Wanawake wenzangu mnawezaje kumsamehe a cheating husband?

Wanawake wenzangu mnawezaje kumsamehe a cheating husband?

Kwanini aachie ngazi wakati mumewe alitoka na hakuachia ngazi. Hapo anaenda kujipa raha nje bila kuathiri ndoa.
Hafu pia ukimchoka mtu kwanini msipeane space hata ya mwaka kila mtu afanye yake.
Kama ataweza kufanya bila kugundulika sawa ila ninalosema akigundulika kwake itakuwa mbaya zaidi ya ilivyokuwa kwa mwanaume. Tumeona wengi waliojaribu hio unalomshauri na wameishia pabaya. Yeye aende tu ila ninalojua litamwongezea matatizo baada ya Faraja. Atakuwa anakwenda huko siyo kwamba amepata mwanaume anayempenda ila kulipiza kwahiyo hata hilo tulizo anaweza asilipate pia na pia akaachika. Maamuzi ni kwake.
 
Na sitaki kugundua, the best way ni kwamb huwa simfatilii wala sifatilii mawasiliano yake, hata akiacha simu yake siigusi, hata ikiita sigusi kabisaa..nimejiwekea hiyo principle

Nafanya hivyo kulinda heshima na upendo uliopo ndani ya ndoa yetu,

Cha msingi anatimiza wajibu wake kama mume, kama baba, na kama kiongozi wa familia, he is always there when we need him na ananiheshimu

Hayo mengine sihitaji kujua. Hakuna viashiria na kama kuna tofauti tunazungumza yanaisha

Kwa kifupi, huyo dada atakua kwenye maumivu makali and it will take time to heal, ila pia kuvunja ndoa au kucheat in return does not make it right, asichukue sana ushauri wa mtandaoni ila afikirie future yake na watoto, na hata akisema atafute mchepuko, its likely possible kuumizwa zaidi ya maumivu aliyoyapata kwenye ndoa
Dada umezungumza yote yaliyo moyoni mwangu. Big up! Wakati mwingine wanawake wanayatafuta wenyewe na wakati hawana uwezo wa kuyahimili. Ni sawa unakwenda kupima lakini hauko tayari kwa matokeo hasi.
 
Mmmh Zoë!!

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kweli kabisa JF sijawahi kumsikia mwanaume anasema eti ana mwanamke mmoja, wala sijawahi kumsikia anayesema hana pesa.
 
Huyo mwanaume kama ameomba msamaha,nae ni kiazi..anatakiwa kukana everything....

Na huyo mwanamke kama anajitia hana mapenzi nae tena,ni well and good,na akijitusu tu nae a-cheat akishikwa ndio ndoa inafia hapo hapo siku hiyo hiyo.

Na kama ukikaa humo ndani ndio unajifanya humpendi tena,viburi,etc,unajipoteza tu maana huo usumbufu wa kukaa kama alien ni wako and he never cares what you actually feel maana nobody is in your heart or brain,she will sit on that shit...

Hivi viwanawake mume aki-cheat vinapaniki kupita maelezo ni visichana vya hovyo vyenye feminism ndani na vyenye theory ya mashindano
Nice kweli mkuu
 
Nikisomaga komenti za wababa humu Jf huwa najikuta nakata tamaa na siku yangu inaharibika kabisa. Ndio maana huwa sipendi kufungua nyuzi zinazohusu mambo ya ndoa
Kwakweli inavunja moyo.
 
Mwenzenu yamenikuta na kusema za ukweli nashindwa kabisa kuelewa namna ya kutoka hapa na kusonga mbele.

Ni mume nilompenda sana sana sana. Mungu katujaalia two beautifull kids na mengine ambayo am greatfull for. Tuliishi kwa upendo,furaha na amani hadi miezi 8 ilopita nilipogundua kuwa nilivyomdhania mume wangu sivyo alivyo.

Kwakuwa nampenda na kumfahamu sana mume wangu, kuna kitu nilikuwa tu nakihisi hakiko sawa kwa muda. Baadae nikagundua he was cheating. Yaani sitaki kuelezea mstuko niloupata na jinsi ninaumia jamani. Japo aliomba sana msamaha and all that ila moyo wangu umekufa ganzi wapendwa.

Mume nilompenda sana kwasasa namuona kama jirani yangu tu, hata hamu nae sina kabisa na hata tendo la ndoa ni kama ananibaka tu. Tushaongea sana, tushakwenda hadi vacation sie wawili tu ila sioni kinachobadilika. Akisafiri kikazi au mimi nikisafiri najisikia amani zaidi and i dont miss him kabisa.

Kuna wakati nilimuomba some alone time nifikirie kuhusu mustakabali wa hii ndoa, alinipa huo muda na kwa kipindi hicho cha wiki moja kichwani mwangu nilishangaa kunazunguka watoto wetu tu na sio mume wangu. Sijamueleza mtu yeyote kuhusu hili hata mama yangu wala mshenga wetu ila linanitafuna hatari.

Wenzangu mnawezaje kusamehe wanaume wanaowacheat na kurudi katika hali zenu za kawaida? Maana mie kwasasa mume wangu namuonaje sijui, nae naona hali hii inamtesa ila ndio hivyo tena[emoji134]
Sijisikii kumpenda wala kumheshimu tena, naona kama hadeserve kwa kutokuithamini na kuivuruga ndoa yetu.
Muache ukaolewe na mwanaume ambaye hacheat.
 
Embu tafuta kidume cha mbegu huko pembeni mi sijaolewa ila nikigundua mwanaume anachepuka huwa siumizi roho nani anapenda kuangalia mashine ile ile kila siku, yeye anatamani uchi mpya hata mimi natamani dushe jipya 😊😊😊😊 ninajifunza na style mpya huko niendako
Utakuta Wewe n mpole na umetulia na mumeo ni kiwembe lakini humu unamshauri mwenzako pumba
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] ndio huwa wanakimbilia kusema hilo neno wakiishiwa hoja. As if single mother ni tusi
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]kuna watu wamesha-iterm singomaza kama tusi.
 
Huwa tunaitumia hiyo excuse kuhalalisha kuendelea kuishi kweye ndoa na hao wazinzi (so far hata ndoa yenyewe kwenye spiritual realm inakuwa imeshavunjika). Inabidi tu niassume na kwa wenzangu kunawaka moto kama kwangu teh; ntafanyaje huku ndoa naitaka. It's wise kusema umeamua tu kuendelea kuishi na huyo mzinzi pamoja na yote (you don't owe anyone an explanation so far); kuliko kujifariji kuwa all men cheat ilhali unagugumia ndani kwa ndani

Hapa wengine tunajishaua all men cheat; ila tukihisi tu kuna mchepuko; tunautafuta then tunaenda kuanzisha timbwili au humo ndani kunawaka moto. Jiulize ni wangapi humu tukifumaniaga huwa tunawaambiwa waume zetu "hongera mume wangu; upo sawa tu kama wanaume wote? Kwa nini tuumie sasa ilhali hiyo ni tabia ya wanaume wote?

Bado wapo wanaume waaaminifu; wanaoheshimu wake zao, na viapo vyao vya ndoa kwa kutokuchepuka. Wengine ni personal decision tu kutokuchepuka; na wengine wanafanya hivyo kwa sababu ya hofu ya Mungu. Ndoa ni kitu chema sana; ndoa si kuishi na maumivu kama wengi wetu tunavyojifariji hapa. Although uaminifu sio chagamoto pekee kwenye ndoa; lakini uaminifu ukikosekana ni jambo la kujeruhi moyo sana. Kuna makosa mengi lakini usaliti sio tu ni kosa; bali ni kuvunja imani ambayo mtu alikuwa nayo juu yako. Ni gharama kubwa sana kurudisha imani ilivunjika; na kwa wengi ni kidonda kisichopona.

Let's stop legitimising nonsense. Usaliti sio tu kitu ambacho mtu anafanya kinapita. Usaliti umevunja ndoa nyingi; umetenganisha wazazi na watoto; watu wameambukizwa magonjwa yasiyotibika; familia zimetelekezwa hazina mbele wala nyuma. Kuna michepuko inaroga na kuua wake ili yenyewe iolewe afu baadaye watoto ndo wanateseka n.k. If one decides to settle for nonsense; it's very ok, but let us not propagate it. Ni upumbavu na ni ubatili

Mithali 6:26, 32-33

26. Maana kwa malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate;Na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani.

32 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa;Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.

33 Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima;Wala fedheha yake haitafutika.
Hiyo mithali 6:32 sijui wanaotetea uzinzi ni nature ya wanaume ndio tuseme wqnajijua kuliko Mungu aliewaumba.

Yani mtu amekomaa kabisa eti kuzini ni nature ya mwanaume aisee.


Kuzini sio nature ni kukosa akili(according to bible)

Asante kwa ushahidi wa vifungu m'am.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kweli kabisa JF sijawahi kumsikia mwanaume anasema eti ana mwanamke mmoja, wala sijawahi kumsikia anayesema hana pesa.
Ukiona hivyo ujuwe tunatamani hayo maisha mazuri ndio tunajaribu kuvaa uhusika[emoji23][emoji23]
 
Embu tafuta kidume cha mbegu huko pembeni mi sijaolewa ila nikigundua mwanaume anachepuka huwa siumizi roho nani anapenda kuangalia mashine ile ile kila siku, yeye anatamani uchi mpya hata mimi natamani dushe jipya 😊😊😊😊 ninajifunza na style mpya huko niendako
Utakuta Wewe n mpole na umetulia na mumeo ni kiwembe lakini humu unamshauri mwenzako pumba
 
wanawake wa laizer kule arusha mbona wametulia tu
Aliyekwambia wametulia nani? Au aliyekwambia wako happy nani? Nishakutana na binti wa kimasai pale namanga akaniambia yeye ni mke wa 6 na anaweza a kakutana na mme wake mara moja kwa mwaka kwa hiyo hamu zake anamalizia akija kufanya biashara zake ila nyumbani kila mke ana pretend ni mwema.
 
Wengi hapo wanamuona muhanga achukulie kawaida lakini haiwezekani kabisa si Duniani mpaka mbinguni

Ila sehemu moja ambayo wanaume wengi tunakosea ni kudhani kwamba sisi wanaume tuna haki miliki ya kusaliti na tunatakiwa kusamehewa ( ambapo huu mtazamo si sahihi)

Halafu usaliti ni hatua ndefu sana msaliti anaanzia mbali sana, usaliti wa bahati mbaya almost ni hakuna
Mungu akubariki.
 
Nawashauri kuwa msishindane na wanaume! Ukitaka kujua Mmeo akifumaniwa mahali bado aibu huja kwako na Wewe mkifumaniwa siku moja aibu bado itabaki kwako na si kwa mmeo! So pale ukaona mmeo kakucheat funga novena umuombee
Aisee
 
Aaaah hahaaa ni mhimu,ila kosa alilofanya ni kumuamini sana jamaa mpaka moyoni,achepuke ila akishikwa ataachwa yeye

California love
Aachwe kwa kipi? Mbona huyo mwanaume hajaachwa? Aaaaah hakuna tena ndoa hapo, waishi kwa mustakabali wa familia, ila upendo, furaha na amani watapata nje.

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom