Hayati Magufuli: Mimi sikuja kutafuta wachumba, nimekuja kufanya kazi

Magufuli 05

JF-Expert Member
May 7, 2023
942
1,986
Rais wetu wa Jamhuri tukufu ya Tanzania Hayati John pombe Magufuli, u hai.

U hai kwasababu Watanzania haipiti siku bila kukutaja kwa mema na kazi yako nzuri.

Rais wangu leo hii tarehe 17.03.2024 tunapoadhimisha siku yako rasmi ya kuitwa katika makazi ya milele, majonzi na huzuni hutawala katika mioyo yetu.

Toka umeondoka Rais wetu nchi yetu imekuwa ni kichwa cha mwendawazimu. Rais wetu miradi yote uliyoiasisi imeshindwa kukamilika. Ngoja nikutajie,
1. SGR haijakamilika
2. Bwawa la mlMwl. Nyerere halijakamilika.
3. Daraja Kigongo Busisi halijakamilika.
4. Uwanja wa mpira Dodoma haujajengwa
5. Barabara ya mwendokasi mbagala haijakamilika.
6. Uwanja wa ndege Mwanza haujakamilika
7. Ujenzi wa meli mpya na ukarabati wa meli ya liemba haujaanza.
8. Ujenzi wa meli mpya ya kwenda Comoro na Mauritius haujaanza.
9. Ujenzi na upanuzi wa viwanja vya ndege vya Shinyanga, Musoma, Iringa, Kigoma haujakamilika.

10. Ujenzi wa meli ya MV mwanza haujakamilika.
11. Ujenzi wa bonde la mto msimbazi haujaanza.

Nakukumbuka Sana hasa ucheshi wako, sauti yako ya mamlaka na umakini wako. Uliwapenda Watanzania, uliwasikiliza bila kujali Hali zao za kiuchumi na uwezo wao wa kufikiri.

Ulitumia muda mwingi kuwatembelea Watanzania, ulipita barabarani na si angani. Watanzania walikupenda na baadhi walitaka hata uongezwe miaka ya kuongoza.

Sauti yako kwa matapeli ilikuwa ni dawa tosha. Hukuwa na utani kwenye kazi. Aliyeharibu ulimuweka kando haraka, hukuwa na urafiki kazini. Wewe uliangalia zaidi kazi kwanza.

Ulisimama nasi hata kwenye nyakati ngumu, ulitutia moyo kuwa Watanzania tunaweza. Ulituhimiza kufanya kazi kwa bidii nasi tulihamasika na tukawa wazalendo wa kulipa Kodi na Kodi yetu tuliiona ikifanya kazi.

Ghafla ukafa, Watanzania walikulilia, akina mama, watoto, akina baba, vijana, askari na pia mzindakaya ambaye naye upo naye huko alikulilia na Mimi nilikulilia mno.

Rais Magufuli ninayo mengi ya kwako. Lakini itoshe kusema tu pumzika shujaa wa Africa, mwanamapinduzi wa kweli.

Hii ni siku yako, jina lako nimeliandika katika moyo wangu Hadi siku yangu ya mwisho Duniani. Sitakukana wala kukusaliti hata kama nitashikiwa bastola.

Hakika kifo hakina huruma
Pumzika JPM hutasahaulika.
 
1. Viongozi wa chadema hawakamatwi kamatwi
2. Hakuna kuunga mkono juhudi
3. Hakuna kesi za ajabu ajabu za kuhujumu uchumi
4. Hakun kujiona mungu mtu.
 
Ngoja nikusaidie kuweka picha ya mtumishi wa wote na mnyenyekevu wa taifa.
Magufuli.jpeg
 
Back
Top Bottom