Kokudo, pole sana kwa kukoseshwa amani na watu haata huwajui. Pengine ulosema yana ukweli au la, lakini kwanini kama umeligundua hilo usitafute njia nyingine kama kuwapotezea, then si lazima uwachangie post zao, waache wachangiane wao kwa wao then changia wale wanaokuchangia. Pia unaweza kutafuta friends humu ambao mtakua mnachat wanakuchangia pia, mfano mimi hua siangalii na mchangia nani, so hata zangu hua siangalii nani kachangia nani kaacha na sina mpango wa kufanya watu flani wanichangie Big No huo ni utumwa, ila yeyote atakae jiskia aspo jiskia anachapa mwendo mi ujumbe unakua umefika. Tatizo lako wewe unadhani watu flani wakikuchangia ndo utakua juu hakuna super star hapa wala nini au unataka watu wakuulize ulikua wapi au sijui nini, kwani wanakujua? Au nirafiki zako kwani? Kwanini uugue vidonda vya tumbo kwa vijimambo vidogo hivi jifunze kutafuta amani na watu wote. Kumbuka ni watu kama wewe, please inaonyesha umeumia sana mkuu, wapo watu mmojawao ni mimi wanachangia bila kujali wala kubagua. Nadhani umenielewa leta post tutakuchangia. Si lazima nani na nani wewe ndo unajichanganya.