Lema Alivuliwa Ubunge Na Mahakama, Alikata Rufaa Lakini Alifukuzwa Bungeni, Spika Hakusubiri Rufaa Yake Isikilizwe, Wabunge 9 wa CUF Walifukuzwa Uanachama. Walienda Mahakamani Lakini Walitolewa Bungeni, Spika Hakusubiri Kesi Yao Isikilizwe, Je Kwa Kina Halima Sheria Imebadilika?
 
Kichekesho mawakili wa kina Mdee wanaiomba mahakama iweke zuio wasivuliwe ubunge, wakati Tulia asubuhi kule bungeni alishasema hatawavua ubunge.

Inaonekana hawa wanawake 19 wakati wakifungua hii kesi hawakuwa wakijua mabosi wao ndani ya CCM wanawaza nini, wakaona bora wajilinde wenyewe..
 
Mbowe ni gaidi?
No Mbowe sio gaidi, hakuna mahakama iliyotoa uamuzi, case ya Mr.Mbowe imamelizwa kisiasa, it's pity na nchi yetu huwezi kuifungulia serikali kesi ya madai kwa muda wake uliopotezwa na wrong arrest kwake&others
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Kichekesho mawakili wa kina Mdee wanaiomba mahakama iweke zuio wasivuliwe ubunge wakati Tulia asubuhi kule bungeni alishasema hatawavua ubunge.

Inaonekana hawa wanawake 19 wakati wakifungua hik kesi hawakuwa wakijua mabosi wao ndani ya CCM wanawaza nini, wakaona bora wajilinde wenyewe..
aibu sana kwa tulia yaani anapwaya sana
 
Wakili Peter Kibatala na Wakili John Malya tayari wapo ndani ya Chumba Cha Mahakama Mbele ya Jaji Mgeta.

Jopo la mawakili wa Chadema lina mawakili wanne Adv. Kibatala Adv. Mtobesya Adv. J. Mndeme Adv. j. Malya Wengine. Kesi namba 16 ya Mwaka 2022, Mdee na Wenzake 18, ilifunguliwa Mahakama Kuu Mbele ya Jaji Mgeta.

Mdee na wenzake 18 Wanawakilishwa na Mawakili Adv Ikupilika Panya, Adv Edson Kilatu na Adv Aliko Mwamanenge. Baadae likaingia Jopo la Mawakili wa Serikali wapo Wanne Wakiongozwa na Wakili Gabriel Mallata.

Mawakili wa Mdee na wenzake wametoa ombi la Mahakama Iweke zuio "Court Injunction"Wasivuliwe Ubunge na Bunge. Wanaomba Kwanza Mahakama itoe zuio la Mdee na wenzake waendelee Kuwa wabunge mpaka pale ambapo Kesi ya msingi Kesi itakapoisha. Baada Wasilisho lao, Mahakama italazimika Kusikiliza Ombi hilo Kwanza kutoka pande zote.

Amesimama wakili Peter Kibatala anachambua kwanza Viapo vyao ambavyo vimesainiwa na Mawakili wao na Wateja (Wakina Mdee)
  1. Viapo havionyeshi waapaji (Wakina Mdee) Wameapa wapi.
  2. Waapaji hawajataja Dini zao katika Viapo vyote
  3. Ombi lao la kubaki na ubunge halijaelekezwa kwa yoyote kati ya wadaiwa (Mdee na wenzake)
  4. Katika maombi yao hawasemi kama wanataka kuendelea kuwa wanachama wa Chadema ila wanataka kuendelea na ubunge tu.
Mawakili wa CHADEMA wanaendelea Kuchambua Viapo na Kutaja Mahitaji ya Kisheria na sifa zinazohitajika katika Viapo wakiwa na Lengo Kuweka Zuio la awali, preliminary Objection (P.O) Mahakama isikubali Kupokea Maombi yao ya kesi.

Mawakili wa Halima Mdee na wenzake kwa pamoja na Mawakili wa Serikali Wanafanya (Re-joinder) Wanasimama kujibu hoja za Jopo la Mawakili wa Chadema Kuhusu hitilafu katika Viapo na Mapungufu yake katika ufunguaji wa Kesi.

Pia, soma=> Wabunge 19 viti maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama kuu
Kibatala kaaanza maswali yake ya kichokozi
 
Back
Top Bottom