَ بِآلِ بَيتِ مُحَمَّدٍ نِسَاءٌ كثيرٌ يَشْكُونَ أزْوَاجَهُنَّ لَيْسَ أولَئكَ بخيَارِكُمْ )) رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .

Na imepokewa kutoka kwake Iyaas bin 'Abdillaah bin Abu Dhubaab (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Msiwapige wajakazi (wanawake) wa Allaah." Akaja 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Wanawake wamekuwa majasiri juu ya waume zao." Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaruhusu wawachape wake zao. Wanawake wakawazungukia wakeze Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakishtaki kupigwa na waume zao. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Hakika wanawake wengi wamezunguka katika nyumba za Muhammad (wakeze) wakiwashtakia waume zao, waume hao si bora miongoni mwenu." [Abu Daawuud kwa Isnaad Swahiyh]





Hadiyth – 8

وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما : أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( الدُّنْيَا مَتَاعٌ ، وَخَيرُ مَتَاعِهَا المَرْأَةُ الصَّالِحَةُ )) رواه مسلم .

'Abdillaah bin 'Ammr bin Al- 'Aasw (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: " Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Dunia ni starehe, na bora ya starehe ni mke mwema." [Muslim]
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب حق الزوج عَلَى المرأة

035-Mlango Wa Haki Ya Mume Juu Ya Mke



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:

الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ ۚ فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ اللَّـهُ﴿٣٤﴾

Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah Amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na pia kwa ambayo wanatoa katika mali zao. Basi wanawake wema ni wale watiifu wenye kujihifadhi katika hali ya kutokuweko waume zao kwa kuwa Allaah Ameamrisha wajihifadhi. [An-Nisaa: 34]





Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( إِذَا دَعَا الرَّجُلُ امرَأتَهُ إِلَى فرَاشِهِ فَلَمْ تَأتِهِ ، فَبَاتَ غَضْبَانَ عَلَيْهَا ، لَعَنَتْهَا المَلائِكَةُ حَتَّى تُصْبحَ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية لهما : (( إِذَا بَاتَت المَرأةُ هَاجِرَةً فِرَاشَ زَوْجِهَا لَعَنَتْهَا المَلاَئِكَةُ حَتَّى تُصْبحَ )) .

وفي رواية قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( والَّذِي نَفْسِي بيَدِهِ مَا مِنْ رَجُلٍ يَدْعُو امْرَأتَهُ إِلَى فِرَاشهِ فَتَأبَى عَلَيهِ إلاَّ كَانَ الَّذِي في السَّمَاء سَاخطاً عَلَيْهَا حَتَّى يَرْضَى عَنها )) .

Na imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mume anapomuita mkewe kitandani mwake wala asije, akalala akiwa amemkasirikia mkewe, Malaaikah watamlaani mke huyo mpaka apambazukiwe." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na katika riwaayah yao wawili: "Mke anapolala kwa kuhama kitanda cha mumewe, Malaaikah humlani mpaka kupambazuke."

Katika riwaayah: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Naapa kwa ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakuna mwanamume yoyote anamuita mkewe kitandani, akamkatalia isipokuwa Aliye mbinguni Humkasirikia mpaka mume Amridhie."





Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه أيضاً : أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( لاَ يَحِلُّ لامْرَأةٍ أنْ تَصُومَ وزَوْجُهَا شَاهدٌ إلاَّ بإذْنِهِ ، وَلاَ تَأذَنَ في بَيْتِهِ إلاَّ بِإذنِهِ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ وهذا لفظ البخاري .

Imepokewa kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Haifai kwa mke kufunga na mumewe yuko (mjini) ila kwa idhini yake. Wala siruhusa (kwa mke) kumruhusu mtu kuingia nyumbani (kwao) ila kwa idhini ya mumewe." [Al-Bukhaariy na Muslim] Na hii ni lafdhi ya Al-Bukhaariy





Hadiyth – 3

وعن ابن عمر رضي الله عنهما، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( كلكم رَاعٍ ، وَكُلُّكُمْ مَسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ : وَالأمِيرُ رَاعٍ ، والرَّجُلُ رَاعٍ عَلَى أهْلِ بَيتِهِ ، وَالمَرْأةُ رَاعِيةٌ عَلَى بَيْتِ زَوْجها وَوَلَدهِ ، فَكُلُّكُمْ رَاعٍ ، وَكُلُّكُمْ مَسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Imepokewa kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhummaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kila mmoja wenu ni mchunga, na kila mmoja wenu ataulizwa alio wachunga. Amiri ni mchunga, na mume ni mchunga wa watu wa nyumbani kwake, na mke ni mchunga katika nyumba ya mumewe na watoto wake; nyote ni wachunga mtaulizwa mlivyovichunga." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]





Hadiyth – 4

وعن أَبي علي طَلْق بن علي رضي الله عنه: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( إِذَا دَعَا الرَّجُلُ زَوْجَتهُ لحَاجَتِهِ فَلْتَأتِهِ وَإنْ كَانَتْ عَلَى التَّنُور)) . رواه الترمذي والنسائي ، وَقالَ الترمذي : (( حديث حسن صحيح )) .

Na imepokewa kutoka kwake Abuu 'Aliy Twalqbin 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Pindi mume anapomuita mkewe kwa haja zake (jimai) aje kwake mara moja hata akiwa kwenye tanuri." [At-Tirmidhiy na An-Nasaa'iy, na akasema At-Tirmidhiy kuwa ni Hadiyth Hasan Swahiyh]





Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( لَوْ كُنْتُ آمِراً أحَداً أنْ يَسْجُدَ لأحَدٍ لأمَرْتُ المَرأةَ أنْ تَسْجُدَ لزَوجِهَا )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Lau ningeliweza kumuamrisha mtu amsujudie binaadamu, ningemuamuru mke kumsujudia mumewe." [At-Tirmidhiy na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]





Hadiyth – 6

وعن أم سَلَمَة رضي الله عنها ، قَالَتْ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: (( أيُّمَا امْرَأةٍ مَاتَتْ ، وَزَوْجُهَا عَنْهَا رَاضٍ دَخَلَتِ الجَنَّةَ )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Umm Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwanamke aliyekufa na mumewe yu radhi naye, ataingia Peponi." [At-Tirmidhiy na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]





Hadiyth – 7

وعن معاذ بن جبل رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( لاَ تُؤْذِي امْرَأةٌ زَوْجَهَا في الدُّنْيَا إلاَّ قَالَتْ زَوْجَتُهُ مِنَ الحُورِ العِينِ لاَ تُؤذِيهِ قَاتَلكِ اللهُ ‍! فَإِنَّمَا هُوَ عِنْدَكِ دَخِيلٌ يُوشِكُ أنْ يُفَارِقَكِ إِلَيْنَا )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن )) .

Na imepokewa kutoka kwa Mu'aadh bin Jabal (Radhwiya Allaahu 'anhu) Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwanamke hamuudhi mumewe duniani ila anasema mkewe katika Huuril 'Iyn watamwambia, 'Usimuudhi, Allaah Akulaani! Hakika yeye ni mgeni aliye kwako na karibuni atakuacha na kuungana nasi." [At-Tirmidhiy na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]





Hadiyth – 8

وعن أسامة بن زيد رضي الله عنهما ، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( مَا تَرَكْتُ بَعْدِي فِتْنَةً هِيَ أضَرُّ عَلَى الرِّجَالِ مِنَ النِّساء )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Usaamah bin Zayd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Sijaacha baada yangu fitna iliyo na madhara makubwa kwa wanaume kuliko ile ya wanawake." [Al-Bukhaariy na Muslim]
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب النفقة عَلَى العيال

036-Mlango Wa kuilisha Familia



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:

وَعَلَى الْمَوْلُودِ لَهُ رِزْقُهُنَّ وَكِسْوَتُهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ﴿٢٣٣﴾

Na ni juu ya mzazi wa kiume kuwapatia chakula chao na nguo kwa mujibu wa ada. [Al-Baqarah: 233]

لِيُنفِقْ ذُو سَعَةٍ مِّن سَعَتِهِ ۖ وَمَن قُدِرَ عَلَيْهِ رِزْقُهُ فَلْيُنفِقْ مِمَّا آتَاهُ اللَّـهُ ۚ لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا مَا آتَاهَا ﴿٧﴾

Ili mwenye wasaa agharimu kwa wasaa wake, na aliyebaniwa riziki yake, basi agharimie katika kile Alichompa Allaah. Allaah Haikalifishi nafsi yeyote ile isipokuwa kwa kile Alichoipa. [Atw-Twalaaq: 7]

وَمَا أَنفَقْتُم مِّن شَيْءٍ فَهُوَ يُخْلِفُهُ ﴿٣٩﴾

Na kitu chochote mtoacho, basi Yeye Atakilipa [Sabaa: 39]





Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( دِينَارٌ أنْفَقْتَهُ في سَبيلِ اللهِ ، وَدِينار أنْفَقْتَهُ في رَقَبَةٍ ، وَدِينارٌ تَصَدَّقْتَ بِهِ عَلَى مِسْكِينٍ ، وَدِينَارٌ أنْفَقْتَهُ عَلَى أهْلِكَ ، أعْظَمُهَا أجْراً الَّذِي أنْفَقْتَهُ عَلَى أهْلِكَ )) رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Dinari unayotumia katika Njia ya Allaah (jihaad), na Dinari unayotumia kumwacha huru mtumwa, na Dinari unayoitoa sadaka kwa maskini, na Dinari unayotumia kwa familia yako, yenye ujira mkubwa zaidi ni ile unayotumia kwa familia yako." [Muslim]





Hadiyth – 2

وعن أَبي عبد الله ، ويُقالُ لَهُ : أَبو عبد الرحمان ثَوبَان بن بُجْدُد مَوْلَى رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( أفْضَلُ دِينَارٍ يُنْفقُهُ الرَّجُلُ : دِينَارٌ يُنْفِقُهُ عَلَى عِيَالِهِ ، وَدينَارٌ يُنْفقُهُ عَلَى دَابَّتِهِ في سَبيلِ الله ، وَدِينارٌ يُنْفقُهُ عَلَى أصْحَابهِ في سَبيلِ اللهِ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu 'Abdillaahi-pia anajulikana kama Abu 'Abdur-Rahman - Thawbaan bin Bujdud, mtumishi wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Dinari iliyo bora zaidi inayotumiwa na mtu ni ile anayotumia kwa familia yake, na Dinari anayoitumia kwa mnyama katika Njia ya Allaah, na kisha Dinari anayoitumia kwa sahibu zake katika Njia ya Allaah." [Muslim]





Hadiyth – 3

وعن أمِّ سَلمَة رَضي الله عنها ، قَالَتْ : قُلْتُ : يَا رَسُول الله ، هَلْ لِي أجرٌ فِي بَنِي أَبي سَلَمَة أنْ أُنْفِقَ عَلَيْهِمْ ، وَلَسْتُ بِتَارِكتهمْ هكَذَا وَهكَذَا إنَّمَا هُمْ بَنِيّ ؟ فَقَالَ : (( نَعَمْ ، لَكِ أجْرُ مَا أنْفَقْتِ عَلَيْهِمْ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Amesema Umm Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa alimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Je, nitakuwa na ujira nitakapotumia kwa ajili ya watoto wa Abi Salamah, ilhali mimi siwezi kuwaacha wakitangatanga huku na kule ambapo wao ni watoto wangu." Akasema: "Ndio, utapata ujira kwa unachotumia kwao." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 4

وعن سعد بن أَبي وقاص رضي الله عنه في حديثه الطويل الَّذِي قدمناه في أول الكتاب في باب النِّيَةِ : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ لَهُ : (( وإنَّكَ لَنْ تُنْفِقَ نَفَقَةً تَبْتَغِي بِهَا وَجْهَ اللهِ إلاَّ أُجِرْتَ بِهَا حَتَّى مَا تَجْعَلُ في فيِّ امرأتِك )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Sa'ad bin Abu Waqqaasw (Radhwiya Allaahu 'anhu) katika hadiyth ndefu tuliyo itanguliza mwanzo wa kitabu hiki katika mlango wa Nia kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Na hakika wewe hutatumia pesa kutaka radhi za Allaah isipokuwa utapata ujira kwayo mpaka utakacho jaalia katika mdomo wa mkeo (kumlisha) [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 5

وعن أَبي مسعود البدري رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( إِذَا أنْفَقَ الرَّجُلُ عَلَى أَهْلِهِ نَفَقَةً يَحْتَسِبُهَا فَهِيَ لَهُ صَدَقَةٌ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Mas'uud Al-Badriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtu akiipa familia yake matumizi akiyatarajia thawabu basi hiyo ni sadaqa yake." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 6

وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( كَفَى بِالمَرْءِ إثْمَاً أنْ يُضَيِّعَ مَنْ يَقُوتُ )) حديث صحيح رواه أَبُو داود وغيره .

ورواه مسلم في صحيحه بمعناه ، قَالَ : (( كَفَى بِالمَرْءِ إثْمَاً أنْ يحْبِسَ عَمَّنْ يَمْلِكُ قُوتَهُ )) .

Na imepokewa kutoka kwa 'Abdillaahi bin 'Amr bin al-'Aasw (Radhwiya Allaahu 'anhummaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Inatosha mtu kuwa na dhambi kwa kumtupa anyemlisha." Hadiyth Swahiyh [ Abu Daawuud na wengineo]

Muslim ameinukuu katika Sahihi yake kwa maana yake: "Yatosha kwa mtu kuwa na dhambi kwa kumzuilia rizki anayemtegemea."





Hadiyth – 7

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( مَا مِنْ يَوْمٍ يُصْبِحُ العِبَادُ فِيهِ إلاَّ مَلَكانِ يَنْزلاَنِ ، فَيقُولُ أحَدُهُمَا : اللَّهُمَّ أعْطِ مُنْفقاً خَلَفاً ، وَيَقُولُ الآخَرُ : اللَّهُمَّ أعْطِ مُمْسِكاً تلَفاً )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna siku yoyote waja wanapambazuka ndani yake, ila Malaika wawili wanateremka, mmoja wao anasema: 'Ee Allaah, mpe badali mwenye kutoa.' Na mwengine anasema: 'Ee Allaah, mpe hasara mwenye kuzuia' " [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 8

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( اليَدُ العُلْيَا خَيْرٌ مِنَ اليَدِ السُّفْلَى ، وَابْدَأ بِمَنْ تَعُولُ ، وَخَيْرُ الصَّدَقَةِ مَا كَانَ عَنْ ظَهْرِ غِنىً ، وَمَنْ يَسْتَعْفِفْ يُعِفَّهُ اللهُ ، وَمَنْ يَسْتَغْنِ يُغْنِهِ اللهُ )) رواه البخاري .

Na imepokewa kutoka kwake Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini. Anza kwa unayemlisha. Sadaka bora inakuwa kwa mwenye kujitosha. Anayejizuia Allaah Humtosheleza, na mwenye kukinai, Allaah Humkinaisha." [Al-Bukhaariy]
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب الإنفاق مِمَّا يحبُّ ومن الجيِّد

037-Mlango Wa Kutoa Ukipendacho Katika Vizuri



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:

لَن تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّىٰ تُنفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ﴿٩٢﴾

Hamtoweza kuufikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda. [Al-'Imraan: 92]



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا كَسَبْتُمْ وَمِمَّا أَخْرَجْنَا لَكُم مِّنَ الْأَرْضِ ۖ وَلَا تَيَمَّمُوا الْخَبِيثَ مِنْهُ تُنفِقُونَ ﴿٢٦٧﴾

Enyi walioamini! Toeni katika vizuri mlivyochuma na katika ambavyo Tumekutoleeni kutoka katika ardhi. Na wala msikusudie vibaya kutoka humo mkavitoa. [Al-Baqarah: 267]





Hadiyth – 1

عن أنس رضي الله عنه، قَالَ : كَانَ أَبُو طَلْحَةَ رضي الله عنه أكْثَرَ الأنْصَار بالمَدِينَةِ مَالاً مِنْ نَخْل ، وَكَانَ أَحَبُّ أمْوالِهِ إِلَيْه بَيْرَحَاء ، وَكَانتْ مُسْتَقْبلَةَ المَسْجِدِ وَكَانَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يَدْخُلُهَا وَيَشْرَبُ مِنْ مَاءٍ فِيهَا طَيِّب . قَالَ أنَسٌ : فَلَمَّا نَزَلَتْ هذِهِ الآيةُ: ( لَنْ تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّى تُنْفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ) قام أَبُو طَلْحَةَ إِلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم، فَقَالَ : يَا رَسُول الله ، إنَّ الله تَعَالَى أنْزَلَ عَلَيْكَ : ( لَنْ تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّى تُنْفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ) وَإنَّ أَحَبَّ مَالِي إِلَيَّ بَيْرَحَاءُ ، وَإنَّهَا صَدَقَةٌ للهِ تَعَالَى ، أرْجُو بِرَّهَا ، وَذُخْرَهَا عِنْدَ الله تَعَالَى ، فَضَعْهَا يَا رَسُول الله حَيْثُ أرَاكَ الله ، فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( بَخ! ذلِكَ مَالٌ رَابحٌ ، ذلِكَ مَالٌ رَابحٌ ، وقَدْ سَمِعْتُ مَا قُلْتَ ، وَإنِّي أرَى أنْ تَجْعَلَهَا في الأقْرَبينَ )) ، فَقَالَ أَبُو طَلْحَةَ : أفْعَلُ يَا رَسُول الله ، فَقَسَّمَهَا أَبُو طَلْحَةَ في أقَارِبِهِ ، وبَنِي عَمِّهِ . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): 'Abu Twalhah (Radhwiya Allaahu 'anhu) alikuwa na mali na mitende mingi kuliko Answari wote. Mali iliyompendeza zaidi ni shamba lilioko Bayrahaa', limeelekeana na Msikiti wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiingia humo na kunywa maji yake matamu. Amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): Ilipoteremka aya hii: "Hamtoweza kuufikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda." Abu Twalhah Radhwiya Allaahu 'anhu) alimwendea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Hakika Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amekuteremshia: "Hamtoweza kuufikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda." Hakika mali niipendayo sana ni shamba la Bayrahaa', nimelitoa sadaka kwa ajili ya Allaah nataraji kheri na ujira kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Ee Rasulu wa Allaah, liweke atakapokuonyesha Allaah." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Bakh! Hiyo ni mali yenye faida, hiyo ni mali yenye faida. Nimesikia uliyosema. Mimi naona uwape jamaa zako wa karibu." Abu Twalhah akasema: "Nitafanya, Ee Rasuli wa Allaah!" Abu Twalhah akaligawa kwa jamaa zake na binamu zake." [Al-Bukhaariy na Muslim]
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn





باب وجوب أمره أهله وأولاده المميزين

وسائر من في رعيته بطاعة الله تعالى ونهيهم عن المخالفة وتأديبهم

ومنعهم من ارتكاب مَنْهِيٍّ عَنْهُ

038-Mlango Wa Wajibu Wa Kuamrisha Mkewe, Wanawe Waliobaleghe na Wote Waliochini Yake Kumtii Allaah Aliyetukuka, na Kuwakataza Kukhalifu, na Kufanya Waliyokatazwa



Alhidaaya.com





قَالَ الله تَعَالَى:

وَأْمُرْ أَهْلَكَ بِالصَّلَاةِ وَاصْطَبِرْ عَلَيْهَا ﴿١٣٢﴾

Na amrisha ahli zako Swalaah, na dumisha kusubiri kwayo. Hatukuombi riziki. Sisi Ndio Tunaokuruzuku. Na khatima njema ni kwa wenye taqwa. [Twaahaa: 132]



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا ﴿٦﴾

Enyi walioamini! Jikingeni nafsi zenu na ahli zenu na moto. [At-Tahriym: 6]





Hadiyth – 1

عن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : أخذ الحسن بن علي رضي الله عنهما تَمْرَةً مِنْ تَمْر الصَّدَقَةِ فَجَعَلَهَا في فِيهِ ، فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( كَخْ كَخْ إرْمِ بِهَا ، أمَا عَلِمْتَ أنَّا لا نَأكُلُ الصَّدَقَةَ !؟ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية : (( أنَّا لا تَحِلُّ لَنَا الصَّدَقَةُ )) .

Amesema Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) Al-Hasan bin 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) Alichukua tende ya sadaqah akaitia mdomoni mwake akitaka kuila. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akamwambia: "Kikh! Kikh! Itupe, kwani hujui kuwa sisi hatuli sadaqah? [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]

Katika riwaayah nyingine: "Sadaqah si halali kwetu sisi."





Hadiyth – 2

وعن أَبي حفص عمر بن أَبي سلمة عبد الله بن عبد الأسدِ ربيبِ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : كُنْتُ غلاَماً في حجر رَسُول الله صلى الله عليه وسلم وَكَانَتْ يَدي تَطِيشُ في الصَّحْفَةِ ، فَقَالَ لي رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( يَا غُلامُ ، سَمِّ الله تَعَالَى ، وَكُلْ بيَمِينكَ ، وَكُلْ مِمَّا يَلِيكَ )) فَمَا زَالَتْ تِلْكَ طِعْمَتي بَعْدُ . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Abu afswi 'Umar bin Abu Salamah 'Abdillaah bin 'Abdil Asad (Radhwiya Allaahu 'anhu) mwanakambo wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nilikuwa mvulana katika nyumba ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), mkono wangu ulikuwa unazunguka kwenye sinia. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akaniambia: "Ee kijana! Mtaje Allaah Aliyetukuka, na kula kwa kulia kwako, na kula cha mbele yako." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]





Hadiyth – 3

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : سمعت رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( كُلُّكُمْ رَاعٍ ، وَكُلُّكُمْ مسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتهِ : الإمَامُ رَاعٍ وَمَسْؤولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ ، والرَّجُلُ رَاعٍ في أهْلِهِ وَمَسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ ، وَالمَرْأةُ رَاعِيَةٌ في بيْتِ زَوْجِهَا وَمَسْؤُولَةٌ عَنْ رَعِيَّتِهَا ، وَالخَادِمُ رَاعٍ في مَالِ سَيِّدِهِ وَمَسؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ ، فَكُلُّكُمْ رَاعٍ وَمَسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhummaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kila mmoja wenu ni mchunga, na kila mmoja wenu ataulizwa aliowachunga. Kiongozi ni mchunga ataulizwa aliowachunga, na mume ni mchunga kwa watu wa nyumbani kwake, na mke naye ni mchunga katika nyumba ya mumewe na watoto wake; hivyo kila mmoja wenu ni mchunga na nyote mtaulizwa kwa mlivyovichunga." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]





Hadiyth – 4

وعن عمرو بن شعيب ، عن أبيه ، عن جدهِ رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( مُرُوا أوْلادَكُمْ بِالصَّلاةِ وَهُمْ أبْنَاءُ سَبْعِ سِنينَ ، وَاضْرِبُوهُمْ عَلَيْهَا ، وَهُمْ أبْنَاءُ عَشْرٍ ، وَفَرِّقُوا بَيْنَهُمْ في المضَاجِعِ )) حديث حسن رواه أَبُو داود بإسناد حسن .

Na imepokewa kutoka kwa 'Amr bin Shu'ayb (Radhwiya Allaahu 'anhu) kutoka kwa babake kutoka kwa babu yake kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Waamrisheni watoto wenu kuswali wakiwa na miaka saba, na wapigeni (kuacha kuswali) wakiwa na miaka kumi na muwatenganishe katika malazi." [Hadiyth Hasan iliyonukuliwa na Abu Daawuud kwa Isnadi iliyo Hasan]





Hadiyth – 5

وعن أَبي ثُرَيَّةَ سَبْرَةَ بن معبدٍ الجُهَنِيِّ رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( عَلِّمُوا الصَّبِيَّ الصَّلاةَ لِسَبْعِ سِنِينَ ، وَاضْرِبُوهُ عَلَيْهَا ابْنَ عَشْرِ سِنِينَ )) حديث حسن رواه أَبُو داود والترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن )) .

ولفظ أَبي داود : (( مُرُوا الصَّبِيَّ بِالصَّلاةِ إِذَا بَلَغَ سَبْعَ سِنِينَ )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Thurayyah Sabrah bin Ma'bad Al-Juhaniyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Wafundisheni watoto Swalaah wakiwa na miaka saba, na wachapeni (wakiacha na kupuuza) wakiwa na miaka kumi." [Hadiyth Hasan iliyonukuliwa na Abu Daawuud na At-Tirmidhiy, naye akasema ni Hadiyth Hasan]

Na lafdhi Abu Daawuud: "Waamrisheni watoto Swalaah wakifika miaka saba."
 
Back
Top Bottom