FT: Simba SC 1-0 Jamhuri SC | Mapinduzi Cup | New Amaan Complex| Robo Fainali | 08.01.2024

uran

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
7,579
10,811
Match Day

Simba SC Vs Jamhuri SC
Mapinduzi Cup
New Amaan Complex
Robo Fainali
08.01.2024

20240108_142109.jpg

Mchuano huu ni kwa ajili ya mchezo wa soka uliosubiriwa kwa hamu huku robo fainali ya nne ikiendelea leo saa 2:15 Usiku kwa kuwakutanisha Simba SC dhidi ya Jamhuri FC katika Uwanja wa Amaan.

Mchezo muhimu huu unaweza kuamua ni timu ipi itakayopata nafasi ya kutia mguu wake kwenye nusu fainali ya mashindano haya.

Huku baadhi ya timu kama APR na Mlandege tayari zikiwa zimefanikiwa kufika hatua ya nusu fainali, shauku kati ya mashabiki wa soka Tanzania iko juu

Mashabiki kote kwenye visiwa na Tanzania kwa Ujumla wanasubiria kwa hamu matokeo ya mchezo kati ya Simba SC na Jamhuri FC ili kujua ni timu ipi itakayosonga mbele kuingia nusu fainali. Kukutana na Azam FC au Singida FG ambao mechi yao itapigwa mchana wa leo.(nitakujuza matokeo yao pia)

Uwanja wa Amaan umekuwa uwanja wa vita kwa mchezo huu mkali, ambapo ujuzi, mkakati, na azma vitacheza jukumu muhimu katika kuamua mshindi.

Mimi Uran, nitakuwa tayari kukupa updates za mchezo huu kwa ueledi na kwa upana kabisa .

UPDATES ....

Mechi ya Azam vs Singida FG
imemalizika kwa Azam kukubali kichapo cha Goli 2-1.
Screenshot_20240108-182242~2.png


Singida FG anasubiria Mshindi Kati ya Simba na Jamhuri kwa ajili ya mchezo wa Nusu Fainali utakaochezwa Kesho kutwa.

KIKOSI CHA SIMBA KINACHOANZA
1704730676119.png

All the Best Mnyama.
#nguvumoja#

Game Updates...
Mpira Umeanza kwa kasi
Dakika ya 1'
Simba wanafanya shambulizi hatari kabisa hapa langoni mwa Jamhuri.

Dakika 4'
Simba wanapata kona ila haizai matunda hapa.
Bado Simba wanafanya mashambulizi langoni mwa Jamhuri.

Dakika 9'
Simba wanafanya shambulizi jingine kupitia kwa Baleke, linaishia kwenye mikono ya kipa.

Dakika ya 12'
Jamhuri wanapata kona inapigwa inakuwa butu.
mpira Unaendelea...

Dakika ya 14'
Simba wanapata kona.
Inapigwa kona fupi haileti madhara kwa Timu pinzani.

Dakika ya 16'
Kona nyingine kwa Simba bado mpira unaishia kwa mpinzani.

Dakika ya 18'
Mpira umesimama kidogo kuna wachezaji 2 wa Jamhuri waligongana katika juhudi za kuokoa.

Game on...

Dakika ya 20'
Simba wanapata free kick eneo la nje kidogo ya box.
Anaipiga Saidoo
anamtengea Luis Miquisonne anupoteza mpira
Game on...

Dakika ya 22'
Mchezaji wa Jamhuri anapatiwa kadi ya Njano.

Dakika ya 31'
Jamhuri wanapata kona haileti madhara kwa simba.

Simba wanapeleka mashambulizi kwa Jamhuri.

Dakika ya 33'
Jamhuri wanafanya shambulizi Ayoub anasimama vizuri

Dakika ya 40'
Baleke anachezewa rafu kali
Inapigwa free kick na Saidoo inaishia kwenye mikono ya kipa.

Dakika ya 42'
Jamhuri wanapata free Kick.
Nje kidogo ya box, inapigwa inagonga mtambaa panya.
Inakuwa goli kick.

Dakika ya 45'
Nyongeza ni 3'
Game On...
Balekeeeeeee
Goal.
45+2'

Half Time.
Simba 1 - 0 Jamhuri.

Kipindi cha Pili kimeanza....

Dakika 45'
Saidooo anapiga inakuwa Goal kick

Dakika ya 60'
Simba wanapata kona ila inaishia kwenye mikono ya Kipa.

Dakika ya 75'
Simba wanapata kona, anaenda kupiga Onana.
Haileti impact mbaya kwa Jamhuri

Dakika ya 83'
linatokea shambulizi kali sana kwenye goli la Simba.
Ayoub anaokoa vizuri.
heko kwa Ayoub

Dakika ya 90'
Nyongeza ni 2'

Full Time
Simba 1 - 0 Jamhuri.

Kwa Matokeo haya Simba ameingia Nusu Fainali na atakutana na Singida FG.


Huku Mlandege Akikipiga na APR.

Jumatano 10th January 2024.
 
Mapinduzi ya mwaka Jana alianza Simba kutoka akatimkia uturuki kucheza friendly na CSKA Moscow ya russia..Akafata Yanga akarudi Avic town...Je mwaka huu na Simba atatolew mapema kama Yanga?? Acha tuone itakuaje

Siba Guvu Moya
By MO✅
 
Back
Top Bottom