Muswada wa Marekebisho Sheria-2020: Unajua watu hawataweza kudai haki kwa niaba ya Wanyonge? Viongozi wa juu Serikalini hawatashtakiwa moja kwa moja!

Hii nchi Ina watawala wa ajabu sana ,naona wstatawala milele ,Mungu atupe uzime tuje tuwaone wsnavyopandishwa the hague.
 
Mabadiliko haya yakipitishwa yatazuia raia wengine kufungua mashtaka kwa maslahi ya umma wanapohisi kuna uvunjifu wa Katiba.

Hutaruhisiwa kumtetea raia mwenzako hata kama hana uwezo wa kujitetea, hutaruhusiwa kutetea nchi yako kupitia mahakama isipokuwa pale tu unapokuwa umenyanyaswa moja kwa moja, na hutaweza kutoa mchango wako kuilinda KatibaYetu. Hii inaondoa uzalendo.

Kutoruhusu mtu au taasisi kufungua mashtaka bila kuathirika moja kwa moja inakulazimisha kujitegemea na kujitetea unapokutwa na unyimwaji wa haki zako unaohitaji mahakama kuingilia.

Mabadiliko haya yatawaathiri sana wasiokuwa na uwezo na ujasiri wa kujisimamia wenyewe kisheria kama vile walemavu, watoto, wajane na makundi mengine mengi ya kijamii ambayo yamekuwa yakisaidiwa na watetezi wa haki za binadamu kwa maslahi ya umma.
Hii ndiyo maana halisi ya 'serikali ya wanyonge'. Mnyonge anyongwe akishakufa apewe haki yake ya maziko.

Huwa nawacheki wale wanao aminishwa kuwa unyonge ni sifa ya maana kuwa nayo nasema hiiiiii...
 
Mabadiliko haya yakipitishwa yatazuia raia wengine kufungua mashtaka kwa maslahi ya umma wanapohisi kuna uvunjifu wa Katiba.

Hutaruhisiwa kumtetea raia mwenzako hata kama hana uwezo wa kujitetea, hutaruhusiwa kutetea nchi yako kupitia mahakama isipokuwa pale tu unapokuwa umenyanyaswa moja kwa moja, na hutaweza kutoa mchango wako kuilinda KatibaYetu. Hii inaondoa uzalendo.

Kutoruhusu mtu au taasisi kufungua mashtaka bila kuathirika moja kwa moja inakulazimisha kujitegemea na kujitetea unapokutwa na unyimwaji wa haki zako unaohitaji mahakama kuingilia.

Mabadiliko haya yatawaathiri sana wasiokuwa na uwezo na ujasiri wa kujisimamia wenyewe kisheria kama vile walemavu, watoto, wajane na makundi mengine mengi ya kijamii ambayo yamekuwa yakisaidiwa na watetezi wa haki za binadamu kwa maslahi ya umma.
Chato regime on fleek
 
Wataondoka na sisi tutairudisha nchi kwenye utawala wa sheria
Wakati ni sasa, wanatakiwa wapingwe nje na ndani, kwa gharama yoyote...hili la kusema wataondoka na sisi tutairudisha ni kukubali kushindwa asubuhi. Hawa wakiishajiwekea hizo kinga hamuwatoi madarakani na ndipo watakapowavuruga kuliko kawaida! Wapingwe sasa
 
Mawazo ya kipumbavu haijawahi kutokea.
Toka lini katiba yetu ikatungwa na mabeberu??
Mnataka kutuambia kwamba Nyerere alikuwa beberu??
Katiba yetu ilitungwa wakati wake,kama una maana hiyo tukufu basi ili kuona namna ya kushughulikia kwa kujibu wa katiba yetu Nyanga'au wewe!
unakaa nyagwa wewe, , unajua maana ya Uhuru wa bendera, au mpaka ukifa ndipo ukamsumbue Nyerere akujuze, ukoloni mamboleo ndio misingi ya katiba zetu hizi za kiafrika sawa mama mdogo
 
Sio kweli, viongozi wa kiafrika wanavunja katiba zao kwa manufaa yao binafsi.
kwasababu katiba zenyewe zimekaa kimtegomtego kuvunjwa na ni rahisi sana kwa kiongozi wa afrika kuvunja katiba ,hilo linawezekana sana tu ,ilihali sio.wote
 
Watu wanafanya maandalizi ya kunajisi katiba ya nchi ndiyo maana wanatunga sheria ya kuwalinda alafu mataga yanakenua kama ngiri
Namkumbuka marehemu Mtikila. Angekuwepo angefungua kesi mahakama ya rufaa kupinga. Anyway, alikuwa mwanasheria. Wanasheria mpo wapi? Ama sisi walala hoi tufanyeje sasa?
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom