Rais Samia Suluhu Hassan ampendekeza Dkt. Philip Isdor Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Bunge lamthibitisha kwa 100%

Kwahiyo hana mamlaka ya kuuliza chochote siyo

Haujanielewa. Waziri ni bosi wa Katibu Mkuu na ana haki ya kuhoji chochote kinachofanyika ndani ya wizara yake na kutoa maelekezo kwa katibu Mkuu. Pamoja na hayo katika shughuli za kiutendaji za Wizara mwenye mamlaka ni Katibu Mkuu. Katibu Mkuu ndie anayewajibika kuhakikisha kuwa taratibu na sheria za uendeshaji wa serikali zina fuatwa. Kwa sababu hiyo, ndio maana barua zote wizarani zinaandikwa kwa Katibu Mkuu na sio kwa Waziri. Malipo yote yanaidhinishwa na katibu Mkuu na sio Waziri. Mikataba yote inaingiwa na Katibu Mkuu na sio Waziri. Bajeti zote zinatayarishwa na Katibu Mkuu ila zina wasilishwa na Waziri Bungeni. Waziri ni msimamizi wa sera wakati Katibu Mkuu anasimamia utendaji. Hawa wanatakiwa wafanye kazi pamoja vizuri kwa kuheshimu mipaka ya kazi zao. Bahati mbaya, mawaziri wengi wanapenda sana kuingilia kwenye kazi za utendaji na hivyo kupunguza ushirikiano kati yao. Utakuta waziri anaagiza mkataba usimamishwe wakati yeye sio sehemu ya mkataba. na mara nyingi hajui athari ya kusimamisha mkataba kiholela. Alitakiwa kumuagiza Katibu Mkuu asitishe, na Katibu Mkuu akiona agizo hilo halina tija anaweza kukataa kulitekeleza na kulipeleka kwa Katibu Mkuu Kiongozi ili alitolee ufafanuzi.

Amandla...
 
Kwani Kakoko aliteuliwa na nani? Utendaji bora ufanywe na Mpango! Halafu wewe unataka nimsifie Magufuli?

Yale yale ya barabara zinajengwa kwa kodi zetu, ila sifa zinaenda kwa magufuli!
Kabla ya Hapo Mpango alikua wapi ?

Alimteua mpango kua mbunge ni nani ?

Aliempa uwaziri mpango ni nani ?

Mpango alikua anafanya kazi chini ya Nani ?

Majibu unayo mwenyewe
Haya Magufuli jembe sio jembe

Na Vice versa kwa kakoko
 
Hahahha.. Tutaomba radhi kwa bavicha wakiwa ikulu
Safari hii mtadhalilika na mtaishia kunywa kimpumu tu kudadadeeki maana hamna pa kuuzia fitina zenu.

Tuwacheni tuijenge nchi yetu sasa na nyinyi wakimbizi rudidni kwenu.
 
Mbali na upusillanimous alioonyesha wakati anaumwa Korona kwa kukubali wamparade kwenye vyombo vya habari bila hata barakoa sioni shida nyingine kwake.
 
Safari hii mtadhalilika na mtaishia kunywa kimpumu tu kudadadeeki maana hamna pa kuuzia fitina zenu.

Tuwacheni tuijenge nchi yetu sasa na nyinyi wakimbizi rudidni kwenu.
Tutakunywa kimpumu huku nyie mkiwa ikulumnakunywa wine.. Hahahhahah
 
Back
Top Bottom