Muswada wa Marekebisho Sheria-2020: Unajua watu hawataweza kudai haki kwa niaba ya Wanyonge? Viongozi wa juu Serikalini hawatashtakiwa moja kwa moja!

Asasi za Kiraia 220 zimefanya uchambuzi wa muswada huo wa sheria na kuwasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya muswada huo kwa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria. Taasisi hizo zimeeleza kuwa japo kuwa zinafahamu muswada huo una lengo wa kusasisha Sheria iliyopo sana huku ikibaki kuendana na Katiba, ni mambo machache sana yanaenda na Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977

Asasi hizo zimesema wakati mambo machache yaliyopendekwa kwenye muswada huo yanaendana na Katiba au yanaifafanua Katiba vema, mambo mengi kwenye muswada huo yanakengeuka na kwenda kinyume na Katiba

Baadhi ya mambo yanayoenda Kinyume na Katiba ni;


1. Kifungu cha 7(b)(2) na 7(b)(3) of Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.3) 2020
Mapendekezo ya mabadiliko ya sheria yanaruhusu wale tu walioathiriwa moja kwa moja na uvunjifu fulani wa haki kufungua mashitaka ya kudai haki zao. Mabadiliko haya yakipitishwa yatazuia raia wengine kufungua mashtaka kwa maslahi ya umma wanapohisi kuna uvunjifu wa Katiba.
Kwa maana nyingine, hutaruhisiwa kumtetea raia mwenzako hata kama hana uwezo wa kujitetea, hutaruhisiwa kutetea nchi yako kupitia Mahakama isipokuwa pale tu unapokuwa umenyanyaswa moja kwa moja, na hutaweza kutoa mchango wako kuilinda Katiba yetu. Hii inaondoa uzalendo.
>>> Mapendekezo hayo yakiwa hivyo, Ibara 26 ya Katiba inampa kila raia jukumu na uhuru wa kuilinda Katiba yetu kupitia Mahakama ya nchi.
Athari kwenye maisha ya kila siku: Kwenye maisha ya kila siku tulio wengi tunakutana na changamoto za hapa na pale. Kuna mifumo tofauti kutusaidia kukabiliana na hizi changamoto ikiwemo, kwa matatizo makubwa na magumu, mifumo ya Mahakama.
Kutoruhusu mtu au taasisi kufungua mashtaka bila kuathirika moja kwa moja inakulazimisha kujitegemea na kujitetea unapokutwa na unyimwaji wa haki zako unaohitaji Mahakama kuingilia.
Kuna watu wengi ambao wamesaidiwa kudai haki zao na mashirika tofauti ambao wanawasaidia kwa utalaamu, rasilimali na mikakati na kusimamia kwa ujumla mashtaka yao. Mabadiliko haya yatawaathiri sana wasiokuwa na uwezo na ujasiri wa kujisimamia wenyewe kisheria kama vile walemavu, watoto, wajane na makundi mengine mengi ya kijamii ambayo yamekuwa yakisaidiwa na watetezi wa haki za binadamu kwa maslahi ya Umma.


2. Kifungu cha 7(b)(4) na 18A na 65A of Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.3) 2020
Mabadiliko ya sheria yanaondoa maana ya kuwa Jamhuri na badala yake tunaanza kulekea kwenye utawala usiokuwa wa kisheria kama vile utawala wa kifalme. Kwenye Jamhuri watu wote, wananchi na viongozi, wanaangaliwa sawa kwa jicho la sheria. Ndio tunaoita utawala wa sheria – kila mtu awe mdogo au mkubwa, anawajibika kwa kile alichofanya mwenyewe.
Kwa kuwatoa watu fulani kutoka mfumo wa kawaida wa haki, mfumo wa Mahakama, na kufanya hawawezi kuwajibishwa moja kwa moja, hata kama wamekiuka Katiba, inatupeleka kuwa na ngazi mbili za raia, wanaofuata sheria na wasiofuata sheria.
Pamoja na haya, misingi ya demokrasia na Jamhuri yetu ni mihimili mitatu ya Serikali, Bunge na Mahakama. Kila mhimili una majukumu yake na haitakiwi kabisa kuingiliana.
Mhimili mmoja unawajibisha mwingine kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo na haki. Hii haijalishi nani anashika cheo cha Rais, ni msingi wa Katiba yetu, nchi yetu na sheria zote za nchi.
>>> Ibara ya 13 ya Katiba inaeleza usawa mbele ya sheria kwa kila mwananchi na Ibara ya 4 inazungumzia mihimili mitatu ya Serikali na jinsi zinavyotakiwa kushirikiana, kila taasisi kwa uhuru wake.
Athari kwenye maisha ya kila siku: Kuna watu wanaopenda kusema demokrasia siyo chakula. Ukweli ni kwamba haki za mfumo wetu wa utawala, zinajulikana kama haki za siasa, hazionekani wazi kwenye maisha ya kila siku kama ilivyo kwa haki nyingine kama za kuishi na kupata chakula.
Tunaporuhusu baadhi ya watu kuwa nje ya sheria ambazo sisi wote tunazifuata, tunatengeneza mazingira tatanishi ya kutegemea utashi mtu moja au watu wachache. Wao ndio wataamua utamu na ugumu wa maisha yetu bila sisi kuwa na mchango wowote.
Mamlaka ya viongozi wetu wote yanatoka kwa wananchi na kila hatua inayotupeleka mbali na hilo, inazidi kupunguza uwezo wetu wa kuamua mwelekeo ya maisha zetu.


3. Kifungu cha 7(b)(2) na 7(b)(3) na 18A na 65A of Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.3) 2020
Haya mabadiliko ya sheria yanawapa kundi la watu Mamlaka juu ya sheria na yanapunguza uwezo wa baadhi ya watu kudai haki nchini. Kwa sababu Mahakama ni sehemu ya mwisho kupeleka kilio chako ukinyimwa haki, hii ni sawa na kutomruhusu mtoto kulia unapompiga.
Tunahitaji kutoa dukuduku letu na kuamini kwamba tunapokanyagwa na mtu yoyote, tutafidiwa. Utawala wa sheria unategemea imani yetu katika mifumo ya sheria. Mifumo yetu ya sheria ikianza kuleta ubaguzi kuanzia kwenye sheria zenyewe ndio tunaelekea kuuua mfumo yenyewe.
>>> Ibara 26 ya Katiba inampa kila raia jukumu na uhuru wa kuilinda Katiba yetu kupitia Mahakama ya nchi
Athari kwenye maisha ya kila siku: Tunapofunga milango ya mfumo wa haki nchini ndio walalahoi wanakosa njia muhimu ya kufidiwa. Watu maarufu na wenye mahusiano na vigogo na wanasiasa wanaweza kuwa na njia tofauti lakini wananchi wa kawaida wanategemea mfumo wa Mahakama wanapodai haki zao. Wapi tupeleke kilio chetu haki zetu zikikiukwa?

Je, una maoni gani kuhusu muswada huu unaotarajiwa kupitishwa Bungeni hivi karibuni?

Pia, unaweza kusoma: Muswada wa Rais, Spika, Waziri Mkuu kutoshitakiwa unapangiwa siku mbili Juni 5&6 tena kwa hati ya dharura

Kusoma zaidi uchambuzi wa Vifungu vinavyokiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tafadhali tembelea PDF hii
IMG-20200608-WA0001.jpg
 
Naomba kujuzwa hapa sijapaelewa kabisa au sijui kichwa changu cha panzi au la,mwenye uelewa wa suala hili atujuze
 
sijaelewa kutoka chini ya sakafu ya moyo wangu juu ya jambo hili kwa nini haya yapo zaidi katika awamu hii ya 5
 
Kwa kifupi sheria inahamasisha ufisadi,sheria ya kinga ilikuwa inamfaa Baba wa Taifa tu
 
Malaika muungwana asiyekuwa na mipango ya kufanya matendo ya kishetani hahitaji kinga ili abakie mbinguni.

Mbinguni ndiyo makao yao waungwana isipokuwa njia pekee ya kubakia mbinguni baada ya kutenda matendo ya kiibilisi Ni kuibadili katiba ya mbinguni.

Jpm akijipa Kinga ya kisheria ya kutoshitakiwa atakuwa amefanya kosa la kuigharimu taifa kwa sababu atakuwa amejiweka juu ya sheria. Tanzania inahitaji mtu msafi asiyeogopa sheria kwa sababu hofu ya sheria Ni evidence ya uchafu wa matendo.

Hata Kama ana mazuri elfu moja lakini kitendo Cha kujiwekea Kinga ya kisheria kinaonyesha yale mazuri Yana harufu ya unafiki na ghilba ndani yake isipokuwa tumefichwa ukweli na tunapigwa propaganda ili tusielewe uhalifu unaoendelea.
 
Mbona kuweka kinga?..unaogopa nini iwapo unafuata haki,taratibu na sheria?.

Sijui wengine mnanonaje ila mhh this looks like a Red Flag!
 
Hiyo ni moja ya dalili kuwa watawala hawataki kutoka madarakani na wanapanga kufanya maovu zaidi na hasa wakati huu wa uchaguzi mkuu. Wajuzi wa mambo tupenì mwongozo tufanye nini ili tudai katiba mpya kabla ya uchaguzi wa October?

Je tunaweza kusaini fomu maalum na kwamba tukifika idadi kadhaa basi lazima serikali ifanye mchakato wa katiba mpya kabla ya uchaguzi?
 
Hapa ndio pale tunasema hii nchi imeshakuwa ya Kidikteta. Halafu inasema inatetea Wanyonge
Inasikitisha kwamba toka 1985 wakati Rais wa kwanza amestaafu hadi hivi leo, hatuna rekodi inayo onyesha, Spika, Naibu,Jaji mkuu,Waziri mkuu ,makamu wa Rais na Rais wote walio staafu kama waliwahi au mmojawao aliwahi shitakiwa kwa makosa aliyotenda akiwa madarakani.

Sasa kama hiyo haijawahi kutokea ,hawa wakubwa zetu wa sasa, wamefanya nini/wanatarajia kufanya nini ambacho wana shaka nacho kwamba kinaweza kuwafikisha mahakamani wakisha staafu nyadhifa zao?

Hivi tulipo nanga inapaa, serikali kaa la moto,mahakamani hakueleweki,bungeni watu wanaingia bila hata udhamini wa vyama! Wakijiwekea uzio hii nchi tutaendeshwa kwa kasi gani?
 
Mabadiliko haya yakipitishwa yatazuia raia wengine kufungua mashtaka kwa maslahi ya umma wanapohisi kuna uvunjifu wa Katiba.

Hutaruhisiwa kumtetea raia mwenzako hata kama hana uwezo wa kujitetea, hutaruhusiwa kutetea nchi yako kupitia mahakama isipokuwa pale tu unapokuwa umenyanyaswa moja kwa moja, na hutaweza kutoa mchango wako kuilinda KatibaYetu. Hii inaondoa uzalendo.

Kutoruhusu mtu au taasisi kufungua mashtaka bila kuathirika moja kwa moja inakulazimisha kujitegemea na kujitetea unapokutwa na unyimwaji wa haki zako unaohitaji mahakama kuingilia.

Mabadiliko haya yatawaathiri sana wasiokuwa na uwezo na ujasiri wa kujisimamia wenyewe kisheria kama vile walemavu, watoto, wajane na makundi mengine mengi ya kijamii ambayo yamekuwa yakisaidiwa na watetezi wa haki za binadamu kwa maslahi ya umma.
 
Sheria za namna hii ni kwa faida ya nani? kwa karne hii ningesikia kua wenye nia ya kufungua kesi kwa faida ya Umma wangepewa usaidizi wa kisheria na serikali.
 
Hii nchi Ina watawala wa ajabu sana ,naona watatawala milele ,Mungu atupe uzime tuje tuwaone wanavyopandishwa the hague na vilevile Mungu asiwaue mapema mpaka wapande ndege kwenda the hague.
 
Back
Top Bottom