Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,730
- 533
Katika nchi yetu kuna sheria za ajabu sana, mojawapo ni hii ya kumlinda Rais Mstaafu kutokana na makosa aliyoyafanya akiwa Rais. Habari juu ya Ufisadi uliofanyika katika awamu ya tatu ya Uongozi wa nchi yetu ni dira tosha ya kutufanya tufikirie upya juu ya Kinga ya Rais Mstaafu ya kutoshitakiwa.
Kashfa za kufanya biashara akiwa Ikulu, Wizi wa Mgodi wa Kiwira uliokuwa na thamani ya mabilioni ya shilingi kwa Mkapa-Yona kujiuzia kwa shilingi milioni 700 tu, Uundaji wa Kampuni za wizi na utapeli za Meremeta na Tangold, Wizi wa EPA BoT na Ujenzi wa Twin Towers za BoT, Ubinafsishaji wa NBC kwa Bei ya kutupa,Ununuzi wa Rada kwa bei ya kuruka, Ununuzi wa ndege ya Rais kwa gharama ya Watanzania "kula nyasi" na nyinginezo ni sababu za kutosha kabisa za kutufnaya Watanzania kupigania kuondolewa kwa sheria ya kinga inayomlinda Raisi mstaafu kutoshiotakiwa kwa wizi, ubadhirifu na Ufisadi aliofanya Rais Mstaafu wakati akiwa madarakani.
Sheria ya Kinga ni Msingi mkuu wa Ufisadi na Utawala wa hovyohovyo kwa gharama za Watanzania kama kashfa hizo nilizotaja hapo juu zilivyotugharimu Kiuchu na Kimaadili. Kuvuja kwa Habari za juzi kuhusu Utajiri wa Waziri Chenge kumiliki dola milioni moja katika akaunti nje ya nchi ni ushuhuda mwingine juu ya Sheria hii Fisadi ambayo inaweka misingi ya Wizi na Uhujumu wa mali ya Umma kwa hasara ya Wananchi wa Tanzania. Hebu tujiulize; Je, itawezekana kumshitaki Chenge aliyekuwa MWanasheria Mkuu wakati wa Mkapa bila kumgusa Mkapa (ambaye sheria inamkinga dhidi ya kushitakiwa?)
Tunaweza kumshitaki Daniel Yona kwa kujiuzia Kiwira kwa bei ya bure bila kumshitaki Mkapa ambaye ni "Mjasiriamali" na Mbia mwenzake? KAtika haya mawili haiwezekani kutenda haki maana haiyumkiniki na ni vigumu sana kuwatia watu hawa hatiani (Yona na Chenge) na kumwachia huru Mkapa ambaye ama alishirikiana nao au alishindwa kuwajibika kwa Makusudi na kuwaachia "Wajasiriamali" na Mafisadi kama Chenge kujineemesha kupitia mikataba hewa na feki ambayo naamini kuwa Aliisaini kwa ahadi ambazo ndizo leo imemfanya Chenge kutuhumiwa kuwa na USD Milioni 1 kwenye akaunti zake nje ya nchi!
Kuondolewa kwa shria hii Fisadi, pia kutasaidia kupunguza idadi ya Wagombea urais ambayo wakati wa kinyam]ng'ang'anyioro cha kwenda kugombe Urasi huwa kunakuwa na orodha ndefu ya watu wanaotaka kuwa Marais maana wanajua fika kuwa wakipata nafasi hiyo Ufisadi wao hautakumbukwa milele. Hii itatusaidia kuwa na Wagombea safi na wnaojiamini kuwa ni Waadilifu na ni safi.
Wito wangu kwa Viongozi wa Dini, NGOs, Wananchi, Wabunge na Wanaharakati wengine ni kuwa wakati umefika wa Kushinikiza kufutwa kwa sheria FISADI inayomkinga Rais dhidi ya Rais Mstaafu. Tuanze sasa na ikiwezekana hata kutumia Mahakama ili sheria hiyo iondolewe haraka na kabla hatujapata Rais wa Awamu ya Tano.
Tukifanikiwa kuondoa sheria hiyo Fisadi, tuanze na Mkapa ambaye ndiye chimbuko, Founder na Pioneer wa Ufisadi tunaouona sasa na unaotula kama kansa Watanzania.
Pia soma
www.jamiiforums.com

Jaji Samatta: Rais hana kinga kwa mambo aliyoyafanya akiwa Rais bali yale aliyoyafanya kama Rais
RAIS MSTAAFU ANAWEZA KUFUNGULIWA MASHTAKA NA OFISI YA DPP Haya yameelezwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta katika Mjadala wa Uwajibikaji uliandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji iitwayo Wajibu katika Chuo cha Sheria Tanzania(Law School of Tanzania) Jijini Dar es Salaam Jaji Samatta...
Jaji Mstaafu Raymond Mwaikasu ataka Rais aondolewe kinga
JAJI mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania,Raymond Mwaikasu, amewataka wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kuondoa kinga inayomlinda rais wakati anapostaafu ili aweze kufikishwa mahakamani pindi inapobainika amevunja katiba wakati wa utawala wake.
Jaji Mwaikasu alitoa wito huo jijini Dar es Salaam jana alipozungumza na viongozi wa dini walipokutana kujadili mwenendo wa Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea mjini Dodoma.
Alisema kuondolewa kwa kinga hiyo kutasaidia kudhibiti baadhi ya watu wanaotarajia kuingia madarakani kwa ajili ya kujinufaisha binafsi badala ya kulinda katiba.
Chanzo: Tanzania Daima la 27/3/2014
Waheshimiwa wana Bodi!
Naheshimu sana utaratibu wa Jf jinsi walivyopanga majukwaa yao humu. Ila ukweli ni kuwa jukwaa ambalo linatembelewa na watu wengi, wenye peo mbalimbali, hasi na chanya, hoja nzito na pia dhaifu ni Jukwaa la Siasa anayebisha apinge.
Hoja hii najua inastahili kuweka jukwaa la Sheria lakini mimi nimeiweka humu kwa sababu nilizotaja hapa juu. Naomba Moderator wanisamehe kwa hili na wasiiondoe hoja hii kwani ina maana kubwa sana kwa jamii inayoamka ya Watanzania.
HOJA
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (matoleo yote tangu tupate uhuru mpaka sasa ) sinawakingia kifua viongozi wakuu wa nchi (Marais - Waliopo madarakani na wastaafu) kutoshtakiwa mahakamani.
Hapa majuzi Rais wetu mstaafu Benjamini Mkapa kaenda kutoa ushahidi mahakamani kwenye kesi ya Costa Mahalu inayohusu uhujumu uchumi. Nilipatwa na mshtuko kidogo kwani ukizama ndani zaidi unaona kuwa na Rais alieoko madarakani anakuwa shahidi muhimu kwenye hii kadhia kwani yote yalifanyika akiwa waziri wa mambo ya nje.
Sasa najiuliza na wale mnaojua sheria naomba michango yenu ili baade iwe rejea kwenye kutoa maoni ya katiba mpya na katiba ilitolee ufafanuzi jambo hili.
Endapo mahakama itagundua kuwa Mkapa kasema uongo vipo vifungu vya kumtia hatiani mtu anayeongea uongo mahakamani Je kwa Mkapa au Kikwete itakuwaje ?
Je, Mtu mwenye kinga ya kushtakiwa ana sifa za kumtetea mtu mahakamani
Je, Mtu anaweza kuhukumiwa kutokana na ushahidi wa mtu asiye kuwa na sifa ya kushatakiwa
Naomba kuwasilisha
Hakuna Rais Mstaafu anayeogopa kushtakiwa na serikali
Rais Mstaafu Kikwete hata asipoambiwa na Magufuli anakila sababu ya kuondoa hofu.
Kwa mujibu wa ibara ya 46 ya katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inasema kwamba Rais akiwa madarakani hawezi kushitakiwa kwa makosa ya jinai wala madai kuhusiana na jambo lolote ambalo Rais alilifanya ama kabla ya kushika kiti cha urais au baada.
Na kama Kesi ilikuwa mahakamani ikimhusu Rais toka mwanzo mara tu mtu huyu anapokuwa Rais kesi hiyo inatakiwa isimame.
Makosa ya jinai ni kama mauaji, wizi, ubakaji nk. wakati makosa ya madai ni kama kutolipa deni, kuvunja mkataba, ugoni nk.
Lakini katiba inatoa mwanya wa kumshitaki Rais kwa makosa ya madai mfano Rais hajalipa deni lako na unataka kumshtaki unatakiwa umtumie notisi mwezi mmoja kabla ya kufungua kesi ukijitambulisha jina lako na anuani yako na ueleze unataka kumshtaki kwa kosa gani.
Hii ni ili kama anaweza akayamaliza ayamalize kabla ya kwenda mahakamani.
Kuhusu Rais Mstaafu ibara hiyo hiyo ya 46(3) inasema kama Rais alimaliza muda wake wa Urais kwa njia ya kawaida (hakuondolewa madarakani na bunge) basi hakuna mashitaka yoyote yatakayofunguliwa mahakamani dhidi ya mtu aliyekuwa Rais kwa jambo lolote alilolifanya akiwa madarakani kama Rais.
Na hata kama sheria na katiba ikibadilishwa kuondoa kinga ya kushtakiwa kwa Marais wastaafu sheria hiyo mpya haiwezi kumgusa Rais mstaafu wa awamu ya nne na waliomtangulia maana sheria hufanya kazi kwenda mbele ikianzia pale ilipotungwa hairudi nyuma. ( The law does not operate retrospectively).
Hivyo Marais wastaafu wanatakiwa wawe na amani tu hata wasipoambiwa na Rais Magufuli.
Bashe ataka kinga ya Rais iondolewe kwenye katiba
Mbunge wa Nzega kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hussein Bashe amefunguka na kutaka katiba ya nchi kubadilika ili ikiwezekana kinga ya Rais iondolewe kwenye katiba kwa kuwa kinga hizi zinawafanya viongozi hao kufumbia macho baadhi ya vitu.
Bashe amesema hayo jana mjini Dodoma baada ya kamati za bunge kutoa ripoti juu ya biashara za madini ya Tanzanite na Almasi ambapo katika ripoti hizo baadhi ya mawaziri wa serikali mbalimbali wametajwa kuhusika katika kufanya maamuzi ambayo yamelitia hasara taifa kwa maslahi yao binafsi.
"Umeona maamuzi yaliyofanywa na mawaziri waliotajwa kwenye hizo ripoti unatakiwa kujiuliza swali la msingi hivi maamuzi yote yale ya kuvunja sheria yaliyofanywa na mawaziri hivi Marais waliokuwa madarakani walikuwa hawajui?
"Leo Rais Magufuli asingekuwa tu amesukumwa na moyo wake kufanya haya anayofanya kwenye uwekezaji wa madini tungeyajua haya? Umefika wakati kama nchi wa kuangalia uwezekano kufanya mabadiliko ya katiba, tuangalie mabadiliko ya sheria tuangalie tunapowapa marais hawa kinga haya mambo ndiyo hutokea" alisema Bashe
Bashe anaamini kuwa maamuzi ambayo hufanywa na mawaziri hao ili kufanya mabadiliko makubwa katika baadhi ya mikataba ambayo imeigharimu serikali na nchi kiujumla kuwa ni lazima viongozi wao wa juu ambao ni Marais walikuwa wakitambua mambo hayo.
Mpekuzi
Spika Ndugai awaonya wapinzani wanaotaka marais wastaafu washtakiwe
Ndugai amesema hayo leo (Jumanne) bungeni baada ya mchango wa Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali kusema haiwezekani mawaziri na watendaji wengine wa Serikali wakafanikisha mikataba mibovu ya madini bila ridhaa ya Rais.
----
Spika wa Bunge, Job Ndugai amewakumbusha wabunge wa upinzani wanaotaka marais wastaafu washtakiwe kuhusu sakata la mchanga wa madini, wakumbuke wanao mawaziri wakuu wastaafu wawili ambao watahusika pia.
Ndugai amesema hayo leo (Jumanne) bungeni baada ya mchango wa Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali kusema haiwezekani mawaziri na watendaji wengine wa Serikali wakafanikisha mikataba mibovu ya madini bila ridhaa ya Rais.
"Haiwezekani mzee wangu (Andrew) Chenge na (Nazir) Karamagi walipitisha mikataba hiyo bila Rais aliyekuwapo kufahamu. Kinga ya Rais kushtakiwa iondolewe ili wahojiwe," amesema Lijualikali.
Baada ya hoja hiyo ya Lijualikali inayofanana na ya Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Ndugai aliwakumbusha juu ya mawaziri wastaafu walionao kwenye chama chao.
"Mabadiliko mnayoyataka yakipitishwa na viongozi mlionao wakikamatwa msije mkalalamika tena," amesemaNdugai.
Chanzo: Mwananchi