Ili mtu awe na imani lazima amuamini Allah ukweli wa kumuamini,kwamba hakuna yeyote anayepaswa kuabudiwa kwa haki au kususudiwa kwa lolote isipokuwa Allah,na kwamba wala hana mshirika katika ufalme wake na uumbaji
Haifai kwa mtu yoyote kufanya ibada kinyume na kumuabudu Allah,haifai kuombwa na kutakwa msaada kwa yeyote isipokuwa Allah
Kufanya ibada na kukusudiwa kiumbe kingine tofauti na Allah,hio ni shiriki au ushirikina ambao ni dhambi kubwa sana mbele ya Allah,na lau mtu akafa na itikadi hii basi huyo ni wa motoni Milele
Lakini kwa masikitiko makubwa kuna waislamu ambao ama kwa kujua au kutokujua wanaingia katika mkumbo wa kushawishiwa na marafiki na majirani zao kwenda kuombewa na hawa manabii na mitume wenye majina yao hapa mjini,pasina kujua kwamba wanamshirikisha Allah
Kule wanaombewa kwa kuegemeza nguvu zao kwa kiumbe ambacho kimeumbwa na Allah,yaani kiumbe cha Allah kimepewa sifa ya uungu ambacho hakina
Katika qur'an inaelezwa siku ya kiama,Issa bin Mariam ataulizwa,je uliwaambiwa watu wakuabudu wewe na mama yako?
Mja huyu wa Allah atasema "hakika haipaswi kwa mimi kusema maneno hayo,hakika ulikuwa na mimi nilipokuwa nao,na hao ni viumbe wako,ama ukiamua utawahukumu au utawasamehe"
Hayo ni maneno ya mja wa Allah,hakika aliondoka duniani na itikadi moja tu kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah,na hii ilikuwa ndio desturi ya mitume wote wa Allah
Changamoto zako za maisha zisikufanye ukafanya shiriki na baadae ukaja kuangamia
Ntakuja kuendelea na kipengele kingine inshallah
Tumche Allah ukweli wa kumcha