Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,494
113,590
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za kwa maslahi ya taifa, zikijadili jambo lolote la kisiasa, kiuchumi na kijamii lenye maslahi kwa taifa letu. Makala hizi huwa na swali, kisha hoja, halafu jibu utalitoa wewe mwenyewe msomaji.

Makala ya leo ni kuhusu maendeleo ya siasa zetu kuelekea uchaguzi wa 2025.

Siku zote Tanzania tumekuwa na siasa za kuhasimiana kati ya Chama tawala CCM na vyama vya upinzani, Kiingereza tukiita ni politics of confrontations, siasa zikiendeshwa kwa uadui na kila aina ya figisu, na kwenye baadhi ya maeneo korofi, ushindi kupatikana kwa bao la mkono!.

Baada ya kutokea kilichotokea, ile Machi 17, Samia Suluhu Hassan, kaingia na kitu cha kwanza alichokifanya kwenye siasa zetu, ni kuliishi tuu jina lake la Suluhu kwa kuleta suluhu ya kisiasa kuachana na siasa za kuhasimiana na kuitroduce, politics of reconciliation and politics of tolerance kwa Samia kukubali kufanya mazungumzo ya maridhiano kati ya CCM chama tawala na Chadema, chama kikuu cha upinzani Tanzania, huku akiunda tume Prof Mukandala na kuwaweka vyama vyote kujadili mustakabali mwema wa nchi yetu.

Kwanza Mama alikaa na vyama vyote kupitia TCD pale Dodoma, katika mkutano huo, kuna chama kilisusa kisa kiongozi wake yuko korokoroni!. Sisi wa ushauri wa bure, tukashauri ... Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!.

Kwenye mkutano huo wa TCD, waungwana wakamuombea mtu msamaha, Rais Mama Samia alivyo mtu mwenye wema wa asili, Psychoanalysis Trends za Viongozi Wetu, Humbleness ya Rais Samia ni Bonafide Genuine, ni asili yake, ni nature yake, ndivyo alivyo, Ila...
, akajibu pale pale "kusameheana kupo", sisi wa kuandika, tukaandika ... Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye?

Na kweli haikupita punde mtu akaachiwa, na sisi wa kuandika tukapongeza... Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!

Mara ghafla nchi ikatulia, Chadema iliyokuwa hoi bin taaban kifedha mara ikapata pumzi, ikaanza kupumua, mara sasa ikawa na uwezo hata wa kuendesha vikao, viongozi wake mara ghafla wakawa na uwezo za kufanya ziara hadi za nje ya nchi, yote haya ni matunda ya maridhiano.

Wakati Rais Mama Samia akiyafanya haya, haimaanishi CCM wote walikuwa wanayafurahia, no, kuna wahafidhina wenye nguvu na ushawishi mkubwa ndani ya CCM, walimpinga Samia, hivyo Samia alishughulika nao wengine wale wenye kelele sana, ilimbidi kuwaondosha kuwaweka mbali kwa kuwapa majukumu mengine ya kiutendaji ili kuwafunga midomo!

Wahafidhina hawa pia walikuwepo Chadema, na miongoni mwa wahafidhina hawa wa Chadema ni M/Mwenyekiti, Mhe. Tundu Lissu!.

Mama Samia alipopita Ubelgiji, Tundu Lissu akachangamkia fursa ya kuonana na kufanya mazungumzo na Tundu Lissu, ila baada tuu ya mazungumzo baina ya Tundu Lissu na Samia, Tundu Lissu akaibuka na haya,
Kwa jinsi Mungu alivyo mkubwa, ikatokea fursa ya Rais Samia akafanya ziara ya Ubelgiji, M/Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, akaichangamkia fursa hiyo, akaomba kuonana na Rais Samia. Na Samia alivyo hana makuu, akakubali kuonana na Lissu na kufanya nae mazungumzo ya faragha.

Kitendo tuu cha Rais Samia kukubali kukutana na Tundu Lissu, ni uthibitisho wa ile nia njema ya dhati ya kuliponya taifa kwa kufuata ile filosofia ya Rais Samia ni rais Watanzania wote, ni rais wa wana CCM, ni rais wa wapinzani ni rais wa Watanzania wote hata wasio na vyama, lengo la kila Mtanzania ni kuijenga Tanzania yetu, hivyo CCM na wapinzani, tunajenga nyumba moja, hatuna sababu yoyote ya kuendelea kugombea fito!.

Kwa vile ni mazungumzo ya faragha, Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu chini ya Mkurugenzi mpya, Zuhura Yunus (hongera), ikaeleza kuhusu mkutano huo wa Rais Samia na Tundu Lissu bila kueleza kilicho zungumzwa.

Rais wa JMT, ndiye raia number moja wa JMT na ndie Mkuu kuliko mtu mwingine yeyote ndani ya JMT, kimamlaka na kimadaraka. Sasa inapotokea mtu yeyote umeomba kumuona rais na kuongea nae jambo lako lolote na rais akakukubalia kumuona na kuongea nae, ile tuu kuongea na rais ni heshima kubwa, ina maana umeaminiwa.

Hivyo Tundu Lissu kukubaliwa kukutana na rais Samia, ni Lissu ameaminiwa. "Ukiaminiwa, jiaminishe". Baada ya mazungumzo, of course, lazima kuna hoja na maombi aliwasilisha kwa rais Samia.

Japo Tundu Lissu ni mtu mkubwa, M/Mwenyeki wa Chadema, lakini Tundu Lissu compared to Rais wa nchi, Tundu Lissu mdogo kuliko Samia, na amekutana na mtu mkubwa, rais wa JMT, baada ya kikao, ukiona mkubwa amenyamaza, na wewe mdogo nyamaza!. Hapa natoa somo kwa wanasiasa wetu, tujifunze kunyamaza!. Somo hili la kujifunza kunyamaza nilianza kulitoa siku nyingi!. Mara baada ya uchaguzi Mkuu wa 2015, mgombea wa Chadema, Edward Lowassa kulalamika kuwa ni yeye alishinda kwa kura nyingi lakini kura zake akapewa mpinzani wake, nilimshauri anyamaze Elections 2015 - Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali Yetu ni Serikali Dhalimu?, Haramu?. Hukumu ya Karma ii Juu Yake!

Moja ya mapungufu makubwa ya upinzani wa Tanzania, ni kupayuka payuka sana, kuropoka ropoka na kupiga sana kelele kuhusu karibu kila kitu!.

Kuna mambo ya kupigia kelele na kelele zikasaidia, lakini kuna mambo ya kufanywa kimya kimya, sio kila kitu ni kupayuka, kuropoka na kupiga kelele!.

Kama Lissu ameaminiwa na kuzungumzia na rais Samia in confidence, kitendo cha kusema alichozungumza in confidence ni breach of confidence!. Mambo mengine ni kujifunza kunyamaza, ukiaminiwa jiaminishe.
Mimi Tundu Lissu nimesoma nae sekondari Ilboru, hivyo namfahamu sana, kwanza ni kichwa sana, Tundu Lissu ni kichwa cha ukweli, very bright and brilliant, tatizo lake ni moja tuu, ambalo nimeisha lisema kwenye bandiko langu hili Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!
Hivyo nimeisha andika mengi humu kumhusu Tundu Lissu miongoni mwake ni haya
Mtu kuwa vocal kwa wanaharakati ni sifa muhimu sana haswa katika utetezi wa haki za binadamu. Hivyo katika harakati za mwanzo za vyama vingi, Chadema kilikuwa ni chama cha kiharakati hivyo wanaharakati kama kina Tundu Lissu, Dr. Wilbrod Slaa, Zitto Kabwe na wengine wengi walikuwa very vocal hivyo kuwa ni asset muhimu sana kwa mapambano ya kudai haki.

Ni kufuatia uanaharakati wa Tundu Lissu, mimi ni miongoni mwa tulimshauri Tundu Lissu, ndie amkabili Magufuli uchaguzi wa 2020 Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli! hicho nilichokisema hapo kuwa Tundu Lissu ni zaidi ya Magufuli, kwenye nini, ndicho kitu kitakuja kuigharimu Chadema mbele ya safari!.

Mara tuu baada ya kumshauri Tundu Lissu amkabili Magufuli, ndipo like tukio la very unfortunately likamtokea Tundu Lissu kwa kushambuliwa na wasiojulikana, na kukimbizwa nje ya nchi kutibiwa. Akiwa matibabuni, aliendelea kuwa vocal, na kwa mambo aliyokuwa akiongea kuhusu Tanzania, mimi nilifika mahali, nikadhania Tundu Lissu hatarejea tena nchini Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela!

Kumbe Tundu Lissu ni very bold, akaomba kuhakikishiwa usalama wake ili arejee nyumbani, japo aliowaomba wamhakikishie usalama, walimkalia kimya, hawakumjujibu, ni akina sisi, ndio tulimmshauri arejee tuu hivyo hivyo na kweli akarejea Kamanda Lissu, Usisubiri Jibu la IGP Kuhusu Usalama Wako, Aliyekulinda na Shambulio Lile Yupo, Yeye Aweza, na Ataendelea Kukulinda, Welcome Back Home!

Moja ya sifa kubwa za pekee za Tundu Lissu, ni mkweli daima na kwenye ukweli, Lissu hana simile wala hakopeshi, hata ukweli huu kuhusu kilichotokea ndani ya Chadema, ni Lissu ndie aliyetoa Tundu Lissu kama JPM, ni mtu mkweli. Asema ukweli jinsi ukomo wa uongozi ulivyoyeyuka CHADEMA

Kwa sasa Tundu Lissu yupo nchini akifanya mikutano yake ya hadhara kwa uhuru, huku akiwa na ulinzi na usalama wa kutosha bila bugudha yoyote, tatizo lake ni lile lile moja, he is very vocal!.

Hebu msikilize hapa



Swali ni kwa hiki anachoongea hapa, Tundu Lissu, sio kuwa ameanza kutoa siri za mazungumzo ya maridhiano kabla the public hatujatangaziwa rasmi na wana maridhiano wenyewe?!.

Kumbe kwenye mazungumzo ya maridhiano watu wameridhiana kugawana nusu mkate!. Nani alilijua hili?. Kumbe wameahidiana kuachiana majimbo!, nani alilijia hili?, kama sio Tundu Lissu kuyasema haya, akina sisi tungejuaje na mazungumzo ya maridhiano ni siri!. Asante Lissu kwa taarifa hii.

Kwa kawaida mazungumzo yoyote ya majadiliano au reconciliation hufanywa behind the camera with honest, truthfulness, trust na the spirit of a win win situation, hakuna mshindi, hakuna mshindwa. No any details za mazungumzo hayo hutolewa nje kwenye public domain kabla ya kufikia muafaka, wanaridhiana nini, but now through Tundu Lissu, the cat is out of basket, you can't hide anymore!, this is breach of trust!.

Lissu anazungumza kwa kutumia lugha kali!, anauliza kama wenzake wana akili timamu kweli, unamjua huyo anayemuulizia kama ana akili kweli ni nani?. Kitendo cha kuyaita maridhiano kuwa ni ujinga, jee maridhiano ya CCM na Chadema kweli ni ujinga?.

Hizi lugha za Tundu Lissu anazotumia, ambazo ni very vocal, jee ni lugha za kistaarabu na kiungwana?, mimi naziona kama zina ukakasi fulani, lakini sijui nyinyi wenzangu.

Hii sio mara yangu ya kwanza kuialert Chadema about the impending doom!, walipompokea Edward Lowassa, niliwaeleza kitu Ujio wa Lowassa CHADEMA: Kuna kundi wamesusa, wanapanga kurejea CCM! japo nilibezwa, lakini la kutokea lilikuja kutokea, hivyo sitashangaa hata hapa nikibezwa, ila litakapotokea la kutokea, nitawakumbusha.

Kwa haya anayoyasema Lissu kutoa siri za maridhiano, je Lissu bado ni asset kwa Chadema, au kwa sasa, Tundu Lissu is liability?. Sisi waona mbali, kuna kitu hapa tunakiona kwa mbali, kisipokuwa handled with care, it's going to cost Chadema very dearly.

Wasalaam

Paskali
 
Hayo ndio mambo ambayo Magufuli aliyakataa, tufanye Siasa kwa nyakati na vipindi maalumu.

Sio kutafuta Tensions zisizo na kichwa wala Miguu. Nachukia mijitu type ya aina yake, uwa yanakuwa na Egoism na yenyewe kila kitu nikupinga tu, mazuri linapinga, mabaya linapinga.

Jinga hilo, litafute kazi ya kufanya sio kutafuta Tensions kwa ku-force.​
 
Kuna mahali niliandika Lissu anaropoka mmoja wa wafuasi wake humu ndani akasema kudai Katiba Mpya, Tume Huru, na mengineyo sio kuropoka..

Sasa nimuulize ndugu mfuasi, Lissu anapouliza viongozi wenzake chamani kama wana akili huyu ana maana gani?

Simply huyu ni mjuaji anayetakiwa kuambiwa ukweli apunguze mihemko, awaheshimu viongozi wenzake, na kufuata taratibu za chama chake.
 
CHADEMA bado ni kitu kimoja; kama ambavyo covid-19 walipata baraka za Mwenyekiti kwenye hayo waliyofanya, ndivyo hivyo Lissu leo anayoyafanya yana baraka za Mwenyekiti.

Katika hali ya kawaida CHADEMA ilianza poteza mvuto kwa jamii baada ya maridhiano, mashabiki waa Chadema ni watu wanaopenda kuwa against CCM hata katika jambo lisilohitaji kupingwa, shabiki wa Chadema ni wale watu wa pinga pinga kila jambo.

Kwa maono yangu, zoezi la kurudisha imani ya mashabiki na wanachama lipo mikononi kwa Lissu. Yote anayofanya yana baraka zote na hata hizo ziara na mikutao ziko funded and facilitated na Chadema wenyewe.

Shortly ni kwamba Lissu na CHADEMA wanajua wafanyalo.
 
Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za kwa maslahi ya taifa, zikijadili jambo lolote la kisiasa, kiuchumi na kijamii lenye maslahi kwa taifa letu. Makala hizi huwa na swali, kisha hoja, halafu jibu utalitoa wewe mwenyewe msomaji.
Aisee! kuna fukuto kubwa CHADEMA. Wametofautiana malengo, Tundu ana pesa za issues zake Ulaya, Heche, Msigwa wanataka ubunge kupata pesa za kusukuma maisha halafu TL anataka wakae tu hadi ccm itakapoondoka madarakani..... hahaaaaa lini sasa
 
Mwananchi Gani aliridhia wagawane majimbo bila uchaguzi kufanyika?

Ubakaji huo wa DEMOKRASIA ni zaidi ya Ule wa 2020.

Siku ukijeruhiwa hata Kwa mshale ndo utajiua Maana ya Hoja ya Lissu.
Nimekuuliza swali hujajibu, narudia, risasi alizopigwa Lissu ndio zimempa immunity ajiongelee chochote, na popote, nje ya vikao halali vya chama chao?
 
Kama kuweka maslahi ya Taifa mbele ndo unaita kuropoka, basi namshauri aropoke zaidi.

Sasa wewe unaona ni sawa watu kupigwa changa la macho kwa kupewa pipi ya viti vichache vya ubunge ili kucompromise maslahi mapana ya vizazi na vizazi kwa kupata tume huru na katiba mpya iliyo bora?.

So far, Lissu anasimamia commonsense na fact.
Huwezi kuibadili nchi hii bila katiba mpya.

Kwenye Chadema wapo wasaka ubunge, wao akili zao, malengo yao na mwisho wa upeo wao ni kuwa wabunge tu baasi. Hawana interest ya kweli na katiba mpya. Wanapay lip service tu.
 
Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za kwa maslahi ya taifa, zikijadili jambo lolote la kisiasa, kiuchumi na kijamii lenye maslahi kwa taifa letu. Makala hizi huwa na swali, kisha hoja, halafu jibu utalitoa wewe mwenyewe msomaji.



Paskali
Huyu lissu ni mtu mbishi na mbinafsi kwa kuzaliwa. Sera ya maridhiano naturaly hatamudu. Hajui kukubali au kuridhia kitu au kujenga chochote ila kubomoa tu na kupata mkate wake kwa njia hiyo.
 
Lissu na Magufuli wanapenda kufanya siasa za Uzalendo.

Tofauti yao Lissu yupo kwenye mfuko wa Mbowe na mabeberu, hawezi kuleta positive impact yoyote kwa Watanzania.

Mbowe anazidi kuiua CHADEMA ambayo aliijenga kwa karibu miongo miwili. He has become a polarising figure kwa kukaa muda mrefu uongozini.

A good dancer must know the right time to leave the stage. Ni muda awaachie wengine waongoze chama.
 
Back
Top Bottom