Wizara ya Afya kutoa Chanjo ya Polio kwenye Mikoa inayopakana na nchi jirani

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Zaidi ya watoto 402,000 wa mkoa wa Songwe wanatarajiwa kupata chanjo ya polio katika zoezi linalotarajia kuanza Septemba 21 hadi Septemba 24 mwaka huu.

Ofisa Program Wizara ya Afya, Idara ya Kinga, Penford Joely amesema hayo alipozungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusu kampeni ya kuanza kutoa chanjo ya Polio kufuatia baadhi ya nchi jirani kubainika kuwa na ugonjwa unaosababishwa na virusi vya ugonjwa huo.

Joely amesema zoezi la utoaji wa chanjo hiyo ni kwa watoto wenye umri wa kuanzia mwaka 0 hadi miaka 8.

Aidha amebainisha mikoa mingine itakayohusika na zoezi hilo kuwa ni pamoja na Mbeya, Katavi, Rukwa, Kagera na Kigoma ambayo imepakana na nchi jirani.

Ofisa huyo amesema ni muhimu wazazi kuhakikisha wanajitokeza kuwapeleka watoto wao katika vituo vya afya kupata chanjo ili kuepusha madhara yanayoweza kuwapata ukiwemo ulemavu wa kudumu na kifo.

Joely amesema Chanjo inatolewa bila malipo yoyote ambapo ametoa wito Kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa wataalamu wa afya watakaopita kwenye kaya zao.

Naye mratibu wa elimu ya afya kwa jamii mkoani hapa, Monica Munisi amewaomba viongozi wa dini, serikali mitaa, viongozi wa Mila na wataalamu wa tiba mbadala kushiriki katika utoaji wa elimu ya chanjo.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom