Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,816
4,566
1691621322805.png

===

Greatest of all time
Leo ni Sikukuu ya Soka.

Mnyama Mkubwa Mwituni. Simba SC itakuwa ikishuka dimbani kuwakabili Singida FG FC katika dimba la Mkwakwani pale jijini Tanga.

Simba ambayo imesheheni wachezaji mafundi kama vile Onana, Baleke, Kramo, Mwalimu Fabrice Ngoma na wengineo wanatarajiwa kutoa burudani kubwa sana kwa wapenda kandanda nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla mara baada ya butua butua na piga nikupige ya jana.

Singida ambayo imefuzu kucheza kimataifa nayo imesajili wachezaji kadhaa akiwemo Kiyombo, Babu Onyango, Yahaya Mbegu na wengineo wanatarajiwa kuleta ushindani.

Ewe mwana Simba uliyepo Kasulu, Jinja, Makambako, Kisumu, Uyui, Ndola, na mahala popote tegemea mpira mkubwa leo na mechi yenye mvuto.

Mechi itapigwa Saa 1:00 Usiku na itakuwa mubashara kupitia Azam Sports 1HD.

---
Kikosi cha Simba kinachoanza
1691683375530.png

Kikosi cha Singida FG kilichoanza

1691683485586.png

---

Mpira umeanza
04' Bado milango ni migumu bado hawajafungana

05' Singida wanapata goli lakini linakataliwa

40' Bado milango migumu kwa timu zote mbli huku zikishambuliana kwa zamu

45' Mapumziko timu bado hazijafungana

46' Anaingia Ngoma na Bocco wanatoka Kanoute na Baleke

55' Milango bado migumu kwa timu zote mbili

75' Bado hakuna goli

80' Bado timu hazijafungana

90' Zimekamilika na sasa matuta yanafuata.

Wapigaji Singida FG
Andabwile ❌
Tchakei ✅
Kagoma ❌
Abuya ✅

Wapigaji Simba SC
Luis ✅
Saido ✅
Mzamiru ✅
Phiri ✅

Mpira umekwisha Simba ameshinda kwa Penati 4 kwa 2
 
Nadhani Kibu D kama anacheza, kocha aangalie uwezekano wa kumpanga katika viungo watatu wa kati kwa mfumo wa 4-3-3 ,Sababu kibu sio mfungaji mzuri ,sio mpiga pasi za mwisho mzuri ila ni mchezaji anayeweza anzisha shambulizi na kupandisha timu kwa uharaka pindi wanapokaba mpira kutoka timu pinzani .
 
Nadhani Kibu D kama anacheza, kocha aangalie uwezekano wa kumpanga katika viungo watatu wa kati kwa mfumo wa 4-3-3 ,Sababu kibu sio mfungaji mzuri ,sio mpiga pasi za mwisho mzuri ila ni mchezaji anayeweza anzisha shambulizi na kupandisha timu kwa uharaka pindi wanapokaba mpira kutoka timu pinzani .
Kesho mnapigwa vizur tu
 
Back
Top Bottom