Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,340
- 51,900
KWA WALIOTUNGA SHERIA HII; KAMA RAIS NI MZALENDO NA MUADILIFU NI SABABU GANI IKAWEPO KINGA YA KUTOSHTAKIWA?
Anaandika, Robert Heriel
Moja ya sheria inayonifanya nione nchi yetu bado hatuko serious ni sheria inayomkingia Kifua Rais KUTOSHTAKIWA. Kwa kweli sheria Hii sio tuu ni ya ajabu Bali ni sheria iliyolenga kumfanya Rais aabudiwe, awe mungu mtakatifu, Wakati kimsingi sivyo.
Hakuna sababu hata Moja yenye mashiko inayoifanya sheria hiyo iwe ya maana. Ati Mimi Robert Heriel kitendo tuu cha kuwa Rais basi sitashtakiwa. Huo sio uungwana. Hiyo sio sheria za kiungwana.
Rais kama binadamu wengine anaweza kufanya Makosa na uhalifu kama wanavyofanya wengine. Ni muhimu sheria Hii ikaondolewa.
Hatutaki kuchagua Rais ambaye atakuwa na kinga akifanya uhalifu au Makosa. Hilo hatutaki. Ninapotumia wingi ninamaanisha Watu wote wenye fikra na mtazamo kama wangu.
Kitendo cha Sheria hiyo kumkinga Rais asistakiwe automatically kinawakinga na vipenzi wa Rais husika. Ikiwa Rais ambaye ni Kiongozi wa nchi sheria inamlinda basi kimantiki ni kuwa sheria hiyo itawalinda na vipenzi wa Rais.
Sheria hiyo pia inawapa ugumu Mahakimu na majaji kufanya kazi Yao vizuri hasa katika kudili na kesi Kwa baadhi ya Watu hasa vipenzi wa Rais. Hii itafanya Na kuwaingiza Mahakimu na majaji katika Wakati mgumu katika kutoa Haki pindi wafanyapo kazi zao.
Sheria hii sio nzuri Kabisa. Kwamba, ili Rais awe comfortable akiongoza bila kuhofia Jambo lolote. Kwa nini hiyo comfortable inayotafutwa na sheria hiyo iwe katika kumlinda Rais endapo atageuka kuwa Mhalifu?
Sheria hiyo tufanye Mpango ifutwe. Rais au kiongozi atakayekuwa madarakani ambaye ataifuta sheria hiyo basi kuna kila sababu ya kumuita kiongozi huyo ni MZALENDO na MUADILIFU.
Uadilifu ni pamoja na kuwajibika pale unapofanya Makosa.
Ikiwa Rais atakuwa tayari kushtakiwa endapo atafanya uhalifu na Makosa na akabadilisha hiyo sheria basi huyo Rais atakuwa anamaanisha Uzalendo halisi.
Kumtenga Rais na Mkono wa sheria ni kuihujumu nchi na taifa. Ni kuligawa taifa na kuweka kundi la Watawala na watawaliwa. Watawala kamwe hawatafungwa Kwa sababu watalindwa na Rais. Hiyo itafanya kila kiongozi kujipendekeza Kwa Rais hata kama Rais anapuyanga. Kwani kujipendekeza Kwa Rais NI kujiwekea na wewe kinga ya KUTOSHTAKIWA.
Acha nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam