Rais Samia Suluhu Hassan ampendekeza Dkt. Philip Isdor Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Bunge lamthibitisha kwa 100%

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
752
3,092
Jina hilo limepelekwa Bungeni na Mpambe wa Rais (ADC) Kanali Nyamburi Mashauri, na kukabidhiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai.

Spika Ndugai akisoma ujumbe wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema..

Mheshimiwa Spika, nawasilisha Bungeni Jina la Mheshimiwa Philip Isdori Mpango kwa Nafasi ya Makamu wa Rais Tanzania.

Soma >>Wasifu wa Dkt. Philip Isdor Mpango


Bunge lamthibitisha kwa kishindo
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitisha Dkt. Philip Isdor Mpango kwa asilimia 100 kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kura zote 363 za wabunge waliopiga kura.







Dk Philip Mpango alizaliwa July 14, 1957 alikuwa ni Waziri wa Fedha na Mipango katika Serikali ya Awamu ya Tano.

Mpango ni mzaliwa wa Kigoma, baba yake ni marehemu Isidori Nzabhayanga Mpango, ambaye alizaliwa Kijiji cha Kasumo, Wilaya ya Kasulu. Dk Mpango alizaliwa hapohapo Kasumo na ni kaka mdogo wa Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanganyika Magharibi – Kasulu mkoani Kigoma, Dk Gerard Mpango.

Dk Mpango ni mchumi mwenye shahada ya uzamivu ya uchumi.

Kuanzia miaka ya 1990 hadi 2000, alifanya kazi akiwa mhadhiri mwandamizi wa uchumi katika kitivo cha Biashara (sasa Shule ya Biashara) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Alikuwa akifundisha “Microeconomics”,

“Macroeconomics” (kwa mwaka wa pili) na “Public Finance” kwa mwaka wa tatu na kozi za uzamili.

Amewahi kuwa Mchumi Mwandamizi wa Benki ya Dunia, Mkuu wa Kamati ya kumshauri Rais Jakaya Kikwete wakati huo kuhusu masuala ya uchumi, Katibu binafsi wa Rais anayeshughulikia masuala ya uchumi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, kabla ya kuhamishiwa Tume ya Mipango, Ofisi ya Rais. Nyadhifa hizi zote amezishika wakati wa utawala wa Kikwete.

Hayati Magufuli alipoingia madarakani alimteua kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na baada ya siku chache akateuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.

Dk Mpango ni kiongozi mwenye msimamo thabiti. Baadhi ya watendaji ambao wamewahi kufanya kazi chini yake kwenye ofisi ya Rais wanamuelezea kama mtu anayetaka waliomzunguka wazungumze kwa takwimu na ushahidi hasa katika masuala ya uchumi. Msimamo huo pia aliuonyesha alipokuwa mtaalamu wa Benki ya Dunia. Hakuwa mwoga kuieleza ukweli Serikali pale ambako ilikuwa haifanyi vizuri.

Mathalan, wakati wasomi wengi wa uchumi wakiwa wanapiga kelele za kuisifia Serikali juu ya ukuaji wa uchumi miaka ya mwanzoni ya 2000, Dk Mpango alieleza wazi kuwa lengo hilo la kukuza uchumi kwa asilimia 5.9 haliwezi kufikiwa kwa sababu katika miaka minne iliyopita, Serikali ilishindwa kulifikia.

Alisema: “Angalia kwa miaka minne hadi mitano iliyopita ambayo tulikuwa na sera nzuri za kibajeti, hakuna mwaka ambao ukuaji huo ulifikiwa, hizo ni dalili tosha kwamba hali hiyohiyo ndiyo itajitokeza mwaka huu.”

Born – July 14, 1957, Kasumo, Kigoma region

Education
*1993-1996 University of Dar, PHD Economics
*1990-1992 Lund University, PHD Course Work, Sweden
*1986-1988 University of Dar, Master in Economics
*1981-1984 University of Dar, BA Economics
*1976-1977 Ihungo High (A) Bukoba
*1974-1975 Itaga Seminary (O) Tabora
*1971-1973 Ujiji Seminary (O) Kigoma
*1968-1970 Munyama Primary Kigoma
× 1965-1967 Kasumo Primary Kigoma
*1964-1965 Kipalapala Primary Tabora

Mpango’s Career
*1980-1980 Public relations assistant, National Provident Fund
*1980-1981 Research assistant, Elimu Supplies Ltd
*1984-1988 Economist, Ministry of Labor
*1988-2002 Economics Lecturer Dar-es-Salaam University
*2002-2006 Senior Economist World Bank
*2007-2009 Economic advisor to the President, President’s Office
*2009-2010 Deputy Permanent Secretary, Ministry of Finance
*2010-2015 Executive secretary, President’s Office Planning Commission
*2015-2015 Acting Commissioner General, Tanzania revenue Authority
*2015 – Appointed Member of Parliament
*2015 – Minister of Finance and Planning
 
Job Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania amesoma jina la Phillip Isidori Mpango kuwa ndiye aliyependekezwa na Rais Samia Suluhu kushika wadhifa wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nyaraka za jina hilo imewasilishwa na Mpambe wa Rais(ADC) na kuikabidhi kwa Spika Ndugai.
 
Spika amesoma jina la Mpango kuwa ndio amependekezwa kuwa makamu wa Rais, Waziri mkuu ana toa hoja sasa ya kudhibitisha mapendekezo ya kuteuliwa kwa Mpango
 
Imepenya hiyooooooo

Hongera sana Philip Mpango kwa uteuzi

Tuna imani kubwa kwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan, Mungu akutunze sana Madame

Rest well our hero President John Pombe Joseph Magufuli, ujue tuu ulituachia viongozi makini sana

Ila aliyetungaga haka kawimbo sijui aliwazaga nini

Chama imara, serikali imara...... ngoja nikajiunge rasmi sasa nipate usajili wa chama kwa mara ya kwanza
 
Back
Top Bottom