Makamu wa Rais, Dkt. Mpango kumwakilisha Rais Samia katika Mkutano wa Dharura wa SADC Nchini Zambia

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Mpango.png
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Utatu wa Asasi mbili za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika Lusaka, Zambia tarehe 23 Machi 2024.

Makamu wa Rais ataondoka nchini tarehe 22 Machi 2024 kushiriki Mkutano huo ambao agenda kubwa ni hali ya ulinzi na usalama katika nchi za SADC, hususan katika Jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji na Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Mkutano huo utatanguliwa na Mikutano ya maandalizi ya ngazi za Wataalam ambayo ilianza tarehe 17 Machi 2024 na itakamilishwa na Mikutano ya Makatibu Wakuu na Mawaziri itakayofanyika tarehe 22 Machi 2024.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) ataungana na Mawaziri wenzake kutoka nchi wanachama katika Mkutano huo muhimu.

Tanzania kama mwanachama wa SADC na ikiwa ni miongoni mwa nchi zinazochangia vikosi vya kulinda amani katika nchi za Msumbiji na DRC inashiriki kikamilifu katika ngazi zote za Mkutano huo.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali

WhatsApp Image 2024-03-20 at 16.29.42_b0b7b6ae.jpg
 
Maajabu haya!

Au Samia ni mgonjwa? Au hayupo nchini?
Ni hivi: Kagame kishamwaga sumu huku.
Makamba alikuwa kwa Kagame siku ziyo nyingi zilizopita, na usisahau tunao watu wa Bw. Fito (wenye asili ya huko) ndani ya serikali yetu ambao sasa ndio wanaendesha Tanganyika.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Utatu wa Asasi mbili za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika Lusaka, Zambia tarehe 23 Machi 2024.

Makamu wa Rais ataondoka nchini tarehe 22 Machi 2024 kushiriki Mkutano huo ambao agenda kubwa ni hali ya ulinzi na usalama katika nchi za SADC, hususan katika Jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji na Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Mkutano huo utatanguliwa na Mikutano ya maandalizi ya ngazi za Wataalam ambayo ilianza tarehe 17 Machi 2024 na itakamilishwa na Mikutano ya Makatibu Wakuu na Mawaziri itakayofanyika tarehe 22 Machi 2024.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) ataungana na Mawaziri wenzake kutoka nchi wanachama katika Mkutano huo muhimu.

Tanzania kama mwanachama wa SADC na ikiwa ni miongoni mwa nchi zinazochangia vikosi vya kulinda amani katika nchi za Msumbiji na DRC inashiriki kikamilifu katika ngazi zote za Mkutano huo.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali

SADC wanajadili nini la maana ,,,, dictators...just discussing how to consolidate power
 
Back
Top Bottom