Muswada wa Marekebisho Sheria-2020: Unajua watu hawataweza kudai haki kwa niaba ya Wanyonge? Viongozi wa juu Serikalini hawatashtakiwa moja kwa moja!

Kwani bunge lina madaraka ya kubadiri katiba?Kazi ya bunge ni kutunga sheria.
Tupe undani wa mabadiriko hayo.
 
Magu anaogopa nini? Kwa nini anatunga sheria ya kumlinda baada ya kustaafu ilhali yeye ni rais mwema wa wanyonge?
Hapo ndipo mzalendo namba moja na rais wa wanyonge anaponishangaza. Mzalendo wa kweli angeweka sheria za kuwabana viongozi wanaotumia madaraka vibaya, mijizi na mafisadi, badala yake anaweka sheria za kuwalinda.
 
Kuna watu wanadhani ni CCM + VYAMA UPINZANI ila kuna jambo wanasahau kuwa wakimpandisha wataweza kumdhibiti?
 
This is insane, na Ndugai ameridhika kabisa kuona hili likitokea ndio maana yupo yupo tu, kusifia kila linalofanywa na serikali, hasara tupu.
 
Jamani, kwa hili nakuomba Mungu wangu kupitia Roho Mtakatifu uwatie wabunge wa CCM hekima, ujasiri,maono na udhubutu japo waweze kulisimamia hili tu lisipite !! !!?
 
Hili ni jambo la kuogofya sana linaelekea kutokea nchini, serikali imepeeleka mswada bungeni ili kumuongezea kinga rais na viongozi wengine wa bunge na mahakama kinga dhidi ya kushatakiwa moja kwa moja kwa kukiuka katiba ya nchi.

Huu ni mswada wa ajabu na wa kuogofya sana, mtu aliyeapa kuilinda na kuitetea katiba ya nchi inakuwaje leo anatafuta uhuru wa kuivunja katiba hiyohiyo?

Inakuaje marais wengine wote waliotangulia hawakuona kikwazo chochote kwenye kufuata katiba lakini huyu wa sasa kwake yeye katiba imekua kero kwake?

Ni nini hatma ya nchi yetu ikiwa tutaruhusu ujinga wa namna hii kuendelea kutokea? Unajua hata Adolf Hitler aliingia madarakani kwa njia halali kabisa, lakini taratibu akaanza kujiongezea mamlaka na kuwanyamazisha wote aliowaona kuwa kikwazo. Mwisho wake sote tunajua kilichotokea. Binadamu wote ni corrupt kwa viwango tofauti tofauti, hauwezi kumpa binadamu mwezako mamlaka yasiyo na mipaka, mwisho wake ni mbaya tu.

Wito wangu kwa wote mlioapa kuilinda na kuitetea katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania, wakati wenu ni sasa kufanya hivyo, the republic as we know it is under attack.
Inamaana waliyomfanyia lisu ben Azory nk wasishitakiwe ? Aaah hapana haitakuwa sawa.
 
Ni wakati sasa wa vyombo vya ulinzi na usalama kuingilia kati na kuwaweka sawa hawa watawala.

Maofisa wote wa jeshi, polisi na hata usalama wa taifa hua wanaapa kuilinda na kuitetea katiba ya nchi.

Wakati ndio huu, tukishindwa kumdhibiti huyu Magufuli atazidi kuitumbukiza nchi kwenye udikteta hatua kwa hatua, tutakuja kuamka ikiwa too late.
Naniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii! Mh watumbuliwe? Kila mmoja anaangalia maslahi yake wote wamejawa na tamaa ya madaraka wanahisi kuwa wapole kutawapelekea kuwa wateule,hilo limepita bila kupingwa labda kwa nguvu ya umaa ndo njia pekee japo kichapo kitatembeaaa
 
Kwan NYIE chadema si mnasema mwaka huu mnachukua nchi mbona mna wasi was na izo Mambo mtarekebisha Wala msijali
 
Back
Top Bottom