Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
25,051
2,000
Kumekucha salama,


Leo tarehe 06.08.2020 mgombea nafasi ya kazi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kwa Chama cha Mapinduzi, atachukua fomu kwenye ofisi ya NEC makao makuu ya Dodoma.

Baada ya kuchukua fomu ataongea na wananchi pia wanachama wa CCM kwenye ukumbi wa White House Jijini Dodoma.

Watanzania wanatakiwa wanaombwa kumsikiliza.

fomu.jpg

UPDATES:

1.jpg
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mh. Jaji Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage akikabidhi fomu za kugombea kiti cha Rais Kwa Mgombea wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto)katika Ofisi za Tume, Njedengwa Jijini Dodoma leo Agosti 6,2020. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera Charles na Wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk.

2.jpg

Mgombea wa Urais, Dkt. Magufuli akiwa na Mgombea Mwenza Mama Samia Suluhu Hassan wakionesha begi lenye fomu ya Urais

Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM:
Ushindi wa mwaka huu ni wa kishindo kikubwa. Tutashinda nafasi za kutosha. Tutashinda nafasi za kutosha za udiwani. Tutaongoza halmashauri zote nchi nzima. Tutakuwa na wingi wa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.


Rais Magufuli:

3.jpg
Napenda nikiri. Sikutegemea ningekuta watu wengi hivi hapa, kwasababu mimi nikawaida yangu kuheshimu sharia.

Kitabu cha mwaka huu cha ilani ni kikubwa kuliko miaka iliyopita, kina mambo mengi sana. Siwezi nikayasema hapa yote. Tutayasema siku ya uzinduzi wa kampeni.

Na ninawaomba viongozi viongozi wenzangu, kuzindua kampeni hizi ikiwezekana kuzianzia hapa Dodoma, kwakuwa Dodoma ni Makao Makuu ya Nchi.

Nilipomaliza kuchukuwa fomu pale kwenye jengo la NEC pamoja na Mama Samia, Mama mchapa kazi, jabali la kwelikweli, nilipokuwa nateremka kwenye gari nikiwa pale juu nikakiangalia Chuo Kikuu cha Dodoma, nikaangalia chini nyumba na maghorofa yalivyojengwa katika eneo hili la Dodoma, nikajaribu kutupa macho yangu mpaka Chuo cha Mipango kule. Nikaangalia kila mahali. Hujagusa Chuo Kikuu cha St. John, unaenda pale CBE na maeneo mengine. Hombolo sijakisahau jirani yetu kule.

Lakini nilivyoiona Dodoma ilivyo, nilijiuliza nikiwa njiani nikasema: “Dodoma kweli imekuwa hivi? Mbona sikuikuta hivi nilivyoteuliwa kuwa Rais” Nikafurahi kuwa ndoto za Baba wa Taifa zimekamilika kwamba Dodoma ni Makao Makuu ya nchi yetu.

Tulipochaguliwa kuongoza taifa hili kupeperusha bendera ya CCM, tumefanya mengi…kila mahali katika nchi hii, pamefanyika kitu.

Kwa kumbukumbu zangu tu, shule zaidi ya 908 za msingi zimejengwa katika nchi hii. Hizo ni za msingi. Za sekondari ni 228, vituo vya afya karibu 500. Mambo mengi.

Sasa hivi tuna program kubwa yankujenga barabara ya njia nne ya km 110 ya kuzunguka mji wa Dodoma, fedha ipo zaidi ya bilioni 700.

Sasa hivi tunataka kujenga uwanja wa ndege wa Msalato, fedha zipo tenda zimeshatangazwa – bilioni 600 zipo.

Nikiangalia tu yaliyopangwa kutekelezwa hapa Dodoma, sioni mtu mwingine wa kuyafanya hapa zaidi ya kiongozi wa CCM.

Tumejenga reli kutoka Dar es Salaam kuja mpaka hapa Dodoma. Upande wa Dar – Morogoro ipo asilimia 87. Kutoka Morogoro kuja hapa ni asilimia 32. Tutahitaji Mabehewa, tuikamilishe iendelee mpaka Mwanza nikaona ni Mimi na Mama Samian a CCM yangu ndiyo tunaweza kuyatekeleza haya yote. Nikiyaacha yataachiwa pale.

Nikafikiria tumejitahidi tulipoingia madarakani mwaka 2015, ni bijiji 3000 tu ndiyo vilikuwa vina umeme Tanzania nzima. Tanzania nzima tuna zaidi ya vijiji 12000. Katika miaka 5 tumepeleka umeme vijiji 9402, tumebakiza vijiji 3000. Nikafikiria kwamba tangia tumepata Uhuru tulifikia vijiji 3000, sasa tuna vijiji 9000, nikipata miaka mingine mitano vijiji 3000 vitanishinda?

Nchi yetu capacity ya umeme mpaka leo ni megawatts 1600, ndizo tulizo nazo sasa pamoja na kuwa na surplus ya Megawatts zaidi ya 300.

Vijana wengi wasomi wa Tanzania wamekosa ajira kwa kukosa viwanda vya kwenda kufanya kazi. Viwanda hivyo kuwepo vinahitaji umeme ndiyo maana tukaona tujenge mradi mkubwa wa Stiegler’s Gorge, utakaozalisha megawatts 2000.

Tukishauwasha huo umeme, viwanda vitafanya kazi. Malighafi zetu yingi za wakulima zitapelekwa kule.

Tumechoka taifa hili, unalima pamba, unaisafirirsha kama malighafi unaipeleka nje wanakwenda ku-process. Ukipeleka nje umeshapeleka ajira nje, alafu wakishategeneza nguo wanakuletea ambazo zimevaliwa; wanazivaa kwanza huko. Alafu wanakuletea wewe mitumba wakati pamba ni yako. Mnalitaka hilo vijana?

Sisis tunataka tukilima pamba yetu tunai-process hapa kwenye viwanda vyetu kwa kutumia umeme wetu wa Stiegler’s Gorge, zle nguo tunawapelekea. Ikiwezekana tunazivaa kwanza alafu mitumba tunawapelekea.

Mapinduzi haya hawawezi wakayapenda.

Tunataka korosho yetu ikishalimwa kule tui-process kwa kutumia viwanda. Viwanda vilivyotengenezwa na Baba wa Taifa vyote vilikufa.

Tunataka ukiwa na ng’ombe wako, tunaprocess hapa ngozi na kutngeneza ajira kwa vijana.

Haya ndiyo nimeyaona katika kipindi cha miaka mitano na kunisukuma kuhitaji kipindi kingine cha miaka miatano nilitumikie hilimtaifa kama mtumishi wenu.

Tumechezewa sana kwenye madini. Wapo watu walizungumza hadaharani kwamba tutashughulikiwa, tutanyooshwa. Nilisimama pamoja na wana CCM wenzangu kwamba ni bora kufa lakini unaifia nchi yako. Ni kwasababu tumechezewa sana. Madini yanachimbwa, mnayasindikiza wanaenda kuyafaidi wengine kwa kisingizio kwamba ni wawekezaji.

Sijaielewa vizuri definition ya Uwekezaji. Kwani Black person hawezi akawa muwekezaji? Mgogo hapa hawezi kuwa muwekezaji? Mjaluo hawezi kuwa muwekezaji? Tunataka uwekezaji uanzie hapa.

Katika kufikiria kwamba tumehangaikia haya, tukiondoka wale wenye rangi zisizo za kijani watakuja kweli kuyafanya haya? Waliokuwa wanashirikiana na mabeberu kutuibia madini yetu leo watageuka wawe watu wema wa kutusaidia sisi Watanzania? Ndiyo maana nimesema potelea mbali nagombea hii miaka mingine.

Tanzania ni nchi Tajiri lakini tulizoeshwa kuambiwa ni nchi masikini.

Tumeingia uchumi wa kati kwakuwa mali yetu tumeidhibiti vizuri.

Bajeti tuliyoikuta ya kununulia madawa mwaka 2015 ilikuwa ni bilioni 31 na ndiyo maana kama munakumbuka historia kila mtu alikuwa akienda hospitali anaumwa, anaandikiwa cheti akanunue mwenyewe dawa kwenye duka la dawa.

Mama Samia akaniambia lazima tuwasaidie akina mama na Watoto. Tukapandisha bajeti kutoka bilioni 31 mpaka bilioni 270. Ndiyo maana tumejenga vituo vya afya karibu 500, na vinafanya operation. Haya hayakuja kwa miujiza.

Kule Tanga treni iliacha kwenda miaka 26. Leo imefika Moshi, imefika Arusha

Kwenye elimu ya juu tumeongeza bajeti.

Nianapata wasiwasi kwamba hao ukiwaachia, inawezekana hizi meli zitapigwa mnada, haya madaraja yatavunjwa yauzwe skrepa. Inawezekana dhahabu hizi zitakuwa zinachimbwa na kuuziana wao. Inawezekana hata hospitali na X-Ray tumeleta nazo zitaharibika.

Yaliyomo kwenye ilani ya CCM ni mengi zaidi ya tuliyoyatelkeleza miaka 5 iliyopita. Nataka Tanzania iwe kama Ulaya

Nataka kuwathibitishia Mimi na Mgombea Mwenza, Mama Samia, pamoja na Chama cha Mapinduzi na ninyi Watanzania wenye mapenzi mema kwa nchi yetu, kuwa tutafanya kampeni za ustaarabu sana, tutaheshimu watu wote. Tuna uhakika Watanzania wa vyama vyote watatupigia kura kwani maendeleo hayana chama.

Ninachowaomba tuendelee kushikamana, tuwe wamoja, tusibaguane na tumtangulize Mungu.

Tulimtanguliza Mungu wakati wa Corona, tukafunga siku tatu na baadaye tukamshukuru siku tatu, leo hakuna mwenye Corona hapa. Tunabanana vizuri tu, hata kitandani bananeni tu vizuri.

Mungu wetu aliyetupoye kwenye gonjwa la Corona hawezi kutuacha.
 

Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,084
2,000
LIVE: MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CCM MHE. RAIS DKT JOHN P MAGUFULI AKI AMBATANA NA MGOMBEA MWENZA NA MAKAMO WA RAIS MHE.SAMIA SULUHU AKICHUKUA FOMU OFISI ZA TUME YA UCHAGUZI NEC DODOMA

 

Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
2,228
2,000
Kwa kweli, kama kuna rais anachukiwa na kada nyingi ni huyu. Namshauri akahutubie ndege, flyover, sgr na meli
Jamaa kama nanilii vile, hana hoja zaidi ya hayo mabarabara na ma flyover na midege ambayo Mungu ameilaani.
Haijawahi kuleta tija na likorona limeyakoronoa madege yenyewe
 

Nazgur

JF-Expert Member
Apr 19, 2020
2,313
2,000
Sijui naye sauti zitakatwa? Sijui wananchi wanyonge watasombwa kwenye malori?
Sijui leo vijembe vitasalimika?
Sijui leo mama zetu watadhalillishwa tena?
Sijui leo....!!??

Hana mda na vijembe, vijembe tunamuachia Lisu maana kila akilala na kuamka anamuona magufuli sasa anabaki kuweweseka.
Hawezi taja sentesi bila magufuli, na bado ataiimba saana.
 

Mcheza Viduku

JF-Expert Member
Jun 24, 2020
375
1,000
Achukue tu ila kama atasoma hii post yangu atambue kuwa sisi watumishi wa umma hatumpendi.
Wafanyabiashara nao hawampendi,
Wakulima wachache about 30 ndio wanampenda.
Yesu Kristo alipendwa na wengi lakin hawakukosekana waliomchukia, Adolph Hitler pamoja na mabaya yake tunayosimuliwa lakin bado kuna waliokuwa wanampenda sana, hata wewe hapo kutoka ktk jamii inayokuzunguka na ukoo wako pia wapo wanaokupenda na wasiokupenda pia wapo, hata watoto wako (kama unao) sio ajabu kukuta wapo wanaokupenda na wanaokuchukia.

Huyu bwana mkubwa aliyetoka kutibiwa juzi pamoja na kupambwa kwa mambo meeeeeengi, lakin wapo wanaompenda sana lakin hauwezi kupinga kwamba hakuna wanaomchukia tena sio ajabu hata alionao humo humo kwenye chama chake, halikadhalika kwa huyo mnaemuita jiwe, kuna watu huwaambii kitu kumuhusu huyo mzee wana mahaba nae ya dhati lakin wengine wanamchukia hadi wanaombea kwenye utawala wake nchi ipate majanga mazito yatakayopelekea vifo vya watu wengi, na ktk hao wengi watakaokufa nae afe
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
3,608
2,000
Hivi kuchukua channel zote na radio zote ni kuhakikisha mtu anao uhakika wa kusikia without kukosa au ni kulazimisha hata yule aliyetaka kusikiliza kingine kukosa channel ya kutizama ?.., Hizi pesa wangepeleka kwenye mfuko wa kusaidia watu huenda wasingehitaji kuwaambia watu walichofanya sababu watu wangekiona bila kukumbushwa
 

Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
25,051
2,000
Hivi kuchukua channel zote na radio zote ni kuhakikisha mtu anao uhakika wa kusikia without kukosa au ni kulazimisha hata yule aliyetaka kusikiliza kingine kukosa channel ya kutizama ?.., Hizi pesa wangepeleka kwenye mfuko wa kusaidia watu huenda wasingehitaji kuwaambia watu walichofanya sababu watu wangekiona bila kukumbushwa
Anaepusha Kuzimiwa Microphone
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom