Ramadhan Special Thread
20250311_121917.jpg
 
Miongoni mwa mambo muhimu sana katika mwezi huu ni kuomba dua,hakika dua katika mwezi huu ni zenye kupokelewa ikiwa utaomba kwa imani na unyenyekevu mkubwa

Inasemwa hakika kipenzi cha umma Muhammad swala na salamu zimfikie alikuwa anaomba dua zake kwa unyenyekevu sana katika ramadhani

Tunapotaka msaada kwa binadamu wenzetu huwa tunaonyesha uhitaji mkubwa sana na kujieleza vizur ili wapate kushawishika kutusaidia

Je inakuwaje tunapomuomba Allah hatuonyeshi unyenyekevu mkubwa na uhitaji wa hali ya juu,yaani mtu hata kunyanyua mikono yake mbele ya Allah kuomba dua anaona uvivu,wenzetu inasemwa walikuwa wananyanyua mikono mpaka baadhi yao makwapa yanaonekana kwa kule kunyanyua mikono yao kwa kuonyesha uhitaji wao

Sisemi nawe ufanye hivyo laa,bali walau nyanyua viganja vyako vya mikono kuonyesha adabu ya kuomba dua,jidhalilishe kwa Allah na nyenyekea kwake kwani yeye ndio mfalme wa wafalme

Na kuomba dua kwa Allah ni lazima kwani inaonyesha jinsi ulivyo kiumbe dhaifu kwake na mhitaji kwani hakika yeye ndio mpaji

Hakika ni dhambi na kosa kubwa sana kwa mtu kutomuomba Allah kwani hiyo ni kibri au kiburi mbele ya Allah

Hakika Allah huchukia mno pale mja wake anapokuwa haombi dua,na anatoa ahadi ya adhabu kwa mtu ambaye anajivuna na ibada hii ya kuomuomba yeye

Kinyume na wanadamu ambao hukasirika pale wanapoombwa au kuliliwa shida mara kwa mara lkn kinyume chake Allah hupenda mno kuombwa na mja wake tena sana,na hii ni ibada kubwa sana

Mtu akiwa tajir anajitoshereza kwakuwa hela ya kula anayo,anaweza kujitibu na anapata chochote anachotaka basi hujiona hamuhitaji Allah kwa chochote,je ni wangapi wana hela na wamelala vitandani mwao,ni wangapi wana uwezo wa kula chochote lkn Allah amewapa mtihani wa maradhi na hawawezi kula chochote wanachotaka ingawa uwezo huo wanao

Hakika ibada ya kumuomba Allah ni ibada muhumu sana kwani vyote tulivyo navyo ni kwa neema yake yeye na si kwa ujanja wetu
 
Inasemwa kuna kipindi watu walimuuliza Muhammad je mola wako yupo mbali au karibu,ili tujue kama yupo mbali tuombe dua kwa sauti kubwa au kama yupo karibu basi tuombe kwa sauti ndogo

Wakati mtume Muhammad swala na salamu zimfie anatafakari swali hilo,hapo hapo Allah akamtuma Jibril alayh salaam kushusha aya hii

" Wakuulizapo waja wangu kuhusu mimi waambie nipo karibu yao,naitikia maombi yao wanaponiomba,basi waniamini,waniitikie na wawe na subira"

Kwahiyo hapo tumeona kwanza Allah amesema anasikia maombi yetu au dua zetu na anajibu,lkn akatupa masharti,kwanza tumuamini yani omba ukiwa unaamini utajibiwa na hakuna lenye kumshinda Allah,pili tumuitikie kwa maana nasi tufuate maamrisho yake anayotaka tuyafuate na sharti la tatu tuwe na subira

Cha kufurahisha zaidi ni kwamba aya hii imeshushwa au ipo sambamba na aya za swaumu,kwa mujibu wa wanazuoni ni kwamba,hii inaonyesha hakika kwamba dua hukubaliwa zaidi wakati wa swaumu au kufunga,na wakati huu ndio waja humuitikia sana Allah kwa maamrisho yake,hatusemi uongo,hatu zini,hatusengenyi na tunajiepusha na madhambi mengi sana,kwahiyo sharti la kumuitikia Allah tunalifanya

Na dua hujibiwa kwa namna tatu,kwanza Allah huenda akakujibu haraka na kupata utakacho,au akakuhifadhia hitaji lako na kukupa kipindi ambacho utakuwa na uhitaji mkubwa sana au badala ya kupata utakacho badala yake ukaepushwa na balaa kubwa sana ambalo lilikuwa likupate,utasikia mtu anasema dah nusura leo nigongwe na gari na huenda nisingekuwq hai,kumbe uliomba gari lkn Allah kwa hekima zake akajibu kwa kukuepusha na ajali mbaya

Na huenda Allah asikupe hapa duniani lkn akaja kukulipa huko akhera,kwahiyo hapo unaona kabisa Allah hapuuzi dua yako tatizo ni sisi hatujui hekima ya Allah pale tunapomuomba mambo yetu

Kikubwa tambua Allah yupo karibu yetu sana kuliko mshipa wa shingo yako,ebu jiulize mshipa upo shingoni mwako lkn yeye yupo karibu zaidi na wewe na huo mshipa upo mbali

Tumche Allah ukweli wa kumcha
 
.7:56 - Wala msifanye uharibifu katika nchi baada ya kuwa imekwisha tengenezwa. Na muombeni kwa kuogopa na kwa kutumai. Hakika rehema ya Mwenyzi Mungu iko karibu na wanao fanya mema.
 
7:157 - Ambao kwamba wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiye soma wala kuandika, wanaye mkuta kaandikwa kwao katika Taurati na Injili, anaye waamrisha mema na anawakanya maovu, na anawahalalishia vizuri, na ana waharimishia viovu, na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyo kuwa juu yao. Basi wale walio muamini yeye, na wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyo teremshwa pamoja naye - hao ndio wenye kufanikiwa.
 
7:158 - Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote, niliye tumwa na Mwenyezi Mungu Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Hapana mungu ila Yeye anaye huisha na anaye fisha. Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake asiyejua kusoma na kuandika, ambaye anamuamini Mwenyezi Mungu na maneno yake. Na mfuateni yeye ili mpate kuongoka.
 
Ndugu zangu waislamu naomba tuulizane hapa,hivi kuna Allah wa ramadhani na Allah wa nje ya Ramadhani?

Kama wapo tofauti ni sahihi sana kufuata maamrisho na makatazo ya huyu wa ramadhani ambaye tuna muheshimu sana

Ila kama Allah ni mmoja sasa inakuwaje hofu yetu na utii wetu ni kipindi cha ramadhani tu?

Je siku nyingine Allah hulala na kujisahau kutufuatilia ndio maana huwa hatumuogopi?

Ndugu zangu maisha ya dunia mwenye dunia yake anasema "maisha ya dunia ni starehe ya mda mfupi sana lkn maisha ya akhera ni yenye kuendelea na ya milele"

Inakuwaje haya maisha ya miaka 60 mpaka 7o tena hapa kwa walio jaaliwa maana si wote ni wenye kufika huko,tunayaona bora kuliko maisha ya milele,ambayo ni starehe kwa watendao mema na mateso kwa watendao maovu na wasio fuata amri ya Allah

Haya maisha ya hapa duniani mfano wake ni kama msafiri ambaye anasafiri kwenda sehemu fulani,akiwa njiani anakuta mti wenye kivuli na anaamua kumpumzika hapo kidogo kisha huyo huendelea na safar yake

Hapa duniani ni kama tupo kivulini tu kwa mda mchache kisha hao tunaelekea kwa Allah,je iweje kivuli cha mda mfupi tu kitusahau lishe safari yetu?

Huu uzima wetu na kuwa kwetu hai tusione tuna miaka mingi sana ya kuishi,hakika kifo ni fumbo kubwa sana,kwani hatujui siku wala saa,juzi tu ijumaa kabla ya swala ya ijumaa tulimswalia jirani yetu na kumkimbiza haraka makaburini kumzika ili tuwahi kuswali swala ya ijumaa

Tukiwa makaburini nikawa natafakari hapa huyu marehemu kitacho msaidia ni amali zake njema/vitendo vyake vyema,sijui alijiandaaje katika uhai wake?

Wakati tunaondoka nikawaza hapa sasa anatusikia tukiondoka na kumwacha peke yake na wakati huo malaika wawili mda si mrefu watamtembelea na kumuhoji maswala mbali mbali,je ana yapi ya kuwaeleza? Maana majibu yake yatategemeana na jinsi gani aliishi hapa duniani

Nilikuwa mnyonge sana,nikasema ipo siku moja watu watasema katika kaburi langu "leta dongo,lete majani na kuanza kufukia kaburi langu na hao wataondoka zao nibaki na malaika wawili,je nitasema nini ikiwa maisha yangu hayakuwa ya ucha mungu?

Allah atunusuru

Tumche Allah ukweli wa kumcha
 
7:170 - Na wale wanao kishikilia Kitabu, na wakashika Sala - hakika Sisi hatupotezi ujira wa watendao mema.

Ndugu zangu katika imani,huu ni mwezi ambao qur'an iliteremshwa na ndio maana tunahimizwa sana kukithirisha kusoma kitabu cha Allah

Aya hapo juu inasema na wale wanao kishikilia kitabu kwa maana wanakisoma na kuzingatia mafundisho yake na kuyafanyia kazi maneno yake,hao ndio wenye kushika kitabu cha Allah

Na sio kusoma tu kwa sauti nzur na kufuata hukumu zake lkn pasina kujua maana ya aya hizo na kuzitafakari,lengo kubwa ni kupata mawaidha ya Allah ndani ya qur'an, na ndio maana tunaambiwa wale wanamuogopa Allah wanaposomewa aya zake huwaongezea imani,sasa imani itaongezeka kwa kujua ujumbe wa qur'an na kuutafakari

Siku hizi kuna misahafu yenye tafsiri na app za qur'an zenye tafsiri yake kabisa,kwahiyo hakuna namna mtu akasema asijue ujumbe wa Allah unasemaje

Basi tukisome kitabu cha Allah na kuzingatia mafundisho yake na kuyafanyia kazi na hapo ndio tutakuwa na ile sifa ya kukishikilia kitabu cha Allah

Mwezi huu Malaika Jibril alikuwa anamjia Mtume rehma na amani ziwe juu yake kumsomesha qur'an mwezi mzima,inaonyesha ni kiasi gani huu ni.mwezi wa kukithirisha sana kusoma qur'an

Hakika sala umuhimu wake unafahamika ndio sehemu pekee ambayo mja anaongea na Mola wake

Allah ametoa ahadi kwa mujibu wa maneno ya Mtume,kwamba wale wenye kuswali Allah atawasamehe siku ya kiyama ila hakutoa ahadi kwa wasio swali,je wewe hujaona tu bado imuhimu wa swala?

Na swala ndio amali ya kwanza kuhesabiwa siku ya kiama,na kama swala ya mtu iko safi basi matendo yake mengine yapo safi na kinyume chake hivyo hivyo

Swali kabla hujaswaliwa

Tumche Allah ukweli wa kumcha
 
Ndugu zangu waislamu naomba tuulizane hapa,hivi kuna Allah wa ramadhani na Allah wa nje ya Ramadhani?

Kama wapo tofauti ni sahihi sana kufuata maamrisho na makatazo ya huyu wa ramadhani ambaye tuna muheshimu sana

Ila kama Allah ni mmoja sasa inakuwaje hofu yetu na utii wetu ni kipindi cha ramadhani tu?

Je siku nyingine Allah hulala na kujisahau kutufuatilia ndio maana huwa hatumuogopi?

Ndugu zangu maisha ya dunia mwenye dunia yake anasema "maisha ya dunia ni starehe ya mda mfupi sana lkn maisha ya akhera ni yenye kuendelea na ya milele"

Inakuwaje haya maisha ya miaka 60 mpaka 7o tena hapa kwa walio jaaliwa maana si wote ni wenye kufika huko,tunayaona bora kuliko maisha ya milele,ambayo ni starehe kwa watendao mema na mateso kwa watendao maovu na wasio fuata amri ya Allah

Haya maisha ya hapa duniani mfano wake ni kama msafiri ambaye anasafiri kwenda sehemu fulani,akiwa njiani anakuta mti wenye kivuli na anaamua kumpumzika hapo kidogo kisha huyo huendelea na safar yake

Hapa duniani ni kama tupo kivulini tu kwa mda mchache kisha hao tunaelekea kwa Allah,je iweje kivuli cha mda mfupi tu kitusahau lishe safari yetu?

Huu uzima wetu na kuwa kwetu hai tusione tuna miaka mingi sana ya kuishi,hakika kifo ni fumbo kubwa sana,kwani hatujui siku wala saa,juzi tu ijumaa kabla ya swala ya ijumaa tulimswalia jirani yetu na kumkimbiza haraka makaburini kumzika ili tuwahi kuswali swala ya ijumaa

Tukiwa makaburini nikawa natafakari hapa huyu marehemu kitacho msaidia ni amali zake njema/vitendo vyake vyema,sijui alijiandaaje katika uhai wake?

Wakati tunaondoka nikawaza hapa sasa anatusikia tukiondoka na kumwacha peke yake na wakati huo malaika wawili mda si mrefu watamtembelea na kumuhoji maswala mbali mbali,je ana yapi ya kuwaeleza? Maana majibu yake yatategemeana na jinsi gani aliishi hapa duniani

Nilikuwa mnyonge sana,nikasema ipo siku moja watu watasema katika kaburi langu "leta dongo,lete majani na kuanza kufukia kaburi langu na hao wataondoka zao nibaki na malaika wawili,je nitasema nini ikiwa maisha yangu hayakuwa ya ucha mungu?

Allah atunusuru

Tumche Allah ukweli wa kumcha
Subhanallah natamani kila mmoja apitie ukumbusho wako, natamani kila mmoja ajue Mola wa shaaban ndie wa ramadhan na miezi yote iliyobakia, natamani kila mmoja yachukue haya maneno yako hasa sehemu hii ambayo watu tunasahau kuwa tupo kwenye mti wa kivuli na safari bado ni ndefu,
Ya Allah tujalie tuwe wenye kusikia nasaha na kuyafanyia kazi
Ya Rabb tufanyie wepesi ktk safari hii tunayoiendea na tujalie hata katk makaburi yetu nuru , tunaomba na siku ya qiyama utujalie tuwe ktk wale watakaopita bila ya hesaba kwani kwa hakika wewe ni hakimu
 
Amiin amiin amiin ukhty,wallah kwa jinsi ambavyo nakuona imani yako waeza sema utadhani ulizaliwa ndani ya uislamu,kumbe ulikuwa upande wa pili na Allah akakuongoza katika nuru yake

Allah azidi kukuzidishia imani pamoja na kizazi chako pia

Nakupenda kwa ajili ya Allah
 
Amesema Mtume swallallahu alaih wasallam,imani ya mtu huwa inashika kutu kama vile chuma kinavyopata au kushika kutu

Kwahiyo namna pekee ya kulainisha kutu hiyo na kuitoa moyoni mwako ni kwakusoma qur'an uelewe aya zake na kufanya dhikri kwa wingi kwa kumtaja sana Allah

Na kutu hiyo husababishwa na maasi ambayo tunayafanya,kadri unavyo bobea kwenye maasi basi imani yako inashuka,lkn utakavyo anza kufanya mambo mema,kufanya ibada,kusikiliza darsa,kusoma qur'an basi kutu katika moyo wako hutoweka na hatimaye unakuwa na imani ya kiwango kikubwa sana

Tumche Allah ukweli wa kumcha
 
Back
Top Bottom