Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki ibada ya kuaga Mwili wa Marehemu Mhe. Bernard Kamillius Membe, Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Viwanja vya Karimjee - Dares Salaam leo tarehe 14 Mei, 2023



Saa 4:00 Asubuhi
Viongozi Mbalimbali wa Kiserikali wakiongozwa na Waziri Mkuu wameanza kuwasili

Saa 5:45 Asubuhi
Mwili wa Marehemu Bernard Membe umewasili Karimjee ukiwa umebebwa kwenye gari Maalum la kubebea Maiti.

Saa 6:00 Mchana
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan anawasili.

Rais Samia amekwenda moja kwa moja kusaini kitabu cha Maombolezo kilichoandaliwa, kisha kusalimia na kuwapa pole wafiwa.

Saa 6:05 Mchana
Dua na Sala kutoka kwa viongozi mbalimbali wa Dini kisha salamu za viongozi wa Kiserikali na Kisiasa wamekaribishwa kutoa salamu zao.

Zitto Kabwe anazungumza; Amemuelezea Bernard Membe kama Mwanasiasa mkomavu aliyepambana kulinda heshima yake dhidi ya watu waoga walioshindwa kumkabili kwa hoja, ambapo baadhi ya viongozi na Watu wenye Mamkala walitumia Wahuni kutukana Viongozi wenzao.

Amesema Ushindi wake katika kesi ile utazika utamaduni huu mbaya wa kushambulia na kuchafua watu.

“Wewe sio tu ulizuia na kukemea upuuzi ule, bali ulihakikisha unatoa mfano kwa mpuuzi aliyebebeshwa upuuzi ule ili kuwa funzo kwa wapuuzi wengine wote”

Amesema kuwa anataraji wale wote waliohusika na mambo yale watamuomba radhi akiwa kwenye umauti.

IMG_7196.jpeg

Zitto Kabwe
Aidha, amemsifu kwa kusimama imara katika nyakati ngumu ambazo taifa lilipitia, nyakati ambazo watu wengi waliogopa kuisimamia kweli.

Amemshukuru kwa kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo ambapo aliwapa mafunzo na kuamsha ari ya kufanya kazi kwa bidii.

“Umetimiza wajibu, upumzike pema Membe… Tangulia BM, umeacha simanzi kubwa kwa watanzania. Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Upumzike pema mzee wangu Membe” Zitto Kabwe

Daniel Chongolo (Katibu Mkuu CCM) anazungumza; Amesema Chama cha Mapinduzi kimepokea kwa Masikitiko na Mshituko mkubwa kifo chake.

IMG_7197.jpeg


Daniel Chongolo, Katibu Mkuu CCM

Amesema CCM imepoteza kada wake mkubwa, na amewaomba watanzania na wana CCM kuenzi mema yake kwa kusimamia maslahi ya watanzania ndani na nje ya nchi.

Stergomena Lawrence Tax, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anazungumza; Ametoa pole kwa mjane wa Marehemu pamoja na watoto kwa kuondokewa mpendwa wao.

Amesema wakati wa uhai wake alitekeleza kazi zake kwa weledi mkubwa hasa katika kukuza uhusiano mwema kati ya Tanzania na mataifa mengine ambao nchi imenufaika sana na kazi zake.

IMG_7198.jpeg

Stergomena Lawrence Tax, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Alichangia katika kujenga mipango mizuri kwenye sera za nje.

Amemshukuru Membe kwa kumtia Moyo wakati alipoteuliwa kugombea ngazi ya kimataifa ambapo alikuwa nae bega kwa bega kuanzia hatua za mwanzo na muda wote wa kazi.

Rais Samia Suhulu Hassan anazungumza; Amesema kifo ni jambo lisiloepulika kwa binadamu, na wote tumepokea kwa huzuni taarifa hizo za kifo cha Membe.

Serikali, Familia ya Rais na watanzania wote tunaungana kwa pamoja kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na wanalindi wote kwa kumpoteza mpendwa wao.

IMG_7199.jpeg

Samia Suhulu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Rais amemsifu kwa kuwa mtu muungwana na kaka wa karibu aliyekuwa tayari kusadia wengine. Amesema maamuzi ya Mungu huwa hayalaumiwi bali hushukuriwa.

Amemalizia kwa kuwaomba watanzania kumuombea Membe roho yake ipumzike kwa amani.

Nape Nnauye anazungumza; Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akizungumza kwa niaba ya familia amemshukuru Rais Samia kwa kusimama bega kwa bega na familia ya Marehemu katika wakati huu mgumu ambapo gharama nyingi za msiba huu ikiwemo usafiri zimebebwa na Rais mwenyewe.

IMG_7200.jpeg

Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
Ameishukuru Wizara ya Mambo ya nje kwa kuwabeba, kwa moyo wa upendo walioonesha. Heshima hii hawataisahau.

Amewashukuru viongozi wote wa Serikali na Mkoa, Madaktari wa Hospitali ya Kairuki, majirani, waombolezaji, ndugu, jamaa na marafiki wote kwa umoja walioonesha.

Saa 7:30 Mchana:
Jeneza linafunguliwa ili waombolezaji watoe heshima za mwisho. Rais Samia anawaongoza waombolezaji.

Saa 7:50 Mchana
Zoezi la kuaga limehitimishwa Rasmi.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki ibada ya kuaga Mwili wa Marehemu Mhe. Bernard Kamillius Membe, Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Viwanja vya Karimjee - Dares Salaam leo tarehe 14 Mei, 2023


Mlio jirani na Karimjee, mmekasikia kale ka kauli kazuri ka wazuri hawafi?
 
Back
Top Bottom