Ni hatua gani zinastahili kuchukuliwa endapo Rais atavunja Katiba kwa kukusudia au kutokukusudia?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Nimekuwa nikijiuliza sana hili swali, kwamba ikiwa iko wazi na dhahiri kabisa kwamba raisi wa Tanzania anaekuwa madarakani, anaamua kwa makusudi na huku akijua hilo, au kwa kushauriwa vibaya, au kwa kutoelewa, anavunja Katiba ya Tanzania (yaani kufanya uamuzi au kuchukua hatua inayoenda kinyume na Katiba ya Tanzania).

Nauliza hivi kwa sababu ninaelewa kwamba huwezi kumshitaki Rais wa Tanzania Mahakamani, iwe yupo madarakani au amemaliza muda wake.

Ili kuelewa suala lililopo labda tuchukue extreme case. Kwa mfano Raisi anaamua kuwauzia Kenya Mlima Kilimanjaro, hakuna tunaloweza kufanya itabidi tusubiri hadi uchaguzi ili tumtoe kwa kura?

Ningeomba wale wenye ufahamu mzuri wa sheria au Katiba ya Tanzania wasaidie kujibu maswali haya hapa chini;
  1. Je, Tanzania tuna utaratibu wowote wa kisheria wa kumwajibisha Rais anaetenda kinyume na Katiba ya nchi kwa makusudi au kwa kutojua akiwa bado madarakani?
  2. Je chama chake kinawezaje kumwajibisha ikiwa raisi ndio anakuwa pia mwenyekiti wa chama chake?
  3. Je kama Rais anavunja katiba kimakusudi bado tunalazimika kusubiri hadi uchaguzi mkuu ili wananchi ndio waamue?
  4. Na je, ni halali chama cha siasa kuteua mtu kuwa mgombea wa Urais ikiwa kuna uthibitisho kwamba akiwa madarakani kama Rais katika awamu inayoisha alikuwa akivunja katiba?
  5. Je unaweza kumwekea pingamizi Rais anaemaliza awamu moja kugombea tena kwa sababu kuna uthibitisho kwamba akiwa Rais alivunja Katiba na hivyo hastahili kugombea uraisi kwa awamu nyingine?
  6. Je kuna uhalali wa kumwondoa Rais madarakani kwa nguvu (yaani mapinduzi) badala ya kungojea uchaguzi mwingine ikiwa anathibitika kuvunja Katiba mara kwa mara na chama chake hakina namna ya kumwajibisha, au hakuna utaratibu wa kidemokrasia unaowezesha Rais aondolewe madarakani?
 
Wana JF nitafutieni Pascal Mayalla, Tundu Lissu nk waje huku watuongoze
 
Kwa katiba iliyopo hatumfanyi kitu,

Ni wale jamaa wasioonekana ndio wanaweza tuleta kati wakitaka!!!
Basi tuna tatizo kubwa sana. Labda hata badala ya kudai Katiba yote ibadilishwe, linalotakiwa kubadilishwa ni hili jambo moja - kuhakikisha raisi anawajibishwa ikiwa atevunja Katiba, na kuwekewa pingamizi la kugombea uraisi kwa mara nyingine ikiwa kuna uthibitisho kuwa alivunja katiba katika utendaji wake akiwa raisi
 
Nimekuwa nikijiuliza sana hili swali, kwamba ikiwa iko wazi na dhahiri kabisa kwamba raisi wa Tanzania anaekuwa madarakani, anaamua kwa makusudi na huku akijua hilo, au kwa kushauriwa vibaya, au kwa kutoelewa, anavunja Katiba ya Tanzania (yaani kufanya uamuzi au kuchukua hatua inayoenda kinyume na Katiba ya Tanzania)

Nauliza hivi kwa sababu ninaelewa kwamba huwezi kumshitaki raisi wa Tanzania mahakamani, iwe yupo madarakani au amemaliza muda wake.

Ningeomba wale wenye ufahamu mzuri wa sheria au Katiba ya Tanzania wasaidie kujibu maswali haya hapa chini;
  1. Je, Tanzania tuna utaratibu wowote wa kisheria wa kumwajibisha raisi anaetenda kinyume na Katiba ya nchi kwa makusudi au kwa kutojua akiwa bado madarakani?
  2. Je chama chake kinawezaje kumwajibisha ikiwa raisi ndio anakuwa pia mwenyekiti wa chama chake?
  3. Je kama raisi anavunja katiba kimakusudi bado tunalazimika kusubiri hadi uchaguzi mkuu ili wananchi ndio waamue?
  4. Na je, ni halali chama cha siasa kuteua mtu kuwa mgombea wa uraisi ikiwa kuna uthibitisho kwamba akiwa madarakani kama raisi katika awamu inayoisha alikuwa akivunja katiba?
  5. Je unaweza kumwekea pingamizi raisi anaemaliza awamu moja kugombea tena kwa sababu kuna uthibitisho kwamba akiwa raisi alivunja Katiba na hivyo hastahili kugombea uraisi kwa awamu nyingine?
  6. Je kuna uhalali wa kumwondoa raisi madarakani kwa nguvu (yaani mapinduzi) badala ya kungojea uchaguzi mwingine ikiwa anathibitika kuvunja Katiba mara kwa mara na chama chake hakina namna ya kumwajibisha, au hakuna utaratibu wa kidemokrasia unaowezesha raisi aondolewe madarakani?
Tuandamane apigwe chini
 
Hii Katiba imeandikwa na Chama chake ndio maana wanaidharau wanaheshimu zaidi Ilani yao.

Tukikimbilia Mahakamani Majaji wanapigiwa Simu sasa tufante nini?
 
Nimekuwa nikijiuliza sana hili swali, kwamba ikiwa iko wazi na dhahiri kabisa kwamba raisi wa Tanzania anaekuwa madarakani, anaamua kwa makusudi na huku akijua hilo, au kwa kushauriwa vibaya, au kwa kutoelewa, anavunja Katiba ya Tanzania (yaani kufanya uamuzi au kuchukua hatua inayoenda kinyume na Katiba ya Tanzania)

Nauliza hivi kwa sababu ninaelewa kwamba huwezi kumshitaki raisi wa Tanzania mahakamani, iwe yupo madarakani au amemaliza muda wake.

Ningeomba wale wenye ufahamu mzuri wa sheria au Katiba ya Tanzania wasaidie kujibu maswali haya hapa chini;
  1. Je, Tanzania tuna utaratibu wowote wa kisheria wa kumwajibisha raisi anaetenda kinyume na Katiba ya nchi kwa makusudi au kwa kutojua akiwa bado madarakani?
  2. Je chama chake kinawezaje kumwajibisha ikiwa raisi ndio anakuwa pia mwenyekiti wa chama chake?
  3. Je kama raisi anavunja katiba kimakusudi bado tunalazimika kusubiri hadi uchaguzi mkuu ili wananchi ndio waamue?
  4. Na je, ni halali chama cha siasa kuteua mtu kuwa mgombea wa uraisi ikiwa kuna uthibitisho kwamba akiwa madarakani kama raisi katika awamu inayoisha alikuwa akivunja katiba?
  5. Je unaweza kumwekea pingamizi raisi anaemaliza awamu moja kugombea tena kwa sababu kuna uthibitisho kwamba akiwa raisi alivunja Katiba na hivyo hastahili kugombea uraisi kwa awamu nyingine?
  6. Je kuna uhalali wa kumwondoa raisi madarakani kwa nguvu (yaani mapinduzi) badala ya kungojea uchaguzi mwingine ikiwa anathibitika kuvunja Katiba mara kwa mara na chama chake hakina namna ya kumwajibisha, au hakuna utaratibu wa kidemokrasia unaowezesha raisi aondolewe madarakani?
Kwani Samia kavunja Katiba? Hebu funguka
 
Basi tuna tatizo kubwa sana. Labda hata badala ya kudai Katiba yote ibadilishwe, linalotakiwa kubadilishwa ni hili jambo moja - kuhakikisha raisi anawajibishwa ikiwa atevunja Katiba, na kuwekewa pingamizi la kugombea uraisi kwa mara nyingine ikiwa kuna uthibitisho kuwa alivunja katiba katika utendaji wake akiwa raisi
Sawa ila tumwambie nani Ili atusikie
 
Kwa vile Rais wa Tanzania ni mungumtu akizingua ni kumshitakia kwa mizimu aondoshwe kwenye uso wa dunia.
 
Nimekuwa nikijiuliza sana hili swali, kwamba ikiwa iko wazi na dhahiri kabisa kwamba raisi wa Tanzania anaekuwa madarakani, anaamua kwa makusudi na huku akijua hilo, au kwa kushauriwa vibaya, au kwa kutoelewa, anavunja Katiba ya Tanzania (yaani kufanya uamuzi au kuchukua hatua inayoenda kinyume na Katiba ya Tanzania)

Nauliza hivi kwa sababu ninaelewa kwamba huwezi kumshitaki raisi wa Tanzania mahakamani, iwe yupo madarakani au amemaliza muda wake.

Ningeomba wale wenye ufahamu mzuri wa sheria au Katiba ya Tanzania wasaidie kujibu maswali haya hapa chini;
  1. Je, Tanzania tuna utaratibu wowote wa kisheria wa kumwajibisha raisi anaetenda kinyume na Katiba ya nchi kwa makusudi au kwa kutojua akiwa bado madarakani?
  2. Je chama chake kinawezaje kumwajibisha ikiwa raisi ndio anakuwa pia mwenyekiti wa chama chake?
  3. Je kama raisi anavunja katiba kimakusudi bado tunalazimika kusubiri hadi uchaguzi mkuu ili wananchi ndio waamue?
  4. Na je, ni halali chama cha siasa kuteua mtu kuwa mgombea wa uraisi ikiwa kuna uthibitisho kwamba akiwa madarakani kama raisi katika awamu inayoisha alikuwa akivunja katiba?
  5. Je unaweza kumwekea pingamizi raisi anaemaliza awamu moja kugombea tena kwa sababu kuna uthibitisho kwamba akiwa raisi alivunja Katiba na hivyo hastahili kugombea uraisi kwa awamu nyingine?
  6. Je kuna uhalali wa kumwondoa raisi madarakani kwa nguvu (yaani mapinduzi) badala ya kungojea uchaguzi mwingine ikiwa anathibitika kuvunja Katiba mara kwa mara na chama chake hakina namna ya kumwajibisha, au hakuna utaratibu wa kidemokrasia unaowezesha raisi aondolewe madarakani?
Katiba hii tuliyonayo haijatoa ulinzi kwa Katiba.
Unakuta mambo yamewekwa kwa ujumla jumla halafu unakutana na kigingi huwezi kumshtaki rais.....
Yaani hatuna jinsi zaidi tu ya kuanika namna alivyovunja katiba hadharani kisha twende tukapange foleni ya umeme na sukari
 
Katiba ilitayarishwa katika assumption kwamba maraisi wote wa Tanzania wangekuwa wazalendo wa aina ya Nyerere!
 
Mkuu
Katiba ilitengenezwa na vipofu wa sheria, Haki na Wajibu.

Assumption huwa inapewa nguvu kwenye nyumba za ibada. Lakini kwenye madaraka ni aibu kubwa kuweka madhania
 
Hapana mkuu. Kufanya assumption ni jambo la kawaida katika maisha, japo mara nyingine assumption tunazofanya zinatuletea matatizo. Hata unapopanda basi usafiri, unafanya assumption utafika salama, na dereva atakuwa mwangalifu japo humfahamu. Lakini mara nyingine haiwi hivyo. Ukienda hotelini huenda inzi waliingia kwenye chai wakaopolewa na ukaletewa chai. Wewe unafanya assumption hakuna kitu kama hicho.

Mara nyingine tunafanya assumption kuwa wake zetu ni waaminifu, na watoto tulionao tulizaa sisi. Lakini mara nyingine hili sio kweli. Je utamlaumu mtu kwa nini ali-assume watoto wake ni wake kweli?

Kwa hiyo kufanya assumption ni sehemu ya maisha yetu, hata kama hizo assumption haziko sahihi
 
Back
Top Bottom