#COVID19 Gerson Msigwa: Watanzania wawasikilize wataalamu, chanjo za COVID-19 zinahakikiwa na TMDA na Mkemia Mkuu

Yaani natamani comment yako hii iwekwe kwenye taa za barabarani ili kila mtu asome. Wajinga Sana hawa waumini wa jiweism.
🤣🤣Mkuu wangu we acha tu.....

Unamkuta mtu ZWAZWA anawaaminisha ujinga na upumbavu MAFULAFULA na kuzidi kuwafanya kuwa MAHOBOBO 🤣

#TujiandaeKuchanjwa
#ChanjoNiBoraKulikoTiba
 
Sister jamaa ameshaikataa hii kitu kuwa ni fake, ameikataa kwenye akaunti yake insta. Watu siku hizi wanatengeneza sana hizi, ni vyema kabla hujaposti uwe unatembelea kwenye pages official za wahusika
Nilitaka kuwashauri Wizara ya Afya watengeneze App itakayoandaliwa na wenye uzoefu wa Public Health kuelimisha wananchi. Si kwa chanjo ya Covid tu bali elimu ya afya kwa ujumla. Mara ninakutana na hii kitu.
 
Kama kweli kuna consent forms waandike kwa kiswahili wengi wapate kuelewa watakacho saini
 
Iko wazi sana kuchanjwa ni hiyari ya mtu.Ukiona kwamba haukubaliani na mkataba huo japo sina uhakika nao huu mkataba then unaacha
Acha kwa manufaa unayoyajua,ila chanja kwa faida yako na taifa,ukichanja utanilinda na mwingine,usipochanja unatuweka wote kama taifa katika hatari.
 
Mtangazaji: Tuanze na suala la chanjo, tumepata taarifa kesho Rais Samia Suluhu atazindua utaratibu wa chanjo na yeye atachanjwa. Utaratibu utakuwaje kama umeshawekwa na Serikali?

Msigwa: Baada ya kuwasili dozi za chanjo zaidi ya milioni 1, kesho asubuhi mheshimiwa Rais atazindua zoezi la chanjo na atapokea chanjo yake kesho. Baada ya hapo Serikali imeandaa utaratibu ambapo katika kipindi cha kati ya siku saba hadi kumi utatolewa utaratibu kwa ajili ya watanzania hasa makundi ambayo yamepewa kipaumbele kwa maana ya wafanyakazi wanaofanya kazi katika mazingira hatarishi wa Afya, watu wenye umri mkubwa na mikoa kama kumi ambayo imeainishwa, watanzania watapokea chanjo kwa hiari kama ambavyo serikali imetangaza

Mtangazaji: Moja ya vitu vinavyotengeneza imani kwa wananchi kuhusiana na hizi chanjo kuona viongozi wao wakiwa wanachanjwa, utaratibu wa kuonyesha utakuwepo?

Msigwa: Hakuna kificho, ni zoezi la wazi na ndio maana kesho mheshimiwa Rais analindua. Wakati mwingine ni vizuri kufanya hivi kiongozi uonyese kwa mfano ili na wananchi wote wapate imani.

Mtangazaji: Kuna fomu zinasambaa zina 'Disclaime' kwamba serikali haitawajibika kama kutakuwa na madhara kuhusiana na hizi chanjo. Hauoni itasababisha watu kutokuwa na imani?

Msigwa: Hili jambo linashangaza sana, sio chanjo hizi tu, ni utaratibu wa kimatibabu mtu kusema napokea matibabu haya na endapo kutatokea madhara ni juu yangu. Zungumza na madaktari, huu ni utaratibu wa kawaida na hata katika hizi chanjo ni hivyo hivyo.

Mtangazaji: Tukiwa hapo kwenye suala la Imani, baadhi ya watu wengine wakiwa maarufu wanatoa hoja kuhusiana na hofu yao kuhusiana na hizi chanjo. Serikali hamuoni kuna haja ya kujibu hoja hizo kutengeneza imani kwa wananchi zaidi.

Msigwa: Kwanza niwatoe hofu wananchi, wasiwe na wasiwasi, wataalamu wetu wanafanya kazi kubwa huhakikisha hizi chanjo zinahakikiwa na niwaeleze tu, chanjo zikitoka huko zinakotoka, zikifika Tanzania Wizara ya Afya imeandaa utaratibu kupitia TMDA na tuna ofisi ya mkemia mkuu wa Serikali ambao wanahakiki kwanza zile chanjo na baada ya hapo zinakwenda kwenye matumizi na ndio maana hizi chanjo zimekuja tarehe 24 lakini kumekuwa na muda kidogo, kuna shughuli za kitaalamu, kwahiyo wataalamu wetu wanafanya kazi kubwa kuhakikisha wanazihakiki hizi chanjo na watanzania wanapata chanjo ambayo ni bora.

Uko sahihi kwamba kumekuwa na maneno mengi, Rai yangu na msimamo wa Serikali, kwa wakati huu Watanzania wawasikilize wataalamu, hiyo ndio njia ambayo sisi Watanzania tumeamua kuichukua. Wataalamu wetu tumewasomesha, wanafahamu mambo mengi na nchi ina wataalamu wana uwezo mkubwa sana.

Tanzania tutakuwa watu wa ajabu sana tukiwaacha wataalamu wetu, tumewasomesha, tumewakabidhi vituo vya afya, hospitali, zahanati, wanatutibu magonjwa mengi, wanatoa chanjo nyingi sio hii, leo hii tusije kuwaamini kwenye hili, nadhani hapana.

==========

Msemaji mkuu wa serikali, Gerson Msigwa yuko (Dodoma) akihojiwa na mtangazaji wa azamtv, Godluck Paul kutoka Dar muda huu kwenye chaneli ya UTV kwenye kipindi cha morning trumpet.

Huyu jamaa yuko smart sana aiseee anajibu kwa kujiamini sana kila swali.
Hatuna wataalamu, wote wamekuwa wanasiasa. Na wanasiasa hawaaminiki, tumsikilize nani?
 
Back
Top Bottom