#COVID19 Serikali: Waliopata chanjo ya UVIKO-19 Tanzania ni asilimia 9.81

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
FOhwvMLWUAMCHMH.png

Kauli za Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati akipokea chanjo aina ya Sinovac dozi milioni moja kutoka Serikali ya Uturuki, leo Machi 23, 2022.

"Kwa niaba ya Serikali chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunaishukuru Serikali ya Uturuki kwa kupokea ufadhili wa chanjo aina ya Sinovac, jumla ya dozi 1,000,000 kati ya dozi 4,000,000 zinazotarajiwa kupokelewa kwa awamu nne.

"Chanjo hizi zinatarajiwa kuchanja watu 2,000,000. Nichukue fursa hii kuishukuru Serikali ya Uturuki kwa kuwezesha upatikanaji wa chanjo hizi Hii ni mara ya kwanza kwa nchi yetu kuanza kutumia chanjo aina ya Sinovac tokea zoezi la uchanjaji lilipozinduliwa rasmi na Rais Samia

"Serikali itaendelea kutoa Chanjo dhidi ya UVIKO-19 katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma za Afya hapa nchini kwa mujibu wa miongozo iliyopo zikiwemo huduma za mkoba na tembezi.

"Hadi kufikia tarehe 21 Marchi, 2022 jumla ya watu 3,016,551 wamepata chanjo kamili kati ya watu milioni 30,740,928 wenye umri wa miaka 18 na kuendelea ikiwa ni sawa na asilimia 9.81.

"Ninachukua fursa hii kuendelea kuwasisitiza viongozi na watendaji wa ngazi zote kuendelea kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea kuhimizwa kwenda kwenye vituo vya huduma za afya ili wakapate elimu kuhusu umuhimu wa chanjo na kuchanja.

"Ninatoa rai kwa Wakuu wa Mikoa yote nchini kuongeza juhudi za uhamasishaji jamii ili kuongeza kiwango cha utoaji wa chanjo na kuhimiza wananchi wakapate chanjo kama inavyoshauriwa na wataalamu. Aidha, ninawahamasisha watoa huduma za afya wao wenyewe wachanje.

"Ninawaelekeza wataalamu kujumuisha huduma za chanjo ya UVIKO 19 sambamba na huduma nyinginezo za afya zikiwemo huduma za uzazi wa mpango, VVU, tohara,macho, lishe,na kifua kikuu.Ninawaelekeza Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kuendelea kuongeza vituo vya kutolea Chanjo.

"Niendelee, kuwasihi Wananchi, wajitokeze kwa wingi kwenda kupata chanjo na waendelee kuchukua tahadhari zote za kinga dhidi ya UVIKO-19 zikiwemo kunawa mikono na maji tiririka na sabuni au kutumia vipukusi, kuvaa barakoa katika maeneo yenye misongamano, kuepuka misongamano.

"Nitumie fursa kuwathibishia wananchi kuwa chanjo hizi ziko salama na mpaka sasa chanjo ndiyo njia pekee iliyothibika kupunguza madhara yatokanayo na janga hili la kidunia. Pia, nishukuru nchi mbalimbali ambazo zimeendelea kutupatia msaada wa chanjo za UVIKO-19.”

FOhwiYOXsAY4Hqg.png

Chanzo: Wizara ya Afya
chanjo 2.png

Tanzania hadi sasa imepokea Dose za Covid-19 kiasi cha 6.37 Milioni

Watu waliochanja chanjo ya Covid-19 Tanzania: 2.78 Milioni

Watu waliopata chanjo ni sawa na Asilimia 4.7 ya Wanaotakiwa Kuchanjwa

Chanzo cha Takwimu: Our World in Data
 
Tanzania kazi tunayo. Wenye corona wameshahama kutoka corona wako katika mkamkati mwengine wa vita vya kutengenezwa hapo Ukraine.

Hangaikeni na chemsheni Bongo zenu mjue mbinu za kupambana na athari zilizoko na zijazo ambazo ni kubwa zinazotokana na vita hii inayoendelea Ukraine.
 
Hapo ndio utamwelewa Mwendazake.

Wazungu wanatupenda kiasi hicho kutuletea chanjo za bure
 
Ina maana anashindwa kuwasoma watanzania kweli anazidi kuagiza hayo machanjo..
 
Unapinga picha bila kuvaa barakoa...hiyo kampeni ikoje?

Haijakaa sawa Kwa kweli.
 
Back
Top Bottom