Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
16,248
2,000
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemuandikia barua mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ya kumuita katika kikao cha kamati ya maadili ya Taifa.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dkt. Charles Mahera amesema hilo leo jijini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa mgombea huyo atafika mbele ya kamati Septemba 29 mwaka huu.

Akizungumzia uratibu na usimamizi wa kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu amesema tume imekumbana na changamoto kwa baadhi ya wagombea wa kiti cha Rais kutoheshimu sheria, taratibu na maadili ya uchaguzi.

Ameongeza kuwa baadhi ya wagombea wamekuwa wakitumia maneno ya kukashifu wagombea wenzao, tume, pamoja na kutoa taarifa zisizo za kweli zenye lengo la kuleta taharuki na uzushi miongoni mwa Watanzania.

Chanzo: TBC

VIDEO:


 

seedfarm

Senior Member
Feb 9, 2020
122
1,000
Parasatic Mind
Ni ngumu sana kujibu hoja za Tundu lissu,kwa ufupi jamaa ana akili

Wamuulize Ana Makinda akiwa spika au Samia Suluhi wakati wa Bunge la katiba

Ni dhahiri Tundu lissu hakukariri darasani bali alielewa na ana exposure kubwa

Suala ni kujibu hoja za Kiwanja chato,Pesa za kununua ndege nani anazikagua na zilijadiliwa bungeni?

Kwanini Profesa Assad aliachishwa uCAG

Story hizo za NEC wanasababisha Tundu lissu kuwa na wafuasi wengi zaidi

CCM inasubiri mbeleko ya NEC na Wakurugenzi

Tatizo watu wana maisha magumu

Fujo na vurugu na Maandamano husababishwa na ugumu wa maisha

Venezuela huko tatizo watu maisha magumu

NEC inajichimbia shimo zaidi

Ongezeni mishahara na wekeni uhuru wa habari watu watawapenda
 

Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
3,664
2,000
Huyu Mkurugenzi Charles Mahera tunajuwa namna alivyopata hii nafasi ya Ukurugenzi wa NEC kwa upendeleo ili aje atumike kumptisha Magufuli akishindwa au atengeneze mazingira ya Magufuli kushinda.

Haiingii akilini kwa kutomuandikia Magufuli kwa vitendo vya wazi wazi anavyovifanya kwenye mikutano ya Kampeni hasa anapotoa maagizo kwa TANROADS kujenga mababara.

Nitoe onyo tu, Mahera akumbuke ana familia inayomtegemea, akimfumbia macho Magufuli na kukubali maagizo anayompa itamgharimu yeye na kizazi chake. Mwaka huu CHADEMA hatuibiwi!!!
 

Omusolopogasi

JF-Expert Member
Aug 31, 2017
4,553
2,000
TL asiende tukianzishe hapa hapa. Haina haja ya uchaguzi tena.

Wamuite Magufuli kwanza - anadhalilisha akina mama, anafokea wapigakura eti hawapati maendeleo wakichagua wapinzani, sasa wanasema eti TL ana uraia wa nchi nchi nyingine! Waache ushenzi Watanzania tuamue kiongozi tunayetaka atuongoze.
 

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
24,072
2,000
Kwa hii kasi ya Lissu inahitaji kifua kuivumilia naona CCM wameanza kushika shati baada ya kuzidiwa mbio.

Ile kauli ya Bashiru kuwa tutatumia Vyombo vya dola kubaki madarakani naona wamenza kuifanyia kazi.

NEC mjipanga vyema kwa hoja, mkikaa vibaya badala ya kumhoji itaonekana mnahojiwa nyinyi..

Kwa hii hatua naona mmeamua kumpa headline kwenye Vyombo vya habari bila gharama.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom