Ramadhan Special Thread
Naam ndugu zangu katika imani,sasa ebu tuangalie mambo ya HESABU

Inaposemwa kuamini juu ya hesabu ni kuamini kwamba tunahesabiwa kwa matendo yetu tunayo fanya,kila jema au ovu unalofanya linaingia katika akaunti ama ya mema au mabaya

Na Allah wallah ni rahim mno,jema moja hulipwa thawabu kumi mfano wake na ovu moja hulipwa kwa ovu moja tu,lakini inashangaza maovu yatashinda mema na mtu kuingia motoni! Allah atujalie tusiwe miongoni mwao

Na jema moja kulipwa thawabu kumi ni kwa uchache lkn malipo hufikia mpaka mara mia saba na zaidi,na hii itatokana na nia yako unapofanya jambo hilo husika,nia yako ikiwa madhubuti kabisa kwa kutaka radhi za Allah basi utapata malipo zaidi

Kwahiyo ni jukumu letu kufanya mambo ya kheri zaidi ili tukusanye thawabu nyingi zaidi ili besabu zetu ziwe nzur zaidi

Kuonyesha ukarimu wa Allah juu ya waja wake,ukinuia tu kufanya jambo jema na bahati mbaya usilifanye basi unalipwa thawabu moja,na lau ukalifanya unapata kumi mfano wake

Na ukinuia kufanya jambo baya na usilifanye unalipwa jema moja au unapata thawabu moja na lau ukalifanya unapata ovu moja,ebu angalia jinsi Mola wetu mtukufu alivyokuwa mkarimu mno

Sijui huwa tunafeli wapi?

Kikubwa jitahidi sana kuwekeza katika mambo ya kheri ili kesho akhera uwe miongoni mwa waja wenye kupata rehma za Allah,na tujitahidi sana kuwekeza katika mambo ya kheri ambayo ya kuendelea hata kama tutaondoka hapa duniani basi tuendelee kupata hesabu nzuri

Mfano chimba kisima,panda miti yenye kivuli na matunda ambapo watu watanufaika,jenga misikiti kwa kuchangia sadaka zako katika ujenzi wa nyumba za Allah,jenga madrassa na mambo kama hayo,haya mambo hata ukifa bado utaendelea kuchuma thawabu

Na mwezi huu wa ramadhani kama uchumi wako unaruhusu toa sana sadaka kwa ajili ya Allah kwani malipo yake ni marudufu

Swali sana swala za sunna ikiwemo tarawehe kwani kipindi cha ramadhani swala ya sunna hulipwa kama swala ya faradhi na swala ya faradhi hulipwa mara sabini,ewe mja wa Allah huu ni mwezi wa kuchuma basi pambana upate machumo bora zaidi

Kwahiyo amini katika hesabu za matendo yako na ndio hizo zitakuwa mustakabali wako wa kuingia peponi au motoni

Tumche Allah
 
Tumalizie darsa yetu juu ya IMANI kwa kuangalia kipengele cha MIZANI

Ndugu zangu hakika Allah amejiharamishia dhuluma yeye binafsi na ametuharamishia na sisi pia,kwahiyo hakika Allah ndio hakimu muadilifu

Siku ya kiama matendo yetu mazuri na mabaya yatapimwa katika mizani ya uadilifu,kama matendo mema yatakuwa mazito zaidi kuliko maovu basi mja huyu ataingia peponi na kama upande wa mzani wa matendo maovu ukawa mzito zaidi kuliko upande wa mema basi mja huyu ataingia motoni milele,Allah atuhifadhi tusiwe miongoni mwao

Katika suratll alqaria,Allah anasema;


101:1 - Inayo gonga!
101:2 - Nini Inayo gonga?
101:3 - Na nini kitacho kujuilisha nini Inayo gonga?
101:4 - Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika;
101:5 - Na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa!
101:6 - Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito,
101:7 - Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza.
101:8 - Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu,
101:9 - Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya!
101:10 - Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo?101:11 - Ni Moto mkali!
 
Na kuna aya nyingi sana zinazo zungumzia na.kusisitiza kwamba hakika matendo yetu yatapimwa kwenye mizani

Na Allah anasema hakika yeyote atakayefanya jambo dogo jema kama mbegu ya hadar au unyuzi wa kokwa ya tende basi utauona wema wake na yeyote atakaye fanya ovu hata kama dogo kama chembe ya hadari atauona uovu wake

Kisha yote hayo hukusanywa na kama ni mambo mema yatawekwa upande mmoja wa mzani na kama mabaya nayo yatakusanywa na kuwekwa upande wa pili mzani kisha majibu tutayapata

Kikubwa tambua mwanadamu upo salama tu pale unapokuwa hauongei au hauandiki,kwa maana kutoa yaliyopo ndani ya nafsi yako,umati huu Mtume Muhammad ambao hata wasio waislamu wapo tumesamehewa mambo ambayo yapo vifuani mwetu au mawazoni mwetu,lkn tukiongea tu wapo waandishi wanaandika kila kitu na mwisho wa siku mzani unahusika

Ndio maana Mtume Muhammad alisema watu wengi sana wataingia motoni kwa sababu ya ulimi na tupu zao,kwa maana mdomo utatuponza na zinaa

Kwahiyo tukijitahidi katika sehemu hizo mbili tutakuwa katika sehemu nzuri

Mwisho kabisa mtu yoyote akikiri kwamba Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah ataingia peponi baada ya kuingizwa motoni kwa madhambi yake

Yani muislamu hata mwenye chembe ndogo ya imani pamoja na kutotenda mema lkn kwanza ataingia motoni kupata adhabu yake kwa miaka kadhaa kisha baadae atasamehewa lkn kwa kafiri ambaye ana mpinga Allah na kuabudu viumbe yeye ataingia motoni milele kwakuwa amemkataa Allah naye atamkataa siku ya kiama

Alhamdulillah tumemaliza darsa.letu juu ya IMANI, kama nimepatia basi ni kwa kuwezeshwa na Allah na kama kuna mapungufu kwakuwa binadamu hajakamilika basi hayo ni mapungufu yangu na Allah naomba unisamehe

Subuhanaka allahuma wabihamdiki ashahadu anlaa ilah ila anta astaghfiruka waatubu ilayk ( dua hii ni kafara ya madhambi baada ya mazungumzo yoyote yale,kwani tunaweza zungumza mambo kumbe hatujui ni makosa mbele ya Allah,kwahiyo jitahidi kuitumia kila baada ya kumaliza mazungumzo yako- amefundisha Mtume swallallahu alaih wassallamu)

Tumcha Allah ukweli wa kuamcha
 
Kesho panapo majaliwa tutaangalia NGUZO ZA IHSANI

Hakikisha unaufollow huu uzi walau waeza kuokoteza chochote kitakacho kukusaidia katika uislamu wako

Jioni njema na iftar njema
 
Tusisahu kuwaombea na Ndugu zetu Wapalestina.
IMG_20250319_182527.jpg
 
Umuhimu Wa Kukimisha Swalaah



Alhidaaya.com









Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْغَيْبِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿٣﴾

Ambao huamini ya ghayb na husimamisha Swalaah na katika vile Tulivyowaruzuku hutoa. [Al-Baqarah: 3]



Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):





وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ ﴿٥﴾

Na hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Allaah wenye kumtakasia Dini, wenye kujiengua na upotofu kuelemea Dini ya haki na wasimamishe Swalaah na watoe Zakaah; na hiyo ndiyo Dini iliyosimama imara. [Al-Bayyinah: 5]



Maana ya kukimisha Swalaah:



Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: “Ni kuswali kwa kuzingatia nguzo na sharti zake.” Adhw-Dhwahaak amesema kuwa Ibn ‘Abbaas alisema: “Iqamaat Asw-Swalaah maana yake ni kukamilisha rukuu, sujuwd, kusoma Qur-aan, khushuu (unyenyekevu), na kuhudhurisha moyo katika Swalaah.” Qataadah alisema: “Iqamaat Asw-Swalaah maana yake ni kuchunga wakati, wudhuu, rukuu na sujuwd za Swalaah.” Muqaatil bin Hayyaan alisema: “Iqaamat Asw-Swalaah ina maana: Kuchunga wakati, kujitwaharisha kwa ajili yake, kukamilisha rukuu, sujuwd na kusoma Qur-aan, tashahhud na kumwombea rahmah Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Hiyo ndiyo Iqaamat Asw-Swalaah.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]





Swalaah ni nguzo ya pili katika Uislamu na nguzo hii Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ametufanyia kuwa ni waajib ili iwe ni hakikisho kuwa tunabaki kwenye njia ya Uislamu ambayo inaongoza kwenye Rahmah Zake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na maghfirah na manufaa yetu ya duniani na Aakhirah.





Swalaah ni kiunganisho chetu kwa Rabb wetu ‘Azza wa Jalla. Ndio maana Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema kuwa pindi tunapotaka msaada Kwake basi tuutafute msaada huo kwa Subira na Swalaah na hapo Yeye Atakuwa pamoja nasi kama Anavyosema:



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الصَّابِرِينَ ﴿١٥٣﴾

Enyi walioamini! Tafuteni msaada kwa subira na Swalaah; hakika Allaah Yu pamoja na wanaosubiri. [Al-Baqarah: 153]

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَاسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ ۚ وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلَّا عَلَى الْخَاشِعِينَ ﴿٤٥﴾

Na tafuteni msaada kupitia subira na Swalaah; na hakika hilo ni kubwa isipokuwa kwa wanyenyekevu. [Al-Baqarah: 45]





Swalaah pia Inafuta madhambi na kutukinga na machafu; Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَأَقِمِ الصَّلَاةَ ۖ إِنَّ الصَّلَاةَ تَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ

na simamisha Swalaah, hakika Swalaah inazuia machafu na munkari. [Al-'Ankabuwt: 45]



Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ ۚ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ۚ ذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّاكِرِينَ﴿١١٤﴾

Na simamisha Swalaah katika ncha mbili za mchana na sehemu ya kwanza ya usiku; hakika mema yanaondosha maovu. Hivyo ni ukumbusho kwa wanaokumbuka. [Huwd: 114]





Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amelinganisha Swalaah na mto ambao mtu akioga ndani yake mara tano kwa siku, basi hakika mtu huyo hatokuwa mchafu. Kwa hivyo kuswali kwetu, daima kunafuta madhambi madogo yaliyotendeka baina ya kila Swalaah.





عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((أَرَأَيْتُمْ لَوْ أَنَّ نَهْرًا بِبَابِ أَحَدِكُمْ يَغْتَسِلُ مِنْهُ كُلَّ يَوْمٍ خَمْسَ مَرَّاتٍ هَلْ يَبْقَى مِنْ دَرَنِهِ شَيْءٌ؟)) قَالُوا: لَا يَبْقَى مِنْ دَرَنِهِ شَيْءٌ. قَالَ: ((فَذَلِكَ مَثَلُ الصَّلَوَاتِ الْخَمْسِ يَمْحُو اللَّهُ بِهِنَّ الْخَطَايَا)) رواه البخاري ومسلم



Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mnaonaje ingelikuwa kuna mto mbele ya nyumba ya mmoja wenu kisha akawa anaoga humo kila siku mara tano, je atabakiwa na uchafu?)) Wakasema: “Habakiwi na uchafu”. Akasema: ((Hivyo ni mfano wa Swalaah ambazo Allaah hufuta madhambi kwayo)) [Al-Bukhaariy na Muslim]





Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ametufaradhishia Swalaah ili daraja zetu zipande, thawabu zetu zizidishwe, na madhambi yetu yafutike, na kwa ajili yake Atuingize Jannah na Atuokoe na Moto.





Walakini, Swalaah ni kama upanga wenye makali pande zote mbili. Tukiihifadhi, itatupa Nuru kwenye nyoyo zetu, makaburi yetu, na Siku ya Qiyaamah. Itatushuhudia wakati ambao tunahitaji shahidi ili tuokoke na adhabu ya Moto.

Faida hizo zinapatikana kutoka katika Hadiyth zifuatazo:





عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو بن العاص عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ ذَكَرَ الصَّلاةَ يَوْمًا فَقَالَ: ((مَنْ حَافَظَ عَلَيْهَا كَانَتْ لَهُ نُورًا وَبُرْهَانًا وَنَجَاةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ، وَمَنْ لَمْ يُحَافِظْ عَلَيْهَا، لَمْ يَكُنْ لَهُ نُورٌ وَلا بُرْهَانٌ وَلا نَجَاةٌ وَكَانَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مَعَ قَارُونَ وَفِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَأُبَيِّ بْنِ خَلَفٍ)) أخرجه الإمام أحمد في مسنده



Kutoka kwa 'Abdullaah bin 'Amru ibn Al-'Aaasw (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba siku moja Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitaja kuhusu Swalaah akasema: ((Atakayeihifadhi atakuwa na nuru na uongofu, na kufuzu siku ya Qiyaamah, na asiyeihifadhi hatokuwa na nuru wala uongofu wala kufuzu, na siku ya Qiyaamah atakuwa pamoja na Qaaruwn, Fir'awn, Haaman na Ubayy bin Khalaf)) [Musnad Ahmad ikiwa na isnaad Swahiyh]



Pia:



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ َقَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ ((إِنَّ أَوَّلَ مَا يُحَاسَبُ بِهِ الْعَبْدُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مِنْ عَمَلِهِ صَلاتُهُ فَإِنْ صَلُحَتْ فَقَدْ أَفْلَحَ وَأَنْجَحَ وَإِنْ فَسَدَتْ فَقَدْ خَابَ وَخَسِرَ فَإِنْ انْتَقَصَ مِنْ فَرِيضَتِهِ شَيْءٌ قَالَ الرَّبُّ عَزَّ وَجَلَّ انْظُرُوا هَلْ لِعَبْدِي مِنْ تَطَوُّعٍ فَيُكَمَّلَ بِهَا مَا انْتَقَصَ مِنْ الْفَرِيضَةِ ثُمَّ يَكُونُ سَائِرُ عَمَلِهِ عَلَى ذَلِكَ)) الترمذي و أبوا داود والنسائي وابن ماجه وأحمد



Imepokelewa na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli wa Allaah wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kitu cha kwanza kinachohesabiwa katika ‘amali za mja wa Allaah Siku ya Qiyaamah ni Swalaah zake. Zikiwa zimetimia, hapo tena atakuwa kaneemeka na kafuzu, na zikiwa zina kasoro atakuwa kaanguka na kala khasara. Ikiwa pana upungufu katika Swalaah zake za fardhi Allaah ‘Azza wa Jalla Atasema: “Tazama ikiwa mja wangu ana Swalaah zozote za Sunnah ambazo zinaweza kufidia zile zilizopungua, hapo tena ‘amali yake iliyobaki itaangaliwa hivyo hivyo)). [At-Tirmidhiy, Abu Daawuwd, An-Nasaaiy, Ibn Maajah na Ahmad]



Hivyo basi tukiipuuza Swalaah, itatoa ushahidi dhidi yetu, wakati ambao tunahitajia shahidi zaidi. Lazima tujihadhari tusiwe miongoni mwa watu waliopoteza Swalaah kisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akawaahidi adhabu ya Moto. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا الصَّلَاةَ وَاتَّبَعُوا الشَّهَوَاتِ ۖ فَسَوْفَ يَلْقَوْنَ غَيًّا ﴿٥٩﴾

Wakafuata baada yao waovu, walipoteza Swalaah na wakafuata matamanio; basi watakutana na adhabu motoni. [Maryam: 59]





Na tuzingatie maneno ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hadiyth:



عن جَابِر بن عبد الله عن النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهم عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قال: ((إِنَّ بَيْنَ الرَّجُلِ وَبَيْنَ الشِّرْكِ وَالْكُفْرِ تَرْكَ الصَّلَاةِ)) رواه مسلم

Kutoka kwa Jaabir bin 'Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Baina ya mtu na shirki, na kufru, ni kuacha Swalaah)) [Muslim]







Cheo cha Swalaah katika Dini ni kama mfano wa mlingoti wa nyumba, ukiwepo, nyumba itakuwa madhubuti na vifaa vyake vyote vitalingana mahali pake. Lakini isipokuweko, basi jengo lote litabomoka na kuwa halina maana.



Na hakika Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Hatuamrishi kuswali tu, bali Anatuamrisha tuimarishe Swalaah, jambo ambalo ‘Ulamaa wa Tafsiyr wamekubaliana kuwa kuimarisha Swalaah, ina uzito zaidi kuliko kuswali tu bila ya kuimarisha ipasavyo. Na kuimarisha Swalaah ina maanisha ni kutimiza shuruti zote za twahara, kuelekea Qiiblah, usafi wa mahali pa kuswali na vasi la kuswalia na mengineyo.





‘Ulamaa hawakuacha kuandika kuhusu Umuhimu wa Swalaah, hivyo vitabu vingi vimeandikwa juu yake.






Wa biLaahit-tawfiyq
 
Naam ndugu zangu katika imani, Nguzo za Ihsan zipo mbili tu

1. Kumuabudu Allah kama unamuona
2. Ingawa wewe humuoni lakini yeye anakuona

Kwahiyo pale unapofanya ibada zako basi fanya kana kwamba unamuona Allah mbele yako,yani fanya ibada zako vizur kabisa na kwa uhakika,nadhan wote tunafahamu ukiwa umesimamiwa na boss wako au kiongozi wako lazima hiyo kazi utaifanya kwa umakini sana

Sasa tambua basi Allah ndio anahitaji umfanyie ibada zake kwa umakini zaidi na kwa uangalifu mkubwa kwani hakika yeye anayajua hata yale ambayo ni siri katika nafsi yako na zaidi ya siri ambayo wewe hujui

Kwahiyo mathalani upo katika Swala umefungua swala yako kwa takbira tul ihram ile kusema Allahu Akbar hapo ndio umeingia katika Swala

Basi hapo mambo yote ya kidunia inabidi uyaweke pembeni kwani hapo upo ndani ya swala na unawasiliana na Mola wako

Yani hapo hudhurisha mawazo yote ndani ya swala,kuwa na hushui yani hudhurisha moyo wako ndani ya ibada ya swala,usiwaze tena mambo ya kidunia,na tambua Allah anakuona

Ndio maana Allah anasema katika qur'an " HAKIKA WAMEFUZU WALE AMBAO KATIKA SWALA ZAO NI WANYENYEKEVU"

Lakini ni msiba mkubwa sana ndani ya swala zetu tunauza na kununua,yani upo ndani ya swala lakini unawaza mambo ambayo yapo nje ya swala,na hii husababisha wengi wetu tunakosa athari ya Swala

Swala iliyoswaliwa vizur kabisa humkinga mja au mswaliji kutokana na maovu na machafu,yani utapata hisia na fikra ndani ya nafsi yako ya kutaka kuachana na machafu na maovu,kila ukikaa nafsi inakusuta juu ya kuacha mambo machafu hii ni kutokana na utukufu wa Swala

Na Allah anasema wamefanikiwa wale ambao huwa wanyenyekevu ndani ya swala,maana yake ni kwamba hawajafanikiwa wale ambao sio wanyenyekevu ndani ya swala zao

Ebu jikague je,huwa unajitahidi kuwa mnyenyekevu ndani ya swala? Au unaswali kimazoea tu huku unawaza mambo mengine ndani ya swala

Hapa ndio nguzo ya ihsan inaposimama mahala pake,hakika mwabudu Allah kama unamuona kwani hakika hata kama wewe humuoni basi tambua yeye anakuona

Ni hapo baadae inshallah

Tumche Allah
 
WATU KATIKA SAUM

الناس في الصيام

١- الصوم واجب على كل مسلم بالغ عاقل قادر مقيم.

1. Saum ni wajib kwa kila muislamu aliyebaleghe, mwenye akili, mwenye uwezo wa kufunga, mkaazi.

٢- الكافر لا يصوم، ولا يجب عليه قضاء الصوم إذا أسلم.

2.Kafiri hafungi (haiwajibu kwake na haisihi) na haiwajibu kwake kulipa saum akisilimu.

٣- الصغير الذي لم يبلغ لا يجب عليه الصوم، لكن يؤمر به ليعتاده.

3. Mtoto mdogo ambaye hajabaleghe haiwajibu kwake saum, lakini anaamrishwa kufunga ili azoee swaum.

٤- المجنون لا يجب عليه الصوم ولا الإطعام عنه وإن كان كبيراً، ومثله المعتوه الذي لا تمييز له، والكبير المهذري الذي لا تمييز له.

4. Mwendawazimu haiwajibu kwake kufunga wala kulisha maskini kwa niaba yake; hata kama ni mzee, na mfano wake punguani wa akili ambaye hatambui, na mzee anayeropoka ambaye hatambui.

٥- العاجز عن الصوم لسبب دائم كالكبير والمريض مرضاً لا يرجى برؤه، يطعم عن كل يوم مسكيناً.

5. Asiyeweza kufunga kwa sababu inayodumu kama mzee na mgonjwa aliye na ugonjwa usiotarajiwa kupoa, basi atalisha badili ya kila siku maskini.


٦- المريض مرضاً طارئاً ينتظر برؤه يفطر إن شق عليه الصوم، ويقضي بعد برئه.

6.Mgonjwa mwenye ugonjwa wa kuja/kuzuka anayengoja kupona atakula ikiwa nzito kwake saum, na atalipa baada ya kupona kwake.

٧- الحامل والمرضع إذا شق عليهما الصوم من أجل الحمل أو الرضاع، أو خافتا على ولديهما، تفطران وتقضيان الصوم إذا سهل عليهما وزال الخوف.

7.Mja mzito na anayenyonyesha ikiwa nzito kwao saum kwa ajili ya uja uzito au kunyonyesha, au wakaogopea watoto wao, watakula na watalipa saum itakapokuwa sahali kwao na hofu kuondoka.

٨- الحائض والنفساء لا تصومان حال الحيض والنفاس، وتقضيان ما فاتهما.

8.Mwanamke mwenye hedhi na nifaas hawatafunga watakapokuwa katika hali ya hedhi na nifaas, na watalipa siku zilizowapita.

٩- المضطر للفطر لإنقاذ معصوم من غرق أو حريق يفطر لينقذه ويقضي.

9.Atakayelazimika kula kwa ajili ya kumuokoa anayezama au anayechomeka, atakula ili amuokoe na atalipa.

١٠- المسافر إن شاء صام وإن شاء أفطر وقضى ما أفطره، سواء كان سفره طارئاً كسفر العمرة أم دائماً كأصحاب سيارات الأجرة (التكاسي والمرسيدس) فيفطرون إن شاءوا ما داموا في غير بلدهم.

10.Msafiri akitaka atafunga na akitaka atakula na atalipa siku alizokula, sawa safari yake iwe ya kuzuka au daima kama watu wa magari ya kukodi (taxi na mercedes) basi watakula wakitaka madamu hawako katika miji yao.


📚[Nubadh Fi Sswiyaam cha Al 'Allamah ibn utheimiin-Allah amrehem(uk2-3)]

════ ❁✿❁ ════

Salafi Da'wah East Africa (Salafi Da'wah Afrika Mashariki)

 
YANAYOMFUNGUZA ALIYEFUNGA



* لا يفطر الصائم إذا تناول شيئاً من المفطرات ناسياً أو جاهلاً أو مكرهاً، لقول الله تعالى: {رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِنْ نَسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا} [البقرة: ٢٨٦] .
وقوله: {إِلَّا مَنْ أُكْرِهَ وَقَلْبُهُ مُطْمَئِنٌّ} [النحل: ١٠٦] وقوله: {وَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ فِيمَا أَخْطَأْتُمْ بِهِ وَلَكِنْ مَا تَعَمَّدَتْ قُلُوبُكُمْ} [الأحزاب: ٥] .

▪Hafungui aliyefunga akifanya chochote kinachofunguza kwa kusahau au kwa kutojua au kwa kulazimishwa kwa nguvu; kwa kauli ya Allah Aliyetukuka [Tarjama] {Ewe Mola wetu usituadhibu tukisahau au tukikosea} [Al Baqarah:286]. Na kauli yake [Tarjama] {ila aliyelazimishwa kwa nguvu na moyo wake umetulia kwa imani} [An-Nahl:106]. Na kauli yake [Tarjama] { Na hamna juu yenu dhambi katika muliyokosea lakini katika yaliyokusudia nyoyo zenu} [Al Ahzaab:5].

* فإذا نسي الصائم فأكل أو شرب لم يفسد
صومه؛ لأنه ناس.

▪Basi akisahau aliyefunga, akala au akanywa, haiharibiki saum yake; kwa sababu amesahau.

* ولو أكل أو شرب يعتقد أن الشمس قد غربت أو أن الفجر لم يطلع لا يفسد صومه؛ لأنه جاهل.

▪Na lau atakula au kunywa akiitakidi kuwa jua limezama au kuwa alfajiri haijachomoza, haiharibiki saum yake; kwa sababu hakujua.

* ولو تمضمض فدخل الماء إلى حلقه بدون قصد، لم يفسد صومه؛ لأنه غير متعمد.

▪Na lau atasukutua, na maji yakaingia kooni mwake bila kukusudia, haiharibiki saum yake; kwa sababu hakukusudia.

* ولو احتلم في نومه، لم يفسد صومه؛ لأنه غير مختار.

▪Na lau ataota na kutokwa manii usingizini, saum yake haiharibiki; kwa sababu hana hiyari.


* المفطرات ثمانية وهي:

Yanayofunguza ni mambo manane, nayo ni:

أ- الجماع: وإذا وقع في نهار رمضان من صائم يجب عليه الصوم، فعليه مع القضاء كفارة مغلطة وهي عتق رقبة، فإن لم يجد فصيام شهرين متتابعين، فإن لم يستطع فإطعام ستين مسكيناً.

1.Tendo la ndoa: akilifanya anayelazimika kufunga katika mchana wa Ramadhani, basi atalazimika -pamoja na kuilipa hiyo siku-kafara kubwa; nayo ni kuacha mtumwa huru, asipopata, atafunga miezi miwili mfululizo, asipoweza, atalisha masikini sitini.

ب- إنزال المني يقظة باستمناء أو مباشرة أو تقبيل أو ضم أو نحو ذلك.

2.Kutoa manii ukiwa macho kwa punyeto (musterbation) au kugusa au kubusu au kukumbatia au mfano wake.

ج- الأكل أو الشرب سواء كان نافعاً أم ضاراً كالدخان.

3.Kula au kunywa sawa iwe na manufaa au madhara kama kuvuta sigara.

د- حقن الإبر المغذية التي يستغني بها عن الطعام؛ لأنها بمعنى الأكل والشرب. فأما الإبر التي لا تغذي فلا تفطر سواء استعملها في العضلات أم في الوريد، وسواء وجد طعمها في حلقه أم لم يجده.

4.Kudunga sindano lishe ambazo zinamtosheleza na chakula, kwa sababu ina maana ya kula na kunywa. Ama sindano ambazo si lishe hazifunguzi sawa azitumie katika misuli au katika mshipa, na sawa askie ladha yake kooni au asiskie.

هـ- حقن الدم مثل أن يحصل للصائم نزيف فيحقن به دم تعويضاً عما نزف منه.
وخروج دم الحيض والنفاس.

5.Kutia damu, kwa mfano; akitokwa damu aliyefunga, akatiwa damu kulipizia kilichomtoka.

6. Na kutokwa damu ya hedhi na nifaas.

ز- إخراج الدم بالحجامة ونحوها. فأما خروج الدم بنفسه كالرعاف أو خروجه بقلع سن أو نحوه فلا يفطر؛ لأنه ليس حجامة ولا بمعنى الحجامة.

7.Kutoa damu kwa Hijama na mfano wake. Ama damu kutoka yenyewe, kama kutokwa damu puani au kwa kutoa jino au mfano wake; hazifunguzi, kwa sababu si hijama wala haina maana ya hijama.

ح- القيء إن تقصده، فإن قاء بغير قصد لم يفطر.

8.Kutapika atakapokusudia, akitapika bila kukusudia hafungui.

📗[Nubadh fi swaiyam; cha Mwanachuoni ibn Utheymin -Allah amrehem]

════ ❁✿❁ ════

Salafi Da'wah East Africa (Salafi Da'wah Afrika Mashariki)

 
Screenshot_20250320_140204_Quran Swahili.jpg


Kama aya hapo juu inavyosema hakika qur'an ni mawaidha kwa wanadamu kutoka kwa Allah mtukufu

Je, kuna maneno bora zaidi ya maneno ya Allah? Hakika hakuna,basi tushikamane na kusoma maneno ya Allah ili tupate uongofu na rehma

Vile vile qur'an ni poza ya maradhi ya yaliyomo vifuani mwetu,ikiwa una hasadi,chuki,roho mbaya,kukata tamaa,basi we soma qur'an na uijue maana yake hakika ni dawa tosha kutoka kwa Allah azza wa jalla

Je ni yupi mkweli zaidi ya Allah?

Tumche Allah
 
Screenshot_20250320_141531_Quran Swahili.jpg


Nilipozungumzia kuhusu Malaika waandishi kuwa wanaandika kila kitu na hii ndio aya yenyewe,suratul Yunus

Wallah lau tukizingatia aya hii,basi huwezi kuandika upuuzi hapa jf kwakuwa unajua unarekodiwa,huwezi kukomenti upuuzi unarekodiwa na mwisho wa siku yanapimwa katika mizani

Ukizingatia aya hii unaacha maovu na machafu kwakuwa unarekodiwa,wallah tatizo huwa tunajisahau tu
 
Ewe mwanadamu tambua kwamba hakika Allah hawapi mali watu kwakuwa anawapenda laa!, ila humpa humpa rehma zake amtakaye hata kama ni mtu mbaya

Allah alimpa mali za kutosha firauni pamoja na ubaya wake,kama nabii Mussa anavyosema hapa chini

Screenshot_20250320_145317_Quran Swahili.jpg


Na hakika Mussa hakuishia hapo bali akaomba na dua ya Allah kumuondolea firauni mali pamoja na kufunga moyo wake ili asiamini mpaka pale adhabu chungu itakapo mfikia

Na Allah akapokea au kukubali dua ya Mussa,na kweli firauni hakuamini mpaka pale bahari ilipoanza kumfunika ndio akaanza kutoa shahada lkn alishachelewa

Screenshot_20250320_145848_Quran Swahili.jpg


Tambua Allah akimpenda mtu basi humpa imani au humzidishia imani

Tumche Allah
 
Back
Top Bottom