Jk haoni ndani kwa safari za kiongozi wa awamu ya 6, naona anaratiba ya kutembelea dunia nzima kwa kutumia ndege ya abiria 150 kubeba abiria 6 ..

Utadhani nyumbani umeme upo na maji yapo..
Screenshot_20240213-231514_YouTube.jpg
20240213_230209.jpg
 
Wewe pata picha mkeo tu hapo nyumbani anunue gauni jipya akipita atataka mtaa mzima wajue anapita au akienda kwenye sherehe atazunguka ukumbi mzima ili ijulikane yupo na amevaa gauni jipya same kwa Samia.

Bado hujaona wewe ngoja siku atakayoomba kikao na Kim Jong Un ndiyo utashangaa vizuri
 
Halafu hilo dege limesitisha kabisa safari za kwenda Guangzhou kisa safari za Hangaya zisizo na tija kwa wananchi wa kawaida, ughaibuni. :oops:
 
Mama toka nchi jirani ya Zanzibar katawala koloni la Tanganyika pasipo kutumia jeshi. Sasa kwann asitanue?
 
Ulishawahi kulala huna hata shilingi mfukoni halafu ile unaamka tu unapata bonge la dili la pesa ndefu.

Wenge lake unaweza hata kununua bucha zima. Hicho ndicho kilichomkuta Bi. Mdashi, alishajikubalia kuwa maisha yake ataishia kuzindua vyoo muda ukifika astaafu akapike kababu na wajukuu.

Ghafla kapata ngekewa ambayo hata hakuiwazia. Hii mizunguko yote ni wenge la madaraka. Haamini bado.
 
Huyo ndiye Rais wa nchi hiyo cheap popularity inaingiaje?

Mkitaka msitake yeye ndiyo kiongozi mkuu wa nchi na ndiye aliyeachiwa hatamu ya uongozi, mbona aliyepita kuna miradi aliiwacha hivyo hivyo?

Tuwe na subira, kwani yeye hajatoka upinzani ni kiongozi wa CCM ileile na ilani ileile kinachotofautiana ni utendaji tu. Ukizingua unazinguliwa.
"Mkitaka msitake yeye ndiyo kiongozi mkuu wa nchi", ni kweli kwani hatukumchagua bali alisimikwa kama usemavyo tukitaka tusitake.
 
Mimi sijui hata dira ya awamu ya sita ni ipi.
Ni awamu iliyoibiwa na inayoibiwa pesa kuliko Hali ya kawaida.
Ni awamu dhaifu kuliko hata udhaifu wenyewe.
Ni awamu iliyoshindwa kila kitu na badala imefanikiwa kwenye misele tu na kutembeza bakuli.
Ni awamu ya wapiga dili tu
Ni awamu ambayo kila mpiga dili aliyetoka kwenye mfumo awamu ya Tano anapambana kurudi kwenye mfumo ili ajiokotee maokoto.
Huduma za umma mbovu .
Ina madeni mpaka balaa.
Ni awamu nzuri kwa wazembe na watu wa dili.
Ni awamu chungu kwa wananchi wanyonge.
Imejaa ubabaishaji na nyimbo za kusifia tu.
Awamu hii itaiacha Tanzania masikini na haitaendelea kama inavyotarajiwa.
Imeshindwa kusambaza umeme wa REA vijijini kama kusudio lilivyokuwa la kufikiwa 2025 kila Kijiji kitakuwa na umeme. Imeshindwa kabisa kustabilize umeme.
Sasa pale tanesco hata mwendawazimu anafundishwa namna ya kukata umeme. Halafu wanasema bila aibu kuna wizi wa transformer. Anayeiba transformer anakwenda kuuza wapi au kwa matumizi Gani? Anaiba muda Gani? Hapigwi shoti yeye? Ana utalaamu Gani?
Awamu ya sita ni kichwa cha mwendawazimu.
Mbaya zaidi anataka kugombea eti naye achaguliwe kuwa Rais Tena. Unataka uwaumize Watanzania kwa miaka mingine mitano?
Mimi sitakuchagua ningali hai kafie mbali.
Aibu yako awamu ya sita na ufe kibudu.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Tundu alituambia 2017 Tanzania haijawahi kupata rais wa hovyo kama dr magufuli, lkn 2023 akiwa chato akaitisha maandamano ili akamwambie magufuli ainuke aje aendeleze kazi nzuri aliyoiacha, so hata rais wa awamu ya saba atakuja kuonekana wa hovyo mbele ya macho ya chadema make huwa hawana jema lolote na Dr samia watammisi.
 
Back
Top Bottom