Ramadhan Special Thread
Hizi ni Baadhi ya post Zangu Za Nyuma

HAWA NDIO WATAIRITHI PEPO YA FIRDAUS

Alhamdulillah ijumaa imeingia tayar na ningependa tukumbushane mawili matatu ili tujiweke tayari kukutana na hiyo siku ya Mwisho tukiwa tumeridhiwa na Mwenyezi Mungu.

Firdaus ndio pepo ya juu zaidi kuliko zote Kwa maana nyingine hii ndio pepo ambayo ni first class,na hii watairithi Mitume na Wacha Mungu.

Kwa taarifa yako Tu inasemekana zipo takribani daraja Mia Moja za pepo (100) na mkubwa wao ni huyo Firdaus.

Lakini cha kusikitisha zaidi pamoja na kuwepo hizo pepo zenye daraja takribani Mia Moja bado kuna watu hawatofanikiwa kuingia na matokeo yake wataingia motoni, Ewe Mwenyezi Mungu utujaalie tusiwe miongoni mwao Amiin.

Je watu wenye sifa gani ambao watairithi au kuingia katika hii pepo?

Kwa mujibu wa Qur'an watu wenye sifa hizi ndio ambao watairithi pepo hiyo;

WA Kwanza ni waumini ambao ni wanyenyekevu katika sala zao,hawa ni Wale ambao wanapokuwa ndani ya sala basi mawazo Yao na fikra zao zote zinakuwa ndani ya ibada ya swala,hawa hakika wamefanikiwa,

lakini kuna baadhi yetu wawapo ndani ya swala basi wanajikuta wanawaza hiki na kile na mambo kibao yanatawala swala yake,ingawa ni vigumu Kwa asilimia Mia moja kutotoka kimawazo,lakini hata ukitoka basi iwe kidogo na mara moja ujikumbushe kuwa upo ndani ya swala na ujue unawasiliana moja Kwa moja na Mola wako.

Sifa ya pili ni ambao wanajiepusha na mambo ya kipuuzi

Sifa ya tatu,na ambao wanatoa zaka,hapa inaingia na sadaka pia,maana zaka ni sehemu ya sadaka. Kwahiyo hakika kutoa sadaka ni Jambo muhimu Sana na ni ibada ambayo ina faida kubwa Sana,kuna maradhi mengine unapona Kwa kutoa sadaka Tu,


Na sadaka ndio ibada ambayo mja ataikumbuka mara Tu atakapoanza kutokwa na roho, ataomba Ewe Mwenyezi Mungu naomba walau unipe nafasi kidogo niweze kutoa sadaka. Sasa usisubir mpaka wakati huo ufike huenda usipate huo Mda wa kutoa sadaka.

Sifa ya nne, ni ambao wanazilinda tupu zao, hapa ndio wale wanachama WA jukwaa la MMU wajitafakari vizuri Sana,maana Yale mambo ya kulana kimasihara basi ujue nawe utaikosa pepo kimasihara,wazee wa Michepuko hapa kazi kwenu,hapa inakatazwa Zinaa Kwa nguvu zote,kwahiyo tujitathimini Sana.

Sifa ya tano,ni Kwa wale ambao wanazitimiza Amana zao na ahadi zao,kuna watu Jambo la kuahidi wanalichukulia kimchezo mchezo Tu,tena hawa wanasiasa hawa mjue Mungu anawaona! Maana nyie Kwa kutupiga sound hamjambo basi endeleeni Tu kutupiga sound halafu muone huko kwa Mungu kama mtafanikiwa.

Hapa Napo Jambo la Amana limeingia pia,mtu amekupa Amana yake umuhifadhie basi fanya hivyo usiingie tamaa ya kuitumia Bila ridhaa au idhini yake.

Na sifa ya sita ni Wale ambao wanazihifadhi swala zao,inamaana ambao wanadumisha swala zao siku zote,maana kuna watu huwa wanaswali ijumaa mpaka ijumaa Tu,au idi mpaka idi Tu,au akiwa na shida basi yeye ndio utamuona anaswali na mambo yake yakiwa fresh Tu basi ndio nitolee na kuswali bye bye.

Hope sauti yangu imetosha na kusikika vizuri kabisa.

Ijumaa Mubaraka!
 
Hizi ni Baadhi ya post Zangu Za Zamani

UBAYA WA KUWA NA DHANA MBAYA


Dhana Mbaya ni Ile hali ya kuwafikiria wenzako vibaya juu ya Tabia zao au Matendo Yao Fulani pasina kuwa na ushahidi wowote ule.

Hii ni dhambi miongoni mwa madhambi ambayo Kwa Mwenyezi Mungu ni makubwa mno, kibinadamu tunaweza kuchukulia ni jambo dogo lakini Kwa Mola wetu ni kubwa mno.

Kuliweka hili Sawa nitahadithia kisa kilichowahi tokea enzi za Mtume Muhammad (rehma na Amani ziwe juu yake) enzi hizo karibia miaka 1400 iliyopita.

Ilikuwa ni kipindi cha Vita ambapo nimesahau ilikuwa ni Vita gani dhidi ya makafiri, kulikuwa na upepo mkali Sana na hali ya hewa ilibadilika Sana, hivyo hivyo ikaamuliwa watu waondoke katika uwanja wa Vita.

Sasa bahati mbaya kipindi Hicho mama wa waumini bi Aisha (r.a) alikuwa ametoka nje ya gari la kuvutwa na farasi na kwenda washroom, huku nyuma wasaidizi wake walisahau kabisa kuwa Mama wa waumini alikuwa hajarejea bado katika hema na wala Mtume pamoja na Askari wengine hawakujua Hilo, basi wakaondoka na kurejea nyumbani huku wakimwacha bi Aisha nyuma pasina kufahamu.

Bi Aisha aliporejea akakuta msafara umeondoka, lakini bahati nzuri huku nyuma kulikuwa na Sahaba mmoja alibakia nyuma kuhakikisha hakuna kitu kilicho sahaulika ndo hamadi akamwona Mama wa waumini na kurejea nae.

Basi kama unavyojua wapuuzi huwa hawakosekani sehemu zote, basi wakazusha upuuzi kuwa bi Aisha alibaki nyuma na kufanya uchafu na Sahaba Yule, hakika ulizuka uzushi mkubwa mno na watu wengi wakiingia katika dhana mbaya juu ya bi Aisha, na walioeneza na kuushadadia ni Wale maadui wakubwa wa Uislamu kipindi kile.

Na Hali hii iliwatesa Sana waumini pamoja na Mtume na mpaka ikabidi Mtume akae mbali na bi Aisha Kwa tukio lile, lakini Alhamdulillah baadae Allah akashusha Aya kumtakasa bi Aisha na kusema hakika ule ulikuwa ni uwongo mkubwa, na hakika wamepata hasara wale wote ambao walizusha habari Ile. Na Allah akasema Hakika Jambo walilolizusha ni dhambi kubwa Sana mbele ya Allah na adhabu kubwa itawafikia wale wote walioshiriki isipokuwa Kwa ambaye atatubu.

Allah akahoji mambo yafuatayo kutokana na uzushi ule.

Je, habari Ile ilipowafikia waumini kwanini hawakuwa na dhana nzuri juu ya bi Aisha?

Kwanini hawakumdhania dhana nzuri bi Aisha na kuona ule ulikuwa ni upuuzi Tu?

Kwanini wasingeacha kueneza ule uzushi na ndimi zao Bila kuwa na uhakika na habari yenyewe?

Nadhani mpaka hapo msomaji wangu mpendwa umepata walau picha nazungumzia nini.

Haya mambo yamejaa Sana mitaani kwetu na majumba yetu, anatokea mpuuzi mmoja anasema Fulani anangoma na wote tunaenda na beat kuyazungumza tusiyokuwa na ushahidi nayo.

Fulani ni mzinzi, Fulani ni mchawi hao moja Kwa moja tunaamini hayo na kuyatangaza Kwa watu na mitaani pasina ushahidi wowote, hakika tunapata dhambi kubwa mbele za Mungu wetu na wallah tusipo tubia na kuacha hizi dhana mbaya Kwa watu hakika tutakuja kuangamia.

Kuna watu kutwa kucha Magufuli kamuua mwanaharakati Fulani, Je ukiitwa utoe ushahidi utaweza? Je siku ya mwisho utamwambia nini Mwenyezi Mungu? Nimetoa mfano wa Jiwe kwasababu tuna mfahamu na tunasema mengi juu yake lakini ole wetu Kwa kuyasema ambayo hatuna ushahidi nayo. Hakika tutakuja kuwajibika Kwa hayo na mengine mengi.

Msomaji wangu always penda kuwa na Dhana nzuri juu ya binadamu wenzako kwani Hilo ni jambo jema Kwa nafsi yako na Mungu wako pia.

Dini yangu inanifundisha kuwa hakika kukataza maovu na kuamrisha mema ni miongoni mwa Sadaka mbele ya Allah mjuzi wa yote.
 
Hizi ni Baadhi ya post Zangu Za Nyuma

TUSOME KUHUSU TABIA NJEMA,KWANI UISLAMU NI KUWA NA TABIA NJEMA


Nimuite Etugrul Bey sio Jina halisi, alikuwa ni boss ambaye alikuwa ana jali Sana utu WA watu, kwake yeye kila binadamu alikuwa na thamani Sawa maadamu tu ni binadamu ni tofauti na watu wengine ambao huwathamini watu kutokana na kitu walinacho,au hadhi waliyo nayo au elimu waliyo nayo.

Tabia hii ilimfanya awapende na kuwathamini wafanyakazi wote iwe WA ngazi ya juu au wa Chini kabisa...na alikuwa na kawaida ya kumsalimia kila mfanyakazi aliyekutana naye pale kazini.

Tabia hii ilimfanya apendwe na kila mtu pale kazini, tofauti na maboss wengine ambao kwao uboss unawafanya wajione miungu watu,wamejawa na kiburi pamoja na majivuno na hivyo kuwafanya wasipendwe na wafanyakazi, kitu ambacho mara nyingi huleta uadui.

Etugrul Bey alikuwa na kawaida ya kuwasalimia walinzi wake pale kazini asubuhi na jioni wakati anapoondoka na alikuwa mkarimu Sana kwao kiasi ambacho kilijenga mahusiano mazuri Sana Kati Yao, siku isiyo na jina iliwadia ambayo ndio ilikuwa ichukue Uhai WA boss huyo, ilikuwa ni mida karibia na jioni boss huyo alikuwa katika kupitiapitia maeneo yake ya kazi basi alikuwa ktk chumba kimoja ambacho ni cold room kinahifadhi samaki wasioze, chumba Hicho kina baridi ya kutosha nikisema ya kutosha ina maana ni baridi haswaa!

Kama unavyojua makosa kaumbiwa mwanadamu, basi afisa anayesimamia chumba kile bahati mbaya nadhani alikuwa na haraka zake, kwahiyo Mda wa kuisha kazi ulipofika yeye kutokana na haraka aliyokuwa nayo alisahau kupitia chumba Hicho kama kawaida yake kuhakikisha kwamba kila kitu kipo Sawa kabla ya kuondoka na kuelekea nyumbani.

Sasa kwakuwa etugrul bey alikuwa na kawaida ya kuaga walinzi wake kabla hajaondoka kurudi nyumbani, walinzi wa zamu wa siku hiyo walijiuliza mbona si kawaida ya boss kuondoka kazini Bila kuwaaga, ndipo walipoenda kuangalia gari lake kweli lipo na kucheki ofisini hayupo, wakaanza kuingiwa na wasi wasi na kuhisi kuna shida ambayo huenda imempata boss wao mpendwa.

Wakaanza msako wa kumtafuta boss wao sehemu mbali mbali mule kiwandani lkn hawakumuona, ndipo mmoja wao akawa na mashaka Sana isije ikawa boss wao akawa amefungiwa ndani ya chumba kile kimakosa kwani alikuwa na kawaida ya kukagua kabla hajaondoka kwenda nyumbani.

Weka pozi Kwanza kidogo hapo. Leo hatuli pop corn wala nini, hakikisha unahesabiwa Sawa? Umuhimu wake ushasemwa Sana kwahiyo naamini kabisa tutalimaliza hili zoezi salama, hata kama hupendi ndo hivyo tena kuhesabiwa lazima!

Haya tuendelee na madini yetu Bbasi wakajadiliana na kuamua wavunje ule mlango wa cold room....lahaula! Kama walivyochezwa na machale baharia alikuwa anakaribia kuganda Kwa baridi Ile Kali...walimkuta ktk Hali mbaya Sana huenda wangechelewa kidogo mwamba angerest in peace! Lkn kama unavyojua kila mtu anakufa Tu siku yake inapofika Hilo halina ubishi! Basi walimuokoa na kumpa huduma ya Kwanza na hatimaye baada ya masaa kadhaa bey alipata nafuu na kuwa Sawa alhamdulillah.

Hekima ya story hii:
Wema unalipa...Utu unalipa ...Ubinadamu unalipa....ebu fikiria kama etugrul bey asingekuwa boss mzuri Kwa wafanyakazi wake bilashaka Leo hii bey angekuwa katika ulimwengu mwingine kabisa....haijalishi wewe Una hadhi gani ktk jamii, Una elimu kiasi gani,unahela kiasi gani, Una cheo kiasi gani...kumbuka mwisho wa siku wote bado ni binadamu na kama binadamu tunategemeana Kwa namna moja au nyingine.

Ukiwa boss mbaya unajenga uadui na watu na huenda hata wafanyakazi wanaweza kupanga kukufanyia ubaya....tafuta hii movie inaitwa THE HORRIBLE BOSSES nadhani wale waliyo icheki hii movie wanajua shughuli yake.
 
Naam kila jioni/usiku tutakuwa na kipengele cha Maswali na Majibu katika nyanja mbali mbali

Ni hapo baadae inshaallah.......
 
Etugrul Bey Allah akuhifadhi na ajaalie hili ktk mizani yako ya kheri, hakika kila atakayepita hapa bila ya uvivu huondoka na kitu kikubwa, jazzakhallahu khair
 
Hizi ni Baadhi ya post Zangu Za Zamani

UBAYA WA KUWA NA DHANA MBAYA


Dhana Mbaya ni Ile hali ya kuwafikiria wenzako vibaya juu ya Tabia zao au Matendo Yao Fulani pasina kuwa na ushahidi wowote ule.

Hii ni dhambi miongoni mwa madhambi ambayo Kwa Mwenyezi Mungu ni makubwa mno, kibinadamu tunaweza kuchukulia ni jambo dogo lakini Kwa Mola wetu ni kubwa mno.

Kuliweka hili Sawa nitahadithia kisa kilichowahi tokea enzi za Mtume Muhammad (rehma na Amani ziwe juu yake) enzi hizo karibia miaka 1400 iliyopita.

Ilikuwa ni kipindi cha Vita ambapo nimesahau ilikuwa ni Vita gani dhidi ya makafiri, kulikuwa na upepo mkali Sana na hali ya hewa ilibadilika Sana, hivyo hivyo ikaamuliwa watu waondoke katika uwanja wa Vita.

Sasa bahati mbaya kipindi Hicho mama wa waumini bi Aisha (r.a) alikuwa ametoka nje ya gari la kuvutwa na farasi na kwenda washroom, huku nyuma wasaidizi wake walisahau kabisa kuwa Mama wa waumini alikuwa hajarejea bado katika hema na wala Mtume pamoja na Askari wengine hawakujua Hilo, basi wakaondoka na kurejea nyumbani huku wakimwacha bi Aisha nyuma pasina kufahamu.

Bi Aisha aliporejea akakuta msafara umeondoka, lakini bahati nzuri huku nyuma kulikuwa na Sahaba mmoja alibakia nyuma kuhakikisha hakuna kitu kilicho sahaulika ndo hamadi akamwona Mama wa waumini na kurejea nae.

Basi kama unavyojua wapuuzi huwa hawakosekani sehemu zote, basi wakazusha upuuzi kuwa bi Aisha alibaki nyuma na kufanya uchafu na Sahaba Yule, hakika ulizuka uzushi mkubwa mno na watu wengi wakiingia katika dhana mbaya juu ya bi Aisha, na walioeneza na kuushadadia ni Wale maadui wakubwa wa Uislamu kipindi kile.

Na Hali hii iliwatesa Sana waumini pamoja na Mtume na mpaka ikabidi Mtume akae mbali na bi Aisha Kwa tukio lile, lakini Alhamdulillah baadae Allah akashusha Aya kumtakasa bi Aisha na kusema hakika ule ulikuwa ni uwongo mkubwa, na hakika wamepata hasara wale wote ambao walizusha habari Ile. Na Allah akasema Hakika Jambo walilolizusha ni dhambi kubwa Sana mbele ya Allah na adhabu kubwa itawafikia wale wote walioshiriki isipokuwa Kwa ambaye atatubu.

Allah akahoji mambo yafuatayo kutokana na uzushi ule.

Je, habari Ile ilipowafikia waumini kwanini hawakuwa na dhana nzuri juu ya bi Aisha?

Kwanini hawakumdhania dhana nzuri bi Aisha na kuona ule ulikuwa ni upuuzi Tu?

Kwanini wasingeacha kueneza ule uzushi na ndimi zao Bila kuwa na uhakika na habari yenyewe?

Nadhani mpaka hapo msomaji wangu mpendwa umepata walau picha nazungumzia nini.

Haya mambo yamejaa Sana mitaani kwetu na majumba yetu, anatokea mpuuzi mmoja anasema Fulani anangoma na wote tunaenda na beat kuyazungumza tusiyokuwa na ushahidi nayo.

Fulani ni mzinzi, Fulani ni mchawi hao moja Kwa moja tunaamini hayo na kuyatangaza Kwa watu na mitaani pasina ushahidi wowote, hakika tunapata dhambi kubwa mbele za Mungu wetu na wallah tusipo tubia na kuacha hizi dhana mbaya Kwa watu hakika tutakuja kuangamia.

Kuna watu kutwa kucha Magufuli kamuua mwanaharakati Fulani, Je ukiitwa utoe ushahidi utaweza? Je siku ya mwisho utamwambia nini Mwenyezi Mungu? Nimetoa mfano wa Jiwe kwasababu tuna mfahamu na tunasema mengi juu yake lakini ole wetu Kwa kuyasema ambayo hatuna ushahidi nayo. Hakika tutakuja kuwajibika Kwa hayo na mengine mengi.

Msomaji wangu always penda kuwa na Dhana nzuri juu ya binadamu wenzako kwani Hilo ni jambo jema Kwa nafsi yako na Mungu wako pia.

Dini yangu inanifundisha kuwa hakika kukataza maovu na kuamrisha mema ni miongoni mwa Sadaka mbele ya Allah mjuzi wa yote.
Kaka naomba sura na aya zilizokuja kubainishi hili
 
Kaka naomba sura na aya zilizokuja kubainishi hili

Suratul Annur:24

Ipitie utitiririke nayo


24:1 - HII NI SURA Tuliyo iteremsha na tukailazimisha; tukateremsha ndani yake Aya zilizo wazi ili mkumbuke.

24:2 - Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume, mtandikeni kila mmoja katika wao bakora mia. Wala isikushikeni huruma kwa ajili yao katika hukumu ya Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na lishuhudie adhabu yao kundi la Waumini.

24:3 - Mwanamume mzinifu hamwoi ila mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina. Na mwanamke mzinifu haolewi ila na mwanamume mzinifu au mshirikina. Na hayo yameharimishwa kwa Waumini.

24:4 - Na wanao wasingizia wanawake mahashumu, kisha wasilete mashahidi wane, basi watandikeni bakora thamanini, na msiwakubalie ushahidi wao tena. Na hao ndio wapotovu

.24:5 - Isipo kuwa wale walio tubu baada ya hayo na wakatengenea; kwani bila ya shaka Mwenyezi Mungu ni Msamehevu, Mwenye kurehemu.

24:6 - Na wale wanao wasingizia wake zao na hawana mashahidi ila nafsi zao, basi ushahidi wa mmoja wao utakuwa kushuhudilia mara nne kwa kiapo cha Mwenyezi Mungu ya kwamba hakika yeye ni katika wasema kweli.

24:7 - Na mara ya tano kwamba laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake ikiwa ni miongoni mwa waongo.

24:8 - Na mke itamwondokea adhabu kwa kutoa shahada mara nne kwa kiapo cha Mwenyezi Mungu ya kwamba huyu mume ni miongoni mwa waongo.

24:9 - Na mara ya tano ya kwamba ghadhabu ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake kama mumewe yu miongoni mwa wanao sema kweli.


24:10 - Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake, na ya kuwa Mwenyezi Mungu ni Mpokeaji toba....

24:11 - Hakika wale walio leta uwongo ni kundi miongoni mwenu. Msifikiri ni shari kwenu, bali hiyo ni kheri kwenu. Kila mtu katika wao atapata aliyo yachuma katika madhambi. Na yule aliyejitwika sehemu yake kubwa miongoni mwao, atapata adhabu kubwa.

24:12 - Kwa nini mlipo sikia khabari hii, wanaume Waumini na wanawake Waumini hawakuwadhania wenzao mema, na kusema: Huu ni uzushi dhaahiri?


24:13 - Kwa nini hawakuleta mashahidi wane? Na ilivyo kuwa hawakuleta mashahidi wane basi hao mbele ya Mwenyezi Mungu ni waongo.

24:14 - Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake katika dunia na Akhera, bila ya shaka ingeli kupateni adhabu kubwa kwa sababu ya yale mliyo jiingiza

.24:15 - Mlipo yapokea kwa ndimi zenu na mkasema kwa vinywa vyenu msiyo yajua, na mlifikiri ni jambo dogo, kumbe mbele ya Mwenyezi Mungu ni kubwa.

24:16 - Na kwa nini mlipo yasikia msiseme: Haitufalii kuzungumza haya. Subhanak Umetakasika! Huu ni uzushi mkubwa!

24:17 - Mwenyezi Mungu anakuonyeni msirejee tena kufanya kama haya kabisa, ikiwa nyinyi ni Waumini!

24:18 - Na Mwenyezi Mungu anakubainisheni Aya. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima.

24:19 - Kwa hakika wale wanao penda uenee uchafu kwa walio amini, watapata adhabu chungu katika dunia na Akhera. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui

.24:20 - Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake, na kuwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mpole, Mwenye kurehemu....

24:21 - Enyi mlio amini! Msizifuate nyayo za Shet'ani. Na atakaye fuata nyayo za Shet'ani basi yeye huamrisha machafu na maovu. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake juu yenu, asingeli takasika miongoni mwenu kabisa hata mmoja. Lakini Mwenyezi Mungu humtakasa amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

24:22 - Na wale katika nyinyi wenye fadhila na wasaa wasiape kutowapa jamaa zao na masikini na walio hama kwa Njia ya Mwenyezi Mungu. Na wasamehe, na waachilie mbali. Je! Nyinyi hampendi Mwenyezi Mungu akusameheni? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.

24:23 - Hakika wanao wasingizia wanawake, wanao jihishimu, walio ghafilika, Waumini, wamelaaniwa duniani na Akhera, nao watapata adhabu kubwa.

24:24 - Siku ambayo zitawashuhudia ndimi zao na mikono yao na miguu yao kwa waliyo kuwa wakiyatenda.

24:25 - Siku hiyo Mwenyezi Mungu atawapa sawa sawa malipo yao ya haki, na watajua kwamba hakika Mwenyezi Mungu ndiye Haki Iliyo Wazi.

24:26 - Wanawake waovu ni wa wanaume waovu, na wanaume waovu ni wa wanawake waovu. Na wanawake wema ni wa wanaume wema, na wanaume wema ni wa wanawake wema. Hao wameepushwa na hayo wanayo yasema; wao watapata msamaha na riziki ya ukarimu.
 
Achague Kuolewa Na Anayependana Naye Japokuwa Si Mcha Mungu Au Ambaye Ni Mcha Mungu?
Maswali: Posa-Sherehe



SWALI:




Asalaam Aleikum Warahmatullah Taala Wabarakatuh, Ninawashukuru sana uongozi mzima wa taasis hii ya Alhidaya, kwani kupitia taasisi yenu nimetoka kwenye giza nene na sasa Alhamdulillah nipo kwenye mwanga na ninatimiza wajibu wangu kama muislam anavyopashwa kutimiza. Swali langu ni kwamba? Kwa kipindi cha nyuma kabla sijatoka gizani! Nilikuwa na mpenzi yaani mvulana ambaye tulishirikiana kutenda maovu hayo na kusema ukweli nampenda sana kijana. Lakini sasa kwa muda mrefu sasa yaani ni zaidi ya miaka minne hatupo pamoja kwani tumekuwa tukiishi mabara tofauti tofauti, lakini mawasiliano yetu yamekuwa ni kwa telephone tu, Sasa baada ya kuusoma Uislam na kuuelewa, nikagundua kama kijana huyo ana walakini kidogo, kwakuwa yeye hajihusishi kabisaa na mambo ya dini na hata ninapomuusia kwake yeye inakuwa tu kama ninatafuta sababu ya kumuacha, na ikiwa nimekwisha elewa kama sifa kubwa ya muoa au muolewaji ni mtu kuwa mchamungu, nami napenda sana kuishi maisha ya kiuchamungu na mpenzi huyu ila ndio hivyo tena kwake inakua ngumu. Na kwa upande mwingine kuna kijana mwingie yeye Maishallah ana muelekea Allah kwa unyenyekevu kabisa na anakila sifa ya uume katika uislam, na yuko tayari kunioa na tukaishi maisha hayo nitakayo mimi kwa sababu naye ndio maisha anayoishi. TATIZO ni kwamba nampenda yule mpenzi wangu alafu familia yake yote inanifahamu na inatambua kama mimi ndiye nitakaeolewa na kijana wao kiasi hata wazazi wanazungumza kwa simu. SASA JE NIFANYE NINI? NINAPENDA NA PIA NINAOGOPA KULAUMIWA NA FAMILIA YAKE NZIMA, LAKINI PIA NINAPENDA NA KUFURAHIA SANA MAISHA YA UCHAMUNGU KAMA KIJANA HUYU ATAKAE KUNIOA. Kwa kweli nahitaji msaada wenu kwa hili kwani wakati flani nahisi kama haya mapenzi yatanipeleka motoni, na vilevile najiuliza nitaweza kumpenda kijana huyu mwingine ili nitekeleze wajibu wangu kama mwanamke wa kiislam? Sababu tutakuwa tunakumbushana na kukatazana batwili na hali ikiwa na yeye anajua maana na hukmu za ndoa katika uislaam,



JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Kwanza tunapenda kukuarifu kwamba hatukuwa tukipokea maswali kama tulivyoweka tangazo. Lakini kutokana na umuhimu wa Swali lako tumeona tulipe kiupambele kwani linahusiana na maamuzi makuu yatakayokuathiri katika maisha yako ya kidunia na Akhera.




Pili tunakupa nasaha kwamba katika maamkizi ya salaam, usiwe unaongeza neno 'Ta'ala' kwenye Salaam kwa kusema 'Assalaamu 'Alaykum wa RahmatuLlaahi Ta'ala wa Barakaatuh', kwani si jambo tulilofundishwa katika Salaam na hivyo ni bora mtu kuliepuka katika Salaam.










Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mapenzi na yaliyopita kabla ya kujua kwako haki na ukweli. Mwanzo tumefurahi sana kwa swali lako kuhusu suala hilo nyeti katika jamii yetu ya Kiislamu.



Inatakiwa ifahamike kwa kila mmoja ambaye ni Muislamu kuwa kupenda ni lazima kuwe kwa ajili ya Allaah Aliyetukuka na kuchukia pia kuwe ni kwa ajili Yake. Haiwezekani kwa Muislamu kuwa Muislamu wa kihakika ikiwa atakuwa anayaendea maaswiya na mambo ya madhambi. Tufahamu kuwa katika huu ulimwengu unalofanya utalaumiwa na waja lakini la muhimu ambalo tunahitajika tuzingatie ni kutopata lawama ya Muumba wetu. Allaah Aliyetukuka Anasema: “Enyi mlioamini! Atakayeiacha miongoni mwenu Dini yake, basi Allaah Atakuja leta watu Anaowapenda nao wanampenda, wanyenyekevu kwa Waumini na wenye nguvu juu ya makafiri, wanapigania Jihadi katika Njia ya Allaah, wala hawaogopi lawama ya anaye laumu. Hiyo ndiyo fadhila ya Allaah, Humpa Amtakaye. Na Allaah ni Mkunjufu na Mwenye kujua” (al-Maa’idah [5]: 54).



Inatakiwa tujue kuwa tuliyoyafanya kabla ya kusilimu yote yamefutwa, lakini ya makosa utakayo yafanya sasa yanaandikwa na yasiyowapita kabisa. Weka mawazo yako pamoja, tilia sana maanani nasaha za Allaah Aliyetukuka na Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na hayo ndiyo yatakayotufanya tufaulu kukubwa sana.



Naomba tusome pamoja yafuatayo:



1. Imaam al-Bukhaariy na Muslim wametunukulia Hadiyth ifuatayo kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mwanamke huolewa kwa mambo manne: Kwa mali yake, nasaba yake, uzuri wake na Dini yake. Chagua mwenye dini au utapata hasara”. Na ndivyo mwanamme anavyochaguliwa.







2. Imaam at-Tirmidhiy naye ametunukulia yafuatayo kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam): “Akikujieni mnaye mridhia Dini yake na maadili yake basi muozeni. Mkitofanya hivyo basi kutakuwa na fitna katika ardhi na uharibifu mkubwa sana”.



Uchaguzi ni wako dada yetu kwani nasaha za hapo juu zipo wazi kabisa. Nasi tuko pamoja nawe katika kuichunga haki, hata hivyo itabidi ufuate mambo yafuatayo ili usighurike na shetani kiumbe ambaye haitaki Dini:



1. Kata mawasiliano na yule rafiki wako wa kwanza kwani huyo atakupeleka motoni baada ya kuongoka. Akikupigia simu mwambie wazi kuwa uhusiano wenu umeisha kwani hutaki kurudi katika dhambi. Watu wa maasiya ni muhimu kususiwa lau sivyo basi wataendelea tu huku wakiona kuwa wako sawa.







2. Ili kuweza kumsahau huyo rafiki wa kwanza fanya haraka kufanya nikaha na huyu wa pili aliyeshika Dini baada ya kuswali Swalatu Istikhaarah. Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo:







Muda Wa Swalah ya Istikhaarah




Kwa Nini Tuswali Istikhaarah Na Iswaliwe Kwa Ajili Ya Nini - Ipi Du'aa Yake




Du’aa Ya Swaalatul-Istikhaarah Ni Kabla Ya Swalah Au Baada Ya Swalah?










Mkiwa wawili hivyo itakusaidia kuishikilia Dini kwani mtakuwa mnahimizana katika ya kheri. Na pia hilo litakufanya mwenzio wa kwanza aone basi yake yashakwisha. Usichelewe kwani kuchelewa kunaweza kukuweka pabaya.



Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Akupatie ujasiri na hima ya kuchagua la kweli na haki na kuweza kushikamana nalo.



Na Allaah Anajua zaidi.
 
Aliyeposa Kisha Akahutumiwa Kuwa Kambaka Mtoto
Maswali: Posa-Sherehe
SWALI:




Asalaam alayku ama baada ya kumshuru Allah Subuhana Huwataala na kutakia rehma Mtume wetu Muhammad Salallah Alayhi Wasalaam. Napenda kuwatakia kila la kheri waislamu wote wa ujumla.




Swali langu lipo hapa me nina jamaa yangu alikuwa nataka kufunga ndoa na jamaa mmoja hivi yaani huyo bwana harusi ni jamaa yao. Sasa ikawa harusi bado kama wiki 2 hivi. Ikatujia habari kuwa bwana harusi amebaka mjukuu wa shangazi yake. Sasa wengine wanasema ni kweli na wako wanaosema si kweli. Yeye mwenyewe anasema si kweli yeye anamuachia Mungu tu na yupo tayari kula kiapo kwa kosa hili hajafanya. Sasa me swali langu lipo hapa. Kuna hukumu gani katika dini yetu. Je, huyu dada anaweza kuolewa nae au laa maana ndio harusi imevunjika na katika familia yao wako wanaosema bora aolewe nae na wako waosema arudishiwe pesa zake. Je hukumu yake na huyo bint alibakwa ni mke wa mtu na anasema kuwa anamuekea kisasi hata siku yoyote yeye atamlipizi. Je, nini hukumu yake hapa? Naomba utsaidie.





JIBU




Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.




Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu posa, harusi na kubaka. Hakika mara nyingi huwa tunajitia katika shida kwa kushindwa au kutotaka kufuata maagizo ya kisheria. Kitendo cha uzinzi (zinaa) si kitendo kidogo katika sheria yetu na sheria hakuacha mlango huo kwa dhana na fikra zetu. Mwanzo tayari kuna utata kama huyo bwana harusi amefanya kitendo hicho au hakufanya. Yeye mwenyewe anasema hajafanya, hivyo inatakiwa tuwe na dhana nzuri kwake.




Ama katika sheria, kitendo cha zinaa ni lazima kishuhudiwe na Waislamu wane, waadilifu, walio baleghe na wenye akili timamu. Ikiwa itakuwa wamepatikana hao, tatizo na utata wote utaondoka. Ikiwa hakuna ushahidi huo basi huyo kijana hana hatia yoyote. Tunaomba kila mmoja awe ni mwenye kusoma tafsiri ya Suratun Nuur (24): 1 – 10, kwa maagizo na mafunzo mengi ndani yake.




Kuondosha utata, huyo bwana anaweza kuozeshwa huyo msichana. Na ikiwa familia ya msichana pamoja na msichana mwenyewe amekuwa hataki tena kuolewa na huyo kijana, inabidi harusi hiyo ivunjwe na huyo kijana arudishiwe pesa zake na pia uhasama usiwepo.




Kwa kuwa sisi tuko mbali hatuwezi kusema zaidi ya hayo. Kwa kupata ufumbuzi wa hayo, inabidi kesi hiyo ipelekwe kwa Qaadhi kama wapo sehemu mnayoishi. Ikiwa hawapo basi pateni Shaykh mwadilifu ili aweze kuwatatulia hayo mengine.




Twawatakia kila la kheri katika kupata suluhisho kwa hilo.




Na Allaah Anajua zaidi
 
Amekubali Posa Ya Muislamu Aliyeshika Dini, Lakini Sasa Anataka Kuolewa Na Aliyesilimu Akikhofu Atapotea Asipomkubali
Maswali: Posa-Sherehe
SWALI:

Asalam aleikum, swali langu ni hili. Mimi nimeposwa na nimekubali posa hii kwakuwa huyo kijana anajua dini kuliko huyu niliyempenda. Kijana niliye mpenda amesilimu na kwao si waislamu. Kwa muda sasa naona amebadili tabia yeke nakuwa kijana mwema, amejua dini vizuri na anifuata kwa kadri ya uwezo wake inshaallah.

Swali ni kwamba naweza vunja posa yangu kwa yule kijana wakwanza ili niolewe na huyu kwani nampenda na nnahofu nikimwacha atakua ni mwenye kupotea. Wa aleikum salaam.



JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.







Shukrani kwa swali lako kuhusu kubadili mawazo na kutaka kuolewa na mwanamme mwengine baada ya kumkubali wa mwanzo.

Ni hakika isiyopingika kuwa mapenzi na huruma ya kikweli baina ya wanandoa yanapatikana tu baada ya kuoana na sio kabla.

Mnaweza kudanganyana kuwa mnapendana lakini uhakika wake unanidhiri tu baada ya kuingia katika uanandoa. Na hilo ndilo Alilotuarifu Allaah Aliyetukuka katika Suratur Ruum (30): Aayah ya 21.

“Na katika Ishara Zake ni kuwa Amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaofikiri.” (Ar-Ruum (30): 21)


Mwanaadamu kwa ujumla wake na haswa Muislamu ni mtu mwenye kutarajia mema na mazuri kwa kiasi kikubwa. Huwa hana khofu kwa sababu yote yanayotokea yameandikwa na Allaah Aliyetukuka Aliye mjuzi wa yote yaliyotokea, yanayotokea na yatakayotokea. Sasa Muislamu huwa hana wasiwasi wa lolote. Yeye anafanya juhudi kwa atakayo kuyafanya na mengine humuachia Allaah Aliyetukuka kutia tawfiki Yake. Kwa hivyo, usiwe na khofu na aliyesilimu, yeye ikiwa anaitaka Dini hii kweli anaweza kupambana na mitihani mwisho ataivuka, atapata mke ampendaye yeye siye anayependwa naye.


Ama ukija katika shari’ah hakuna wasiwasi kuwa mwanamke anaweza kuivunja posa ya mwanamme aliyemposa kwa sababu moja au nyengine. Na ikiwa mwanamme ametoa mahari kwa ajili ya mke mtarajiwa basi mke anatakiwa ailipe au kurudisha mahari hayo ili yeye ajiondoe na mume asiwe ni mwenye kupata hasara.


Hata hivyo, ikiwa kijana mwema amekuja kukuposa kwa njia ya sawa inayotakiwa na Dini ya Uislamu ni vyema wewe baada ya kukubali uwe utatimiza hiyo ahadi kwani kukataa baada ya kukubali, na sio kukataa kuwa kijana hakushika Dini kunaweza kumvunja moyo asiwe ni mwenye kutaka tena kuoa baada ya kupata hayo.


Nasaha ambayo tunaweza kukupa ni wewe ufikirie sana kuhusu suala hilo na kabla ya kufikia uamuzi wowote, fanya yafuatayo:




1. Swali Swalaah ya Istikhaarah, kwani hatokhasirika mwenye kumshauri Allaah Aliyetukuka.




2. Shauriana na watu wa nyumbani kwako, kama wazazi, dada na marafiki wa karibu wenye kukutakia kheri.




Ule uamuzi utakaochukua mtegemee Allaah Aliyetukuka nasi tunakuombea kila la kheri na fanaka katika Dini na dunia yako.




Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Posa-Sherehe



SWALI




Je, Baba mdogo anayoruhusa ya kuwa walii kama baba mzazi wa mtoto yupo ila ameidhinisha iwe hivyo?










JIBU:




Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.




Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu ami kuwa walii wa mtoto. Ami kisheria hawezi kuwa walii ikiwa baba mzazi yupo. Hata hivyo, ikiwa baba mzazi amemuwakilisha ndugu kuwa ndiye awe anatoa idhini ya binti zake basi uwakala huo wa uwalii unakuwa sawa.




Na Allaah Anajua zaidi.
 
SWALI:
Assalam alykum warahmatullahi wabarakatu shukran kwanza kwa kazi yenu murwa ALLAH (subhanahu wataallah) awabariki na atujalie tuwe wenye kuupokea uongofu ameen ama kuhusu swali langu ni kuwa pana shabab ambaye ni muumin na dhamira yake ilikua kuoa, kwa kuwa ashaafikia, sasa dada wa mamake aliyekuwa anaishi nae wakiwa pamoja na mume wake wakamwashiria kijana huyo wao kwangu, lakini rijali huyu hakupiga hatua yoyote kuhusu swala hilo la kuashiriwa kwangu, basi kwa vile mimi na wao ni majirani, na yule mama nina uhusiano mzuri nae wakijirani mimi huenda sana hapo kwao kuwajulia hali nikipata muda, na niliwahi kusikia mara kadha wakinitaja bila kunihusisha hadi siku, akanambia kama utani, hutaki nikuoze mwanangu, nami sikuchukulia sana jambo hilo uzito, baada ya muda hivi nikawa simuoni rijali yule pale nyumbani kwa halati yake, bahati nikakutana na kakake nikamuuliza akanieleza kuwa kwa ajili ya kazi yuko mjini, basi nami nikachukua no yake hapo kwa kuwa nilikua nikimtaja moyoni sana nikawasiliana nae na hapo ndipo pia aliwahi sasa kunieleza kinagaubaga mambo yalivyokuwa pale nyumbani kwao, kuwa walitaka anioe mimi, sasa sababu aliyonipa kwa nini hakupiga hatua ni, alikua hanijui vyema ni kuniona 2, kisha kuna shangazile aliwahi kumwambia kuwa huyu halati yake ana moyo wa huruma na akiona yatima hasa kama mimi nilivyo hutaka amsaidie kivyovyote ili awe pahala pazuri bila kufikiria baadaye mara akuletee balaa pengine ukimuoa, na akanambia pia alikuwa amekwenda mpaka rwanda kwa ajili ya kutafuta mke, ila hakupata, kisha akanambia nikae nifikirie na niwahusie wazee huyu kijana, lakini kila nikitafakari na kupima niliona anapata pressha kwa huyu halati lakini yeye sikumuona na interest, tukakaa muda bila mawasiliano kisha halati na mume wake wakanifuata kutaka kujua nani wali wangu wa haki kuposwa mimi, nikawaambia kwani babangu yuko hai japo hakunilea kwa ajili ya kutengana, mama ndo alifariki, lakini sikufurahia utaratibu huo kwani yule kijana hakuniambia chochote na hakukua na mawasiliano ndipo nikawaambia siko tayari kwa ndoa, basi baada ya muda wa mwezi hivi jambo hili likawa lanizunguka kichwani, na sasa amesafiri tena saudia lakini kikazi , sasa mimi nimekua nikimtumia mail za kukumbushana mema ya kidini kama vile ninavyowatumia ndugu zangu waislamu ambao ninazo adress zao, sasa mawazo ya mimi kuolewa nae yamenijia tena moyoni na sina uhakika nikumbane nalo jambo hili vipi kwani sijamwambia kitu tena na hajanambia kitu ila halati kila akiniona aniuliza, hakuna mabruk yoyote bado, naswali istikhara na nataraji kupata jibu kwa kumtegeme Mola Aliye mjuzi, na pia niliona niwatake ushauri wenu, samahani kwa maelezo yangu marefu ila nimetaka munielewe vyema, je mutanishauri vipi? Jazakallahu kheir


JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihiwasallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Kwanza tunakukumbusha kuwa hakutakiwi kwa mwanamke au mwanamme wa Kiislamu kuwa na mawasiliano na jinsia nyingine na hata kufikia kuomba namba ya simu au mawasiliano na asiye Mahram wake. Hali hiyo ni katika zile hali za kukaribia zinaa na haifai inapaswa iepukwe kabisa.

Ndoa ni katika ‘Ibaadah nzuri kabisa kwa Muislamu – kwa mwanamme na mwanamke. Na haifai kwa mwanamme kukaa kwa muda mrefu baada ya kubaleghe na ana uwezo naye asioe. Na vile vile mwanamke naye hafai kukataa posa pasi na sababu yoyote ya kishari’ah, kwani kufanya hivyo kunaweza kumtumbukiza Muislamu katika dimbwi la madhambi makubwa ya zinaa.

Hata hivyo, mara nyingi hutokea shida kubwa sana kwa wanandoa kwa ajili ya wao kusukumwa kumuoa au kuolewa na asiyempenda. Na kwa ajili ya kuridhishana mnakuja baada ya kuoana kusumbuana na mwisho kuachana jambo ambalo si zuri Kiislamu.

Nasaha ambazo tunaweza kukupata ni kuendelea kuswali Swalaah hiyo ya Istikhaarah, na hujatuambia umeona ishara gani kutoka kwa Allaah Aliyetukuka. Ikiwa ishara ni nzuri basi kubali posa ya huyo kijana lakini ikiwa ni kinyume basi achana naye na Allaah Aliyetukuka Atakuletea mwenye kheri nawe katika maisha yako.

Ikiwa mpaka sasa hakuna ishara yoyote, anza kuuliza kuhusu huyo kijana, kuhusu utekelezaji wake wa Dini kama Swalaah, Funga na amali nyengine na vile vile tabia yake. Ikiwa ameshika Dini na tabia yake ni nzuri basi tawakali kwa Allaah Aliyetukuka na In-shaa-Allaah, Allaah Atakutilia tawfiq. Na kama sifa hizo mbili hana achana naye. Na kufanya hivyo utapata msaada wa Allaah Aliyetukuka kwa kukutunukia aliye na kheri nawe.

Nasaha nyengine ambayo tunaweza kukupa ni wewe kukata mawasiliano uliyonayo hivi sasa na kijana huyo kwani hiyo ni njia ya kujikurubisha na zinaa na kuwemo katika maasi.

Tunakuombea kila la kheri hapa duniani na Kesho Akhera.

Na Allaah Anajua zaidi
 
SWALI:

Assalaamu alaikum.

Kwanza natoa shukurani zangu kwa msaada wenu wa kutuelimisha kunako dini yetu. Allah awalipe pepo yake, ameen. Swali langu ni vipi muislamu mwanaume kama amkwishafikia uamuzi wa kwamba yuko tayari kuoa, uwezo akawa anao, lakini hana mchumba kama ilivyozoeleka leo ndani ya jamii zisizokuwa za kiislamu; ni upi utaratibu wa kuanzisha uchumba unaokubaliana na sheria zetu za kiislamu?





JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Kwanza tunakushukuru kwa du’aa zako na tunamuomba Allaah Atutakabalie hizi ‘amali zetu na pia Awazidishie nyinyi elimu ya Dini yenu na muweze kupata mwelekeo mwema wa kuweza kuifikia pepo inshaAllaah.

Na shukrani zetu kwa swali lako kuhusu taratibu za uchumba na kuoa. Hakika Uislamu umeweka utaratibu mzuri wa mvulana au msichana kutafuta wa pili wake katika maisha ya kindoa bila ya kupitia mifumo ambayo ni ya kumtweza mwenziwe.

Msichana pia anaweza kutafuta mchumba katika mipaka ya Uislamu bila ya kuwa na tatizo lolote lile. Hata hivyo, mara nyingi ni mvulana ndiye mwenye kutafuta mchumba kulingana na mipaka iliyowekwa na Uislamu. Ama kuhusu njia za Kiislamu za kutafuta mchumba zipo kadhaa na hapa tutaangazia kama mbili ambazo zinatumika sana. Nazo ni kama zifuatazo:

1. Kumjua msichana kwa njia moja au nyingine. Inawezekana umemjua kwa kuwa mlisoma Madrasah moja, au shule au chuo kimoja na ukamuona kulingana na nadharia yako ni msichana anayejistahi na kuchunga mipaka ya Dini. Hata hivyo, kwa sababu hamjaingiliana sana inabidi uulizie kwa wanaomjua kuhusu undani zaidi wa Dini na maadili yake. Wale ambao wanaweza kukusaidia ni madada zako au jamaa wako wa kike ambao wanaweza kumfuatilia katika mipaka ya Kiislamu na hivyo kufuata taratibu nyingine baada ya hapo.




2. Njia hii ni ile ambayo pindi mvulana anapokuwa tayari kuoa, anakaa chini na kuzungumza na mamake, dada zake, shangazi au halati zake na kuwaelezea lengo lake la kutaka kuoa. Hapo inabidi uwape sifa za mke unayemtaka na baada ya hapo watakutafutia mwenye sifa hizo kwani wao ndio wanaingiliana sana na wenziwao kuliko wewe au jamaa zako wa kiume. Mbali na kuwa jamaa zako wa kiume huenda wakawajua wale wasichana wengine walio na ujamaa na wao wa karibu hivyo kuweza kukusaidia katika hilo.

Baada ya kuridhika na yale uliyoambiwa na katika uchaguzi huo, utaratibu unaofuata ni kuswali Swalah ya Istikhaarah na kisha kinachofuatia ni kupeleka posa kwa wazazi wa msichana na kuonana ana kwa ana na unayemposa. Kuonana huko si faragha bali uonane naye mbele ya maharimu yake. Ikiwa umeridhika na Dini na maadili yake na ukaridhishwa na umbile lake mtaendelea na posa hiyo na kupanga siku ya harusi. Ikiwa hukuridhika basi utatafuta mwengine.

Huku kuonana na huyo unayetaka kumuoa ni kwa mujibu wa nasiha aliyopatiwa Mughiyrah bin Shu'bah (Radhiya Allaah 'anhu) na Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam), kwani kufanya hivyo kunajenga mapenzi. Wapo wanawake wengine ambao katika macho yao wana kitu kama walivyokuwa wanawake wa Kianswaar wa Madiynah. Na kimaumbile unaweza ukawa hupendezewi na hilo, hivyo utajitoa mapema.




Na Allaah Anajua zaidi
 
002-Riyaadhw Asw-Swalihiyn: Mlango Wa Tawbah
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب التوبة

002 - Mlango Wa Tawbah



Alhidaaya.com



قَالَ العلماءُ: التَّوْبَةُ وَاجبَةٌ مِنْ كُلِّ ذَنْب، فإنْ كَانتِ المَعْصِيَةُ بَيْنَ العَبْدِ وبَيْنَ اللهِ تَعَالَى لا تَتَعلَّقُ بحقّ آدَمِيٍّ فَلَهَا ثَلاثَةُ شُرُوط:
أحَدُها: أنْ يُقلِعَ عَنِ المَعصِيَةِ.
والثَّانِي: أَنْ يَنْدَمَ عَلَى فِعْلِهَا.
والثَّالثُ: أنْ يَعْزِمَ أَنْ لا يعُودَ إِلَيْهَا أَبَدًا. فَإِنْ فُقِدَ أَحَدُ الثَّلاثَةِ لَمْ تَصِحَّ تَوبَتُهُ.
وإنْ كَانَتِ المَعْصِيةُ تَتَعَلقُ بآدَمِيٍّ فَشُرُوطُهَا أرْبَعَةٌ: هذِهِ الثَّلاثَةُ، وأنْ يَبْرَأ مِنْ حَقّ صَاحِبِها، فَإِنْ كَانَتْ مالًا أَوْ نَحْوَهُ رَدَّهُ إِلَيْه، وإنْ كَانَت حَدَّ قَذْفٍ ونَحْوَهُ مَكَّنَهُ مِنْهُ أَوْ طَلَبَ عَفْوَهُ، وإنْ كَانْت غِيبَةً استَحَلَّهُ مِنْهَا. ويجِبُ أنْ يَتُوبَ مِنْ جميعِ الذُّنُوبِ، فَإِنْ تَابَ مِنْ بَعْضِها صَحَّتْ تَوْبَتُهُ عِنْدَ أهْلِ الحَقِّ مِنْ ذلِكَ الذَّنْبِ وبَقِيَ عَلَيهِ البَاقي.
وَقَدْ تَظَاهَرَتْ دَلائِلُ الكتَابِ والسُّنَّةِ، وإجْمَاعِ الأُمَّةِ عَلَى وُجوبِ التَّوبةِ.
التوبة: الرجوع عن معصية الله تعالى إلى طاعته، وطلب الاستحلال مِنَ المقذوف ونحوه إن بلغه ذلك، وإلا كفى الاستغفار



‘Ulamaa wamesema: ni wajibu kutubia kwa kila dhambi anayoitenda mtu. Maasi yanapokuwa ni baina ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’aalaa) na mja Wake yasiyofungamana na haki ya mwana Aadam, yana shuruti tatu:

1- Aache maasi

2- Ajute juu ya kuyatenda

3- Aazimie kutoyarudia tena kabisa. Moja katika shuruti hizo ikikosekana, tawbah yake haitosihi.

4- Maasi yanapofungamana na haki ya mwana Aadam, basi shuruti za tawbah ni nne: ni hizo tatu zilizotangulia na ya nne ni: aache haki ya mwenyewe; ikiwa ni mali na mfano wake amrejeshee, ikiwa ni haddi (adhabu) ya kutukana au mfano wake, atammakinisha au amuombe msamaha. Na ikiwa ni kusengenya basi atamuomba amhalalishie. Yapasa atubie dhambi zote. Akitubia baadhi yake, tawbah yake itasihi kutokana na dhambi ile kwa watu wa haki, na atabakiwa na dhambi nyinginezo. Dalili ya Qur-aan, Hadiyth na ijmaa’ ya ummah zipo nyingi katika kuthibitisha namna inavyotakiwa mtu kutubia.

قَالَ الله تَعَالَى:

وَتُوبُوا إِلَى اللَّـهِ جَمِيعًا أَيُّهَ الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

Na tubuni kwa Allaah nyote, enyi Waumini mpate kufaulu. [An-Nuwr: 31]

وَأَنِ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ

Na kwamba: “Mwombeni Rabb wenu maghfirah kisha tubuni Kwake.” [Huwd: 3]

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّـهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا

Enyi walioamini! Tubieni kwa Allaah tawbah ya nasuha (kwelikweli). [At-Tahriym: 8]





Hadiyth – 1

عن أبي هريرةَ رضي الله عنه قَالَ: سمعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((واللهِ إنِّي لأَسْتَغْفِرُ الله وأَتُوبُ إِلَيْه في اليَوْمِ أَكْثَرَ مِنْ سَبْعِينَ مَرَّةً)). رواه البخاري

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Wa-Allaahi mimi namuomba Allaah maghfirah na natubia Kwake zaidi ya mara sabini kwa siku.” [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 2



وعن الأَغَرِّ بنِ يسار المزنِيِّ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((يَا أَيُّهَا النَّاسُ، تُوبُوا إِلى اللهِ واسْتَغْفِرُوهُ، فإنِّي أتُوبُ في اليَومِ مائةَ مَرَّةٍ)). رواه مسلم.

Al-Agharri bin Yasaar Al-Muzaniyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Enyi watu, tubieni kwa Allaah na mumuombe maghfirah. Hakika mimi natubia Kwake mara mia kwa siku.” [Muslim]





Hadiyth – 3



وعن أبي حمزةَ أنسِ بنِ مالكٍ الأنصاريِّ- خادِمِ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم رضي الله عنه- قَالَ: قَالَ رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((للهُ أفْرَحُ بِتَوْبَةِ عَبْدِهِ مِنْ أَحَدِكُمْ سَقَطَ عَلَى بَعِيرهِ وقد أضلَّهُ في أرضٍ فَلاةٍ)). مُتَّفَقٌ عليه.

وفي رواية لمُسْلمٍ: ((للهُ أَشَدُّ فَرَحًا بِتَوبَةِ عَبْدِهِ حِينَ يتوبُ إِلَيْهِ مِنْ أَحَدِكُمْ كَانَ عَلَى رَاحِلَتهِ بأرضٍ فَلاةٍ، فَانْفَلَتَتْ مِنْهُ وَعَلَيْهَا طَعَامُهُ وَشَرَابهُ فأَيِسَ مِنْهَا، فَأَتى شَجَرَةً فاضطَجَعَ في ظِلِّهَا وقد أيِسَ مِنْ رَاحلَتهِ، فَبَينَما هُوَ كَذَلِكَ إِذْ هُوَ بِها قائِمَةً عِندَهُ، فَأَخَذَ بِخِطامِهَا، ثُمَّ قَالَ مِنْ شِدَّةِ الفَرَحِ: اللَّهُمَّ أنْتَ عَبدِي وأنا رَبُّكَ! أَخْطَأَ مِنْ شِدَّةِ الفَرَحِ))

Abuu Hamzah, Anas bin Maalik Al-Answaariyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) mtumishi wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amehadithia kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah Huifurahia mno tawbah ya mja Wake kuliko mmoja wenu aliyempata kwa ghafla ngamia wake baada ya kwisha kumpoteza katika ardhi ya jangwa.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

Riwaayah nyingine ya Muslim inasema: “Allaah Ana furaha mno kwa mja Wake wakati anapomuomba tawbah kuliko mmoja wenu aliyekuwa juu ya ngamia wake katika ardhi ya jangwa, akimkimbia naye amebeba chakula chake na maji yake, akakata tamaa kuwa atampata; akauendea mti na akalala kivulini mwake naye ameshakata tamaa ya kumpata ngamia wake. Alipokuwa yuko katika hali hiyo, ghafla akamuona amemsimamia mbele yake, akamshika hatamu yake, halafu akasema kutokana na furaha kubwa: Ee Rabb! Wewe ni mja wangu nami ni Rabb wako! Amekosea kutokana na furaha kubwa (aliyonayo).”





Hadiyth – 4



وعن أبي موسَى عبدِ اللهِ بنِ قَيسٍ الأشْعريِّ رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((إنَّ الله تَعَالَى يَبْسُطُ يَدَهُ بالليلِ لِيَتُوبَ مُسِيءُ النَّهَارِ، ويَبْسُطُ يَدَهُ بالنَّهَارِ لِيَتُوبَ مُسِيءُ اللَّيلِ، حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ مِنْ مَغْرِبِها)). رواه مسلم

Abuu Muwsa, 'Abdullaah bin Qays Al-Ash’ariyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Hunyoosha Mkono Wake usiku ili yule aliyekosea mchana apate kutubia, na Hunyoosha mkono Wake mchana ili yule aliyekosea usiku apate kutubia, (hali hiyo huendelea) mpaka jua lichomozapo upande wa magharibi” [Muslim]





Hadiyth – 5



وعن أبي هُريرةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ تَابَ قَبْلَ أنْ تَطْلُعَ الشَّمْسُ مِنْ مَغْرِبِها تَابَ اللهُ عَلَيهِ)). رواه مسلم

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mwenye kutubia kabla ya jua kuchomoza upande wa magharibi, Allaah Atamkubalia tawbah yake.” [Muslim]





Hadiyth – 6



وعن أبي عبد الرحمن عبد الله بنِ عمَرَ بنِ الخطابِ رضيَ اللهُ عنهما عن النَّبي صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((إِنَّ الله عز وجل يَقْبَلُ تَوبَةَ العَبْدِ مَا لَمْ يُغَرْغِرْ)). رواه الترمذي، وَقالَ: ((حديث حسن))

Abuu ‘Abdir-Rahmaan, ‘Abdullaah bin ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu anhumaa) amehadithia kwamba: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika Allaah ‘Azza wa Jallaa Huikubali tawbah ya mja madamu roho yake haijafika kooni.” [At-Tirmidhiy na amesema: Hadiyth hii ni Hasan]





Hadiyth – 7



وعن زِرِّ بن حُبَيْشٍ، قَالَ: أَتَيْتُ صَفْوَانَ بْنَ عَسَّالٍ رضي الله عنه أسْألُهُ عَن الْمَسْحِ عَلَى الخُفَّيْنِ، فَقالَ: ما جاءَ بكَ يَا زِرُّ؟ فقُلْتُ: ابتِغَاء العِلْمِ، فقالَ: إنَّ المَلائكَةَ تَضَعُ أجْنِحَتَهَا لطَالبِ العِلْمِ رِضىً بِمَا يطْلُبُ. فقلتُ: إنَّهُ قَدْ حَكَّ في صَدْري المَسْحُ عَلَى الخُفَّينِ بَعْدَ الغَائِطِ والبَولِ، وكُنْتَ امْرَءًا مِنْ أَصْحَابِ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم فَجئتُ أَسْأَلُكَ هَلْ سَمِعْتَهُ يَذكُرُ في ذلِكَ شَيئًا؟ قَالَ: نَعَمْ، كَانَ يَأْمُرُنا إِذَا كُنَّا سَفرًا- أَوْ مُسَافِرينَ- أنْ لا نَنْزعَ خِفَافَنَا ثَلاثَةَ أَيَّامٍ وَلَيالِيهنَّ إلا مِنْ جَنَابَةٍ، لكنْ مِنْ غَائطٍ وَبَولٍ ونَوْمٍ. فقُلْتُ: هَلْ سَمِعْتَهُ يَذْكرُ في الهَوَى شَيئًا؟ قَالَ: نَعَمْ، كُنّا مَعَ رسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم في سَفَرٍ، فبَيْنَا نَحْنُ عِندَهُ إِذْ نَادَاه أَعرابيٌّ بصَوْتٍ لَهُ جَهْوَرِيٍّ: يَا مُحَمَّدُ، فأجابهُ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم نَحْوًا مِنْ صَوْتِه: ((هَاؤُمْ)) فقُلْتُ لَهُ: وَيْحَكَ! اغْضُضْ مِنْ صَوتِكَ فَإِنَّكَ عِنْدَ النَّبي صلى الله عليه وسلم، وَقَدْ نُهِيتَ عَنْ هذَا! فقالَ: والله لا أغْضُضُ. قَالَ الأعرَابيُّ: المَرْءُ يُحبُّ القَوْمَ وَلَمَّا يلْحَقْ بِهِمْ؟ قَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم: ((المَرْءُ مَعَ مَنْ أَحَبَّ يَومَ القِيَامَةِ)). فَمَا زَالَ يُحَدِّثُنَا حَتَّى ذَكَرَ بَابًا مِنَ المَغْرِبِ مَسيرَةُ عَرْضِهِ أَوْ يَسِيرُ الرَّاكبُ في عَرْضِهِ أرْبَعينَ أَوْ سَبعينَ عامًا- قَالَ سُفْيانُ أَحدُ الرُّواةِ: قِبَلَ الشَّامِ- خَلَقَهُ الله تَعَالَى يَوْمَ خَلَقَ السَّمَاواتِ والأَرْضَ مَفْتوحًا للتَّوْبَةِ لا يُغْلَقُ حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ مِنْهُ. رواه الترمذي وغيره، وَقالَ: ((حديث حسن صحيح)).

Zirru bin Hubaysh amesema: “Nilimuendea Swafwaan bin ‘Assaal (Radhwiya Allaahu ‘anhu) nikimuuliza kuhusu kupangusa juu ya khuffu mbili. Akaniuliza: Ni jambo lipi limekuleta Ee Zirru? Akasema: “Hakika Malaika humuwekea mbawa zao mwenye kutafuta ‘Ilmu kwa kumridhia anachokitafuta. Nikamwambia: “Kwa hakika nimeingiwa na shaka moyoni mwangu na kupangusa juu ya khuffu baada hajja kubwa na ndogo, nami nilikuwa mmoja katika Swahaba wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kwa hivyo nimekuja kukuuliza je, uliwahi kumsikia akisema chochote katika hilo?” Akajibu: “Ndio. Alikuwa akituamuru tunapokuwa safarini tusivue khuffu zetu michana mitatu na masiku yake, isipokuwa tu kutokana na janaba, lakini kutokana na haja kubwa, ndogo na kulala (tusivue).” Nikamuuliza: “Je, ulimsikia akisema chochote juu ya mapenzi?” Akajibu: “Ndio. Tulikuwa na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) safarini, tulipokuwa tupo kwake, kwa ghafla akaitwa na Bedui kwa sauti kubwa: “Ee Muhammad!” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamuitikia kwa sauti kama yake: “Njoo.” Nikamwambia (Bedui): “Nakuhurumia, teremsha sauti yako kwani upo mbele ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na umekatazwa jambo hili!” Akasema: “Wa-Allaahi siteremshi!” Yule Bedui akasema: “Unaonaje kuhusu mtu anapenda watu na bado hajakutana nao?” Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: “Mtu atakuwa pamoja na ampendae siku ya Qiyaamah.” Basi akaendelea kutuzungumzia mpaka akautaja mlango upande wa magharibi mwendo wa upana wake au atasafiri mpandaji kwa upana huu miaka miaka arobaini au sabini. Akasema Sufyaan mmoja wa wapokezi: “Upande wa Shamu. Allaah Aliuumba tokea siku Aliyoumba mbingu na ardhi hali ya kuwa umefunguliwa kwa ajili ya tawbah, haufungwi mpaka jua lichomoze upande huo.” [At-Tirmidhiy na wengineo, na akasema: Hadiyth hii ni Hasan Swahiyh]





Hadiyth – 8



وعن أبي سَعيد سَعْدِ بنِ مالكِ بنِ سِنَانٍ الخدريِّ رضي الله عنه أنّ نَبِيَّ الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((كَانَ فِيمَنْ كَانَ قَبْلَكمْ رَجُلٌ قَتَلَ تِسْعَةً وتِسْعينَ نَفْسًا، فَسَأَلَ عَنْ أعْلَمِ أَهْلِ الأرضِ، فَدُلَّ عَلَى رَاهِبٍ، فَأَتَاهُ. فقال: إنَّهُ قَتَلَ تِسعَةً وتِسْعِينَ نَفْسًا فَهَلْ لَهُ مِنْ تَوبَةٍ؟ فقالَ: لا، فَقَتَلهُ فَكَمَّلَ بهِ مائَةً، ثُمَّ سَأَلَ عَنْ أَعْلَمِ أَهْلِ الأَرضِ، فَدُلَّ عَلَى رَجُلٍ عَالِمٍ. فقَالَ: إِنَّهُ قَتَلَ مِائَةَ نَفْسٍ فَهَلْ لَهُ مِنْ تَوْبَةٍ؟ فقالَ: نَعَمْ، ومَنْ يَحُولُ بَيْنَهُ وبَيْنَ التَّوْبَةِ؟ انْطَلِقْ إِلى أرضِ كَذَا وكَذَا فإِنَّ بِهَا أُناسًا يَعْبُدُونَ الله تَعَالَى فاعْبُدِ الله مَعَهُمْ، ولا تَرْجِعْ إِلى أَرْضِكَ فَإِنَّهَا أرضُ سُوءٍ، فانْطَلَقَ حَتَّى إِذَا نَصَفَ الطَّرِيقَ أَتَاهُ الْمَوْتُ، فاخْتَصَمَتْ فِيهِ مَلائِكَةُ الرَّحْمَةِ ومَلائِكَةُ العَذَابِ. فَقَالتْ مَلائِكَةُ الرَّحْمَةِ: جَاءَ تَائِبًا، مُقْبِلًا بِقَلبِهِ إِلى اللهِ تَعَالَى، وقالتْ مَلائِكَةُ العَذَابِ: إنَّهُ لمْ يَعْمَلْ خَيرًا قَطُّ، فَأَتَاهُمْ مَلَكٌ في صورَةِ آدَمِيٍّ فَجَعَلُوهُ بَيْنَهُمْ- أيْ حَكَمًا- فقالَ: قِيسُوا ما بينَ الأرضَينِ فَإلَى أيّتهما كَانَ أدنَى فَهُوَ لَهُ. فَقَاسُوا فَوَجَدُوهُ أدْنى إِلى الأرْضِ التي أرَادَ، فَقَبَضَتْهُ مَلائِكَةُ الرَّحمةِ)). مُتَّفَقٌ عليه

وفي رواية في الصحيح: ((فَكَانَ إلى القَريَةِ الصَّالِحَةِ أقْرَبَ بِشِبْرٍ فَجُعِلَ مِنْ أهلِهَا))

Abuu Sa’iyd bin Maalik bin Sinaan Al-Khudriyy (Radhiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kulikuwepo mtu kabla yenu aliua watu tisini na tisa (99) akaulizia aliye mjuzi zaidi katika watu katika nchi ile. Akajulishwa mtawa (miongoni mwa Bani Israaiyl). Akamwendea, akamuuliza: “Nimeua watu tisini na tisa, je, nina tawbah?” Akamjibu: “Hapana!” Akamuua, akawa mtu wa mia. Kisha akauuliza mjuzi zaidi katika watu katika nchi ile. Akafahamishwa kuhusu Mwanachuoni. Akamuuliza: “Nimeua watu mia. Je, nina tawbah?” Akamjibu: “Ndio, ni nani atakayezuia baina yako na tawbah? Nenda katika nchi fulani, huko kuna watu wanaomuabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) basi nenda ukamuabudu Allaah pamoja nao wala usirejee katika nchi yako, kwani hiyo ni nchi ya maovu.” Akaenda, hata alipofika nusu ya njia, alifikwa na mauti. Malaika wa rahmah wakaanza kuvutana na Malaika wa adhabu. Malaika wa rahmah wakasema: “Alikuja hali ya kutubia na ameelekea moyo wake kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).” Malaika wa adhabu wakasema: “Yeye hakutenda khayr katu!” Akaja Malaika (mwengine) katika sura ya mwana Aadam, wakamfanya ndiye hakimu baina yao. Akawaambia: “Pimeni baina ya nchi mbili, katika nchi yoyote iliyopo karibu naye, atakuwa ni wa huko.” Wakapima, wakamkuta kuwa yupo karibu zaidi na nchi anayokusudia kwenda. Malaika wa rahmah wakamchukua.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

Riwaayah nyingine ya Swahiyh Al-Bukhaariy, imesema: “Akawa katika kijiji cha watu wema yu karibu nacho kwa shubiri moja. Akajaaliwa ni wa huko.”

Riwaayah nyingine ya Swahiyh Al-Bukhaariy, imesema: “Allaah Akakiambia kijiji alichotoka: “Kuwa mbali!” na kijiji anachoenda: “Kuwa karibu!” Na Akawaambia pimeni baina yake.” Wakampata kuwa yupo karibu zaidi ya kijiji anachokwenda kwa shubiri moja; akasamehewa.”

Riwaayah nyingine inasema: “Akakaribia kwa kifua chake upande ule.”





Hadiyth – 9



وعن عبدِ الله بن كعبِ بنِ مالكٍ، وكان قائِدَ كعبٍ رضي الله عنه مِنْ بَنِيهِ حِينَ عمِيَ، قَالَ: سَمِعتُ كَعْبَ بنَ مالكٍ رضي الله عنه يُحَدِّثُ بحَديثهِ حينَ تَخلَّفَ عن رسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم في غَزْوَةِ تَبُوكَ. قَالَ كعبٌ: لَمْ أتَخَلَّفْ عَنْ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم في غَزْوَةٍ غزاها قط إلا في غزوة تَبُوكَ، غَيْرَ أنّي قَدْ تَخَلَّفْتُ في غَزْوَةِ بَدْرٍ، ولَمْ يُعَاتَبْ أَحَدٌ تَخَلَّفَ عَنْهُ؛ إِنَّمَا خَرَجَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم والمُسْلِمُونَ يُريدُونَ عِيرَ قُرَيْشٍ حَتَّى جَمَعَ الله تَعَالَى بَيْنَهُمْ وبَيْنَ عَدُوِّهمْ عَلَى غَيْر ميعادٍ. ولَقَدْ شَهِدْتُ مَعَ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم لَيلَةَ العَقَبَةِ حينَ تَوَاثَقْنَا عَلَى الإِسْلامِ، وما أُحِبُّ أنَّ لي بِهَا مَشْهَدَ بَدْرٍ، وإنْ كَانَتْ بدرٌ أذْكَرَ في النَّاسِ مِنْهَا. وكانَ مِنْ خَبَري حينَ تَخَلَّفْتُ عَنْ رسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم في غَزْوَةِ تَبُوكَ أنِّي لم أكُنْ قَطُّ أَقْوى ولا أَيْسَرَ مِنِّي حِينَ تَخَلَّفْتُ عنْهُ في تِلكَ الغَزْوَةِ، وَالله ما جَمَعْتُ قَبْلَهَا رَاحِلَتَيْنِ قَطُّ حَتَّى جَمَعْتُهُمَا في تِلْكَ الغَزْوَةِ وَلَمْ يَكُنْ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يُريدُ غَزْوَةً إلا وَرَّى بِغَيرِها حَتَّى كَانَتْ تلْكَ الغَزْوَةُ، فَغَزَاها رسولُ الله صلى الله عليه وسلم في حَرٍّ شَديدٍ، واسْتَقْبَلَ سَفَرًا بَعِيدًا وَمَفَازًا، وَاستَقْبَلَ عَدَدًا كَثِيرًا، فَجَلَّى للْمُسْلِمينَ أمْرَهُمْ ليتَأهَّبُوا أُهْبَةَ غَزْوِهمْ فأَخْبرَهُمْ بوَجْهِهِمُ الَّذِي يُريدُ، والمُسلِمونَ مَعَ رسولِ الله كثيرٌ وَلا يَجْمَعُهُمْ كِتَابٌ حَافِظٌ (يُريدُ بذلِكَ الدّيوَانَ) قَالَ كَعْبٌ: فَقَلَّ رَجُلٌ يُريدُ أنْ يَتَغَيَّبَ إلا ظَنَّ أنَّ ذلِكَ سيخْفَى بِهِ ما لَمْ يَنْزِلْ فِيهِ وَحْيٌ مِنَ الله، وَغَزا رَسُول الله صلى الله عليه وسلم تِلْكَ الغَزوَةَ حِينَ طَابَت الثِّمَارُ وَالظِّلالُ، فَأنَا إلَيْهَا أصْعَرُ، فَتَجَهَّزَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم وَالمُسْلِمُونَ مَعَهُ وطَفِقْتُ أغْدُو لكَيْ أتَجَهَّزَ مَعَهُ، فأرْجِعُ وَلَمْ أقْضِ شَيْئًا، وأقُولُ في نفسي: أنَا قَادرٌ عَلَى ذلِكَ إِذَا أَرَدْتُ، فَلَمْ يَزَلْ يَتَمادى بي حَتَّى اسْتَمَرَّ بالنَّاسِ الْجِدُّ، فأصْبَحَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم غَاديًا والمُسْلِمُونَ مَعَهُ وَلَمْ أقْضِ مِنْ جِهَازي شَيْئًا، ثُمَّ غَدَوْتُ فَرَجَعْتُ وَلَمْ أقْضِ شَيئًا، فَلَمْ يَزَلْ يَتَمَادَى بي حَتَّى أسْرَعُوا وتَفَارَطَ الغَزْوُ، فَهَمَمْتُ أنْ أرْتَحِلَ فَأُدْرِكَهُمْ، فَيَا لَيْتَني فَعَلْتُ، ثُمَّ لم يُقَدَّرْ ذلِكَ لي، فَطَفِقْتُ إذَا خَرَجْتُ في النَّاسِ بَعْدَ خُرُوجِ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَحْزُنُنِي أنِّي لا أرَى لي أُسْوَةً، إلا رَجُلًا مَغْمُوصًا عَلَيْهِ في النِّفَاقِ، أوْ رَجُلًا مِمَّنْ عَذَرَ اللهُ تَعَالَى مِنَ الضُّعَفَاءِ، وَلَمْ يَذْكُرْنِي رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم حَتَّى بَلَغَ تَبُوكَ، فَقَالَ وَهُوَ جَالِسٌ في القَوْمِ بِتَبُوكَ: ((ما فَعَلَ كَعْبُ بْنُ مَالِكٍ؟)) فَقَالَ رَجُلٌ مِنْ بَنِي سَلِمَةَ: يا رَسُولَ اللهِ، حَبَسَهُ بُرْدَاهُ والنَّظَرُ في عِطْفَيْهِ. فَقَالَ لَهُ مُعَاذُ بْنُ جَبَلٍ رضي الله عنه: بِئْسَ مَا قُلْتَ! واللهِ يا رَسُولَ اللهِ مَا عَلِمْنَا عَلَيْهِ إلا خَيْرًا، فَسَكَتَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم. فَبَيْنَا هُوَ عَلى ذَلِكَ رَأى رَجُلًا مُبْيِضًا يَزُولُ بِهِ السَّرَابُ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم: ((كُنْ أَبَا خَيْثَمَةَ))، فَإذَا هُوَ أبُو خَيْثَمَةَ الأنْصَارِيُّ وَهُوَ الَّذِي تَصَدَّقَ بِصَاعِ التَّمْرِ حِيْنَ لَمَزَهُ المُنَافِقُونَ.
قَالَ كَعْبٌ: فَلَمَّا بَلَغَنِي أنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَدْ تَوَجَّهَ قَافِلًا مِنْ تَبُوكَ حَضَرَنِي بَثِّي، فَطَفِقْتُ أتَذَكَّرُ الكَذِبَ وأقُولُ: بِمَ أخْرُجُ مِنْ سَخَطِهِ غَدًا؟ وأسْتَعِيْنُ عَلى ذَلِكَ بِكُلِّ ذِي رأْيٍ مِنْ أهْلِي، فَلَمَّا قِيْلَ: إنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قّدْ أظَلَّ قَادِمًا، زَاحَ عَنّي البَاطِلُ حَتَّى عَرَفْتُ أَنِّي لَنْ أَنْجُوَ مِنْهُ بِشَيءٍ أَبَدًا، فَأجْمَعْتُ صدْقَهُ وأَصْبَحَ رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم قَادِمًا، وَكَانَ إِذَا قَدِمَ مِنْ سَفَرٍ بَدَأَ بِالمَسْجِدِ فَرَكَعَ فِيهِ رَكْعَتَيْنِ ثُمَّ جَلَسَ لِلنَّاسِ، فَلَمَّا فَعَلَ ذلِكَ جَاءهُ المُخَلَّفُونَ يَعْتَذِرونَ إِلَيْه ويَحْلِفُونَ لَهُ، وَكَانُوا بِضْعًا وَثَمانينَ رَجُلًا، فَقَبِلَ مِنْهُمْ عَلانِيَتَهُمْ وَبَايَعَهُمْ واسْتَغْفَرَ لَهُمْ وَوَكَلَ سَرَائِرَهُمْ إِلى الله تَعَالَى، حَتَّى جِئْتُ، فَلَمَّا سَلَّمْتُ تَبَسَّمَ تَبَسُّمَ المُغْضَبِ. ثُمَّ قَالَ: ((تَعَالَ))، فَجِئْتُ أمْشي حَتَّى جَلَسْتُ بَيْنَ يَدَيْهِ، فقالَ لي: ((مَا خَلَّفَكَ؟ ألَمْ تَكُنْ قَدِ ابْتَعْتَ ظَهْرَكَ؟)) قَالَ: قُلْتُ: يَا رسولَ الله، إنّي والله لَوْ جَلَسْتُ عِنْدَ غَيْرِكَ مِنْ أهْلِ الدُّنْيَا لَرَأيتُ أنِّي سَأخْرُجُ مِنْ سَخَطِهِ بِعُذْرٍ؛ لقَدْ أُعْطِيتُ جَدَلًا، ولَكِنِّي والله لَقَدْ عَلِمْتُ لَئِنْ حَدَّثْتُكَ اليوم حَدِيثَ كَذبٍ تَرْضَى به عنِّي لَيُوشِكَنَّ الله أن يُسْخِطَكَ عَلَيَّ، وإنْ حَدَّثْتُكَ حَدِيثَ صِدقٍ تَجِدُ عَلَيَّ فِيهِ إنّي لأَرْجُو فِيهِ عُقْبَى الله- عز وجل، والله ما كَانَ لي مِنْ عُذْرٍ، واللهِ مَا كُنْتُ قَطُّ أَقْوَى وَلا أَيْسَرَ مِنِّي حِينَ تَخَلَّفْتُ عَنْكَ. قَالَ: فقالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((أمَّا هَذَا فقَدْ صَدَقَ، فَقُمْ حَتَّى يَقْضِيَ اللهُ فيكَ)). وَسَارَ رِجَالٌ مِنْ بَنِي سَلِمَة فاتَّبَعُوني فَقالُوا لِي: واللهِ مَا عَلِمْنَاكَ أذْنَبْتَ ذَنْبًا قَبْلَ هذَا لَقَدْ عَجَزْتَ في أنْ لا تَكونَ اعتَذَرْتَ إِلَى رَسُول الله صلى الله عليه وسلم بما اعْتَذَرَ إليهِ المُخَلَّفُونَ، فَقَدْ كَانَ كَافِيكَ ذَنْبَكَ اسْتِغْفَارُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم لَكَ. قَالَ: فَوالله ما زَالُوا يُؤَنِّبُونَنِي حَتَّى أَرَدْتُّ أَنْ أرْجعَ إِلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم فأُكَذِّبَ نَفْسِي، ثُمَّ قُلْتُ لَهُمْ: هَلْ لَقِيَ هذَا مَعِيَ مِنْ أَحَدٍ؟ قَالُوا: نَعَمْ، لَقِيَهُ مَعَكَ رَجُلانِ قَالا مِثْلَ مَا قُلْتَ، وَقيلَ لَهُمَا مِثْلَ مَا قيلَ لَكَ، قَالَ: قُلْتُ: مَنْ هُما؟ قَالُوا: مُرَارَةُ بْنُ الرَّبيع الْعَمْرِيُّ، وهِلاَلُ ابنُ أُمَيَّةَ الوَاقِفِيُّ؟ قَالَ: فَذَكَرُوا لِي رَجُلَينِ صَالِحَينِ قَدْ شَهِدَا بَدْرًا فيهِما أُسْوَةٌ، قَالَ: فَمَضَيْتُ حِينَ ذَكَرُوهُما لِي. ونَهَى رَسُول الله صلى الله عليه وسلم عَنْ كَلامِنا أيُّهَا الثَّلاثَةُ مِنْ بَيْنِ مَنْ تَخَلَّفَ عَنْهُ، فاجْتَنَبَنَا النَّاسُ- أوْ قَالَ: تَغَيَّرُوا لَنَا- حَتَّى تَنَكَّرَتْ لي في نَفْسي الأَرْض، فَمَا هِيَ بالأرْضِ الَّتي أعْرِفُ، فَلَبِثْنَا عَلَى ذلِكَ خَمْسِينَ لَيْلَةً. فَأمّا صَاحِبَايَ فَاسْتَكَانا وقَعَدَا في بُيُوتِهِمَا يَبْكيَان. وأمَّا أنَا فَكُنْتُ أشَبَّ الْقَومِ وأجْلَدَهُمْ فَكُنْتُ أخْرُجُ فَأشْهَدُ الصَّلاَةَ مَعَ المُسْلِمِينَ، وأطُوفُ في الأَسْوَاقِ وَلا يُكَلِّمُنِي أَحَدٌ، وَآتِي رسولَ الله صلى الله عليه وسلم فأُسَلِّمُ عَلَيْهِ وَهُوَ في مَجْلِسِهِ بَعْدَ الصَّلاةِ، فَأَقُولُ في نَفسِي: هَلْ حَرَّكَ شَفَتَيْه برَدِّ السَّلام أَمْ لا؟ ثُمَّ أُصَلِّي قَريبًا مِنْهُ وَأُسَارِقُهُ النَّظَرَ، فَإِذَا أقْبَلْتُ عَلَى صَلاتِي نَظَرَ إلَيَّ وَإِذَا الْتَفَتُّ نَحْوَهُ أعْرَضَ عَنِّي، حَتَّى إِذَا طَال ذلِكَ عَلَيَّ مِنْ جَفْوَةِ المُسْلِمينَ مَشَيْتُ حَتَّى تَسَوَّرْتُ جِدارَ حائِط أبي قَتَادَةَ وَهُوَ ابْنُ عَمِّي وأَحَبُّ النَّاس إِلَيَّ، فَسَلَّمْتُ عَلَيهِ فَوَاللهِ مَا رَدَّ عَليَّ السَّلامَ، فَقُلْتُ لَهُ: يَا أَبَا قَتَادَةَ، أنْشُدُكَ بالله هَلْ تَعْلَمُنِي أُحِبُّ الله وَرَسُولَهُ صلى الله عليه وسلم؟ فَسَكَتَ، فَعُدْتُ فَنَاشَدْتُهُ فَسَكَتَ، فَعُدْتُ فَنَاشَدْتُهُ، فَقَالَ: اللهُ ورَسُولُهُ أَعْلَمُ. فَفَاضَتْ عَيْنَايَ، وَتَوَلَّيْتُ حَتَّى تَسَوَّرْتُ الجِدَارَ، فَبَيْنَا أَنَا أمْشِي في سُوقِ الْمَدِينة إِذَا نَبَطِيٌّ مِنْ نَبَطِ أهْلِ الشَّام مِمّنْ قَدِمَ بالطَّعَامِ يَبيعُهُ بِالمَدِينَةِ يَقُولُ: مَنْ يَدُلُّ عَلَى كَعْبِ بْنِ مَالِكٍ؟ فَطَفِقَ النَّاسُ يُشِيرُونَ لَهُ إلَيَّ حَتَّى جَاءنِي فَدَفَعَ إِلَيَّ كِتَابًا مِنْ مَلِكِ غَسَّانَ، وَكُنْتُ كَاتبًا. فَقَرَأْتُهُ فإِذَا فِيهِ: أَمَّا بَعْدُ، فإِنَّهُ قَدْ بَلَغَنا أنَّ صَاحِبَكَ قَدْ جَفَاكَ وَلَمْ يَجْعَلْكَ اللهُ بدَارِ هَوانٍ وَلا مَضْيَعَةٍ، فَالْحَقْ بنَا نُوَاسِكَ، فَقُلْتُ حِينَ قَرَأْتُهَا: وَهَذِهِ أَيضًا مِنَ البَلاءِ، فَتَيَمَّمْتُ بهَا التَّنُّورَ فَسَجَرْتُهَا، حَتَّى إِذَا مَضَتْ أَرْبَعُونَ مِنَ الْخَمْسينَ وَاسْتَلْبَثَ الْوَحْيُ إِذَا رسولُ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم يَأتِيني، فَقالَ: إنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يَأمُرُكَ أنْ تَعْتَزِلَ امْرَأتَكَ، فَقُلْتُ: أُطَلِّقُهَا أمْ مَاذَا أفْعَلُ؟ فَقالَ: لا، بَلِ اعْتَزِلْهَا فَلا تَقْرَبَنَّهَا، وَأَرْسَلَ إِلَى صَاحِبَيَّ بِمِثْلِ ذلِكَ. فَقُلْتُ لامْرَأتِي: الْحَقِي بِأهْلِكِ فَكُوني عِنْدَهُمْ حَتَّى يَقْضِيَ اللهُ في هَذَا الأمْرِ. فَجَاءتِ امْرَأةُ هِلاَلِ بْنِ أُمَيَّةَ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم فَقَالَتْ لَهُ: يَا رَسُولَ الله، إنَّ هِلاَلَ بْنَ أمَيَّةَ شَيْخٌ ضَائِعٌ لَيْسَ لَهُ خَادِمٌ، فَهَلْ تَكْرَهُ أنْ أخْدُمَهُ؟ قَالَ: ((لا، وَلَكِنْ لا يَقْرَبَنَّكِ)) فَقَالَتْ: إِنَّهُ واللهِ ما بِهِ مِنْ حَرَكَةٍ إِلَى شَيْءٍ، وَوَالله مَا زَالَ يَبْكِي مُنْذُ كَانَ مِنْ أمْرِهِ مَا كَانَ إِلَى يَومِهِ هَذَا. فَقَالَ لي بَعْضُ أهْلِي: لَو اسْتَأْذَنْتَ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم في امْرَأَتِكَ فَقَدْ أَذِن لاِمْرَأةِ هلاَل بْنِ أمَيَّةَ أنْ تَخْدُمَهُ؟ فَقُلْتُ: لا أسْتَأذِنُ فيها رسولَ الله صلى الله عليه وسلم وَمَا يُدْرِيني مَاذَا يقُول رسولُ الله صلى الله عليه وسلم إِذَا اسْتَأْذَنْتُهُ، وَأَنَا رَجُلٌ شَابٌ! فَلَبِثْتُ بِذَلِكَ عَشْرَ لَيَالٍ فَكَمُلَ لَنا خَمْسُونَ لَيْلَةً مِنْ حِينَ نُهِيَ عَنْ كَلاَمِنا، ثُمَّ صَلَّيْتُ صَلاَةَ الْفَجْرِ صَبَاحَ خَمْسِينَ لَيْلَةً عَلَى ظَهْرِ بَيْتٍ مِنْ بُيُوتِنَا، فَبَيْنَا أَنَا جَالِسٌ عَلَى الْحالِ الَّتي ذَكَرَ الله تَعَالَى مِنَّا، قَدْ ضَاقَتْ عَلَيَّ نَفْسي وَضَاقَتْ عَلَيَّ الأرْضُ بِمَا رَحُبَتْ، سَمِعْتُ صَوْتَ صَارِخٍ أوفَى عَلَى سَلْعٍ يَقُولُ بِأعْلَى صَوتِهِ: يَا كَعْبَ بْنَ مَالِكٍ أبْشِرْ، فَخَرَرْتُ سَاجِدًا، وَعَرَفْتُ أنَّهُ قَدْ جَاءَ فَرَجٌ. فآذَنَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم النَّاسَ بِتَوْبَةِ الله عز وجل عَلَيْنَا حِينَ صَلَّى صَلاةَ الفَجْر فَذَهَبَ النَّاسُ يُبَشِّرُونَنَا، فَذَهَبَ قِبَلَ صَاحِبَيَّ مُبَشِّرونَ وَرَكَضَ رَجُلٌ إِلَيَّ فَرَسًا وَسَعَى سَاعٍ مِنْ أسْلَمَ قِبَلِي، وَأَوْفَى عَلَى الْجَبَلِ، فَكانَ الصَّوْتُ أسْرَعَ مِنَ الفَرَسِ، فَلَمَّا جَاءني الَّذِي سَمِعْتُ صَوْتَهُ يُبَشِّرُني نَزَعْتُ لَهُ ثَوْبَيَّ فَكَسَوْتُهُمَا إيَّاهُ بِبشارته، وَاللهِ مَا أمْلِكُ غَيْرَهُمَا يَوْمَئِذٍ، وَاسْتَعَرْتُ ثَوْبَيْنِ فَلَبسْتُهُما، وَانْطَلَقْتُ أتَأمَّمُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يَتَلَقَّاني النَّاسُ فَوْجًا فَوْجًا يُهنِّئونَني بالتَّوْبَةِ وَيَقُولُونَ لِي: لِتَهْنِكَ تَوْبَةُ الله عَلَيْكَ. حَتَّى دَخَلْتُ الْمَسْجِدَ فَإِذَا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم جَالِسٌ حَوْلَه النَّاسُ، فَقَامَ طَلْحَةُ بْنُ عُبَيْدِ اللهِ رضي الله عنه يُهَرْوِلُ حَتَّى صَافَحَني وَهَنَّأَنِي، والله مَا قَامَ رَجُلٌ مِنَ المُهَاجِرينَ غَيرُهُ- فَكَانَ كَعْبٌ لا يَنْسَاهَا لِطَلْحَةَ.
قَالَ كَعْبٌ: فَلَمَّا سَلَّمْتُ عَلَى رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم قَالَ وَهُوَ يَبْرُقُ وَجْهُهُ مِنَ السُّرُور: ((أبْشِرْ بِخَيْرِ يَومٍ مَرَّ عَلَيْكَ مُذْ وَلَدَتْكَ أُمُّكَ)) فَقُلْتُ: أمِنْ عِنْدِكَ يَا رَسُول الله أَمْ مِنْ عِندِ الله؟ قَالَ: ((لا، بَلْ مِنْ عِنْدِ الله- عز وجل))، وَكَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم إِذَا سُرَّ اسْتَنَارَ وَجْهُهُ حَتَّى كَأَنَّ وَجْهَهُ قِطْعَةُ قَمَرٍ وَكُنَّا نَعْرِفُ ذلِكَ مِنْهُ، فَلَمَّا جَلَسْتُ بَيْنَ يَدَيْهِ قُلْتُ: يَا رسولَ الله، إنَّ مِنْ تَوْبَتِي أنْ أنْخَلِعَ مِنْ مَالِي صَدَقَةً إِلَى اللهِ وَإِلَى رَسُولهِ. فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((أَمْسِكَ عَلَيْكَ بَعْضَ مَالِكَ فَهُوَ خَيْرٌ لَكَ)). فقلتُ: إِنِّي أُمْسِكُ سَهْمِي الَّذِي بِخَيبَر. وَقُلْتُ: يَا رسولَ الله، إنَّ الله تَعَالَى إِنَّمَا أنْجَانِي بالصِّدْقِ، وإنَّ مِنْ تَوْبَتِي أنْ لا أُحَدِّثَ إلا صِدْقًا مَا بَقِيتُ، فوَالله مَا عَلِمْتُ أَحَدًا مِنَ المُسْلِمينَ أبْلاهُ الله تَعَالَى في صِدْقِ الحَدِيثِ مُنْذُ ذَكَرْتُ ذلِكَ لِرسولِ الله صلى الله عليه وسلم أحْسَنَ مِمَّا أبْلانِي الله تَعَالَى، واللهِ مَا تَعَمَّدْتُ كِذْبَةً مُنْذُ قُلْتُ ذلِكَ لِرسولِ الله صلى الله عليه وسلم إِلَى يَومِيَ هَذَا، وإنِّي لأرْجُو أنْ يَحْفَظَنِي الله تَعَالَى فيما بَقِيَ، قَالَ: فأَنْزَلَ الله تَعَالَى: {لَقَدْ تَابَ اللهُ عَلَى النَّبِيِّ وَالْمُهَاجِرِينَ وَالأَنْصَارِ الَّذِينَ اتَّبَعُوهُ فِي سَاعَةِ الْعُسْرَةِ} حَتَّى بَلَغَ: {إِنَّهُ بِهِمْ رَؤُوفٌ رَحِيم وَعَلَى الثَّلاثَةِ الَّذِينَ خُلِّفُوا حَتَّى إِذَا ضَاقَتْ عَلَيْهِمُ الأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ} حَتَّى بَلَغَ: {اتَّقُوا اللهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ} [التوبة: 117: 119] قَالَ كَعْبٌ: واللهِ ما أنْعَمَ الله عَليَّ مِنْ نعمةٍ قَطُّ بَعْدَ إذْ هَدَاني اللهُ للإِسْلامِ أَعْظَمَ في نَفْسِي مِنْ صِدقِي رسولَ الله صلى الله عليه وسلم أنْ لا أكونَ كَذَبْتُهُ، فَأَهْلِكَ كما هَلَكَ الَّذينَ كَذَبُوا؛ إنَّ الله تَعَالَى قَالَ للَّذِينَ كَذَبُوا حِينَ أنْزَلَ الوَحْيَ شَرَّ مَا قَالَ لأَحَدٍ، فقال الله تَعَالَى: {سَيَحْلِفُونَ بِاللهِ لَكُمْ إِذَا انْقَلَبْتُمْ إِلَيْهِمْ لِتُعْرِضُوا عَنْهُمْ فَأَعْرِضُوا عَنْهُمْ إِنَّهُمْ رِجْسٌ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ يَحْلِفُونَ لَكُمْ لِتَرْضَوْا عَنْهُمْ فَإِنْ تَرْضَوْا عَنْهُمْ فَإِنَّ اللهَ لا يَرْضَى عَنِ الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ} [التوبة: 95، 96]
قَالَ كَعْبٌ: كُنّا خُلّفْنَا أيُّهَا الثَّلاَثَةُ عَنْ أمْرِ أُولئكَ الذينَ قَبِلَ مِنْهُمْ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم حِينَ حَلَفُوا لَهُ فَبَايَعَهُمْ وَاسْتَغْفَرَ لَهُمْ وأرجَأَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم أمْرَنَا حَتَّى قَضَى الله تَعَالَى فِيهِ بذِلكَ. قَالَ الله تَعَالَى: {وَعَلَى الثَّلاثَةِ الَّذِينَ خُلِّفُوا} وَليْسَ الَّذِي ذَكَرَ مِمَّا خُلِّفْنَا تَخلُّفُنَا عن الغَزْو، وإنَّمَا هُوَ تَخْلِيفُهُ إيّانا وإرْجَاؤُهُ أمْرَنَا عَمَّنْ حَلَفَ لَهُ واعْتَذَرَ إِلَيْهِ فقبِلَ مِنْهُ. مُتَّفَقٌ عليه
وفي رواية: أنَّ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم خَرَجَ في غَزْوَةِ تَبْوكَ يَومَ الخَميسِ وكانَ يُحِبُّ أنْ يخْرُجَ يومَ الخمِيس
وفي رواية: وكانَ لا يقْدمُ مِنْ سَفَرٍ إلا نَهَارًا في الضُّحَى، فإِذَا قَدِمَ بَدَأَ بالمَسْجِدِ فَصَلَّى فِيهِ رَكْعَتَيْنِ ثُمَّ جَلَسَ فِيهِ

'Abdullaah bin Ka’b bin Maalik alikuwa miongoni mwa watoto wake anamuongoza Ka’b (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alipokuwa kipofu; amesema: “Nilimsikia Ka’b bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akihadithia kisa chake alipobaki nyuma ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika vita vya Tabuwk; Ka’b ameeleza: “Sijawahi kamwe kubaki nyuma ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika vita vovote alivyopigana ila katika vita vya Tabuwk. Sikushiriki vita vya Badr. Hakulaumiwa yeyote yote aliyebaki nyuma. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka pamoja na Waislamu wakiukusudia msafara wa Maquraysh hadi Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Aliwakutanisha na adui zao bila ya maagano. Nilishuhudia pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) usiku wa ‘Aqabah wakati tulipoandikiana mkataba juu ya Uislamu. Sipendelei kulinganisha hayo na vita vya Badr japokuwa Badr vinatajwa zaidi kuliko ‘Aqabah.



Ama khabari yangu kuhusu vita hivi vya Tabuwk ni pale nilipobaki nyuma ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nami sijapatapo kuwa ni mwenye nguvu na pesa kama nilipobakia nyuma katika vita hivi. Wa-Allaahi sijawahi kuwa na ngamia wawili katu kabla ya hapo isipokuwa wakati wa vita hivyo. Alipokuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anataka kupigana vita alikuwa anaficha niyyah yake kwa kutaja vita vingine mpaka ilipofikia vita hivyo ambavyo alipigana katika siku za joto kali na akaelekea kwenye safari ya mbali na bara refu lenye maji kidogo. Akawapokea watu wengi, akawabainishia wazi Waislamu jambo lao (sehemu wanayokwenda) ili wajiandae kwa maandalizi ya vita hivyo. Akawaeleza sehemu anayoikusudia. Wakati huo Waislamu walikuwa wengi pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wala hakuna kitabu kinachoweza kuwajumuisha (yaani kitabu cha majina yao). Yeyote anayetaka kutoroka angelidhani kuwa anaweza kufanya hivyo madamu Wahyi haujateremka kutoka kwa Allaah. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akapigana vita hivyo wakati matunda yalipokuwa tayari (msimu wa mavuno), nami nilikuwa nikiyapendelea (mazao). Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akajiandaa pamoja na Maswahaba zake, na nikawa nimepambaukiwa ili kujitayarisha pamoja naye.

Nikarudi wala sikufanya chochote, nikajiambia: “Naweza kufanya hivyo.” Hivyo nikawa najichelewesha mpaka Waislamu wakawa tayari na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakaondoka nami sijajitayarisha chochote. Asubuhi baada ya kuwa wao wameondoka nilitoka ili kujitayarisha lakini nilirudi bila ya kufanya chochote. Kisha pia asubuhi ya pili yake nilitoka na kurudi bila kufanya chochote. Hivyo ndivyo hali yangu mpaka wakawa wametoka na nikakosa hivyo vita. Hata hivyo nilitia niyyah kuondoka na kuwapata njiani; natamani kuwa ningefanya hivyo! Nikawa kila ninapotoka nje kutembea kati ya watu waliobaki ilinihuzunisha kuwa sikumuona mtu isipokuwa aliyetuhumiwa kwa unafiki au mtu dhaifu aliyepewa udhuru na Allaah.

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakunikumbuka mpaka alipofika Tabuwk. Akasema akiwa amekaa na watu huko: “Ka’b bin Maalik amefikwa na nini?” Mtu mmoja katika kabila la Banu Salamah akasema: “Ee Rasuli wa Allaah, amezuiliwa kutazama nguo zake (yaani: anajiona).” Mu’aadh bin Jabal (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akamwambia: “Umesema jambo baya! Wa-Allaahi ee Rasuli wa Allaah, hatumjui ila kwa khayr tu.” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akanyamaza. Alipokuwa yupo katika hali hiyo, alimuona mtu aliyevaa nguo nyeupe akipeperushwa na sarabi. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Kuwa Abuu Khaythamah.” Akawa ndiye Abuu Khaythamah Al-Answaariyy, naye ndiye aliyetoa swadaqah pishi la tende pale wanafiki walipombeza.

Nilipopata khabari kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameelekea kuanza kurudi kutoka Tabuwk, nilijiwa na huzuni, nikawa nawaza niseme uongo, nikasema: “Vipi kesho nitaweza kuepuka na ghadhabu Zake Allaah?” Nikawa nikiomba usaidizi kwa jambo hilo kwa kila mwenye maoni miongoni mwa jamaa zangu. Nilipoambiwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameshakaribia kufika, uongo uliniondokea hata nikawa najua siwezi kumuepuka kwa lolote kabisa. Nikaamua kumueleza ukweli.

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaporejea safari yoyote, huanza kuteremkia Masjid kuswali rakaa mbili kisha huketi na watu. Alipofanya hivyo alijiwa na wale watu waliorudi nyuma wakimtolea nyudhuru na wakimuapia. Walikuwa ni watu zaidi ya themanini. Akawakubalia nyudhuru zao, akachukua bay'ah (kiapo cha utiifu), akawaombea maghfirah na siri zao akamuachia Allaah (Subhaanhu wa Ta’aalaa).

Nikaja mimi, nikamtolea salaam akatabasamu, tabasamu ya mtu aliyekasirishwa, akaniambia: “Njoo.” Nikaenda mpaka nikakaa kitako mbele yake. Akaniuliza: “Ni jambo gani lililokubakisha nyuma? Hukuwa umenunua ngamia?” Nikamwambia: “Ee Rasuli wa Allaah, Wa-Allaahi mimi lau ningalikuwa niko mbele ya mtu mwengine asiyekuwa wewe katika watu wa kidunia, ningaliona naweza kuepuka hasira zake kwa udhuru. Hakika nimepewa ufasaha na nguvu ya kusema, Lakini Wa-Allaahi najua kuwa iwapo nitakuzungumzia uongo leo utakaoniridhia, itakaribia Allaah Akutie hasira juu yangu. Na nikizungumza mazungumzo ya kweli, utanikasirikia. Mimi nataraji mwisho mwema wa Allaah ‘Azza wa Jallaa. Wa-Allaahi sikuwa nina udhuru. Wa-Allaahi, nilikuwa nina nguvu na wepesi nilipobakia nyuma!” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Ama huyu amesema kweli. Nenda mpaka Allaah Atakapokuhukumu.”



Watu katika kabila la Banu Salamah wakanifuata, wakanambia: “Wa-Allaahi hatukujui kama umeshawahi kufanya kosa kabla ya hili. Umeshindwa kutoa udhuru kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama walivyotoa wale wengine waliokuwa wamebaki nyuma? Dhambi yako ingalifutwa na istighfaar na du’aa ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) “Basi Wa-Allaahi, hawakuacha kunilaumu mpaka nikataka kumrudia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ili nijikadhibishe. Kisha nikawauliza: “Kuna yeyote aliyemkabili na jambo kama langu?” Wakajibu: “Ndio, watu wawili walimkabili wakasema mithli ya ulivyosema, wakaambiwa kama ulivyoambiwa.” Nikauliza: “Ni nani hao?” Wakajibu: “Muraarah bin Rabiy’ Al-‘Amriy na Hilaal bin Umayyah Al-Waaqify.” Wakanitajia watu wawili wema waliohudhuria vita vya Badr wenye kiigizo. Waliponitajia hao, nikaenda zangu.

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawakataza watu kuzungumza nasi watu watatu pekee miongoni mwa watu waliobaki nyuma. Watu wakatuepuka, au wakatubadilikia mpaka ardhi nikaiona moyoni mwangu imebadilika, si ardhi niijuayo! Tukawa katika hali hiyo masiku khamsini. Ama wale wenzangu wawili, walikuwa wametulia kwa unyenyekevu majumbani mwao wakilia tu. Lakini mimi nilikuwa kijana na mwenye nguvu. Nikawa nikitoka nikihudhuria Swalaah (za jamaa’ah) pamoja na Waislamu wengine, nilitembea masokoni wala hakuna yoyote anayenizungumzisha. Nikamuendea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nikamtolea salaam naye yupo katika majlis yake baada ya kuswali; nikajiuliza moyoni mwangu: “Ameitikia midomo yake kwa kuirejesha salaam?” Kisha nikaswali karibu yake naye nikimtazama kwa kuibia, nikielekea katika Swalaah yangu naye hunitazama, nikielekea upande wake hugeuka.

Jambo hilo likarefuka kwangu kutokana na Waislamu kujitenga. Nikauparamia ukuta wa bustani ya Abuu Qataadah naye ni bin 'ammi yangu na ni kipenzi zaidi kwangu; nikamsalimia; basi wa-Allaahi hakunirejeshea salaam. Nikamwambia: “Ee Abuu Qataadah, nakuomba kwa jina la Allaah, je, unajua kuwa mimi nampemda Allaah na Rasuli Wake?” Akanyamaza, nikarejea tena nikamuomba akanyamaza. Nikarejea tena nikamuomba, akasema: “Allaah na Rasuli Wake Wanajua Zaidi.” Macho yangu yakabubujika machozi, nikaenda na kuuparamia ukuta.

Nilipokuwa natembea katika soko la Madiynah, nikamuona mkulima kutoka Shaam aliyekuja kuuza nafaka Madiynah, akaniuliza: “Ni nani atakayenionesha Ka’b bin Maalik?” Watu wakawa wanamuelekeza kwangu, akanijia na kunipatia barua inayotoka kwa mfalme Ghassaan, nami nilikuwa nikijua kusoma na kuandika. Nikaisoma ilikuwa imeandikwa: “Ama baada ya haya. Tumepata habari kuwa mwenzako amekuepuka, wala Allaah hajakujaalia kuwa katika nchi ya unyonge wala haki yako kupotea. Njoo kwetu tutakunafisi.” Nilipomaliza kuisoma, nilisema: “ Hii ni balaa nyingine!” Nikaichukua barua nikaitia katika tanuri na nikaichoma.

Zikapita siku arubaini kati ya zile siku khamsini, wahyi ukachelewa. Mara kwa ghafla mjumbe wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akanijia, akaniambia: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anakuambia umuepuke mkeo.” Nikauliza: “Nimtaliki au nifanyeje?” Akaniambia: “Hapana, kuwa mbali naye wala usimkurubie kabisa.” Akawatumia wenzangu kama hivyo. Nikamwambia mke wangu: “Nenda kwa jamaa zako uwe huko mpaka Allaah Atakapotoa hukumu katika jambo hili.” Mke wa Hilaal bin Umayyah akamwendea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: “Ee Rasuli wa Allaah, hakika Hilaal bin Umayyah ni mzee dhaifu na hana mtumishi, je, utachukia nikimhudumia?” Akajibu: “Hapana, lakini asijaribu kukukurubia.” Akasema: “Wa-Allaahi hawezi kutaharaki kukaribia chochote, na wa-Allaahi bado analia tokea yalipomtokea hadi leo hii!” Baadhi ya jamaa zangu wakaniambia: “Lau ungalimuomba udhuru Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu mkeo; kwani mke wa Hilaal bin Umayyah ameruhusiwa amhudumie. Nikasema: “Siwezi kumuomba idhini (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya mke wangu, nitajua lipi atakaloniambia (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwani mimi ni kijana!

Nikakaa kitako katika hali hiyo masiku kumi. Yakakamilika masiku khamsini tangu watu walipokatazwa nasi. Asubuhi ya kupambaukiwa siku ya khamsini, Niliswali Swalaah ya Alfajiri juu ya nyumba miongoni mwa majumba yetu. Nilipokuwa nimekaa kitako katika hali Aliyoitaja Allaah kutuhusu, nafsi yangu ikadhikika kwangu na ardhi ikawa dhiki kwangu ingawa ardhi hiyo ni kunjufu, nikaisikia sauti ya ukelele kutoka katika jabali la Sal’i, mtu akisema kwa sauti ya juu kabisa: “Ee Ka’b bin Maalik! Pokea bishara njema!” Nikaanguka kifudifudi kwa kusujudu, nikajua kuwa faraja imekuja. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kuswali Swalaah ya Alfajiri amewajulisha watu juu ya tawbah yetu kwa Allaah (‘Azza wa Jallaa). Watu wakawa wakitupa bishara njema, watoaji biashara wakawaendea wenzangu wawili. Mtu mmoja akapanda farasi akanijia mbio, na mwengine katika kabila la Aslam aliyepanda juu ya jabali sauti yake ikanifikia haraka zaidi kulikoni yule mpanda farasi. Na aliponijia yule niliyemsikia sauti akinibashiria. Nilimvulia nguo zangu mbili na nikamvisha kwa sababu ya ile bishara yake. Wa-Allaahi siku hiyo nilikuwa sikumiliki isipokuwa nguo hizo tu. Nikaazima nguo mbili nikazivaa. Nikaondoka nikimkusudia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Nilipokuwa njiani, watu walikuwa wakikutana na mimi makundi kwa makundi wakinipa pongezi ya tawbah na wakiniambia: “Hongera kwa kupokelewa Tawbah na Allaah.”

Nilipoingia Masjid, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawa amekaa kitako kando yake kuna watu. Twalhah bin ‘Ubaydillaah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akainuka mbio kunipa mkono na kunipa pongezi. Wa-Allaahi hakuna yoyote katika Muhaajiriyn aliyeinuka isipokuwa ni yeye tu. Nikawa simsahau Twalhah kwa jambo hilo. Nilipomsalimia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema huku sura yake ikimeremeta kwa furaha: “Pokea bishara ya khayr siku iliyo bora toka uzaliwe.” Nikauliza: “Ni kutoka kwako ee Rasuli wa Allaah?” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akipatwa na furaha basi sura yake hung’aa kama kipande cha mwezi, jambo hilo tulikuwa tukilijua kwake. Nilipokaa kitako mbele yake, nilimwambia: “Ee Rasuli wa Allaah, kwa sababu ya kukubaliwa tawbah yangu nitatoa mali yangu yote kwa ajili ya Allaah na Rasuli Wake.” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaniambia: “Zuia baadhi ya mali yako, kwani hiyo ni khayr kwako.” Nikamwambia: “Mimi naizuia sehemu yangu iliopo Khaybar.” Na nikamwambia: “Ee Rasuli wa Allaah, hakika Allaah Ameniokoa kwa sababu ya ukweli wangu. Hivyo naahidi kuwa katika uhai wangu wote sitosema isipokuwa ukweli.”

Wa-Allaahi simjui yeyote kati ya Waislamu ambaye Allaah Alimsaidia kusema ukweli kuliko mimi. Wa-Allaahi sikusema uongo tangu nilipomwambia ukweli Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mpaka siku yangu hii leo. Nami nataraji Allaah Atanihifadhi kusema uongo maisha yangu yote. Allaah Akateremsha:

لَّقَد تَّابَ اللَّـهُ عَلَى النَّبِيِّ وَالْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ الَّذِينَ اتَّبَعُوهُ فِي سَاعَةِ الْعُسْرَةِ مِن بَعْدِ مَا كَادَ يَزِيغُ قُلُوبُ فَرِيقٍ مِّنْهُمْ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّهُ بِهِمْ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿١١٧﴾

Kwa yakini Allaah Amepokea tawbah ya Nabiy na Muhajirina na Answaar ambao wamemfuata (Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) katika saa ya dhiki (vita vya Tabuwk) baada ya nyoyo za kundi miongoni mwao zilikaribia kuelemea mbali na haki (Allaah) Akapokea tawbah yao. Hakika Yeye kwao ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu.



وَعَلَى الثَّلَاثَةِ الَّذِينَ خُلِّفُوا حَتَّىٰ إِذَا ضَاقَتْ عَلَيْهِمُ الْأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ وَضَاقَتْ عَلَيْهِمْ أَنفُسُهُمْ وَظَنُّوا أَن لَّا مَلْجَأَ مِنَ اللَّـهِ إِلَّا إِلَيْهِ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ لِيَتُوبُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ﴿١١٨﴾

Na (pia Allaah Akapokea tawbah) ya wale watatu waliobaki nyuma (kutokwenda vita vya Tabuwk; wakajuta mno) mpaka ardhi ikadhikika kwao juu ya kuwa ni pana na zikadhikika nafsi zao, na wakatambua kwamba hakuna pa kumkimbia Allaah isipokuwa (kuelekea) Kwake; kisha (Allaah) Akapokea tawbah yao, ili watubie. Hakika Allaah Yeye Ndiye Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu.



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ﴿١١٩﴾

Enyi walioamini! Mcheni Allaah na kuweni pamoja na wakweli. [At-Tawbah: 117- 119]

Wa-Allaahi Hakunineemesha neema yoyote katu baada ya kuniongoza katika Uislamu, neema iliyo kubwa moyoni mwangu kuliko kumwambia ukweli Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Lau ningesema uongo Angeniangamiza kama Alivyowaangamiza wale waliosema uongo. Hakika Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Amewaonya vibaya zaidi wasemao uongo kuliko yeyote; Akasema:

سَيَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ لَكُمْ إِذَا انقَلَبْتُمْ إِلَيْهِمْ لِتُعْرِضُوا عَنْهُمْ ۖ فَأَعْرِضُوا عَنْهُمْ ۖ إِنَّهُمْ رِجْسٌ ۖ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿٩٥﴾

Watakuapieni kwa Allaah, mtakaporudi kwao ili muwapuuze. Basi wapuuzeni; hakika wao ni rijs (uchafu) na makazi yao ni (Moto wa) Jahannam. Ni jazaa kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.

يَحْلِفُونَ لَكُمْ لِتَرْضَوْا عَنْهُمْ ۖ فَإِن تَرْضَوْا عَنْهُمْ فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يَرْضَىٰ عَنِ الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ﴿٩٦﴾

Watakuapieni ili muwaridhie. Mkiwaridhia, basi hakika Allaah Haridhii watu mafasiki. [At-Tawbah 95-96]

Sisi watatu tulitofautiana na wale walioapa mbele ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawakubalia nyudhuru zao, akachukua bay'ah yao na kuwaombea maghfirah. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliacha kadhia yetu ibakie mpaka Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Akahukumu. Allaah Anasema:

وَعَلَى الثَّلاثَةِ الَّذِينَ خُلِّفُوا

Na (pia Allaah Akapokea tawbah) ya wale watatu waliobaki nyuma (kutokwenda vita vya Tabuwk; wakajuta mno) [At-Tawbah; 118]

Hapa haizungumziwi kuhusu kubaki kwetu nyuma kutokwenda vitani. Bali muradi wake ni vile Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alivyoiakhirisha kadhia yetu kinyume na kadhia ya wale walitoa nyudhuru kwa kula viapo akawakubalia.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

Riwaayah nyingine inasema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka katika vita vya Tabuwk siku ya Alkhamisi na alikuwa akipenda kusafiri siku ya Alkhamisi.

Riwaayah nyingine pia inasema: “Na alikuwa harudi kutoka safari ila mchana katika wakati wa Dhwuhaa anapokuja huanza kuteremkia Masjid akiswali humo rakaa mbili kisha akikaa kitako.





Hadiyth – 10



وَعَنْ أبي نُجَيد- بضَمِّ النُّونِ وفتحِ الجيم- عِمْرَانَ بنِ الحُصَيْنِ الخُزَاعِيِّ رضي الله عنهما: أنَّ امْرَأةً مِنْ جُهَيْنَةَ أتَتْ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم وَهِيَ حُبْلَى مِنَ الزِّنَى، فقالتْ: يَا رسولَ الله، أصَبْتُ حَدًّا فَأَقِمْهُ عَلَيَّ، فَدَعَا نَبيُّ الله صلى الله عليه وسلم وَليَّها، فقالَ: ((أَحْسِنْ إِلَيْهَا، فإذا وَضَعَتْ فَأْتِني)) فَفَعَلَ فَأَمَرَ بهَا نبيُّ الله صلى الله عليه وسلم، فَشُدَّتْ عَلَيْهَا ثِيَابُهَا، ثُمَّ أَمَرَ بِهَا فَرُجِمَتْ، ثُمَّ صَلَّى عَلَيْهَا. فقالَ لَهُ عُمَرُ: تُصَلِّي عَلَيْهَا يَا رَسُول الله وَقَدْ زَنَتْ؟ قَالَ: ((لَقَدْ تَابَتْ تَوْبَةً لَوْ قُسِمَتْ بَيْنَ سَبْعِينَ مِنْ أهْلِ المَدِينَةِ لَوَسِعَتْهُمْ، وَهَلْ وَجَدْتَ أَفضَلَ مِنْ أنْ جَادَتْ بنفْسِها لله- عز وجل-؟!)). رواه مسلم

Abuu Nujayd, ‘Imraan bin Huswayn Al-Khuza'iy (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amehadithia kwamba: Mwanamke kutoka kabila la Juhaynah alimuendea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) naye ana mimba ya zinaa, akamwambia: “Ee Rasuli wa Allaah, nimetenda dhambi inayopaswa haddi (adhabu), kwa hiyo nipitishie.” Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwita msimamizi wake, akamwambia: “Mfanyie ihsaan atakapojifungua mlete.” Yule msimamizi akafanya kama alivyoamrishwa, halafu akaja naye. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaamuru, akafungwe kwa nguo zake, halafu akaamuru arajimiwe, kisha akamswalia. ‘Umar akamwambia: “Ee Rasuli wa Allaah, unamswalia na hali alikuwa amezini?” Akamwambia: “Kwa yakini ametubia tawbah ambayo lau ingeligawanya kwa watu sabini miongoni mwa watu wa Madiynah, ingewatosha. Je, ushawahi kuona lililo bora kuliko yeye kujileta mwenyewe kwa Allaah (‘Azza wa Jalla)?” [Muslim]





Hadiyth – 11



وعن ابنِ عباسٍ رضي الله عنهما أنَّ رَسُولَ الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((لَوْ أنَّ لابنِ آدَمَ وَادِيًا مِنْ ذَهَبٍ أحَبَّ أنْ يكُونَ لَهُ وَادِيانِ، وَلَنْ يَمْلأَ فَاهُ إلا التُّرَابُ، وَيَتْوبُ اللهُ عَلَى مَنْ تَابَ)). مُتَّفَقٌ عليه

'Abdullaah bin ‘Abbaas na Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) wamehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“Lau mwana Aadam angalikuwa na bonde la dhahabu, angalipendelea awe na mabonde mawili, wala hakuna kitakachoweza kumtosheleza mdomo wake isipokuwa ni mchanga. Na Allaah Humkubalia tawbah ya yule mwenye kutubia.” [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 12



وعن أبي هريرة رضي الله عنه أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((يَضْحَكُ اللهُ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَى إِلَى رَجُلَيْنِ يقْتُلُ أَحَدهُمَا الآخَرَ يَدْخُلانِ الجَنَّةَ، يُقَاتِلُ هَذَا في سَبيلِ اللهِ فَيُقْتَلُ، ثُمَّ يتُوبُ اللهُ عَلَى القَاتلِ فَيُسْلِم فَيُسْتَشْهَدُ)). مُتَّفَقٌ عليه

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Huwacheka watu wawili, mmoja anamuua mwengine, wote wakaingia Jannah. Huyu atapigana na huyu katika njia ya Allaah, atauliwa. Kisha Allaah Atamsamehe aliyeua kwa kusilimu naye akafa shahiyd.” [Al-Bukhaariy na
 
Mlango wa Subir

Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اصْبِرُوا وَصَابِرُوا وَرَابِطُوا وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

Enyi walioamini! Subirini na zidini kuvuta subira na bakieni imara na mcheni Allaah ili mpate kufaulu. [Aal-'Imraan: 200]



وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ ۗ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ

Na bila shaka Tutakujaribuni kwa kitu katika khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na mazao. Na wabashirie wenye kusubiri. [Al-Baqarah: 155]



قُلْ يَا عِبَادِ الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا رَبَّكُمْ ۚ لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةٌ ۗ وَأَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةٌ ۗ إِنَّمَا يُوَفَّى الصَّابِرُونَ أَجْرَهُم بِغَيْرِ حِسَابٍ

Sema: “Enyi waja Wangu ambao mmeamini, mcheni Rabb wenu. Kwa wale waliofanya mazuri katika dunia hii watapata mazuri. Na ardhi ya Allaah ni pana. Hakika wanaosubiri watalipwa kikamilifu ujira wao bila ya hesabu. [Az-Zumar: 10]



وَلَمَن صَبَرَ وَغَفَرَ إِنَّ ذَٰلِكَ لَمِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ

Na atakayevuta subira na akasamehe, hakika hilo bila shaka ni katika mambo ya kuazimiwa. [As-Shuwra: 43]



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الصَّابِرِينَ

Enyi walioamini! Tafuteni msaada kwa subira na Swalaah; hakika Allaah Yu pamoja na wanaosubiri. [Al-Baqarah: 153]



وَلَنَبْلُوَنَّكُمْ حَتَّىٰ نَعْلَمَ الْمُجَاهِدِينَ مِنكُمْ وَالصَّابِرِينَ وَنَبْلُوَ أَخْبَارَكُمْ

Na bila shaka Tutakujaribuni mpaka Tutambue wenye kufanya jihaad miongoni mwenu na wenye kuvuta subira na tutazitahini habari zenu. [Muhammad: 31]



Aayah zinazoamrisha subira na kubainisha fadhila zake ni nyingi na mashuhuri.





Hadiyth – 1

وعن أبي مالكٍ الحارث بن عاصم الأشعريِّ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((الطُّهُورُ شَطْرُ الإِيمان، وَالحَمدُ لله تَمْلأُ الميزَانَ، وَسُبْحَانَ الله والحَمدُ لله تَملآن- أَوْ تَمْلأُ- مَا بَينَ السَّماوات وَالأَرْضِ، والصَّلاةُ نُورٌ، والصَّدقةُ بُرهَانٌ، والصَّبْرُ ضِياءٌ، والقُرْآنُ حُجةٌ لَكَ أَوْ عَلَيْكَ. كُلُّ النَّاسِ يَغْدُو فَبَائعٌ نَفسَهُ فَمُعْتِقُهَا أَوْ مُوبِقُها)). رواه مسلم

Abuu Maalik, Al-Haarith bin ‘Aaswim Al-Ash’ariy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Wudhuu ni nusu ya iymaan, (kusema🙂 AlhamduliLLaah hujaza miyzaan, Subhaana Allaah wal-HamduliLLaah hujaza baina ya mbingu na ardhi, Swalaah ni nuru, Swadaqah ni hojja (kwa mwenye iymaan na kuitoa), subira ni mwangaza na Qur-aan ni hojja ya kukuokoa au kukuangamiza. Kila mtu huifanyia ‘amali nafsi yake, kuna mwenye kujiuza, mwenye kujiacha huru au mwenye kujiangamiza.” [Muslim]





Hadiyth – 2

وعن أبي سَعيد سعدِ بن مالكِ بنِ سنانٍ الخدري رضي الله عنهما: أَنَّ نَاسًا مِنَ الأَنْصَارِ سَألوا رسولَ الله صلى الله عليه وسلم فَأعْطَاهُمْ، ثُمَّ سَألوهُ فَأعْطَاهُمْ، حَتَّى نَفِدَ مَا عِندَهُ، فَقَالَ لَهُمْ حِينَ أنْفْقَ كُلَّ شَيءٍ بِيَدِهِ: ((مَا يَكُنْ عِنْدي مِنْ خَيْر فَلَنْ أدَّخِرَهُ عَنْكُمْ، وَمَنْ يَسْتَعْفِفْ يُعِفهُ اللهُ، وَمَنْ يَسْتَغْنِ يُغْنِهِ اللهُ، وَمَنْ يَتَصَبَّرْ يُصَبِّرْهُ اللهُ. وَمَا أُعْطِيَ أَحَدٌ عَطَاءً خَيْرًا وَأوْسَعَ مِنَ الصَّبْر)). مُتَّفَقٌ عليه

Abuu Sa’iyd, Sa’d bin Maalik bin Sinaan Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: “Watu fulani miongoni mwa Answaar walimuomba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), naye akawapa, kisha wakamuomba tena, naye akawapa mpaka akamaliza chote alichokuwa nacho. Akawaambia baada ya kuwa ameshatoa kila kitu: “Khayr yoyote niliyonayo siwezi kuwanyima, mwenye kujizuia kuomba Allaah Atamlipa kwa kutoomba, mwenye kutosheka basi na Allaah Atamtosheleza zaidi, na Atakae jisubirisha basi na Allaah Atamzidishia subira. Hakuna yoyote yule aliyepewa zawadi bora na iliyokunjufu zaidi kulikoni subira.” [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 3

وعن أبي يحيى صهيب بن سنانٍ رضي الله عنه، قَالَ: قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((عَجَبًا لأمْرِ المُؤمنِ إنَّ أمْرَهُ كُلَّهُ لَهُ خيرٌ ولَيسَ ذلِكَ لأَحَدٍ إلا للمُؤْمِن: إنْ أَصَابَتْهُ سَرَّاءُ شَكَرَ فَكانَ خَيرًا لَهُ، وإنْ أصَابَتْهُ ضرَاءُ صَبَرَ فَكانَ خَيْرًا لَهُ)). رواه مسلم

Abuu Yahyaa, Swuhayb bin Sinaan (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Ajabu kwa jambo la Muumin; hakika mambo yake ni khayr, wala hakuna anayepata hilo isipokuwa Muumin pekee; akipatwa na furaha hushukuru basi huwa ni khayr kwake, na akipatwa na madhara husubiri basi huwa khayr kwake.” [Muslim]





Hadiyth – 4

وعن أنَسٍ رضي الله عنه قَالَ: لَمَّا ثَقُلَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم جَعلَ يَتَغَشَّاهُ الكَرْبُ، فَقَالَتْ فَاطِمَةُ رضي الله عنها: وَاكَربَ أَبَتَاهُ. فقَالَ: ((لَيْسَ عَلَى أَبيكِ كَرْبٌ بَعْدَ اليَوْمِ)) فَلَمَّا مَاتَ، قَالَتْ: يَا أَبَتَاهُ، أَجَابَ رَبًّا دَعَاهُ! يَا أَبتَاهُ، جَنَّةُ الفِردَوسِ مَأْوَاهُ! يَا أَبَتَاهُ، إِلَى جبْريلَ نَنْعَاهُ! فَلَمَّا دُفِنَ قَالَتْ فَاطِمَةُ رَضي الله عنها: أَطَابَتْ أنْفُسُكُمْ أنْ تَحْثُوا عَلَى رَسُول الله صلى الله عليه وسلم التُّرَابَ؟! رواه البخاري.

Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mambo yalivyomzidia uzito, ukamjia uchungu wa mauti, Faatwimah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) akasema: “Ee uchungu gani unaomshika baba yangu.” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Baba yako hatoteseka baada ya leo.” Alipofariki Faatwimah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) akasema: “Ee baba yangu ameitika wito wa Rabb wake! Ee baba yangu Jannah ya Al-Firdaws ndio mashukio yake. Ee baba yangu! Kwa Jibriyl tunamuombeleza!” Alipozikwa, Faatwimah alisema: “Nyoyo zenu zimeridhika kwa kumiminia mchanga Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)?” [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 5

وعن أبي زَيدٍ أُسَامَةَ بنِ زيدِ بنِ حارثةَ مَوْلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم وحِبِّه وابنِ حبِّه رضي اللهُ عنهما، قَالَ: أرْسَلَتْ بنْتُ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم إنَّ ابْني قَد احْتُضِرَ فَاشْهَدنَا، فَأَرْسَلَ يُقْرئُ السَّلامَ، ويقُولُ: ((إنَّ لله مَا أخَذَ وَلَهُ مَا أعطَى وَكُلُّ شَيءٍ عِندَهُ بِأجَلٍ مُسَمًّى فَلتَصْبِرْ وَلْتَحْتَسِبْ)) فَأَرسَلَتْ إِلَيْهِ تُقْسِمُ عَلَيهِ لَيَأتِينَّهَا. فقامَ وَمَعَهُ سَعْدُ بْنُ عُبَادَةَ، وَمُعَاذُ بْنُ جَبَلٍ، وَأُبَيُّ بْنُ كَعْبٍ، وَزَيْدُ بْنُ ثَابتٍ، وَرجَالٌ رضي الله عنهم، فَرُفعَ إِلَى رَسُول الله صلى الله عليه وسلم الصَّبيُّ، فَأقْعَدَهُ في حِجْرِهِ وَنَفْسُهُ تَقَعْقَعُ، فَفَاضَتْ عَينَاهُ فَقالَ سَعدٌ: يَا رسولَ الله، مَا هَذَا؟ فَقالَ: ((هذِهِ رَحمَةٌ جَعَلَها اللهُ تَعَالَى في قُلُوبِ عِبَادِهِ)) وفي رواية: ((فِي قُلُوبِ مَنْ شَاءَ مِنْ عِبَادِهِ، وَإِنَّما يَرْحَمُ اللهُ مِنْ عِبادِهِ الرُّحَماءَ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Abuu Zayd, Usaamah bin Zayd bin Haarithah muachwa huru wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kipenzi chake na ni mwana wa kipenzi chake (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: Binti mmoja wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimpelekea salaamu Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa “Mwana wangu amejiwa na umauti, basi njoo.” Naye akamtuma mtu akimpelekea salaamu na akamwambia: “Allaah Ana khiyari ya kuchukua Anachotaka na kutoa Anachotaka. Kila kitu Kwake kina muda maalumu, basi asubiri na taraji malipo kwa Allaah.” Akamtumia tena ujumbe akimuapia aende. Akasimama, pamoja naye alikuwepo Sa’d bin ‘Ubaadah, Mu’aadh bin Jabal, Ubayyi bin Ka’b, Zayd bin Thaabit na wengineo (Radhwiya Allaahu ‘anhum). Yule mtoto akapelekewa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), akamkalisha katika paja lake na nafsi ya yule mtoto ikiwa katika hali ya woga, macho ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yakabubujikwa na machozi, Sa’d akauliza: “Una nini yaa Rasula-Allaah?” Akamwambia: “Hii ni rahmah, Allaah Amejaalia katika nyoyo za waja Wake.”

Riwaayah nyingine imesema: “Katika nyoyo za Anaowataka miongoni mwa waja Wake. Hakika Allaah Huwarehemu wenye huruma katika waja Wake.” [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 6

وعن صهيب رضي الله عنه: أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((كَانَ مَلِكٌ فيمَنْ كَانَ قَبلَكمْ وَكَانَ لَهُ سَاحِرٌ فَلَمَّا كَبِرَ قَالَ للمَلِكِ: إنِّي قَدْ كَبِرْتُ فَابْعَثْ إلَيَّ غُلامًا أُعَلِّمْهُ السِّحْرَ؛ فَبَعثَ إِلَيْهِ غُلامًا يُعَلِّمُهُ، وَكانَ في طرِيقِهِ إِذَا سَلَكَ رَاهِبٌ، فَقَعدَ إِلَيْه وسَمِعَ كَلامَهُ فَأعْجَبَهُ، وَكانَ إِذَا أتَى السَّاحِرَ، مَرَّ بالرَّاهبِ وَقَعَدَ إِلَيْه، فَإذَا أَتَى السَّاحِرَ ضَرَبَهُ، فَشَكَا ذلِكَ إِلَى الرَّاهِب، فَقَالَ: إِذَا خَشيتَ السَّاحِرَ، فَقُلْ: حَبَسَنِي أَهْلِي، وَإذَا خَشِيتَ أهلَكَ، فَقُلْ: حَبَسَنِي السَّاحِرُ.

فَبَيْنَما هُوَ عَلَى ذلِكَ إِذْ أَتَى عَلَى دَابَّةٍ عَظِيمَةٍ قَدْ حَبَسَتِ النَّاسَ فَقَالَ: اليَوْمَ أعْلَمُ السَّاحرُ أفْضَلُ أم الرَّاهبُ أفْضَلُ؟ فَأخَذَ حَجَرًا، فَقَالَ: اللَّهُمَّ إنْ كَانَ أمْرُ الرَّاهِبِ أَحَبَّ إِلَيْكَ مِنْ أمْرِ السَّاحِرِ فَاقْتُلْ هذِهِ الدّابَّةَ حَتَّى يَمضِي النَّاسُ، فَرَمَاهَا فَقَتَلَها ومَضَى النَّاسُ، فَأتَى الرَّاهبَ فَأَخبَرَهُ. فَقَالَ لَهُ الرَّاهبُ: أَيْ بُنَيَّ أَنْتَ اليَومَ أفْضَل منِّي قَدْ بَلَغَ مِنْ أَمْرِكَ مَا أَرَى، وَإنَّكَ سَتُبْتَلَى، فَإن ابْتُلِيتَ فَلا تَدُلَّ عَلَيَّ؛ وَكانَ الغُلامُ يُبْرىءُ الأكْمَهَ وَالأَبْرصَ، ويداوي النَّاسَ مِنْ سَائِرِ الأَدْوَاء. فَسَمِعَ جَليسٌ لِلملِكِ كَانَ قَدْ عَمِيَ، فأتاه بَهَدَايا كَثيرَةٍ، فَقَالَ: مَا هاهُنَا لَكَ أَجْمعُ إنْ أنتَ شَفَيتَنِي، فَقَالَ: إنّي لا أشْفِي أحَدًا إِنَّمَا يَشفِي اللهُ تَعَالَى، فَإنْ آمَنْتَ بالله تَعَالَى دَعَوتُ اللهَ فَشفَاكَ، فَآمَنَ بالله تَعَالَى فَشفَاهُ اللهُ تَعَالَى، فَأَتَى المَلِكَ فَجَلسَ إِلَيْهِ كَما كَانَ يَجلِسُ، فَقَالَ لَهُ المَلِكُ: مَنْ رَدّ عَلَيْكَ بَصَرَكَ؟ قَالَ: رَبِّي، قَالَ: وَلَكَ رَبٌّ غَيري؟ قَالَ: رَبِّي وَرَبُّكَ اللهُ، فَأَخَذَهُ فَلَمْ يَزَلْ يُعَذِّبُهُ حَتَّى دَلَّ عَلَى الغُلامِ، فَجيء بالغُلاَمِ، فَقَالَ لَهُ المَلِكُ: أيْ بُنَيَّ، قَدْ بَلَغَ مِنْ سِحْرِكَ مَا تُبْرئ الأَكْمَهَ وَالأَبْرَصَ وتَفْعَلُ وتَفْعَلُ! فَقَالَ: إنِّي لا أَشْفي أحَدًا، إِنَّمَا يَشفِي الله تَعَالَى. فَأَخَذَهُ فَلَمْ يَزَلْ يُعَذِّبُهُ حَتَّى دَلَّ عَلَى الرَّاهبِ؛ فَجِيء بالرَّاهبِ فَقيلَ لَهُ: ارجِعْ عَنْ دِينكَ، فَأَبَى، فَدَعَا بِالمِنْشَارِ فَوُضِعَ المِنْشَارُ في مَفْرق رَأسِهِ، فَشَقَّهُ حَتَّى وَقَعَ شِقَّاهُ، ثُمَّ جِيءَ بِجَليسِ المَلِكِ فقيل لَهُ: ارْجِعْ عَنْ دِينِكَ، فَأَبَى، فَوضِعَ المِنْشَارُ في مَفْرِق رَأسِهِ، فَشَقَّهُ بِهِ حَتَّى وَقَعَ شِقَّاهُ، ثُمَّ جِيءَ بالغُلاَمِ فقيلَ لَهُ: ارْجِعْ عَنْ دِينكَ، فَأَبَى، فَدَفَعَهُ إِلَى نَفَرٍ مِنْ أصْحَابهِ، فَقَالَ: اذْهَبُوا بِهِ إِلَى جَبَلِ كَذَا وَكَذَا فَاصْعَدُوا بِهِ الجَبَل، فَإِذَا بَلَغْتُمْ ذِرْوَتَهُ فَإِنْ رَجَعَ عَنْ دِينِهِ وَإلا فَاطْرَحُوهُ. فَذَهَبُوا بِهِ فَصَعِدُوا بِهِ الجَبَلَ، فَقَالَ: اللَّهُمَّ أكْفنيهمْ بِمَا شِئْتَ، فَرَجَفَ بهِمُ الجَبلُ فَسَقَطُوا، وَجاءَ يَمشي إِلَى المَلِكِ، فَقَالَ لَهُ المَلِكُ: مَا فَعَلَ أصْحَابُكَ؟ فَقَالَ: كَفَانِيهمُ الله تَعَالَى، فَدَفَعَهُ إِلَى نَفَرٍ مِنْ أَصْحَابِهِ فَقَالَ: اذْهَبُوا بِهِ فاحْمِلُوهُ في قُرْقُورٍ وتَوَسَّطُوا بِهِ البَحْرَ، فَإنْ رَجعَ عَنْ دِينِهِ وإِلا فَاقْذِفُوهُ. فَذَهَبُوا بِهِ، فَقَالَ: اللَّهُمَّ أكْفِنيهمْ بمَا شِئْتَ، فانْكَفَأَتْ بِهمُ السَّفينةُ فَغَرِقُوا، وَجَاء يَمْشي إِلَى المَلِكِ. فَقَالَ لَهُ المَلِكُ: مَا فعلَ أصْحَابُكَ؟ فَقَالَ: كَفَانيهمُ الله تَعَالَى. فَقَالَ لِلمَلِكِ: إنَّكَ لَسْتَ بقَاتلي حَتَّى تَفْعَلَ مَا آمُرُكَ بِهِ. قَالَ: مَا هُوَ؟ قَالَ: تَجْمَعُ النَّاسَ في صَعيدٍ وَاحدٍ وتَصْلُبُني عَلَى جِذْعٍ، ثُمَّ خُذْ سَهْمًا مِنْ كِنَانَتي، ثُمَّ ضَعِ السَّهْمَ في كَبدِ القَوْسِ ثُمَّ قُلْ: بسْم الله ربِّ الغُلاَمِ، ثُمَّ ارْمِني، فَإنَّكَ إِذَا فَعَلْتَ ذلِكَ قَتَلتَني، فَجَمَعَ النَّاسَ في صَعيد واحدٍ، وَصَلَبَهُ عَلَى جِذْعٍ، ثُمَّ أَخَذَ سَهْمًا مِنْ كِنَانَتِهِ، ثُمَّ وَضَعَ السَّهْمَ في كَبِدِ القَوْسِ، ثُمَّ قَالَ: بِسمِ اللهِ ربِّ الغُلامِ، ثُمَّ رَمَاهُ فَوقَعَ في صُدْغِهِ، فَوَضَعَ يَدَهُ في صُدْغِهِ فَمَاتَ، فَقَالَ النَّاسُ: آمَنَّا بِرَبِّ الغُلامِ، فَأُتِيَ المَلِكُ فقيلَ لَهُ: أَرَأَيْتَ مَا كُنْتَ تَحْذَرُ قَدْ والله نَزَلَ بكَ حَذَرُكَ. قَدْ آمَنَ النَّاسُ. فَأَمَرَ بِالأُخْدُودِ بأفْواهِ السِّكَكِ فَخُدَّتْ وأُضْرِمَ فيهَا النِّيرانُ وَقَالَ: مَنْ لَمْ يَرْجعْ عَنْ دِينهِ فَأقْحموهُ فيهَا، أَوْ قيلَ لَهُ: اقتَحِمْ فَفَعَلُوا حَتَّى جَاءت امْرَأةٌ وَمَعَهَا صَبيٌّ لَهَا، فَتَقَاعَسَتْ أنْ تَقَعَ فيهَا، فَقَالَ لَهَا الغُلامُ: يَا أُمهْ اصْبِري فَإِنَّكِ عَلَى الحَقِّ!)). رواه مسلم

Swuhayb (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Alikuwepo mfalme kabla ya zama zenu. Alikuwa anae mchawi, yule mchawi alipozeeka alimwambia mfalme: “Mimi nimezeeka, niletee kijana nitakaemfunza uchawi.” (mfalme) akampelekea kijana ili amfunze. Alikuwa (yule kijana) katika njia anayoelekea kuna Rahibu (mtawa mwanaume). Akakaa kumsikiliza, akapendezewa na maneno yake, na alikuwa akitaka kumuendea mchawi yule hupita kwa Rahibu yule na kukaa naye na kumsikiliza, anapomwendea mchawi, humpiga. Jambo hili akamshitakia yule mtawa. (Mtawa) akamwambia: “Utakapomuendea mchawi mwambie: ‘Nimezuiliwa na watu wangu,’ na unapowarudia watu wako, waambie: Nimezuiliwa na mchawi.” Alipokuwa akiendelea katika hali hiyo, kwa ghafla akaona mnyama mkubwa aliyezuia watu. Akasema: “Leo ndiyo nitajua kati ya mtawa na mchawi nani aliye bora.” Akachukua jiwe na akasema: “Ee Rabb, ikiwa jambo la yule Mtawa linapendeza Kwako kuliko jambo la yule mchawi, basi muuwe mnyama huyu ili watu waweze kupita.” Akamrushia (jiwe) na akamuua, watu wakapita. Akamuendea Mtawa na kumueleza habari ile. Yule Mtawa akamwambia: “Ee mwanangu leo hii wewe ni bora kulikoni mimi, jambo lako limefikia jinsi ninavyoliona, kwa yakini utapata mtihani; basi utakapopata mtihani, usimjulishe yoyote yule kwangu.” Yule kijana akaanza kuwaponya waliozaliwa vipofu, wenye ukoma na akiwatibu watu kila aina ya maradhi. Jalisi wa mfalme aliyekuwa amepofoka, akasikia habari hii. Akampelekea zawadi nyingi, akamwambia: “Mimi sina uwezo wa kumponya yoyote, hakika Anaeponya ni Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa). Ukimuamini Allaah nitamuomba Naye Atakuponya.” Akamuamini Allaah, Allaah Akamponya. Akaenda kwa mfalme na kukaa nae kama anavyokaa nae (kila siku). Mfalme akamuuliza: “Ni nani aliyekuponya macho yako?” Akajibu: “Ni Rabb wangu.” Akamuuliza: “Unae Rabb asiyekuwa mimi?” Akamjibu: “Rabb wangu na Rabb wako ni Allaah.” Akamchukua na akamuadhibu mpaka akamtaja yule kijana. Yule kijana akaletwa mbele ya mfalme, akamuuliza: “Ee kijana wangu, uchawi wako umefikia kiwango cha kuwaponya vipofu na wenye ukoma, na unafanya kadhaa na kadhaa?” Akamwambia: “Mimi sina uwezo wa kumponya yoyote yule, kwa yakini Anaeponya ni Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).” Akamchukua na kumuadhibu mpaka akamtaja yule Mtawa. Mtawa akaletwa, akaambiwa: “Acha dini yako.” Akakataa. Akaitisha msumeno akauweka utosini mwake, akampasua vipande viwili vikaanguka (akamgawanya pande mbili). Halafu akaletwa jalisi wa mfalme. Akaambiwa: “Acha dini yako.” Akakataa. Msumeno ukawekwa utosini mwake, akapasuliwa pande mbili zikaanguaka. Kisha akaletwa yule kijana. Akaambiwa: “Wacha dini yako.” Akakataa. Akamkabidhi kwa askari wake, akawaambia: “Nendeni naye katika jabali kadhaa wa kadhaa, mtakapofika katika kilele chake na akawa ameiwacha dini yake, basi muacheni, ikiwa hakuacha basi mtupeni chini.” Wakaenda nae na wakapanda nae juu ya jabali. Yule kijana akaomba: “Ee Rabb! Nitosheleze na shari yao namna Upendavyo.” Lile jabali likatikisika wakaanguka. Akarudi kwa mfalme huku akitembea. Mfalme akamuuliza: “Wamekuaje watu wako?” Akamwambia: Allaah Amenitosheleza.” Akamkabidhisha kwa kundi (lingine) la maaskari wake. Akawaambia: “Mpelekeni na mumpandishe jahazi ndogo hadi katikati ya bahari, akiwacha dini yake muacheni, akikataa basi mtoseni.” Wakaenda naye, akaomba: “Ee Rabb! Nitosheleze na shari yao namna Upendavyo.” Jahazi likapinduka wakazama. Akarudi kwa mfalme akitembea. Mfalme akamuuliza: “Wamekuaje watu wako?” Akamwambia: “Allaah Amenitosheleza.” Akamwambia mfalme: “Hakika huwezi kuniua mpaka ufanye nitakalokuamuru.” Akamuuliza: “Ni jambo gani hilo utakaloniamuru?” Akamwambia: “Wakusanye watu katika uwanja ulio wazi, halafu unisulubishe juu ya gogo, halafu uchukue mshale utakaokuwa katika ziaka yangu, kisha utauweka mshale katika upinde, halafu useme: “Kwa jina la Allaah, Rabb wa kijana huyu”. Kisha unirushie. Hakika ukifanya hivyo, utafanikiwa kuniua.” Yule mfalme akawakusanya watu katika uwanja mmoja, akamtundika juu ya gogo, halafu akachukua mshale kutoka katika ziaka yake, kisha akauweka mshale katikati ya upinde, halafu akasema: “Kwa jina la Allaah, Rabb wa kijana huyu,” kisha akamrushia ule mshale ukaingia katika panda lake uso, akauweka mkono wake katika panda lake na akafa. Watu wakasema: “Tumemuamini Rabb wa kijana huyu.” Mfalme akaendewa na kuambiwa: “Je, umeliona ulilokuwa ukilitahadhari? Wa-Allaahi limekuwa ulilolikataa, watu wamekuwa na iymaan.” Akaamuru kuchimbwe mahandaki barabarani, mioto ikawashwa humo. Akasema: “Ambae hatoacha dini yake mtupeni humo.” Au huambiwa: “Jitoseni wenyewe.” Wakafanya hivyo. Akaletwa mwanamke aliye na mtoto wake. Akasimama na akafanya uoga kuingia humo, yule mtoto wake akamwambia: “Ee mama yangu, subiri hakika wewe upo katika haki!” [Muslim]





Hadiyth – 7

وعن أنس رضي الله عنه قَالَ: مَرَّ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم بامرأةٍ تَبكي عِنْدَ قَبْرٍ، فَقَالَ: ((اتّقِي الله واصْبِري)) فَقَالَتْ: إِليْكَ عَنِّي؛ فإِنَّكَ لم تُصَبْ بمُصِيبَتي وَلَمْ تَعرِفْهُ، فَقيلَ لَهَا: إنَّه النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم فَأَتَتْ بَابَ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم، فَلَمْ تَجِدْ عِنْدَهُ بَوَّابينَ، فقالتْ: لَمْ أعْرِفكَ، فَقَالَ: ((إنَّمَا الصَّبْرُ عِنْدَ الصَّدْمَةِ الأُولى)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

وفي رواية لمسلم: ((تبكي عَلَى صَبيٍّ لَهَا)).

Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipita akamuona mwanamke akilia mbele ya kaburi. Akamwambia: “Mche Allaah na usubiri.” Yule mwanamke akasema: “Niondokee, kwani hujapatwa na msiba kama wangu!” Wala hakumjua. Akaambiwa: Huyo alikuwa ni Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), akaenda hadi kwenye mlango wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na hakuwakuta walinzi, akamwambia: “Nilikuwa sijakujua kama ni wewe.” Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: “Hakika subira ni mwanzo wa kupatwa na msiba.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

Riwaayah nyingine ya Muslim imesema: “Alikuwa akimlilia mwanawe.”





Hadiyth – 8

وعن أبي هريرة رضي الله عنه: أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((يَقُولُ اللهُ تَعَالَى: مَا لعَبدِي المُؤْمِنِ عِنْدِي جَزَاءٌ إِذَا قَبَضْتُ صَفِيَّهُ مِنْ أهْلِ الدُّنْيَا ثُمَّ احْتَسَبَهُ إلا الجَنَّةَ)). رواه البخاري

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema: “Mja wangu Muumin ni mwenye malipo nitakapomchukua mpenzi wake katika watu wa dunia kisha akataraji thawabu isipokuwa jazaa yake ni Jannah.” [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 9

وعن عائشةَ رضيَ الله عنها: أَنَّهَا سَألَتْ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم عَنِ الطّاعُونِ، فَأَخْبَرَهَا أنَّهُ كَانَ عَذَابًا يَبْعَثُهُ اللهُ تَعَالَى عَلَى مَنْ يشَاءُ، فَجَعَلَهُ اللهُ تعالى رَحْمَةً للْمُؤْمِنينَ، فَلَيْسَ مِنْ عَبْدٍ يَقَعُ في الطَّاعُونِ فيمكثُ في بلدِهِ صَابرًا مُحْتَسِبًا يَعْلَمُ أنَّهُ لا يصيبُهُ إلا مَا كَتَبَ اللهُ لَهُ إلا كَانَ لَهُ مِثْلُ أجْرِ الشّهيدِ. رواه البخاري

‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) alimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu twaa’uwn (ugonjwa wa tauni), akamwambia kuwa: “Ilikuwa ni adhabu ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Akimpelekea Anayemtaka; Allaah Akaijaalia kuwa ni rahmah kwa Waumini. Hakuna mja yoyote yule atakaepata twaa’uwn akakaa katika mji ule kwa kusubiri na kutaraji thawabu akijua kuwa hakuna kitakachompata ila alichoandikiwa na Allaah, isipokuwa na ujira mfano wa (aliyekufa) shaahid.” [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 10

وعن أنس رضي الله عنه قَالَ: سمعتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((إنَّ الله- عز وجل، قَالَ: إِذَا ابْتَلَيْتُ عبدي بحَبيبتَيه فَصَبرَ عَوَّضتُهُ مِنْهُمَا الجَنَّةَ)) يريد عينيه، رواه البخاري

Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Hakika Allaah (‘Azza wa Jalla) Amesema: “Nitakapomjaribu mja Wangu kwa kukosa vipenzi vyake (macho mawili) na akasubiri, Nitambadilishia Jannah badala yake.” [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 11

وعن عطَاء بن أبي رَباحٍ قَالَ: قَالَ لي ابنُ عَباسٍ رضي اللهُ عنهما: ألا أُريكَ امْرَأةً مِنْ أَهْلِ الجَنَّة؟ فَقُلْتُ: بَلَى، قَالَ: هذِهِ المَرْأةُ السَّوداءُ أتتِ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم، فَقَالَتْ: إنّي أُصْرَعُ، وإِنِّي أتَكَشَّفُ، فادْعُ الله تَعَالَى لي. قَالَ: ((إنْ شئْتِ صَبَرتِ وَلَكِ الجَنَّةُ، وَإنْ شئْتِ دَعَوتُ الله تَعَالَى أنْ يُعَافِيكِ)) فَقَالَتْ: أَصْبِرُ، فَقَالَتْ: إنِّي أتَكَشَّفُ فَادعُ الله أنْ لا أَتَكَشَّف، فَدَعَا لَهَا. مُتَّفَقٌ عَلَيه

‘Atwaa bin Abiy Rabaah amesema: “’Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) aliniambia: Je, nikuonyeshe mwanamke ambae ni katika watu wa Jannah?” Nikwambia: “Ni mwanamke huyu mweusi, alimuendea Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kamwambia: “Mimi nina kifafa na huwa nafichulika wazi (sehemu za siri kinaponijia), niombee kwa Allaah.” Akamwambia: “Ukitaka subiri na ukitaka nitamuomba Allaah Akuponye.” Akasema: “Nitasubiri lakini mimi nafichulika wazi basi niombee kwa Allaah nisifichulike wazi (nisitirike nguo isinifunuke).” Akamuombea. [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyh -12



وعن أبي عبد الرحمنِ عبدِ الله بنِ مسعودٍ رضي الله عنه قَالَ: كَأَنِّي أنْظُرُ إِلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم يَحْكِي نَبِيًّا مِنَ الأَنْبِياءِ، صَلَواتُ الله وَسَلامُهُ عَلَيْهمْ، ضَرَبه قَوْمُهُ فَأدْمَوهُ، وَهُوَ يَمْسَحُ الدَّمَ عَنْ وَجْهِهِ، يَقُولُ: ((اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِقَومي، فَإِنَّهُمْ لا يَعْلَمونَ)). مُتَّفَقٌ علَيه

Abuu ‘Abdir-Rahmaan, ‘Abdulaah bin Mas’uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Kana kwamba namuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akieleza kuhusu Nabiy fulani, (‘Alayhimus-Salaam). Watu wake walimpinga na kumtoa damu usoni mwake, akiomba: “Ee Rabb! Waghufurie kaumu yangu, kwani wao hawajui!” [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 13



وعن أبي سعيدٍ وأبي هريرةَ رضيَ الله عنهما، عن النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((مَا يُصيبُ المُسْلِمَ مِنْ نَصَبٍ، وَلا وَصَبٍ، وَلا هَمٍّ، وَلا حَزَنٍ، وَلا أذَىً، وَلا غَمٍّ، حَتَّى الشَّوكَةُ يُشَاكُهَا إلا كَفَّرَ اللهُ بِهَا مِنْ خَطَاياهُ)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

Abuu Sa’iyd na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) wamepokea kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa amesema: “Muislaam hatopatwa na tabu, wala maradhi, wala hamu, wala huzuni, wala udhia, wala ghamu (sononeko) hata akichomwa na mwiba, isipokuwa Allaah Humfutia madhambi yake kwa sababu ya (matatizo) hayo.” [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 14

وعن ابنِ مسعودٍ رضي الله عنه قَالَ: دخلتُ عَلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم وهو يُوعَكُ، فقلت: يَا رسُولَ الله، إنَّكَ تُوْعَكُ وَعْكًا شَدِيدًا، قَالَ: ((أجَلْ، إنِّي أوعَكُ كمَا يُوعَكُ رَجُلانِ مِنكُمْ)). قلْتُ: ذلِكَ أن لَكَ أجْرينِ؟ قَالَ: ((أَجَلْ، ذلِكَ كَذلِكَ، مَا مِنْ مُسْلِمٍ يُصيبُهُ أذىً، شَوْكَةٌ فَمَا فَوقَهَا إلا كَفَّرَ اللهُ بهَا سَيِّئَاتِهِ، وَحُطَّتْ عَنْهُ ذُنُوبُهُ كَمَا تَحُطُّ الشَّجَرَةُ وَرَقَهَا)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

‘Abdullaah bin Mas’uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Nilimuendea Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) naye akiwa na homa. Nikamwambia: Yaa Rasula-Allaah, hakika huwa ukishikwa na homa basi huwa kali mno.” Akasema: “Ndiyo, hakika mimi hushikwa na homa kama vile watu wawili wanavyoshikwa na homa kati yenu.” Nikamuuliza: “Ni kwa vile una ujira mara mbili?” Akasema: “Ndiyo, ni hivyo. Hakuna Muislaamu yoyote anasibiwa na udhia kuanzia mwiba na kuendelea, isipokuwa Allaah humsamehe mabaya yake kwa udhia huo, na dhambi zake hupuputishwa kama vile mti unavyopuputika majani yake.” [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 15

وعن أبي هريرة رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ يُرِدِ اللهُ بِهِ خَيْرًا يُصِبْ مِنْهُ)). رواه البخاري

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Anayependelewa khayr na Allaah Humpa msiba.” [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 16

وعن أنس رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((لا يَتَمَنَّيَنَّ أَحَدُكُمُ المَوتَ لضُرٍّ أَصَابَهُ، فَإِنْ كَانَ لابُدَّ فاعلًا، فَليَقُلْ: اللَّهُمَّ أحْيني مَا كَانَتِ الحَيَاةُ خَيرًا لِي، وَتَوفّنِي إِذَا كَانَتِ الوَفَاةُ خَيرًا لي)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Asitamani mauti mmoja wenu kwa sababu ya madhara yaliyompata, akiwa hana budi ila atamani, basi aombe: Ee Rabb, Nihuishe madamu kuishi kuna khayr kwangu, na Unifishe iwapo kufa kuna khayr kwangu.” [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 17

وعن أبي عبد الله خَبَّاب بنِ الأَرتِّ رضي الله عنه قَالَ: شَكَوْنَا إِلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم وَهُوَ متَوَسِّدٌ بُرْدَةً لَهُ في ظلِّ الكَعْبَةِ، فقُلْنَا: أَلا تَسْتَنْصِرُ لَنَا ألا تَدْعُو لَنا؟ فَقَالَ: ((قَدْ كَانَ مَنْ قَبْلَكُمْ يُؤْخَذُ الرَّجُلُ فَيُحْفَرُ لَهُ في الأرضِ فَيُجْعَلُ فِيهَا، ثُمَّ يُؤْتَى بِالمِنْشَارِ فَيُوضَعُ عَلَى رَأسِهِ فَيُجْعَلُ نصفَينِ، وَيُمْشَطُ بأمْشَاطِ الحَديدِ مَا دُونَ لَحْمِه وَعَظْمِهِ، مَا يَصُدُّهُ ذلِكَ عَنْ دِينِهِ، وَاللهِ لَيُتِمَّنَّ الله هَذَا الأَمْر حَتَّى يَسيرَ الرَّاكبُ مِنْ صَنْعَاءَ إِلَى حَضْرَموتَ لا يَخَافُ إلا اللهَ والذِّئْب عَلَى غَنَمِهِ، ولكنكم تَسْتَعجِلُونَ)). رواه البخاري.

وفي رواية: ((وَهُوَ مُتَوَسِّدٌ بُرْدَةً وَقَدْ لَقِينا مِنَ المُشْرِكِينَ شدَّةً))

Abuu ‘Abdillaah, Khabbaab bin Al-Arrat (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Tulimlalamika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) naye alikuwa ameegemea shuka yake katika kivuli cha Al-Qa’bah. Tukamwambia: “Hutuombei nusra, hutuombei du’ah?” Akatuambia: “Walikuwa waliopita kabla yenu, mtu alikuwa akifukuliwa ardhi na akitiwa humo, halafu ukiletwa msumeno ukiwekwa juu ya kichwa chake, akigawanywa pande mbili, na (mwengine) akichanwa kwa chanuo la chuma akitolewa nyama na mifupa, jambo hilo haliwi kipingamizi katika dini yake. Wa-Allaahi, Allaah Atalikamilisha jambo hili hata msafiri atembee kutoka Sanaa hadi Hadhwramawt hana anachoogopa isipokuwa Allaah, na kumkhofia mbwa mwitu asije akala mbuzi wake; lakini ninyi mnaharaka. [Al-Bukhaariy]

Riwaayah nyingine imesema: “Nae alikuwa ameegemea shuka yake. Kwa hakika tulipata mateso makubwa kutoka kwa mushirikiynah.”





Hadiyth – 18

وعن ابن مسعودٍ رضي الله عنه قَالَ: لَمَّا كَانَ يَومُ حُنَينٍ آثَرَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم نَاسًا في القسْمَةِ، فَأعْطَى الأقْرَعَ بْنَ حَابسٍ مائَةً مِنَ الإِبِلِ، وَأَعْطَى عُيَيْنَة بْنَ حصن مِثْلَ ذلِكَ، وَأَعطَى نَاسًا مِنْ أشْرافِ العَرَبِ وآثَرَهُمْ يَوْمَئِذٍ في القسْمَةِ. فَقَالَ رَجُلٌ: واللهِ إنَّ هذِهِ قِسْمَةٌ مَا عُدِلَ فِيهَا، وَمَا أُريدَ فيهَا وَجْهُ اللهِ، فَقُلْتُ: وَاللهِ لأُخْبِرَنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم، فَأَتَيْتُهُ فَأخْبَرتُهُ بمَا قَالَ، فَتَغَيَّرَ وَجْهُهُ حَتَّى كَانَ كالصِّرْفِ. ثُمَّ قَالَ: ((فَمَنْ يَعْدِلُ إِذَا لم يَعْدِلِ اللهُ وَرسولُهُ؟)) ثُمَّ قَالَ: ((يَرْحَمُ اللهُ مُوسَى قَدْ أُوذِيَ بأكْثَرَ مِنْ هَذَا فَصَبر)). فَقُلْتُ: لا جَرَمَ لا أرْفَعُ إِلَيْه بَعدَهَا حَدِيثًا. مُتَّفَقٌ عَلَيه

‘Abdullaah bin Mas’uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Siku ya vita vya Hunayn, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwafadhilisha baadhi ya watu katika mgao; akampa Al-Aqra’ bin Haabis ngamia mia moja, akampa Uyaynah bin Hiswn mfano wake, na akawapa watu watukufu wa Kiarabu na akawafadhilisha katika mgao siku hiyo. Mtu mmoja akasema: “Wa-Allaahi huu ni mgao usio na uadilifu! Wala haujakusudiwa radhi ya Allaah!” Nikasema: “Wa-Allaahi nitamueleza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam); nikaenda na kumueleza aliyosema. Uso wake Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ukabadilika hata ukawa mwekundu. Kisha akasema: “Ni nani atakaefanya uadilifu ikiwa Allaah na Rasuli wake Hawakufanya uadilifu?” Halafu akasema: “Allaah Amraham Muwsa, hakika aliudhiwa zaidi ya hivi na akasubiri!” Nikasema: “Kwa hakika sitomueleza tena (mazungumzo kama haya ya kumuudhi).” [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyh – 19

وعن أنسٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((إِذَا أَرَادَ الله بعبدِهِ الخَيرَ عَجَّلَ لَهُ العُقُوبَةَ في الدُّنْيا، وَإِذَا أَرَادَ اللهُ بِعَبدِهِ الشَّرَّ أمْسَكَ عَنْهُ بذَنْبِهِ حَتَّى يُوَافِيَ بِهِ يومَ القِيَامَةِ)).

وَقالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم: ((إنَّ عِظَمَ الجَزَاءِ مَعَ عِظَمِ البَلاَءِ، وَإنَّ اللهَ تَعَالَى إِذَا أَحَبَّ قَوْمًا ابْتَلاَهُمْ، فَمَنْ رَضِيَ فَلَهُ الرِّضَا، وَمَنْ سَخِطَ فَلَهُ السُّخْطُ)). رواه الترمذي، وَقالَ: ((حديث حسن))

Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah Anapompendea khayr mja Wake, Humuharakishia adhabu duniani. Na anapomtakia shari mja Wake, Huzuia dhambi zake ili Amlipe siku ya Qiyaamah.”



Na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Malipo makubwa yapo pamoja na mitihani kubwa. Hakika Allaah Anapowapenda watu, Huwapa mitihani; atakayeridhika, basi atapata Radhi (za Allaah), na atakayechukia, atapata Hasira (za Allaah).” [At-Tirmidhiy, na amesema hadiyth hii ni Hassan]





Hadiyth – 20

وعن أنسٍ رضي الله عنه قَالَ: كَانَ ابنٌ لأبي طَلْحَةَ رضي الله عنه يَشتَكِي، فَخَرَجَ أبُو طَلْحَةَ، فَقُبِضَ الصَّبيُّ، فَلَمَّا رَجَعَ أَبُو طَلْحَةَ، قَالَ: مَا فَعَلَ ابْنِي؟ قَالَتْ أمُّ سُلَيم وَهِيَ أمُّ الصَّبيِّ: هُوَ أَسْكَنُ مَا كَانَ، فَقَرَّبَتْ إليه العَشَاءَ فَتَعَشَّى، ثُمَّ أَصَابَ منْهَا، فَلَمَّا فَرَغَ، قَالَتْ: وَارُوا الصَّبيَّ فَلَمَّا أَصْبحَ أَبُو طَلْحَةَ أَتَى رسولَ الله صلى الله عليه وسلم فَأخْبَرَهُ، فَقَالَ: ((أعَرَّسْتُمُ اللَّيلَةَ؟)) قَالَ: نَعَمْ، قَالَ: ((اللَّهُمَّ بَارِكْ لَهُمَا))، فَوَلَدَتْ غُلامًا، فَقَالَ لي أَبُو طَلْحَةَ: احْمِلْهُ حَتَّى تَأْتِيَ بِهِ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم، وَبَعَثَ مَعَهُ بِتَمَراتٍ، فَقَالَ: ((أَمَعَهُ شَيءٌ؟)) قَالَ: نَعَمْ، تَمَراتٌ، فَأخَذَهَا النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم فَمَضَغَهَا، ثُمَّ أَخَذَهَا مِنْ فِيهِ فَجَعَلَهَا في فِيِّ الصَّبيِّ، ثُمَّ حَنَّكَهُ وَسَمَّاهُ عَبدَ الله. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

وفي رواية للبُخَارِيِّ: قَالَ ابنُ عُيَيْنَةَ: فَقَالَ رَجُلٌ مِنَ الأَنْصارِ: فَرَأيْتُ تِسعَةَ أوْلادٍ كُلُّهُمْ قَدْ قَرَؤُوا القُرْآنَ، يَعْنِي: مِنْ أوْلادِ عَبدِ الله المَولُودِ.

وَفي رواية لمسلمٍ: مَاتَ ابنٌ لأبي طَلْحَةَ مِنْ أمِّ سُلَيمٍ، فَقَالَتْ لأَهْلِهَا: لا تُحَدِّثُوا أَبَا طَلْحَةَ بابْنِهِ حَتَّى أَكُونَ أَنَا أُحَدِّثُهُ، فَجَاءَ فَقَرَّبَتْ إِلَيْه عَشَاءً فَأَكَلَ وَشَرِبَ، ثُمَّ تَصَنَّعَتْ لَهُ أَحْسَنَ مَا كَانَتْ تَصَنَّعُ قَبْلَ ذلِكَ، فَوَقَعَ بِهَا. فَلَمَّا أَنْ رَأَتْ أَنَّهُ قَدْ شَبِعَ وأَصَابَ مِنْهَا، قَالَتْ: يَا أَبَا طَلْحَةَ، أَرَأَيتَ لو أنَّ قَومًا أعارُوا عَارِيَتَهُمْ أَهْلَ بَيتٍ فَطَلَبُوا عَارِيَتَهُمْ، أَلَهُمْ أن يَمْنَعُوهُمْ؟ قَالَ: لا، فَقَالَتْ: فَاحْتَسِبْ ابْنَكَ، قَالَ: فَغَضِبَ، ثُمَّ قَالَ: تَرَكْتِني حَتَّى إِذَا تَلطَّخْتُ، ثُمَّ أخْبَرتني بِابْنِي؟! فانْطَلَقَ حَتَّى أَتَى رسولَ الله صلى الله عليه وسلم فَأخْبَرَهُ بِمَا كَانَ فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((بَارَكَ اللهُ في لَيْلَتِكُمَا))، قَالَ: فَحَمَلَتْ. قَالَ: وَكانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم في سَفَرٍ وَهيَ مَعَهُ، وَكَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم إِذَا أَتَى المَدِينَةَ مِنْ سَفَرٍ لا يَطْرُقُهَا طُرُوقًا فَدَنَوا مِنَ المَدِينَة، فَضَرَبَهَا المَخَاضُ، فَاحْتَبَسَ عَلَيْهَا أَبُو طَلْحَةَ، وانْطَلَقَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم. قَالَ: يَقُولَ أَبُو طَلْحَةَ: إنَّكَ لَتَعْلَمُ يَا رَبِّ أَنَّهُ يُعْجِبُنِي أنْ أخْرُجَ مَعَ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم إِذَا خَرَجَ وَأَدْخُلَ مَعَهُ إِذَا دَخَلَ وَقَدِ احْتَبَسْتُ بِمَا تَرَى، تَقُولُ أُمُّ سُلَيْمٍ: يَا أَبَا طَلْحَةَ، مَا أَجِدُ الَّذِي كُنْتُ أجدُ انْطَلِقْ، فَانْطَلَقْنَا وَضَرَبَهَا المَخَاضُ حِينَ قَدِمَا فَوَلدَت غُلامًا. فَقَالَتْ لِي أمِّي: يَا أنَسُ، لا يُرْضِعْهُ أحَدٌ حَتَّى تَغْدُو بِهِ عَلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم، فَلَمَّا أصْبَحَ احْتَمَلْتُهُ فَانْطَلَقْتُ بِهِ إِلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم. وَذَكَرَ تَمَامَ الحَدِيثِ.

Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Alikuwa mtoto wa Abuu Twalhah akiugua. Abuu Twalahah akapata safari na kusafiri. Yule mtoto akafariki. Abuu Twalhah aliporudi”, aliuliza: “Vipi hali ya mwanangu?” Ummu Sulaym (mama wa mtoto) akamwambia: “Ametulia zaidi ya alivyokuwa.” Akampelekea chakula cha jioni akala, kisha akalala na mkewe (akamjamii). Alipomaliza, Ummu Sulaym akamwambi: “Kamzikeni mtoto.” Abuu Twalhah alipopambaukiwa, alikwenda moja kwa moja mpaka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamueleza yaliyotokea. Akamuuliza: “Usiku mlifanya tendo la ndoa?” Akajibu: “Ndiyo” Akaomba: “Ee Rabb, Wabarikie.” Akazaa mvulana. Abuu Twalhah akaniambia: “Mbebe na umepeleke kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akapeleka na tende kadhaa. Akauliza: “Ana kitu?” Akajibu: “Ndiyo, tende kadhaa.” Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akazichua na kuzitafuna, kisha akachukua zile tende zilizokuwa kinywani mwake akazitia kwenye kinywa cha mtoto, halafu akamsugua na kumpa jina la ’Abdullaah”. [Al-Bukhaariy na Muslim]

Riwaayah nyingine ya Al-Bukhaariy imesema: “Ibnu Uyaynah amesema: “Mtu mmoja katika Answaariy akasema: “Nikawaona watoto tisa, wote wamehifadhi Qur-aan.” Yaani watoto wa ‘Abdullaah huyu aliezaliwa.

Riwaayah nyingine ya Muslim imesema: “Abuu Twalhah alifiwa na mtoto aliyezaa naye kwa Ummu Sulaym akawaambia jamaa zake: “Msimueleze Abuu Twalhah habari ya mwanawe mpaka mimi niwe ndiye nitakaemueleza.” Akaja, akampelekea chakula jioni, akala na akanywa, halafu akajipamba kulikoni alivyojipamba siku zote. Akamjamii. Ummu Sulaym alipoona kuwa Abuu Twalhah ameshiba na amemjamii, alimwambia: “Ee Abuu Twalhah niambie lau watu wameazima kitu kwa watu fulani kisha hao watu wakataka kitu cha kilichoazimwa, je, wao wanahaki ya kuwanyima?” Akajibu: “Hapana.” Akamwambia: Basi taraji thawabu kwa msiba wa mwanao.” Abuu Twalhah akakasirika, na akasema: “Umeniwacha mpaka nimejichafua (kwa tendo la ndoa) halafu unaniambia habari ya mwanangu?” Akaenda kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamueleza mambo yalivyokuwa. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawaombea “Allaah Awabarikie katika usiku wenu.” Ummu Sulaym akabeba ujauzito. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa safarini pamoja na Ummu Sulaym. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapowasili Madiynah akitoka safari, alikuwa haingii usiku. Walipowasili Madiynah Ummu Sulaym alianza kuhisi uchungu wa uzazi, Abuu Twalhah alibaki nyuma, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaendelea na safari. Abuu Twalhah akasema: “Ee Rabb, hakika Unajua ya kuwa mimi hufurahishwa kusafiri pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anaposafiri, na hupenda kurudi pamoja nae anaporudi, na nimezuilika kama Uonavyo.” Ummu Sulaym akasema: “Ee Abuu Twalhah sisikii uchungu tena niliousikia, tuondoke.” Tukaondoka. Akapatwa na uchungu tena wa kuzaa tulipokuwa tumeshawasili Madiynah, akajifungua mtoto wa kiume. Mama yangu akaniambia: “Ee Anas, mtoto huyu asinyonyeshwe na yoyote mpaka uende nae kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).” Kulipopambauka, nilimbeba na kwenda nae kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ...” Akaendelea mpaka mwisho wa Hadiyth.





Hadiyth – 21

وعن أبي هريرةَ رضي الله عنه أنّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((لَيْسَ الشَّدِيدُ بالصُّرَعَةِ، إنَّمَا الشَدِيدُ الَّذِي يَملكُ نَفْسَهُ عِنْدَ الغَضَبِ)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mwenye nguvu si yule awashindae watu kwa miereka, bali mwenye nguvu ni yule anayemiliki nafsi yake wakati wa hasira.” [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 22

وعن سُلَيْمَانَ بن صُرَدٍ رضي الله عنه قَالَ: كُنْتُ جالِسًا مَعَ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، وَرَجُلانِ يَسْتَبَّانِ، وَأَحَدُهُمَا قدِ احْمَرَّ وَجْهُهُ، وانْتَفَخَتْ أوْدَاجُهُ، فَقَالَ رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم: ((إنِّي لأَعْلَمُ كَلِمَةً لَوْ قَالَهَا لَذَهَبَ عَنْهُ مَا يَجِدُ، لَوْ قَالَ: أعُوذ باللهِ منَ الشَّيطَانِ الرَّجِيمِ، ذَهَبَ عنْهُ مَا يَجِدُ)). فَقَالُوا لَهُ: إنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((تَعَوّذْ باللهِ مِنَ الشَّيطَانِ الرَّجِيمِ)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

Sulaymaan bin Swurad (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Nilikuwa nimekaa pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na watu wanatukanana, mmoja kati yao uso wake ulikuwa umeiva na mishipa yake ya shingoni imevimba. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Mimi nalijua neno, lau utalisema basi utaondokewa na hasira:



أعُوذ باللهِ منَ الشَّيطَانِ الرَّجِيمِ

“Aa’uwdhu biLLaahi mina shaytwaani rajiym (najilinda kwa Allaah dhidi ya shaytwaan aliyelaaniwa), ataondokewa na hasira.” Wakaenda wakamwambia kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekwambia ujikinge kwa Allaah kutokana na shaytwaan aliyelaaniwa.” [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 23

وعن معاذِ بنِ أَنسٍ رضي الله عنه أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((مَنْ كَظَمَ غَيظًا، وَهُوَ قَادِرٌ عَلَى أنْ يُنْفِذَهُ، دَعَاهُ اللهُ سُبحَانَهُ وَتَعَالى عَلَى رُؤُوسِ الخَلائِقِ يَومَ القِيامَةِ حَتَّى يُخَيِّرَهُ مِنَ الحُورِ العِينِ مَا شَاءَ)). رواه أَبو داود والترمذي، وَقالَ: (حديث حسن)

Mu’aadh bin Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema kuwa: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakaezuia hasira na akawa anaweza kuitekeleza, Allaah Atamuita siku ya Qiyaamah mbele ya halaiki ili Amchagulishe Huwrul ‘ayn anayemtaka.” [Abuu Daawud na At-Tirmidhiy, na amesema hadiyth hii ni Hasan]





Hadiyth – 24

وعن أبي هريرةَ رضي الله عنه: أنَّ رَجُلًا قَالَ للنبي صلى الله عليه وسلم: أوصِني. قَالَ: ((لا تَغْضَبْ)) فَرَدَّدَ مِرارًا، قَالَ: ((لاَ تَغْضَبْ)). رواه البخاري

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema kuwa: “Mtu mmoja alimwambia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Niusie.” Akamwambia: “Usighadhibike.” Akarudia ombi lake mara nyingi, (Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: “Usighadhibike.” [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 25

وعن أبي هريرة رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((مَا يَزَالُ البَلاَءُ بالمُؤمِنِ وَالمُؤْمِنَةِ في نفسِهِ ووَلَدِهِ وَمَالِهِ حَتَّى يَلْقَى الله تَعَالَى وَمَا عَلَيهِ خَطِيئَةٌ)). رواه الترمذي، وَقالَ: (حديث حسن صحيح)

Abuu Hurayrah (Rahwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) “Muumin hatowacha kupatwa na balaa katika nafsi yake, watoto wake na mali yake mpaka akutane na Allaah ilihali hana dhambi.” [At-Tirmidhiy, na amesema: Hadiyth hii ni Hasan Swahiyh]





Hadiyth – 26

وعن ابْنِ عباسٍ رضي الله عنهما قَالَ: قَدِمَ عُيَيْنَةُ بْنُ حِصْنٍ، فَنَزَلَ عَلَى ابْنِ أخِيهِ الحُرِّ بنِ قَيسٍ، وَكَانَ مِنَ النَّفَرِ الَّذِينَ يُدْنِيهِمْ عُمرُ رضي الله عنه، وَكَانَ القُرَّاءُ أصْحَابَ مَجْلِس عُمَرَ رضي الله عنه وَمُشاوَرَتِهِ كُهُولًا كانُوا أَوْ شُبَّانًا، فَقَالَ عُيَيْنَةُ لابْنِ أخيهِ: يَا ابْنَ أخِي، لَكَ وَجْهٌ عِنْدَ هَذَا الأمِيرِ فَاسْتَأذِنْ لِي عَلَيهِ، فاسْتَأذَن فَأذِنَ لَهُ عُمَرُ. فَلَمَّا دَخَلَ قَالَ: هِي يَا ابنَ الخَطَّابِ، فَواللهِ مَا تُعْطِينَا الْجَزْلَ وَلا تَحْكُمُ فِينَا بالعَدْلِ. فَغَضِبَ عُمَرُ رضي الله عنه حَتَّى هَمَّ أنْ يُوقِعَ بِهِ. فَقَالَ لَهُ الحُرُّ: يَا أميرَ المُؤْمِنينَ، إنَّ الله تَعَالَى قَالَ لِنَبيِّهِ صلى الله عليه وسلم: {خُذِ الْعَفْوَ وَأْمُرْ بِالْعُرْفِ وَأَعْرِضْ عَنِ الْجَاهِلِينَ} [الأعراف: 199] وَإنَّ هَذَا مِنَ الجَاهِلِينَ، واللهِ مَا جَاوَزَهاَ عُمَرُ حِينَ تَلاَهَا، وكَانَ وَقَّافًا عِنْدَ كِتَابِ اللهِ تَعَالَى. رواه البخاري

‘Abdullaah ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: “’Uyaynah bin Hiswn alikuja kutoka safari, akashukia kwa mtoto wa dada yake Al-Hurri bin Qays, naye alikuwa ni katika watu ambao ‘Umar alikuwa akiwakurubisha karibu naye, wanavyuoni walikuwa ndio wa majilisi ya ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) na katika ushauri wake; wawe ni wazee au vijana. ‘Uyaynah akamwambia mtoto wa dada yake: “Ee mtoto wa dada yangu, wewe una nafasi kwa huyu Amiyr, basi niombee idhini (niingie kwake).” Akamuombea idhini, ‘Umar akamruhusu. Alipoingia alisema: “Hii! Ee mwana wa Khattwaab! Wa-Allaahi hutupatii vitu vingi, wala huhukumu kwa audilifu kati yetu.” ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akakasirika hata akataka kumuadhibu. Al-Hurru akamwambia: “Ee Amiyr wa Waumini, hakika Allaah Alimwambia Nabiy Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)

خُذِ الْعَفْوَ وَأْمُرْ بِالْعُرْفِ وَأَعْرِضْ عَنِ الْجَاهِلِينَ

“Shikamana na usamehevu, na amrisha mema na jiepushe na majahili” [Al-A’raaf: 199]

Hakika huyu ni katika majahili. Basi wa-Allaahi ‘Umar hakumfanya kitu Al-Hurru alipoisoma Aayah hii. Alikuwa ‘Umar amesimama wima katika kitabu cha Allaah.” [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 26

وعن ابن مسعود رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إنَّهَا سَتَكونُ بَعْدِي أثَرَةٌ وأُمُورٌ تُنْكِرُونَها!)) قَالُوا: يَا رَسُول الله، فَمَّا تَأْمُرُنا؟ قَالَ: ((تُؤَدُّونَ الْحَقَّ الَّذِي عَلَيْكُمْ، وَتَسأَلُونَ الله الَّذِي لَكُمْ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

‘Abdullaah bin Mas’uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika baada yangu kutakuwepo ubinafsi na mambo ambayo hamtokubaliyana nayo.” Maswahaba wakauliza: “Yaa Rasula-Allaah, kwahiyo unatuamrisha tufanye nini?” Akawaambia: “Mutaitekeleza haki inayowapasa, na mumuombe Allaah ambacho ni chenu.” [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 27

وعن أبي يحيى أُسَيْد بن حُضَير رضي الله عنه: أنَّ رَجُلًا مِنَ الأنْصارِ قَالَ: يَا رسولَ الله، ألا تَسْتَعْمِلُني كَمَا اسْتَعْمَلْتَ فُلانًا؟ فَقَالَ: ((إنكُمْ سَتَلْقَونَ بَعْدِي أَثَرَةً فَاصْبِرُوا حَتَّى تَلْقَوني عَلَى الحَوْضِ)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

Abuu Yahyaa, Usayd bin Hudhwayr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Mtu mmoja katika Answaari alimwambia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Yaa Rasula-Allaah, mbona hunifanyi kuwa hakimu kama ulivyomfanya fulani?” Akamwambia: “Hakika baada yangu mtaona ubinasfi, basi subirini mpaka mkutane nami katika hodhi.” [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 28

وعن أبي إبراهيم عبدِ الله بن أبي أوفى رضي الله عنهما: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم في بعْضِ أيامِهِ التي لَقِيَ فِيهَا العَدُوَّ، انْتَظَرَ حَتَّى إِذَا مالَتِ الشَّمْسُ قَامَ فيهمْ، فَقَالَ: ((يَا أيُّهَا النَّاسُ، لا تَتَمَنَّوا لِقَاءَ العَدُوِّ، وَاسْأَلُوا الله العَافِيَةَ، فَإِذَا لقيتُمُوهُمْ فَاصْبرُوا، وَاعْلَمُوا أنّ الجَنَّةَ تَحْتَ ظِلالِ السُّيوفِ)). ثُمَّ قَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم: ((اللَّهُمَّ مُنْزِلَ الكِتَابِ، وَمُجْرِيَ السَّحَابِ، وَهَازِمَ الأحْزَابِ، اهْزِمْهُمْ وَانصُرْنَا عَلَيْهمْ)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

Abuu Ibraahiym ‘Abdillaah bin Abiy Awfa (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika baadhi ya siku alizokutana na adui, alingoja hadi jua lilipopinduka, akasimama na akawaeleza: “Enyi watu, msitamani kukutana na adui, muombeni Allaah al-‘afiyah (salama), na mtakapo kutana nao, subirini, na fahamuni kuwa Jannah ipo chini ya vivuli vya panga.” Halafu Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaomba: “Ee Rabb Mteremsha Kitabu, Mwenye kuendesha mawingu, Mwenye kuyashinda makundi, Washinde na Utunusuru.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
 
004-Riyaadhw Asw Swaalihiyn: Mlango Wa Ukweli

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب الصدق

004 – Mlango Wa Ukweli



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ

Enyi walioamini! Mcheni Allaah na kuweni pamoja na wakweli. [At-Tawbah: 119]

وَالصَّادِقِينَ وَالصَّادِقَاتِ

Na wanaume wakweli na wanawake wakweli. [Al-Ahzaab: 33]

فَلَوْ صَدَقُوا اللَّـهَ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ

Basi kama wangekuwa wakweli kwa Allaah, bila shaka ingalikuwa kheri kwao. [Muhammad: 21]



Hadiyth – 1



عن ابن مسعود رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((إنَّ الصِّدقَ يَهْدِي إِلَى البرِّ، وإنَّ البِرَّ يَهدِي إِلَى الجَنَّةِ، وإنَّ الرَّجُلَ لَيَصدُقُ حَتَّى يُكْتَبَ عِنْدَ اللهِ صِدِّيقًا. وَإِنَّ الكَذِبَ يَهْدِي إِلَى الفُجُورِ، وَإِنَّ الفُجُورَ يَهدِي إِلَى النَّارِ، وَإِنَّ الرَّجُلَ لَيَكْذِبُ حَتَّى يُكتَبَ عِنْدَ الله كَذَّابًا)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

‘Abdullaah bin Mas’uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amepokea kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa amesema: “Hakika ukweli unaongoza katika wema, na hakika wema unaongoza Jannah na mtu ataendelea kusema ukweli mpaka aandikiwe mbele ya Allaah kuwa ni mkweli. Na hakika uongo unaongoza katika uovu, na hakika uovu unapeleka motoni, na mtu ataendelea kusema uongo mpaka aandikiwe mbele ya Allaah kuwa ni muongo,” [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 2



عن أبي محمد الحسن بنِ عليِّ بن أبي طالب رضي الله عنهما قَالَ: حَفظْتُ مِنْ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((دَعْ مَا يَرِيبُكَ إِلَى مَا لا يَرِيبُكَ؛ فإنَّ الصِّدقَ طُمَأنِينَةٌ، وَالكَذِبَ رِيبَةٌ)). رواه الترمذي، وَقالَ: ((حديث صحيح))

Abuu Muhammad, Al-Hasan bin ‘Alliy bin Abiy Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: Nimehifadhi kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) maneno haya: “Acha linalokutia shaka ufuate lisilokutia shaka; hakika ukweli ni utulivu na uongo ni mashaka.” [At-Tirmidhiy, na amesema Hadiyth hii ni Hasan]





Hadiyth – 3

عن أبي سفيانَ صَخرِ بنِ حربٍ رضي الله عنه في حديثه الطويلِ في قصةِ هِرَقْلَ، قَالَ هِرقلُ: فَمَاذَا يَأَمُرُكُمْ؟ يعني: النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ أبو سفيانَ: قُلْتُ: يقولُ: ((اعْبُدُوا اللهَ وَحدَهُ لا تُشْرِكوُا بِهِ شَيئًا، وَاتْرُكُوا مَا يَقُولُ آبَاؤُكُمْ، ويَأْمُرُنَا بالصَلاةِ، وَالصِّدْقِ، والعَفَافِ، وَالصِّلَةِ)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

Abuu Sufyaan, Swakhr bin Harb (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia katika Hadiyth yake ndefu katika kisa cha Hiraqli (Heraclius). Hiraqli akauliza: Anawaamrisha nini? Yaani Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nikasema: Anatuambia: “Muabuduni Allaah Mmoja Pekee wala msimshirikishe kwa chochote. Na muwache walivyokuwa wakiabudu baba zenu.” Na akituamuru kuswali, kusema kweli, kujiepusha na machafu na kuunga undugu.” [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 4

عن أبي ثابت، وقيل: أبي سعيد، وقيل: أبي الوليد، سهل بن حُنَيْفٍ وَهُوَ بدريٌّ رضي الله عنه: أنَّ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((مَنْ سَأَلَ الله تَعَالَى الشَّهَادَةَ بِصِدْقٍ بَلَّغَهُ اللهُ مَنَازِلَ الشُّهَدَاءِ وَإِنْ مَاتَ عَلَى فِرَاشِهِ)). رواه مسلم

Abuu Thaabit, na inasemekana: Abiy Sa’iyd, na inasemekana: Abil Waliyd, Sahl bin Hunayf (Radhwiya Allaahu ‘anhu) naye ni mpiganaji wa vita vya Badr amesimulia kuwa: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayemuomba Allaah kufa kifo cha shaahid kwa ukweli, Allaah Atamfikisha daraja za Mashuhadaa hata akifa kitandani mwake.” [Muslim]





Hadiyth – 5

عن أبي هريرةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((غَزَا نبيٌّ مِنَ الأنْبِياءِ صَلَوَاتُ اللهِ وَسَلاَمُهُ عَلَيْهمْ فَقَالَ لِقَومهِ: لاَ يَتْبَعَنِّي رَجُلٌ مَلَكَ بُضْعَ امْرَأةٍ وَهُوَ يُريدُ أنْ يَبْنِي بِهَا وَلَمَّا يَبْنِ بِهَا، وَلا أحَدٌ بَنَى بُيُوتًا لَمْ يَرْفَعْ سُقُوفَهَا، وَلا أحَدٌ اشْتَرَى غَنَمًا أَوْ خَلِفَاتٍ وَهُوَ يَنْتَظِرُ أَوْلادَها. فَغَزا فَدَنَا مِنَ القَرْيَةِ صَلاةَ العَصْرِ أَوْ قَريبًا مِنْ ذلِكَ، فَقَالَ لِلشَّمْسِ: إِنَّكِ مَأمُورَةٌ وَأنَا مَأمُورٌ، اللَّهُمَّ احْبِسْهَا عَلَيْنَا، فَحُبِسَتْ حَتَّى فَتَحَ اللهُ عَلَيهِ، فَجَمَعَ الغَنَائِمَ فَجَاءتْ- يعني النَّارَ- لِتَأكُلَهَا فَلَمْ تَطعَمْها، فَقَالَ: إنَّ فِيكُمْ غُلُولًا، فَلْيُبايعْنِي مِنْ كُلِّ قَبيلةٍ رَجُلٌ، فَلَزِقَتْ يد رجل بِيَدِهِ فَقَالَ: فِيكُمُ الغُلُولُ فلتبايعني قبيلتك، فلزقت يد رجلين أو ثلاثة بيده، فقال: فيكم الغلول، فَجَاؤُوا بِرَأْس مثل رأس بَقَرَةٍ مِنَ الذَّهَبِ، فَوَضَعَهَا فَجاءت النَّارُ فَأكَلَتْها. فَلَمْ تَحلَّ الغَنَائِمُ لأحَدٍ قَبْلَنَا، ثُمَّ أحَلَّ الله لَنَا الغَنَائِمَ لَمَّا رَأَى ضَعْفَنا وَعَجْزَنَا فَأحَلَّهَا لَنَا)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kuna Nabiy mmoja alitaka kwenda kupigana jihaad, akawaambia qaumu yake: “Yeyote aliyeoa na hajamleta mkewe kwake lakini ana niyyah ya kufanya hivyo au yule aliyejenga kuta za nyumba lakini hajati paa, au yule aliyenunua mbuzi au ngami wenye mimba anangojea wazae, basi anifuate kwa kujiunga katika jihaad.” Baada ya hapo akaanza kuelekea na mujaahidina wake katika mji aliokusudia. Alipofika hapo karibu na mji karibu na Swalaah ya Alasiri, aliliambia jua: “Hakika wewe unafuata amri za Allaah, name nimeamrishwa, Ee Rabb, lizuie kwa ajili yetu.” Likazuiliwa mpaka Allaah Alipompa ushindi. Akazikusanya ghanima, moto ukaja ili upate kuziteketeza, lakini haukuweza kuziteketeza. Akawaambia: “Hakika kati yenu kuna aliyefanya khiyana, kwa hiyo katika kila kabila anbai (afunge kiapo cha ahadi) mtu mmoja.” Mkono wa mtu mmoja ukanata katika mkono wake. Akawaambia: “Kwenu kuna khiyana, kwa hivyo kabila lako lote linibai” Mikono ya watu wawili au watatu ikanata kwenye mkono wake.” Akawaambia: “Kwenu kuna khiyana,” Wakaleta dhahabu mfano wa kichwa cha ng’ombe. Yule Nabiy akaiweka, moto ukaja na ukaiteketeza. Ghanima haikuhalalishwa kwa yoyote kabla yetu. Kisha Allaah Akatuhalalishia ghanima Alipoona udhaifu wetu na ajizi yetu (na kukosa hila), Akatuhalalishia.” [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyh – 6

عن أبي خالد حَكيمِ بنِ حزامٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((البَيِّعَانِ بالخِيَار مَا لَمْ يَتَفَرَّقَا، فَإنْ صَدَقا وَبيَّنَا بُوركَ لَهُمَا في بيعِهمَا، وإنْ كَذَبَا وَكَتَمَا مُحِقَتْ بركَةُ بَيعِهِما)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Abuu Khaalid, Hakiym bin Hizaam (Radhwiya ALlaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amasema: “Wenye kuuziana wapo katika khiyari kabla hawajaachana. Watakaposema kweli na wakabainisha (kasoro au upungufu wa bidhaa), watabarikiwa katika biashara yao. Na wakificha na wakasema uongo; basi itaondolewa baraka ya biashara yao.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
 
005-Riyaadhw Asw-Swaalihiy

باب المراقبة

005 – Mlango Wa Kuchunga (Kukmhofu Allaah Kwa Siri Na Dhahiri)



Alhidaaya.com





قَالَ الله تَعَالَى:

الَّذِي يَرَاكَ حِينَ تَقُومُ

Ambaye Anakuona wakati unaposimama. [Ash-Shu’araa: 218]



وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ

Naye Yu Pamoja nanyi (kwa ujuzi Wake) popote mlipo. [Al-Hadiyd: 4]



هَلْ فِي ذَٰلِكَ قَسَمٌ لِّذِي حِجْرٍ

Je, hakuna katika hayo kiapo kwa mwenye welekevu (akawa na taqwa)? [Al-Fajr: 5]



إِنَّ رَبَّكَ لَبِالْمِرْصَادِ

Hakika Rabb wako bila shaka Yu tayari Awavizia. [Al-Fajr: 14]



يَعْلَمُ خَائِنَةَ الْأَعْيُنِ وَمَا تُخْفِي الصُّدُورُ

(Allaah) Anajua khiyana za macho na yale yanayoficha vifua. [Ghaafir: 19]





Hadiyth – 1

عن عمر بن الخطاب رضي الله عنه قَالَ: بَيْنَما نَحْنُ جُلُوسٌ عِنْدَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ذَاتَ يَومٍ، إذْ طَلَعَ عَلَينا رَجُلٌ شَديدُ بَياضِ الثِّيابِ، شَديدُ سَوَادِ الشَّعْرِ، لا يُرَى عَلَيهِ أثَرُ السَّفَرِ، وَلا يَعْرِفُهُ مِنَّا أحَدٌ، حَتَّى جَلَسَ إِلَى النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، فَأَسْنَدَ رُكْبَتَيهِ إِلَى رُكْبتَيهِ، وَوَضعَ كَفَّيهِ عَلَى فَخِذَيهِ.

وَقالَ: يَا مُحَمَّدُ، أخْبرني عَنِ الإسلامِ، فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((الإسلامُ: أنْ تَشْهدَ أنْ لاَّ إلهَ إلاَّ الله وَأنَّ مُحمَّدًا رسولُ الله، وتُقيمَ الصَّلاةَ، وَتُؤتِيَ الزَّكَاةَ، وَتَصومَ رَمَضَانَ، وَتَحُجَّ البَيتَ إن اسْتَطَعْتَ إِلَيْهِ سَبيلًا)). قَالَ: صَدَقْتَ. فَعَجِبْنَا لَهُ يَسْأَلُهُ وَيُصَدِّقهُ!

قَالَ: فَأَخْبرنِي عَنِ الإِيمَانِ. قَالَ: ((أنْ تُؤمِنَ باللهِ، وَمَلائِكَتِهِ، وَكُتُبهِ، وَرُسُلِهِ، وَاليَوْمِ الآخِر، وتُؤْمِنَ بالقَدَرِ خَيرِهِ وَشَرِّهِ)). قَالَ: صَدقت. قَالَ: فأَخْبرني عَنِ الإحْسَانِ. قَالَ: ((أنْ تَعْبُدَ اللهَ كَأنَّكَ تَرَاهُ فإنْ لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فإنَّهُ يَرَاكَ)).

قَالَ: فَأَخْبِرني عَنِ السَّاعَةِ. قَالَ: ((مَا المَسْؤُولُ عَنْهَا بأعْلَمَ مِنَ السَّائِلِ)). قَالَ: فأخبِرني عَنْ أمَاراتِهَا. قَالَ: ((أنْ تَلِدَ الأَمَةُ رَبَّتَهَا، وأنْ تَرَى الحُفَاةَ العُرَاةَ العَالَةَ رِعَاءَ الشَّاءِ يَتَطَاوَلُونَ في البُنْيَانِ)).

ثُمَّ انْطَلقَ فَلَبِثْتُ مَلِيًّا، ثُمَّ قَالَ: ((يَا عُمَرُ، أَتَدْري مَنِ السَّائِلُ؟)) قُلْتُ: اللهُ ورسُولُهُ أعْلَمُ. قَالَ: ((فإنَّهُ جِبْريلُ أَتَاكُمْ يعْلِّمُكُمْ دِينَكُمْ)). رواه مسلم

‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Siku moja tulikuwa tumekaa mbele ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kwa ghafla akatutokea mtu mmoja ambaye nguo zake zilikuwa nyeupe pepe na nywele zake zilikuwa nyeusi sana; hakuwa na alama ya machofu ya safari na wala hapakuwa na hata mmoja katika sisi aliyemtambua. Alienda akakaa karibu na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaweka magoti yake karibu na magoti yake (Rasuli) na akaweka viganja vyake juu ya mapaja yake kisha akasema; Ee Muhammad! Niambie kuhusu Uislaamu. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Uislamu ni kukiri kuwa hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, na Muhammad ni Rasuli wake, kusimamisha Swalaah, kutoa Zakaah, kufunga swawm Ramadhwaan na kwenda kuhiji (Makkah) ukiweza.” (Akasema yule mtu yaani Jibriyl): “Umesema kweli.” Tulipigwa na mshangao kwa kumuuliza kwake Rasuli na kumsadikisha. Na akasema tena: Niambie kuhusu Iymaan. Akasema: “Ni kumwamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Rasuli Wake na siku ya Qiyaamah, na kuamini Qadar (majaaliwa ya Allaah) ya kheri zake na shari zake.” (Akasema Jibriyl): “Umesema kweli.”. Akasema: “Hebu nielezee kuhusu Ihsaan.” Akasema Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Ni kumuabudu Allaah kama vile unamuona na kama humuoni basi Yeye Anakuona.” Akasema (Jibriyl): “Niambie kuhusu Qiyaamah.” Akajibu Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Muulizwaji si mjuzi kama asivyo vilevile Muulizaji.” Kisha akamwambia: “Nijulishe alama zake.”: Akajibu Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Kijakazi atazaa bibi yake, na utaona wachunga wenda miguu chini, wenda uchi (wasio na uwezo wa kumiliki hata mavazi), mafukara (wasiokuwa hata na sehemu ya kuishi kwa umaskini) wakishindana kujenga majumba ya fahari.” Kisha akaondoka (Jibriyl) na nilitulia kidogo (nikitafakari). Kisha akasema Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): "Ee 'Umar! Je, unamjua ni nani yule aliyekuwa akiuliza? Nikasema: Allaah na Rasuli wake wanajua zaidi. Akasema Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Ni Jibriyl, alikuja kuwafundisha dini yenu.” [Muslim]




Hadiyth – 2

عن أبي ذر جُنْدُب بنِ جُنادَةَ وأبي عبدِ الرحمنِ معاذِ بنِ جبلٍ رضي الله عنهما عن رسولِ الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((اتَّقِ الله حَيْثُمَا كُنْتَ وَأتْبعِ السَّيِّئَةَ الحَسَنَةَ تَمْحُهَا، وَخَالِقِ النَّاسَ بِخُلُقٍ حَسَنٍ)). رواه الترمذي، وَقالَ: (حديث حسن)

Abuu Dharr, Jundub bin Junaadah na Abuu ‘Abdir-Rahmaan Mu’aadh bin Jabal (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) wamehadithia kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mche Allaah popote ulipo, ufuatishe tendo jema baada ya tendo baya ili lifute, na utangamane na watu kwa tabia njema.” [At-Tirmidhiy, na amesema: Hadiyth hii ni Hasan]



Hadiyth – 3

عن ابنِ عباسٍ رضي الله عنهما، قَالَ: كنت خلف النَّبيّ صلى الله عليه وسلم يومًا، فَقَالَ: ((يَا غُلامُ، إنِّي أعلّمُكَ كَلِمَاتٍ: احْفَظِ اللهَ يَحْفَظْكَ، احْفَظِ اللهَ تَجِدْهُ تُجَاهَكَ، إِذَا سَألْتَ فَاسأَلِ الله، وإِذَا اسْتَعَنْتَ فَاسْتَعِنْ باللهِ. وَاعْلَمْ: أنَّ الأُمَّةَ لَوْ اجْتَمَعَتْ عَلَى أنْ يَنْفَعُوكَ بِشَيءٍ لَمْ يَنْفَعُوكَ إلا بِشَيءٍ قَدْ كَتَبهُ اللهُ لَكَ، وَإِن اجتَمَعُوا عَلَى أنْ يَضُرُّوكَ بِشَيءٍ لَمْ يَضُرُّوكَ إلا بِشَيءٍ قَدْ كَتَبَهُ اللهُ عَلَيْكَ، رُفِعَتِ الأَقْلاَمُ وَجَفَّتِ الصُّحفُ)). رواه الترمذي، وَقالَ: ((حديث حسن صحيح)).

وفي رواية غيرِ الترمذي: ((احْفَظِ الله تَجِدْهُ أَمَامَكَ، تَعرَّفْ إِلَى اللهِ في الرَّخَاءِ يَعْرِفكَ في الشِّدَّةِ، وَاعْلَمْ: أنَّ مَا أَخْطَأكَ لَمْ يَكُنْ لِيُصِيبكَ، وَمَا أصَابَكَ لَمْ يَكُنْ لِيُخْطِئَكَ، وَاعْلَمْ: أنَّ النَّصْرَ مَعَ الصَّبْرِ، وَأَنَّ الفَرَجَ مَعَ الكَرْبِ، وَأَنَّ مَعَ العُسْرِ يُسْرًا))

‘Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: Siku moja nilikuwa nyuma ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) (juu ya mnyama). Akaniambia: “Ee kijana, mimi nitakufundisha maneno: Mhifadhi Allaah Naye Atakuhifadhi. Mhifadhi Allaah utamkuta yupo mbele yako. Unapoomba, muombe Allaah. Unapotaka msaada, mtake Allaah. Fahamu kuwa, lau ummah (wote) utajikusanya ili wakunufaishe kwa jambo, basi hawataweza kukunufaisha ila kwa jambo Alilokuandikia Allaah; na wakijumuika ili wakudhuru kwa jambo, hawataweza kukudhuru ila kwa jambo Alilokuandikia Allaah. Kalamu zimeshasimama na karatasi zimeshakauka.” [At-Tirmidhiy, na amesema: Hadiyth hii ni Hasan Swahiyh]

Riwaayah nyingine isiyokuwa ya At-Tirmidhiy imesema: “Mhifadhi Allaah utamkuta Yupo mbele yako. Mjue Allaah katika raha Naye Atakujua katika shida. Ujue kuwa, lililokukosa halikuwa ni lenye kukupata, na lililokusibu halikuwa ni lenye kukukosa. Ujue kuwa nusura ipo pamoja na subira, faraja ipo pamoja na dhiki, na kwenye uzito kuna wepesi.”



Hadiyth – 4

عن أنسٍ رضي الله عنه قَالَ: إِنَّكُمْ لَتعمَلُونَ أعْمَالًا هي أدَقُّ في أعيُنِكُمْ مِنَ الشَّعْرِ، كُنَّا نَعُدُّهَا عَلَى عَهْدِ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم مِنَ المُوبِقاتِ. رواه البخاري

Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Kwa hakika ninyi mnafanya matendo ambayo machoni mwenu (mnayaona kuwa) ni madogo kulikoni unywele. Kwa hakika matendo hayo tulikuwa tukiyahesabu wakati wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni matendo yanayoangamiza.” [Al-Bukhaariy]



Hadiyth – 5

عن أبي هريرةَ رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إنَّ الله تَعَالَى يَغَارُ، وَغَيرَةُ الله تَعَالَى، أنْ يَأتِيَ المَرْءُ مَا حَرَّمَ الله عَلَيهِ)). متفق عَلَيه

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah Hufanya ghera, na ghera ya Allaah ni mtu kutenda Aliyoharamisha Allaah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]



Hadiyth – 6

عن أبي هريرةَ رضي الله عنه: أنَّه سَمِعَ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم، يقُولُ: ((إنَّ ثَلاثَةً مِنْ بَني إِسْرَائِيلَ: أبْرَصَ، وَأَقْرَعَ، وَأَعْمَى، أَرَادَ اللهُ أنْ يَبْتَليَهُمْ فَبَعَثَ إِليْهمْ مَلَكًا، فَأَتَى الأَبْرَصَ، فَقَالَ: أَيُّ شَيءٍ أَحَبُّ إلَيْكَ؟ قَالَ: لَوْنٌ حَسنٌ، وَجِلدٌ حَسَنٌ، وَيَذْهبُ عَنِّي الَّذِي قَدْ قَذِرَنِي النَّاسُ؛ فَمَسَحَهُ فَذَهَبَ عَنْهُ قَذَرُهُ وَأُعْطِيَ لَونًا حَسنًا وجِلْدًا حَسَنًا. فَقَالَ: فَأيُّ المَالِ أَحَبُّ إِليكَ؟ قَالَ: الإِبلُ- أَوْ قالَ: البَقَرُ شكَّ الرَّاوي- فَأُعطِيَ نَاقَةً عُشَرَاءَ، فَقَالَ: بَاركَ الله لَكَ فِيهَا. فَأَتَى الأَقْرَعَ، فَقَالَ: أَيُّ شَيءٍ أَحَبُّ إلَيْكَ؟ قَالَ: شَعْرٌ حَسَنٌ، وَيَذْهَبُ عَنِّي هَذَا الَّذِي قَذِرَني النَّاسُ؛ فَمَسَحَهُ فَذَهبَ عَنْهُ وأُعْطِيَ شَعرًا حَسَنًا. قالَ: فَأَيُّ المَالِ أَحَبُّ إِليْكَ؟ قَالَ: البَقَرُ، فَأُعْطِيَ بَقَرَةً حَامِلًا، وَقالَ: بَارَكَ الله لَكَ فِيهَا.

فَأَتَى الأَعْمَى، فَقَالَ: أَيُّ شَيءٍ أَحَبُّ إِلَيْكَ؟ قَالَ: أَنْ يَرُدَّ الله إِلَيَّ بَصَرِي فَأُبْصِرُ بِهِ النَّاسَ؛ فَمَسَحَهُ فَرَدَّ اللهُ إِلَيْهِ بَصَرهُ. قَالَ: فَأَيُّ المَالِ أَحَبُّ إِليْكَ؟ قَالَ: الغَنَمُ، فَأُعْطِيَ شَاةً والدًا، فَأَنْتَجَ هذَانِ وَوَلَّدَ هَذَا، فَكانَ لِهذَا وَادٍ مِنَ الإِبلِ، وَلِهذَا وَادٍ مِنَ البَقَرِ، وَلِهَذَا وَادٍ مِنَ الغَنَمِ.

ثُمَّ إنَّهُ أَتَى الأَبْرَصَ في صُورَتِهِ وَهَيئَتِهِ، فَقَالَ: رَجلٌ مِسْكينٌ قَدِ انقَطَعَتْ بِيَ الحِبَالُ في سَفَري فَلا بَلاغَ لِيَ اليَومَ إلا باللهِ ثُمَّ بِكَ، أَسْأَلُكَ بِالَّذي أعْطَاكَ اللَّونَ الحَسَنَ، والجِلْدَ الحَسَنَ، وَالمَالَ، بَعِيرًا أَتَبَلَّغُ بِهِ في سَفَري، فَقَالَ: الحُقُوقُ كثِيرةٌ. فَقَالَ: كأنِّي اعْرِفُكَ، أَلَمْ تَكُنْ أَبْرَصَ يَقْذَرُكَ النَّاسُ فقيرًا فأعْطَاكَ اللهُ!؟ فَقَالَ: إِنَّمَا وَرِثْتُ هَذَا المالَ كَابِرًا عَنْ كَابِرٍ، فَقَالَ: إنْ كُنْتَ كَاذِبًا فَصَيَّرَكَ الله إِلَى مَا كُنْتَ.

وَأَتَى الأَقْرَعَ في صُورَتِهِ وَهَيْئَتِهِ، فَقَالَ لَهُ مِثْلَ مَا قَالَ لِهَذا، وَرَدَّ عَلَيهِ مِثْلَ مَا رَدَّ هَذَا، فَقَالَ: إنْ كُنْتَ كَاذِبًا فَصَيَّرَكَ اللهُ إِلَى مَا كُنْتَ.

وَأَتَى الأَعْمَى في صُورَتِهِ وَهَيْئَتِهِ، فَقَالَ: رَجُلٌ مِسْكينٌ وابنُ سَبيلٍ انْقَطَعتْ بِيَ الحِبَالُ في سَفَرِي، فَلا بَلاَغَ لِيَ اليَومَ إلا بِاللهِ ثُمَّ بِكَ، أَسأَلُكَ بالَّذِي رَدَّ عَلَيْكَ بَصَركَ شَاةً أَتَبَلَّغُ بِهَا في سَفري؟ فَقَالَ: قَدْ كُنْتُ أعمَى فَرَدَّ اللهُ إِلَيَّ بَصَرِي فَخُذْ مَا شِئْتَ وَدَعْ مَا شِئْتَ فَوَ اللهِ لا أجْهَدُكَ اليَومَ بِشَيءٍ أخَذْتَهُ للهِ- عز وجل-. فَقَالَ: أمْسِكْ مالَكَ فِإنَّمَا ابْتُلِيتُمْ. فَقَدْ رضي الله عنك، وَسَخِطَ عَلَى صَاحِبَيكَ)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amemsikia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Allaah Alitaka kuwapa mtihani watu watatu katika wana Israaiyl: Mwenye ukoma, mwenye kunyonyoka nywele (kipara) na kipofu. Akawapelekea Malaaika. Akamwendea mwenye ukoma. Akamuuliza: “Kitu gani unachokipenda zaidi?” Akamjibu: “Napenda niwe na rangi nzuri, ngozi nzuri na niondokewe na hali hii ambayo watu wananidharau.” Yule Malaaika akampangusa, ukoma ukamuondokea na akapewa rangi na ngozi nzuri. Akamuuliza: “Unapenda mali gani?” Akajibu: “Ngamia.”. Au alisema: Ng’ombe, (mpokezi amekuwa na mashaka kama ni ng’ombe au ngamia). Akapewa ngamia mwenye mimba (karibu na kuzaa). Akamuombea: “Allaah Akubariki”.

Akamuendea mwenye upara. Akamuuliza: “Kitu gani unachokipenda zaidi?” Akamjibu: “Nywele nzuri, na niondokewe na hali hii ambayo watu wananidharau.” Akampangusa, akaondokewa na upara na akawa na nywele nzuri. Akamuuliza: “Unapenda mali gani?” Akamjibu: “Ng’ombe.” Akapewa ng’ombe mwenye mimba. Akamuombea: “Allaah Akubarikie.” Akamuendea kipofu akamuuliza: “Kitu gani unachonapenda zaidi?” Akamjibu: “Napenda Allaah Anirudishie macho yangu ili nione watu.” Akampangusa. Allaah Akamrudishia macho yake. Akamuuliza. “Unapenda mali gani?” Akamjibu: “Mbuzi.” Akapewa mbuzi mwenye mtoto. Wale wenye ngamia na ng’ombe wanyama wao wakazaa, na mwenye mbuzi nae akazalisha. Mmoja wao akawa na bonde lililojaa ngamia, na mwengine ana bonde lililojaa ng’ombe na huyu ana bonde lililojaa mbuzi. Kisha, akamuendea mwenye ukoma katika sura yake na umbile lake (kama siku ile aliyokutana nae kwanza). Akamwambia: “Mimi ni masikini, rizki imenikatikia safarini, sina njia leo, (sina matumaini) isipokuwa kwa Allaah kisha kwako. Nakuomba kwa Ambaye Amekupa rangi nzuri, ngozi nzuri na mali, unipe ngamia ili nimalize safari yangu.” Akamjibu: “Haki zipo nyingi (nina majukumu mengi, kwa hiyo siwezi kukusaidia). Akamwambia: “Kana kwamba nakujua, si ulikuwa na ukoma na watu wanakudharau na ulikuwa fukara, na Allaah Akakupa?” Akamwambia: “Mali hii nimerithi kutoka kwa mababu na mababu.” Akamwambia: “Ikiwa unasema uongo, Allaah Akurudishe kama ulivyokuwa.” Akamuendea mwenye upara katika sura yake na umbile lake (kama siku ile aliyokutana naye kwa mara ya kwanza). Akamwambia kama alivyomwambia wa mwanzo. Naye akamrudishia jibu kama alivyomrudishia wa mwanzo. Akamwambia: “Ikiwa unasema uongo, Allaah Akurudishe kama ulivyokuwa.” Akamuendea kipofu katika sura yake na umbile lake (kama siku ile aliyokutana naye kwa mara ya kwanza). Akamwambia: “Mimi ni masikini, rizki imenikatikia safarini, sina njia leo, (sina matumaini) isipokuwa kwa Allaah kisha kwako. Nakuomba kwa Ambaye Amekurudishia macho yako, unipe mbuzi ili nimalizie safari yangu.” Akamjibu: “Kwa hakika nilikuwa kipofu, Allaah Akanirudishia kuona kwangu. Chukua unachotaka, wacha unachotaka. Wa-Allaahi sikufanyia uzito kwa kitu ulichokichukua kwa Ajili ya Allaah.” Akamwambia “Zuia mali yako. Hakika mumepewa mtihani. Hakika Allaah Ameshakuridhia na Amewaghadhibikia wenzio wawili.” [Al-Bukhaariy na Muslim]



Hadiyth – 7

عن أبي هريرة رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((مِنْ حُسْنِ إسْلامِ المَرْءِ تَرْكُهُ مَا لا يَعْنِيهِ)). حديث حسن. رواه الترمذي وغيرُه

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Katika uzuri wa Uislaamu wa mtu, ni kuacha lisilomuhusu.” [Hadiyth hii ni Hasan. At-Tirmidhiy na wengine]



Hadiyth – 8

عن عُمَرَ رضي الله عنه عَنِ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((لا يُسْأَلُ الرَّجُلُ فِيمَ ضَرَبَ امْرَأَتَهُ)). رواه أبو داود وغيره

‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mtu haulizwi sababu ya kumpiga mkewe.” [Abuu Dawuud na wengineo]
 
Skip to main
Akienda Kazini ndio talaka Yake – Mume Hamhudumii yeye wala watoto wake Afanyeje?
Maswali: Talaka - Eda


SWALI:


InshaAllaah mungu akulipeni kheri duniani na akhera kwa msaada wenu. Mimi nina rafiki yangu mume wake amimuabia akitoka kuenda kazini ndio talaka yake, na huyo mume wenyewe hamtizami kwa chochote si yeye wala watoto na pia kuna wazee wake wanamtegemea. Wamembiwa wazee waseme naye lakini msimamo wake uko pale pale. Je, afanye nini?






JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa ndugu yetu muulizaji swali. Hakika ni kuwa tumekuwa tukilizungumzia suala hili mara kadhaa. Hili ni tatizo ambalo limezagaa katika jamii yetu kwa kiasi kikubwa sana. Hili tatizo linarudi kwa wazazi na pia wanandoa ambao wameshindwa kufuata muongozo wa Kiislamu katika kuchagua mwenzi wa maisha.


Uislamu umetuekea sifa za kuchagua mwenza ambaye mtasaidiana kwa hali na mali, furaha na huzuni, shida na raha. Kukosa kufanya hivyo na kutoafikiana hapo mbeleni ndio kunatokea matatizo aina hii. Lau mke angekuwa ni mwenye kuweka masharti yanayokubaliwa katika ndoa mushkeli kama huu haungekuwa ni wenye kutokea na lau ungetoka basi ingekuwa rahisi kusuluhisha. Kwa hali zote tatizo tayari limetokea kwetu ni kutoa nasaha ili hali za wanandoa ziwe njema na nzuri.


Hilo ni tatizo la unyumba na mume ameacha majukumu aliyopewa na Allaah Aliyetukuka. Hivyo, ni vyema kutumia njia zilizopangwa na sheria ili kutatua tatizo hilo. Jambo la kwanza ambalo mke anafaa kufanya ni kujaribu kukaa kitako yeye na mumewe ili wazungumze ki-uanandoa na kutatua tatizo hilo dogo sana. Ikiwa haikuwezekana basi mke itabidi aitishe kikao ambacho kitajumlisha kuwepo yeye, mumewe, wawakilishi wa mume na mke ili wajadili suala hilo kwa kutaka suluhisho. Ikiwa kweli nia ni kutaka kutatua mushkeli basi Allaah Aliyetukuka Ataleta suluhisho la kudumu baina yao. Lau kila mmoja atavutia kwake basi tatizo hilo litabakia nao mpaka waache na kila mmoja apate mwingine mwenye kheri naye.


Ikiwa hilo halikuleta natija yoyote, basi itabidi uende mbele ukashitaki kwa Qaadhi kwa kumuelezea yote yanayojiri. Sijui kama hapo mnapoishi wapo ma-Qaadhi au vipi? Ikiwa hawapo basi unaweza kwenda kwa Shaykh anayetegemewa na muadilifu umweleze shida yake yote. Qaadhi au Shaykh huyo atamwita mumeo nawe pia utakuwepo ili apate kusikiliza pande zote mbili na baada ya hapo kutoa uamuzi muafaka. Suala la kutoa nafaka kwa mke ni suala ambalo Qaadhi anaweza kumuachisha mke kutoka kwa mume wake.


Twatumai kwa kufuata hayo yaliyo juu atapata ufumbuzi wa suala hilo na tatizo lake kusuluhishwa kwa njia nzuri.




Na Allaah Anajua zaidi
 
Akiwa Amemdanganya Mumewe Atakuwa Ametalikika (Talaka)?
Maswali: Talaka - Eda


SWALI

Assalam aleikum,
Nina watoto watatu nimezaa kila mwaka na watoto wangu wa wili wa mwisho nimezaa kwa operation.niko kwenye nchi ambayo sina msaada wowote kwa yeyote hata mume wangu hanisaidii sina nguvu za kuzaa kwa sasa watoto wangu bado wadogo. Mume wangu alinipa ruhusa kutumia family planning kwa miezi sita sasa amenilazimisha niwache kutumia. Nimemdanganya kumwambia kuwa nishawacha asema kama sio ukweli ameniacha jee talaka imepita




JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwish

Mas-ala ya family planning kwa dharura inaruhusiwa katika sheria ya Kiislamu lakini hapa si mahali pake kwani katika suala hili limejibiwa kwa kina katika viungo vifuatavyo:

Kupanga Uzazi Na Sio Kuzuia Uzazi

Njia Gani Inayopasa Katika Sheria; Kuzuia Au Kupanga Uzazi?

Kuzuia Mimba Na Madhara Yake

Inafaa Kufunga Uzazi Kwa Sababu Ya Umri Mkubwa?

20 Kuhalalishwa ‘Azl (Kuchopoa Kabla Ya Kushusha)

21 Kutofanya ‘Azl Ni Bora Zaidi

Kuhusu mas-ala ya talaqa kwa hakika huwa mara nyingi wanaume wanachukulia ni kama mchezo lakini talaqa si jambo la mchezo hata ukisema kwa dhihaka huwa talaqa imepita. Ama wewe ukiwa umemdanganya na hiyo talaqa yake imeegemea kwenye sharti, hivyo sharti hiyo ikipatikana inakuwa talaqa imepita kama katika mfano uliotoa.

Kwa hivyo, nyinyi wawili si mume na mke tena lakini bado mnaweza kurudiana.

Hakika ni kuwa mume na mke wanatakiwa wawe makini na wawe wakweli baina yao la si hivyo ndoa itavurugika. Nasaha kwa dada yetu ni kuwa akae na mume wake amueleze ukweli na kuwa hatarudia kosa hilo ili waweze kurudiana kama mume na mke kama awali. Ikiwa miezi mitatu haijamaliza mume anaweza kumrudia bila mahari mapya wakawa wanaishi kama mume na mke. Lakini ikiwa miezi mitatu imepita itabidi mfunge nikaha upya na mahari mapya na kwa kuwa wewe ndio umefanya makosa na unataka kuishi na mumeo unaweza kumsamehe mahari hayo.



Baada ya hapo sasa kwa sababu za kiafya ambazo huenda zikakuletea shida unaposhika mimba itakuwa ni bora uweze kuzungumza na mumeo na umueleze shida unayopata. Ikiwa mumeo ni Muislamu mzuri na barabara itakuwa ni rahisi sana kuelewana na kukubalia kutumia njia ya kuzuia kizazi. Ikiwa pia mumeo ni binadamu basi atakufikiria na hatataka uingie katika shida.



Na nasaha nyingine ambayo inaweza kukusaidia katika kupanga uzazi ni kunyonyesha kwa muda wa miaka miwili ambapo itakufanya usiingie damuni kwa muda wa kunyonyesha hivyo kutoshika mimba. Japokuwa ufanisi wa kufanya hivi unapatikana kwa 50% peke ya wanawake. Wapo wanawake wanaonyoyesha na bado wanaingia ada yao ya mwezi kama kawaida.

Na Allah Anajua zaidi.
 
Alimuoa Mwanamke Bila Ya Kumpenda Ila Ameshika Dini Sana, Sasa Hana Raha Naye, Ana Khofu Kumuacha
Maswali: Talaka - Eda
SWALI:



Assalaam aleikum.



Mimi ni kijana wa miaka 32, miezi michache iliyopita nilioa binti ambaye kwa hakika mi sijampenda sana, na nilimuoa hasa kutokana na ushawishi nilioupata kutoka kwa watu wangu wa karibu na huruma niliyokuwa nae baada ya kutaka kumwacha nisimuoe nae alihuzunika sana, ila kusema ukweli binti ameshika dini kisawasawa hata kunizidi mimi. Sasa bahati mbaya kwa sasa sina raha kabisa kuwa nae na hata wakati tunakutana kama mke na mume mi hamu zote sina na najihisi karaha, nafikiria kumwacha ila nakosa hoja ya kushika, nahisi kama nitamwacha kwa sababu hiyo watu watasema kwa nini umemuoa mtu usiyempenda. Naomba mnisaidie nifanye nini?



JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kumuoa mwanamke usiyempenda.

Hakika mwanaadamu huenda akachukia jambo na likawa na kheri ndani yake kama Alivyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Kadhalika mwanamke mwenye sifa kama hiyo uliyoitaja ndio sifa ambazo Mtume wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alizipendekeza na akatusisitiza tuolee kwazo. Na wewe umebahatika kulipata hilo lakini inasikitisha kuona kuwa hujaridhika na unapata karaha! Je, karaha ni za nini? Maumbile? Chumbani? Au ni nini zaidi?





Jambo la pekee ambalo unaweza kufanya ni kumuomba Allaah Aliyetukuka katika Swawm zako na Swalah za usiku akupatie mahaba kwa mke aliyeshika Dini kama huyo.



Na kwa kuwa ana mazuri mengi inafaa ujipatie moyo kuwa karaha hiyo itaondoka. Allaah Aliyetukuka Anasema:

“Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Allaah Ametia kheri nyingi ndani yake” (An-Nisaa’ [4]: 19).

Au njia nyingine ni wewe ukiwa umeshindwa kabisa kuishi naye na unaona utafanya dhuluma kwake na kwa Diyn yako, basi litakalofuatia ni kumpatia talaka, kwani hiyo ndio njia iliyowekwa na Allaah Aliyetukuka ikiwa wanandoa hawapendani. Na kwa kuwa wewe humpendi na ndiye mwenye talaka inafaa umtaliki na si lazima katika kumuacha utoe sababu bali ni riziki ya kuishi pamoja imeisha. Na ikiwa mtafanya hivyo, basi Allaah Aliyetukuka Atampatia kila mmoja wenu wapili wake watakaoridhiana.



Tunakuombea kila la kheri katika kuchagua lenye busara na jema. Na ikiwa imepita talaka basi usiingie katika dhulma nyingine kwa kuoa mke kwa kushawishiwa.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Back
Top Bottom