Ramadhan Special Thread
20-Je, Inajuzu kustaghithi (kuomba uokovu) maiti na wasiokuwepo?



Hapana! Haijuzu kustaghithi kwa maiti na wasiokuwepo, bali tustaghithi (tuombe uokovu) kwa Allaah.



إِذْ تَسْتَغِيثُونَ رَبَّكُمْ فَاسْتَجَابَ لَكُمْ

Na (kumbukeni) pale mlipomuomba uokovu Rabb wenu Naye Akakuitikieni [Al-Anfaal: 9]



((كَانَ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا أصابه هَمٌّ أَوْ غَمٌّ قَالَ: ((يَا حيُّ يَا قيّوم برحمتك أستغيث)) رواه الترمذي

Alikuwa (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anapofikwa na wahka au dhiki husema: ((Yaa Hayyu Yaa Qayyuwm bi Rahmatika astaghiythu - Ee Uliye hai daima, Msimamia wa kila kitu, kwa rahmah Zako naomba uokozi)) [At-Tirmidhy Hadiyth Hasan]
 
Naam kuhusu aqydah tuna darsa mpaka nambari 60,,,kwahiyo ni wewe tu kufuatilia huu uzi

Sasa tuhamie katika darsa la swalaa ya Nabii swallallahu alaih wasallam
 
046-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kumswalia Mtume Pahala Pake Na Matamshi Yake Mbali Mbali



KUMSWALIA MTUME PAHALA PAKE NA MATAMSHI YAKE MBALI MBALI




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akijiswalia mwenyewe katika Tashahhud ya kwanza na nyingineo([1]). Na akaifanya kuwa ni amrisho kwa Ummah wake, kwani aliwaamrisha kumswalia yeye baada ya kumuombea amani([2]), na aliwafundisha matamshi mbali mbali ya kumswalia.

1-


Allaahumma Swalli ‘Alaa Muhammadin, Wa ‘Alaa Ahli Baytihi, Wa ‘Alaa Az-Waajihi Wa Dhurriyaatihi, Kamaa Swallayta ‘Alaa Aali Ibraahiyma, Inaka Hamiydun Majiydun, Wa Baarik ‘Alaa Muhammadin, Wa ‘Alaa Aali Baytihi, Wa ‘Alaa Az-Waajihi Wa Dhurriyaatihi, Kamaa Baarakta ‘Alaa Aali Ibraahiyma, Inaka Hamiydun Majiydun



Ee Allaah! Mswalie Muhammad([3]) Na Watu Wa Nyumbani Kwake, Na Wake Zake, Na Kizazi Chake Kama Ulivyowaswalia Jamaa Zake Ibraahiym, Hakika Wewe Ni Mwenye Kusifika Mtukufu. Na Mbariki Muhammad([4]) Na Jamaa Wa Nyumba Yake, Na Wake Zake, Na Kizazi Chake Kama Uliyowabariki Jamaa Zake Ibraahiym, Hakika Wewe Ni Mwenye Kusifika Mtukufu.




Du'aa hii alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiitumia kwa kuomba yeye mwenyewe([5]).

2-





Allaahumma Swalli ‘Alaa Muhammadin, Wa ‘Alaa Aali Muhammadin, Kamaa Swallayta ‘Alaa [Ibraahiyma, Wa ‘Alaa] Aali Ibraahiyma, Inaka Hamiydun Majiydun, Allaahumma Baarik ‘Alaa Muhammadin, Wa ‘Alaa Aali Muhammadin, Kamaa Baarakta ‘Alaa [Ibraahiyma Wa ‘Alaa] Aali Ibraahiyma, Inaka Hamiydun Majiydun



Ee Allaah! Mswalie Muhammad, Na Jamaa Wa Muhammad, Kama Ulivyomswalia [Ibraahiym Na Juu Ya]([6]) Jamaa Zake Ibraahiym, Hakika Wewe Ni Mwenye Kusifika Mtukufu. Ewe Allaah! Mbariki Muhammad Na Jamaa Zake Muhammad Kama Ulivyombariki [Ibraahiym Na Juu Ya]([7]), Jamaa Zake Ibraahiym, Hakika Wewe Ni Mwenye Kusifika Mtukufu.([8])




3-


Allaahumma Swalli ‘Alaa Muhammadin, Wa ‘Alaa Aali Muhammadin, Kamaa Swallayta ‘Alaa Ibraahiyma [Wa Aali Ibraahiyma], Inaka Hamiydun Majiydun, Wa Baarik ‘Alaa Muhammadin, Wa ‘Alaa Aali Muhammadin, Kamaa Baarakta ‘Alaa [Ibraahiyma Wa] Aali Ibraahiyma, Inaka Hamiydun Majiydun



Ee Allaah! Mswalie Muhammad Na Jamaa Zake Muhammad Kama Ulivyomswalia Ibraahiyhm [Na Jamaa Zake Ibraahiym], Hakika Wewe Ni Mwenye Kusifika Mtukufu. Na Mbariki Muhammad Na Jamaa Zake Muhammad Kama Ulivyombariki [Ibraahiym Na] Jamaa Zake Ibraahiym Hakika Wewe Ni Mwenye Kusifika Mtukufu.([9])




4-


Allaahumma Swalli ‘Alaa Muhammadin [An Nabiyyil Ummiyyi], Wa ‘Alaa Aali Muhammadin, Kamaa Swallayta ‘Alaa [Aali] Ibraahiyma, Wa Baarik ‘Alaa Muhammadin [An Nabiyyil Ummiyyi], Wa ‘Alaa Aali Muhammadin, Kamaa Baarakta ‘Alaa [Aali] Ibraahiyma Fil ‘Aalamiyna, Inaka Hamiydun Majiydun



Ee Allaah! Mswalie Muhammad [Nabii Ummiy (Asiyejua Kusoma Au Kuandika)] Na Jamaa Zake Muhammad Kama Ulivyowaswalia [Jamaa Zake] Ibraahiym, Na Mbariki Muhammad [Nabii Ummiy] Na Jamaa Zake Muhammad Kama Ulivyowabariki [Jamaa Zake] Ibraahiym Miongoni Mwa Ummah, Hakika Wewe Ni Mwenye Kusifika Mtukufu.([10])







5-





Allaahumma Swalli ‘Alaa Muhammadin ‘Abdika Wa Rasuulika, Kamaa Swallayta ‘Alaa [Aali] Ibraahiyma, Wa Baarik ‘Alaa Muhammadin [‘Abdika Wa Rasuulika], [Wa ‘Alaa Aali Muhammadin], Kamaa Baarakta ‘Alaa Ibraahiyma [Wa ‘Alaa Aal Ibraahiyma]



Ee Allaah! Mswalie Muhammad Mja Wako Na Mjumbe Wako Kama Ulivyowaswalia [Jamaa Zake] Ibraahiym, Na Mbariki Muhammad [Mja Wako Na Mjumbe Wako] [Na Jamaa Zake Muhammad] Kama Ulivyowabariki Jamaa Zake Ibraahiym [Na Jamaa Zake Ibraahiym]([11])




6-





Allaahumma Swalli ‘Alaa Muhammadin, Wa [‘Alaa] Az-Waajihi Wa Dhurriyaatihi, Kamaa Swallayta ‘Alaa [Aali] Ibraahiyma, Wa Baarik ‘Alaa Muhammadin, Wa [‘Alaa] Az-Waajihi Wa Dhurriyaatihi, Kamaa Baarakta ‘Alaa [Aali] Ibraahiyma, Inaka Hamiydun Majiydun



Ee Allaah! Mswalie Muhammad Na Wake Zake Na Kizazi Chake, Kama Ulivyowaswalia [Jamaa Zake] Ibraahiym, Na Mbariki Muhammad Na Wake Zake Na Kizazi Chake Kama Ulivyowabariki [Jamaa Zake] Ibraahiym, Hakika Wewe Ni Mwenye Kusifika Mtukufu.([12])







7-


Allaahumma Swalli ‘Alaa Muhammadin Wa ‘Alaa Aal
Muhammaadin, Wa Baarik ‘Alaa Muhammadin, Wa ‘Alaa Aal Muhammadin, Kamaa Swallayta ‘Alaa Ibraahiyma Wa ‘Alaa Aal Ibraahiyma Inka Hamiydin Majiydun




Ee Allaah! Mswalie Muhammad Na Jamaa Zake Muhammad, Na Mbariki Muhammad Na Jamaa Zake Muhammad Kama Ulivyomswalia Na Ukambariki Ibraahiym Na Jamaa Zake Ibraahiym, Hakika Wewe Ni Mwenye Kusifika Mtukufu.([13])










[1] Abu 'Awaanah katika Swahiyh yake (2/324) na An-Nasaaiy.

[2] Wamesema, "Ewe Mjumbe wa Allaah! Tumefundishwa kukuombea amani (yaani katika Tashahhud) lakini vipi tukuswalie?" Akasema: "Semeni Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad…" n.k. Hivyo hakubainisha kuwa khaswa kwa Tashahhud moja na bila ya nyingine. Hivyo kuna dalili hapa ya kuamrishwa kumswalia katika Tashahhud ya kwanza pia. Hii ni madhehebu ya Imaam Ash-Shaafi'iy kama alivyonukuu katika kitabu chake Al-Umm, nayo ni Swahiyh kwa wafuasi wake kama alivyoeleza An-Nawawiy katika Al-Majmuu' (3/460) na ikatiliwa nguvu na Rawdhwah At-Twaalibiyn (1/263). Ni rai pia ya Al-Waziyr bin Hubayrah Al-Hanbaliy katika Al-Ifswaah kama Ibn Rajab alivyonukuu na akaipa nguvu katika Dhayl Twabaqaat (1/280). Hadiyth nyingi zimekuja kuhusu kumswalia (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Tashahhud. Hakuna hata mojawapo iliyoeleza bayana kuhusu yaliyotajwa, bali Hadiyth hizo ni za ujumla zimejumuuisha Tashahhud zote. Na nimetaja hii katika Al-Aswl kama ni ta'liyq (kiambatisho) lakini sio katika matini kuu kwani haziridhishi shuruti zetu za (kutambulisha) usahihi. Lakini zinakubaliana katika maana, na wale wanaokanusha na kupinga hii, hawana dalili sahihi kutumia kama ni ushahidi, kama nilivyopambanua katika Al-Aswl. Kama kauli ya kuonyesha kuongeza chochote katika 'Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad' ni Makruuh (inachukiza), pia haina asili katika Sunnah, wala hakuna dalili inayokinaisha. Bali tunaona kwamba anayesema hivi hafuati maamrisho ya nyuma ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), 'Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad ...' na hoja zaidi za hii zipo katika Al-Aswl.

[3] Rai ya mwanzo kabisa kuhusu maana ya 'kumswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)" ni ya Abu Al-'Aaliyah (kwa marejeo ya Suratul-Ahzaab 33: 56), 'Swalah ya Allaah kwa Mtume ina maana kudhibiti na kumpa utukufu; Swalah ya Malaika na wengineo ni kuomba hivyo kwa Allaah, na hapa inamaanisha kuomba Swalah zizidishwe na sio asili ya Swalah yenyewe". Ibn Hajar amenukuu katika Fat-h Al-Baariy, na amepinga kauli mashuhuri kwamba Swalah ya Mola ni Rahmah, akaipambanua hii Ibn Al-Qayyim katika Jalaa Al-Ahkaam, akiacha nafasi ndogo kwa maoni zaidi.

[4] Kutokana na barakah: ukuaji, uongezaji na kukua, kubarikika. Hivyo du'aa hii inamdhamini Muhammad mema ambayo Allaah Amewajaalia familia ya Ibraahiym, kumdumishia na kumthibitishia na pia kumuongezea maradufu.

[5] Ahmad na Atw-Twahaawiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[6] Taz. Tanbihi ifuatayo.

[7] Nyongeza hizi mbili ni ushahidi wenye kuthibitika katika Al-Bukhaariy, Atw-Twahaawiy, Al-Bayhaqiy, Ahmad na An-Nasaaiy. Pia zimekuja katika njia mbali mbali za usimulizi katika aina nyinginezo za du'aa (Taz. Namba 3, 7). Hivyo usichanganywe na rai ya Ibn Al-Qayyim katika Jalaa Al-Afhaam (Uk. 198) akifuata nyayo za Mwalimu wake mkuu Ibn Taymiyyah katika Al-Fataawa (1/16). "Hakuna Hadiyth Swahiyh kuhusu ibara 'Ibraahiym wa aali Ibraahiym' pamoja". Hapa tumekuonyesha Hadiyth zilizo Swahiyh. Kosa la Ibn Al-Qayyim limebainika kutokana na mwenyewe kukiri kuwa (aina ya kumswalia) Namba 7 (inayofuatia) ni Swahiyh ambayo imetaja aliyokanusha kabla!

[8] Al-Bukhaariy, Muslim, Al-Humaydiy (138/1) na Ibn Mandah (68/2) ambaye amesema kuwa kuna makubaliano kuwa Hadiyth hii ni Swahiyh.

[9] Ahmad, An-Nassaiy na Abu Ya'laa katika Musnad yake (44/2) ikiwa na isnaad Swahiyh.

[10] Muslim, Abu 'Awaanah, Ibn Abi Shaybah (2/132/1) na Abu Daawuud, na Al-Haakim amekiri ni Swahiyh.




[11] Al-Bukhaariy, An-Nasaaiy, Atw-Twahaawiy, Ahmad na Ismaa'iyl Al-Qaadhwi katika Fadhwl As-Swalaah 'alan-Nabiyy (صلى الله عليه وآله وسلم) (Uk. 28 Chapa ya mwanzo, Uk. 62 Chapa ya pili ikiwa na utafiti wangu).

[12] Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nasaaiy.

[13] An-Nasaaiy, Atw-Twahaawiy, Abu Sa'iyd bin Al-'Araabiy katika Al-Mu'jam (79/2) ikiwa na isnaad Swahiyh. Ibn al-Qayyim ametoa chanzo chake katika Al-Jalaa Al-Afhaam (Uk. 14-15) ya Muhammad bin Is-haaq As-Siraaj na akakiri kuwa ni Swahiyh. Kauli hii inajumuisha zote mbili 'Ibraahiym na jamaa zake Ibraahiym' jambo lililokanushwa na wote wawili; Ibn Al-Qayyim na Mwalimu wake Ibn Taymiyah, kama ilivyoelezwa juu.
 
047-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Faida Muhimu Kuhusu Kumswalia Mtume Wa Ummah ‘Swalaatu 'Alan-Nabbiyy’ (Faida Ya Kwanza Na Ya Pili)
FAIDA MUHIMU KUHUSU KUMSWALIA MTUME WA UMMAH ‘SWALAATU 'ALAN-NABBIYY’




FAIDA YA KWANZA




Kinachoonekana ni kuwa nyingi katika hizi namna mbali mbali za kumswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), hakuna utajo wa Ibraahiym pekee bila ya jamaa zake, lakini imo ndani yake: 'kama Swallayta 'alaa aali Ibraahiym' [Kama Ulivyowaswalia jamaa zake Ibraahiym], na sababu ya hii ni kwamba katika Lugha ya Kiarabu, kizazi cha mtu kinajumuisha mtu mwenyewe kama kinavyojumuisha na wenginewe katika wanaomtegemea, kama katika kauli ya Allaah (تعالى ):





((Hakika Allaah Alimteua Aadam na Nuuh na kizazi cha Ibraahiym na kizazi cha 'Imraan juu ya walimwengu wote)). [Al-'Imraan 3:33]





((Hakika Sisi Tuliwapelekea kimbunga cha vijiwe, isipokuwa wafuasi wa Luutw. Hao Tuliwaokoa karibu na Alfajiri)). [54: 34]




Na katika hayo pia, ni kauli yake : (صلى الله عليه وآله وسلم) ((Ewe Allaah! Waswalie jamaa zake Abu Awfaa)). Pia lipo tamshi la Ahlul-Bayt (watu wa nyumba), kama kauli ya Allaah (تعالى ):


((Rehema ya Allaah na Baraka Zake ziko juu yenu, enyi watu wa nyumba hii!)) [Huud 11: 73]



"Kwani hakika Ibraahiym ni katika wao. (amejumuishwa katika 'jamaa zake Ibraahiym) "




Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

"Na kwa sababu hiyo, ndio ikaja katika matamshi mengi: 'Kamaa Swallayt 'alaa Aali Ibraahiym' [Kama Ulivyowaswalia jamaa zake Ibraahiym], na 'Kamaa Baarakta 'alaa Aal Ibraahiym' [Kama Ulivyowabariki jamaa zake Ibraahiym]. Na ikaja katika baadhi yake Ibraahiym mwenyewe, na hii ni kwa kuwa, yeye ndiye shina katika Swalah na Utakaso, na waliobakia katika watu wa nyumbani kwake wanapata hayo kufuatana na hilo. Na imekuja katika baadhi yake kutaja haya, na hii ni kutanabahisha juu ya yote mawili.

Ukisha elewa hayo, kumezagaa maulizano baina ya Maulamaa kuhusiana na namna ya kushabihisha katika kauli yake: 'Kamaa Swallayta 'alaa… mpaka mwisho wake' (kama Ulivyomswalia mpaka mwisho wake), kwani ki kawaida katika kushabihisha ni kuwa anayeshabihishwa huwa si bora kuliko anayeshabihishwa naye. Na kwa hakika, hali hii hapa ni kinyume kabisa na ile ya kawaida, kwani Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni mbora zaidi kuliko Ibraahiym, na kwa kuwa yeye ni mbora, basi Swalah zinazoombwa zinakuwa ni bora zaidi kuliko Swalah zilizopatikana au zitakazopatikana. Maulaamaa wametoa majibu mengi kuhusu haya yanayopatikana katika Fat-h Al-Baariy na Al-Jalaa Al-Ifhaam. Majibu hayo yamefikia kumi. Baadhi yake ni dhaifu sana kupita kiasi kulinganisha na mengineyo, isipokuwa kauli moja tu ambayo ina nguvu na imependezeshwa na Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah na Ibn al-Qayyim kwa kusema ni nzuri. Nayo ni ile kauli ya aliyesema:

“Hakika kizazi cha Ibraahiym kinajumuisha Mitume ndani yake, Mitume ambao kama wao hakuna katika jamaa zake Muhammad. Hivyo, inapoombwa Swalah kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) na jamaa zake kama Swalah aliyoswaliwa Ibraahiym na jamaa zake ambao kuna Mitume ndani yake, jamaa zake Muhammad wanapata katika hayo yanayolingana nao, kwa vile wao - jamaa zake Muhammad - hawafikii daraja ya Mitume. Hivyo kinachozidi katika kilichoombwa ambacho wanastahiki kupewa Mitume tu akiwemo Ibraahiym, hubakia kuwa cha Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). Hivyo yeye hupata heshima ya cheo cha pekee ambacho hawafikii wengineo".




Ibn Al-Qayyim amesema:

"Hii ni rai bora kuliko zote (za nyuma), na kilicho bora zaidi ya hii ni kusemwa kwamba Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni katika jamaa zake Ibraahiym, bali yeye ni mbora wao kama alivyosimulia 'Aliy Ibn Twalha kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) kuhusu kauli yake تعالى :


((Hakika Allaah Alimteua Aadam na Nuuh na kizazi cha Ibraahiym na kizazi cha 'Imraan juu ya walimwengu wote)). [Al-'Imraan 3:33]




Ibn 'Abbaas amesema: "Muhammad ni katika jamaa zake Ibraahiym". Na hii ni Matini ikiwa wataingia Mitume wengine ambao ni vizazi vya Ibraahiym katika jamaa zake, basi kuingia kwa Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kunafaa zaidi. Hivyo kauli yetu huwa: "… Kama Swallayta 'alaa ali Ibraahiym [kama Ulivyowaswalia jamaa zake Ibraahiym]", inajumuisha kuswaliwa yeye (صلى الله عليه وآله وسلم) na kuswaliwa Mitume wote wengine waliotokana na kizazi cha Ibraahiym. Kisha Allaah Ametuamrisha kumswalia Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) na jamaa zake khaswa, kwa kadiri tunavyomswalia yeye (صلى الله عليه وآله وسلم) pamoja na wengine wote katika jamaa zake Ibraahiym kwa ujumla na yeye (صلى الله عليه وآله وسلم) ni miongoni mwao. Kwa hiyo jamaa zake Mtume wanapata yanayowastahiki wao na yanayobakia yote huwa yake yeye (صلى الله عليه وآله وسلم).




Akasema: Wala hakuna shaka kwamba (jumla ya) Swalah wanayoipata jamaa zake Ibraahiym (pamoja) na Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) huwa pamoja nao ila Swalah iliyo bora zaidi na kamilifu kuliko zote huipata Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) pekee. Kwa hiyo, anayoombewa yeye (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Swalah –kuswaliwa- ni hili jambo tukufu ambalo nalo ndilo lililo bora zaidi kuliko anayoombewa Ibraahiym bila ya shaka yo yote ile.

Na hapo ndipo inapodhihiri ile faida ya kushabihisha na kwamba inakwenda sambamba na asli -kawaida- yake, na kwamba Swalah anayoombewa yeye (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa maneno haya ni ile iliyo tukufu na iliyo bora zaidi kuliko anayoombewa mwengineo. Basi ikiwa kusudio la du'aa ni kuwa yeye(صلى الله عليه وآله وسلم) kashabihiana na yule anayeshabihishwa naye na kwamba Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) anayo sehemu iliyo kubwa zaidi, basi huwa kwake yeye aliyeshabihishwa kusudio zaidi ya aliyopewa Ibraahiym na mwengineo.




Na ikiongezewa hayo ni kuwa yule aliyeshabihishwa naye anapata mambo ambayo hawayapati wengineo.

Kwa hivyo, imedhihirisha fadhila za Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) na utukufu wake juu ya Ibraahiym na juu ya kila jamaa zake wakiwemo miongoni mwao Mitume kama anavyostahiki (utukufu). Ndio ikawa Swalah hii inathibitisha ubora huu na ni kitu kilichoshikamana naye. Na hivyo ndivyo itakiwavyo, kwani hayo ni katika masharti na matakwa yake.



‘Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa ‘Alaa Aalihi Wa Sallam Tasliyman Kathiyran, Wa Jazaahu ‘Annaa Af-Dhwal Maa Jazaa Nabiyyan ‘An Ummatihi. Allaahumma Swalli ‘Alaa Muhammad Wa ‘Alaa Aali Muhammad, Kamaa Swallayta ‘Alaa Aali Ibraahiym Innaka Hamiydum-Majiyd, Wa Baarik ‘Alaa Muhammad Wa ‘Alaa Aali Muhammad Kama Baarakta ‘Alaa Aali Ibraahiym Innaka Hamiydum-Majiyd’.




‘Basi Allaah Amswalie pamoja na jamaa zake, na Amshushie amani juu yake, maamkizi mengi ya amani, na Ampe jazaa njema kutokana na sisi (du'aa zetu) jaza bora kuliko zote Alizompa Mtume yeyote kutokana na Ummah wake. Ee Allaah! Mswalie Muhammad na jamaa zake Muhammad kama Ulivyowaswalia jamaa zake Ibraahiym, hakika Wewe ni Mwenye kusifika Mtukufu. Na Mbariki Muhammad na jamaa zake Muhammad kama Ulivyowabariki jamaa zake Ibraahiym, hakika Wewe ni Mwenye kusifika Mtukufu.’







FAIDA YA PILI




Msomaji mtukufu ataona kwamba matamshi haya yote ya Swalah juu ya tofauti ya aina zake, yote yana kuswaliwa kwa jamaa zake Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), wake zake, kizazi chake pamoja na yeye mwenyewe (صلى الله عليه وآله وسلم). Kwa hiyo basi, sio katika Sunnah wala mtu hatokuwa anatekeleza amri ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) ikiwa atafupisha kwa kusema tu: 'Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad' pekee, bali hakuna budi kuleta aina mojawapo ya Swalah hizi kwa ukamilifu kama ilivyokuja kutokana na yeye (صلى الله عليه وآله وسلم), wala hakuna tofauti baina ya Tashahhud ya kwanza na ya mwisho. Hii ni matini kutoka kwa Imaam Ash-Shaafi'iy katika Al-Umm akisema: "Tashahhud katika ya kwanza na ya pili ni sawa sawa -tamshi moja- hayatofautiani. Na maana ya kauli yangu “Tashahhud” ni “Tashahhud was Swalaatu ‘alaan Nabiyyi“ ni kushuhudia na kumswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), haitoshi moja bila ya nyingine."




Na katika maajabu ya zama hizi na katika fujo za kielimu ni kuwa baadhi ya watu -naye ni Ustaadh Muhammad Is-'aaf An-Nashaashiyby katika kitabu chake 'Al-Islaamus-Swahiyh' (Uislamu Sahihi),- wana ushupavu wa kukanusha kuwaswalia jamaa zake Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) wakati wa kumswalia yeye (صلى الله عليه وآله وسلم) juu ya kuthibiti hayo katika Swahiyhayn (Al-Bukhaariy na Muslim), na kwengineko na kutoka kwa kundi la Maswahaba mbali mbali wakiwemo Ka'ab bin 'Ujrah, Abu Humayd As-Saa'idy, Abu Sa'iyd Al-Khudriyy, Abu Mas'uud Al-Answaariy, Abu Hurayrah na Twalha bin 'Ubaydullaah. Na katika Hadiyth zao (imeonekana kwamba) walimuuliza Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم): "Vipi tukuswalie?" Akawafundisha(صلى الله عليه وآله وسلم) aina hizi. Na hoja ya An-Nashaashiyby katika kukanusha ni kwamba Allaah تعالى Hakutaja katika kauli Yake mtu mwengine yeyote yule pamoja na Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم):

إِنَّ اللَّهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

((Hakika Allaah na Malaika Wake wanamswalia Mtume. Enyi mlioamini! Mswalieni na muombeani rahma)). [Al-Ahzaab: 56].




Kisha akaendelea kukanusha bali alipindukia mipaka katika kukanusha kwamba Maswahaba wamemuuliza (صلى الله عليه وآله وسلم) swali kama hilo, kwa sababu ya maana ya 'Swalah' ilijulikana kwao, nayo ni 'du'aa'. Hivyo, itakuwaje wamuulize?!




Huku ni kuchanganyikiwa kuliko wazi kabisa, kwani swali lao -Maswahaba- halikuwa kuhusu maana ya kumswalia yeye (صلى الله عليه وآله وسلم) hata akajibu alivyotaja, bali lilikuwa ni vipi kumswalia yeye ,(صلى الله عليه وآله وسلم) kama ilivyothibiti katika riwaayah zote zilizotangulia kuashiriwa. Na wakati huo hapatokuwa na la kushangaza, kwani walimuuliza (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu namna ya utekelezaji kishari’ah -kama ilivyo katika Shari’ah- jambo ambalo hawawezi kulielewa isipokuwa kwa njia ya uongofu kutoka kwa Mjuzi na Mwenye Hikima na Muwekaji wa Shari’ah. Na hii ni kama lau walimuuliza kuhusu vipi utekelezaji wa Swalah ya Faradhi kutokana na kauli ya Allaah تعالى:

وََأَقِيمُوا الصَّلَاةَ

Kwani elimu yao ya maana ya asili ya Swalah katika lugha haiwatoshelezi kuuliza kuhusu vipi unakuwa utekelezaji wake kishari’ah, na hii ni dhahiri kabisa.




Ama hoja yake -An-Nashaashiyby- iliyohusishwa si lolote, kwani ni jambo linaloeleweka vizuri miongoni mwa Waislamu kwamba Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) ndie mbainishaji wa maneno ya Mola wa Walimwengu kama Anavyosema:

وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ

((Nasi Tumekuteremshia wewe Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyo teremshwa kwao, wapate kufikiri)) [An-Nahl: 44]




Hivyo Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) amebainisha wazi namna gani aswaliwe na ndani yake imejumuisha kutaja jamaa zake. Hivyo ni wajibu kukubali hivyo kutokana na yeye (صلى الله عليه وآله وسلم), na kwa kauli yake Allaah:

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ




((Na anachokupeni Mtume chukueni, …)) [al-Hashr: 7]




Na kwa kauli yake (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth Swahiyh mash-huur([1]): ((Nimepewa Qur-aan pamoja na iliyofanana nayo)).([2])




Nashangazwa na wala sielewi ni nini hasa anachotaka kusema An-Nashaashiyby na kila aliyedanganyika na uongo wa maneno yake yenye majivuno. Itakuwaje kwa anaekanusha Tashahhud katika Swalah kabisa, au kukanusha mwanamke mwenye hedhi kuacha kuswali na kufunga akiwa katika masiku yake, yote kwa hoja kwamba Allaah (تعالى) Hakutaja Tashahhud kwenye Qur-aan; bali Ametaja kisimamo na kusujudu tu, na kwamba Yeye (تعالى) katika Qur-aan Hakumuondoshea mwanamke mwenye hedhi kuswali na kufunga, bali ni wajibu juu yake -mwenye hedhi– kuzitekeleza! Hivyo, wanakubali na hoja kama hizi ambazo zinakwenda sambamba na hoja zake za asili au sivyo. Je, wanakubaliana naye huyu mkanushaji katika kukanusha kwake, au wanapingana nae? Wakiwa wanakubaliana naye jambo ambalo hatulitarajii, basi watakuwa kwa uhakika wamepotea upotofu wa mbali, na wamefarikiana na Waislamu. Na ikiwa wanapingana naye, basi watakuwa wamewafikishwa na wamesibu na walichomjibu mkanushaji. Na sisi ndio jawabu letu kwa An-Nashaashiybiy, na tumekubainishia hivyo.




Basi tahadhari ewe Muislamu kujaribu kufahamu Qur-aan bila ya kurejea kwenye Sunnah, kwani hakika hutoweza kufanya hivyo hata kama utakuwa katika lugha (Ya Kiarabu) ni Siybawayh([3]) wa zama zako. Huu hapa mfano mbele yako. Huyu An-Nashaashiybiy alikuwa ni mmoja kati ya Wataalamu bingwa na wakubwa wa lugha ya Kiarabu wa zama hizi, na wewe unamuona namna alivyopotoka baada ya kughururika kwa elimu yake katika lugha bila ya kutafuta msaada wa Sunnah katika kuweza kuifahamu Qur-aan, bali yeye ameikanusha hiyo Sunnah kama unavyoelewa. Na kuna mifano mingi tu kwa haya tuyasemayo, lakini hakuna nafasi ya kuitaja, (lakini) na katika tuliyoyataja yatatosheleza. Na Allah Ndie Muwafiqishaji.




[1] Ni Hadiyth ambayo idadi ya wapokezi wake haijafikia idadi ya wapokezi wa Hadiyth ya Mutawaatir.

[2] Abu Daawuud na Ahmad ikiwa na isnaad Swahiyh.

[3] Mwanasarufi mashuhuri na bingwa wa lugha ya Kiarabu katika karne ya pili Hijriyah.
 
048-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Faida Muhimu Kuhusu Kumswalia Mtume Wa Ummah ‘Swalaatu 'Alan-Nabbiyy’ - (Faida ya Tatu, Nne, Tano Na Sita)
Faida Ya Tatu


Msomaji pia atagundua kuwa katika aina zote hizi za kumswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), hakuna neno la 'as siyad' (bwana), na kwa sababu hiyo Maulama waliokuja mwisho wamekhitilafiana kuhusu hukmu ya kuingiza neno hili –Sayyidinaa/Bwana wetu- katika Swalah ya Ibraahiymiyyah. Kutokana na upungufu wa nafasi, hatutoingia katika kuchambua kauli wala kutaja waliokataa jambo hili kwa kushikamana na kufuata mafunzo kamili ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa Ummah wake alipoulizwa vipi kumswalia (صلى الله عليه وآله وسلم). Akajibu hali kuwa anaamrisha kwa kusema: ((Semeni, Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad…….)). Lakini napenda kuwanukulia wasomaji rai ya Al-Haafidhw bin Hajar Al-'Asqalaaniy katika hayo, tukizingatia kuwa yeye ni mmoja wa Maulamaa wakubwa wa Ki-Shaafi'iy waliokusanya baina ya Hadiyth na Fiqh. Imeenea kwa waliokuja mwisho katika ash-Shaafi'iyyah kwenda kinyume na mafunzo haya ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم).

Al-Haafidhw Muhammad bin Muhammad bin Muhammad Al-Ghuraabiyly (790-835 AH) mwenziwe Ibn Hajr amesema na nimenukuu kutoka mswada wake.([1])

Aliulizwa (Ibn Hajr) - Allaah Atunufaishe kwa maisha yake - kuhusu namna ya kumswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Swalah au nje ya Swalah, sawa sawa kama imesemwa ni wajibu au inapendekezeka. Je, ni sharti mojawapo kuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) asifiwe kwa ubwana, mfano mtu kusema: 'Allaahumma Swalli 'alaa Sayyidinaa Muhammad...', au 'sayyidil-khalq' (bwana wa viumbe), au 'sayyid walad Aadam' (bwana wa watoto wa Aadam)?" Au mtu afupishe kwa kusema: 'Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad"? Na ni ipi katika mbili hizi ni bora zaidi; kulitamka neno la 'sayyid' kwa vile ni sifa iliyothibiti kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), au kutoitamka kwa vile halijapokewa katika mapokezi?

(Ibn Hajr رضي الله عنه) akajibu:

"Ndio, kushikamana na matamshi yaliyopokewa, ndio ni bora zaidi, na wala pasisemwe kuwa labda Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) ameacha hivyo –hakujiita mwenyewe sayyid- kwa sababu ya unyenyekevu wake (صلى الله عليه وآله وسلم), kama alivyoacha (صلى الله عليه وآله وسلم) kujiswalia (صلى الله عليه وآله وسلم) anapotaja jina lake, ingawa Ummah wake wamehimizwa kufanya hivyo kila anapotajwa (صلى الله عليه وآله وسلم). Kwani sisi tunasema, kama ingelikuwa hivyo ni bora, basi ingelipokelewa kutoka kwa Maswahaba kupitia Mataabi'yna, lakini hatukupata hata kukutana na cho chote kile katika yaliyopokewa kutokana na mmoja miongoni mwa Maswahaba wala Mataabi'yna waliowafuata. Akasema: Juu ya wingi wa hayo yaliyopokewa kutokana na wao kuhusiana na hilo. Na huyu hapa Imaam Ash-Shaafi'iy, Allaah Ampandishe daraja yake, ni miongoni mwa watu wenye kumuheshimu Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) zaidi. Amesema katika utangulizi wa kitabu chake ambacho ni tegemezi kwa watu wa madhehebu yake: 'Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad….' hadi mwisho wa ilipomfikisha juhudi yake, nayo ni kauli yake: 'kila wanapomkumbuka wanaomkumbuka, na kila wanapoghafilika kumkumbuka wanaoghafilika', kama kwamba ametoa hayo kutokana na Hadiyth Swahiyh ambayo ndani yake kuna: ”Subhaana Allaahi 'adada Khalqihi”. Imethibiti kuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwambia Mama wa Waumini alipomuona amekithirisha at-tasbiyh na akarefusha: ((Umesema maneno ambayo lau yangelipimwa katika mizani kwa hivyo ulivyosema, basi mizani yake itakuwa nzito)). Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akipendezwa na kuomba du'aa zilizokuwa fupi lakini zikiwa nzito katika maana.

Al-Qaadhwi 'Iyaadhw ameweka mlango katika namna za kumswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) katika kitabu chake Ash-Shifaa (Kitabu cha Tiba). Amenukuu ndani yake mapokezi mar-fuu’an -usimulizi wa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) - kutoka kwa kundi la Maswahaba na Mataabi'iyn. Na hakuna katika yote hayo au kutoka kwa yeyote yule miongoni mwa Swahaba na wengineo tamshi la 'sayyidinaa'. Miongoni mwa hayo mapokezi ni:




a) Hadiyth ya 'Aliy kwamba alikuwa akiwafundisha namna ya kumswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kusema:




اللَّهُمَّ دَاحِي الْمَدْحُوَّات وَبَارِئ الْمَسْمُوكَات اِجْعَلْ سوابق صَلَوَاتك وَنَوَامِي بَرَكَاتك زائد تَحَنُّنِك عَلَى مُحَمَّد عَبْدك وَرَسُولِك الْفَاتِح لِمَا أُغْلِقَ




Allaahumma Daahiy al-Mad-huwaat, wa Baari al-Masmuukaat, Ij-'Al-Sawaabiq Swalahwaatak, wa Nawaamiy BaRak’ahtak, wa Zaaid Tahiyyaatak 'alaa Muhammad 'Abduka wa Rasuulak, Al-Faatih Limaa Ughliq'




“Ee Allaah! Mtandazaji wa ardhi, Mwanzishi wa mbingu, Zijaalie Swalah Zako bora kabisa zilizojaa rutuba ya Baraka Zako na yote mema yaliyozidi, kwa Muhammad, Mja (wako) na Mjumbe (wako), mfunguaji wa yaliyofungwa”.




b) Na kutoka kwa 'Aliy pia, alikuwa akisema:




صلواتُ اللهِ البرِّ الرحيمِ والملائكةِ المقرّبين والنبيّينَ والصدّيقينَ والشهداءِ الصَّالحين، وما سبح لك من شيء يا رب العالمين، على محمّدِ بنِ عبدِ الله خاتمِ النبيّينَ وإمامِ المتقين




'Swalawaatu-LLaahil-Barrur-Rahiym, wal-Malaaikatil-Muqarrabiyn, wan-Nabiyyiyn was-Swiddiyqiyn was-Shuhadaais-Swaalihiyn, wa Maa Sabaha Laka min shayin Yaa Rabbal-'Aalamiyn, 'alaa Muhammad Ibn 'Abdillaahi Khaatamin-Nabiyyiyn wa Imaamil-Mutaqqiyn…' n.k.



“Swalah za Allaah Mhisani Mkunjufu wa rehema, na za Malaika walio karibu Naye, na Mitume na Wasema kweli na Mashahiyd na watu wema, na kila kinachosabbih kwa ajili Yako ewe Mola wa walimwengu wote, juu ya Muhammad bin 'Abdillaah mwisho wa Manabii na kiongozi wa wamchao Mungu”.




c) Kutoka kwa 'Abdullaah bin Mas'uud ambaye alikuwa akisema:




اللَّهُمَّ اجْعَلْ صَلَوَاتِكَ وَبَرَكَاتِكَ وَرَحْمَتَكَ عَلَى مُحَمَّدٍ إمام الخيروَرَسُول الرحمة




Allaahummaj-'Al-Swalahwaatika wa BaRak’ahtik, wa Rahmataka 'alaa Muhammad 'Abdika wa Rasuulik, Imaamil-Khayr wa Rasuulir-Rahmah…




“Ee Mola zijaalie Swalah Zako na Baraka Zako na Rehma Zako juu ya Muhammad kiongozi wa wema na Mtume wa Rehma”.




d) Kutoka kwa Hasan Al-Baswriy ambaye alikuwa akisema: "Anayetaka kunywa katika kikombe kinachokata kiu kutoka hawdh (chemchem) ya Mustwafaa, aseme:




اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَعَلَى آلِهِ وَأَصْحَابِهِ وَأَزْوِاجِهِ وأولاده وَذُرَّيَّاتِهِ وأهل بيته وَأًصْهَارِهِ وَأَنْصَارِهِ وَأَشْيَاعِهِ وَمُحِبِّيهِ




'Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aailihi wa Aswhaabihi, wa azwaajihi, wa awlaadihi wa dhurriyaatihi wa ahli baytihi wa aswhaarihi wa answaarihi wa ashyaa'ihi wa muhibbihi'




“Ee Mola Mswalie Muhammad na Aali zake na Swahaba zake na Wake zake na Wanawe na Vizazi vyake na Watu wa nyumba yake na Shemeji na wakwe zake na Waliomnusuru na Wenzake na Wapenzi wake”




Hivyo ndivyo (Al-Qaadhwiy 'Iyaadhw) alivyoandika katika Ash-Shifaa kuhusu namna ya kumswalia Mtume kutoka kwa Maswahaba na waliowafuatia na akataja mengineyo.




Ndio, imesimuliwa katika Hadiyth ya Ibn Mas'uud kwamba kumswalia kwake kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisema:




اللَّهُمَّ اجْعَلَ فَضَائِلَ صَلَواتِكَ ورَحْمَتِكَ وَبَرَكَاتِكَ علَّى سَيِّدِ المرْسَلِينَ




'Allaahummaj-'Al-fadhwaail Swalahatak wa Rahmatak wa BaRak’ahtak 'alaa Sayyidil-Mursaliyn…




Imesimuliwa na Ibn Maajah, lakini isnaad yake ni dhaifu kwa hiyo Hadiyth ya 'Aliy iliyosimuliwa na At-Twabaraaniy ikiwa na isnaad inayokubalika inaongoza. Hadiyth hii ina maneno magumu ambayo nimeyataja na kuelezea katika kitabu Fadhwl An-Nabbiy (Ubora wa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)) cha 'Abdul Hasan Ibn Al-Faaris. Baadhi ya Mashaafi'iy wamesema kwamba mtu akiapa kwa kumswalia Swalah Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) Swalah bora kabisa ili kutekeleza kiapo chake iwe:




اللهم صَلَّ الله عَلَى مُحَمَّدٍ كُلَّما ذَكَرَهُ الذَّاكِرُونَ وسها عَنْ ذِكْرِهِ الْغَافَلُونَ




'Allaahuuma Swalli 'alaa Muhammad kullamaa dhakarahudh-dhaakiruun, wa sahaa 'an dhikrihil-ghaafiluun'




An-Nawawy kasema: "Inayopasa kutekelezwa ni kusema:




اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى ‏ ‏مُحَمَّدٍ ‏وعلى َآلِ ‏ ‏مُحَمَّدٍ ‏ ‏كَمَا صَلَّيْتَ عَلَى ‏إِبْرَاهِيمَ.....




Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad, kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym …




Maulamaa wengi wa mwishoni wamejibu hii, kwa kusema kwamba hakuna dalili inayothibitisha kuhusu aina mbili zilizotajwa kuhusu ubora katika usimulizi. Am kuhusu maana basi ya mwanzo ndio bora.

Mas-ala haya ni mashuhuri katika vitabu vya Fiqh, na Maulamaa wote wa Fiqh waliozungumzia mas-ala haya kwa pamoja hawajanukuu neno la 'sayyid'. Ingelikuwa neno hili limependekezwa, lisingeliwakwepa wote hata wawe wameghafilika. Mazuri yote ni kufuata waliyosimulia na Allaah Anajua zaidi"




Rai ya Ibn Hajar ya kutokukubali kumsifia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa 'usayyid' (ubwana) ni kutokana na amri ya Qur-aan, na hii pia ni rai ya Maulamaa wa Kihanafi. Ni rai ipasayo kufuatwa kwani ndio udhihirisho mkweli wa mapenzi yake (صلى الله عليه وآله وسلم),

â ö@è% bÎ) óOçFZä. tbq7Åsè? ©!$# ÏRqãèÎ7¨?$$sù ãNä3ö7Î6ósã ª!$# á

((Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Allaah basi nifuateni mimi, Allaah Atakupendeni)) [Aal-I’mraan – 31]




Kwa sababu hii, Imaam An-Nawawy amesmea katika Rawdhwatut-Twaalibiyn (1/265): "Swalah iliyo kamilifu kabisa ya kumswaliwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) ni:

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى ‏ ‏مُحَمَّدٍ

'Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad…"




inayowafikiana aina ya 3 iliyotajwa ambayo haikutajwa sayyid.







Faida Ya Nne


Itambulike kwamba aina ya 1 na ya 4 ndizo Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alizowafundisha Maswahaba walipomuuliza kuhusu vipi kumswalia, kwa hiyo hii imetumika kama ni dalili kwamba hizi ndizo bora kabisa za kumswalia kwani asingeliwachagulia au kujichagulia mwenyewe isipokuwa kilicho bora na utukufu. Imaam An-Nawawy kama ilivyotajwa, amenukuu (katika Radhwatut-Twaalibiyn) kwamba kama mtu anataka kuapa kwa kumswalia Swalah bora kabisa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), basi haiwezi kutimizwa isipokuwa kwa njia hizi.




As-Subkiy ametoa sababu nyingine: "Yeyote anayemswalia kwa Swalah hizi basi amemswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa yakini na atakayemswalia kwa maneno mengine, ameingia katika mashaka au hakutimiza kumswalia kama ipasavyo kwa sababu waliuliza: "Vipi tukuswalie?" Alijibu: "Semeni: …" Hivyo wakiilezea Swalah yao kwake kama kauli yao kadhaa na kadhaa. Hii imetajwa na Al-Haytamiy katika Ad-Darr Al-Mandhwuud (25/2) kisha akasema, (27/1) kwamba lengo linapatikana katika aina zote zilizokuja katika Ahaadiyth Swahiyh.







Faida Ya Tano


Ijulikane kwamba sio shari’ah kuunganisha aina zote hizi kuwa ni aina moja ya Swalah, hali kadhalika Tashahhud zote zilizotolewa kabla, kwani hiyo itakuwa ni bid'ah (uzushi) katika dini; Sunnah ni kusema mara hivi mara vile katika nyakati mbali mbali kama Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah alivyoelezea katika utafiti wake wa Takbiyr za 'Iyd mbili (Majmuu' Al-Fataawa 29/253/1)







Faida Ya Sita


'Allaamah Swiddiyq Hasan Khaan amesema katika kitabu chake Nuzuul Al-Abraar bil 'Ilm Al-Manthuur minal-Ad'iya wAl-Adkhaar, baada ya kutoa Hadiyth nyingi kuhusu fadhila za kumswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) na kukithiri katika kumswalia (Uk. 161):

"Hakuna shaka kwamba wengi miongoni mwa Waislamu wanaomswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Ahlul-Hadiyth (wenye kufuata Hadiyth sahihi) na wasimulizi wa Sunnah iliyotwahirika, kwani ni mojawapo wa kazi yao katika elimu hii sharifu kumswalia kablaa ya kila Hadiyth, kwa hiyo ndimi zao zimerutubika daima kwa kumtaja (صلى الله عليه وآله وسلم). Hakuna kitabu cha Sunnah au mkusanyo wa Hadiyth; ikiwa ni Jaami', Musnad, Mu'jam, Juz'u n.k ila imekusanya maelfu ya Hadiyth, hata kilichokuwa cha chini yao kabisa kwa uzito; Jaami' As-Saghiyr cha As-Swuyuutiy, kilichokuwa na Hadiyth elifu kumi na hivyo ndivyo ilivyo katika vitabu vyote vya elimu ya hadiyth. Hivyo hawa ni makundi waliookoka, na Jamaa wa Hadiyth ambao watakaokuwa karibu kabisa na Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) siku ya Qiyaamah, na ndio watakaofurahi kwa shifaa (ombolezi) yake (صلى الله عليه وآله وسلم), mama yangu na baba yangu wawe fidia kwake. Fadhila hii ya watu wa Hadiyth haiwezi kushindwa ya yeyote mwingine ila afanye kama wafanyavyo na zaidi, jambo ambalo takriban haliwezekani. Kwa hiyo Ee mpenda kheri, mtafutaji kuokoka, vyovyote ilivyo, unapaswa uwe Muhaddith au uwe karibu na Muhaddithiyn; usiwe vinginevyo…. Kwani mbali na hivyo hakuna kitakachokunufaisha".

Namuomba Allaah (سبحانه وتعالى) anifanye miongoni wa watu hawa wa Hadiyth, ambao ni miongoni mwa watu waliokaribu kabisa na Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), na labda kitabu hiki kitakuwa ni ushahidi kwayo. Allaah Amerehemu Imaam Ahmad aliyesema:

Dini ya Muhammad iko katika usimulizi

Kipando bora kwa vijana ni Sunnah athari zake

Usizigeukie nyuma Hadiyth na watu wake

Kwani rai ni usiku na Hadiyth ni mchana

Kijana anaweza kuwa mjinga wa uongofu….

Ingawa jua linang'ara katika mwanga wake!





[1] Iliyohifadhiwa katika Maktaba ya Adhw-Dhwaahiriyyah
 
049-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kusimama Kwa Ajili Ya Rak’ah Ya Tatu, Kisha Ya Nne
Kusimama Kwa Ajili Ya Rak’ah Ya Tatu, Kisha Ya Nne



Kisha, alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)akinyanyuka kwa ajili ya Rak’ah ya tatu pamoja na takbiyr([1]) na alimuamrisha "aliyeswali vibaya" kufanya hivyo: “….kisha akifanya hivyo katika kila Rak’ah na Sajdah kama ilivyotangulia”

Na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)anaposimama kutoka kikao alisema takbiyr, kisha akasimama"([2]) na "Alikuwa akinyanyua (صلى الله عليه وآله وسلم)mikono yake([3]) pamoja na takbiyr mara nyingine.




Na alikuwa anapotaka kusimama kwa ajili ya Rak’ah ya nne, akisema: ((Allaahu Akbar))"([4]) na alimuamrisha "aliyeswali vibaya" hivyo kama kabla na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akinyanyua mikono yake([5]) pamoja na takbiyr mara nyingine.




Alikuwa akiketi barabara juu ya mguu wake wa kushoto, kwa utulivu hadi kila mfupa ulirudi sehemu yake kisha akisimama, akijisaidia kwa mikono yake, alikunja ngumi([6]) na kutegemea mikono yake katika kuinuka.([7])

Alikuwa akisoma Suratul-Faatihah kaitka Rak’ah zote mbili na alimuamrisha "aliyeswali vibaya" kufanya hivyo. Katika Swalah ya adhuhuri aliongeza mara nyingine Aayah chache kama ilivyoelezewa katika 'Kisomo cha Swalah ya Adhuhuri'.





[1]Al-Bukhaariy na Muslim.

[2]Abu Ya'alaa katika Musnad yake (284/2) ikiwa na isnaad nzuri. Imetolewa katika Silsilatul Al- Ahaadiyth As-Swahiyhah (604).

[3] Al-Bukhaariy na Muslim.

[4]Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[5]Abu 'Awaanah na An-Nasaaiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[6]Ina maana 'kama mtu anayekanda unga'.

[7] Al-Harbiy katika Hadiyth Al-Ghariyb. Maana yake inapatikana katika Al-Bukhaariy na Abu Daawuud. Ama kuhusu Hadiyth kuwa 'alimkataza mtu kujisaidia kwa mikono yake anapoinuka katika Swalah', ni Munkar na sio Swahiyh kama nilivyoelezea katika Silsilatul-Ahaadityh Adhwa'iyfah (967).
 
050-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Qunuut An-Naazilah Katika Swalah Tano (Qunuut Wakati Waislamu Inapowafikia Janga, Au Maafa)
Qunuut An-Naazilah Katika Swalah Tano (Qunuut Wakati Waislamu Inapowafikia Janga, Au Maafa)



Alipotaka (صلى الله عليه وآله وسلم) kuomba dhidi ya mtu, au kumuombea mtu, alifanya Qunuut ([1]) katika Rak’ah ya mwisho baada ya rukuu, na baada ya kusema: 'Sami'a Allaahu Liman Hamidah, Allaahumma Rabbana lakal Hamd’([2]) "Aliomba kwa sauti"([3]) "alinyanyua mikono"([4]) "ya walionyuma yake walisema Aamiyn"([5])

"Alikuwa akifanya Qunuut katika Swalah zote tano"([6])lakini "hakuwa akifanya Qunuut humo ispokuwa alipoomba dhidi ya watu au kuwaombea watu"([7]) Mfano, mara alisema: ((Ee Allaah! Muokoe Al-Waliyd Ibn Al-Waliyd na Salamah Ibn Hishaam na 'Ayyaash Ibn Abi Rabiy'ah. Ee Allaah! Zidisha adhabu Yako kwa (kabila la) Mudhwar, na wajalie miaka (ya ukame) kama miaka ya Yuusuf. [Ee Allaah! Malaani Lahyaan na Ru'lan, na Dhakwaan, na 'Uswayyah waliomuasi Allaah na Mjumbe Wake]))([8])

Kisha "alikuwa akisema: 'Allaahu Akbar' anapomaliza Qunuut na kusujudu"([9])





[1] "Qunuut" inabeba maana nyingi kama unyenyekevu na uchaji. Na

ilivyokusudiwa hapa ni du'aa khaswa wakati wa kusimama katika Swalah.
[2] Al-Bukhaariy na Ahmad.

[3] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[4] Ahmad na Atw-Twabaraaniy ikiwa na isnaad Swahiyh. Kunyanyua

mikono katika qunuut ni madhehebu ya Ahmad na pia Is-haaq bin Raahawaih kama ilivyo katika Masaail ya Al-Marwazy (Uk. 23). Ama kufuta uso kwa mikono, hili halikuripotiwa katika hali hii, hivyo ni bid'ah. Ama nje ya Swalah, haikusimuliwa kuwa ni Swahiyh. Yote yaliyosimuliwa kuhusu hili, ni dhaifu au dhaifu sanakama nilivyohakikisha katika Dhwa'iyf Abu Daawuud (2) na Silsilatul-Al-Ahaadiyth As-Swahiyhah (597). Hii ndio maana Al-'Izz bin 'Abdus-Salaam amesema katika fatwa zake, "Mtu mjinga tu ndiye anayefanya" Taz. Kiambatisho 8.
[5] Abu Daawuud na Siraaj. Al-Haakim amekiri ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy na wengineo wamekubali.

[6] Abu Daawuud, Siraj na Ad-Daaraqutniy ikiwa na isnaad mbili Hasan.

[7] Abu Khuzaymah katika Swahiyh yake (1/78/2) na Al-Khatwiyb katika Kitabu Al-Qunuut ikiwa na isnaad Swahiyh.

[8] Al-Bukhaariy na Ahmad, ziada kutoka kwa Muslim.

[9] An-Nasaaiy, Ahmad, Siraaj (109/1) na Abu Ya'laa katika Musnad yake ikiwa na isnaad nzuri.
 
Naam baadae inshaallah tutakuja kusoma kipengele cha Maswali na Majibu

Usipishane na huu uzi kher kubwa itapatikana

........................................................................................................
 
VISA VYA WACHA MUNGU

Imamu hassan,imamu hussein na Abdulla bin Jafar (radhiallahu anahum) kipindi fulani walikuwa wanaenda hijja,lakini bahati mbaya ngamia ambaye alibeba chakula chao na maji aliwapotea

Hivyo wakiwa jangwani walifika kwenye hema moja na kumkuta bibi kizee,na wakamuuliza kama kitu chochote cha kukila,akasema hana zaidi ya mbuzi mmoja dhaifu sana,wakamue maziwa yake kisha wanywe,basi wakafanya hivyo na kugawana hayo maziwa

Baada ya kunywa,wakamwambia hakuna kitu kingine ambacho wanaweza kula,akajibu ni hiko kibuzi tu,wakichinje kisha awapikie wale nyama,kweli wakachinja na kula ile nyama

Kisha wakati wanataka kuondoka wakamwabia sisi tunatoka kabila la ban hashim,hivyo siku ukitembelea madina basi uje kututembelea,baadae baada ya hao wageni kuondoka ,mda si mrefu mume wa bibi huyo akarejea

Baada ya kuelezwa tukio zima,huyo mume alihamaki kwanini awachinjie mbuzi watu asio wajua,na je ana uwakika gani kwamba hao ni ukoo wa ban hashim

Basi ikafika wakati ambao huyu bibi na mumewe wakawa maskini sana,hivyo wakaenda Madina kutafuta shughuli ya kuwafanya ili wapate mkate wao wa kila siku,na walikuwa wanakusanya kinyesi cha ngamia kikavu na kwenda kuuza,kinatumika kama nishati ya kupikia

Siku moja huyo bibi akiwa anaokota kinyesi alipita karibu na nyumba ya Imamu Hassan,na imamu akamkumbuka huyu bibi,akamwambia je bibi unanikumbuka? Bibi hakuwa na kumbu kumbu,akamwambia sisi ndio ulituchinjia mbuzi kule jangwani

Ndio bibi akahamaki ndio wewe? Imamu akajibu naam,akamkabidhi yule bibi mbuzi 1000 na dinari 1000 kama zawadi kwa ukarimu aliowafanyia kule jangwani,kisha Hassan akampe yule bibi kwa Hussein nae akatoa mbuzi 1000 na dinari 1000

Kisha akapelekwa kwa Abdulla nae akatoa mbuzi 2000 na dinar 2000,kisha akasema lau kama ungeanzia kwangu kwanza basi ningekupa zaidi ya hivyo

Yule bibi aliondoka pale kwenda kwa mumewe na mbuzi 4000 na dinar 4000,akamwambia mumewe haya ndio malipo ya kibuzi chetu dhaifu

Naam huyo ndio Allah,hakika rehema zake ni kubwa mno,hakika kumkirimu mgeni ni jambo kubwa mno ingawa wengi wetu hatujui tu,tena siku hizi hatutaki wageni kabisa,wallah tunakosa baraka nyingi sana toka kwa Allah Subhaanahu Wataala

Huko mbeleni tutakutana na visa vingi kuhusiana na ukarimu na rehema zake

Kadri Allah atakavyo niwezesha nitakuwa naandika Visa vya Wacha Mungu ili tupate ibra na mazingatio na nyoyo zetu zipate kuathirika na mambo ya kheri
 
Ana Haki Kudai Talaka Ikiwa Mume Hawezi Tendo La Ndoa?
Maswali: Maingiliano
SWALI:



asalaam alaykum warahmatullahi wabarakat, naam sheikh mm nimfatiliaji mzuri wamakala zenu. na inshaallah Mwenyezi Mungu awape hidaya kwa kutuelimisha tusioyajua. mimi swali langu nnamume ambae anamatatizo ya nguvu za kume. Tushahangaika sana hospital, ktk dawa za kisunnah bado haijakuwa soud. na mimi bado msichana mdogo jee nnahaki yakudai talaka?

nimulizia kwa mashekhe huku tz wamesema mpaka iwe sijafanya tendo la ndoa kwa mwaka mzima. na sisi huwatunakaa miezi kimi ndo anaweza siku moja, tunakaa tena miezi kumi na moja. jee hapo ni swahihi namimi binaadam nnamatamanio. nasiwezikuzini. naomba jibu tafadhali, WABILLAHI TAUFIK WA SALAAM ALAYKUM WARAHMATULLAHI WABARAKAAT





JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.





Shukrani kwa swali lako kuhusu mumeo kutoweza kufanya tendo la ndoa.

Msingi wa Dini hii ni kutodhulumu wala kutodhulumiwa. Ndio Mtume wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatuambia:

“Haifai kudhuru wala kulipana madhara” (Ibn Maajah, Maalik na ad-Daaraqutwniy).



Mume kutojiweza ni sababu moja ya mke kuomba talaka na ni haki kwake kupewa na Qaadhi ikiwa mume amekataa kuitoa.



Miezi kumi au kumi na moja ni mingi kwa mwanamke kuweza kuvumilia na kuvumilia huko kunamfanya awe ni mwenye kudhulumika. Ni kwa ajili ya hiyo ndio ‘Umar bin al-Khatwtwaab (Radhiya Allaahu ‘anhu) akaaamrisha kuwa haifai kwa waume walio kwenye Jihaad kukaa zaidi ya miezi minne bila kuja kuwatazama na kukaa kwa muda na wake zao.


Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:




Anafaa Kuachika Ikiwa Mume Hawezi Tendo La Ndoa?

Mume Hamtoshelezei Matamanio Yake Ya Tendo La Ndoa, Anaomba Ushauri

Mume Kahama Chumba Kwa Miezi 3 Hafanyi Tendo La Ndoa, Akiulizwa Anasema Anachoka Kazini

Mke Analalamika Mume Ana Mashetani Yanamfanya Asiweze Kukamilisha Tendo La Ndoa

Anampenda Sana Mume Wake Lakini Hawana Raha Katika Tendo La Ndoa, Wafanyeje?

Mume Au Mke Hawezi Tendo La Ndoa Kwa Zaidi Ya Miaka 5, Hukmu Ni Nini?



Na Allaah Anajua zaidi
 
Ana Matatizo Ya Kutomridhisha Mkewe Kwenye Tendo La Ndoa
Maswali: Maingiliano


SWALI:



Aaww. NAOMBA MNISAIDIE MIMI NINA NDOA YAPATA MIEZI 4 SASA ILA NIA TATIZO LA KUWAHI KUFKA KILELENI NA MKE WANGU LINA MCHUKIZA .LICHA YA KUFANYA YOTE YA KUMWANDAA NA KILA KTU BADO HANA RAHA NA SASA HATAKI KUFANYA TENDO HILO NA MIMI JE ANAHAKI HIYO? NA MIMI PIA NINA HAKI GANI? JE TUACHANE SASA? NA DAWA NINI HASA YA TATTIZO HILI? NAOMBA MSAADA MKUBWA NIA UMRI WA MIKA 24 TU. (tutawasialan kupitia ******** nisaidien juu ya hili kuokoa ndoa hii naona sasa ndoa ni dhuruba ya matatizo tuuu!!!!!

AAWW

NAOMBA KUULIZA JE MIMI KAMA MWANAUME MKE WANGU NAJARIBU KUMBEMBELEZA KWA NAMNA ZOTE NA BDO HATAKI KUINGILIANA NAMI NIFANYEJE HII IMEKUJA TUU KWA SABABU NINA TATIZO LA KUWAHI KUFIKA KILELENI KABLA YAKE NIMEFUATA MAFUNDISHO YENU NINAMFANYIA KILA KITU LAKIN HATIMAYE SASA HATAKI HATA KULALA NAMI HATA NIKIMWAMBIA NJOO HATAKI JE NIMWACHE SASA? JAMANI NAHISI IKIFANYA HILI LA MWAISHO NARUDIN KWENYE ZINZAA ISYO KIFANI. NAOMBA MNISAIDIE HARAKA IWEZEKANAVYO KWA KUZINGATIA NIMEWATOA HOFU VIJANA WENGI NA SASA WAPO MBIONI NAO KUFANYA JAMBO KAMA LANGU LA NDOA NA KUACHANA NA ZINAA HUKU TULIPO.

JE MWANAMKE ANAYO HAKI YA KUKATAA KUINGILIWA NA MUME WAKE IKWA TUU ETI MUME ANATATIZO LA KUWAHI KUFIKA KILELENI? NA MWAMUME HUYU ANAJITAHIDI KUMTAYARISHA IPASAVYOO ILA KE HATAKI KABISAAA NINI LA KUFANYA.







JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani kwa swali lako kuhusu tatizo ulilonalo na ndoa na mkeo.



Katika mas-ala ya wanandoa kustarehe na mwenziwe haifai kwa mume kumkatalia mkewe na kinyume chake. Na ikiwa mke atakataa kumstarehesha mumewe, na mume akalala akiwa amekasirika basi mke analaaniwa na kila kiumbe mpaka mume amridhie. Kwa hiyo, si haki kwa mkeo kukataa kukustarehesha kwa sababu una tatizo.



Huenda ikawa anaumia na anapata machungu lakini kukiwa na tatizo ni muhimu kwa wanandoa kusaidiana ili kufikia suluhisho muafaka. Katika kutatua tatizo hilo inabidi wewe na mkeo mkae kitako kama wanandoa na kutazama ni njia gani mnaweza kutumia ili mpate suluhisho na muishi kwa wema na uzuri. Mke ni muhimu akusaidie ili kila mmoja aridhike. Kwa ajili hiyo, inafaa mkeo apewe ushauri nasaha kuhusiana na hilo.



Pili kuna haja kubwa sana kwako kwenda kwa daktari au twabibu ili upate dawa kwani huo ni ugonjwa. Na hakika ni kuwa Allaah Aliyetukuka hakuteremsha ugonjwa isipokuwa Ameleta na dawa yake. Hivyo, tafuta dawa kuhusiana na tatizo lako hilo.



Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

Mume Ana Tatizo La Kumaliza Kabla Ya Mkewe Kwenye Tendo La Ndoa

Ikiwa Hawaridhiani Katika Kitendo Cha Ndoa Wafanye Nini?

Mume Hamtoshelezei Matamanio Yake Ya Tendo La Ndoa, Anaomba Ushauri



Na Allaah Anajua zaidi
 
Anampenda Sana Mume Wake Lakini Hawana Raha Katika Tendo La Ndoa, Wafanyeje?
Maswali: Maingiliano
SWALI:



A'laykum.



Mimi nina matatizo katika ndoa yangu hatuna hamu ya kufanya tendo ila tunafanya kwa ada tu ya ndoa. Hatusisimkwi katika tendo huwa hakuna raha ya aina yoyote kati yetu. Mimi huwa sijawahi kusikia raha hata mara moja na pia mume wangu amenithibitishia hilo. Na kuoa mke mwengine hana uwezo wa kifedha wala kumtimizia mahitaji yake ya lazima ni mgonjwa, anachoumwa huwa hakijulikani na pia kuniacha anasema hawezi nahofia atavunja msikiti na kujenga kanisa. Na pia anahofia watoto wake. Ni kiwa kwetu hunipenda sana na kunitamani.



Naomba kwa ajili ya allah munieleweshe nini nifanye kwa huyu mume mimi nampenda mume wangu sana









JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kumpenda sana mume lakini kutokuwa na raha katika tendo la ndoa.

Furaha ni kwetu kwa kutuelezea kwa uwazi bila kuficha tatizo mlilo nalo. Matatizo kama hayo hutokea katika maisha ya ndoa baina ya wanandoa. Zipo sababu nyingi ambazo hupelekea hilo:



1. Huenda mume aliingia katika ndoa bila kuwa tayari au kutayarishwa katika hilo.




2. Huenda kuwa alichaguliwa bila mwanzo kuwa alikuwa na hamu ya kukuoa.




3. Huenda ya kuwa mume na mke hawajafahamu cha kufanya katika tendo la ndoa.




4. Kukifanya kitendo hicho kuwa ni ada na sio Ibaadah.




5. Huenda mume ana ugonjwa ambao unamfanya asiwe na raghba ya kitendo hicho.




6. Huenda mume amefanyiwa sihri na hivyo kutakiwa kufarakanishwa na mkewe kwa sababu moja au nyingine. Au huenda ikawa ni hasad.



Yale yanayotakiwa kufanywa kuhusu matatizo yanayowakumbwa ni kujaribu kwa kiasi kikubwa kufanya yafuatayo:






1. Ikiwa aliingia katika ndoa bila kuwa tayari au alichaguliwa bila kupenda ajitayarishe na akuridhie kwa Niyah safi kama mke wako na aache yote mengine nyumbani. Aanze kuganga yajayo. Na kubadilisha kwake kwa Niyah kutawapatia fursa ya kutengeneza hayo msiyosikia kwayo raha.




2. Huenda ikawa hampati starehe kwa kuwa hamjajaribu kupata maelekezo ya Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu raha hiyo. Kinachotakiwa ni kujitayarisha kwa kitendo hicho kila mmoja kwa mwenziwe. Na huko ni kuoga mkawa safi, kila mmoja kujirembesha kwa mwenziwe kwa kujipaka manukato ili yafumuke mahaba baina yenu. Na inatakiwa mume na mke wapeane mazungumzo matamu yanayohusiana na kitendo ambacho mnataka kukifanya. Na kabla ya kuanza kitendo chenyewe inatakiwa muanze na kushikana sehemu nyeti, kupigana busu na mengineo ambayo yataongeza ashiki ya kila mmoja wenu. Ikiwa mnahisi karibu ya kufikia kilele hapo ndio mnaweza kukamilisha kwa jimai.




3. Mnatakiwa mfahamu kuwa kitendo hicho si ada bali ni ‘Ibaadah kama Swalah, Zakah au Hijjah. Kwa kuwa shughuli hiyo ni ‘Ibaadah ifanywe kwa hamu na kwa ukamilifu.




4. Muwe mnasoma Qur-aan kwa wingi na huku katika nyakati za kujibiwa muwe mnamuomba Allaah Aliyetukuka Awaondolee tatizo hilo. Kwa mfano kuomba mnapofunga kama Jumatatu na Alkhamiys, mnapoinuka usiku wa manane kwa ajili ya Tahajjud na kadhalika

.

5. Aende mume akasomewe na Shaykh ambaye ni mchaji Mungu na kisomo cha kishari’ah ili ibainike kama amefanyiwa sihri au la.



Kwa kufanya hayo tunaamini kuwa kwa uwezo wa Allaah Aliyetukuka atakuwa ni mwenye kupona na kuwa katika hali njema na nzuri inshaAllaah.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Anapata Dhambi Akimkatalia Mumewe Kitendo Cha Ndoa Kwa Ajili Ya Machofu Ya Kazi?
Maswali: Maingiliano
SWALI:



Asalam alaikum warahma tullah wabarakat



Ama baad, Mimi ni mfanyakazi nimeajiriwa natoka kazini nimechoka sana na mume wangu anataka jimai kila siku mimi nakataa kwa kuwa nahitaji huruma yake ikiwa mimi ndio natoa mchango mkubwa katika familia je napata dhambi au niko sawa maana nimesikia mungu hakalifishi nafsi ya mtu inakuwaje binadam anikalifishe hili ni tatizo kwangu



JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Asli katika kustarehe na kuingiliana baina ya mume na mke ni kuwa hakuna siku maalumu au mara maalum, bali kila ikiwepo hamu ndio vizuri tendo la ndoa kupatikana, na kama mmoja hayuko na hamu kwa sababu yoyote ile basi huwa hakuna raha katika tendo hilo. Hata hivyo wako Maulamaa waliosema kuwa ni wajibu wa mume kumuingilia -kima cha chni - japo mara moja mkewe katika kila miezi minne ikiwa hana udhuru wowote ule, vyenginevyo atakuwa amekwenda kinyume na mafundisho ya dini.



Hata hivyo hilo tendo la ndoa ni haki ya kila mmoja wenu kwa mwenziwe na ikiwa mumeo ni mtu ambae anahitaji jimaa kila siku basi lililobora na ndio mafundisho ya Uislamu kumtafutia mke mwengine ili asije kuingia katika uchafu kama wewe huwezi kukidhi haja yake kwa sababu moja au nyingine. Vinginevyo unaweza ukawa miongoni mwa wenye kulaaniwa na Malaika kama ilivyothibiti katika Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“Atapomwita mume mkewe kuelekea kwenye kitanda chake -kwa tendo la ndoa- basi mke akikataa kuitikia wito huo na mume akalala hali ya kuwa ameghadhibika -hakuridhia- basi mwanamke huyo huwa analaaniwa na Malaika mpaka kupambazuke” Imepokelewa na Muslim, kitabu cha ndoa, mlango uharamu wa kujizuilia mke na firaashi ya mumewe.



Hivyo basi ni wajibu wa mke kumkubalia mumewe anapomwita kitandani kwa ajili ya tendo la ndoa, isipokuwa akiwa mgonjwa ama hali yako wewe ya kuchoka kwa sababu ya kuchapa kazi bila ya kujifikiria majukumu yako mengine. Kufanya kazi ni jambo zuri lakini jifikirie pia kuwa na wakati wa kupumzika; kwani ikiwa hiyo ndio sababu ya kutoweza kuitikia wito wa mume basi yawezekana ikawa kila siku wewe ni mja wa kuchoka kwa kufanya kazi, na fahamu kuwa si wajibu kwako kutoa mchango wowote ule katika familia hilo ni jukumu la huyo mume; na huenda ikawa sababu moja ya kuwa mumeo anataka kila siku ni kuwa yeye hana la kufanya ila hilo na kama akifanya kazi basi huenda akapunguza siku ya kutaka tendo la ndoa badala ya siku zote.



Pia mshauri mumeo awe anafunga Swawm za Sunnah ili apunguze matamanio yake, na mpunguzie vyakula vyenye kuongeza nguvu mwilini na mpendekezee kujitafutia cha kufanya kama kuogelea, kukimbia, au mazoezi mengineyo ili achoke na kasi yake ipungue.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Amejimai Na Mumewe Akiwa Katika Hedhi Kwa Kughafilika Je, Afanyeje?
Maswali: Maingiliano
ASSAALAAM ALAYKUM,



MIMI NINA SWALI MOJA AMBALO NINANITATIZA MIE NA MUME WANGU. KWA BAHATI MBAYA, SIKU MOJA WAKATI NILIKUWA KATIKA SIKU ZANGU ZA HEDHI TULIFANYA TENDO LA NDOA ILIKUWA BAHATI MBAYA WALA HATUKUSUDIA. TULIZIDIWA NGUVU WOTE WAWILI. NILIKUWA KATIKA SIKU YANGU YA MWISHO NA ILIKUWA SIKU YA PILI TU NIJITOHARISHE, LAKINI BAADA YA KUFANYA TENDO HILO NIMEJIKUTA NIMETOKA DAMU TENA KWA WAKATI ULE ILA HAIKUENDELEA. MUME WANGU SIKU YA PILI HAKUWA NA RAHA NA KUJILAUMU KWA NINI TULIJISAHAU. JAMBO HILI LIMEKATAZWA NA S.W JEE TUFANYE NINI ILI TUOMBE MAGHFIRA KWA MOLA WETU?




JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kujimai na mume, mke akiwa katika hedhi.

Haifai kwa mume kujamiiana na mkewe akiwa katika hedhi au nifasi mpaka atwaharike (al-Baqarah [2]: 222). Hata hivyo, Uislamu umemuacha huru mume na mke kufanya mengine yote mbali na jimai. Ikiwa mke atakuwa amefunga sehemu zake za siri basi mumewe anaweza kufanya naye mengine yote ambayo mume anaweza kufanya na mkewe ila kumuingilia mbele au kwa nyuma. Kufanya moja ya hayo mawili ni madhambi kwa wenye kufanya hilo.


Inayotakiwa kwa mume kujitahidi sana asiingie katika kufanya tendo la ndoa wakati mke yuko katika hedhi ili wasiingie katika haramu kama mlivyofanya. Ni vyema muweze kushindana na matamanio, kwani matamanio yakiwa hayatawekewa vikwazo yatampeleka mtu katika ushirikina...wakawa kama wale waliofanya matamanio yao kuwa ndio mungu wao! Ikiwa mume na mke wanaona hawawezi kujizuilia ni vyema wachukue tahadhari ya ziada ili wasiingie katika haramu na madhambi.


Nyinyi wanandoa ndio mnaojua kuwa hilo tendo mlilofanya ni bahati mbaya au vinginevyo. Ikiwa kweli ni bahati mbaya basi mtatubia kwa kutimiza masharti yafuatayo:



1. Kuacha dhambi hilo, usilirudie tena.

2. Kujuta kwa kutekeleza kosa hilo.

3. Kuazimia kutorudia tena dhambi hilo.



Kulingana na swali lako ni kuwa mmetekeleza masharti hayo tuliyoyataja hapo juu. Mbali ya hayo ya kutubia iko kafara kama anavyotueleza Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika uhusiano wa mtu atakayemuingilia mkewe wakati yuko kwenye hedhi kama ifuatavyo: “Mwache atoe dinari moja katika sadaka au nusu ya dinari” (at-Tirmidhiy, Abu Daawuud na atw-Twabaraaniy, nayo ni Swahiyh).


Kwa hiyo, yeyote aliyeteleza akafanya kosa la jimai na mkewe wakati yuko katika hedhi na kabla ya kuwa ametohirika, itampasa atoe thamani ya uzito wa dinari ya dhahabu au kwa wakati huu ni kiasi cha thamani ya gramu 4.25 ya dhahabu au nusu yake.


Bonyeza viungo vifutavyo kwa malezo zaidi:

Hukmu Ya Kitendo Cha Ndoa Katika Hedhi

Nimemuingilia Mke Wangu Akiwa Katika Hedhi. Je, Ndio Sababu Ya Kukosa Uzazi/Watoto?

Na Allaah Anajua zaidi
 
Alama Za Mapenzi Unaweza Kuswali Nazo
Maswali: Maingiliano

SWALI:

Asalam alaikum, nashukuru alhamdulillah kwa kuwepo chomba hichi ambacho tunaweza kuuliza maswali ambayo yanatutatiza na inshallah mtanijibu kamaa inavyotakiwa kwa uwezo wake allah (s.w). Suala langu hili eti kufanya tendo la ndoa na mumeo au mkeo na kuwa na kwenye mwili wako ukawa mna love bite ni vibaya na eti huwezi kusali sala yako haikubaliwi? Samahanini sana kuweka neno hili kwani sijui nielezee vipi lkn nategemea inshallah mtakuwa mmelifaham. nategemea jibu lenu






JIBU:

Shukrani zote anastahiki Allah, Muumba wa kila kitu Swalah na salamu zimfikie kipenzi chetu, Mtume Muhammad (s.a.w.), ali zake na Masahaba zake na wanaowafuata kwa wema mpaka siku ya Kiyama.

Katika mas-ala ya kidini hapana haya kwani wanawake wa Kiansari walikuwa wanauliza zaidi ya hayo na bila kuuliza jambo ambalo una shaka nalo basi hakutapatikana ufumbuzi.

Hakika ni kuwa love bites (alama za kimapenzi) si moja katika mambo yenye kuvunja Swalah, kwa hivyo unaweza kuswali nazo na Swalah yako ipo sawa sawa.

Na Allah Anajua zaidi.
 
Mume Kahama Chumba Kwa Miezi 3 Hafanyi Tendo La Ndoa, Akiulizwa Anasema Anachoka Kazini
Maswali: Maingiliano
SWALI



asalaam alaikum

nilituama maswali yangu wiki iliyopita naona bado sijapata jibu kuhusu mume wangu anavyoninyanyasa na hatuishi kama mtu na mume wake ndani ya nyumba yeye analala kwake na mimi chumba changu bila sababu na hata kitendo cha ndoa inafika muda wa mienzi 3 or 4 kila nikimhitaji ananiambia yeye sio robort sasa katika sheria ya dini itakuaje? na mimi nimestahmaili muda wa miaka 8 sasa maisha yangu yote kama hivi sina haki kwake kama mkewe,sasa nilikuwa naomba msaada wenu nifanye nini?



mimi …… nilikuwa nataka kufahamu vizuri kuhusu ndoa yangu,mimi na mume wangu kuna matatizo fulani hataki kuwa na mimi kwenye kitendo cha ndoa amehama chumba muda wa miwnzi 3 on and off sifahamu kwa nini nasema nae ananijibu anachoka kwa kazi sasa kidini inakuaje si mara ya kwanza tangu tuoane miaka 8 kama tabia sasa tafadhali nisaidieni hii ndoa gani mpaka sasa sijijui vipi maisha yangu naona siyafaham na umri unapotea nimevumilia sana almost 7yrs naona hakuna mabadiliko so nimewauliza swali langu nashukuru mmenijibu kuwa mtanfahamisha. sasa ndugu zanguni naomba mnisaidie maswala yangu naona sijifahamu shukran salaam alaikum



JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.





Moja katika haki ya mke na mume ni kuingiliana na kama ulivyosema, mimi na mume wangu kuna matatizo fulani hataki kuwa na mimi kwenye kitendo cha ndoa amehama chumba muda wa miezi 3 on and off sifahamu kwa nini nasema nae ananijibu anachoka kwa kazi. Basi elewa kuwa katika ndoa hii kuna tatizo la kimsingi la watu kutakiwa kuoana. Na utatuzi wake ni kuwa kama huyo mume baada ya kuwa na kazi ambayo inaonyesha imemvunja na kufikia kuwa hawezi kukutimizia haki yako basi mke unayo haki ya kudai talaka kwani huenda ukajikuta katika maasi kwa kutamani kuingiliwa. Ikiwa mwenye uhalali huu hana uwezo na si lengo la ndoa katika Uislamu kukaa mwanamke chini ya mwanamume asiyeweza kumuingilia. Na kama tatizo ni kuchoka kwa maana ya kuchoka tu basi msharui mumeo apunguze muda wa kazi au atafute kazi nyengine itayomuwezesha kuweza kuifanya kazi ya kumuingia mkewe kwani hiyo pia ni katika kazi anazotarajiwa kuzifanya.

Ikiwa umeshindwa kumshauri mwenyewe basi tafuta jamaa zako na jamaa zake ushitaki hali yako upatiwe suluhisho.

Na Allaah Anajua zaidi
 
Mume Au Mke Hawezi Tendo La Ndoa Kwa Zaidi Ya Miaka 5, Hukmu Ni Nini?
Maswali: Maingiliano


SWALI:



A friend asked me on the standpoint of Islam on the following issues:-

if a husband/ or wife has failed/ cannot perform the act of marriage to his lawful wife due to incapability (either health, accidents among the reasons) and this has persisted for a duration of more than 5 years and would like to raise up a family:- Should the couple remain as pairs? What options are there if this situation persists?









JIBU:




Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.







Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu tendo la ndoa kwa mume au mke asiyejiweza. Uislamu uliokamilishwa na Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam) umekuja kutazama maslahi ya mwanadamu. Uislamu wenyewe unakwenda sambamba na maumbile ya mwanaadamu.



Uislamu umekuja kumuondolea madhara klila mmoja wetu kwa njia tofauti. Katika hayo ni matatizo yanayopatikana kwa wanandoa pindi tatizo linapoibuka kwa njia moja au nyingine kama ugonjwa, madhara, na kadhalika. Katika hali ya ugonjwa au mume kutoweza kutenda tendo la ndoa, uamuzi unaachiwa mke mwenyewe. Ikiwa mke ameamua kubaki na mumewe ili kuendelea kumtunza na kumhudumikia basi atapata thawabu zake. Ama ikiwa hawezi kujizuia kwa kuwa hataweza kutimiziwa mahitaji yake ya kimwili, anaweza kwenda kwa Qaadhi na kulingana na sababu hizo ambazo zinaweza kumletea madhara makubwa zaidi. Qaadhi atamwachisha na baada ya eda ataweza kuolewa na mwingine.



Ama ikiwa mgonjwa ni mwanamke, basi mume anatakiwa amfanyie ihsani kwa kumbakisha mke huyo kama mke wake naye aoe mke wapili kwani sheria ya Kiislamu imempatia yeye fursa hiyo ya kuoa zaidi ya mke mmoja. Lau ataona uzito wa kuwaweka wake wawili kwa pamoja basi yeye amepatiwa ruhusa na sheria ya kumpatia talaka mkewe ili aweze kuoa mke mwengine. Hata hivyo, atakuwa na thawabu zaidi lau ataweza kumwangalia mkewe ambaye ni mgonjwa kwa kubaki naye.



Kwa muhtasari ni kuwa Uislamu umewaachia wanandoa uamuzi kunapotokea tatizo kama mme kutojiweza, ugonjwa, madhara na kadhalika.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Mume Hamtoshelezei Matamanio Yake Ya Tendo La Ndoa, Anaomba Ushauri
Maswali: Maingiliano
SWALI:

Salaam alaykum warahmatullah wabarakatuu, Mimi ni mwanamke mwenye miaka 22 nimejaaliwa kupa ndoa ambayo mpaka sasa imetimia miaka 2 na tumejaaliwa kupata mtoto mmoja ila cha kunishangaza kwa sasa hivi mume wangu kabadilika sana sielewi kwa nini kila ninalojaribu kumueleza hanisikii na ananipangia mpaka siku za kufanya tendo la ndoa na kuniambia kuwa anachoka ndio maana pengine inaweza ikafikia hata siku 5 sijapewa haki yangu na mpaka siku ingine naililia lakini mafanikio yangu hayatokei. Na pengine tunapokuwa faradha huwa anamaliza kabla yangu mimi nakua sijatoshelezeka lakini ninastahmili, sasa sielewi mwenzangu ana nini naomba ushauri



JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kupata shida katika tendo la ndoa na mumeo. Tufahamu kuwa tatizo hilo huweza likampata mume au mke kwa sababu moja au nyingine.

Kulingana na swali lako inaonyesha kuwa mlikuwa mkiishi baada ya harusi katika hali iliyo nzuri na tendo la ndoa lilikuwa sawa. Tatizo hili limeanza kujitokeza hivi karibuni. Tatizo hili huenda likawa limetokea kwa kupatikana moja wa sababu hizi:

Huenda akawa mumeo ameanza kutumia uraibu wa mirungi au miraa.
Huenda ikawa ni maumbile yake yamebadilika kwa kupungua kwa ashiki yake na nguvu zake za kiume.
Huenda akawa amebadilika tabia na ana uhusiano mwengine wa nje ya ndoa.
Sababu zote hizi ambazo tumezitaja zinaweza kuondoka kwa kutumia dawa ya sawasawa kutegemea na tatizo lenyewe. Ikiwa ni mtumiaji wa miraa/ mirungi, utumiaji huo unamfanya awe ni mwenye kutokwa na madhii anapokuwa akitumia, hivyo anapofika kwako huwa anamaliza haja yake mara moja.

Ama kwa tatizo la pili, ni lazima mumeo aone kuwa ana tatizo na hivyo akubali kufanya dawa. Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam) anatueleza kuwa Allaah Aliyetukuka Hakuleta ugonjwa isipokuwa Ametupatia na dawa yake. Mnaweza kwenda naye kwa daktari mahiri katika magonjwa hayo ili aweze kumpatia dawa kwa ugonjwa wake huo. Na dawa ambazo hazina madhara ni zile za tiba asilia au tiba ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam) na tajruba iliyopatikana na matabibu wa Kiislamu waliofanya utafiti kuhusu magonjwa tofauti. Na moja katika dawa ni hawlinjaan, ambayo inatumiwa na mwanamme nusu saa kabla ya kitendo cha ndoa. Kijiko kimoja cha chai hutiwa katika kikombe cha maziwa au maji na kunywa. Lakini itakuwa ni bora aonane na tabibu ambaye atamchunguza na kumpatia dawa muafaka.

Tatizo la tatu, ikiwa utahakikisha hilo kwa dalili mbalimbali, basi ni bora umkalishe na mzungumze kwa uwazi kabisa na umpe onyo aache tabia hiyo chafu kabisa inayomuudhi Allaah na kumchumia madhambi makubwa, na pia umweleze hatari ya magonjwa makubwa yaliyozuka na pia athari anayoweza kupata yeye, wewe na hata mtakachokizaa. Ikiwa kweli tatizo ni hili la tatu, basi baada ya kumketisha na asisikie, jaribu kuitisha kikao cha jamaa zako na jamaa zake ili mlijadili hilo kwa kina.

Tunawaombea tawfiki na kurudi katika hali yenu ya kawaida kama hapo awali.

Na Allaah Anajua zaidi
 
Mke Analalamika Mume Ana Mashetani Yanamfanya Asiweze Kukamilisha Tendo La Ndoa
Maswali: Maingiliano


SWALI:



Mimi ni mwana ndoa na bahati mbaya mume wangu ana matatizo ya mashetani, wakati wa tendo la ndoa huwa hawezi kufanya lolote au muda mwengine kuwa anashindwa njiani, jee Sheikh kuna dawa gani za kidini na za kiislamu ambazo mwanadamu mwenye tatizo kama hili hutumia na kuondokana na tabu hii?naomba msaada wenu ishAllaah, Wabillah Tawfiq.







JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa dada yetu muuliza swali na tunapenda kukutoa wasiwasi kuwa hatuweki majina ya waulizaji.



Hili ni tatizo ambalo mwanaume au mwanamke anaweza kukumbwa. Akiwa mwanaume anaweza kukumbwa na jini la kike ambalo linamuhangaisha na hivyo kushindwa kumtimizia mkewe kitendo cha ndoa. Na akiwa mwanamke anaweza kukumbwa na jini la kiume ambalo linalala naye na kumuhangaisha kimapenzi hivyo kutoweza kukutana na mumewe kwani nguvu za jini ni kubwa. Baada ya jimai na mwanamke huwa mchofu hivyo kutoweza kufanya tendo la ndoa na mumewe.



Tatizo hilo lina tiba na tiba yake si kwenda na wachawi kama wanavyofanya wengi miongoni mwetu. Bali tiba yake mwanzo ni wewe kujitibu mwenyewe kwa kusoma kisomo cha Qur-aan na Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambazo zinampatia kinga mwenye kusoma. Hizi inatakiwa mtu asome asubuhi na jioni. Na kinga hii huitwa Ruqyah. Unaweza zaidi kusoma kuhusu Ruqyah hapa:





Taratibu Za Ruqyah Na Yapasayo Kufanywa Kabla Ya Kusoma Ruqyah





Pia kusoma Aayah kadhaa za Suratul Baqarah (1 – 5, 255 – 257 na 284 – 286), Suratul Ikhlaas na Mu'awwidhatayn (Qul A'udhu birabbil Falaq na Qul A'udhu birabbin Naas). Na ikiwa mtu amekumbwa na jini basi anaweza kwenda kwa Shaykh mwenye kuaminika elimu yake na ucha Mungu wake ambaye atasoma baadhi ya Aayah za Qur-aan ili kumtoa, kisomo ambacho kitafahamika na kinacho kwenda sambamba na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).



Soma pia Adhkaar za asbuhi na jioni kwa mfululilzo bila kuacha ni tiba na kinga kubwa:




Hiswnul-Muslim: Du’aa Na Adhkaar Kusoma Na Kwa Kusikiliza (Toleo Lilohaririwa)



027-Hiswnul-Muslim: Nyiradi Za Asubuhi Na Jioni





Soma pia Swali na jibu lifuatalo ambalo lina maelezo zaidi kuhusu matatizo kama hayo:



Mke Wangu Amevaliwa Na Majini Wa Mahaba? Hapendi Kutenda Kitendo Cha Ndoa Na Mimi



Pia ni muhimu kwa kumkinga mtoto kabla ya kuzaliwa kwa wanandoa kusoma dua wakati wanapofanya jimai nayo ni kusema duaa katika kiungo kifuatacho:



081-Hiswnul-Muslim: Du’aa Kabla Kujimai (Kumuingilia Mke)



Anasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akizaliwa mtoto hatasogelewa na Shaytani (al-Bukhaariy).



Na Allaah Anajua zaidi
 
Naam kama nilivyo sema huko nyuma lengo letu ni watu kupata elimu ya dini,hivyo tutaelimika kwa mambo mengi sana

Tutapitia pia kitabu hiki

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Kitabu Cha Utangulizi Wa Maudhui Mbalimbali

Kutakuwa na masomo.mbali mbali ambayo tutanufaika nayo
 
Back
Top Bottom