Makamu wa Rais Dkt. Mpango: Mwigulu na Kitila "Chukueni maoni ya Wafanyabiashara"

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
54.jpg
Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewaagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo (Mb), na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), kuchukua maoni ya Wafanyabiashara na wawekezaji ili kuboresha sera na sheria za kodi.

Makamu wa Rais, ametoa agizo hilo leo Februari 27, 2024 alipozindua Jukwaa la Kodi na Uwekezaji Jijini Dar es Salaam, ambapo amesema hatua hiyo itasaidia kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.

42.jpg

55.jpg
“Kusanyeni na mtumie maoni ya wadau ili kuathiri upya mifumo ya kodi iendane na mabadiliko makubwa ya uchumi wa nchi,” amesema Dkt. Mpango.

Kabla ya kufungua Kongamano hilo, Dkt. Mpango alitembelea mabanda ya washiriki wa mkutano huo akafurahishwa na utekelezaji wa maboresho ya mazingira ya uwekezaji na biashara nchini na hivyo kuipongeza Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji inayoratibu na kuhamasisha uwekezaji nchini.

Katika salamu zake kwa washiriki wa Kongamano hilo, Prof. Kitila Mkumbo (Mb.), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, amesema Tanzania imekidhi vigezo vyote vya nchi inayovutia wawekezaji.

58.jpg

66.jpg

70.jpg
“ Uzoefu wa miaka 27 ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), unaonesha nchi inayovutia uwekezaji lazima ikidhi vigezo kumi, ambavyo ni amani na utulivu, mazingira ya kisera na urekebu….” amesema Prof. Mkumbo.

Vigezo vingine alivyovianisha ni; Uwepo wa soko kwa bidhaa watakazozalisha wawekezaji, utulivu wa kiuchumi na utulivu wa fedha kwa ujumla, uwepo wa vipaji na nguvu kazi, ubora wa miundombinu, viwango vya chini vya kodi, gharama ndogo za kuajiri wafanyakazi, Uwepo wa ardhi, na uwepo wa fedha za kugharamia miradi ya uwekezaji wa ndani.

Jukwaa la Kodi na Uwekezaji ni fursa ya wafanyabiarasha na wawekezaji kutoa maoni na kushiriki mjadala unaolenga kuibua changamoto mbalimbali za kisera, kisheria ili kusaidia maboresho ya uwekezaji na biashara nchini.
 
Back
Top Bottom