Dodoma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe avamiwa, apigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana

Mawazo mafupi kama ulrefu wa nzi
Wanzinzi utawajua tu! Wanajua sana kuteteana!! Mume wa mtu usiku wa manane ndo unarudi halafu unategemea tukuamini? Mtu mwenyewe ni mtu wa bilicanas!! Usitufanye sisi kama watoto wadogo!!
 
View attachment 1472626
View attachment 1472650

Salaam,

Taarifa nilizozipata hivi punde toka chanzo changu kinanihabarisha kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman A. Mbowe amevamiwa na kikundi cha watu wasiojulikana akielekea nyumbani kwake usiku huu na kupigwa na wamemuumiza.

Tukio hili limetokea majira ya saa 6-7 usiku.

Mhe. Mbowe amekimbizwa Hospitali ya Ntyuka iliyopo jijini Dodoma.

Kamanda Muroto amesema wamepata taarifa kuwa kavunjwa mguu wa kulia na amelazwa Wodi namba 4 hospitalini hapo. Amesema taarifa zaidi zitafuata

MAONI YANGU:
Mhe. Mbowe kuvamiwa na kupigwa eneo la Area D, jijini Dodoma, Mtaa wa Sengia; linalotajwa kuwa na ulinzi wa kutosha, kama ilivyotokea kwa Lissu kunaacha maswali mengi, je, hili linaweza kuwa limechochewa na Lissu kutangaza nia ya kugombea Urais wa JMT October 2020? Ni hasira au kitu gani? No one knows.

Bado najiuliza; hivi kama Taifa kwa tabia hizi za kihuni tunaelekea wapi? Hawa wanaojichukulia sheria mikononi kila siku wanafanya hivyo kwa kutumwa na nani? Matendo haya yataendelea kwa viongozi wa upinzani mpaka lini?

We need to wake up, better late than never.


Kudadadeki Lissu ni noma jamani.....kakaa benchi miaka yote akipanga mashambulzi yake.....japo katangaza nia ya kutaka kugombea urais sidhani kama atagombea tena kwani serikali ikishakamilisha uchunguzi wake by then atakuwa na misukosuko ama ndani baada ya kutajwa na wahusika kuwa ndiye yeye aliyepanga mashambulizi ya kutaka kumuua Mbowe kwa kisasi. I said it first, watch and listen.
 
Siasa maji taka katika ubora wake.

Wewe unaejitapa una nguvu ya kuondoa uhai wa wengine, huna uwezo wa kurejesha uhai hata wa sisimizi mmoja.

You are just a mere wicked mortal.

Mbegu ya uchungu inayopandwa Sasa itakapomea na kuzaa kisasi msimtafute mbaya nani. Na msishangae watakaokuwa targets za hao walipiza kisasi.

Won't be good days to think about.
 
Mwenyezi Mungu,ikikupendeza,tunaomba utuondolee duniani mtu/watu wanaohusika kubariki matendo haya ambayo sasa yanataka kuwa ni sehemu ya maisha yetu.

Ikiwezekana,mpe/wape gonjwa linaloweza hata kuwapelekea ulemavu wa kudumu ili watu wako wasio na hatia wawe salama.

Bila kupewa pigo,mtu au watu hawa wataumiza watu wengi hivyo ni bora wao watangulie au waathirike ili watu wako wapone.

These people are no longer human being, but they are something else probably animals!!!
 
Mimi nina mashaka Inawezekana hizi ni njama ndani ya chama kumpoteza Mbowe ili kuwapokonya watu wa Kilimanjaro Chama chao
 
Kuna watu wanataka kuitengeneza Tanzania ya kipumbavu haijawahi kutokea! Kuna watu walishaanza kujenga Tanzania ya Watanzania lakini kuna waharibifu wa hayo mambo mazuri
 
Mbona maelezo yamenyooka au uwezo wako ni kusoma vichwa vya habari tu?

Haya maelezo hayaja nyooka na maelezo haya yanazua maswali mengi kuliko majibu.

1) Usiku huo mwingi alikuwa anatoka wapi au anaenda wapi ?.
2) Alikuwa na nani ?
3) Walinzi wake wa kila muda walikuwa wapi?
4) Dreva wake alikuwa wapi ?
5) Alikuwa eneo gani na nini hali ya uasalama ya eneo hilo?
6) Alikuwa peke yake au aliongozana na watu wengine?
7) Kama alikuwa na watu wengine, jee na wao wameumizwa ?

Habari muhimu kama hii inayo muhusu kiongozi mkubwa lazima iwekwe wazi ili tujue na tuweze kuhukumu tukio kwa uhalisia wake. Haitawezekana matukio kama haya yatokee kama Taifa tufumbie macho lakini pia Lazima tuhoji kwa ndani ili tupate ufahamu wa pamoja au basi ufahamu wa Watanzania wengi.

Tusihukumu suala la picha ya kutengenezwa na wenye madaraka au sisi wachadema kwa kutafuta huruma.
 
Mmh hizi si dalili nzuri kabisa kuelekea uchaguzi mkuu. Njia zote zimeshindikana sasa hii ya kuumizana ndio silaha yao ya mwisho iliyobaki. KUKICHWA KUTAMBAZUKA. WAKATI SI MILELE.

Jr
Mkuu hata wewe unarukia kwenye HITIMISHO? Hivi siasa ndio tumezipa kipaumbele kuliko ubongo wetu na Imani zetu? Hata tukashindwa kujiuliza matukio machache tu yaliyopita Mfano wa lile la Makamu Mwenyekiti Bara Philip Mangula kupewa sumu tena ndani ya kikao cha CCM?

Tujipeni muda kutafakari kabla ya kushutumu. MAAMUZI YANAYOTOLEWA WAKATI WA HASIRA HAYAZAI ISIPOKUA MAJUTO
 
Walisema mpaka 2020 atakuwa ameufuta upinzani nchini. Upinzanj bado upo licha ya dhulma kubwa uliofanyiwa.

Hii inaonekana ni last option ya kutaka kushindana kinyang'au badala ya kikanuni.
 
Kuna Katazo la kutembea usiku nchi hii?
Seriously,unatembea usiku mnene na hauwezi kujihakikishia ulinzi wako?,,
Sawa na yule alikuwa akilalamika anafuatiliwa na watu kisha akashauliwa achukue tahadhari,yeye akachukulia poa,matokeo yake akashambuliwa,
Hii sio game,,be serious
 
Ile timu ya Mbowe ya ulinzi ilikua wapi? Mbowe anaweza kuwa mwenyewe muda huo huku akiimba kila siku nchi ni hatari kwa maisha ya viongozi wa upinzani? Mbona sioni uhalisia hapa jamani?
 
Back
Top Bottom