Dodoma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe avamiwa, apigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana

View attachment 1472626
View attachment 1472650

Salaam,

Taarifa nilizozipata hivi punde toka chanzo changu kinanihabarisha kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman A. Mbowe amevamiwa na kikundi cha watu wasiojulikana akielekea nyumbani kwake usiku huu na kupigwa na wamemuumiza.

Tukio hili limetokea majira ya saa 6-7 usiku.

Mhe. Mbowe amekimbizwa Hospitali ya Ntyuka iliyopo jijini Dodoma.

Kamanda Muroto amesema wamepata taarifa kuwa kavunjwa mguu wa kulia na amelazwa Wodi namba 4 hospitalini hapo. Amesema taarifa zaidi zitafuata

MAONI YANGU:
Mhe. Mbowe kuvamiwa na kupigwa eneo la Area D, jijini Dodoma, Mtaa wa Sengia; linalotajwa kuwa na ulinzi wa kutosha, kama ilivyotokea kwa Lissu kunaacha maswali mengi, je, hili linaweza kuwa limechochewa na Lissu kutangaza nia ya kugombea Urais wa JMT October 2020? Ni hasira au kitu gani? No one knows.

Bado najiuliza; hivi kama Taifa kwa tabia hizi za kihuni tunaelekea wapi? Hawa wanaojichukulia sheria mikononi kila siku wanafanya hivyo kwa kutumwa na nani? Matendo haya yataendelea kwa viongozi wa upinzani mpaka lini?

We need to wake up, better late than never.
Duh...!.
Hii ni hatari sana!.
Pole sana Mhe. Mbowe,
Get well soon.
P
 
Hii kitu sio bure, ni mpango mkakati mwovu wa kisiasa...

## Hebu fikiri hili;

å Jana tarehe 8/6/2020, Tundu Lissu katangaza nia ya kugombea Urais rasmi ktk hotuba bora kabisa moja kwa moja toka Belgium...

å Kwa vyovyote na kwa dalili zote, Tundu Lissu ana uwezekano wa 95% kupitishwa na chama kuwa mgombea wa Urais kuchuana na huyu wa CCM (John Pombe Magufuli) ambaye anatetewa na kuuzwa kwa nguvu kubwa kupita kiasi za kihuni (violence) na wafuasi wake kwa sbb yeye mwenyewe kama alivyo hawezi kujiuza...

å Hili la Tundu Lissu lazima limewashitua sana CCM na "diehard" wa Magufuli. Obviously, kwa sasa wanatafuta namna yoyote ya kulizuia ama kulififisha nguvu yake kwa gharama yoyote hata kama ni kumuabudu shetani...

å Likely, wameshaona kabisa kuwa kwa njia za kawaida za kisheria/mahakama na kisiasa na kikatiba, haiwezekani kumzuia Tundu Lissu. Sasa wana option moja tu, KUUA kila connection...

## Kupigwa kwa Mbowe, Je ni sehemu ya mpango mkakati huo;

å Uwezekano wa kusema, YES ni 100%..!

å Mbowe ni Party chairman wa chama kitakachomdhamini Lissu. Kwa vyovyote, Mwenyekiti ni kiungo muhimu...

å Tayari zilishaanza kusambaa clips na maneno mengi kwenye social medias kwamba, Mbowe hatakubali Tundu Lissu agombee nafasi hiyo...

å Tukio hili laweza kuwa ni mkakati wa ku - twist mjadala mzima uwe; "....mnaona sasa, tayari wameshaanza kutafutana kuuana wenyewe kwa wenyewe kwa sbb ya Urais. Tukisema Mbowe ndiye aliye organize mpango wa Lissu kupigwa risasi mwaka 2017 muwe mnaelewa. Jamaa naye (Lissu) anataka kulipa kisasi...."

Haya ama yanayofanana na haya ndiyo yanateka mjadala ktk mitandao ya kijamii si muda mrefu..

## Mnadhani Jeshi la polisi litakuja na taarifa/ripoti gani baada ya uchunguzi?

å Nothing tangible, nothing meaningful....!

å Kama ilivyokuwa kwa Tundu Lissu, ndivyo itakavyokuwa kwa tukio hili la Freeman .A.Mbowe. Longo longo na danadana nyingi mara hili mara lile...

å Tusije kushangaa hata tukisikia toka kwa akina Polepole na idara yake ya Lumumba Propaganda wakisema;

"...jamaa amejipangia kujishambulia ili akwepe uchunguzi wa matumizi ya mabaya ya fedha na kulala na wabunge wanawake wa chama chake unaofañywa na PCCB....!!"

Kwa hiyo, kuna kila dalili kuwa huu ni mpango uliopikwa mahali ndani ya "secret force" ya CCM na obviously majibu yake wanayo tayari na kidogo kidogo watakuwa wanayaachilia...

å Ndiyo, tukubali ama tusikubali, right now, CCM is a dying horse...

Wote kuanzia mwenyekiti wao, Spika wa bunge na wafuasi wao waliopewa jina la "diehards" na national chairman wao kwa sasa wako "so desperate" kiasi ambacho tunaweza kuona mambo ya ajabu yakitendeka ktk kipindi cha kuanzia sasa hadi uchaguzi wenyewe, mwezi oktoba....

å Mtu unaweza kushangaa sana, kwamba, kwanini hawa viumbe wanatumia nguvu nyingi mpaka njia za uhalifu wa kijambazi kumtetea mtu wao Bwana John Pombe Magufuli, mtu wanayedai, "...alishushwa toka mbinguni kuikomboa Tanzania...?"

å Unajiuliza kwanini huyu "mtakatifu" ama "mtu mshuka toka mbinguni" asiachwe ili "utakatifu" wake umtetea wenyewe?

å Yesu Kristo alikuwa mtakatifu kwelikweli.
Utakatifu wake, matendo yaje na kazi zake njema i.e kuponya wagonjwa, kufufua watu, kufungua waliofungwa na kuonewa na Ibilisi shetani, kutenda miujiza mbalimbali nk ndizo zilizokuwa zinamtetea na kumshuhudia kuwa yeye ni Mungu menyewe akitenda kazi ndani yake mtu. Kamwe hakutumia "violence" ama nguvu kujitetea japo uwezo huo alikuwa nao wa kuwageuza adui zake wawe hata mavumbi palepale....

å Sasa huyu "mtakatifu wetu fake" ndugu John Pombe Magufuli sijui kwanini kazi zake kama vile ujenzi wa SGR ama Bwawa la umeme la Stiglers Gorge ama ndege za Bombardier na dreamliner ama ikulu ya chamwino ama Chato International Airport nk nk zisimtetee na kumsemea na badala yake ana opt fujo (violence) na mauaji...???
 
Ila vitu vingine jamani, inamaana Mbowe hana bodigadi,yaani anatembea bila walinzi?? Diamond ana bodgad sembuse Kub?? Tuache maigizo basi
Kajivunja mwenyewe mguu, au sio!? Sawa sawa. Endeleenj kujenga chuki. Damu ya Akwilina mliyomwaga haijatosha.
 
Mbaya sana
Basi shangilieni, semeni ni vita ya uraisi.

Tanzania nzima inafahamu nani ana chuki kubwa na wanaomkosoa, nani aliapa ataufuta upinzani kabla ya 2020 kuisha!!

May nzima Mbowe na CHADEMA yake ameandamwa sana bungeni kupitia subwoofer, wakatumiwa wabunge wake,ikatumika TAAKUUKUU kumulika ruzuku,wakatumiwa wanunuliwaji ubunge kumshambulia amewadhalilisha kingono, yote hayo hayajawafurahisha!!!
 
Mkuu kwani mbowe kutembea mwisho saa ngapi?
Hata kama! SAA saba za usiku mume wa mtu unakuwa bado kwenye matembezi? Tuwe wakweli unakuwa unatembea na nani saa saba za usiku? Bila shaka utakuwa unatembea na ambao saa kama hizo wao ndo kazi zao zinakuwa zimechanganya! Unawajua sina haja ya kuwataja!! Ukitilia mhusika ni mshabiki wa bilicanas!! Mzee alikuwa anakumbukia vitu vya bilicanas!
 
Diamond mtoto wa juzi awe na walinzi, huyu mzee anayepigana kuongoza nchi akose ulinzi, serious hivi ruzuku wanafanyia kazi gani? Kiongozi mkubwa wa chama kuwa na ulinzi ni moja ya maendeleo.
We unafkir uyo mlinzi atafanya kazi masaa 24?? Hana familia, hapumziki, muda wote kulinda tu??? Think twice
 
Hata kama! SAA saba za usiku mume wa mtu unakuwa bado kwenye matembezi? Tuwe wakweli unakuwa unatembea na nani saa saba za usiku? Bila shaka utakuwa unatembea na ambao saa kama hizo wao ndo kazi zao zinakuwa zimechanganya! Unawajua sina haja ya kuwataja!! Ukitilia mhusika ni mshabiki wa bilicanas!! Mzee alikuwa anakumbukia vitu vya bilicanas!
Mwanaume hana limitation ya kurudi nyumbani kwake. Muda atakao rudi ndio sahihi kwake.
 
Jombaa, madhaifu yako ya kupenda milupo usiyafananishe na watu mwingine. Watu makini hufanya "networking" nyakati za usiku kwa ajili ya "vital issues".
Hiyo networking ya nyakati za usiku tu aidha ni networking ya kuwanga au ya uzinzi si zaidi ya hapo!
 
Mmh hizi si dalili nzuri kabisa kuelekea uchaguzi mkuu. Njia zote zimeshindikana sasa hii ya kuumizana ndio silaha yao ya mwisho iliyobaki. KUKICHWA KUTAMBAZUKA. WAKATI SI MILELE.

Jr
Wanaelekea kushindwa wameamua kuumiza viongozi kama Njia ya kutisha
 
Haya maelezo hayaja nyooka na maelezo haya yanazua maswali mengi kuliko majibu.

1) Usiku huo mwingi alikuwa anatoka wapi au anaenda wapi ?.
2) Alikuwa na nani ?
3) Walinzi wake wa kila muda walikuwa wapi?
4) Dreva wake alikuwa wapi ?
5) Alikuwa eneo gani na nini hali ya uasalama ya eneo hilo?
6) Alikuwa peke yake au aliongozana na watu wengine?
7) Kama alikuwa na watu wengine, jee na wao wameumizwa ?

Habari muhimu kama hii inayo muhusu kiongozi mkubwa lazima iwekwe wazi ili tujue na tuweze kuhukumu tukio kwa uhalisia wake. Haitawezekana matukio kama haya yatokee kama Taifa tufumbie macho lakini pia Lazima tuhoji kwa ndani ili tupate ufahamu wa pamoja au basi ufahamu wa Watanzania wengi.

Tusihukumu suala la picha ya kutengenezwa na wenye madaraka au sisi wachadema kwa kutafuta huruma.
we mpuuzi kaa kimy tu, hii ncbi tupo huru hata kutoka saa tisa usiku kwenda mahali popote kufanya chochote halali, hayo mambo ya kuhoji ni uminywaji wa uhuru,,,, yeyote aliefanya huu upuuzi ni yule yule aliemwagia lisu risasi,
 
Back
Top Bottom