#COVID19 Gerson Msigwa: Watanzania wawasikilize wataalamu, chanjo za COVID-19 zinahakikiwa na TMDA na Mkemia Mkuu

Shida ni pale wataalam hao hao na yeye mwenyewe akiwa msemaji wa Ikulu walishindwa kutuonyesha utaalam wao awamu ya tano wakaacha watu wapotoshwe na kushindwa kujua nani anasema ukweli na yupi anatupotosha. walipoteza sifa ya kuitwa wataalam.

Mawaziri wa afya na naibu wake ni hawa hawa walikua wanatembez na mabeseni ya mvuke kuelekeza namna ya kujifukiza. Pia wakaja na dawa za kienyeji huku wakisisitiza chanjo haziko salama, hawaoni wanawachanganya wananchi?
 
Wengi tumeshituka kusikia hii
Tunadanganyana, hakuna mtaalamu wa Tanzania anaweza ku-reverse engineer akatuhakikishia usalama. India walishindwa wakaomba wapewe contents tu Ili watengeneze ya kwao. Sijui waliishia wapi
 
Gwajima anapaswa atoke hadharani awaombe Radhi watanzania. vinginevyo atawajibika kwa kauli zake za upotoshaji wakati Taifa lipo ktk mapambano ya janga hili la korona.
 
Tunadanganyana,hakuna mtaalamu wa Tanzania anaweza ku-reverse engineer akatuhakikishia usalama...India walishindwa wakaomba wapewe contents tu Ili watengeneze ya kwao..Sijui waliishia wapi
Tunaishi katika nyakati za hatari sana, eti Msigwa ndiyo mshawishi wa serikali? Ukimtazama uso anaonekana wazi ni chumia tumbo
 
Huyu Msigwa asijibu Mambo asiyoyaelewa.

Kwanza unajua consent form hutumika kwa procedure zipi hosiptali? Je umeshawahi kujaza consent form kwenye chanjo za surua, tetenasi, polio?

Unadai wataalamu wanahakiki? Unapangaje siku ya kuzindua wakati uhakiki bado? Je Kama hazifai mtawarudishia?

Wanauwezo wa kuhakiki long term side effects kuanzia miaka 5 nazaidi kwenye chanjo ambayo haikuchukua hata mwaka kuigundua?

Unafikiri kuhakiki ni swala la siku mbili?

Mzigo huu ni mzito kwako,mwache aliyerikoroga alinywe,dhamana ya Watanzania na damu zao zitatakwa mikononi mwake.
Mungu yupo na atajua tu hata Kama hajui.
 
Hii hoja dhaifu sana, kwa hiyo kipindi cha magufuli hao TMDA hawakuepo? Dozi 1000,000 ndo wanafanyia utafiti kwa siku 4?
 
Kwakweli mwili wangu si wa mwanasesere nitasubiri kwanza na kwa bahati waswahili walishasema harakaharaka haina baraka na mwenda pole hajikwai na akitokea kaumia anaumia kidogo tu! Hivyo wacha tusubiri kwa kuwa mvumilivu hura mbivu.

Lakini kinachonifurahisha kwa chanjo hii sioni mawaziri wakibeba familia zao nao wakijitoa kuhakikisha wanachanjwa kwanza kama tulivyozoea.
 
Hivi karibuni kumeibuka malumbano na watu wa kawaida kama Dewji na wana siasa kama January nk wakimshtumu Gwajima kwa kuuliza au kutaka ufafanuzi wa jambo la uviko kisayansi ingawa yeye sio mwana sayansi au kwa kuwa wana sayansi wamekosa uthubutu wa kuuliza au kuliongelea.

Ni imani yangu iwe mtu wa kawaida, mwana siasa, mwana sayansi au Chama dola kumuelimisha Gwajima na Watanzania wote kwa jumla kitaalamu na kwa ustaarabu jambo hilo na sio vitisho ndio tutajenga nchi , demokrasia na elimu ya Watanzania.
 
Je, tuna Lab za kisasa kabisa za kupima ubora wa chanjo nchini.
Kwanza, ubora wa chanjo unapimwaje? Ni kwamba achanjwe mtu au mnyama (panya), halafu ukae siku, miezi, miaka - ndipo ujue hiyo chanjo inafaa. Sasa chanjo inaletwa, mara tu waganga kwenye zahanat zeu wameisha jua hii chanjo ni sawa sawa? Na sisi tuwaamini! Uongo mwingine bwana!
 
Back
Top Bottom