CCM ndio hii, angalia anguko lake! Fomu ya Urais iuzwe Milioni 200!

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,411
1. Je, katika kumpata mgombea wake wa Urais kwa muhula wa pili, CCM inataka kurudi kwenye utaratibu wake uliokuwa ukitumika wakati wa mfumo wa chama kimoja ?

1.1 Wakati wa uchaguzi chini ya mfumo wa chama kimoja (1965, 1970, 1975 & 1980) Rais JK Nyerere hakuwahi kujaza fomu ya kugombea Urais, iwe kupitia TANU au CCM. Aidha, mwaka 1985 & 1990, Rais AH Mwinyi hakujaza fomu ya kugombea ya Urais. Hii ni kwasababu enzi hizo hakukuwa na utaratibu wa kujaza fomu bali jina la mgombea lilikuwa likipendekezwa na kisha kupitishwa kwenye Vikao vya juu vya chama.

1.2. Utaratibu wa wanachama wa CCM kujaza fomu ya kugombea Urais kupitia chama hicho ulianza mwaka 1995 baada ya kurudishwa mfumo wa vyama vingi. Mwaka huo, wanachama 17 walijaza fomu ya kugombea Urais kupitia CM ambapo Mhe Ben Mkapa alipitishwa na Mkutano Mkuu Julai 12, 1995 kuwa mgombea wa CCM.

1.3 Mwaka 2000, wakati muhula wa pili na wa mwisho wa Rais Mkapa, CCM ilisema mwanachama wake yeyote mwenye sifa anaruhusiwa kuchukua fomu ya kugombea Urais. Hata hivyo, hakuna aliyejitokeza zaidi ya Rais Mkapa.

1.4 Mwaka 2010, CCM ilialika wanaccm wenye sifa kujitokeza kuchukua fomu ya urais lakini ni Rais Kikwete pekee aliyechukua na kurudisha fomu hivyo akapitishwa na kisha kumalizia muhula wake wa pili.

1.5 Julai 12, 2020, Dkt. Bashiru Ali Kakurwa, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, alitangaza kuwa kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na "Jembe" Rais Dkt. John Magufuli, CCM imekuja na ubunifu mpya ambapo itachapisha fomu moja tu ya kugombea Urais kwaajili yake. Rais Magufuli akawa mgombea pekee.

1.6 Januari 2, 2024, Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa & M/Mwenyekiti wa CCM Mhe A. Kinana wakiwa Lindi, walishauri CCM ichapishe fomu moja tu kama ilivyokuwa 2020.

1.7 Mhe Stephen Wassira amekuja na ubunifu mpya kuwa hakuna haja ya kuchapisha hata hiyo fomu moja iwapo Rais aliyepo amehudumu kwa muhula mmoja bali jina litapendekezwa kwenye Vikao vya juu vya chama ili amalizie muhula wake wa pili na wa mwisho.

2. Je, kwa ubunifu huu mpya, CCM haioni kuwa inabinya demokrasia ndani ya chama licha ya kusema kuwa ndiyo utamaduni wake?*

3. Je, CCM haioni kuwa inapoteza chanzo kikubwa cha mapato?* ( fomu moja huuzwa Tshs 1,000,000/=).

4. Je, wazo hili la kutochapisha kabisa fomu ya kugombea Urais likipitishwa, nini itakuwa hatma ya mamilioni yaliyochangwa ili kumuwezesha Rais Samia kuchukua fomu?* TAHOSA (Umoja wa Waalimu wa Shule za Secondari nchini) licha ya changamoto lukuki walizonazo na licha ya kufahamu fika kuwa Sheria za Utumishi wa Umma zinawakataza, walijizima data na kumchangia Rais Samia !.

Aidha, CCM Tanga nao wakamchangia, Walimu Kagera nao pia. Aidha, Wakinamama nao wamemchangia. Hawa walitia fora kwani mbele ya Waziri Mkuu Majaliwa, wakichanga Tshs 120,000,000/= !. Kama ilivyoelezwa kwa weledi wa hali ya juu na viongozi mbalimbali wakati wa kutimiza miaka mitatu ya Rais Samia Machi 19, 2024, Rais Samia amefanya mambo makubwa katika kipindi kifupi na hata Steve Wonder au Morris Nyunyusa wanaweza kuona hakuna mtu pale CCM awezaye kupambana naye kwenye kinyanga'nyiro cha kuwa mgombea wa CCM 2025 lakini huu ubunifu mpya wa CCM una tija?
 
Usiseme CCM sema kikundi cha wachache ndani yake ambacho kinatengeneza wigo wa kuwatenganisha wao kama wao na wale bendera fuata upepo.
 
Kwanza kabisa namshukuru Mama kwa kuwa mwoga na kuhofia upinzani ndani ya chama chake licha ya yeye kuwa Mwenyekiti wa Chama na Amiri Jeshi Mkuu
 
Sasa nyie malaika Chadema leteni wagombea badala ya kulalamika mambo ya CCM yanawahusu Nini? Kama hamuwezi kushindana nyamazeni. Alipogombea Lowassa mlichapisha fomu ngapi?
Kila anayelalamika ni CHADEMA, kwahiyo ukiacha Wanachama 10 milion wa CCM waliobaki 40 milion ni CHADEMA?
 
1. Je, katika kumpata mgombea wake wa Urais kwa muhula wa pili, CCM inataka kurudi kwenye utaratibu wake uliokuwa ukitumika wakati wa mfumo wa chama kimoja ?

1.1 Wakati wa uchaguzi chini ya mfumo wa chama kimoja (1965, 1970, 1975 & 1980) Rais JK Nyerere hakuwahi kujaza fomu ya kugombea Urais, iwe kupitia TANU au CCM. Aidha, mwaka 1985 & 1990, Rais AH Mwinyi hakujaza fomu ya kugombea ya Urais. Hii ni kwasababu enzi hizo hakukuwa na utaratibu wa kujaza fomu bali jina la mgombea lilikuwa likipendekezwa na kisha kupitishwa kwenye Vikao vya juu vya chama.

1.2. Utaratibu wa wanachama wa CCM kujaza fomu ya kugombea Urais kupitia chama hicho ulianza mwaka 1995 baada ya kurudishwa mfumo wa vyama vingi. Mwaka huo, wanachama 17 walijaza fomu ya kugombea Urais kupitia CM ambapo Mhe Ben Mkapa alipitishwa na Mkutano Mkuu Julai 12, 1995 kuwa mgombea wa CCM.

1.3 Mwaka 2000, wakati muhula wa pili na wa mwisho wa Rais Mkapa, CCM ilisema mwanachama wake yeyote mwenye sifa anaruhusiwa kuchukua fomu ya kugombea Urais. Hata hivyo, hakuna aliyejitokeza zaidi ya Rais Mkapa.

1.4 Mwaka 2010, CCM ilialika wanaccm wenye sifa kujitokeza kuchukua fomu ya urais lakini ni Rais Kikwete pekee aliyechukua na kurudisha fomu hivyo akapitishwa na kisha kumalizia muhula wake wa pili.

1.5 Julai 12, 2020, Dkt. Bashiru Ali Kakurwa, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, alitangaza kuwa kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na "Jembe" Rais Dkt. John Magufuli, CCM imekuja na ubunifu mpya ambapo itachapisha fomu moja tu ya kugombea Urais kwaajili yake. Rais Magufuli akawa mgombea pekee.

1.6 Januari 2, 2024, Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa & M/Mwenyekiti wa CCM Mhe A. Kinana wakiwa Lindi, walishauri CCM ichapishe fomu moja tu kama ilivyokuwa 2020.

1.7 Mhe Stephen Wassira amekuja na ubunifu mpya kuwa hakuna haja ya kuchapisha hata hiyo fomu moja iwapo Rais aliyepo amehudumu kwa muhula mmoja bali jina litapendekezwa kwenye Vikao vya juu vya chama ili amalizie muhula wake wa pili na wa mwisho.

2. Je, kwa ubunifu huu mpya, CCM haioni kuwa inabinya demokrasia ndani ya chama licha ya kusema kuwa ndiyo utamaduni wake?*

3. Je, CCM haioni kuwa inapoteza chanzo kikubwa cha mapato?* ( fomu moja huuzwa Tshs 1,000,000/=).

4. Je, wazo hili la kutochapisha kabisa fomu ya kugombea Urais likipitishwa, nini itakuwa hatma ya mamilioni yaliyochangwa ili kumuwezesha Rais Samia kuchukua fomu?* TAHOSA (Umoja wa Waalimu wa Shule za Secondari nchini) licha ya changamoto lukuki walizonazo na licha ya kufahamu fika kuwa Sheria za Utumishi wa Umma zinawakataza, walijizima data na kumchangia Rais Samia !.

Aidha, CCM Tanga nao wakamchangia, Walimu Kagera nao pia. Aidha, Wakinamama nao wamemchangia. Hawa walitia fora kwani mbele ya Waziri Mkuu Majaliwa, wakichanga Tshs 120,000,000/= !. Kama ilivyoelezwa kwa weledi wa hali ya juu na viongozi mbalimbali wakati wa kutimiza miaka mitatu ya Rais Samia Machi 19, 2024, Rais Samia amefanya mambo makubwa katika kipindi kifupi na hata Steve Wonder au Morris Nyunyusa wanaweza kuona hakuna mtu pale CCM awezaye kupambana naye kwenye kinyanga'nyiro cha kuwa mgombea wa CCM 2025 lakini huu ubunifu mpya wa CCM una tija?
CCM ni shetani,na shetani hana Rafiki kwa waache wamalizane wao kwao kwa sababu wanachama wa CCM ni misukule tupu
 
Mama kaja kivingine huyu. Akiachwa aendelee hivi atakuja na gia ya kufuta ulazima wa kuhesabu kura za urais ktk uchaguzi mkuu 2025
 
Adhibitiwe,

Anaweza kuhujumu hata vyama vya upinzani visisimamishe mgombea urais.
 
Back
Top Bottom