Makamu wa Rais DKT. Philip Mpango ahutubia Mkutano wa Idadi ya Watu nchini Hungary

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
e51c70c1-4a7a-41ab-9947-c9fd1bb3eb11.jpeg

5e89bdcc-58d0-4ef1-a3d6-f8f1c847bdac.jpeg

e56173d2-c47e-4133-b18e-9c5840223809.jpeg

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia katika Mkutano wa Tano wa Idadi ya Watu (5th Budapest Demographic Summit) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Museum of Fine Arts Jijini Budapest nchini Hungary. (Tarehe 14 Septemba 2023).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa mataifa kutambua umuhimu kuweka mkazo katika taasisi ya familia ya kiutamaduni ili kuifanya kuwa kiini cha maendeleo ulimwenguni.
fc1b8dab-7037-44c7-a07b-66ae23871ed4.jpeg

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Museum of fine arts Jijini Budapest nchini Hungary kushiriki Mkutano wa Tano wa Idadi ya Watu (5th Budapest Demographic Summit) unaofanyika leo tarehe 14 Septemba 2023.
80872a69-d20f-4c9a-a0ec-ff86d04e0de8.jpeg

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na kuzungumza na Rais wa Hungary Mhe. Katalin Novàk wakati alipowasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Museum of fine arts Jijini Budapest nchini Hungary kushiriki Mkutano wa Tano wa Idadi ya Watu (5th Budapest Demographic Summit) unaofanyika leo tarehe 14 Septemba 2023.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akihutubia kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Tano wa Idadi ya Watu (5th Budapest Demographic Summit) unaofanyika Jijini Budapest nchini Hungary. Amesema inahitajika nguvu ya pamoja kimataifa katika kuimarisha ustawi wa familia ikiwemo kuzingatia kanuni na desturi za kiutamaduni pamoja na kuunga mkono mafundisho ya dini ambayo yanakuza maadili ya familia na kulinda usalama na mwendelezo wa familia.

Pia Makamu wa Rais ametoa wito kwa serikali ulimwenguni kutengeneza na kutekeleza sera, programu na sheria zitakazohakikisha usalama na uendelevu wa familia. Aidha ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kushirikiana na Bara la Afrika katika kukabiliana na changamoto zinazotokana na ongezeko la idadi ya watu zikiwemo uhitaji wa huduma za afya na elimu, ukosefu wa ajira, upungufu wa chakula na uhamiaji haramu.

Akitoa mfano wa Tanzania katika mkutano huo wenye kauli mbiu ya “Familia Msingi wa Usalama” Makamu wa Rais amesema nchini Tanzania familia inatambuliwa kama msingi imara na muhimu ambayo ni mwanzo wa ujenzi wa mtandao wa mahusiano ya jamii nzima. Ameongeza kwamba Tanzania familia inahusisha muunganiko wa ndoa ya watu wa jinsia mbili tofauti,watoto wao pamoja na ndugu au wategemezi wao ambapo pamoja na mambo mengine, familia hutumika kuimarisha utaratibu na utulivu katika jamii na pia husaidia katika uwezo wa kufanya maamuzi na utatuzi wa matatizo pamoja na utulivu wa kifedha, utoaji wa elimu na huduma za afya kwa wanafamilia na malezi.

Makamu wa Rais amesema pamoja na kuendelea kusisitiza na kuimarisha ustawi wa familia, serikali ya Tanzania imeendelea kuwekeza katika kujenga uchumi na kuboresha miundombinu ya kijamii kwa maendeleo ya watu ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya maji, umeme, elimu pamoja na utoaji wa elimu bila malipo kuanzia ngazi ya awali hadi sekondari. Ameongeza kwamba serikali imeongeza jitihada katika kuwavutia vijana ambao ni idadi kubwa iliopo nchini kushiriki katika kilimo biashara kwa kuanzisha programu maalum ya Jenga Kesho iliyobora (BBT).

Halikadhalika Makamu wa Rais amesema sababu za kiuchumi na migogoro zinazopelekea ongezeko la wahamiaji ndizo zinazopelekea athari ya mienendo ya idadi ya watu Barani Afrika. Amesema Tanzania imekuwa ikihifadhi wakimbizi zaidi ya laki nne kutoka mataifa Jirani ambao wamekua wakitafuta amani na ustawi wa Maisha yao. Makamu wa Rais ametoa wito kwa kwa nchi na mataifa kuiunga mkono Tanzania katika kuwahudumia wakimbizi ambapo uwepo wao huongeza mahitaji kama vile ya ardhi, maji, huduma za kijamii na miundombinu. Pia ametoa wito wa kuboresha usalama wa kitaifa na kikanda, kuzuia migogoro, kuimarisha na kulinda amani pamoja na kuongeza juhudi katika kuzuia na kupambana na ugaidi.

Vilevile Makamu wa Rais amesema Tanzania inathamini ushirikiano na Jamhuri ya Hungary katika nyanja ya Elimu na kuinua ujuzi. Amesema serikali imedhamiria kuimarisha uhusiano na nchi ya Hungary katika ukuzaji wa ujuzi kwa vijana, uwekezaji hususani katika kilimo na biashara ya kilimo, uongezaji wa thamani, utengenezaji wa bidhaa, utalii na teknolojia.

Mkutano huo wa siku mbili unahudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali, Watunga Sera, Viongozi wa Taasisi na Mashirika ya Kimataifa, Viongozi wa Dini na Wanataaluma.
 
Huyu sasa ndo Makamu wa Rais hata likitokea kama la 17/3 poa tu. Mabeyo ali feli pakubwa sana. Matokeo yake ndo haya Sasa anataka na Hafidh Ameir alipwe mafao
 
Mkutano wa Tano wa Idadi ya Watu (5th Budapest Demographic Summit) unaofanyika Jijini Budapest

14 September 2023
Budapest, Hungary

Demográfiai csúcs 2023 - Philip Isdor Mpango tanzániai alelnök beszéde - HÍR TV

View: https://m.youtube.com/watch?v=kDTzHoZTXp4
Philip Isdor Mpango, the Vice President of the United Republic of Tanzania, among other things, drew attention to the fact that the demographic situation in the world today revolves around two pivot points. On one side of this there are aging societies, while on the other side there is an enormous population growth rate, with relatively strong family ties. As a result of this demographic disparity, both sides of the world face enormous challenges and opportunities..

According to his report, the family in Tanzania is made up of a man and a woman, the family is responsible for basic social security and provides for its members. However, as he added, the lives of families are also made difficult by serious challenges, such as poverty, violence against women and children, unemployment, difficulties in accessing basic services, and weather that has become more extreme due to climate change.

The Tanzanian government is trying to help the most vulnerable households, but numerous infrastructure investments and a free education package available for both girls and boys will also improve their quality of life, said the vice-president, who also thanked Hungary for its support in the field of education.

Philip Isdor Mpango emphasized that Tanzania is not one of the big migration emitters, on the contrary: it has accepted more than 400,000 refugees from neighboring countries.

We believe that the problems must be tackled at their roots: unemployment and emigration in Africa can be remedied by providing economic assistance and improving the efficiency of governance, said Philip Isdor Mpango, calling for international cooperation in order for Africa to deal with its demographic problems

Source: Philip Isdor Mpango: Egyszerre van öregedő társadalom és óriási népességnövekedés
 
16 September 2023
Budapest, Hungary

Makamu wa Rais awapa kongole Watanzania Hungary

1694968046777.png

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameipongeza Jumuiya ya Watanzania waishio nchini Hungary pamoja na Ubalozi wa Tanzania unaowakilisha nchini humo kwa msaada waliotoa wakati wa kuwaondoa watanzania waliokuwa wakiishi na kusoma nchini Ukraine mara baada ya kuanza kwa vita.

Makamu wa Rais ametoa pongezi hizo wakati alipokutana na kuzungumza na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi na wale wanaopata elimu ya ngazi mbalimbali nchini Hungary, mazungumzo yaliofanyika Jijini Budapest nchini Hungary. Amewataka kuendelea kushikamana na kushirikiana wakati wote na kuwa na moyo wa huruma na upendo kama baadhi yao walivyojitolea hali na mali kusaidia watanzania waliokuwa wakiondoka eneo la vita.

Makamu wa Rais amewasihi watanzania waishio nchini Hungary kuhakikisha wanaishi kwa kufuata sheria katika nchi hizo na kujiepusha na vitendo vya kihalifu vitakavyoharibu taswira ya Tanzania. Aidha amewaasa kuendelea kuitangaza vema Tanzania, kuvutia wawekezaji pamoja na wao kuchangamkia fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali nchini. Pia amewasihi kuendelea kusaidia kwa karibu ndugu na jamaa wenye uhitaji katika familia zao nchini Tanzania kwa kutumia mifumo rasmi ya utumaji fedha.

Halikadhalika Makamu wa Rais amesema kutokana na lugha ya Kiswahili kuanza kutumika katika Jumuiya mbalimbali kama lugha rasmi, Diaspora wanapaswa kuendeleza lugha hiyo kwa kuitangaza na kuanzisha vituo vya kujifunzia lugha ya Kiswahili katika maeneo waliopo. Aidha amewataka watanzania waishio nje ya Tanzania kutambua jukumu la kwanza la ujenzi wa Tanzania litafanywa na watanzania wenyewe hivyo wanapaswa kutoa mchango wa kila hali katika kuliletea taifa maendeleo.

Amewasisitiza wanafunzi kutumia fursa waliopata vema kwa kuvuna maarifa na kutengeneza mahusiano mazuri na mataifa mengine ili kuweza kuijenga Tanzania.

Makamu wa Rais amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuleta mabadiliko yenye tija kwa watanzania wote na kueleza kwamba serikali imefanya jitihada katika kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo afya, sekta ya elimu, kuimarisha sekta ya nishati, ujenzi wa mindombinu kama vile barabara, reli viwanja vya ndege na barabara. Pia amesema serikali inaendelea na jitihada za kuimarisha demokrasia, sekta ya madini, maji na sekta ya kilimo kwa kuanzisha programu za kuvutia vijana katika kilimo cha biashara.

Pia Makamu wa Rais amesema Serikali kwa kutambua ongezeko la watu nchini imedhamiria kuwekeza katika kuimarisha rasilimali watu ili iweze kutumika vema katika kuleta maendeleo. Makamu wa Rais amesema kwa kuzingatia hali hiyo huduma za afya na elimu zimeboreshwa kwa kuongeza vifaa tiba na miundombinu ya afya, kutoa fursa kwa madkatari kupata elimu zaidi pamoja na ujenzi wa vyuo vya ufundi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Mbarouk amesema pamoja na kazi ya kukuza na kudumisha mahusiano ya kirafiki na kidiplomasia kati ya Tanzania na mataifa mengine pia serikali imeendelea kutekeleza kikamilifu kazi ya uratibu wa masuala ya diaspora. Amesema kuanzishwa kwa mfumo wa kuwasajili diaspora kidijitali (Diaspora Digital Hub) umesaidia katika kurahisisha kutambua takwimu za watanzania waishio nje ya Tanzania.

Balozi Mbarouk amesema takwimu zitakazopatikiana katika mfumo huo zitawezesha serikali kupanga na kuandaa kwa usahihi mahitaji yanayohitajika ili kuwapa diaspora huduma wanazohitaji kama vile huduma za kibenki, hati za kusafiria, vitambulisho vya taifa na vitambulisho rasmi vya utambuzi wa diaspora wakati wa utekelezaji wa hadhi maalum.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi Watanzania wanaopata Elimu nchini Hungary Michael Matonya ameishukuru serikali kwa ufadhili wa wanafunzi wanaosoma nchini humo na kuomba kuongezwa kwa idadi ya wanafunzi wanaosoma nchini humo hasa katika fani za kimkakati za sayansi na teknolojia.

Pia ametoa wito kwa serikali kuwekeza zaidi katika kushirikiana na nchi ya Hungary katika sekta ambazo nchi hiyo imepiga hatua kama vile na utaalamu katika sayansi ya kompyuta, tehama, uhandisi, urubani, afya, elimu ya mimea na wanyama.
Source: tovuti : vpo.go.tz
 
Back
Top Bottom