Tamu au chungu kesi ya Halima Mdee na wenzake kujulikana kesho Desemba 14

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Mahakama Kuu kesho inatarajia kutoa uamuzi wa kesi ya kina Halima Mdee ambao ni wabunge wa viti maalumu waliofukuzwa uanachama katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa kesho Alhamisi Desemba 14, na Jaji Cyprian Mkeha aliyesikiliza kesi hiyo.

Mdee ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), na wenzake 18 walifungua kesi hiyo Mahakama Kuu Masjala Kuu, wakipinga kufukuzwa uanachama; kwa utaratibu wa Mapitio ya Mahakama.

Katika kesi hiyo kina Mdee wanapinga uamuzi wa Baraza Kuu la Chadema kutupilia mbali rufaa zao za kupinga uamuzi wa Kamati Kuu kuwafukuza uanachama kwa tuhuma za kuapishwa kuwa wabunge bila ridhaa ya chama.

Kamati Kuu iliwavua uanachama wa chama hicho Novemba 27, 2020. Walikata rufaa Baraza Kuu kupinga uamuzi huo wa Kamati Kuu lakini Baraza Kuu katika uamuzi wake wa Mei 11, 2022, lilitupilia mbali rufaa hiyo.

Baada ya uamuzi huo wa Baraza Kuu kutupilia mbali rufaa yao, ndipo wakakimbilia mahakamani ambako kwanza waliomba na wakapata kibali kufungua shauri hilo.

Kina Mdee wanaowakilishwa na jopo la mawakili wanne, Ipilinga Panya (kiongozi wa jopo), Aliko Mwananenge, Edson Kilatu na Emmanuel Ukashu wanapinga uamuzi wa Baraza Kuu la Chadema pamoja na mambo mengine wakidai kuwa hawakupewa haki ya kusikilizwa ambayo ni ya msingi.

Kutokana na hilo, wanaiomba Mahakama itengue mchakato na uamuzi huo, iamuru Chadema kutimiza wajibu wake kisheria, yaani kuwapa haki ya kuwasikiliza na itoe zuio kwa Spika wa Bunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuchukulia hatua yoyote mpaka malalamiko yao yatakapoamuriwa.

Hivyo Mahakama katika uamuzi wake huo inatarajiwa kuamua kama utaratibu uliotumika kuwavua uanachama wabunge hao ni sahihi ama laa kwa mujibu wa katiba ya chama hicho, sheria na Katiba ya nchi.

Kama Mahakama itaridhika kuwa utaratibu huo ulikuwa sahihi basi uanachama wao utakuwa umekoma ndani ya Chadema na moja kwa moja ubunge wao pia utakuwa umekoma.

Lakini kama Mahakama itaridhika kuwa utaratibu uliotumika haukuwa sahihi na ikakubaliana na hoja yao kwamba hawakupewa nafasi ya kusikilizwa katika rufaa yao ndani ya Baraza Kuu la Chadema, itabatilisha uamuzi huo wa baraza hilo kutupilia mbali rufaa zao.

Badala yake itaelekeza mchakato wa usikilizwaji wa rufaa zao uanze upya na wapewe nafasi ya kusikilizwa kabla ya baraza hilo kufikia uamuzi.

Hata hivyo upande wowote ambao hautaridhika na uamuzi huo wa kesho unaweza kukata rufaa kupinga, kama utaona kuna sababu na umuhimu wa kuchukua hatua hiyo.

Awali wakati kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa, jopo la mawakili wa Chadema likiongozwa na Peter Kibatala liliwaita kwa amri ya Mahakama wabunge wanane kati ya 19 akiwemo Mdee, wafike kizimbani kwa ajili ya kuwahoji kuhusiana na malalamiko yao waliyoyaweka katika kiapo chao walichokiwasilisha mahakamani ambao ni ushahidi wao.

Mbali na Mdee, wengine walioitwa walikuwa ni Nusrati Hanje, Ester Matiko, Ester Bulaya, Grace Tendega, Jesca Kishoa, Cecilia Pareso na Hawa Mwaifunga.

Hata hivyo mawakili wa Chadema waliamua kufunga mahojiano bila kuwahoji Mdee Bulaya na Matiko, licha ya kuwaita.

Baada ya mawakili hao wa Chadema kumaliza kuwahoji wabunge hao, mawakili wa kina Mdee pia waliiomba Mahakama iamuru wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Chadema waliosaini viapo kinzani walivyoviwasilisha mahakamani kupinga madai ya kina Mdee, ili kuwahoji kuhusiana na uhalali wa utaratibu uliotumika kuwavua uanachama.

Waliohojiwa ni Dk Azavery Lwaitama, Silivester Masinde, Ruth Mollel, Ahmed Rashid Hamis, Maulida Anna Komu na Francis Joseph Mushi, ambaye alikuwa wa mwisho kuhojiwa, huku Mary Joachim akishindwa kuhojiwa na mawakili hao kutokana na kushindwa kufika mahakamani kwa sababu ya ugonjwa.

Chanzo: Mwananchi
 
Kwakuwa maridhiano yamekufa then serikali itaikomoa Chadema kwa kumpa ushindi Mdee.

Na ikitokea mdee ameshinda basi makosa yatajirudia 2025. Wasishangae uchaguzi mkuu wa chama wakasikia umefanyika kichochoroni na Mdee ndio kashinda alafu msajili atabariki matokeo.

So ichukuliwe on a serious note.
 
denoo JG vipi ikitokea wakashinda ? Tuwafanye nn waliohusika kufanya uhuni huu?
Waliohusika wapo mpaka sasa wanaendelea kutuchezea kwa mambo mengi mengine na bado hatuna chakuwafanya, mgao wa umeme usio na ukomo na kupanda nauli za mabasi hivi karibuni, ni kielelezo vile wanavyotupeleka wanavyopenda.

Ndio maana sikuwataja makusudi pale juu, haikuwa bahati mbaya kutowazungumzia mkuu.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Waliohusika wapo mpaka sasa wanaendelea kutuchezea kwa mambo mengi mengine na bado hatuna chakuwafanya, mgao wa umeme usio na ukomo na kupanda nauli za mabasi hivi karibuni, ni kielelezo vile wanavyotupeleka wanavyopenda.

Ndio maana sikuwataja makusudi pale juu, haikuwa bahati mbaya kutowazungumzia mkuu.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Ok . Sawa. Hii ndiyo TanzaGIZA
 
Back
Top Bottom