#COVID19 Gerson Msigwa: Watanzania wawasikilize wataalamu, chanjo za COVID-19 zinahakikiwa na TMDA na Mkemia Mkuu

beijing_07

Senior Member
Jul 19, 2021
113
145
Mtangazaji: Tuanze na suala la chanjo, tumepata taarifa kesho Rais Samia Suluhu atazindua utaratibu wa chanjo na yeye atachanjwa. Utaratibu utakuwaje kama umeshawekwa na Serikali?

Msigwa: Baada ya kuwasili dozi za chanjo zaidi ya milioni 1, kesho asubuhi mheshimiwa Rais atazindua zoezi la chanjo na atapokea chanjo yake kesho. Baada ya hapo Serikali imeandaa utaratibu ambapo katika kipindi cha kati ya siku saba hadi kumi utatolewa utaratibu kwa ajili ya watanzania hasa makundi ambayo yamepewa kipaumbele kwa maana ya wafanyakazi wanaofanya kazi katika mazingira hatarishi wa Afya, watu wenye umri mkubwa na mikoa kama kumi ambayo imeainishwa, watanzania watapokea chanjo kwa hiari kama ambavyo serikali imetangaza

Mtangazaji: Moja ya vitu vinavyotengeneza imani kwa wananchi kuhusiana na hizi chanjo kuona viongozi wao wakiwa wanachanjwa, utaratibu wa kuonyesha utakuwepo?

Msigwa: Hakuna kificho, ni zoezi la wazi na ndio maana kesho mheshimiwa Rais analindua. Wakati mwingine ni vizuri kufanya hivi kiongozi uonyese kwa mfano ili na wananchi wote wapate imani.

Mtangazaji: Kuna fomu zinasambaa zina 'Disclaime' kwamba serikali haitawajibika kama kutakuwa na madhara kuhusiana na hizi chanjo. Hauoni itasababisha watu kutokuwa na imani?

Msigwa: Hili jambo linashangaza sana, sio chanjo hizi tu, ni utaratibu wa kimatibabu mtu kusema napokea matibabu haya na endapo kutatokea madhara ni juu yangu. Zungumza na madaktari, huu ni utaratibu wa kawaida na hata katika hizi chanjo ni hivyo hivyo.

Mtangazaji: Tukiwa hapo kwenye suala la Imani, baadhi ya watu wengine wakiwa maarufu wanatoa hoja kuhusiana na hofu yao kuhusiana na hizi chanjo. Serikali hamuoni kuna haja ya kujibu hoja hizo kutengeneza imani kwa wananchi zaidi.

Msigwa: Kwanza niwatoe hofu wananchi, wasiwe na wasiwasi, wataalamu wetu wanafanya kazi kubwa huhakikisha hizi chanjo zinahakikiwa na niwaeleze tu, chanjo zikitoka huko zinakotoka, zikifika Tanzania Wizara ya Afya imeandaa utaratibu kupitia TMDA na tuna ofisi ya mkemia mkuu wa Serikali ambao wanahakiki kwanza zile chanjo na baada ya hapo zinakwenda kwenye matumizi na ndio maana hizi chanjo zimekuja tarehe 24 lakini kumekuwa na muda kidogo, kuna shughuli za kitaalamu, kwahiyo wataalamu wetu wanafanya kazi kubwa kuhakikisha wanazihakiki hizi chanjo na watanzania wanapata chanjo ambayo ni bora.

Uko sahihi kwamba kumekuwa na maneno mengi, Rai yangu na msimamo wa Serikali, kwa wakati huu Watanzania wawasikilize wataalamu, hiyo ndio njia ambayo sisi Watanzania tumeamua kuichukua. Wataalamu wetu tumewasomesha, wanafahamu mambo mengi na nchi ina wataalamu wana uwezo mkubwa sana.

Tanzania tutakuwa watu wa ajabu sana tukiwaacha wataalamu wetu, tumewasomesha, tumewakabidhi vituo vya afya, hospitali, zahanati, wanatutibu magonjwa mengi, wanatoa chanjo nyingi sio hii, leo hii tusije kuwaamini kwenye hili, nadhani hapana.

==========

Msemaji mkuu wa serikali, Gerson Msigwa yuko (Dodoma) akihojiwa na mtangazaji wa azamtv, Godluck Paul kutoka Dar muda huu kwenye chaneli ya UTV kwenye kipindi cha morning trumpet.

Huyu jamaa yuko smart sana aiseee anajibu kwa kujiamini sana kila swali.
 
Ushawishi wa JPM kwa tahadhari chanjo uliwaingia Watanzania ipo kazi kubwa elimu.
Alichofanya JPM Mungu 'anamuona'. Ilikuwa ni kazi ya kupandikiza ujinga kwa wananchi. Hatukatai kuwepo umakini, lakini sio kupinga tu bila hoja zenya mashiko. Haya chanjo za 'wazungu' hutaki, basi tengeneza zako. Huwezi! Ujinga unapoambatana na umaskini ni laana!
 
Msigwa: Kwanza niwatoe hofu wananchi, wasiwe na wasiwasi, wataalamu wetu wanafanya kazi kubwa huhakikisha hizi chanjo zinahakikiwa na niwaeleze tu, chanjo zikitoka huko zinakotoka, zikifika Tanzania Wizara ya Afya imeandaa utaratibu kupitia TMDA na tuna ofisi ya mkemia mkuu wa Serikali ambao wanahakiki kwanza zile chanjo na baada ya hapo zinakwenda kwenye matumizi na ndio maana hizi chanjo zimekuja tarehe 24 lakini kumekuwa na muda kidogo, kuna shughuli za kitaalamu, kwahiyo wataalamu wetu wanafanya kazi kubwa kuhakikisha wanazihakiki hizi chanjo na watanzania wanapata chanjo ambayo ni bora.
Hao wataalamu wameshindwa kitengeneza za kwetu, wanawezaje kuhakiki za wengine?
 
Alichofanya JPM Mungu 'anamuona'. Ilikuwa ni kazi ya kupandikiza ujinga kwa wananchi. Hatukatai kuwepo umakini, lakini sio kupinga tu bila hoja zenya mashiko. Haya chanjo za 'wazungu' hutaki, basi tengeneza zako. Huwezi! Ujinga unapoambatana na umaskini ni laana!
Maoni yako ni nini, mkuu tufate chanjo au tuachane na chanjo?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom