Tundu Lissu ahoji sababu za Mwenyekiti Mbowe kutokuwepo kwenye mapokezi uwanja wa ndege

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,173
27,223
Tulisema Ila wanachadema wenye mihemko wakaishia kututukana. Na wengine wakasema protocal hairuhusu.

Gazeti la mwananchi limemnukuu Lissu akihoji alipo Mbowe, Lissu amehoji sababu za Mbowe Kutokuwepo.

Sasa ni rasmi ule mnyukano, makundi na mgawanyiko upo hadharani.

Kazi ndjo imeanza.

----

Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara) Tundu Lissu ametua nchini, akitokea Ubelgiji alikokimbilia baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 huku akimuulizia aliko Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ambaye alitajwa kuwepo kwenye orodha ya kumpokea katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Lissu amewasili leo Jumatano, Januari 25, 2023 na kupokewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika aliyeongoza na viongozi wa Kamati Kuu waliokwenda kumpokea uwanjani hapo.

Mara baada ya kutoka nje ya geti la kuwapokea wageni uwanjani hapo, Lissu alionekana kuwa mwenye furaha alisalimiana na viongozi kwa kuwashika mikono ghafla akauliza, " Mwenyekiti (Mbowe)yupo wapi? Si mliniambia atakuwepo? Eeeeh.

Hata hivyo, Mnyika alionekana kutabasamu huku baadhi ya viongozi walisikika wakimwambia kwamba atakutana naye Temeke viwanja vya Bulyaga katika mkutano wa hadhara alioandaliwa na chama hicho.

Lissu aliondoka nchini kwa mara ya kwanza Septemba 7, 2017 baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana jijini Dodoma alikokuwa akihudhuria vikao vya Bunge.

Lissu alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma alipopatiwa matibabu ya awali na baadae kukimbiza jijini Nairobi nchini Kenya kwa matibabu zaidi.

Januari 6,2018 alihamishiwa nchini Ubelgiji kwa matibabu zaidi hadi Julai 27, 2020 aliporejea nchini na kuwania urais lakini alishindwa na mgombea wa CCM, John Magufuli.

Hata hivyo Novemba 10, 2020, baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu, Lissu aliondoka nchini kwenda Ubelgiji kwa madai ya kutishiwa usalama wake.

Chanzo: Mwananchi
 
Tulisema Ila wanachadema wenye mihemko wakaishia kututukana. Na wengine wakasema protocal hairuhusu.

Gazeti la mwananchi limemnukuu Lissu akihoji alipo mbowe, Lissu amehoji sababu za mbowe Kutokuwepo.

Sasa ni rasmi ule mnyukano, makundi na mgawanyiko upo hadharani.

Kazi ndjo imeanza........
View attachment 2495346
Mwenyekiti hawezi kwenda kumpokea Makamu
 
Kiukweli sijui ni lini Lissu will grow into a mature politician?!. Hilo ni la kuhoji in public, anadhani ananyenyekewa na wote?.
P

..Mbowe yupo kwenye mkutano Temeke.

..Hivi kama umefika mahali na unatarajia kuonana na mtu fulani, Je usipomuona hutamuulizia?

..Na kama umefuatilia tukio Lissu alionekana yuko so excited and happy, mambo ya itifaki,.siasa, na uongozi, sidhani kama yalikuwa mawazoni mwake.
 
😁😁😁
16538044797770.jpg
 
Back
Top Bottom