Huyu Mkurugenzi Charles Mahera tunajuwa namna alivyopata hii nafasi ya Ukurugenzi wa NEC kwa upendeleo ili aje atumike kumptisha Magufuli akishindwa au atengeneze mazingira ya Magufuli kushinda.

Haiingii akilini kwa kutomuandikia Mahufuli kwa vitendo vya wazi wazi anavyovifanya kwenye mikutano ya Kampeni hasa anapotoa maagizo kwa TANROADS kujenga mababara.

Nitoe onyo tu, Mahera akumbuke ana familia inayomtegemea, akimfumbia macho Magufuli na kukubali maagizo anayompa itamgharimu yeye na kizazi chake. Mwaka huu CHADEMA hatuibiwi!!!
Mwaka huu hamna pa kutokea ccm bado ni chaguo la wengi na tutashinda kwa kishindo kikubwa sana. Iyo mikwara yako haina nafasi.
 
Mahera ni nani? Mtu yeyote ambaye anaishi kwa kulamba nyayo za wanasiasa badala ya kuegemea taaluma yake na maadili ya ofisi aliyokabidhiwa, anakuwa takataka mbele ya jamii.
Labda jamii ya wanachadema
 
TL asiende tukianzishe hapa hapa. Haina haja ya uchaguzi tena. Wamuite Magufuli kwanza - anadhalilisha akina mama, anafokea wapigakura eti hawapati maendeleo wakichagua wapinzani, sasa wanasema eti TL ana uraia wa nchi nchi nyingine! Waache ushenzi Watanzania tuamue kiongozi tunayetaka atuongoze.
Ukianzishe nyuma ya keyboard??? Uyo TL hana fikra finyu kama zako anajua madhara ya kutoitikia wito yalivyo sidhani kama atachukua ushauri wa ovyo kabisa kutoka kwako.
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemuandikia barua mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ya kumuita katika kikao cha kamati ya maadili ya Taifa.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dkt. Charles Mahera amesema hilo leo jijini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa mgombea huyo atafika mbele ya kamati Septemba 29 mwaka huu.

Akizungumzia uratibu na usimamizi wa kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu amesema tume imekumbana na changamoto kwa baadhi ya wagombea wa kiti cha Rais kutoheshimu sheria, taratibu na maadili ya uchaguzi.

Ameongeza kuwa baadhi ya wagombea wamekuwa wakitumia maneno ya kukashifu wagombea wenzao, tume, pamoja na kutoa taarifa zisizo za kweli zenye lengo la kuleta taharuki na uzushi miongoni mwa Watanzania.

Chanzo: TBC Online
FB_IMG_1574277425198.jpg
 
Baada ya wagombea urais kuapishwa DEDs wanawajibika kwa NEC. Kitendo cha Magufuli kuwaita DEDs Dodoma yeye akiwa mgombea alivunja sheria za uchaguzi kwa kiwango cha kutishia amani.
Wewe hujui kitu wameitwa lini mbona imekanushwa hiyo na Katibu Mkuu wa Tamisemi? Sababu haupo TZ ndiyo maana unabwabwaja tu.
 
Kwani Tanzania tuna Tume ya uchaguzi au tuna tawi la ccm linaloitwa tume ya uchaguzi?

Katiba Mpya ndiyo mwarobaini wa haya madudu yote.
Na uchaguzi unafanyika chini ya iyo tume unayoiita tawi la ccm, Lissu amekubali kuingia kwenye uchaguzi chini ya tume halafu kajamba nani unakuja hapa kupiga porojo zako.
 
Wewe unaamini kuwa chini ya Mahera kuna Tume ya Uchaguzi au kakitengo ka CCM kanakofanyia kazi kwenye ofisi za NEC?

Hawa ndio watu ambao hata siku watakapoondoka Duniani hakuna kitu cha maana watakachokiacha cha kukumbukwa kwa mema. Hata watoto wao watashindwa kutumia majina ya wazazi wao kutokana na aibu iliyoachwa na wazazi wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa mbona unashiriki uchaguzi?
 
Hivi msemaji wa Chama anaongea kwa niaba ya nani?
Mimi tume hainijui na CCM Mimi sio mgombea akili ikifyatuka naweza poromoshea matusi ya nguoni CCM na tume ya ya uchaguzi na hawezi nifanya lolote sana sana CCM waweza nifukuza uanachama lakini tume haina meno kwangu wala kwa Pole Pole sababu sisi sio wagombea tuliopitishwa na tume na kupewa masharti
 
Majibu ni marahisi tu, kuwa tume ya uchaguzi sio huru. Wagombea kibao wa upinzani wameenguliwa na tume ya uchaguzi kwa hila, na wagombea wa ccm wanavunja sheria wazi wazi bila kuchukuliwa hatua. Ni hivi, safari hii kuchezea kokote matokeo hakutakuwa na kumuachia Mungu fullstop.
Mashujaa wa nyuma ya keyboard mtafanya nini Lissu akishindwa? Ipo wazi Lissu anaenda kushindwa kwa aibu kubwa sana
 
Ila jamaa anaropoka aisee hana breki , lolote linalokuja kichwani anaongea tu bila kudigest.
Jiwe anavyolopokaga mdomo wake huwa na breki?mdomo wa magu ni mchafu unaongea hovyo lisu yeye anazungumza ya kweli
 
Back
Top Bottom