Bunge limepitisha muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali namba 4 wa mwaka 2023 ambapo moja ya marekebisho katika sheria ya Mafao ya Kustaafu katika Utumishi wa kisiasa inapendekezwa Wenza (Mke/Mume) wa Marais Wastaafu, Wenza wa Makamu wa Rais Wastaafu na Wenza wa Mawaziri Wakuu Wastaafu walipwe kiinua mgongo kwa kipindi cha uongozi wa Wenza
wao.

Akiwasilisha marekebisho hayo leo Oktober 31,2023 wakati wa kikao cha Bunge Mjini Dodoma, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dk. Eliezer Feleshi amesema kuwa vifungu vipya vya 9A, 12A na 14A vinapendekezwa kuongezwa katika Sheria ya Mafao ya Kustaafu katika Utumishi wa Kisiasa, Sura ya 225.

Sambamba na marekebisho hayo, vifungu vya 11, 13 na 15 vinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka utaratibu wa malipo ya fadhila kwa Wenza wa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu endapo watafariki wakiwa madarakani au baada ya kumaliza muda wao na kufariki kabla ya kulipwa mafao au stahiki zao.

Kwa mujibu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kifungu cha 18 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka utaratibu wa wenza wa Spika Mstaafu aliyefariki kupokea mafao ya pensheni ya kila mwezi.

Muswada huo uliopitishwa utawasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aweze kuutazama muswada huo na akiuridhia atasaini ili iwe sheria.

#MillardAyoBUNGENI
Kujipendekeza kumezidi kiasi mpaka inaboa.
 
Pana jamaa nilikua namsikia sehemu kaongea kwa Uchungu sana aisee daah wacha niendelee kuwasikiliza ndugu zangu maana vitu vingine kwa akili ya kawaida hauwezi kufikiri kuwa watu watafikiri iwe sheria ila kwa kuwa wanapenda mazingira ya kuchota tuu kwa kutumia sheria zao wacha tuwasikilize ila huu ujinga wao una mwisho tu..
 
Maharamia wameteka mifumo yote, Maharamia wameiteka serikali, Maharamia wamevitaka vyama vya siasa, Maharamia wameteka baadhi ya raia wenye influence, Maharamia wameteka wasanii nk.

Maharamia wanatujua vizuri sana, wanazijua tamaa zetu, wanatujua tunapenda hivi vipande vya shillingi kuliko hata ustawi wa Taifa letu na watu wetu, wameweka brake hapo nakuteka kila kitu.

Nguvu ya pamoja na yenye nia ya dhati kabisa inahitajika kuusambaratisha mfumo wa kiharamia na kujenga misingi imara na mifumo strong itakayoilinda nchi dhidi ya uharamia wowote ule maana mpaka sasa hata ile mifumo tunayoamini inapaswa kutulinda na uharamia nayo imetekwa.

Lets be serious, kila mwenye uchungu na Taifa hili ni wakati sasa wa kusimama na kupambana na huu uharamia mpaka pale mifumo rafiki itakapozaliwa hata kwa sisi wote kufa..

Lazima tujitoe kuiokoa hii nchi ili vizazi vyetu vione namna gani babu zao tulikuwa serious, akina Mkwawa, Kimweri nk walipigana na kuupinga ukoloni ili tujitawale na tunufaike na rasilimari zetu wote kwa ujumla wetu lakini imekwenda vinginevyo maana uhuru feki umezalisha wahuni waliojitwalia Taifa hili na kulifanya lao na familia zao.... TUAMKE SASA.
 
Bunge limepitisha muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali namba 4 wa mwaka 2023 ambapo moja ya marekebisho katika sheria ya Mafao ya Kustaafu katika Utumishi wa kisiasa inapendekezwa Wenza (Mke/Mume) wa Marais Wastaafu, Wenza wa Makamu wa Rais Wastaafu na Wenza wa Mawaziri Wakuu Wastaafu walipwe kiinua mgongo kwa kipindi cha uongozi wa Wenza
wao.

Akiwasilisha marekebisho hayo leo Oktober 31,2023 wakati wa kikao cha Bunge Mjini Dodoma, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dk. Eliezer Feleshi amesema kuwa vifungu vipya vya 9A, 12A na 14A vinapendekezwa kuongezwa katika Sheria ya Mafao ya Kustaafu katika Utumishi wa Kisiasa, Sura ya 225.

Sambamba na marekebisho hayo, vifungu vya 11, 13 na 15 vinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka utaratibu wa malipo ya fadhila kwa Wenza wa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu endapo watafariki wakiwa madarakani au baada ya kumaliza muda wao na kufariki kabla ya kulipwa mafao au stahiki zao.

Kwa mujibu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kifungu cha 18 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka utaratibu wa wenza wa Spika Mstaafu aliyefariki kupokea mafao ya pensheni ya kila mwezi.

Muswada huo uliopitishwa utawasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aweze kuutazama muswada huo na akiuridhia atasaini ili iwe sheria.

Ikumbukwe mwaka mmoja uliopita aliyewasilisha Ombi hilo la wake wa marais walipwe, ni mke wa Kikwete Mama Salma Kikwete wakati akiwasilisha hoja hiyo Bungeni, ambapo tangu mwaka 2017 amekuwa akihudumu kama mbunge wa kuchaguliwa wa jimbo la Mchinga. Tizama video hii akiwasili hoja hiyo

View: https://youtu.be/pc9ZyIa6wkE?si=UwkRkNd9SoCT0jU5

Uroho tu, mtu alikua mwalimu, akawa mke wa Rais, bado akapewa ubunge , ana privileges kibao.
Bado anataka mafao mengine?
This is rubbish
 
Bunge limepitisha muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali namba 4 wa mwaka 2023 ambapo moja ya marekebisho katika sheria ya Mafao ya Kustaafu katika Utumishi wa kisiasa inapendekezwa Wenza (Mke/Mume) wa Marais Wastaafu, Wenza wa Makamu wa Rais Wastaafu na Wenza wa Mawaziri Wakuu Wastaafu walipwe kiinua mgongo kwa kipindi cha uongozi wa Wenza
wao.

Akiwasilisha marekebisho hayo leo Oktober 31,2023 wakati wa kikao cha Bunge Mjini Dodoma, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dk. Eliezer Feleshi amesema kuwa vifungu vipya vya 9A, 12A na 14A vinapendekezwa kuongezwa katika Sheria ya Mafao ya Kustaafu katika Utumishi wa Kisiasa, Sura ya 225.

Sambamba na marekebisho hayo, vifungu vya 11, 13 na 15 vinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka utaratibu wa malipo ya fadhila kwa Wenza wa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu endapo watafariki wakiwa madarakani au baada ya kumaliza muda wao na kufariki kabla ya kulipwa mafao au stahiki zao.

Kwa mujibu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kifungu cha 18 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka utaratibu wa wenza wa Spika Mstaafu aliyefariki kupokea mafao ya pensheni ya kila mwezi.

Muswada huo uliopitishwa utawasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aweze kuutazama muswada huo na akiuridhia atasaini ili iwe sheria.

#MillardAyoBUNGENI
Yaani wake za ma-Rais wastaafu walipwe pensheni kwa kazi ya kupigwa pumb*u na Marais??!??
Utawala wa nchi hii unatutia hasira sana sisi wananchi.
 
Back
Top Bottom