Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iondolewe haraka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iondolewe haraka!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ibrah, Apr 14, 2008.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Katika nchi yetu kuna sheria za ajabu sana, mojawapo ni hii ya kumlinda Rais Mstaafu kutokana na makosa aliyoyafanya akiwa Rais. Habari juu ya Ufisadi uliofanyika katika awamu ya tatu ya Uongozi wa nchi yetu ni dira tosha ya kutufanya tufikirie upya juu ya Kinga ya Rais Mstaafu ya kutoshitakiwa.

  Kashfa za kufanya biashara akiwa Ikulu, Wizi wa Mgodi wa Kiwira uliokuwa na thamani ya mabilioni ya shilingi kwa Mkapa-Yona kujiuzia kwa shilingi milioni 700 tu, Uundaji wa Kampuni za wizi na utapeli za Meremeta na Tangold, Wizi wa EPA BoT na Ujenzi wa Twin Towers za BoT, Ubinafsishaji wa NBC kwa Bei ya kutupa,Ununuzi wa Rada kwa bei ya kuruka, Ununuzi wa ndege ya Rais kwa gharama ya Watanzania "kula nyasi" na nyinginezo ni sababu za kutosha kabisa za kutufnaya Watanzania kupigania kuondolewa kwa sheria ya kinga inayomlinda Raisi mstaafu kutoshiotakiwa kwa wizi, ubadhirifu na Ufisadi aliofanya Rais Mstaafu wakati akiwa madarakani.

  Sheria ya Kinga ni Msingi mkuu wa Ufisadi na Utawala wa hovyohovyo kwa gharama za Watanzania kama kashfa hizo nilizotaja hapo juu zilivyotugharimu Kiuchu na Kimaadili. Kuvuja kwa Habari za juzi kuhusu Utajiri wa Waziri Chenge kumiliki dola milioni moja katika akaunti nje ya nchi ni ushuhuda mwingine juu ya Sheria hii Fisadi ambayo inaweka misingi ya Wizi na Uhujumu wa mali ya Umma kwa hasara ya Wananchi wa Tanzania. Hebu tujiulize; Je, itawezekana kumshitaki Chenge aliyekuwa MWanasheria Mkuu wakati wa Mkapa bila kumgusa Mkapa (ambaye sheria inamkinga dhidi ya kushitakiwa?), Tunaweza kumshitaki Daniel Yona kwa kujiuzia Kiwira kwa bei ya bure bila kumshitaki Mkapa ambaye ni "Mjasiriamali" na Mbia mwenzake? KAtika haya mawili haiwezekani kutenda haki maana haiyumkiniki na ni vigumu sana kuwatia watu hawa hatiani (Yona na Chenge) na kumwachia huru Mkapa ambaye ama alishirikiana nao au alishindwa kuwajibika kwa Makusudi na kuwaachia "Wajasiriamali" na Mafisadi kama Chenge kujineemesha kupitia mikataba hewa na feki ambayo naamini kuwa Aliisaini kwa ahadi ambazo ndizo leo imemfanya Chenge kutuhumiwa kuwa na USD Milioni 1 kwenye akaunti zake nje ya nchi!

  Kuondolewa kwa shria hii Fisadi, pia kutasaidia kupunguza idadi ya Wagombea urais ambayo wakati wa kinyam]ng'ang'anyioro cha kwenda kugombe Urasi huwa kunakuwa na orodha ndefu ya watu wanaotaka kuwa Marais maana wanajua fika kuwa wakipata nafasi hiyo Ufisadi wao hautakumbukwa milele. Hii itatusaidia kuwa na Wagombea safi na wnaojiamini kuwa ni Waadilifu na ni safi.

  Wito wangu kwa Viongozi wa Dini, NGOs, Wananchi, Wabunge na Wanaharakati wengine ni kuwa wakati umefika wa Kushinikiza kufutwa kwa sheria FISADI inayomkinga Rais dhidi ya Rais Mstaafu. Tuanze sasa na ikiwezekana hata kutumia Mahakama ili sheria hiyo iondolewe haraka na kabla hatujapata Rais wa Awamu ya Tano.

  Tukifanikiwa kuondoa sheria hiyo Fisadi, tuanze na Mkapa ambaye ndiye chimbuko, Founder na Pioneer wa Ufisadi tunaouona sasa na unaotula kama kansa Watanzania.


   
 2. Allah's Slave

  Allah's Slave JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2008
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hii sheria ikiondolewa ndio mwanzo wa Tanzania kuwa na maraisi kama Mugabe. Hii sheria iko kuzuia maraisi wasing'ang'anie madarakani pindi time yao itakapokwisha. Kama mimi najua nikiachia ngazi brake ya kwanza jela unadhani ntfanya nini?
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,882
  Likes Received: 83,364
  Trophy Points: 280
  Hakuna Mtanzania yeyote anayestahili kuwa juu ya sheria pamoja na Rais wa Tanzania. Katiba yetu ina mapungufu mengi sana hata Mzee Warioba ameshatamka kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kuandika katiba mpya. Na kwa maoni yangu hiki kipengele chenye kinga ya Rais kutoshtakiwa kwa yale aliyoyafanya alipikuwa Rais inabidi kiondolewe. Hatuwezi kuwa na Marais mafisadi kama Mkapa wanafanya biashara wakiwa Ikulu wanaiba rasilimali za Watanzania mchana kweupe, halafu wasifunguliwe mashtaka na kufilisiwa kwa ufisadi walioufanya walipokuwa madarakani.

  Tunataka viongozi waadilifu ambao wanagombea nafasi za juu za uongozi ili kuwatumikia Watanzania kwa moyo mmoja, na siyo mafisadi ambao wanataka kutumia nyadhifa tulizowakabidhi kujitajirisha wao, familia zao, marafiki na jamaa zao.
   
 4. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hivi ndugu zangu ni kwanini uwezo wetu wa kufikilia unakuwa duni sana kiasi hichi.

  Unataka kuniambia hawa wabunge na viongozi wengine wote hawaoni upungufu wa sheria hii kuwa ni mwanzo wa maovu kama haya, angalia mambo ambayo mkapa kayafanya mpaka anaona aibu kuongea na watu, lakini eti sheria inamlinda.

  Nadhani sheria hii ilikuwa inastaili enzi hizo za Baba wa Taifa waliokuwa waadilifu na wazalendo kweli ambao mpaka sasa tunatamani wangekuwepo, lakini sio enzi hizi za akina mkapa kikwete, tunaoomba hata wapate matatizo yoyote na watoweke muda wowote kwa jinsi walivyotutesa na wanavyoendela kututesa watanzania,

  Na ni kwanini hata wabunge wasishirikiana hata katika hili jamani, hii katiba yetu mbona mbovu namna hii jamani, watu wanaiangalia tu kwa sababu ndo inawapa ulaji tu sio

  Poa, ila iko siku itafika tu na mambo yataenda kama tunavyotaka
   
 5. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  Manung'uniko na mijadala mingi imeonekana ikisema Mheshimiwa Rais Mstaafu angefaa kupelekwa mahakamani, na wengine hudiriki kusema 'angestahili kuozea jela'.

  Jambo ambalo najiuliza hata akiondolewa kinga,je katiba inaruhusu rais mstaaf kushtakiwa?

  na kama inaruhusu, DPP atamshtaki kwa kosa gani na lililopo katika sheria ipi?, Je ushaidi upo wakutosha?

  Adhabu ya makosa au kosa hilo ni ipi?, kifungo au fine?

  je na kama kinga yakatiba ikitolewa itakua applied retrospectively?yani namaanisha itamgusa Mpaka Rais mwinyi au ni kwa marais wanaofuatia?

  Dhumuni lakuuliza maswali haya ni kwasababu inaonekana kama jamii ya Kitanzania tunashabikia tu kwakusema Mkapa apelekwe mahakamani bila ya kusema kwa kosa lipi na lililokatika sheria ipi, na kujua ugum wa kikatiba unaomlinda. Si maanishi kusema tu Kiwira, la hasha hiyo haitoshi. Si maanishi kufungua kampuni ikulu, tunaweza kusema hayo yote, lakini cha muhimu sheria zetu zinasemaje kuhusu mambo kama hayo? na process yake ikoje ya kikatiba?kama nilivyouliza hapo juu.

  Naomba tujadili bila matusi au shutuma.
  Asanteni.
   
 6. a

  alibaba Senior Member

  #6
  Nov 27, 2009
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 185
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa kufupisha stori MKAPA ni Mwizi na Mlarushwa. Ndani ya hayo mawili kuna mlolongo wa tuhuma za ubadhirifu na coraption ukianzia Manunuzi ya Ndege ya Raisi , Rada, Kujiuzia Kiwira na mengineyo the list is long enough.
   
 7. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Kosa pekee ambalo halina kinga kwa Rais Mstaafu Mkapa ni kufanya biashara wakati akiwa IKULU. Hilo litaingia kwenye kutumia madaraka vibaya.
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  Nov 27, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,610
  Likes Received: 3,911
  Trophy Points: 280
  Semenya maswali yako mazuri ndugu yangu,

  ebu soma kisa hiki;

  Kuna kijiji kimoja Malangali kila anayeingia kuchukua uenyekiti wa kijiji anaingia na nyumba ya nyasi, akimaliza muda wake anatoka na nyumba ya bati kali, achilia mbali rasilimali zingine! ishu hii ni ya mjadala wa kitaifa kwa kila mwenye cheo chochote alipo popote pale Tz, Mkapa kaingia na yumo kwenye culture hii ya kitanzania ''wizi''

  Solution sio kwa rais, inaanzia chini kabisa , yeye ni matokeo na ni alama tosha ya kuonyesha kuwa mfumo wetu ni mbovu, kumbuka akienda jela leo kwa kisu kile kile wengi sana nao wataenda jela! swali ni nani msafi wa kumpeleka jela,USHAIHIDI WA KUWA HAKUNA WA KUMPELEKA JELA KUNAASHIRIA HATA HAWA WENGINE SIO WASAFI!! kama hakuna sheria kwa nini? rais malaika??

  njia pekee ya kubadili mfumo ni kuleta watu wapya serikalini, watakaosafisha uozo uliokuwepo na kuzuia yasitokee tena hapo baadaye.

  Hii kulala na kuamka kuandika kuhusu Mkapa mwaka wa tano , serikali ile ile, kuna watu wanajidanganya kuwa JK na MKapa sio marafiki!

  System, mahakama, n.k vingi wanaoviongoza mpaka leo hii ni haoa hao akina mkapa, uteuzi wa majji wakuu n.k ni kinga tosha sana

  Katiba ibadilishwe, rais kuteua hawa watu azuiliwe.
   
 9. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #9
  Nov 27, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,427
  Likes Received: 22,347
  Trophy Points: 280
  Kibaka anachomwa moto....
  Jizi kubwa namna hii linakula a/c...
  Nyumbani a/c, kwenye gari a/c, kila aendako a/c
  Hiyo ndio tofauti kubwa kati ya vijibaka na jizi mkapa
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Kama tungeweza kumonitor kwa wiki tu huyu bwana anaishi katika hali gani, tungelijua jinsi majuto alivyo mjukuu. Kitu kimoja hakiwezekani! Kurudisha muda nyuma maana yote yaliyotokea yametokea. Ila imekuwa ngumu sana kwake kukubaliana na hali halisi.

  Mi najua kama angekuwa uswazi basi kashachomwa moto maana mwizi wa uswazi watu hutolea uamuzi hapo hapo.

  Sasa kwa kuwa ni mtu mkubwa, anayetembea na ving'ora na kupigiwa saluti, hili jambo la hatari ya kufanya kosa la hujuma linakuwa kama ndoto za mchana.

  Pekee kilichopotea ni heshima yake ambayo imepotea na itakuwa ngumu sana kuirudisha especially imani kwa watanzania.

  Ni kweli nchi yetu wizi umekuwa kama mfumo. wanayeweza kubadili haya bado ni viongozi kwa kuondoa system zinazo hamasisha watu wezi kuingia katika madaraka na kula fedha za umma.

  Wakibadilika wao, hata huku chini kutabadilika. Vinginevyo ni kupoteza muda tu kumjadili mtu ambaye is underestimating people who put him in power.
   
 11. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #11
  Nov 27, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Hiyo kinga iko kwenye katiba ya nchi, swali lako hapo limejichanganya kidogo. Kwa hiyo kinga ikitolewa, it will be a fair game kumfikisha mahakamani.

  Kumfikisha mahakamani kutategemea uchunguzi na ushaidi ambao DPP atapelekewa. Kwa hiyo kama kuna ushahidi kwamba alihujumu uchumi, kula rushwa, kutumia ofisi kwa manufaa yake binafsi, n.k. atashitakiwa kama kibaka yeyote yule aliyekamatwa na makosa hayo kama sheria inavyosema. Kifungo kitategemea na sheria inavyosema kwa makosa atakayo kuwa nayo.

  Sidhani kama watafanya hivyo kumlenga mtu mmoja. Itabidi iwalenge marais wote wastaafu ndio maana inakuwa ngumu hata kwa rais aliye madarakani kuipa green light hiyo sheria.

  Just my opinion!
   
 12. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #12
  Nov 27, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Hata nyinyi wote hapa ni wezi wa aina yake kwa kuwa mnatumia muda vibaya badala ya kuchapa kazi mnabwata! Kipimo ni number of posts. Jipime ni mwizi grade gani mwenyewe kisha uone kama mkapa anastahili kufunguliwa mashitaka. Mkapa alifanya yaliyomhusu. Wewe je?
   
 13. M

  Magezi JF-Expert Member

  #13
  Nov 27, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nilishangaa yule askari kigoma amewaua wenzake ktk lindo badala angeua fisadi kama mkapa au RA
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Nov 27, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Semenya,
  Umeuliza Mkapa ashtakiwe kwa kosa gani. Kosa kubwa alilofanya Mkapa ni kula rushwa akiwa rais wa TZ. Aliuza NBC kwa rushwa. Alileta Net Problems kwa rushwa. Alijiuzia Kiwira kwa kukiuka taratibu za nchi. Hii inaweza kuangukia chini ya sheria za uhujumu uchumi. Na ushahidi upo.
   
 15. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #15
  Nov 27, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mwacheni Mkapa apumzike zake, amefanya na muda wake umeisha...hakuna fundisho lolote litakalopatikana kwa kumshitaki rais mstaafu zaidi ya kuongeza uwizi, ikulu kwa atakayekuwa rais...kwani atakuwa anahofia..maisha baada ya kustaafu..

  Nafikiri tuwe na tabia na utaratibu wa kuanza tulipo na kuendelea mbele..siyo kila siku kurudi kwa mkapa,mwinyi,nyerere..upuuzi huu.
   
 16. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #16
  Nov 27, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Yes tufike mahala sasa tuchague. Tumepiga kelele imetosha, tuanze kusaka maendeleo yetu
   
 17. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #17
  Nov 27, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  You're right hapo mkuu, ila uoni tatizo lingine hapo ki haki itabidi turudi na kwa Ruksa kwani nae anamakosa haya haya, alafu tuna mawaziri nao wanajinai hizi hizi ambao bado wako huru ingawa awatumikii taifa ki-ngazi ya juu.

  Kama ni sheria kuchukua mkondo wake hivyo orodha ni ndefu wenye tuhuma hizi. Na walio hai leo hii Tanzania. Kwa upande wangu hayo ni madhambi ambayo yalikua ni-inevitable kutokana na hii hii katiba mbovu. Hivyo solution kung'oa katiba mbovu ili kuweza kuzuia future embezellment na tabia mbaya. Hila tunapo ng'ang'ana na kuwa peleka mahakamani atu likomboi taifa bali tunafanya wajilinde na hizo kinga.

  Hivyo ni better ku-forget whith these fools hili tanzania iweze okoa hasara zake leo na kuwa na huhakika wa kumkaba yeyote in the future through the change of katiba yetu leo. Vinginevyo mi naona kama vile tunaruhusu mafisadi wapya watoke through hizi kinga zao na uwoga wa kubadilisha sheria kwa kujuwa wazi watafungwa.

  Point ni kwamba katiba mpya ije na promise ya kwamba kesi za zamani azito sikilizwa hili tuweze pata mabadiliko na kuwatoa uwoga hawa wa sasa kama wanadhani wataenda jela chini ya sheria mpya.
   
 18. Mgosi wa Sui

  Mgosi wa Sui Member

  #18
  Nov 27, 2009
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kushitakiwa hata mwinyi na nyerere nao pia kuna makosa walifanya wakiwa madarakani.

  Mwinyi :mnakumbuka loliondo,IPTL, na ile dhahabu iliyokamatwa airpot na mrema.

  Nyerere:sababu ya actionalis personalis mortum cum personna in criminal law hawezi kushitakiwa
   
 19. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #19
  Nov 27, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kitu kinacho zuia rais au rais mstaafu asiweze kushtakiwa ni kinga. Ikisha tolewa kinga rais anaweza kushtakiwa.

  Kusema kuwa hakuna sheria za kumshtaki raisi hata akiondolewa kinga ni kukosa logic.

  Rais kama mfanyakazi yoyote yule mwingine anaongozwa na katiba ya nchi na pia muongozo wa ofisi yake.

  Kwa maana anaweza kushtakiwa kwa kukiuka katiba na pia miiko ya ofisi yake.

  Hauwezi kuniambia rais kaiba au kula rushwa halafu ikosekane sheria ya kumshtaki. Ingekua hivyo basi ina maana kusingekua na miiko ya ofisi ya raisi kabisa.
   
 20. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #20
  Nov 28, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  Ushaidi upo wakutosha, maana in law its not what u know, but what u can prove before the court of law.
   
Loading...