Ramadhan Special Thread
Maswali: Wanawake


Inafaa Mwanamke Kuvaa ‘Abayah Zenye Vito Na Marembo Japokuwa Amejifunika Vizuri?



Alhidaaya.com





SWALI:



Asalamy Aleikum



Kwanza nawashkuru kwa ku2elimisha allaah subhana wa taala) atawalipa mimi nilikuwa naomba munifafanulie kuhusu vazi analotakiwa kuvaa mwanamke wakiislam je haya mabaibui 2nayoyavaa yanafaa je kati ya jilbab na haya mabaibui ambayo yana vito vinavyowaka pamoja mitandio mifupi naomba u2eleweshe mana vaz la baibui sasa limekuwa kama ni fashen nategemea majibu mazuri yatakayo2fundisha inshaalla





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho





Vazi la mwanamke Muislamu kuwa ni la sawa ni lazima litimize masharti kadhaa. Ikiwa vazi hilo litatimiza basi litakuwa la Kiislamu la, sivyo basi itakuwa mwanamke huyo amevaa nguo lakini si ya Kiislamu. Kabla ya kuingilia masharti, hebu tutazame Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anavyosema:



يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٥٩﴾

Ee Nabiy! Waambie wake zako, na mabinti zako, na wanawake wa Waumini wajiteremshie jilbaab zao. Hivyo kunapeleka karibu zaidi watambulikane (kwa heshima) wasiudhiwe. Na Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Al-Ahzaab 33: 59].





Tufahamu kuwa vazi hilo ni amri kutoka kwa Allaah Aliyetukuka, hivyo hatuwezi kuvaa tunavyotaka.



Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema tena:



وَقُل لِّلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ ۖ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ ...

Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao na wahifadhi tupu zao, na wala wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa yale yanayodhihirika. Na waangushe khimaar (shungi) zao mpaka vifuani mwao, na wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao, au baba zao, au... [An-Nuwr: 31].



Ama kuhusu masharti kwa vazi la kike kuitwa la Kiislamu ni kama yafuatayo:



1. Vazi la mwanamke wa Kiislamu ni lazima lisitiri mwili mzima: Wanachuoni wametofautiana kuhusu viganja vya mkono na uso kwa kauli mbili – wapo wanaosema ni lazima vifunikwe na wanaokubali kuwa vinafaa viachwe. Wengine wameunganisha kauli hizo kwa kusema hadi ya chini ni kuacha vitanga vya mkono na uso kuwa lakini vikifunikwa ni bora zaidi. Kuhusu kusitiri tayari tumenukuu aayah mbili – Suwrah Al-Nuwr Aayah ya 31 na Suwrah Al-Ahzaab Aayah ya 59.



2. Vazi lenyewe lisiwe ni pambo: Hii ni kwa kauli ya Aliyetukuka: "wala wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa yale yanayodhihirika." [An-Nuwr: 31). Na kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): "Watu aina tatu hata usiwaulize: … Na mwanamke ambaye mumewe hayupo lakini amemtosheleza na mahitaji yake yote ya kidunia, naye akafanya Tabarruj" [Ahmad na al-Haakim]. Tabarruj ina maana mwanamke kuonyesha pambo lake na uzuri wake ambao unatakiwa usitiriwe, ambavyo vinamfanya mwanamme awe na matamanio. Na kusudio ya amri ya kuvaa Jilbaab ni kusitiri pambo la mwanamke, hivyo haingii akilini iwe Jilbaab lenyewe liwe ni pambo.



3. Vazi liwe zito, kisionekane kilicho ndani yake: Hii ni kwa kauli yake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Watu aina mbili wa Ummah ni wa Motoni nami sijawaona… na wanawake waliovaa nguo lakini wapo uchi. Hao hawatoingia Peponi wala hawatopata harufu yake japokuwa harufu yake inafika masafa kadhaa na kadhaa” [Muslim]. Lengo ni kwa wale wanawake wanaovaa nguo hafifu ambayo inatoa sifa kamili na wala haisitiri. Hao kwa jina wamevaa lakini kwa uhakika wako uchi.



4. Vazi liwe pana, sio la kubana: Kwani vazi likimbana mwanamke itamtoa umbile lake lote hivyo kumfanya kama kwamba hajajisitiri. Hii ni kwa mujibu wa kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kumwambia Usaamah bin Zayd (Radhwiya Allaahu ‘anhuma): “Muamuru mkeo ajaalie Ghulaalah (shuka inayovaliwa chini ya nguo), kwani nakhofia isije ikasifu ukubwa wa mifupa yake” [Ahmad na Abu Daawuud].



5. Vazi lisitiwe manukato: Hii ni kutokana na kauli ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Mwanamke yeyote anayejitia manukato, akawapita mbele ya watu ili wapate harufu yake, basi yeye ni mzinifu” [Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na an-Nasaa’iy].



6. Vazi lisifanane na vazi la Kiume: Huku ni kwa kule kulaaniwa na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wanaume wanaoshabihiana na wanawake na wanawake wenye kujifananisha na wanaume [al-Bukhaariy, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na Ibn Maajah]. Na pia amesema (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amelaaniwa mwanamme mwenye kuvaa nguo za kike, na mwanamke mwenye kuvaa nguo za kiume [Ahmad na Abu Daawuud].



7. Vazi lisifanane na vazi la kikafiri: Shari’ah imekariri kutojuzu kwa Waislamu wanaume kwa wanawake kujifananisha na makafiri sawa katika ‘Ibaadah, au sherehe, au katika mavazi yao na kadhalika. Ama kuhusiana na kivazi, ni ile Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Amru (Radhwiya Allaahu ‘anhuma) aliyesema: Alimuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa amevaa nguo mbili za njano, akamwambia: “Hakika hizi nguo ni za makafiri kwa hivyo usivae” [Ahmad, Muslim na an-Nasaa’iy].



8. Vazi lisiwe ni la kujionyesha: Hii ni kwa kauli yake Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): "Mwenye kuvaa nguo ya umaarufu na kujionyesha hapa duniani, Allaah Atamvisha nguo ya udhalili Siku ya Qiyaamah, kisha Atamuingiza Motoni" [Abu Daawuud na Ibn Maajah].





Haya ndio masharti ambayo yanafaa yawepo katika vazi la mwanamke ili lijulikane kuwa ni la Kiislamu. Ikikosekana sharti hata moja basi litakuwa basi lenyewe ni la Kiislamu. Kwa ajili hiyo, ma ‘Abaaya mengi hayatimizi masharti haya wala yale mabaibui ya fesheni. Nasaha kwa dada zetu waepukane na hayo.





Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:



Mwanamke Anavaa Hijaab Lakini Anavaa Suruwali Ya Kubana Anaposwali, Inakubaliwa Swalah Yake?



Kuvaa Niqaab Ni Fardhi? Nini Hukmu Ya Mwanamke Kuvaa Suruwali?





Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Wanawake


Kunyofoa Au Kunyoa Au Kuchonga Nyusi Ni Kulaaniwa na Allaah



Alhidaaya.com





Swali La Kwanza:



Sheikh, Asaalam-aleiakum



Swala langu mimi nimeolewa mimi toka zamani sipendi kutowa nyusi najuwa kuwa ni dhambi lakini nilipoolewa natowa lakini sio ile kuonesha sana lakini hata hivyo sipendi lakini mume wangu anapenda nitowe na mimi mpaka nangombana na yeye kuwa sitaki kutowa hivyo natowa kwa sababu yake. Jee ikiwa natowa kwa sababu yake sio kwa watu jee nimusikilize yeye niendelee kutowa? Naomba unijibu. Shukuran



Swali La Pili:



Je, kunyoa nyusi ni kupata laana ya Allah?.



Swali La Tatu:

Kunyoa nyusi kwa mwanamke inajuzu? Niliwahi kumuuliza Shekhe mmoja akaniambia kuwa inafaa kuzitengeneza.



Mimi nikamuuliza mbona kuna Hadiyth inasema kuwa " Amelaaniwa yule wenye kunyoa nyusi na mwenye kunyolewa ..............." Shekhe huyo akanifahamisha yakuwa hadithi hii wengi hawaifahamu maana yake, akaendelea kusema " Zamani Wanawake wa kureshi walikuwa wakinyoa nyusi zote na kutia wanja kwa mtindo waupendao lakini sio kuzitengeneza. Kufanya hivo ni katika kujiweka safi kwa mwanamke na hasa kama atafanya kwa ajili ya mumewe na pia akifanya hivo mwanamke anatakiwa aufunike uso wake au ashushe shungi lake kuzifunika zile nyusi zake wasizione wale wasiomstahikia.



Mimi nikawa ninafanya hivo na wezangu waliponiuliza nami nikawafahamisha kama vile nilivyouliza lakini la kushangaza Nilipokutana nae tena huyo Shekhe katika mazungumzo tu akawa anasema kuwa "Haifai kunyoa nyusi na akawa anasisitiza kauli ileile ya kuwa "Wamelaaniwa wenyekufanya hivo" mimi nikamwambia mbona wewe uliniambia yakuwa inafaa jinsi kadhaaaaa . akasema mimi sikusema hivo wala sikimbuki lakini hadithi iko wazi kabsaaaaaaaaa.



Kwanza naomba nifafanuliwe zaidi juu ya Hadithi hiyo kama inafaa au laa. Pili nifanye nini kwani na mimi niliwafahamisha wenzangu kuwa inafaa.



Swali La Nne:



Mwanamke kutengeneza nyusi kwa ajili ya harusi ni dhambi??





JIBU:


AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Maswali matatu hayo tutajaribu kuyajibu hapa yote kwa umoja.



Kunyoa nyusi au kuzichonga ni haramu, sawa ikiwa ni kwa kujipodoa kwa ajili ya mume, au kwa kujipamba mwanamke binafsi.



Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa Anasema:

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ۚ

Na lolote analokupeni Rasuli ((صلى الله عليه وآله وسلم basi lichukueni, na analokukatazeni, basi acheni. [Al-Hashr: 7]



Na katika jumla ya mambo aliyotukataza Nabiy (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni kunyoa nyusi.



عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه قال ((لعن الله الواشمات والمستوشمات والنامصات والمتنمصات والمتفلجات للحسن المغيرات خلق الله ((البخاري و مسلم))

Kutoka kwa 'Abdullahi bin Mas'uud (Radhwiya Allahu 'anhu) kwamba: ((Allaah Amewalaani watu wenye kuwachanja wenzao (tattoo) na wenye kuchanjwa, na wenye kuwanyoa wenzao nyusi na wenye kunyolewa na wenye kuchonga meno yao (kama kufanya mwanya) kwa ajili ya kujipamba kubadilisha maumbile ya Allah) [Al-Bukhaariy Hadiyth Namba 5948 na Muslim Namba 2125]



Ama nini cha kufanya, baada ya kuwa mlikuwa ni katika wafanyao hivyo? Jukumu lenu ni kurejea kwa Allah kwa kufanya toba ya kweli, sambamba na kuwalingania dada zenu wengine waachane na mwenendo huo, kwa lugha nzuri na mawaidha mema.



Jambo hili la kumuasi Allah na Nabiy Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakika halikutiliwa mkazo na dada zetu kabisa. Na mara nyingi linapokemewa kwa dada zetu wao hawalioni kama ni jambo la maana kukatazwa, wengine hulazimishwa japokuwa wao hawataki na waume zao kama ilivyo hali ya muulizaji wa kwanza. Ama wengine husema "Lakini si najipamba kwa ajili ya mume wangu" au "Mume wangu anapenda nitoe nyusi" au "Itakuwaje nyusi zinijae nisizitoe?" na mengi husemwa ambayo yanadhihirisha kutotilia mkazo jambo hili ovu la kuasi amri. Amesema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



((لا طاعة لمخلوق في معصية الخالق)) رواه أحمد وهو صحيح

"Hakuna kumtii kiumbe katika kumuasi Muumba". [Ahmad ikiwa sahiyh]



Vile vile:



قال صلى الله عليه وسلم: ((على المرء المسلم السمع والطاعة فيما أحب وكره إلا أن يؤمر بمعصية، فإن أمر بمعصية فلا سمع ولا طاعة)) رواه مسلم

Kasema Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa Sallam) ((Muislamu inampasa asikie na atii katika anayoyapenda na anayoyachukia isipokuwa anapoamrishwa katika maasiya. Anapoamrishwa kufanya maasiya basi asisikie wa kutii)) [Muslim]



وقال🙁( لا طاعة في معصية الله إنما الطاعة في المعروف)) رواه مسلم

Na kasema (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa Sallam): ((Hakuna kutii katika kumuasi Allaah, ama kutii ni katika mema)) [Muslim]



Tuchukue mfano mwema aliotuonyesha pia Abu Bakr wakati wa ukhalifa wake:



وقال أبو بكر رضي الله عنه حين بويع بالخلافة:"أطيعوني ما أطعت الله فيكم، فإن عصيته فلا طاعة لي عليكم"

"Nitiini nitakapomtii Allah kwenu, na nitakapomuasi basi msinitii"



Muislamu inampasa atambue kuwa kumtii kiumbe katika maasiya ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) haitomsaidia kitu akhera kwani huko yatakuja ni majuto tu na adhabu na pia hata kiumbe unachomtii inampasa na yeye amche Allah na akhofu adhabu siku ya Qiyaamah kwani ajue kuwa kumuamrisha mwenziwe katika maasi au kutomkataza basi yeye atamuombea apewe adhabu mara mbili na juu ya hivyo atamuombea laana kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):



يَوْمَ تُقَلَّبُ وُجُوهُهُمْ فِي النَّارِ يَقُولُونَ يَا لَيْتَنَا أَطَعْنَا اللَّـهَ وَأَطَعْنَا الرَّسُولَا ﴿٦٦﴾ وَقَالُوا رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءَنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَا ﴿٦٧﴾رَبَّنَا آتِهِمْ ضِعْفَيْنِ مِنَ الْعَذَابِ وَالْعَنْهُمْ لَعْنًا كَبِيرًا ﴿٦٨﴾

Siku zitakapopinduliwa nyuso zao motoni, watasema: Laiti tungelimtii Allaah, na tungelimtii Rasuli. Na watasema: Rabb wetu! Hakika sisi tumewatii mabwana zetu, na wakuu wetu, basi wametupoteza njia. Rabb wetu! Wape adhabu maradufu, na walaani laana kubwa. [Al-Ahzaab: 66-68]



Hivyo hakuna mmoja atakayemfaa mwenzake katika kuamrishana au kuridhishana katika maasi.



Pia ndugu zetu wa kike wajihadhari sana na baadhi ya wanaojiita Mashekhe wanapoulizwa kama ilivyo katika hali ya muulizaji wa tatu, akamjibu kwanza inafaa, kisha mara ya pili akakanusha. Bila shaka huyo hakuwa na elimu ya kutosha kuweza kutambua katazo lililokuja katika Hadiythi hiyo ya kulaaniwa mwanamke mwenye kunyoa nyusi.



Anapotaka Muislamu kuuuliza Swali la dini hasa linalohusu mambo ya haram na halali na yenye hatari kama hii, ni bora kumtafuta Shaykh mwenye elimu hasa ya dini ili asije kupata Fatwa itakayompotoza badala ya kumuongoza, na kisha bila ya kujua naye Muislamu akawapa wenzake Fatwa hiyo kama alivyofanya bila ya kujua muulizaji wa Swala la tatu.



Inampasa muulizaji wa Swali la tatu naye arudie kuwakanya aliowapa Fatwa hiyo isiyo sahihi na awafahamishe vilivyo, naye arudi kwa Mola wake na kuomba Maghfirah.



Tuwe na tahadhari na baadhi ya mashekhe kwani kuna wanaohalalisha hilo kwa sababu itikadi yao potofu inaruhusu mwanamke kunyofoa nyusi kwa ajili ya mumewe! Wajiulize hao wanaoambiwa hivyo na hao wenye itikadi hizo, ikiwa atanyofoa au kunyoa nyusi kwa mumewe, je, pindi akitoka nje atazuiaje wale wasio maharimu zake kuwaona bila nyusi zao na hali wenye itikadi hizo hawavai Niqaab? Hata ikiwa wataamua kuvaa Niqaab, maadam ni jambo limeshaharamishwa, hivyo haliwezi kuhalalika kwa vijisababu kama hivyo vya kumrembea mume au kuvaa Niqaab ukitoka n.k.



Kwa manufaa zaidi tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo:



Kuzinyoa Nyusi Za Katikati Zilizozidi Sana Na Kuungana



Mwanamke Anayetoa Nyusi Ambaye Keshalaaniwa, Ibada Yake Inakubaliwa?



Makatazo Ya Kishari’ah Kwa Wanawake - 2



Kutoa Nywele Za Uso Na Za Mwilini





Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Wanawake


Khitaan (Twahara) Kwa Mwanamke



Alhidaaya.com



SWALI



Assalaam Alaykum,



Naomba unifahamishe kama kumfanyia tohara mwanamke ni sahihi au la. Kama ni sahihi je kuna ushahidi wa aayah au hadiyth?



Wabillah Tawfiq





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





'Khitaan' (Twahaarah au Tohara) kwa mwanamke ni jambo lisilokatazwa kwenye Uislam, na ni jambo mtu ana khiyari ya kulifanya au kutolifanya lakini si jambo linalokatazwa kama wengi wanavyodhani! Tofauti ya kutahiri huku kunavyofanywa Kiislam na jinsi wanavyofanya baadhi ya makabila na watu wengine, ni tofauti kubwa. Tutazame dalili zifuatazo na maelezo mbalimbali ili tuweze kujua ruhsa ya kufanyika kwake na njia sahihi za kuifanya;



Abu Hurayrah amesimulia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Vitu vitano ni katika fitrah, kutahiri, kunyoa nywele za chini, kupunguza masharubu, kukata kucha na kunyofoa nywele za kwapa" [Imepokewa na Al-Bukhaariy, mj. 7, kitabu 72, namba 779]..



Baada ya kuona Hadiyth hiyo inayozungumzia 'Twahaarah' kwa ujumla, tuangalie Twahaarah kwa mwanamke katika sheria ya Kiislam:



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema, “Itakapogusa [kitakapokutana] kilichotahiriwa kimoja kugusa kilichotahiriwa kingine, basi yapasa kuoga.” [Al-Bukhaariy].



Na amesema tena Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), "Vitakapokutana viwili vilivyotahiriwa, basi ni wajibu kuoga." [Ibn Maajah 611].



Na vilivyotahiriwa viwili hapo makusudio ni sehemu ya ngozi inayokatwa katika utupu wa mwanamme na ile ya utupu wa mwanamke. Na ni ushahidi kuwa wanawake walikuwa wakitahiriwa. [Rejea Swahiyh Fiqhus Sunnah mj.1, uk.99].



Hadiyth hizo mbili ni sahihi kwa itifaki ya wanachuoni. Na vilevile kuna Hadiyth nyinginezo zenye kuweka wazi zaidi Twahaarah kwa mwanamke kama Hadiyth ya Ummu 'Atwiyah isemayo kwamba yeye alikuwa akitahiri na Nabiy kusikia akasema, "Ukipunguza usimalize kwani ni pendezo kwa uso na tulizo kwa mume."

Na nyingine iliyopokewa na Imam Ahmad kwenye Musnad yake yenye maneno kama hayo, ingawa wametofautiana wanachuoni kuhusu usahihi na udhaifu wa Hadiyth hizo.



Baada ya kuona Hadiyth zenye kuthibitisha kuwepo na kuthibiti jambo hilo kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ni vizuri pia tutazame nao Wanachuoni wamefahamu vipi kuhusu suala hilo:



Baadhi ya wanachuoni wameona ni wajibu kwa mwanamme na mwanamke pia, na wengine wameona ni 'Mustahab' (lenye kupendeza) kwani hiyo 'Khitaan' kwa mwanamke ni 'Makrumah' (pendezo). Na wanasema kuwa sio wajibu. Na dalili yao ni kuwa 'Khitaan' kwa mwanamme ni jambo la lazima kwa sababu kuna maslaha yanayopatikana katika kutekelezeka masharti ya Swalah ndani yake, nayo ni Twahaarah; kwa maana kama hajatahiriwa, basi mkojo na uchafu ni rahisi kubaki katika ile sehemu ya ngozi ambayo haijakatwa

.

Na kwa upande wa wanawake ni kupunguza matamanio yake ya kijinsia, na ndio faida inayopatikana kwake, na kwa hivyo, kwa kuwa si jambo la kuondosha madhara, inakuwa si wajibu bali ni mapendekezo.

'Khitaan ni wajibu kwa mwanamme na ni Sunnah kwa mwanamke' [Kitabu 'Mukhtasar al-Fiqhil Islaamiy, uk.381]. 'Khitaan kwa mwanamke inazunguka katika hukmu ya wajibu na istihbaab'[Kitabu 'Swahiyh Fiqhus Sunnah' Mj.1, uk.100].



Naye mwanachuoni maarufu wa Fiqh, Dr. Wahbah Az-Zuhayliy katika kitabu chake cha Al-Fiqhul Islaamiy wa Adillatuh, anasema katika Juzuu ya 1, ukurasa wa 460, ''Khitaan ni kukata kigozi kilichozidi hadi kichwa kitokeze kwa mwanamme na kwa mwanamke ni kukata kipande kidogo cha juu kwenye kisimi 'clitoris' .

Ama Imamu wanne maarufu wao wana miono ifuatayo:



Imam Abu Haniyfah na Imaam Maalik wanasema ni Sunnah kwa wanaume na ni pendezo kwa wanawake.



Imaam ash-Shaafi'iy na Imaam Hanbal wao wanasema ni wajibu kwa wanaume na ni wajib vilevile kwa wanawake.



Pia katika kauli nyingine ya Imaam Hanbal ni 'Makrumah' kwa Hadiyth ya Nabiy aliposema, "...kata kipande kidogo na wala usimalize", na Hadiyth "Khitaan ni Sunnah kwa wanaume na Pendezo kwa wanawake." [Hadiyth hizi tumeeleza juu hukmu zake].



Kuna baadhi ya watu wakiwemo Waislam, na jumuiya za haki za binaadam, haki za wanawake, Umoja wa Mataifa na Nchi za Magharibi wanaopinga kitendo hiki na kukilaani pamoja na kutafuta njia za kila namna za kuzuia na kuharamisha moja kwa moja kwa kigezo kuwa ni 'UKATILI' na kuwa unakiuka haki za wanawake.

Lakini wao ima wanachanganya tohara ya Kiislam na tohara ya kimila na kikabila inayofanywa na wengineo, au wanafanya makusudi kutaka kuzipinga na kuzikosoa sheria zinazohusiana na Uislam kama wafanyavyo katika suala la Mirathi na Adhabu za kukatwa mkono kwa mwizi na zinginezo.



Ni jambo ambalo si SAHIHI kulinganisha au kupinga tohara hii ya Kiislam kwa kuwa kuna wanaofanya tohara vibaya na kimakosa.



Kwani wao kigezo chao kikubwa ni baadhi ya nchi zifanyazo 'TOHARA' kimila na si Kiislam, tunasema kimila na si Kiislam, kwa sababu, nchi nyingi haswa za Afrika kaskazini na mashariki, kama vile Somalia, Chad, Sudan, Misr, Tanzania n.k, hizi wao wanachofanya ni KUFYEKA kabisa na sio kupunguza, nako kunaitwa 'UKEKETAJI'!!! Na matokeo yake kumepatikana madhara mengi kama wanawake kupata saratani, kupata taabu wakati wa uzazi, kukosa raha ya tendo la ndoa na hata wengine kufariki kutokana na kupoteza damu nyingi wakati wa kutahiri.



Wao wanaondosha kisimi 'clitoris' (clitorectomy) chote pamoja na sehemu ya 'labia minora', ambacho kinashonwa chote na kubakiza uwazi. Au kuondosha kisimi 'clitoris' chote, 'labia minora' na sehemu ya kati ya 'labia majora', pamoja na sehemu yote ya kiungo cha mwanamke kushonwa na kubakizwa tundu dogo tu. Na utaratibu huu unahitaji kumfunga miguu mtoto kwa kiasi cha wiki tatu. Na hii ndio wengine wakaita kuwa ni tendo au ada ya Ki-Firauni.



Na hivyo wafanyavyo, ni kinyume kabisa na ilivyo Kiislam, na wala Uislam haukubaliana na njia hizo zifanywazo na wafanyao hata kama ni WAISLAM!! Kwani si taratibu zilizofundishwa na Mtukufu Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)



Hivyo, kama tulivyoona, ni jambo lenye kupendezwa na si jambo la lazima. Mwenye kutaka kufanya ni bora, na asiyetaka ni khiyari yake, lakini asilaumu wala kuponda kwani ni jambo ambalo lililopo na limethibiti katika Dini.





Na Allaah Anajua Zaidi
 
Assalaam alaikum warahamatullah wabarakatuh

NASAHA ZA IJUMAA

Leo ni ijumaa alhamdulillah,moja ya siku bora kabisa kwa waislamu,ni sikukuu

Kikubwa baada ya kuadhiniwa adhana ya Swala ya Ijumaa basi tuwahi katika majumba ya Allah,ambayo kwa mujibu wa hadith,hakika Misikiti inang'aa kama nyota angani kwa wakazi wa mbinguni kama ambavyo vyota zina ng'aa kwa wakazi duniani

Na tufanye dhikri sana (kuleta adhkar mbali mbali) pamoja na kumswalia sana kipenzi chetu Nabii Muhammad swallallahu alaih wasallam

Naihusia nafsi yangu na yako juu ya kumcha Allah azza wa jallah

Nasaha zangu leo ni juu ya watu aina nne walio laaniwa kuhusiana na kushiriki katika shughuli za pombe

Katika mfumo wa hadith, Nabii amesema watu aina nne wamelaaniwa:

Mosi, mwenye kupika ulevi,huyu ni mtayarishaji au mzalishaji, kwahiyo hawa wamelaaniwa,kwahiyo ukiwa unafanya kazi katika viwanda vya ulevi,iwe bia,spirit kwa maana pombe kali na mfano wake,basi upo na sifa ya mpika pombe

Maadam tu upo kwenye sehemu ya kufanikisha shughuli hizo basi wewe upo katika laana,na ukiwa katika laana maana yake hupati rehma ya Allah,je utakuwa katika mazingira gani?


Pili, msafirishaji wa pombe nae anapata laana ya Allah,madereva wa makampuni ya pombe,hapa nyie mnahusika,hiyo kazi yako ni moto unaotembea,kama una mcha Allah fanya haraka kuikimbia kazi hiyo

Tatu,muuzaji wa pombe hiyo,hapa sales man/woman mna laana yenu,hiyo siyo kazi bali mnajikaribisha motoni

Nne,mtumiaji mwenyewe wa pombe,huyu ndio mteja mwenyewe,hakika pombe ni mama wa huasi,maana pombe ndio chanzo cha maasi yote,hapa utazini,utatukana,utawakosea watu heshima na list inaendelea

Tumche Allah kwa kukaa mbali na kazi hizi,kama upo huko fanya mpango uache kazi na utubie kwa Mola wako naye ni msamehevu sana kwa waja wake

Nawakumbusha tena juu ya kumcha Allah subhaanahu wa taala,kwani hakika ametuambia :

"Tusife bali hali ya kuwa tumekuwa Waislamu kamili kwa maana tuwe tumejisalimisha katika amri zake na kuacha makatazo yake"

Ijumaa Mubarak!
 
Baadhi ya post zangu za zamani...

FAIDA YA KUCHUNGA ULIMI

Alhamdulillah Ijumaa ishaingia na si vibaya kukumbushana mawili matatu.

Hakika Ulimi ni kiungo kidogo lakini hakika madhara yake ni makubwa mno katika Maisha yetu hapa duniani na kesho Akhera.

Watu wengi huenda hatutambui kuwa hakika halitoki Neno lolote kinywani kwetu isipokuwa linaandikwa na Waandishi watukufu ambao ni Malaika,hata huku kuandika kwetu kuna ratibiwa pia.

Mwanadamu hujiona yupo huru kuongea chochote atakacho lakini hajui hakika Mwenyezi Mungu ana waandishi Maalum ambao wapo tayar 24/7 kuweka kumbukumbu zetu katika madaftari maalum ambayo yataletwa siku ya Mwisho kama ushahidi WA Yale tulivyo Kwisha kuyatanguliza.

Allah (Subhanahu wataala) anasema:
(Hatoi kauli yoyote isipokuwa karibu naye yupo mpokeaji tayari (kuandika)).
[Hujurat : 6 ]

Katika hadith Mtume (rehma na Amani iwe juu yake) amesema "Yule atakayenipa dhamana ya kile kilichopo baina ya midomo yake miwili,na kile kilicho baina ya miguu yake miwili. Nitampa dhamana ya Jannah."
(Bukhari).

Kwa maana Yule atakaye chunga Ulimi wake na kulinda tupu yake asifanye zinaa basi ataombewa aingie peponi

Harith bin Hishim (r.a) amesimulia "Nilimuomba Mtume (s.a.w) "Nipe habar juu ya Jambo ninalo weza kulishika vizuri". Mtume akamwambia "akiashiria katika Ulimi wake na kusema: "Udhibiti huu" akimaanisha ULIMI.

Uqbah bin Amr (r.a) amesimulia kuwa nilisema "Ewe Rasullallahi! Ni ipi njia ya uokovu?" Akasema " Uchunge Ulimi wako,Baki ndani ya nyumba yako na Lia Kwa madhambi yako" (Tirmidhi).

Maelezo: Kuuchunga Ulimi wake ina maana usitumiwe Kwa maovu mfano kusengenya,kuzua,mazungumzo ya utovu wa adabu, mazungumzo yasiyo ya lazima, mazungumzo ya ovyo ovyo, kuzozana, kutukana, kuwalaani watu na wanyama, kushughulika na mashairi Kwa wingi, kufanya mzaha, kufichua Siri, kutoa ahadi za uongo, viapo vya uongo, udanganyifu, kusifu mno Bila kiasi na kuuliza maswali yasiyo hitajika.

Kwahiyo hakika Ulimi ni wa Kuuchunga Sana, mifarakano mingi katika familia zetu na jamii yetu chanzo chake ni Ulimi, mtu atatoa huku neno na kuipeleka Kule na mwisho wa siku fitina inaanzia hapo.

Ndio maana watu wenye hekima zao wanasema "Kunyamaza wakati mwingine ni Bora zaidi kuliko Kuongea". Na mara nyingi mtu atakujaji kutokana na mazungumzo yako, kutokana na kauli zako utafahamika Tabia zako na mitazamo yako pia.

Kama hakuna sababu ya kuzungumza basi kaa kimya kwani ni kheri kwako kuliko kuzungumza mazungumzo yasiyo faa na yenye kuchukiza na matokeo yake unapata dhambi.

Na vile vile tunashauriwa Sana tuepuke Sana mazungumzo ya kipuuzi, Mwenyezi Mungu anasema waumini WA kweli ni wale ambao hata wanapo kuta mazungumzo ya kipuuzi wao hupita mbali na kuyaepuka.

Mtume Muhammad (rehma na Amani ziwe juu yake) aliulizwa ni mambo gani yatawaingiza watu Sana Motoni? Akajibu ni kile kilicho katikati ya midomo miwili na kilicho katikati ya miguu miwili, navyo ni Ulimi na Uchi ( Kwa maana ya zinaa).

Waswahili Wana msemo wao wanasema "Mdomo uliponza kichwa" kuashiria kwamba hakika mdomo ndio chanzo cha matatizo na mabalaa
 
Naam kwenye mukhtasari wa aqiydah tuliishia swali nambari 20...

Leo tunaendelea inshaallah

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com







21-Je, Inajuzukuomba Isti’aanah kwa asiyekuwa Allaah?





Hapana! Haijuzu kuomba Isti’aanah kwa mwengine asiye Allaah.

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ ﴿٥﴾

Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada. [Al-Faatihah: 5]



((إِذَا سَأَلْتَ فاسْألِ الله وَإِذَا اسْتَعَنْتَ فاسْتَعِنْ بالله)) رواه الترمذي

((Unapoomba muombe Allaah na unapotaka Isti’aanah (msaada) taka isti’aanah kwa Allaah)) [At-Tirmidhiy]
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com







22-Je, Inajuzu kuomba msaada kwa walio hai?



Naam, inajuzu kuomba msaada kwa walio hai katika mambo ambayo wana uwezo nayo.



وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ ۚ

Shirikianeni katika wema na taqwa, na wala msishirikiane katika dhambi na uadui [Al-Maaidah: 2]

((واللهُ فِي عَوْنِ الْعَبْد مَا دام الْعَبْدُ فِي عَوْنِ أخِيه)) رواه مسلم

((Allaah Yuko katika kumsaidia mja Wake maadam mja huyo yuko katika kumsaidia nduguye)) [Muslim]
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com









23 Je, Inajuzu kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah?



Hapana! Haijuzu kuweka nadhiri isipokuwa kwa sababu ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).



رَبِّ إِنِّي نَذَرْتُ لَكَ مَا فِي بَطْنِي مُحَرَّرًا فَتَقَبَّلْ مِنِّي ۖ

“Rabb wangu, hakika mimi nimeweka nadhiri Kwako kilichomo katika tumbo langu kuwa ni wakfu kukutumikia, basi nitakabalie. [Aal-‘Imraan: 35]



((مَنْ نَذَرَ أَنْ يُطِيعَ اللَّهَ فَلْيُطِعْهُ ، وَمَنْ نَذَرَ أَنْ يَعْصِيَهُ فَلَا يَعْصِهِ))رواه البخاري

((Anayeweka nadhiri kumtii Allaah basi amtii, na aliyeweka nadhiri kumuasi Allaah basi asimuasi))
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com







24-Je, Inajuzu kuchinja bila kumkusudia Allaah?



Hapana! Haijuzu kuchinja kwa malengo yasiyo ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa sababu ni shirki kubwa.



فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ ﴿٢﴾

Basi swali kwa ajili ya Rabb wako na chinja kwa ajili Yake. [Al-Kawthar: 2]



((لَعَنَ الله مَنْ ذبح لِغير الله)) رواه مسلم

((Allaah Humlaani anayechinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah)) [Muslim]
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com







25-Je, Inajuzu kutufu makaburi?



Hapana! Haijuzukutufu (kuzunguka) makaburi, bali kutufu ni kwa ajili ya Ka'abah pekee.



وَلْيَطَّوَّفُوا بِالْبَيْتِ الْعَتِيقِ ﴿٢٩﴾

Na watufu kwenye Nyumba ya Kale. (Al-Ka’bah) [Al-Hajj: 29]



((مَنْ طافَ بِالْبَيْتِ سَبْعاً وَصَلّى رَكَعَتينِ كَانَ كَعتق رَقَبة)) رواه ابن ماجه و صححه الألباني

((Atakayezunguka Ka'bah mara saba kisha akaswali rakaa mbili ni kama mfano kamwacha huru mtumwa mmoja)) [Ibn Maajah na ameisahihisha Al-Albaniy katika Swahiyh Al-Jaami’ (6379)]
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com







26-Je, Inajuzu kuswali na kaburi liko mbele yako?



Hapana! Haijuzu kuswali kulielekea kaburi.



فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِۚ

Basi elekeza uso wako upande wa Al-Masjidil-Haraam [Al-Baqarah: 144]



Yaani: Qiblah

((لا تَجْلِسُوا عَلَى الْقُبُورِ وَلا تُصَلُّوا إِلَيْهَا)) رواه مسلم

((Msikalie makaburi wala msiswali kuyaelekea)) [Muslim]
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com







27-Nini hukumu ya mwenye kufanya sihri (uchawi)?



Mwenye kufanya sihri ni kukufuru.



وَلَـٰكِنَّ الشَّيَاطِينَ كَفَرُوا يُعَلِّمُونَ النَّاسَ السِّحْرَ

lakini mashaytwaan ndio waliokufuru; wanafundisha watu sihiri [Al-Baqaarah: 102]



((اجْتَنِبُوا السَّبْعَ الْمُوبِقَاتِ:الشِّرْكُ بِاللَّهِ وَالسِّحْرُ)) متّفق عليه

((Jiepusheni na mambo saba yanayoangamiza; kumshirikisha Allaah, sihri (uchawi)) [Al-Bukhaariy, Muslim]
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com







28-Je, Inajuzu kumwendea kahini na mpiga ramli?



Hapana! Haijuzu kumwendea kahini wala mpiga ramli.



هَلْ أُنَبِّئُكُمْ عَلَىٰ مَن تَنَزَّلُ الشَّيَاطِينُ ﴿٢٢١﴾

Je, nikujulisheni wanaowateremkia mashaytwaan?

تَنَزَّلُ عَلَىٰ كُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٍ ﴿٢٢٢﴾

Wanateremka juu ya kila mzushi mkubwa mwingi wa kutenda dhambi. [Ash-Shu’araa: 221-222]



((مَنْ أَتَى عَرَّافًا فَسَأَلَهُ عَنْ شَيْءٍ لَمْ تُقْبَلْ لَهُ صَلَاةٌ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً)) مسلم

((Atakayekwenda kwa mtabiri akamuuliza kitu haitokubaliwa Swalaah yake siku arubaini))
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com







29-Je, Inajuzu kuwaamini wanaopiga ramli na makahini?



Hapana! Haijuzu kuwaamini wala kuamini wayasemayo ya ghayb. (yaliyofichika ambayo hakuna mwenye ujuzi nao isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).





قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّـهُ ۚ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ ﴿٦٥﴾

Sema: “Hakuna aliyoko katika mbingu na ardhi ajuaye ghayb isipokuwa Allaah. Na wala hawatambui lini watafufuliwa.” [An-Naml: 65]



((مَنْ أَتَى كَاهِنًا، أَوْ عَرَّافًا، فَصَدَّقَهُ بِمَا يَقُولُ، فَقَدْ كَفَرَ بِمَا أُنْزِلَ عَلَى مُحَمَّدٍ صلى الله عليه وسلم)) صحيح رواه أحمد

((Atakayemwendea kahini au mpigaji ramli akamuamini asemayo, basi atakuwa ameshakufuru yale aliyoteremshiwa nayo Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)). [Ahmad, na Aswhaabus-Sunan wanne, na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Targhiyb wat-Tarhiyb (3047)]
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com





30-Je, Mtu anaweza kuyajua mambo ya ghayb?



Hakuna awezaye kuyajua ya ghayb isipokuwa Mwenyewe Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).



وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ ۚ

Na Kwake (Allaah) zipo funguo za ghayb; hakuna azijuaye ila Yeye tu. [Al-An’aam: 59]



((لاَ يَعْلَمُ الْغَيْبَ إِلاَّ الله)) حسن رواه الطّبراني

((Hakuna ajuaye mambo ya ghayb isipokuwa Allaah. [Hadiyth Hasan ameipokea Atw-Twabaraaniy]
 
Naam tunakumbushana kila jioni/usiku tunakuwa na kipengele cha Maswali na Majibu

Faida kubwa inapatikana......
 
Baadhi ya post zangu za zamani

WANA WA ADAMU TUNAKWAMA WAPI?


Imeandikwa katika Maandiko kwamba tuepukane na zinaa.

Na imesemwa pia hata kile kitendo cha kuleta mazingira Tu ya kuzini nacho ni Sawa Sawa kama umezini!

Ebu tuangalie Maandiko yanasemaje:


Mathayo 5:27-30
[27]Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;
Ye have heard that it was said by them of old time, Thou shalt not commit adultery:
[28]lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
But I say unto you, That whosoever looketh on a woman to lust after her hath committed adultery with her already in his heart.
[29]Jicho lako la kuume likikukosesha, ling’oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
And if thy right eye offend thee, pluck it out, and cast it from thee: for it is profitable for thee that one of thy members should perish, and not that thy whole body should be cast into hell.
[30]Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
And if thy right hand offend thee, cut it off, and cast it from thee: for it is profitable for thee that one of thy members should perish, and not that thy whole body should be cast into hell.

Tunaona hapo Kristo amekemea Kwa makatazo makali kabisa


Na Qur'an nayo imesema hivi:

Wala msikaribie zinaa. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya.

Suratul israa :32

quran hapo imeongelea Kwa uchache lakini ikibeba maana kubwa mno.

Usikaribie sio kufanya Bali usikaribie Kwa maana usilete hata Yale mazingira ambayo yatapelekea Hilo tendo kufanyika,hapo kuna mambo mengi Sana ndani yake.

Je Wana wa Adamu ndio tumekuwa viburi kiasi kwamba hatumuogopi Mwenyezi Mungu ?
 
Baadhi ya post zangu za zamani....

HEKIMA TATU BORA


Kuna mwanafunzi mmoja alienda Kwa watu WA elimu na kujifunza mambo matatu makubwa.

1) Usimfanyie Ubaya mtu aliyekufanyia wema
2) Ukipita sehemu ukaiona kheri usiiache
3) Usihukumu kitu ambacho hauna uhakika nacho

Alipewa Ngamia watatu na wazazi wake kama gharama ya kusomea hayo mambo matatu, baada ya masomo hakuwa na nauli ya kurudi kwao,hivyo ikabidi atafute mtu ambaye amtasaidia nauli.

Akamkuta bwana mmoja ambaye akamwambia Mimi nitakupa nauli lkn Kwa sharti kwamba utakaa kwangu Kwa Mda fulani ukinisaidia kazi halafu nitakupa nauli,bwana mdogo hakuwa na namna zaidi ya kukubali sharti hilo.

Basi kwakuwa kijana ana elimu,mke WA boss akamwambia naomba utufindishie watoto wetu pia,basi kijana hakuwa na hiana akafanya hivyo. Mwisho wa siku mke wa boss akamtamani Yule kijana,mfano wa Yale yaliyo mtoea Nabii Yusuph Kwa Zuleikha Kule misri.

Kijana akakumbuka kuwa somo la Kwanza kusoma lilikuwa ni "Usimfanyie Ubaya mtu aliyekufanyia wema" Akaona hapana boss wangu amekuwa mwema kwangu na kutaka kunisaidia iweje nitembee na mkewe? Akakataa lo salale! Hakika vitimbi vya wanawake ni vikubwa. Mke akamwambia mumewe huyu kijana ni mjeuri Hana adabu na bla bla nyingine kibao,na akatoa ushauri Kwa mumewe kuwa anafaa akatwe kichwa/auwawe,daah mume kaingia king Kwa ushauri WA mkewe.

Basi wakapanga kesho apeleke chakula shambani kwao,Kule kuna watumwa wanafanya kazi,akifika huko atakatwa kichwa na watumwa,na kumbuka watumwa wameambiwa mtu atakaye leta chakula ndo huyo huyo. Basi bwana hakika Mwenyezi Mungu ni bingwa wa kupindua hila za watu.

Jamaa kachukua chakula anaenda zake shambani,basi njiani akakuta watu Wana mtaja Allah Kwa kufanya dhikri mbali mbali na wengine wanasoma Qur'an,akakumbuka somo la pili "Ukipita sehemu ukaiona kheri usiiache" basi Akaona hapa watu wanamkumbuka Mwenyezi Mungu na wanasoma Kitabu chake hakika hii ni kheri na siwezi kuiacha. Basi akakaa kitako na kushiriki Jambo lile.

Huku Kwa watumwa chakula hakijaenda,ndo ikabidi atoke mtoto wa Yule Mzee akacheki imekuwaje tena mbona jamaa alitoka Mda mrefu,akiwa njiani ndo akamkuta jamaa kwenye kikao cha kheri,akamsema pale na kuchukua kile chakula Kwa ahadi kuwa ataenda kumwambia Mzee wake kilicho tokea. Basi bwana kafika Kule,na watumwa waliambiwa atakaye leta chakula ndio halali yenu.

Watumwa wakamuua Yule kijana pasina kujua ni kijana wa boss wao,boss baadae anapewa taarifa kwamba huku kazi tayar, laa haula boss anafika anakuta kumbe mwanae,daah tui limezidi maji ikabidi pale vilio vitawale,mpaka watu WA mashamba ya jirani kuja pale ndio ikajulikana hiyo Siri.

Baada Yule kijana kamaliza kikao cha watu wema akasema ngoja niende shambani sasa,anakuta makelele mengi,kuuliza akaambiwa mtoto w boss kauwawa Kwa bahati mbaya,aliyekusudiwa hakuleta yeye chakula,jamaa akajua dah kumbe ilikuwa Mimi,Akaona isiwe tabu inabidi aondoke sehemu Ile chap maana sio salama kwake.

Akafika nyumbani kwake akamkuta mkewe nje anaosha vyombo ,basi baada ya salamu akaingia ndani fasta,akamkuta mwanaume kitandani kwake amelala akataka kufanya uamuzi WA kuchukua mkuki na kumchoma,akakumbuka somo la Tatu " Usihukumu kitu ambacho hauna uhakika nacho".

Anatoka nje na kumuuliza mkewe yule ni Nani,ndo akaambiwa huyo ni Baba yako amekuja hapa anaumwa Sana,hivyo amejipumzisha kidogo. Je kama angekurupuka kama wale watu ambao wanacomment Bila kusoma Uzi wote unafikiri ingekuwaje?.
 
Anaona Kinyaa Kupokea Mkono Anaposalimiwa Kwa Sababu Ya Uchafu
Maswali: Twahara Najsi
SWALI:




suala langu la pili kuhusu utulivu ndani ya swala tunakuta wenzetu wengine wanakuja hali ya kuwa wanajikuna kila wakati na katika kujikuna kwao unafikia unakuwa unaona kinyaa kwani kuna baadhi ya watu ni kawaida yao wanafikia mpaka wanajichokoa pua na kutoa uchafu ndani ya swala halafu baada ya swala anakupa mkono kwa kukusalimia sasa suala langu linakuja mimi ninatakiwa nimsalimie kwa kurejesha mkono au nini nifanye na kama ninaona kinyaa sitakuwa mkosa kwa ALLAH kuwa labda nina kiburi au kitu kama hicho ninaogopa adhabu za ALLAH ninawaombeni ndugu zangu munisaidie kwa hili na niweze kuchapisha kwa kuwaelimisha wenye mtindo kama huu ASSALLAM ALLAIKUA WARAHMATULLAH WA BARAKATU





JIBU:




Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.




Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuona kinyaa kusalimiana kwa mkono. Hakika hilo ni jambo la kimaumbile kabisa lakini, bora tueleze ili kila mmoja aweze kuelewa.




Uislamu umeweka nidhamu yake ambayo inatakiwa ifuatwe kikamilifu na kila anayejiita Muislamu. Katika hilo ni usafi, na Muislamu ni lazima awe msafi. Kwa ajili ya hiyo ndio Allaah Aliyetukuka Akamuagizia Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

"Na nguo zako uzisafishe" (74: 4).

Na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:

"Uislamu ni usafi, basi jisafisheni kwani haingii Peponi ila aliye safi".

Na tena:

"Hakika Allaah Aliyetukuka ni Mzuri na Hakubali ila zuri" (Muslim).




Uzuri umechanganya mambo mengi sana mojawapo ikiwa ni usafi na unadhifu.




Kutoa uchafu katika pua kisha bila ya kusafisha mikono ni hatari kwani sehemu hiyo ya pua inakusanya viini vingi vya ugonjwa na hivyo kumweka katika hatari yule unayemsalimia na yeye mwenyewe pia. Jambo la busara ni kumpatia nasaha huyo kaka kuhusu unadhifu na usafi ili asiwe ni mwenye kujiingiza katika matatizo.




Usiwe ni mwenye kukataa tu bali mnasihi na kumwelezea Uislamu unasema nini kuhusu hilo kwa njia nzuri na ya busara bila kumkemea wala kumkejeli. Kuhusu hilo, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

"Dini ni nasiha'. Tukauliza kwa nani, akajibu: 'Kwa Allaah, na Kitabu Chake, na Mtume Wake, na kwa viongozi wa Waislamu na watu wa kawaida'" (Muslim, Abu Daawuud na an-Nasaa'iy).




Kwa kufanya hivyo utakuwa umefanya ulinganizi na utalipwa na Allaah Aliyetukuka kwa hilo. Twakuombea kila la kheri.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Anataka kuunganisha Swalah Kwa Khofu Ya Kuweko Najasa Ya Mbwa
Maswali: Twahara Najsi
SWALI:



Assalam alaikum,



I have a question about prayers. I am living in Netherlands. Since it’s a Christian country praying inside our office is kind of hard, because there are dogs coming inside and they lick you. But I heard that I can pray my Dhuhr and Asr prayer in the morning. Is it allowed? I talked to one of my family member that he is also living here and he said I should ask by Alhidaaya. Thank you,











JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuunganisha Swalah kwa ajili ya hofu ya najasa.

Mwanzo inafaa tuelewe Muislamu hawezi kuswali kabla ya wakati wake kuingia, kwani kuingia wakati ni sharti katika kutimia Swalah. Kwa ajili hiyo lau mtu ataswali kabla ya kuingia wakati kama vile kusema kuswali asubuhi Swalah za adh-Dhuhr na al-‘Aswr ni jambo ambalo halikubaliki kishari’ah. Kuhusu umuhimu wa kuswali kwa wakati wake Allaah Aliyetukuka Amesema:

“Hakika Swalah kwa Waumini ni faradhi iliyowekewa nyakati maalumu” (an-Nisaa’ [4]: 103). Na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amehimiza sana Waislamu waswali Swalah tano kwa wakati wake makhsusi uliowekwa.



Kisha kuunganisha Swalah kuna masharti yake na njia zake, na kuwa na najisi si miongoni mwa sababu za watu kuunganisha Swalah. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuambia kuwa ardhi yote ni Msikiti na twahara. Sisi ndio tunajitia katika mashaka.

Ikiwa hapo ndipo pekee mnaweza kuswali mnaweza kutafuta karatasi za kuweka juu yake au mikeka au miswala na wakati wa Swalah ukifika mkaswali. Au mnaweza mkatafuta sehemu nyingine kwenye uwanja, nyasi nje, maadamu najisi haionekani unaweza kuswali tu sehemu hiyo. Ama kunuswa na mbwa mnatakiwa mtahadhari, kwani wanyama wenyewe wana maradhi kwa yale maji maji yao.



Njia nyingine ni nyinyi kuzungumza na idara ya sehemu mnayofanya kazi ili wawadhibiti hao mbwa wasiwe ni wenye kuingia. Ni ajabu kwa nchi hizo zinazosema zimeendelea kuacha mbwa kuzurura ovyo hata katika maofisi. Inatakiwa mfanye bidii kuhusu ‘Ibaadah muhimu kama Swalah kuiswali kwa wakati wake na bila shaka Allaah Aliyetukuka Atawasaidia.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Back
Top Bottom