Ramadhan Special Thread
Baadhi ya post zangu za Zamani....

JE QUR'AN NI NAKALA YA BIBLIA?

MFUMO WA UZAZI / HUMAN PRODUCTION

Kwanza nianze na mambo machache au utaratibu ambao unahusika moja Kwa moja na uzazi wa binadamu.

Mwanzo ni kurutubishwa Kwa Yai kwenye sehemu inaitwa fallopian tube,kinachotumika kurutubisha ni mbegu ya kiume (sperm) au kitalaam spermatozoon,kwahiyo kinachotakiwa ni tone dogo la manii ambalo Lina mbegu kama million 10. Na maji haya au tone hili la manii hutengenezwa na testicles (makende) na kuhifadhiwa hapo,halafu kuna glands ambazo zipo karibu na maeneo hayo ambazo huongeza au kutengeneza maji maji katika sperm.
Kwahiyo upandikizaji wa Yai ambalo tayar limepevuka hufanyika katika system ya uzazi ya mwanamke,na kupitia katika follopiana tube na kuelekea katika uterus na huko hujishikiza na hatimaye placenta inatengenezwa au inajitengeneza, na Kwa mfano kama upandikizaji wa Yai ukifanyika katika follopian tube badala ya uterus basi huo ujauzito utaharibika.

Na baada ya embryo kuweza kuonekana na jicho la kawaida basi huonekana kama muunganiko WA kanyama kadogo ambako si rahisi kujua kama binadamu,na inaendelea kukua katika hatua mbali mbali ambazo hujulikana Leo,na kuwa umbile la mifupa,misuli (muscles), mifumo ya ufahamu na kadhalika.

Sasa tuje katika mkabala au maelezo ya qura'n :

Qur'an katika mfumo mzima wa uzazi inazungumzia katika maeneo yafuatayo;

1) Utungwaji WA mimba unafanywa na kiasi kidogo cha manii/shahawa
2) kuna maji maji ya uzazi
3) kuna Utungwaji WA Yai lililo pevuka
4) mabadiliko ya embryo

1) Utungwaji WA mimba unafanywa na kiasi kidogo cha manii/shahawa

Hapa quran inazungumzia swala hili mara Kumi na moja,nitaandika baadhi ya Aya Tu:

((Amemuumba mtu kwa tone la manii. Naye mara amekuwa mshindani dhaahiri.))
16:4


((Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa?))
75:37

((Kisha tukamjaalia awe tone ya mbegu ya uzazi katika kalio madhubuti.))
23:13


2) Maji maji ya Uzazi
Qur'an inazungumzia maji maji ya Uzazi ambayo inafurahisha kuyafanyia uchambuzi hapa;


((Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyo changanyika, tumfanyie mtihani. Kwa hivyo tukamfanya mwenye kusikia, mwenye kuona.))
76:2

((Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa,))
86:6

Sasa ebu tuangalie haya maji ambayo huambatana na sperm Yana mchanganyiko upi?

a) secretion of male genital gland contains spermatozoons
b) seminal vesicles - hizi organs zina hifadhi spermatozoons zipo karibu na prostate gland,zinatoa maji maji yake ingawa hazina fertilizing agent
c) prostate gland - maji maji yake inaipa sperm creamy texture and characteristic odour
d) glands annexed to the urinary tract

Na hizi ni Aina za maji maji ambazo Qur'an imezigusia na kudhibitishwa na modern science.

3) Utungwaji WA Yai lililo pevuka
Baada ya Yai kuwa fertilized katika fallopian tube inakwenda kwenye uterus na hapo inasemwa implantation of the egg.
Na Qur'an inasema hivi katika tukio Hilo;

((Nasi tunakiweka katika matumbo ya uzazi tunacho kitaka mpaka muda ulio wekwa))
22:5

Na Ile Hali ya Yai kuwa katika uterus na kujishikiza katika ukuta mwembamba Kwa AJILI ya kukua, na huo ndio ugunduzi wa modern time.
Na Hali hii pia imeelezwa katika Qur'an tangu zamani huko;

((Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji.))
23:14


((Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa?
Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo.)
)
75:37-38

4) Mabadiliko ya Embryo ndani ya Uterus;
Qur'an imezungumzia mabadiliko ya kiumbe ndani ya uterus kama ambavyo modern science imedhibitisha hivyo, na yanashahabiana Sawa Sawa.

((Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji.))
23:14

Modern sayansi inasema Kwanza kunakuwa na umbile kama big g/nyama iliyotafunwa ( chewing gum/chewing fresh) ,katika udogo wake kabisa ambao unaweza kuonekana na jicho la kawaida inakuwa kama nyama iliyotafunwa,halafu umbile la mifupa hujitokeza ( mesenchyma) ,halafu mifupa iliyoundwa hufunikwa na misuli ( muscle), halafu baadae organ za fahamu na kufuatiwa na jinsia za kiumbe.

((Kisha akamtengeneza, na akampulizia roho yake, na akakujaalieni kusikia na kuona, na nyoyo za kufahamu. Ni uchache mnavyo shukuru.))
32:9

((Na kwamba Yeye ndiye aliye umba jozi, dume na jike

Kutokana na mbegu ya uzazi inapo miminwa))

53:45-46

Huyo ndio Mwenyezi Mungu,,hakika tukiacha ushabiki wa Imani zatu na kuziweka pembeni,unaona kabisa elimu hii ni ufunuo wa Mwenyezi Mungu Kwa mja wake Muhammad ( s.a.w).

Na kumbuka katika Karne Ile hakukuwa na maendeleo ya kufahamu nini kinaendelea ndani ya tumbo la mwanadamu kuhusiana na uzazi na kubwa zaidi kila hatua ambayo Qur'an imeeleza hakika haikutofautiana na tafiti zilizo fanywa na wavumbuzi wa Karne ya 20.

Na Mwenyezi Mungu alimchagua Mtume ambaye hajui kusoma wala kuandika ili adhibitishe maneno yake kuwa Ni ufunuo usio na Shaka ndani yake na unatoka Kwa Yule ambaye ni mjuzi WA mambo yote,yawe na Siri na yasiyo ya Siri na mambo ya ghaibu.

Mambo ni mengi na Mda ni mchache,next time panapo majaliwa INSHAALLAH
 
Assalaam.alaykum....

Katika hadith hizo mbali mbali tulizo soma wallahi unaweza kujiuliza kwanini watu hatutaki kuchuma mithawabu kiulaini kabisa

Ninayokumbuka kwa uchache;
Mwanamke usimsahau jiran japo hata kwa kwato ya mbuzi,je vipi ukimpa jirani yako mboga au matunda

Msalimie muislamu mwenzako japo kwa uso mkunjufu

Toa udhia njiani,iwe mwiba au chochote kile,kuna mtu kaonekana peponi kwa kukata mti unao wakera waislamu njiani

Kuna kahaba wa israel alisamehewa kwa kumpa maji mbwa mwenye kiu kikali

Kuwapa viumbe hai maji ni swadaka

Kusema subhaanallah,alhamdulillah,laa ilaha illallah,alllahu akbar vyote ni sadaka

Kuamrisha mema na kukataza mabaya ni sadaka

Kusema maneno mazur ni sadaka

Kujizuia na shari ni sadaka

Na mengine mengi,hivi tukikosa pepo kuna wa kumlaumu?
 
Niwatake radhi jana sikuchapisha kipengele cha Maswali na Majibu

Tunaendelea na darsa.......




Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب في الأمر بالمحافظة عَلَى السنة وآدابها

016 – Mlango Wa Maarisho Wa Kuzihifadhi Sunnah Na Adabu Zake



Alhidaaya.com





قَالَ الله تَعَالَى:



وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ﴿٧﴾

Na lolote analokupeni Rasuli (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) basi lichukueni, na analokukatazeni, basi acheni. [Al-Hashr: 7]





وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾

Na wala hatamki kwa hawaa.

إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤﴾

Hayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa. [An-Najm: 3-4]





قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ﴿٣١﴾

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. [Aal-‘Imraan: 31]



لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّـهَ كَثِيرًا ﴿٢١﴾

Kwa yakini mna kigezo kizuri kwa Rasuli wa Allaah kwa mwenye kumtaraji Allaah na Siku ya Mwisho na akamdhukuru Allaah kwa wingi. [Al-Ahzaab: 21]



فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٦٥﴾

Basi Naapa kwa Rabb wako, hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni mwamuzi katika yale wanayozozana baina yao, kisha wasipate katika nyoyo zao karaha katika yale uliyohukumu na wajisalimishe, kwa kujisalimisha (kikamilifu). [An-Nisaa: 65]



فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ ﴿٥٩﴾

Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli. [An-Nisaa: 59]



مَّن يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللَّـهَ ﴿٨٠﴾

Atakayemtii Rasuli basi kwa yakini amemtii Allaah. [An-Nisaa: 80]



إِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٥٢﴾

Na hakika wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) bila shaka unaongoza kuelekea njia iliyonyooka.

صِرَاطِ اللَّـهِ ﴿٥٣﴾

Njia ya Allaah… [As-Shuwraa: 52-53]



فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٦٣﴾

Basi watahadhari wale wanaokhalifu amri yake, isije kuwasibu fitnah au ikawasibu adhabu iumizayo. [An-Nuwr: 63]



وَاذْكُرْنَ مَا يُتْلَىٰ فِي بُيُوتِكُنَّ مِنْ آيَاتِ اللَّـهِ وَالْحِكْمَةِ ﴿٣٤﴾

Na kumbukeni yale yanayosomwa majumbani mwenu katika Ayaat za Allaah na Hikmah (Sunnah). [Al-Ahzaab: 34]





Hadiyth – 1



عن أبي هريرةَ رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((دَعُونِي مَا تَرَكْتُكُمْ، إِنَّمَا أَهْلَكَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ كَثْرَةُ سُؤالِهِمْ واخْتِلافُهُمْ عَلَى أنْبيَائِهِمْ، فَإِذَا نَهَيْتُكُمْ عَنْ شَيْء فَاجْتَنِبُوهُ، وَإِذَا أمَرْتُكُمْ بشيءٍ فَأْتُوا مِنْهُ مَا اسْتَطَعْتُمْ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amepokea kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Jiepusheni kwa mambo ambayo sijawatajia, kwani hakika waliangamia wale walio kabla yenu kwa sababu ya kuuliza kwao maswali mengi na kukhitalifiana na Rasuli wao. Basi ninapowakataza jambo liepukeni, na ninapowaamuru jambo, basi fanyeni kwa kadiri muwezavyo.” [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 2



عن أَبي نَجيحٍ العِرباضِ بنِ سَارية رضي الله عنه قَالَ: وَعَظَنَا رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم مَوعظةً بَليغَةً وَجِلَتْ مِنْهَا القُلُوبُ، وَذَرَفَتْ مِنْهَا العُيُونُ، فَقُلْنَا: يَا رسولَ اللهِ، كَأَنَّهَا مَوْعِظَةُ مُوَدِّعٍ فَأوْصِنَا، قَالَ: ((أُوصِيكُمْ بِتَقْوَى اللهِ، وَالسَّمْعِ وَالطَّاعَةِ وَإنْ تَأمَّر عَلَيْكُمْ عَبْدٌ حَبَشِيٌّ، وَإِنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ فَسَيَرَى اختِلافًا كَثيرًا، فَعَليْكُمْ بسُنَّتِي وسُنَّةِ الخُلَفاءِ الرَّاشِدِينَ المَهْدِيِيِّنَ عَضُّوا عَلَيْهَا بالنَّواجِذِ، وَإِيَّاكُمْ وَمُحْدَثَاتِ الأُمُورِ؛ فإنَّ كلَّ بدعة ضلالة)). رواه أَبُو داود والترمذي، وَقالَ: ((حديث حسن صحيح))

Abuu Najiyh Al-‘Irbaadhw bin Saariyah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitupa mawaidha mazito (yenye maana pana), nyonyo zikaingia khofu na macho yakabubujikwa na machozi. Tukamwambia: Ee Rasuli wa Allaah, inaonekana kana kwamba haya mawaidha ni yakutuaga, basi tuusie. Akasema: “Nawausia taqwa ya Allaah, kusikiliza na kutii, hata kama mkiongozwa na mtumwa mhabeshi. Hakika atakayeishi umri mrefu miongoni mwenu ataona khitilafu nyingi. Kwa hivyo ninyi shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za Khulafaa Ar-Rashidiyna (Makhalifah waongofu) wenye kuongoza. Ishikilieni (Sunnah) kwa magego. Na tahadharini mambo yenye kuzushwa, hakika kila bid’ah ni upotevu.” [Abuu Daawuud na At-Tirmidhy, na amesema: Hadiyth hii ni Hasan Swahiyh]





Hadiyth – 3



عَنْ أَبي هريرةَ رضي الله عنه: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((كُلُّ أُمَّتِي يَدخُلُونَ الجَنَّةَ إلا مَنْ أبَى)). قيلَ: وَمَنْ يَأبَى يَا رَسُول الله؟ قَالَ: ((مَنْ أَطَاعَنِي دَخَلَ الجَنَّةَ، وَمَنْ عَصَانِي فَقَدْ أبَى)). رواه البخاري

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesimulia: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Ummah wangu wote wataingia Jannah isipokuwa atakayekataa.” Akaulizwa: “Ni yupi atakayekataa Ee Rasuli wa Allaah? Akajibu: “Atakayenitii mimi ataingia Jannah, na atakayeniasi basi amekataa.” [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 4



عن أَبي مسلم، وقيل: أَبي إياس سَلمة بنِ عمرو بنِ الأكوع رضي الله عنه أنَّ رَجُلًا أَكَلَ عِنْدَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم بِشِمَالِهِ، فَقَالَ: ((كُلْ بِيَمِينكَ)) قَالَ: لا أسْتَطيعُ. قَالَ: ((لاَ استَطَعْتَ)). مَا مَنَعَهُ إلا الكِبْرُ، فمَا رَفَعَهَا إِلَى فِيهِ. رواه مسلم

Abuu Muslim, pia anaitwa Abuu Iyaas, Salamah bin ‘Amruw bin Al-Akwa’ (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesimulia: Mtu mmoja alikula kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa mkono wake wa kushoto. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: “Kula kwa mkono wako wa kulia.” Yule mtu akasema siwezi. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: “Hutaweza!” Hakuna kilichomzuia isipokwa ni kibri. Basi hakuweza tena kuinua mkono wake hadi kinywani mwake. [Muslim]





Hadiyth – 5



عن أَبي عبدِ الله النعمان بن بشير رَضيَ الله عنهما، قَالَ: سمعت رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((لَتُسَوُّنَّ صُفُوفَكُمْ، أَوْ لَيُخَالِفَنَّ اللهُ بَيْنَ وُجُوهِكُمْ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

وفي رواية لمسلم: كَانَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يُسَوِّي صُفُوفَنَا حتى كأنَّما يُسَوِّي بِهَا القِدَاحَ حَتَّى إِذَا رَأَى أَنَّا قَدْ عَقَلْنَا عَنْهُ. ثُمَّ خَرَجَ يَومًا فقامَ حَتَّى كَادَ أنْ يُكَبِّرَ فرأَى رَجلًا بَاديًا صَدْرُهُ، فَقَالَ: ((عِبَادَ الله، لَتُسَوُّنَّ صُفُوفَكُمْ أَوْ لَيُخَالِفَنَّ اللهُ بَيْنَ وُجُوهِكُمْ))

Abuu ‘Abdillaah, An-Nu’maan bin Bashiyr (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: Nilimsikia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Wa-Allaahi mtazisawazisha safu zenu au Allaah Atazibadilisha nyuso zenu (ziwe kama wanyama au nyoyo zikhitilafiane).” [Al-Bukhaariy na Muslim]

Riwaayah nyingine ya Muslim imesema:

Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akizisawazisha safu kana kwamba alikuwa anasawazisha kwazo mshale, mpaka atuone kuwa tumefahamu juu ya umuhimu huo. Kisha siku moja akatoka, akasimama hata alipokaribia kupiga Takbiyr, akamuona mtu kifua chake kimetokeza, akasema: “Enyi waja wa Allaah, mtasawazisha safu zenu au Allaah Atazibadilisha nyuso zenu (ziwe kama wanyama au nyoyo zikhitilafiane).”





Hadiyth – 6



عن أَبي موسى رضي الله عنه قَالَ: احْتَرقَ بَيْتٌ بالمَدِينَةِ عَلَى أهْلِهِ مِنَ اللَّيلِ، فَلَمَّا حُدِّثَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم بشَأنِهِمْ، قَالَ: ((إنَّ هذِهِ النَّارَ عَدُوٌّ لَكُمْ، فَإِذَا نِمْتُمْ، فَأطْفِئُوهَا عَنْكُمْ)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

Abuu Muwsaa (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesimulia: Siku moja nyumba iliteketea Madiynah wakati wa usiku na wenyewe wamo ndani. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipohadithhiwa habari hiyo, alisema: “Hakika huo moto ni adui yenu, mnapolala uzimeni.” [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 7



عَنْهُ، قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((إنَّ مَثَلَ مَا بَعَثَنِي الله بِهِ مِنَ الهُدَى والعِلْم كَمَثَلِ غَيثٍ أَصَابَ أرْضًا فَكَانَتْ مِنْهَا طَائِفةٌ طَيِّبَةٌ، قَبِلَتِ المَاءَ فَأَنْبَتَتِ الكَلأَ والعُشْبَ الكَثِيرَ، وَكَانَ مِنْهَا أَجَادِبُ أمسَكَتِ المَاء فَنَفَعَ اللهُ بِهَا النَّاسَ فَشَربُوا مِنْهَا وَسَقُوا وَزَرَعُوا، وَأَصَابَ طَائفةً مِنْهَا أخْرَى إنَّمَا هِيَ قيعَانٌ لا تُمْسِكُ مَاءً وَلا تُنْبِتُ كَلأً، فَذَلِكَ مَثَلُ مَنْ فَقُهَ في دِينِ اللهِ وَنَفَعَهُ بمَا بَعَثَنِي الله بِهِ فَعَلِمَ وَعَلَّمَ، وَمَثَلُ مَنْ لَمْ يَرْفَعْ بِذَلِكَ رَأسًا وَلَمْ يَقْبَلْ هُدَى اللهِ الَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Abuu Muwsaa (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mfano wa Aliyonituma kwayo Allaah katika uongofu na elimu, ni mfano wa mvua nyingi iliyonyesha katika nchi, ikawa ina rutuba, ikakubali maji, ikaotesha nyasi na maji mengi. Na sehemu nyingine ikawa ni kavu na ngumu inayozuia maji, Allaah Akawanufaisha watu kwa mvua hiyo. Wakanywa, wakanywesha mifugo na kulimia kwayo. Na ikanyesha sehemu nyingine ambayo ni kavu haizuii maji, wala haioteshi nyasi. Basi mifano hiyo ni mfano wa mtu aliyekuwa na ufahamu mzuri katika Dini ya Allaah, yakamnufaisha yale Aliyonituma kwayo Allaah, akajifunza na akafundisha. Na mfano wa mwisho ni mfano wa mtu ambaye, hakuinua kichwa kwa jambo hilo na wala hakuukubali uongofu wa Allaah niliyotumwa nao.” [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 8



عن جابر رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((مَثَلِي وَمَثَلُكُمْ كَمَثَلِ رَجُلٍ أوْقَدَ نَارًا فَجَعَلَ الجَنَادِبُ والفَرَاشُ يَقَعْنَ فِيهَا وَهُوَ يَذُبُّهُنَّ عَنْهَا، وَأَنَا آخذٌ بحُجَزكُمْ عَنِ النَّارِ، وَأنْتُمْ تَفَلَّتونَ مِنْ يَدَيَّ)). رواه مسلم

Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mfano wangu na mfano wenu ni kama mtu aliyewasha moto, panzi na vipepeo wakawa wanaingia naye humo (mtu huyo) akawa anazuia wasiingie. Nami nimewashika viuno vyenu (sehemu ya kuifungia mkanda) kuwaokoa na moto, lakini mnaniponyoka mkononi mwangu (nashinda kuwazuia)!” [Muslim]





Hadiyth – 9



عَنْهُ أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم أَمَرَ بِلَعْقِ الأَصَابِعِ وَالصَّحْفَةِ، وَقَالَ: ((إنَّكُمْ لا تَدْرونَ في أَيِّها البَرَكَةُ)). رواه مسلم.

وفي رواية لَهُ: ((إِذَا وَقَعَتْ لُقْمَةُ أَحَدِكُمْ فَلْيَأخُذْهَا، فَليُمِطْ مَا كَانَ بِهَا مِنْ أذىً، وَلْيَأكُلْهَا وَلا يَدَعْهَا لِلشَّيطَانِ، وَلا يَمْسَحْ يَدَهُ بالمنْدِيلِ حَتَّى يَلْعَقَ أصَابعَهُ فَإِنَّهُ لا يَدْرِي في أيِّ طَعَامِهِ البَرَكَةُ)).

وفي رواية لَهُ: ((إنَّ الشَّيطَانَ يَحْضُرُ أَحَدَكُمْ عِنْدَ كُلِّ شَيءٍ مِنْ شَأنِهِ، حَتَّى يَحْضُرَهُ عِنْدَ طَعَامِهِ، فَإذَ سَقَطَتْ مِنْ أَحَدِكُمْ اللُّقْمَةُ فَليُمِطْ مَا كَانَ بِهَا مِنْ أذَىً، فَلْيَأكُلْهَا وَلا يَدَعْهَا لِلشَّيطَانِ))

Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesimulia: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameamrisha kulamba vidole na sahani, akasema: “Ninyi hamjui ni wapi penye baraka.” [Muslim]

Riwaayah nyingine ya Muslim imesema:

“Linapoanguka tonge la chakula la mmoja wenu, aliokote na aondoe taka iliyoingia na alile, wala asimuachie shaytwaan, wala asiupanguse mkono wake kwa kitambaa mpaka avilambe kidole vyake; kwani hajui ni katika chakula kipi kuna baraka.”

Riwaayaha nyingine tena ya Muslim imesema:

“Hakika shaytwaan anahudhuria katika kila jambo la mmoja wenu hata anahudhuria kwenye chakula chake. Basi linapoanguka tonge la chakula la mmoja wenu, aondoe sehemu iliyoingia taka na alile, wala asimuachie shaytwaan.”





Hadiyth – 10




عن ابن عباس رضي الله عنهما، قَالَ: قَامَ فِينَا رَسُول الله صلى الله عليه وسلم بِمَوعِظَةٍ، فَقَالَ: "يَا أيُّهَا النَّاسُ، إنَّكُمْ مَحْشُورونَ إِلَى الله تَعَالَى حُفَاةً عُرَاةً غُرْلًا" كَمَا بَدَأْنَا أَوَّلَ خَلْقٍ نُعِيدُهُ وَعْدًا عَلَيْنَا إِنَّا كُنَّا فَاعِلِينَ

ألا وَإنَّ أَوَّلَ الخَلائِقِ يُكْسى يَومَ القِيَامَةِ إبراهيمُ صلى الله عليه وسلم، ألا وَإِنَّهُ سَيُجَاءُ بِرجالٍ مِنْ أُمَّتي فَيُؤخَذُ بِهِمْ ذَاتَ الشَّمالِ، فَأَقُولُ: يَا رَبِّ أصْحَابِي. فَيُقَالُ: إنَّكَ لا تَدْرِي مَا أحْدَثُوا بَعْدَكَ. فَأقُولُ كَما قَالَ العَبدُ الصَّالِحُ: {وَكُنْتُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا مَا دُمْتُ فِيهِمْ} إِلَى قولِهِ: {العَزِيزُ الحَكِيمُ} [المائدة: 117- 118] فَيُقَالُ لِي: "إنَّهُمْ لَمْ يَزَالُوا مُرْتَدِّينَ عَلَى أعْقَابِهِمْ مُنْذُ فَارَقْتَهُمْ" مُتَّفَقٌ عَلَيه

‘Abdullaah bin ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: Siku moja Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisimama na kututolea mawaidha akasema: “Enyi watu, hakika mtafufuliwa na Allaah haliyakuwa hamna viatu, mpo uchi na bila kutahiriwa (na magovi) Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

كَمَا بَدَأْنَا أَوَّلَ خَلْقٍ نُّعِيدُهُ

Kama Tulivyoanza umbo la awali Tutalirudisha tena [Al-Anbiyaa: 104]



Tanabahini! Hakika mtu wa kwanza atakayevishwa nguo ni Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام). Tanabahini! Wataletwa watu katika Ummah wangu na watapelekwa upande wa kushoto (motoni), nami nitasema: “Ee Rabb wangu, Swahaba wangu!” Nitaambiwa: “Wewe hujui watu hawa walichokizua baada yako.” Hapo nitasema kama alivyosema mja mwema (Nabiy ‘Iysaa):



وَكُنتُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا مَّا دُمْتُ فِيهِمْ ۖ فَلَمَّا تَوَفَّيْتَنِي كُنتَ أَنتَ الرَّقِيبَ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنتَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿١١٧﴾

Na nilikuwa juu yao shahidi wakati nilipokuwa nao. Uliponikamilishia muda Ukanichukua juu, Ulikuwa Wewe Ndiye Mwangalizi juu yao. Na Wewe Ni Mwenye Kushuhudia kila kitu.



إِن تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ ۖ وَإِن تَغْفِرْ لَهُمْ فَإِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١١٨﴾

Ukiwaadhibu, basi bila shaka hao ni Waja Wako, na Ukiwaghufuria basi hakika Wewe Ndiye Mwenye Enzi na Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote. [Al-Maaidah (5:117-118]



Nitaambiwa: “Wao waliendelea kukengeuka na kugeuka nyuma kuondokelea mbali ulipowaacha.” [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 11



عن أَبي سعيد عبد الله بن مُغَفَّلٍ رضي الله عنه قَالَ: نَهَى رَسُول الله صلى الله عليه وسلم عَنِ الخَذْفِ، وقالَ: ((إنَّهُ لا يَقْتُلُ الصَّيْدَ، وَلا يَنْكَأُ العَدُوَّ، وإنَّهُ يَفْقَأُ العَيْنَ، وَيَكْسِرُ السِّنَّ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

وفي رواية: أنَّ قَريبًا لابْنِ مُغَفَّل خَذَفَ فَنَهَاهُ، وَقالَ: إنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم نَهَى عَن الخَذْفِ، وَقَالَ: ((إنَّهَا لا تَصِيدُ صَيدًا)) ثُمَّ عادَ، فَقَالَ: أُحَدِّثُكَ أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم نَهَى عَنْهُ، ثُمَّ عُدْتَ تَخذفُ!؟ لا أُكَلِّمُكَ أَبَدًا.

Abuu Sa’yd, ‘Abdullaah bin Mughaffal (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza al-khadhaf’ (kurusha vijiwe kwa kutumia kidole gumba na cha shahaadah) akasema: “Kwani hakiuwi windo wala hakimuuwi adui, bali hutoboa jicho na kuvunja jino tu.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

Riwaayah nyingine ya Muslim imesema:

“Jamaa mmoja wa karibu kwa Ibn Mughaffal alifanya khadhaf. Akamkataza na akamwambia: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kitendo hiki (khadhaf), akasema: “Kwani hakiwindi windo” Kisha yule jamaa akarudia kitendo hicho. Akamwambia: Nimekuhadithia kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza jambo hilo kisha umerudia kitendo hicho cha khadhaf? Sitazungumza nawe kamwe!





Hadiyth – 12



وعَن عابس بن رَبيعة، قَالَ: رَأيْتُ عُمَرَ بن الخطاب رضي الله عنه يُقَبِّلُ الحَجَرَ- يَعْنِي: الأسْوَدَ- وَيَقُولُ: إني أَعْلَمُ أنَّكَ حَجَرٌ مَا تَنْفَعُ وَلا تَضُرُّ، وَلَولا أنِّي رَأيْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يُقَبِّلُكَ مَا قَبَّلْتُكَ. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

‘Aabis bin Rabiy’h amesema: Nilimuona ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akilibusu Hajarul Aswad (jiwe jeusi) na akasema: Hakika najua wewe ni jiwe, hunufaishi wala hudhuru, lau kama nisingelimuona Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akikubusu nisingelikubusu. [Al-Bukhaariy na Muslim]
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب وجوب الانقياد لحكم الله تعالى

وما يقوله من دُعِيَ إلى ذلك وأُمر بمعروف أو نُهي عن منكر

017–Wajibu Wa Kuifuata Hukumu Ya Allaah (Ta'aalaa)

Na Yale Anayotakiwa Mtu Kuyasema Pindi Anapoitwa Katika Hayo,

Akaamrishwa Mema Au Akakatazwa Munkari



Alhidaaya.com





قال الله تعالى:



فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٦٥﴾

Basi Naapa kwa Rabb wako, hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni mwamuzi katika yale wanayozozana baina yao, kisha wasipate katika nyoyo zao karaha katika yale uliyohukumu na wajisalimishe, kwa kujisalimisha (kikamilifu). [An-Nisaa: 65]



إِنَّمَا كَانَ قَوْلَ الْمُؤْمِنِينَ إِذَا دُعُوا إِلَى اللَّـهِ وَرَسُولِهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ أَن يَقُولُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٥١﴾

Hakika kauli ya Waumini wa kweli wanapoitwa kwa Allaah na Rasuli Wake ili Awahakumu baina yao; husema: “Tumesikia na Tumetii.” Na hao ndio wenye kufaulu. [An-Nuwr: 51]





Hadiyth - 1



عن أَبي هريرة رضي الله عنه قَالَ: لَمَّا نَزَلَتْ عَلَى رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((لِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَإِنْ تُبْدُوا مَا فِي أَنْفُسِكُمْ أَوْ تُخْفُوهُ يُحَاسِبْكُمْ بِهِ اللَّهُ)) [البقرة: 284] الآية.

اشْتَدَّ ذلِكَ عَلَى أصْحَابِ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، فَأتَوا رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ثُمَّ بَرَكُوا عَلَى الرُّكَبِ، فَقَالُوا: أيْ رسولَ الله، كُلِّفْنَا مِنَ الأَعمَالِ مَا نُطِيقُ: الصَّلاةَ والجِهَادَ والصِّيامَ والصَّدَقَةَ، وَقَدْ أُنْزِلَتْ عَلَيْكَ هذِهِ الآيَةُ وَلا نُطيقُها. قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((أتُرِيدُونَ أنْ تَقُولُوا كَمَا قَالَ أَهْلُ الكتَابَينِ مِنْ قَبْلِكُمْ: سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا؟ بَلْ قُولُوا: سَمِعنَا وَأَطَعْنَا غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ المَصِيرُ)) قَالُوا: سمعنا وأَطعنا غفرانك ربنا وإِليك المصير

فَلَمَّا اقْتَرَأَهَا القومُ، وَذَلَّتْ بِهَا ألْسنَتُهُمْ أنْزَلَ اللهُ تَعَالَى في إثرِهَا: ((آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنْزِلَ إِلَيْهِ مِنْ رَبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ كُلٌّ آمَنَ بِاللهِ وَمَلائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِنْ رُسُلِهِ وَقَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ)) [البقرة: 285]



فَلَمَّا فَعَلُوا ذلِكَ نَسَخَهَا اللهُ تَعَالَى، فَأنزَلَ الله- عز وجل: ((لا يُكَلِّفُ اللهُ نَفْسًا إِلا وُسْعَهَا لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ رَبَّنَا لا تُؤَاخِذْنَا إِنْ نَسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا)) قَالَ: نَعَمْ

((رَبَّنَا وَلا تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِنَا)) قَالَ: نَعَمْ

((رَبَّنَا وَلا تُحَمِّلْنَا مَا لا طَاقَةَ لَنَا بِه)) قَالَ: نَعَمْ

((وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا أَنْتَ مَوْلانَا فَانْصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ)) قَالَ: نَعَمْ. رواه مسلم

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa salaam) alipoteremshiwa Aayah hii: “Ni vya Allaah Pekee vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na mkidhihirisha yale yaliyomo ndani ya nafsi zenu au mkiyaficha; basi Allaah Atakuhesabuni kwayo.” Mpaka mwisho wa Aayah. [Al-Baqarah: 284]



Jambo hilo likawa zito kwa Maswahaba wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa salaam) wakamwendea Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa salaam) wakapiga magoti, wakasema: Ee Rasuli wa Allaah, tumekalifishwa ‘amali tunazoziweza; Swalaah, Jihaad, Swawm na kutoa Zakaah. Na kwa hakika umeteremshiwa Aayah hii, lakini hatuiwezi! Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa salaam) akawauliza: “Je, mnataka kusema kama walivyosema Ahlul-Kitaabayni (Mayahudi na Manaswara) kabla yenu? “Tumesikia na tumeasi” Bali semeni: “Tumesikia na tumetii, tunakuomba maghfirah Rabb wetu Kwako ni mahali pa kuishia.”

Maswahaba walipoisoma na ndimi zao zikaandama. Allaah Aliteremsha:

“Rasuli ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Rabb wake na Waumini (pia wameamini). Wote wamemwamini Allaah, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake, na Rasuli Wake. (Nao husema): “Hatutofautishi baina ya yeyote kati ya Rasuli Wake.” Na wakasema: “Tumesikia na tumetii, tunakuomba maghfirah Rabb wetu na Kwako ni mahali pa kuishia.” [Al-Baqarah: 285]



Walipofanya hivyo, Allaah Aliifuta (hukmu ya) Aayah hiyo, Akateremsha:

“Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake. Itapata (thawabu) iliyoyachuma, na ni dhidi yake (kwa maovu) iliyojichumia. “Rabb wetu Usituchukulie tukisahau au tukikosea.” Akasema: “Na’aam”.



“Rabb wetu, Usitubebeshe mzigo kama Ulivyoubebesha juu ya wale waliokuwa kabla yetu.” Akasema: “Na’aam”.



“Rabb wetu, Usitutwike tusiyoyaweza, na Tusamehe, na Tughufurie na Turehemu, Wewe ni Mola Mlinzi wetu, basi Tunusuru dhidi ya watu makafiri.” Akasema: “Na’aam”. [Muslim]
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب النهي عن البدع ومحدثات الأمور

018 - Mlango Wa Kukataza Bid’ah Na Uzushi



Alhidaaya.com





قَالَ تَعَالَى:



فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ إِلَّا الضَّلَالُ ۖ

Na kuna nini baada ya haki ila upotofu? [Yuwnus: 32]



مَّا فَرَّطْنَا فِي الْكِتَابِ مِن شَيْءٍ ۚ

Hatukusuru katika Kitabu kitu chochote. [Al-An’aam: 38]



فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ

Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli. [An-Nisaa: 59]



وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ

Na kwamba hii njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Na wala msifuate njia nyinginezo zitakufarikisheni na njia Yake. [Al-An’aam: 153]



قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. [Aal-‘Imraan: 31]





Hadiyth – 1

عن عائشة رَضِي الله عنها، قَالَتْ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ أحْدَثَ في أمْرِنَا هَذَا مَا لَيْسَ مِنْهُ فَهُوَ رَدٌّ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

وفي رواية لمسلم: ((مَنْ عَمِلَ عَمَلًا لَيْسَ عَلَيهِ أمرُنا فَهُوَ رَدٌّ))

‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Mwenye kuzua katika jambo letu hili lisilokuwemo humo litakataliwa.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

Riwaayah nyingine ya Muslim: “Mwenyekufanya amali isiyokuwa na hukmu yetu, itakataliwa.”





Hadiyth – 2

وعن جابر رضي الله عنه قَالَ: كَانَ رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم إِذَا خَطَبَ احْمَرَّتْ عَينَاهُ، وَعَلا صَوتُهُ، وَاشْتَدَّ غَضَبُهُ، حَتَّى كَأنَّهُ مُنْذِرُ جَيشٍ، يَقُولُ: ((صَبَّحَكُمْ وَمَسَّاكُمْ)) وَيَقُولُ: ((بُعِثتُ أنَا والسَّاعَةُ كَهَاتَينِ)) وَيَقْرِنُ بَيْنَ أُصبُعَيهِ السَّبَّابَةِ وَالوُسْطَى، وَيَقُولُ: ((أمَّا بَعْدُ، فَإنَّ خَيْرَ الحَديثِ كِتَابُ الله، وَخَيرَ الهَدْيِ هَدْيُ مُحَمَّدٍ صلى الله عليه وسلم، وَشَرَّ الأُمُورِ مُحْدَثَاتُهَا، وَكُلَّ بِدْعَة ضَلالَةٌ)) ثُمَّ يَقُولُ: ((أنَا أوْلَى بِكُلِّ مُؤمِنٍ مِنْ نَفسِهِ، مَنْ تَرَكَ مَالًا فَلأَهْلِهِ، وَمَنْ تَرَكَ دَيْنًا أَوْ ضَيَاعًا فَإلَيَّ وَعَلَيَّ)). رواه مسلم

وعن العرباض بن سَارية رضي الله عنه حدِيثه السابق في بابِ المحافظةِ عَلَى السنةِ

وفيه: ((فإنه من يعش منكم فسيرى اختلافًا كثيرًا فعليكم بسنَّتي...))

Kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema kwamba: Alipokuwa akikhutubia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) macho yake yalikuwa yakibadilika rangi na kuwa mekundu, na akinyanyua sauti yake na ghadhabu ilikuwa kali kana kwamba alikuwa akitutahadharisha na jeshi la adui. Alikuwa akisema: “Maadui watawashambulieni asubuhi na usiku.” Na pia akisema: “Nimetumwa mimi kuja siku mwisho kama hivi.” Na alikuwa anavishikanisha vidole vyake (kidole cha kati na cha shahada), na akisema tena: Ama baada (ya salamu): “Hakika mazungumzo bora ni maneno ya Allaah (Qur-aan) na uongofu bora ni uongofu wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam), na mambo yaliyomaovu ni yale yenyekuzuliwa na kila bid’ah ni upotevu.” [Muslim]

Kisha alikuwa akisema: “Mimi ni mwenyekumtakia kila Muumin masilahi yake kuliko anavyojitakia nafsi yake, hivyo yoyote atayeacha mali ni kwa watu wake, na yoyote atakayeacha deni au watoto na familia basi hayo yatakuwa juu yangu.”

Na imepokewa kwa ‘Irbaadhw bin Saariyah (Radhwiya Allaahu 'anhu) Hadiyth iliyotangulia katika mlango wa: Amri ya kuhifadhi Sunnah na adabu zake: “Hakika atakayeishi umri mrefu miongoni mwenu ataona khitilafu nyingi.”
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب فيمن سن سنة حسنة أَوْ سيئة

019 – Mlango Wa Mwenye Kuzua Sunnah Nzuri Na Mbaya



Alhidaaya.com



قَالَ تَعَالَى:



وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا ﴿٧٤﴾

Na wale wanaosema: “Rabb wetu! Tutunukie katika wake zetu na dhuria wetu viburudisho vya macho yetu, na Tujaalie kuwa waongozi kwa wenye taqwa. [Al-Furqaan: 74]



وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا

Na Tukawajaalia Maimaam wanaongoza kwa amri Yetu. [Al-Anbiyaa: 73]





Hadiyth - 1

عن أَبي عمرو جرير بن عبد الله رضي الله عنه قَالَ: كنا في صَدْرِ النَّهَارِ عِنْدَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم فَجَاءهُ قَومٌ عُرَاةٌ مُجْتَابي النِّمَار أَوْ العَبَاء، مُتَقَلِّدِي السُّيُوف، عَامَّتُهُمْ من مُضر، بَلْ كُلُّهُمْ مِنْ مُضَرَ، فَتَمَعَّرَ وَجْهُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم لما رَأَى بِهِمْ مِنَ الفَاقَة، فَدَخَلَ ثُمَّ خَرَجَ، فَأَمَرَ بِلالًا فَأَذَّنَ وَأَقَامَ، فصَلَّى ثُمَّ خَطَبَ، فَقَالَ: (({يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ مِنْ نَفْسٍ وَاحِدَةٍ} إِلَى آخر الآية: {إِنَّ اللهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا}، والآية الأُخْرَى التي في آخر الحَشْرِ: {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللهَ وَلْتَنْظُرْ نَفْسٌ مَا قَدَّمَتْ لِغَدٍ} تَصَدَّقَ رَجُلٌ مِنْ دِينَارِهِ، مِنْ دِرهمِهِ، مِنْ ثَوبِهِ، مِنْ صَاعِ بُرِّهِ، مِنْ صَاعِ تَمْرِهِ- حَتَّى قَالَ: وَلَوْ بِشقِّ تَمرَةٍ)).

فَجَاءَ رَجُلٌ مِنَ الأَنْصَارِ بِصُرَّةٍ كَادَتْ كَفُّهُ تَعجَزُ عَنهَا، بَلْ قَدْ عَجَزَتْ، ثُمَّ تَتَابَعَ النَّاسُ حَتَّى رَأيْتُ كَومَيْنِ مِنْ طَعَامٍ وَثِيَابٍ، حَتَّى رَأيْتُ وَجْهَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يَتَهَلَّلُ كَأنَّهُ مُذْهَبَةٌ. فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ سَنَّ في الإسلامِ سنَّةً حَسَنَةً فَلَهُ أجْرُهَا، وَأجْرُ مَنْ عَمِلَ بِهَا مِنْ بَعْدَهُ، مِنْ غَيرِ أنْ يَنْقُصَ مِنْ أُجُورهمْ شَيءٌ، وَمَنْ سَنَّ في الإسْلامِ سُنَّةً سَيِّئَةً كَانَ عَلَيهِ وِزْرُهَا، وَوِزْرُ مَنْ عَمِلَ بِهَا مِنْ بَعْدِهِ، مِنْ غَيرِ أنْ يَنْقُصَ مِنْ أوْزَارِهمْ شَيءٌ)). رواه مسلم

Abuu ‘Amruw Jariyr bin ‘Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema kwamba: Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) mchana na siku moja. Wakati huo mara wakaja watu waliokuwa hawakuvaa nguo bali nguo za magunia katika miili yao, na wengine walikuwa na kama majoho, panga zao zikiwa zinagusa chini. Takriban wote walikuwa wanatoka kabila ya Mudhar, bali wote walikuwa ni kutoka kabila la Mudhar. Uso wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) ulibadilika kwa kuwaona hawa watu katika hali hii ya shida na njaa. Akaingia nyumbani kwake kisha akatoka. Alimuamuru Bilaal (Radhwiya Allaahu 'anhu) aadhini kisha akimu, baada ya hapo aliswalisha na kuwahutubia watu baada ya Swalah, akasema: “Enyi watu! Mcheni Rabb wenu Ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi moja (Aadam) na Akaumba kutoka humo mke wake (Hawwaa) na Akaeneza kutoka hao wawili wanaume na wanawake wengi. Na mcheni Allaah Ambaye Kwake mnaombana (haki zenu kwa kuunga) undugu. Hakika Allaah ni Mwenye kuwachunga daima.”



”Kisha akasoma ile aayah nyingine ambayo ipo mwisho wa Suwratu Al-Hashr: “Enyi walioamini! Mcheni Allaah, na nafsi itazame imetanguliza nini kwa ajili ya kesho, na mcheni Allaah.”

Baada ya hayo akawaomba watu watoe sadaka katika dinari zao, dirhamu, nguo, kipimo maalumu cha ngano na tende mpaka akasema: “Hata kama ni kipande cha tende.” Kusikia haya mtu mmoja wa ki Answaar alikuja na mzigo mkubwa, ambao ulimuelemea sana kuubeba. Wengine wakamfuata kwa kuleta sadaka zao mpaka nikaona milima miwili ya chakula na nguo. Hapo nikauona uso wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) unang’aa kama dhahabu. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) alisema baada ya hayo: “Yeyote atakayezua katika Uislamu Sunnah nzuri atapata thawabu ya kitendo hicho na ujira (thawabu) za wenye kufanya kitendo hicho baada yake bila ya wale waliokuja baada yake kupunguziwa thawabu zao. Na yeyote atakayezua katika Uislamu Sunnah mbaya, atapata madhambi ya kufanya jambo hilo na madhambi ya wenye kumfuata yeye baada yake bila ya wao kupunguziwa chochote katika madhambi yao. [Muslim]





Hadiyth – 2

وعن ابنِ مسعود رضي الله عنه أن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((لَيْسَ مِنْ نَفْسٍ تُقْتَلُ ظُلْمًا إلا كَانَ عَلَى ابْنِ آدَمَ الأوْلِ كِفْلٌ مِنْ دَمِهَا، لأَنَّهُ كَانَ أوَّلَ مَنْ سَنَّ القَتلَ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Kutoka kwa Ibn Mas’uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Hakuna nafsi yeyote inayouliwa kwa dhulma isipokuwa yule mwanadamu wa kwanza atapata sehemu yake ya madhambi (ya mauaji) kwani yeye ndiye wa mwanzo kuanzisha mauaji.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب في الدلالة عَلَى خير والدعاء إِلَى هدى أَوْ ضلالة

20 – Mlango Wa Kuhimiza Mema Na Kuwaita Watu Katika Uongofu Au Upotevu



Alhidaaya.com





قَالَ تَعَالَى:



وَادْعُ إِلَىٰ رَبِّكَ ۖ

Na lingania kwa Rabb wako… [Al-Qaswasw: 87]



ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ

Lingania katika njia ya Rabb wako kwa hikmah na mawaidha mazuri. [An-Nahl: 125]



وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ

Na shirikianeni katika wema na taqwa… [Al-Maaidah: 2]



وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ

Na watokeze kutoka kwenu umati wa watu unaolingania kheri… [Aal-‘Imraan: 104]







Hadiyth – 1

وعن أَبي مسعود عُقبةَ بنِ عمرو الأنصاري البدري رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ دَلَّ عَلَى خَيْرٍ فَلَهُ مِثْلُ أجْرِ فَاعِلِهِ)). رواه مسلم

Kutoka kwa Abuu Mas’uwd ‘Uqbah bin ‘Amru Al-Answaar Al-Badriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba amesema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam): “Yeyote mwenye kumuelekeza mtu katika jambo jema atapata ujira wa mfano wa yule mwenye kufanya (hilo jambo jema).” [Muslim]





Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((مَنْ دَعَا إِلَى هُدَىً، كَانَ لَهُ مِنَ الأَجْرِ مِثْلُ أجُورِ مَنْ تَبِعَه، لاَ يَنْقُصُ ذلِكَ مِنْ أجُورِهمْ شَيئًا، وَمَنْ دَعَا إِلَى ضَلاَلَةٍ، كَانَ عَلَيهِ مِنَ الإثْمِ مِثْلُ آثَامِ مَنْ تَبِعَهُ، لا يَنْقُصُ ذلِكَ مِنْ آثَامِهِمْ شَيئًا)). رواه مسلم

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Yeyote anayewaita wengine katika uongofu atapata thawabu mfano wa wale wenye kumfuata wala hilo haliwapunguzii thawabu zao hata kidogo. Na yeyote atakayewaita watu katika upotevu atapata madhambi mfano wa madhambi ya wale wenye kumfuata na wala hilo halitawapunguzia madhambi hata chembe.” [Muslim]





Hadiyth – 3

وعن أَبي العباس سهل بن سعد الساعدي رضي الله عنه: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ يوم خَيبَر: ((لأُعْطِيَنَّ الرَّايَةَ غَدًا رجلًا يَفْتَحُ الله عَلَى يَدَيهِ، يُحبُّ اللهَ وَرَسولَهُ، ويُحِبُّهُ اللهُ وَرَسُولُهُ))، فَبَاتَ النَّاسُ يَدُوكُونَ لَيْلَتَهُمْ أيُّهُمْ يُعْطَاهَا. فَلَمَّا أصْبَحَ النَّاسُ غَدَوْا عَلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم كُلُّهُمْ يَرْجُو أنْ يُعْطَاهَا. فَقَالَ: ((أينَ عَلِيُّ بنُ أَبي طالب؟)) فقيلَ: يَا رسولَ الله، هُوَ يَشْتَكي عَيْنَيهِ. قَالَ: ((فَأَرْسِلُوا إِلَيْه)) فَأُتِيَ بِهِ فَبَصَقَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم في عَيْنَيْهِ، وَدَعَا لَهُ فَبَرِئَ حَتَّى كأنْ لَمْ يكُن بِهِ وَجَعٌ، فأعْطاهُ الرَّايَةَ. فقَالَ عَليٌّ رضي الله عنه: يَا رَسُول اللهِ، أقاتِلُهمْ حَتَّى يَكُونُوا مِثْلَنَا؟ فَقَالَ: ((انْفُذْ عَلَى رِسْلِكَ حَتَّى تَنْزِلَ بسَاحَتهمْ، ثُمَّ ادْعُهُمْ إِلَى الإسْلاَمِ، وَأخْبِرْهُمْ بِمَا يَجِبُ عَلَيْهِمْ مِنْ حَقِّ اللهِ تَعَالَى فِيهِ، فَوَالله لأَنْ يَهْدِيَ اللهُ بِكَ رَجُلًا وَاحِدًا خَيرٌ لَكَ مِنْ حُمْرِ النَّعَم)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Kutoka kwa Abul-‘Abbaas Sahl bin Sa’d As-Saa’idiy (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) alisema siku ya Khaybar: “Kesho nitampatia mtu bendera ambaye kwa mikono yake Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa) atafungua (mji huu). Mtu huyo anampenda Allaah na Rasuli wake, basi Allaah na Rasuli wake wanampenda.” Watu wakakesha wakifikiria na kuzungumza juu ya nani atayepatiwa bendera hiyo. Kulipopambazuka watu wote walikwenda kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) kila mmoja anatarajia kuwa atapatiwa yeye jukumu hilo. Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam): “Yuko wapi ‘Aliy bin Abiy Twaalib?” Wakasema: “Ee Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)! Yeye anaumwa macho.” Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam): “Mleteni kwangu.” Akaletwa kwake, na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) akampaka mate yake katika macho na kumwombea kwa Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa). ‘Aliy akapona kabisa na ugonjwa huo (wa macho) mpaka ikaonekana kama kwamba hakuwa na tatizo lolote na hapo akapatiwa bendera. ‘Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) akasema: “Ee Mjumbe wa Allaah! Nipigane nao mpaka wawe kama sisi?” Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam): “Endelea kwenda kwa kasi yako ya kawaida mpaka ufike katika bonde lao na hapo muweke kambi yenu. Kisha waite katika Uislamu na uwapashe habari kuhusu wajibu wao na majukumu yao kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ndani yake. Naapa kwa Allaah! Allaah akimuongoa mtu mmoja kupitia kwako ni bora kuliko kundi la ngamia wekundu. [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 4

وعن أنس رضي الله عنه: أن فتىً مِنْ أسلم قَالَ: يَا رَسُول الله، إنِّي أُرِيدُ الغَزْوَ وَلَيْسَ معي مَا أتَجَهَّز بِهِ، قَالَ: ((ائتِ فُلاَنًا فإنَّهُ قَدْ كَانَ تَجَهَّزَ فَمَرِضَ)) فَأتَاهُ، فَقَالَ: إنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يُقْرِئُكَ السَّلامَ، وَيَقُولُ: أعْطني الَّذِي تَجَهَّزْتَ بِهِ، فَقَالَ: يَا فُلاَنَةُ، أعْطِيهِ الَّذِي تَجَهَّزْتُ بِهِ، وَلا تَحْبِسي مِنْهُ شَيئًا، فَواللهِ لا تَحْبِسِين مِنْهُ شَيئًا فَيُبَاركَ لَكِ فِيهِ. رواه مسلم

Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba kijana katika kabila la Aslam alikuja na kusema: “Ee Mjumbe wa Allaah! Mimi ninataka kushiriki katika vita, lakini sina chochote cha kujitayarisha kwayo?” Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam): “Nenda kwa Fulani kwani yeye amejitayarisha lakini akashikwa na maradhi.” Huyu kijana akaenda kwa huyo mtu na kumwambia: “Kwa hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) anakutolea salamu na anakwambia: Nipatie mimi vifaa ulivyovitayarisha ili kuvitumia katika vita.” Akasema yule Fulani: “Ewe mke wangu mpatie kila kitu nilichotayarisha wala usibakishe chochote. Naapa kwa Allaah, kisha ikiwa hutamnyima chochote katika vifaa nilivyotayarisha, Allaah atakubariki kwayo.” [Muslim]
 
Baadhi ya post zangu za zamani.....

JE QUR'AN NI NAKALA YA BIBLIA?

MAMBO YA ANGA / ASTRONOMY IN THE QURAN

Qur'an imegusia Sana elimu ya anga kuna karibia Aya 40 zinazungumzia mambo ya anga na hii yote ni kwasababu Mwenyezi Mungu anampa hoja mwanadamu atafakari na kuona uwepo wa Mwenyezi Mungu na uwezo juu ya kila kitu.
Nitazitaja chache kabla sijaenda kwenye hoja rasmi:

((Je! Hawaangalii mbingu zilizo juu yao! Vipi tulivyo zijenga, na tukazipamba. Wala hazina nyufa.))
50:6


((Na akalifanya jua na mwezi kwa manufaa yenu daima dawamu, na akaufanya usiku na mchana kwa manufaa yenu))
14:33

((Na mwezi tumeupimia vituo, mpaka unakuwa kama karara kongwe))
36:39


((Na amefanya ukutumikieni usiku na mchana, na jua na mwezi, na nyota zikutumikieni kwa amri yake. Hakika katika hayo zipo ishara kwa watu wenye akili))
16:12

Hayo nimeyaleta Kwa uchache Tu! Sasa fuatana nami ule Asali!
Watu wanasema Muhammad amekopi Maandiko ya Biblia lakini elimu aliyoleta huyu Mtume ni kubwa zaidi ya Biblia,kwakawaida anayekopi Hana anachokijua isipokuwa kile alichokopi lakini mbona Kwa Muhammad (s.a.w) ni tofauti?

Biblia imesema kwamba Mungu akaumba mianga miwili moja kubwa na moja ndogo ili zimulike anga, ebu tuangalie Maandiko:

Mwanzo 1:16
[16]Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia.
And God made two great lights; the greater light to rule the day, and the lesser light to rule the night: he made the stars also.


Hapana Shaka yoyote nimekoti Maandiko hapo na mmeyaona,katika Biblia imesemwa mianga miwili,moja mdogo na mmoja mkubwa,Kwa maana mkubwa jua limulike mchana na mdogo ni mwezi umulike usiku.

Lakini Qur'an imesema kuwa Mwenyezi Mungu ameumba jua Hali ya kuwa Ni Taa na Mwezi ni nuru, tuangalie Maandiko:

((Ametukuka aliye zijaalia nyota mbinguni, na akajaalia humo taa na mwezi wenye nuru))
25:61


((Kwani hamwoni jinsi Mwenyezi Mungu alivyo ziumba mbingu saba kwa matabaka?

Na akaufanya mwezi ndani yake uwe nuru, na akalifanya jua kuwa taa?))
71:15-16


Sasa tuje kwenye hoja ya msingi hapa, Qur'an haija sema jua na Mwezi zote ni mianga laa! Bali imetofautisha kuwa jua ni Taa na Mwezi ni nuru, je kuna kutofauti gani hapa?

Tuje kuangalia hoja Kisayansi,,jua ni Nyota ambayo kutokana na mlipuko wake wenyewe unazalisha joto na moto na hivyo kuwa kama taa ambayo inatoa mwanga mkali Sana,na Kwa faida yako Tu jua ni mkusanyiko WA gesi tupu haina ardhi Kama mwezi.

Na Mwezi hauzalishi mwanga Bali ni nuru ambayo inapatikana baada ya kuakisi mwanga kutoka kwenye jua,kwahiyo maelezo ya qura'n kuhusu jua na Mwezi hakika yanafanana Sawa kabisa na hoja za Kisayansi za Karne ya 20.

Je bado unataka kusema Muhammad kakopi Biblia? Utakuwa sio mzima wewe kabisa!

Hayo ni maneno ya Mwenyezi Mungu ambaye ndie aliyeumba mbingu na ardhi anaujua ulimwengu wake vizuri Sana,ni hii ndio inadhibitisha kuwa hakika Qur'an ni ufunuo kutoka Kwa Mwenyezi Mungu wa haki,na huwez kuta mapungufu yoyote katika Qur'an yake.

Tuje kwenye mambo mengine kama Nyota,Biblia imezungumzia au imetaja kuwepo Kwa Nyota lakini Qur'an imetaja neno Nyota karibia mara 13 katika Qur'an, na ikaelezwa kuwa nyota ina mwanga mkali.


((Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku!
Na nini kitakacho kujuulisha ni nini hicho Kinacho kuja usiku?
Ni Nyota yenye mwanga mkali.)
)
86:1-3

Na neno Nyota likatajwa vile vile kumaanisha the shooting star (vimondo)

((Isipo kuwa anaye nyakua kitu kidogo, na mara humfwatia kimondo kinacho ng'ara.))
37:10

Na ikaelezwa vile vile Nyota huwasaidia wasafiri wa baharini na barani wakati WA usiku kuwaonyesha mwelekeo.

Tuje kwenye mambo ya solar system,hapa Qur'an inazungumzia obit ya Jua na Mwezi;

((Na Yeye ndiye aliye umba usiku na mchana na jua na mwezi, vyote katika anga vinaogelea))
21:33


((Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia zao))
36:40

Allahu Akbar! Wote tunajua kuwa Jua na Mwezi vyote vinajizungusha katika Mihimili Yao kutokana na modern sayansi, hapo kuogelea ina maana kuzunguka angani kwenye space.

Haya tujiulize Kwa Karne Ile wanasayansi hawakuenda katika space/angani je Muhammad angejuaje mambo yenye elimu kubwa kiasi Hicho?
Je bado unadhana kwamba Muhammad amekopi Biblia? Tafuta mwanasaikolojia fasta akuweke Sawa.

Mambo ni mengi ya kuandika lakini Mda ni mchache.

Panapo majaliwa inshallah nitakuja na mambo mengine.

##Tutaelewana Tu!##
 
Baadhi ya post zangu za zamani....

MAMBO MANNE YA KUJIFUNZA KUTOKA KWA VIJANA WA PANGONI

Sura hii kama inavyojulikana inahusu vijana wa pangoni....lakini kuna matukio mengine ambayo ni mafunzo tosha katika Maisha yetu ya kila siku,na ndio maana imesisitizwa tuisome kila siku ya ijumaa.

Funzo la Kwanza - siku zote tusitetereke katika kumwabudu Mwenyezi Mungu ambaye ndie WA kweli,tuilinde Imani yetu thabiti na tusiichanganye na ushirikina,,,,kama tulivyoona vijana hawa WA pangoni walikuwa katika jamii ambayo ni watu wachache Sana ndio walimwamini Mungu wa kweli na jamii kubwa ilikuwa inaabudu miungu ya uongo,,,,wakaona ili wasalimike na Imani Yao wakaona Bora waende wakajifiche pangoni kuliko kuiharibu Imani Yao,,,,,na siku zote ukimwamini Mwenyezi Mungu hakika atakulinda,basi Mola wao akawajaalia usingizi ndani ya pango lile na walikaa mule pangoni takribani miaka 309,na baadae akaja kuwaamsha na kukuta jamii ya pale imebadilika na watu wote Wanamwamini Mungu Mmoja,,,,na katika tukio Hilo la kukaa Miaka yote usingizini na kuja kuamshwa, Allah anasema hiyo ni ishara Kwa wale ambao hawaamini hiyo siku ya kiama kuwa hakika IPO na itakuja bilashaka.

Funzo la pili - fitina ya Mali, kuna bwana mmoja alijaaliwa mabustani mawili ambayo katikati yake kuna mito,kulikuwa na mizabibu na mitende na matunda mbali mbali,hakika bustani ilibarikiwa na kusheheni mazao,,,akiwa na mwenzake katika bustani yake,alijigamba kuwa yeye ana Mali nyingi na watoto wengi kuliko huyo mwenzake,na akasema kuwa hadhani kama kiama kitatokea na akaenda mbele zaidi Kwa kusema kuwa hata kikitokea basi atapewa Mali nyingi zaidi ya hizo.Hakika Mali zilimfanya akufuru na kusahau hiyo yote ni neema ya Mola wake,na mwenzake akamwambia Lau kuwa baada ya kuona Mimi Nina Mali kidogo kuliko wewe,basi ungesema hakuna hila wala nguvu isipokuwa Kwa Mwenyezi Mungu na alitakalo huwa,lakini huenda ukajitapa Kwa Mali nyingi na Mola wako akaja futilia mbali bustani yako! Na ndio Hicho kilicho tokea, Mola wake akaleta tufani na kulimalizia mbali shamba lake akabaki kujuta Kwa kauli zake.

Tukijaaliwa Utajiri na Mali basi inatakiwa tumshukuru Mwenyezi Mungu Kwa neema aliyotujaalia na wala tusikufuru Kwa kuona kuwa Ni ujanja wetu na tuitumie Mali hiyo katika njia yake inayompendeza ili tupate mwisho mwema.

Funzo la Tatu - Cheo au Uongozi,,, hivi vitu ni dhamana hivyo basi hatuna budi kuvitumia Kwa uadilifu Sana,,,hapa tunaonyeshwa Dhurqarnain alikuwa ni mfalme muadilifu Sana alikuwa anatembea maeneo mbali mbali kuwasaidia watu wenye uhitaji,na alitumia Cheo chake Kwa hekima na Busara,,,,alipofika katika vilima viwili aliwakuta watu ambao walitaka msaada dhidi ya yajuju na majuju,hawa walikuwa watu ambao walikuwa wanaleta uharibufu katika ardhi,hivyo Dhurqarnain akaombwa kuwadhibiti hawa watu,basi aliwajengea ukuta wa Chuma na kumimina Shaba juu yake,wale watu wabaya wakashindwa kuukwea ule ukuta,na utakuja kuvunjwa na Mwenyezi Mungu siku ya kiama. Na siku zote mfalme huyu hakumsahau Mola wake,,,,hivyo Kwa dhamana yoyote utakayo pewa basi hekima na Busara viwe sehemu ya Uongozi wako.


Funzo la nne - Ni fitna ya Elimu,,, hapa tunakutana na habari ya Nabii Musa na bwana Khizir. Nabii Musa kwakuwa alikuwa anaongea na Mwenyezi Mungu basi alijiona kuwa yeye ndio binadamu mwenye elimu kubwa zaidi,,,lakini Mola wake akamkutanisha na mja wake mmoja Anaitwa Khizir huyu amejaaliwa elimu zaidi kuliko ya Musa,na anajua mambo yajayo au ya ghaibu,IPO siku nitagusia mambo yake aliyomfundisha Musa,Ila hapa ni kuelezea Tu kuwa Kwa kila mjuzi kuna mjuzi zaidi. Na hata uwe na elimu kiasi gani basi Mwenyezi Mungu ndio mjuzi zaidi,,,kwahiyo tuitumie elimu zetu kuleta faida Kwa jamii zetu.
 
Ndugu zangu katika imani miongoni mwa hadith za Nabii swallallahu alaih wasallam,alisema :

"Hakika dunia ni gereza kwa muumini na ni pepo kwa kafiri"

Muumini ni yule anayemwamini Allah subhaanahu wa Taala na Mtume wake swallallahu alaih wasallam,kisha akaishi maisha yake kana kwamba yupo gerezani kwa kujiepusha na starehe zote za dunia na kuiminya nafsi yake na matamanio mbali mbali ya dunia hii ili mradi tu apambanie akhera yake na hivyo kujihisi kama yupo gerezani

Maana wewe warembo unawapenda lakini unasema siwataki kwa ajili ya kutaka radhi za Allah hufanyi machafu

Unapenda pombe kama vijana wengi wa mjini lkn unasema namwogopa Allah

Unapenda kwenda night clubs lkn unawacha kwa ajili ya Allah

Hakika Allah hatokutupa atakulipa ujira wako kamili na mwingi zaidi

Lakini

Kafiri yeye hamwamini Allah,huyu dunia kwake ni pepo,anazini bila hofu,anakunywa pombe ,anabeti,na anasa zote kwake ni sawa tu

Huyu siku akifumba macho ndio atajua hakika Uislamu ni haki na Allah ni haki,hapo atabakia kujuta tu na moto ndio mafakio yake

Basi tuzikandamize nafsi zetu hakika dunia ni starehe ndogo sana idanganyayo lakini maisha ya kudumu na ya milele yapo huko akhera

Naihusia nafsi yangu na yako Tumche Allah

Uwe na siku njema

Nawapenda wote mkono kwa mkono hadi peponi inshaallah...
 
VISA VYA WACHA MUNGU

Nafay (radhiallahu anhu) ameeleza kuwa wakati fulani Abdulla bin Umar (radhiallahu anhu) alikuwa anakwenda safar nje ya Madina Munawwarah,pamoja na wanafunzi wake,walipofika sehemu wakati wa mchana,watakatafuta sehemu na kupumzika ili wapate chakula chao cha mchana

Hapo hapo akapita mchunga mbuzi,anapita na mbuzi wake akawasalimia kwa kusema "Assalaam alaikum" Ibnu Umar (radhiallahu anhu ) akamkaribisha wale pamoja

Akasema yeye amefunga mchana huo

Kisha Ibnu Umar akamwambia katika kumjaribu " Tunataka kununua mbuzi toa bei na tutakulipa ,kisha tutamchinja mbuzi na kisha tutakugawia sehemu ya nyama itakusaidia kwa futari"

Akajibu " Mbuzi hawa si wangu,mimi ni mtumwa tu,na mbuzi wanamilikiwa na bwana wangu"

Ibnu Umar akamwambia vipi bwana wako anaweza kujua? Utamwambia mbwa mwitu amemla mbuzi

Yule mchungaji akaangalia juu mbinguni kisha akasema "Vipi basi Allah? Ambaye anatuangalia mda wote? Vipi nitamdanganya na kumwambia mbwa mwitu amemla mbuzi?"

Ibnu Umar alipendezwa na maneno ya yule mchungaji wa kawaida tu,na akajiambia nafsi yake

"Mchungaji wa kawaida tu anasema vipi kuhusu Allah! Ambaye anatuangalia muda wote."

Ibnu Umar alivyorudi Madinna alimnunua mtumwa yule kutoka kwa bwana wake pamoja na kundi la mbuzi,akamuacha huru na kumpa kundi lile la mbuzi

Naam hayo ndio maisha ya muislamu muumini,muda wote anachunga mipaka ya Allah kwakuwa anajua Allah anajua na kuona kila kitu

Tumche Allah
 
Maswali: Wanawake


Anadhani Kapoteza Bikra Kwa Kujichua, Hajui La Kumwambia Atakayemuoa



Alhidaaya.com





SWALI:



Mimi ni mzima kwa uwezo wa ALLAH (SWT) natumai wewe pia. Swali langu ni hivi mie ni msichana wa kiislam ila nimekua nafanya mambo kinyume na maadili ya kiislam. Imefikia wakati sasa ninajionea huruma na sijui hata nifanyaje nina maika 24 sijaolewa bado na sijawahi kuwa na rafiki wa kiume kwasababu nilikua najichunga sana na wanaume ila ilifikia wakati hamu ya kufanya tendo zikaanza kunijia basi nikaanza kujichua kwa vidole kuna siku moja nikatokwa na damu kidogo nilikua sijui kitu chochote kuhusu tendo la ndoa nilipatwa na hofu sana mpaka sasa sijui nitafanyaje. Naomba nijibu hiyo damu inamaanisha bikra yangu imetoka na nitamwambiaje mume wangu wa baadae kuwa sina bikra na sijawahi kufanya tendo la ndoa inaniuma sana kwasbabu nimejitunza sana halafu nimepoteza bikra yangu bila kujua kwasababu ya kutojua ni nini maana ya tendo la ndoa asant natumai utanijibu vizuri.





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Hakika kufanya ulivyokuwa ukifanya ni kosa Kiislamu na huko ni kama kuuoa au kuolewa na mkono wako ambako Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza.





Unapaswa uombe msamaha kwa Allaah Aliyetukuka kikweli kweli, utie Niyah ya kutorudia, ujute kwa uliyoyafanya na ufanye mazuri ili hilo baya lifutwe.





Baada ya kufanya hivyo nenda kwa daktari wa kike ili akupime kama ubikra umeondoka ama bado upo. Ikiwa upo mshukuru Allaah Aliyetukuka, rudi Kwake kwa kuomba toba na kufanya mazuri. Ukiwa ubikira umetoka vumilia kwani huo ni mtihani ambao umekukumba na umuombe Allaah Aliyetukuka Akusitiri usiwe ni mwenye kuingia aibu.





Ikiwa ubikra wako umeondoka na mume amekuja kukuoa na tunaomba awe wa kheri kwako katika Dini yako na maisha yako na hatima yako, na endapo baada ya kukuoa akataka kujua sababu za kupoteza ubikra wako, itabidi umweleze yaliyotendeka bila ya kumficha kwani ukweli huo ndio utakaomfanya kujua ukweli na kuridhika kwa hilo na kuishi kwa kuaminiana bila kujengeka wasiwasi wowote ule na wewe na maisha yako ya nyuma.





Na bila shaka Allaah Atakusitiri kwa kujuta kwa kitendo chako hicho.





Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo na manufaa zaidi:



Wanawake Wanaojichua, Bikira Huweza Kuondoka?



Kurudisha Ubikra Haifai Na Ni Udanganyifu



Dawa Gani Za Kurudisha Ubikra





Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Wanawake


Wanawake Wanaojichua, Bikira Huweza Kuondoka?



Alhidaaya.com





SWALI:



Assalaamu Alaykum Nashukuru Sana Kwa Kuweza Kusaidiana Sisi Waislam Wenyewe Kwa Wenyewe Allaah Atuzidishie Mie Nilikuwa Langu Naomba Mnijibu. Je Wanawake Wanaofanya Punyeto Bikira Yao Inaweza Kutoka. Asanteni Sana Kwa Kutuelimisha Allaah Wazidishie Amiiin





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho





Ubikira au ule ugozi ambao Kiswahili inaitwa kizinda, ni ngozi nyembamba sana ambayo hukatika kwa kutumiliwa nguvu.





Kujichua ni mojawapo ya njia ambayo inaweza kumfanya msichana akose ubikira wake. Mbali na kuwa kujichua ni haramu katika Dini yetu ya Uislamu. Allaah Aliyetukuka Anasema:



وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ ﴿٥﴾إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ ﴿٦﴾فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ ﴿٧﴾

Na ambao wanazihifadhi tupu zao. Isipokuwa kwa wake zao, au kwa iliyowamiliki mikono yao ya kuume basi hao hawalaumiwi.Lakini atakayetaka kinyume ya hayo; basi hao ndio wapindukao mipaka. [Al-Mu’minuun: 5 – 7]. Na makusudio mojawapo ya ‘anayetaka kinyume cha haya...’ ni kujichua.





Soma zaidi kuhusu masuala ya kujichua:



Nini Hukumu Ya Kujichua Sehemu Za Siri Au Kujisaga?



Kutumia Kitu Kujitoa Matamanio Nini Hukmu Yake



Mwanamke Kujichezea Hadi Apate Matamanio Afanye Ghuslu?



Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Atuepushe na jambo hilo.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Wanawake


Kurudisha Ubikra Haifai Na Ni Udanganyifu



Alhidaaya.com



SWALI:



Nimesoma nakala yenu, nimevutiwa sana na ushauri wenu. lakini kama ilivyo kwa wanaume zipo dawa za kienyeji za kuongeza uume ambazo hazina madhara. Sasa naomba kuuliza hakuna dawa za kienyeji za kuweza kurudisha bikira ambazo hazina madhara? Tafadhali naomba unijibu kwenye email yangu. asanteni sana.





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Hakika ni kuwa zipo dawa za kienyeji za kurudisha ubikira bandia. Hapa lakini tunataka kuuliza kwa nini mwanamke wa Kiislamu anataka kurudisha ubikira? Hii ni njia ya udanganyifu inayotumiwa na wasichana wanaoolewa hasa kwa siku hizi . Kwa nini wanafanya hivyo? Wao wanafanya hivyo ili kuwadanganya ma-bwana harusi kwa ule usiku wa mwanzo kuwa wao bado ni watahirifu na wamejihifadhi kutokana na zinaa. Wenye kufanya hayo aghalabu huwa wamezunguka na wanaume wengine kabla ya ndoa katika kitendo cha zinaa. Mume anadhania kwa usiku huo wa mwanzo kuwa mkewe ni bikira naye ni wa mwanzo kufungua kizibo ilhali si hivyo.



Ikiwa tayari umeolewa na unaishi na mumeo unatakia nini tena ubikira kwani ubikira ni kama ujana unapopita haurudi tena baada ya kukutana na mumeo.



Tutahadharini hayo kwani Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



" Mwenye kutughushi sisi (kutudanganya) si katika sisi" [Muslim].



Na tufahamu kuwa udanganyifu ni alama moja ya unafiki.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Maasi


Dawa Gani Za Kurudisha Ubikra



Alhidaaya.com





Swali:



Nimesoma nakala yenu, nimevutiwa sana na ushauri wenu. Lakini kama ilivyo kwa wanaume zipo dawa za kienyeji za kuongeza uume ambazo hazina madhara. Sasa naomba kuuliza hakuna dawa za kienyeji za kuweza kurudisha bikira ambazo hazina madhara? Tafadhali naomba unijibu kwenye email yangu. Asanteni sana





Jibu:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Tunataka kuuliza kwa nini mwanamke wa Kiislamu anataka kurudisha ubikira? Hii ni njia ya udanganyifu inayotumiwa na wasichana wanaoolewa hasa kwa siku hizi katika mwambao wa Tanzania na Kenya. Kwa nini wanafanya hivyo?



Bila shaka wengi wao wanafanya hivyo ili kuwadanganya ma-bwana harusi kwa ule usiku wa mwanzo kuwa wao bado ni watwahirifu na wamejihifadhi kutokana na zinaa.



Wenye kufanya hayo aghalabu huwa wamezunguka na wanaume wengine kabla ya ndoa katika kitendo cha zinaa. Mume anadhania kwa usiku huo wa mwanzo kuwa mkewe ni bikira naye ni wa mwanzo kufungua kizibo ilhali si hivyo.



Kadhaalika, hata ikiwa kuna dawa za kuukuza uume, vilevile hazifai kutumia kwani ni katika kubadili maumbile mtu aliyopewa na Allaah na vilevile kuna madhara mengine yanayopatikana kwa kufanya hilo kama kudhoofisha nguvu za uume.



Lililo bora ni mtu kubaki na maumbile yake yalivyo kama ni mwanamme na kama ni mwanamke ni kujihifadhi na kulinda utupu wake hadi kwa lililo la halali yake (mume wake). Na kurejesha ubikira wa bandia ili aje kuonekana na atakayemuoa kuwa ni msafi, aliyejitunza, mwaminifu... huo utakuwa ni uongo na haufai katika Dini. Isitoshe atakayekuoa akibainikiwa na hilo mbeleni, hatokuwa na imani na wewe na huenda ndoa ikavunjika.



Tutahadharini hayo kwani Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



"Mwenye kutughushi sisi (kutudanganya) si katika sisi" [Muslim].



Na tufahamu kuwa udanganyifu ni alama moja ya unafiki.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Wanawake


Bi Harusi Kujipamba Katika Mipaka Ya Shariy’ah Ya Dini



Alhidaaya.com





Swali:



In Shaa Allaah mutakuwa katika hali ya uzima na malipo mema kwa Allah amin.



Swali langu vp biharusi ajipambe kama ilivyokua ktk wake wa Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam na watoto wake? jee mapambo ya sasa inakubalika katika sharia kama vile mamekap na kupaka piko na utowaji wa halawa (yaani malaika za mwilini) na ma bleach? Naomba munijibu mapema shukran In Shaa Allaah Allah atawalipa. nami munikumbuke ktk email yangu iwe uepesi kwangu.





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Hakika si bi harusi tu ambaye anafaa kujipamba katika mipaka ya Shariy’ah, bali mwanamke ambaye ameolewa na mume ambaye ameoa wanafaa wote kujipamba kwa ajili ya mwenziwe. Mume anafaa ampambie mkewe na mke kumpambia mumewe.



Kuhusu pambo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anatueleza:



قُلْ مَنْ حَرَّمَ زِينَةَ اللَّـهِ الَّتِي أَخْرَجَ لِعِبَادِهِ وَالطَّيِّبَاتِ مِنَ الرِّزْقِ ۚ قُلْ هِيَ لِلَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا خَالِصَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٣٢﴾

Sema: “Nani aliyeharamisha mapambo ya Allaah ambayo Amewatolea waja Wake na vilivyo vizuri katika riziki?” Sema: “Hivyo ni kwa ajili ya wale walioamini katika uhai wa dunia; makhsusi (kwa Waumini) Siku ya Qiyaamah. Hivyo ndivyo Tunavyofasili waziwazi Aayaat kwa watu wanaojua.” [Al-A’raaf: 32]



Baada ya hayo itakuwa vyema tuangazie mapambo yanayokwenda sawa na Shariy’ah na yale ambayo yanakiuka mipaka ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).





Ama kuhusu vipodozi (make-up) havina tatizo kuvitumia kwa kujipamba ukiwa kwa mumeo au nyumbani kwako na Maharimu zako, ikiwa havitakuwa na madhara. Tunavyofahamu vipodozi hivi vya sasa vinatengenezwa na kemikali. Ikiwa kutapatikana kuwa utumiaji una madhara na mwana Aadam, basi havitakubaliwa na Shariy’ah kutumiwa. Hiyo ni kuwa msingi mkubwa wa Shariy’ah ni Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inayosema:



"Haitakiwi kujidhuru wala kudhuriana" [Ibn Maajah na Ad-Daaraqutwniy, nayo ni Hasan]



Piko nayo ni aina ya urembo au pambo kama hinna hivyo hakutokuwa na utata wowote kuhusu matumizi yake. Hata hivyo imetambulika kwamba piko huwa ina athari kwa wengine wenye ugonjwa wa hasasiya (allergy - kuwa na mzio) na hivyo kumletea kuvimba kwa mwili na matatizo mengine ya kiafya. Pia zipo piko ambazo zinafanya ugozi kwenye ngozi hivyo kuzuia maji kufika kwenye ngozi wakati wa kutawadha au kuoga josho la janaba. Ikiwa piko kwako ina sifa ya kwanza au ya pili au zote mbili itakuwa haifai kwako kuitumia kwa misingi tuliyoeleza hapo juu.





Uislamu umetuletea mambo ya Fitwrah (maumbile ya asli ya Uislam). Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alituagizia: " Mambo kumi ni katika Fitwrah (maumbile ya asli ya Kiislamu): 'Kupunguza masharubu, kufuga ndevu, kupiga mswaki, kupitisha maji puani (kusafisha), kukata kucha, kusafisha penyo za vidole, kung'ofoa (kunyoa) nywele za kwapa, kunyoa nywele za sehemu za siri, na kujisafisha kwa maji baada ya kujisaidia na msimuliaji akasema kasahau la kumi, lakini inaweza kuwa ni kusafisha mdomo (kusukutua)" [Muslim na Abu Daawuwd kutoka kwa mama wa waumini 'Aaishah Radhwiya Allaahu 'anhaa].





Ukiyatizama mambo haya kumi utakuta yafuatayo ni kuweka unadhafa wa mwili, kwa mfano Kupunguza masharubu, kupiga mswaki, kupitisha maji puani (kusafisha), kukata kucha, kusafisha penyo za vidole, kung'ofoa (kunyoa) nywele za kwapa, kunyoa nywele za sehemu za siri, na kujisafisha kwa maji baada ya kujisaidia na lakini inaweza kuwa ni kusafisha mdomo (kusukutua). Hivyo, Muislamu amehimizwa kuweka usafi kwa kuosha viungo kadhaa, kutoa nywele ambazo ndio chanzo cha kuleta uchafu isipokuwa kunyoa ndevu (mwanaume) kumekatazwa kabisa.





Ama utoaji wa nywele ndogo ndogo ambazo baadhi ya watu huziita malaika hakuna tatizo lolote katika Dini ikiwa ni kwa sababu ya kujiremba au kujiweka katika hali ya usafi kama vile kunyoa nywele za kwapani na sehemu za siri. Ama katazo lililokuja ni kupunguza au kunyoa nyusi kwa dalili ya Hadiyth ifuatayo:




عَنْ عَلْقَمَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، لَعَنَ اللَّهُ الْوَاشِمَاتِ، وَالْمُسْتَوْشِمَاتِ، وَالْمُتَنَمِّصَاتِ وَالْمُتَفَلِّجَاتِ لِلْحُسْنِ، الْمُغَيِّرَاتِ خَلْقَ اللَّهِ تَعَالَى، مَالِي لاَ أَلْعَنُ مَنْ لَعَنَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم وَهْوَ فِي كِتَابِ اللَّهِ ‏ ‏وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ‏ ‏‏.‏

Amesimulia ‘Alqamah (رضي الله عنه): Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه) amesema: Allaah Amewalaani wenye kuchanja, na wenye kuchanjwa, na wenye kunyoa nyusi, na wenye kuchonga meno kwa urembo, na wenye kubadilisha umbile la Allaah (سبحانه وتعالى). Kwa nini nisimlaani yule aliyelaaniwa na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na aliyelaaniwa katika Kitabu cha Allaah?:



وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ﴿٧﴾

“Na lolote analokupeni Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) basi lichukueni, na analokukatazeni, basi jiepusheni.” [Al-Hashr (59:7) Hadiyth amepokea Imaam Al-Bukhaariy Kitabu Cha Mavazi (77)]





Na katika Hadiyth nyingine tunaongezewa mapambo ambayo hayafai kufanywa na Muislamu. Na imepokewa kwa Asmaa' (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba mwanamke fulani alimuuliza Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):





"Ee Rasuli wa Allaah! Binti yangu amepatwa na surua zikapuputika nywele zake, nami nimemuozesha; Je, niziunganishe?" Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamjibu: "Allaah Amemlaani mwenye kuunganisha nywele zake (au nywele za mwengine kwa nywele nyengine) na mwenye kuungwa (au kuvaa nywele hizo )" [Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nasaaiy].





Na Hadiyth ya 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) imenukuliwa na al-Bukhaariy, Muslim na an-Nasaa'iy). Na katika riwaayah nyengine:



"Mwenye kuunganisha nywele na mwenye kumtaka mwengine amfanyie kazi hiyo (mwenye kutamani kuzivaa nywele hizo za bandia)". Na 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anha) amepokea mfano wake.





Katika Hadiyth hizi na nyingine zilizo sahihi tunaelezewa kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza baadhi ya mapambo nayo ni, kutoa au kuchonga nyusi, kuunga nywele, kuchonga meno kwa urembo, kuchanja kwenye mwili kwa kujichora tattoo. Hivyo ni juu yetu kutahadhari na mapambo hayo kwani kuyafanya huwa tunaingia katika laana ya Allaah ('Azza wa Jalla) Naye Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:



إِن يَدْعُونَ مِن دُونِهِ إِلَّا إِنَاثًا وَإِن يَدْعُونَ إِلَّا شَيْطَانًا مَّرِيدًا ﴿١١٧﴾لَّعَنَهُ اللَّـهُ ۘ وَقَالَ لَأَتَّخِذَنَّ مِنْ عِبَادِكَ نَصِيبًا مَّفْرُوضًا ﴿١١٨﴾وَلَأُضِلَّنَّهُمْ وَلَأُمَنِّيَنَّهُمْ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُبَتِّكُنَّ آذَانَ الْأَنْعَامِ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلْقَ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَتَّخِذِ الشَّيْطَانَ وَلِيًّا مِّن دُونِ اللَّـهِ فَقَدْ خَسِرَ خُسْرَانًا مُّبِينًا ﴿١١٩﴾

Hawaombi badala Yake isipokuwa miungu ya kike na hawaombi isipokuwa shaytwaan muasi.

Allaah Amemlaani. Na (shaytwaan) akasema: "Kwa hakika nitashika katika waja Wako sehemu maalumu. Na hakika nitawapoteza, na nitawashawishi matamanio ya kulaghai, na nitawaamrisha. Basi watakata masikio ya wanyama (wawatukuze), na nitawaamrisha watabadili maumbile ya Allaah.” Na atakayemfanya shaytwaan kuwa rafiki mwandani badala ya Allaah basi kwa yakini amekhasirika khasara bayana. [An-Nisaa: 117-119]



Ama kuhusu kutia bleach ili kubadili rangi ya mwili au kwa pambo hilo haliruhusiwi na Uislamu. Sababu ni kuwa huwa unabadilisha umbile alilokuumba nalo Allaah ('Azza wa Jalla) ambako kumekatazwa kama ilivyo Aayah iliyo juu [An-Nisaa 117 – 119]. Na pia bleach ni mchanganyiko wa makemikali ambayo yana madhara makubwa kwa mwili. Kwa sababu ya hiyo leo tunaona wanawake wenye kumea ndevu na kuwia vigumu kufanyiwa upasuaji kwa sababu ya ngozi ya juu kuathirika na kemikali na madhara mengine mengi.





Kwa ajili hiyo ni juu yetu kuwakumbusha wenye kutumia wasijitie kwenye maangamivu na hivyo kuhasirika hapa duniani na Kesho Aakhirah.





Vifuatavyo ni baadhi ya vipodozi vya asli ambavyo vinafaa kutumia na vimeonekana kuwa vinaleta manufaa katika kuiboresha ngozi na nywele za mwanamke:



1. Hinna kwenye nywele.



2. Mchanganyiko wa mafuta ya lozi, nazi na zaytuni.



3. Majani ya mkunazi yaliyosagwa kwa ajili ya kusafishia uso na mwili.



4. Mchanganyiko wa Habba Sawdaa iliyosagwa na mafuta ya zaytuni upake usoni kisha ukae nayo katika jua kwa muda kidogo kisha uoshe.





Na Allaah Anajua zaidi.
 
Maswali: Wanawake


Hana Muda Wa Kujipamba Mbele Ya Mume Akijipamba Wakati Mwengine Inafaa?



Alhidaaya.com





SWALI:



Assalamu alaykum warahmatullah wabarakatuh.



Ningependa kumshukuru Allaah kwa kuwapa nguvu na mafanikio katika kuiendesha Alhidaaya. Mimi ni msomaji mkubwa na nimefaidika sana na website hii. Allah aienzi Alhidaaya.



Ndugu zangu waislam nina swali kuhusu kujipamba kwa ajili ya mume. Mimi ni mwanamke ninaye enda kazini na nina watoto ambao nikirudi jioni ni lazima kuwahudumia. Nikiingia nyumbani nashughulika na kazi. Mume wangu yuko nje. Akija ni saa tatu, nimechoka hata wakati mwengine huwa nimelala. Mwisho wa wiki nikiwa nyumbani yeye hutoka, hata saa nyengine humwambia akae ili nipate kujipamba lakini hakai. Jee, nikijipamba na yeye hayupo ni sawa? Na je nisipojipamba itakuwaje? Naomba ufafanuzi ndugu zangu.





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Hakika ni kuwa mume anafaa ajipambe kwa ajili ya mkewe na vile vile mke kwa ajili ya mumewe. Hivyo ndivyo alivyokuwa akifanya Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhuma).





Kulingana na swali lako japokuwa ni la upande mmoja inaonyesha kuna tatizo baina yako na mumeo. Itabidi mwanzo mkae na kulizungumzia swali hilo kwa kina na uwazi. Hujasema ikiwa mumeo anafanya kazi hadi saa hizo, au ana mizunguko yake tu.





Wanandoa na haswa ikiwa mke pia anafanya kazi wasaidiane ili kuweka hali kuwa nzuri katika mazingira ya nyumbani. Ndio Allaah Aliyetukuka Akatuambia:

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ

Na shirikianeni katika wema na taqwa,...[Al-Maaidah 5: 2].





Haifai kabisa kwa mume kuchelewa kuja nyumbani pasi na udhuru wa aina yoyote, na hata ikiwa ni mwisho wa wiki asiwe ni mwenye kutoka nje ilhali mke atamtaka abakie naye.





Ama kujipamba kwako kwa Niyah ya kumpambia mume ni ‘Ibaadah, ikiwa atakuwepo nyumbani au hatokuwepo. Wewe unahitajika kufanya hivyo ili upate thawabu kutoka kwa Allaah Aliyetukuka na huenda pia kufanya hivyo kukamvutia mumeo akawa anarudi mapema na kuwa karibu zaidi nawe.





Itabidi mkae kitako kama wanandoa mjadili mahusiano yenu ya kinyumba na mrekebishe kasoro zozote zile. Ikiwa mtachelewa kuyazungumzia hayo machache, bai yanaweza kulimbikizana matatizo na kukazuka matatizo makubwa zaidi ambayo yanaweza kukosa suluhisho.





In shaa Allaah tunamuomba Allaah Awafanyie wepesi na Awaweke karibu zaidi katika ndoa yenu.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Wanawake


Hukmu Ya Hijaab - Je, Inasababisha Kutoka Nywele?



Alhidaaya.com





SWALI:



Assalaamu Alaykum Ndugu Zangu, Naomba Kuwa Uliza Nipate Kujua.



Mwanamke Ni Lazima Kufunika Kichwa Mbele Za Muhreem. Ryt Lakini Mbele Za Watu Wake Wa Nyumbani Na Muhreem Wake Akae Kichwa Wazi-----ryt Tumesisitizwa Tufanye Dhikrullah Saa Zote Na Jina La Allaah Huwezi Au



Una Weza Kutaja Kichwa Wazi ??? Sasa Mwanamke Wakati Gani Ata Vua Hijaab?



Mimi Nime Nyonyoka Nywele Na Nimeambiwa Sababu Ni Hijaab. Inawezekana Allah Atuwekee Sharia Ya Kutudhuru???? Plz Help.



Jazaakallaahu Kheir Fiamaanillah





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Mwanamke akiwa nyumbani na mumewe au maharimu zake (wanaume wasioweza kumuoa) Shariy’ah imempa ruhusa kutokuwa katika vazi la hijaab. Isipokuwa kuweko na mipaka ya kuonyesha mwili wake asjiweke wazi sana hadi akaonyesha zaidi kwao sehemu ya mwili wake, au kuvaa nguo iliyobana au inayoonyesha mwili wake wa ndani n.k. Ni muhimu kuweko stara baina yao japokuwa ni maharimu wake.





Na ikiwa upo na mume wako chumbani basi unaruhusiwa kupunguza mavazi yako kadiri unavyopenda na kadiri mumeo atakavyotaka. Hilo halina shaka.





Kuhusu kumdhukuru Allaah ('Azza wa Jalla), inaruhusiwa kumdhukuru bila ya kujifunika kichwa.





Ama kuhusu kunyonyoka nywele haina uhusiano wowote na uvaaji wa hijaab. Lau ingekuwa kuwa hivyo hawangepiga marufuku jambo hilo katika nchi za Magharibi Wangewaacha Waislam wawe na uhuru wao katika kuvaa kama walivyoamrishwa na Rabb wao, ili wanyonyoke nywele kwani ingelikuwa ndio furaha yao.





Mwaka 2005 katika gazeti moja Kenya lilitaja utafiti uliofanywa nchi ya Uzunguni kuwa kuvaa Hijaab kunaleta ugonjwa wa baridi yabisi. Kama hilo lingekuwa kweli, basi leo hii wanawake wote wangekuwa wapo nyumbani hawawezi kutembea! Lakini hizo ni propaganda maarufu zinazoongozwa na nchi za kimagharibi.





Ugonjwa wa kupuputika (kunyonyoka) nywele ni kawaida kwa wanawake na wanaume ikiwa watakosa protini katika vyakula. Ugonjwa kama huu huweza kutibika kwa kutumia aina fulani ya mafuta ambayo inazipatia nguvu Hivyo jambo hilo si la kumshitua wala kumtia taharuki mtu yeyote yule.





Kuliweko na Swahaabiyyah katika enzi za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliyepata tatizo hilo. Asmaa (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amesema: Mwanamke mmoja alimuuliza Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Ee Rasuli wa Allaah! Binti yangu alipatikana na shurua zikatoka nywele zake, nami sasa ninamuoza, je, niziunge nywele zake [kwa kuziunganisha na nywele zingine]?)) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamjibu: ((Allaah Amemlaani muunga nywele na muungwaji)) [Al-Bukhaariy].





Bila shaka inafahamika kuwa Allaah ('Azza wa Jalla) Ndiye Muumba wetu, hivyo, Anajua yale mambo yanayotudhuru na yanayotunufaisha katika maisha yetu. Hatuamuru kufanya kitu ila kina faida kemkemu kwetu japokuwa huenda tusilifahamu hilo na jambo lolote Analotukataza basi lina madhara makubwa kwetu.





Kunyonyokwa na nywele ni magonjwa ambayo yanaweza kumpata mmoja miongoni mwetu, na kila ugonjwa una dawa yake kama alivyotueleza hayo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



عن أبي الدرداء رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((إن الله تعالى أنزل الداء والدواء وجعل لكل داء دواء فتداووا ولا تداووا بالحرام))

Imetoka kwa Abuu Ad-Dardaa (Radhwiya Allahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Ameteremsha maradhi na dawa zake. Kwa kila maradhi kuna dawa yake, basi jitibuni wala msijitibu kwa yaliyo haraamu)) [Al-Bukhaariy na Abu Daawuwd]



Na pia:



عن عبدالله بن مسعود :قال رسول الله صلى الله عليه وآله وسلم (( ما أنزلَ اللَّهُ داءً إلَّا أنزلَ لَه شفاءً فعليكُم بألبانِ البقرِ فإنَّها تَرُمُّ من كلِّ الشَّجرِ))

Imetoka kwa 'Abdullah bin Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Hakuteremsha maradhi ila Ameteremsha dawa zake, basi juu yenu (kunyweni) maziwa ya ng'ombe kwani yanatokana na kila aina ya miti)) [Hadiyth Swahiyh au hasan, ameisahihisha Al-Albaaniy katika As-Silsilah Asw-Swahiyhah (4/208), Swahiyh Al-Jaami’ (1808)]





Hivyo, Kwa kuwa hakika ni hiyo basi suluhisho ni kutafuta tiba endapo tunakuwa wagonjwa.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Wanawake



Hijaab Ya Sharyi'ah Inahusu Kufunika Uso Na Miguu?




Alhidaaya.com







SWALI:



Naomba nifahamishwe hijabu ipasavyokuwa, je uchi wa wa mwanamke does it include miguu? since summer is nearing most of us are shoping for open shoes, is it allowed, I know other madh-habs say we should infact cover our whole faces but I don’t think the qur'an specifies that in particular?



JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Kuhusu kufunika Miguu:



Naam miguu ya mwanamke inalazimu kufunikwa kwa dalili:



Imepokewa kutoka kwa Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amesema: nilimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakati lilipozungumzwa suala la kipimo cha nguo ya chini ya mwanamume (ambayo inatakiwa isivuke mafundo ya miguu): Ee Rasuli wa Allaah, na ipi hukumu ya kipimo cha nguo ya mwanamke? Akasema: "Ataiteremsha (kiasi cha) shubiri).” Akasema Ummu Salamah kwa maana hiyo si itaonekana (miguu yake)? Akasema: (Na aiteremshe) kiasi cha dhiraa moja wala asizidishe zaidi ya hapo." (Abuu Daawuwd: 4117 na Maalik katika Muwatwa: 2017).





Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyah (Rahimahu Allaah) amesema katika Majmuw’ Al-Fataawaa 22/110:



“…….Ni dhahiri kwamba rai ya Imaam Ahmad iko wazi kabisa kuwa kila kiungo cha mwanamke ni ‘awrah’ (uchi) hata pia kucha zake. Na hii pia ni rai ya Imaam Maalik.



Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

وَلَا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِن زِينَتِهِنَّ ۚ

Na wala wasipige miguu yao yakajulikana yale wanayoyaficha katika mapambo yao. [An-Nuwr: 31]





Imaam Ahmad amesema: “…. Mapambo ambayo yaliyodhihirika ni nguo ….. kila kiungo cha mwanamke ni ‘awrah’ hata kucha zake. Imesimuliwa katika Hadiyth “Mwanamke ni ‘Awrah”. Hii ni umbo lote la mwanamke. Na sio makruwh (haichukizi) kufunika mikono yake wakati wa kuswali, kwa hiyo pia ni sehemu ya ‘awrah kama ilivyo miguu. Hivyo Qiyaas imekusudiwa kwamba uso pia ni ‘awrah’ japokuwa haukutakiwa kufunikwa wakati wa Swalaah na sio kama mikono…” [Sharh Al-‘Umdah 4/267-268]





Dalili anayoichukulia Imaam Ahmad ni:



Imesimuliwa na ‘Abdullaah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwanamke ni ‘awrah’ na anapotoka nje basi matumaini ya shaytwaan huwa juu)) [At-Tirmidhiy, 1173 na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy 935]



Kuhusu kufunika uso:



Kuhusu kauli yako dada yetu kuwa Qur-aan haikutaja kuhusu kufunika uso, si sahihi kwa sababu imetajwa katika Suwrah Al-Ahzaab wanawake kujigubika jilbaab. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:



يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٥٩﴾

Ee Nabiy! Waambie wake zako, na mabinti zako, na wanawake wa Waumini wajiteremshie jilbaab zao. Hivyo kunapeleka karibu zaidi watambulikane (kwa heshima) wasiudhiwe. Na Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Al-Ahzaab: 59]



Na kutokana na kauli iliyo sahihi kabisa ni kwamba jilbaab ni guo ambalo mwanamke anaivaa juu ya khimaar kutoka kichwani na inashuka kumfunika uso wake.



Ingawa ‘Ulamaa wamekhitilafiana katika swala hilo ila rai iliyo ya nguvu kabisa ni kujuzu kujifuniko uso. Na baadhi ya dalili ni kama ifuatavyo:



Kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba ilipoteremeshwa kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ ۖ

Na waangushe khimaar (shungi) zao mpaka vifuani mwao… [An-Nuwr: 31]



Wanawake wa Ki-Muhaajirina walichana na kukata gauni zao pembeni ili kufunikia nyuso zao )) [Al-Bukhaariy]



Na 'Aliy bin Abiy Twalhah amerepoti kwamba Ibn 'Abbaas amesema kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amewaamrisha wanawake waumini wajifunike nyuso zao kutoka vichwani mwao wakiacha jicho moja tu, wanapotoka nje ya nyumba zao kwa ajili ya kutafuta mahitajio yao. [Tafsiyr Ibn Kathiyr: 8: 45].



Na dalili nyengine ni pindi mwanamke anayeingia katika ihraam amekatazwa kujifunika uso. Hii bila shaka ina maanisha kwamba mwanamke pindi akiwa hayuko katika ihraam, anapaswa kujifunika uso. Na pia dalili ni kauli ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



((لَا تَنْتَقِبُ الْمَرْأَةُ الْمُحْرِمَةُ وَلَا تَلْبَسُ الْقُفَّازَيْنِ))

((Mwanamke katika Ihraam asivae niqaab wala glavu)) [Al-Bukhaariy]



Na pia katika safari ya Hajj, 'Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amesema: "Wapandaji (wanaume) walipita mbele yetu tukiwa na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Walipokuwa sambamba mbele yetu tuliteremsha utaji (shungi) zetu usoni na vichwani mwetu, kisha walipotoweka tulijifunua)) [Abu Daawuwd na Ibn Maajah]



Bonyeza kiungo kifuatacho upate faida zaidi:





Je, Inafaa Mume Kumlazimisha Mke Kuvaa Niqaab?





Mwanamke wa Kiislamu analazimika kuyafahamu masharti ya hijaab kama yafuatavyo:



1. Jilbaab liwe refu la kukufunika mwili mzima mpaka miguu, na kama halikufunika miguu basi mwanamke avae soksi.





2. Jilbaab liwe pana na sio lenye kuonyesha umbo, yaani lisiwe lenye kubana popote mwilini.





3. Jilbaab liwe zito na si jepesi la kuonyesha mwili.





4. Jilbaab lisiwe na marembo yoyote yale ya kuvutia.





5. Jilbaab halitakiwi lifanane na mavazi ya makafiri.





6. Jilbaab halitakiwi liwe ni katika mavazi ya fakhari.





7. Wanawake kutokuvaa nguo zinazofanana na nguo za kiume.





8. Kutotia manukato.







Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Wanawake


Inafaa Kutokuvaa Hijaab Kwa Khofu Ya Wazazi Wake Kujua Kama Kasilimu?



Alhidaaya.com





SWALI:

Shukrani zote zinamstahikia Allaah, kuna mwanafunzi mwenye asili ya kihindi anayeendlea na masomo yake nchini urusi amesilimu na hataki wazazi wake wajue ili kukamilisha azma hiyo ameamua kutojitofautisha kama alivyo kuwa mwanzo ikwa pamoja na kutovaa hijaab, je inajuzu kufanya hivyo?





JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Mas-alah ya Dini ya hasa ya kuvaa Hijaab kwa mwanamke wa Kiislamu si mas-alah ya khiyari bali ni wajibu kwake akiwa ni Muislamu au amesilimu kutekeleza wajibu huo. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:



وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ ۗ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا ﴿٣٦﴾

36. Na haiwi kwa Muumini mwanamme na wala kwa Muumini mwanamke, Anapohukumu Allaah na Rasuli Wake jambo lolote, iwe wana hiari katika jambo lao. Na anayemuasi Allaah na Rasuli Wake, basi kwa yakini amepotoka upotofu bayana. [Al-Ahzaab: 36]



Naye ikiwa amejisalimisha katika kukubali dini ya haki basi inampasa asiogope mtu yeyote ila Muumba wake pekee. Hivyo ni lazima athibitishe Uislamu wake na atambue kuwa ni kawaida ya wengi wanaosilimu bila ya wazazi wao kupatwa na mitihani kama hiyo. Kuvumilia na kuwa imara katika dini yake ya haki ni jambo linalompasa. Wazazi wake hawana majukumu naye tena katika mas-alah ya dini, bali ni yeye mwenyewe ajiamulie yanayompasa kutekeleza amri za Mola. Wazazi wanabakia kuwapa heshima yao na kuwafanyia ihsaan (wema) kama kawaida.



Ingawa wazazi wanayo haki kwako ya kuwatii amri zao, lakini haipasi kuwatii katika maasi au amri zozote za Rabb Muumba. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):



وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ وَهْنًا عَلَىٰ وَهْنٍ وَفِصَالُهُ فِي عَامَيْنِ أَنِ اشْكُرْ لِي وَلِوَالِدَيْكَ إِلَيَّ الْمَصِيرُ ﴿١٤﴾وَإِن جَاهَدَاكَ عَلَىٰ أَن تُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا ۖ وَصَاحِبْهُمَا فِي الدُّنْيَا مَعْرُوفًا ۖوَاتَّبِعْ سَبِيلَ مَنْ أَنَابَ إِلَيَّ ۚ ثُمَّ إِلَيَّ مَرْجِعُكُمْ فَأُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٥﴾

14. Na Tumemuusia insani kwa wazazi wake wawili. Mama yake ameibeba mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumwachisha ziwa katika miaka mwili; ya kwamba, unishukuru Mimi, na wazazi wako; Kwangu ndio mahali pa kuishia. Lakini wakikushikilia kuwa Unishirikishe na ambayo huna elimu nayo, basi usiwatii. Na suhubiana nao kwa wema duniani, na fuata njia ya anayerudi kutubia Kwangu. Kisha Kwangu ndio marejeo yenu, na Nitakujulisheni yale mliyokuwa mkiyatenda. [Luqmaan:14- 15]



Swahaba wa mwanzo kuingia katika Uislamu walipatwa na mitihani mikubwa zaidi ya mateso kutoka kwa Makafiri na wengine kutoka kwa wazazi wao lakini hawakurudi katika ukafiri bali walithibitika katika Uislamu na kupokea hiyo mitihani ambayo ni kama majaribio ya kuhakisha Uislamu wa mtu:



أَحَسِبَ النَّاسُ أَن يُتْرَكُوا أَن يَقُولُوا آمَنَّا وَهُمْ لَا يُفْتَنُونَ ﴿٢﴾وَلَقَدْ فَتَنَّا الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۖ فَلَيَعْلَمَنَّ اللَّـهُ الَّذِينَ صَدَقُوا وَلَيَعْلَمَنَّ الْكَاذِبِينَ ﴿٣﴾

Je, wanadhani watu kwamba wataachwa kwa kuwa wanasema: Tumeamini. Nao ndio wasijaribiwe? Kwa yakini Tuliwajaribu wale wa kabla yao, ili Allaah Awatambulishe wale walio wakweli na ili Awatambulishe walio waongo. [Al-'Ankabuut: 2-3]



Ama kuhusu Hijaab Allaah Anatubainishia wazi kabisa pale Aliposema:



يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٥٩﴾

Ee Nabiy! Waambie wake zako, na mabinti zako, na wanawake wa Waumini wajiteremshie jilbaab zao. Hivyo kunapeleka karibu zaidi watambulikane (kwa heshima) wasiudhiwe. Na Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Al-Ahzaab: 59].



Jambo muhimu la sisi kujiuliza je, Hijaab ya Kiislamu inafaa iwe vipi? Au masharti ya kivazi cha Kiislamu ni yepi? Masharti ni kama yafuatayo:



- Vazi kuwa pana.

- Kutoonyesha maumbile wala vilivyo ndani.

- Kusitiri uchi.

- Kutokuwa na mapambo aina yoyote.

- Kutofanana na vazi la kikafiri.

- Kutokuwa vazi la kujionyesha na kujifakharisha.

- Liwe halifanani na vazi la mwanamme.



Ushauri wetu utakuwa ni yeye awe ni mwenye kuvaa vazi lenye sifahizo.



Tunamuombea dada yetu kila la khayr aweze kuvuka mtihani huo kwa salama kabisa.





Na Allaah Anajua zaidi.
 
Back
Top Bottom