Wanawake wenzangu mnawezaje kumsamehe a cheating husband?

nyakoo

JF-Expert Member
Dec 4, 2014
255
322
Mwenzenu yamenikuta na kusema za ukweli nashindwa kabisa kuelewa namna ya kutoka hapa na kusonga mbele.

Ni mume nilompenda sana sana sana. Mungu katujaalia two beautifull kids na mengine ambayo am greatfull for. Tuliishi kwa upendo,furaha na amani hadi miezi 8 ilopita nilipogundua kuwa nilivyomdhania mume wangu sivyo alivyo.

Kwakuwa nampenda na kumfahamu sana mume wangu, kuna kitu nilikuwa tu nakihisi hakiko sawa kwa muda. Baadae nikagundua he was cheating. Yaani sitaki kuelezea mstuko niloupata na jinsi ninaumia jamani. Japo aliomba sana msamaha and all that ila moyo wangu umekufa ganzi wapendwa.

Mume nilompenda sana kwasasa namuona kama jirani yangu tu, hata hamu nae sina kabisa na hata tendo la ndoa ni kama ananibaka tu. Tushaongea sana, tushakwenda hadi vacation sie wawili tu ila sioni kinachobadilika. Akisafiri kikazi au mimi nikisafiri najisikia amani zaidi and i dont miss him kabisa.

Kuna wakati nilimuomba some alone time nifikirie kuhusu mustakabali wa hii ndoa, alinipa huo muda na kwa kipindi hicho cha wiki moja kichwani mwangu nilishangaa kunazunguka watoto wetu tu na sio mume wangu. Sijamueleza mtu yeyote kuhusu hili hata mama yangu wala mshenga wetu ila linanitafuna hatari.

Wenzangu mnawezaje kusamehe wanaume wanaowacheat na kurudi katika hali zenu za kawaida? Maana mie kwasasa mume wangu namuonaje sijui, nae naona hali hii inamtesa ila ndio hivyo tena
Sijisikii kumpenda wala kumheshimu tena, naona kama hadeserve kwa kutokuithamini na kuivuruga ndoa yetu.
 
Pole dada
Najua inauma but trust me...muda ndo utakua tiba kwako.
Jipe muda ...endelea tu kujisikia unavyojisikia.

Na ili usaidike zaidi mtumie rafiki yako amjulishe jamaa kuwa asiache kucheat....aendelee tu mpaka hiyo ganzi unayoisikia itakapoondoka just like dat...

Hii solution imehakikiwa kisayansi na wala sio adithi. Nimeitumia na nimemsaidia mpenzi wangu. Siku hizi anajua kabisaaaaa me hawezi toshelezwa na ke mmoja
 
Hii inatokea , ila unapaswa kujua kuwa mwanaume yeyote aliye kamilika hanaga mwanamke mmoja hata awe rais wa nchi .

Kwahivyo unapaswa kumpenda tu mme wako na jua kuwa unaumia sana , ila hakuna namna nyingine!

Samahe maisha yaende mbele maana hautakuta mwanaume asiye toka nje ya ndoa sisi wanaume wote ndivyo tulivyo!
 
Unaongelea ndoa au kitu gani hiki?
 
Hii inatokea , ila unapaswa kujua kuwa mwanaume yeyote aliye kamilika hanaga mwanamke mmoja hata awe rais wa nchi .

Kwahivyo unapaswa kumpenda tu mme wako na jua kuwa unaumia sana , ila hakuna namna nyingine!

Samahe maisha yaende mbele maana hautakuta mwanaume asiye toka nje ya ndoa sisi wanaume wote ndivyo tulivyo!
"sisi wanume wote" is such a strong word. Things are not the same and i dont think they will ever be. Kama unaelewa maana ya ndoa lakini.
 
Jambo la msingi mwanaume ni kuipenda na kuijali familia yake yaani mke na watoto na kutimiza majukumu yake kama baba kakini hilo jambo unalipa uzito mkubwa kuliko uhalisia wake,ushauri ni kwamba hizo hasira weka pembeni fanya kama hakuna kilichotokea manufaa yake utakuja kuyaona.
 
kwanza elewa tuu sisi wanaume hatujaumbiwa mwanamke 1.kumbuka pia hata akicheat nje mapenz kwako hayataisha wala hatapunguza matumiz na watoto watasoma.ndio udhaifu tulio nao km nyie pia mna udhaifu wenu ingawa hamjielewi.unachofanya au kukosea ni kukosa apetite na huyo mmeo hilo ni kosa cha msingi wee mbadilishie style zile ambazo hamjawai kufanya yaani kiufupi ubadilike na usimtuhumu kwa chochote au kuonyesha hisia mbaya.mpende hivyo hivyo mpikie chakula kizuri umkaribishe kwa unyenyekevu badili mazingira yote ya mazoea!mfanye aone nyumbani ulipo wewe ni vantage point yake akute vitu ambavyo tofauti na anapochepukia na sio kumfanya ajione dhaifu kwa tuhuma unazompa.yaani mfanyie vitu ambavyo ataona siku zote alikuwa wapi kukufahamu.sisi wanaume akili yetu ndogo kututeka ni rahisi mno km kumpiga teke chura.soma hata majarida au tafuta watalam wakueleweshe jinsi ya kumkamata mume ili miaka yote aone hakuna mke km wee na sio kuonyesha chuki wazi waz au kuzira
 
Hukuwahi kujiandaa kuhusu mmeo kuchepuka, ukweli utabaki hivyo tu wanaume haturidhiki na mwanamke mmoja, hata ikitokea mmeshindwana kabisa usitegemee kumpata wa peke yako, utajihisi uko peke yako lkn nyuma ya pazia anawala sana.
Wewe tuliza akili utafakari upya, humpendi tena sawa, huna hamu nae tena sawa, je mkiachana unakoenda ni salama zaidi ya ulipo?
Pia kua makini unaweza jikuta umeadhirika kisaikolojia kiasi kwamba maisha yako yote hutakua na amani tena,
Kukosewa na kukosea pia kupo, kikubwa ni kusameheana tu maisha yaendelee
 
Mkosaji ni mume wako, kama amekiri na kuomba msamaha,basi,amani ya Nafsi yako na mwenza wako itategemeana na maamuzi yako ya kusamehe na kupuuza.

Kama unampenda kweli usije ukajaribu kulipa kisasi kwa kuchepuka,pia usipende kutegemea ushauri kwa watu wengine kwenye masuala ya ndoa maana unaye muomba ushauri yeye mwenyewe yupo kwenye mgogoro japo utakuwa tofauti na wako. Ukisikia "wanaume wote ni mambwa tu" ujue naye kaumizwa ila kiukweli sisi sio mambwa. Tukiomba msamaha ujue ni wa dhati kabisa.

Msamehe baby wako pluziii,anateseka huko aliko
tapatalk_1590244400462.gif
 
Mwenzenu yamenikuta na kusema za ukweli nashindwa kabisa kuelewa namna ya kutoka hapa na kusonga mbele.

Ni mume nilompenda sana sana sana. Mungu katujaalia two beautifull kids na mengine ambayo am greatfull for. Tuliishi kwa upendo,furaha na amani hadi miezi 8 ilopita nilipogundua kuwa nilivyomdhania mume wangu sivyo alivyo.
Kwakuwa nampenda na kumfahamu sana mume wangu, kuna kitu nilikuwa tu nakihisi hakiko sawa kwa muda. Baadae nikagundua he was cheating. Yaani sitaki kuelezea mstuko niloupata na jinsi ninaumia jamani. Japo aliomba sana msamaha and all that ila moyo wangu umekufa ganzi wapendwa.

Mume nilompenda sana kwasasa namuona kama jirani yangu tu, hata hamu nae sina kabisa na hata tendo la ndoa ni kama ananibaka tu. Tushaongea sana, tushakwenda hadi vacation sie wawili tu ila sioni kinachobadilika. Akisafiri kikazi au mimi nikisafiri najisikia amani zaidi and i dont miss him kabisa.

Kuna wakati nilimuomba some alone time nifikirie kuhusu mustakabali wa hii ndoa, alinipa huo muda na kwa kipindi hicho cha wiki moja kichwani mwangu nilishangaa kunazunguka watoto wetu tu na sio mume wangu. Sijamueleza mtu yeyote kuhusu hili hata mama yangu wala mshenga wetu ila linanitafuna hatari.

Wenzangu mnawezaje kusamehe wanaume wanaowacheat na kurudi katika hali zenu za kawaida? Maana mie kwasasa mume wangu namuonaje sijui, nae naona hali hii inamtesa ila ndio hivyo tena
Sijisikii kumpenda wala kumheshimu tena, naona kama hadeserve kwa kutokuithamini na kuivuruga ndoa yetu.
Utajijua bwana...

Muache uende huko duniani udhani wa huko ndio hawa-cheat ndio utaelewa vizuri...

Achika,wanawake wengine wamchukue na wewe uchukuliwe na hao wanaume ambao "hawacheat" wa kufikirika!

Hivi mwanaume ku-cheat ni ishu siku hizi?

Kwanza ulijuaje ana-cheat kwa kidhibiti kipi,tuanzie hapo maana utatuletea utoto wa nilikagua simu,ulitokana nayo wapi to begin with?
 
Back
Top Bottom