Hizi ni baadhi ya post zangu za zamani
JE QUR'AN NI NAKALA YA BIBLIA?
UUMBAJI WA MBINGU NA ARDHI
Ni mara nyingi Ulaya na humu JF watu wamekuwa wakileta hoja kuwa Muhammad amekopi Biblia katika Maandiko ya Qur'an, lakini kibaya Zaidi wanasema maneno Bila kuthibitisha. Kwahiyo hawana tofauti na watu ambao wanaweweseka Tu na mambo ambayo hawayajui.
Nimeona nilete hoja Kwa kuthibitisha kupitia Maandiko ili tuwatoe uchafu katika ubongo wao.
Sasa nitaanza na Biblia,katika biblia uumbaji wa Mbingu na Ardhi umeelezwa Kwa mfulululizo wa story,kwamba siku ya Kwanza kuliumbwa hiki na ya pili hiki na kadhalika. Tuone Maandiko yanasemaje:
Mwanzo 1:1-31
[1]Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
In the beginning God created the heaven and the earth.
[2]Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
And the earth was without form, and void; and darkness was upon the face of the deep. And the Spirit of God moved upon the face of the waters.
[3]Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.
And God said, Let there be light: and there was light.
[4]Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza.
And God saw the light, that it was good: and God divided the light from the darkness.
[5]Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.
And God called the light Day, and the darkness he called Night. And the evening and the morning were the first day.
[6]Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji.
And God said, Let there be a firmament in the midst of the waters, and let it divide the waters from the waters.
[7]Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo.
And God made the firmament, and divided the waters which were under the firmament from the waters which were above the firmament: and it was so.
[8]Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili.
And God called the firmament Heaven. And the evening and the morning were the second day.
[9]Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo.
And God said, Let the waters under the heaven be gathered together unto one place, and let the dry land appear: and it was so.
[10]Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
And God called the dry land Earth; and the gathering together of the waters called he Seas: and God saw that it was good.
[11]Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo.
And God said, Let the earth bring forth grass, the herb yielding seed, and the fruit tree yielding fruit after his kind, whose seed is in itself, upon the earth: and it was so.
[12]Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
And the earth brought forth grass, and herb yielding seed after his kind, and the tree yielding fruit, whose seed was in itself, after his kind: and God saw that it was good.
[13]Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tatu.
And the evening and the morning were the third day.
[14]Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka;
And God said, Let there be lights in the firmament of the heaven to divide the day from the night; and let them be for signs, and for seasons, and for days, and years:
[15]tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya nchi; ikawa hivyo.
And let them be for lights in the firmament of the heaven to give light upon the earth: and it was so.
[16]Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia.
And God made two great lights; the greater light to rule the day, and the lesser light to rule the night: he made the stars also.
[17]Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi
And God set them in the firmament of the heaven to give light upon the earth,
[18]na kuutawala mchana na usiku na kutenga nuru na giza; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
And to rule over the day and over the night, and to divide the light from the darkness: and God saw that it was good.
[19]Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya nne.
And the evening and the morning were the fourth day.
[20]Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu.
And God said, Let the waters bring forth abundantly the moving creature that hath life, and fowl that may fly above the earth in the open firmament of heaven.
[21]Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
And God created great whales, and every living creature that moveth, which the waters brought forth abundantly, after their kind, and every winged fowl after his kind: and God saw that it was good.
[22]Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi.
And God blessed them, saying, Be fruitful, and multiply, and fill the waters in the seas, and let fowl multiply in the earth.
[23]Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tano.
And the evening and the morning were the fifth day.
[24]Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo.
And God said, Let the earth bring forth the living creature after his kind, cattle, and creeping thing, and beast of the earth after his kind: and it was so.
[25]Mungu akafanya mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
And God made the beast of the earth after his kind, and cattle after their kind, and every thing that creepeth upon the earth after his kind: and God saw that it was good.
[26]Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
And God said, Let us make man in our image, after our likeness: and let them have dominion over the fish of the sea, and over the fowl of the air, and over the cattle, and over all the earth, and over every creeping thing that creepeth upon the earth.
[27]Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
So God created man in his own image, in the image of God created he him; male and female created he them.
[28]Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
And God blessed them, and God said unto them, Be fruitful, and multiply, and replenish the earth, and subdue it: and have dominion over the fish of the sea, and over the fowl of the air, and over every living thing that moveth upon the earth.
[29]Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;
And God said, Behold, I have given you every herb bearing seed, which is upon the face of all the earth, and every tree, in the which is the fruit of a tree yielding seed; to you it shall be for meat.
[30]na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.
And to every beast of the earth, and to every fowl of the air, and to every thing that creepeth upon the earth, wherein there is life, I have given every green herb for meat: and it was so.
[31]Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.
And God saw every thing that he had made, and, behold, it was very good. And the evening and the morning were the sixth day.
Mwanzo 2:1-2
[1]Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote.
Thus the heavens and the earth were finished, and all the host of them.
[2]Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.
And on the seventh day God ended his work which he had made; and he rested on the seventh day from all his work which he had made.
Mpaka hapo tumeona uumbaji upande wa Biblia.
Sasa tofauti na Biblia,katika Qura'n uumbaji umefanyika katika nyakati sita na hakuna maelezo ya mfuatano WA kutoka moja mpaka Sita juu ya uumbaji,Bali habar za uumbaji zimeelezwa katika Aya tofauti tofauti katika kipindi chote cha kushuka qura'n Kwa miaka 23. Na kama haitoshi maelezo ya qura'n juu ya uumbaji Yana dhibitishwa na hoja za Kisayansi ambazo ni sahihi kama ilivyoelezwa na Muhammad (s.a.w)
Qur'an inaeleza kuwa Mwenyezi Mungu aliumba ardhi Kwa siku mbili:
"Sema: Hivyo nyinyi mnamkataa aliye umba ardhi katika siku mbili, na mnamfanyia washirika? Huyu ndiye Mola Mlezi wa walimwengu wote."
41:9
Kisha Mwenyezi Mungu akailekea mbingu ambayo ilikuwa Moshi akaiita pamoja na ardhi zikaambatana pamoja.
"Kisha akazielekea mbingu, na zilikuwa moshi, akaziambia hizo na ardhi: Njooni, kwa khiari au kwa nguvu! Vyote viwili vikasema: Tumekuja nasi ni wat'iifu."
41:11
"Basi akazifanya mbingu saba kwa siku mbili, na akazipangia kila mbingu mambo yake. Na tukaipamba mbingu ya chini kwa mataa na kwa ulinzi. Hichi ndicho kipimo cha Mwenyezi Mungu Mwenye Kujua."
41:12
Mpaka hapo tunaona kwamba uumbaji WA mbingu na ardhi umefanyika nyakati nne au siku nne.
Qur'an inasema halafu mbingu ambayo ni Moshi ili ambatanishwa na ardhi Kwa pamoja zikawa zimeshikamana,tuangalie Maandiko:
"Je! Hao walio kufuru hawakuona kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeambatana, kisha Sisi tukazibabandua? Na tukajaalia kwa maji kila kilicho hai? Basi je, hawaamini?"
21:30
Kwahiyo mpaka hapa tunaona kwamba,uumbaji WA mbingu na ardhi Kwa mujibu wa Qur'an,ulikuwa kama ifuatavyo;
Mwenyezi Mungu aliumba ardhi kisha akaichukua mbingu ambayo ilikuwa Moshi akaziambatanisha pamoja zikawa zimeshikana kisha baadae akaziachanisha na kuumbwa Kwa mbingu Saba na viliomo baina ya mbingu na ardhi.
Ukija katika Sayansi inadhibitisha utaratibu ule ule ulio elezwa na Qur'an
Sayansi inasema katika uumbaji, kulikuwa na gaseous mass with fine particles ambazo Kwa kiarabu (dukan) ambao INA maanisha Moshi,ambapo Moshi unaundwa na gaseous substratum na fine particles ambazo zinakuwa katika Hali ya ugumu na Hali ya kimiminika katika high temperature or low temperature.
Halafu baadae zikaachana baada ya kutokea mlipuko mkubwa,ambao ulipelekea kurushwa Kwa materials mbali mbali angani na kuundwa Kwa mbingu na vitu vingine kama sayari na nyota na bodies nyingine mbali mbali,rejea kwenye Bing Bang Theory.
Na kwakuongezea Tu ndio maana ukiangalia sayar kama Jupiter utakuta kuna gaseous kama helium na hydrogen, nyota kama jua ni gaseous tupu,hizo Kwa uchache Tu.
Na vile vile Qur'an imeeleza dunia katika uwingi na hivyo ikamaanisha huenda kukawa na uwezekano WA kuwepo dunia nyingine kama yetu ingawa Sayansi bado haijagundua Hilo swala,ingawa wanasema uwezekano huo upo katika galaxy nyingine ambayo IPO nje ya galaxy yetu,waliosoma au ambao wanapenda kusoma mambo ya anga nadhani wanajua nikisema Milk way galaxy namaanisha nini?
Kwahiyo kuna mambo mengi ambayo yameelezwa katika Qur'an ambapo bado. Sayansi haija yagundua huenda yakaja kugundulika na vizazi vijavyo huko.
Kwahiyo maelezo haya ni Uongo mkubwa Sana kusema kwamba Muhammad amekopi Maandiko ya Biblia wakati kuna tofauti kubwa Sana ya uumbaji WA Biblia na Qur'an.
Basi Muhammad atakuwa ni mtu mwenye akili Sana aone Maandiko ya Biblia ambayo hayawezi kudhibitishwa na Sayansi halafu ayabadilishe na yawe mazuri kiasi kwamba Sayansi iweze kuyadhibitisha yashahabiane na Quran. Na kumbuka Muhammad aliishi Karne ya 14 na Sayansi imedhibitisha Karne ya 20 baada ya kuwepo kwa dhana za kisasa za kiutafiti.
Hakika huo ndio ukubwa wa Maneno ya Mwenyezi Mungu,na ukweli siku zote ni WA kudumu na unashinda changamoto zote.
Naomba atayekuja kuchallenge huu Uzi wangu asije na Maneno matupu,Bali athibitishe Kwa maandiko kama Mimi nilivyofanya,vinginevyo zitakuwa porojo Tu.
Panapo majaliwa inshallah nitakuja na muendelezo wa part (2), lengo ni kuweka mambo Sawa maana uzushi umezidi sana humu ndani