Usikubali kuonewa huruma, unastahili heshima

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
4,597
Reaction score
18,822
Happy Sabbath wanajamvi.

Si rahisi kugundua ni Kwa kiwango gani unapendwa,ni ngumu mno,ila bahati mbaya wanaume Tunajikuta si wapembuzi wa mambo.mtu anajikuta anaingia kwenye mtego wa SUBIRA na UVUMILIVU.

Leo ni siku nzuri ya jumamosi,siku ya mapumziko Kwa wahangaikaji ,wengi.nitumie fursa hii kuongea na wadogo zangu wengi ambao,Tukikutana mtaani ni wababe,wakatili wanajua vitu vingi ila nyuma ya pazia mahusiano yanawatesa mno.

Wengi wapo kwenye ndoa nzuri na zinatambulika kwenye jamii, lakini hiyo ndoa wanaijua wao,mke na mume🤔

Kwa utafiti wangu mdogo,yaani mdogo tu ni kama 80%.
Wanaume wanalizwa na kuumizwa na mapenzi kuliko wanawake,ni vile tu mambo huenda vibaya.

Na hata mizani inaonesha mwanaume ndiye anayeifurahia zaidi ndoa kuliko mwanamke.hii mizani ni Kwa utafiti wangu siyo utafiti rasmi.

Kwanini mwanaume anahitaji zaidi ndoa?

👉Inaleta utulivu na heshima kwenye jamii.

👉 Uwezo wa kujiamini na maamuzi makini.

👉Utulivu kazini. (Ukiwa na stress za mapenzi ni rahisi Sana kuharibu kazi)

👉 Utulivu na utimamu kiakili na kimwili.

Haya yote humpata mwanaume mwenye mwenza sahihi.

Lakini je wote tunaishi na wenza wanaotupenda?😂

Jibu hapa huenda ni hakuna,lakini niseme tu wengi wanaishi na wanawake waliokosa watu wanaowataka kisha kuwa na watu wengine ili maisha yaende.

Kwa mfano Mimi Daniel.

1. Ukiachana na NDOA yangu kudumu Kwa miaka yote hadi leo,japo vitimbi,misukosuko vilitokea mara nyingi,ila najua mke wangu alinipenda sana,tena sana na ukipendwa unajua tu.
Kupendwa Raha.

STORI NZIMA IKO HAPA
👇

2. Niliwahi kuwa na mpenzi nje ya mke wangu,wengi mnaita mchepuko,
Yeah ni mtu nilimpenda Sana,tena sana ila ,nilichukua muda kidogo kumpata ,japo kulikuwa na mawasiliano mara nyingi ila hakuwa tayari kuwa na Mimi,japo tuliweza kupiga stori za kawaida mara kadhaa.

Joto la mapenzi lilikuwa juu ,(wanaume wengi tunajua haswa Kwa Yule mtu ambaye hamjakutana kimwili) hakika alinitesa na kunivuruga,siku za mwanzo hakuwa anapokea zawadi zangu hili lilinitesa zaidi. Unajua niwaambie ukweli,

Mwanamke akila hela zako kisha akakukimbia inauma,lakini pia yule ambaye unamtaka kindakindaki halafu hataki kupokea chochote inaumiza pia (wachache watanielewa)

Basi niliendelea kuwa king'ang'anizi huku nikijipa kitu kinaitwa SUBIRA nikiamini MVUMILIVU hula mbivu na lazima nitafaidi,kweli nilianza kuona mwanga mbele ,baada ya kuombwa kitu fulani ambacho nilikuwa nacho.
Kiukweli nilifurahi sana nilijikuta mwili unasisimka mithili ya mtu aliyepigwa electric shock.

Nilitoa mara 5 ya nilichoombwa,hadi ikawa kero Kwa muhusika.maana ni kama alinimaindi fulani Ila nilijitetea kwani nilifanya tu Kwa upendo.

Iko hivi nisifiche,mtu alitaka atengenezewe TV yake inayozima kila ikijisikia.mimi nikaamua kununua TV mpya brand ileile nikaipeleka,kiasi cha kumkwaza Kwa namna fulani.

Basi bwana ,tuliendelea hivyo hivyo ,kila nikiomba naambiwa nitapewa kwani Nina haraka gani,😂muda si upo? Nikawa MVUMILIVU huku nikipiga hesabu ya vitu vilivyonitoka ni vingi na sijawahi kuombwa automatically ni kujipendekeza na kufosi mapenzi.

Kumbuka Nina mke na kuna wanawake kibao nawakataa ila nipo na mtu ambaye naona ni hadhi yangu na nitaingia kwenye rekodi ya kupiga mtu wa maana kabisa😂.

Lakini nisichokijua Kwa wakati huo ni kwamba mwanamke alikuwa ana mtu wake ambaye alikuwa Abroad na walipanga akirudi waoane,hili sikujua,ningejuaje sasa?
Wakati Mimi mwenyewe nachepuka tu. Ila laiti ningejua ...............,..................

Siku moja ,nakumbuka nilikuwa nipo kijiweni tu napiga stori na washikaji,

Mwanamke nayempenda na kumkubali akanitext,

Hello Dani mzima!!
Ningependa tuonane kama upo free.tuongee jambo.

Moyo ulilipuka,nilikuwa na kaulimbukeni fulani,sikuaga mtu yeyote huku Ile meseji nikiichungulia kila nikipata muda wa kufanya hivyo.

Kweli nilifika home nikajimwagia maji maana kule si kuoga,nikachagua casual clothes nikaelekea sehemu husika huku nikiwa na bashasha,nikipanga kutumia fursa Ile kuzidi kukumbushia mambo yangu.

Kweli,tulikutana tukaongea huku tukianzisha rasmi mahusiano na kiukweli mwanamke wa watu alikuwa very romantic na mwenye mapenzi ya kweli,Hadi Mimi nikawa najisifu Kwa kuwa mwenye SUBIRA na UVUMILIVU.😋😋😋

Tuliweza kukutana kila nikimuhitaji hakukuwa na nyodo wala maringo nikawa najiona ndiye mwanaume mwenye mchepuko mzuri kuliko wote

Sasa siku moja bwana washikaji zangu walinialika sehemu tukapate kilaji,so kama ilivyo kawaida wanaume kuringishiana na kutambiana nikampigia yule demu haoo Hadi sehemu husika,halooo wanaume wenzangu wote walinipigia saluti
, Dani huwa hukosei,Dani wee ni mnoma vicheko vikatawala mambo yanaenda.
Na mchepuko wangu alikuwa very very very Educated kwahiyo ukikaa naye hakika unajivunia kuwa naye ,lakini pia Sura nzuri

Kigezo namba moja Kwangu Kwa mwanamke siyo figga,umbile au nini ni Sura kwanza.

Basi bwana tumeenda miezi ikapita demu akaanza kubadilika simu hapokei Kwa wakati,text hajisumbui kujibu lakini kubwa zaidi majibu ya mkato,na kusisitiza nijikite zaidi Kwa mke wangu Mimi nisimtegemee.

👉Sikia Dani Mimi si mkeo,kwahiyo usifanye kama Una wake wawili unagawa zamu,nikiwa Nina hamu na wewe nitakutafuta.📌

Mimi:Lakini my love unajua ni jinsi gani nimejitoa kwako ,naweza sema nimehamisha upendo wote nimeleta kwako,sihitaji sex. Nahitaji muda ,nahitaji kufurahi pamoja na wewe.tafadhali niambie kama kuna mahali nimekukwaza sema nirekebishe,Mimi pia ni binadamu.

👉 Daniel Acha ujinga, yaani uhamishe upendo Kwa mke aliyekuzalia,anakupikia,anakupa chochote Kwa muda sahihi,halafu uhamishie kwangu,Acha ushamba wewe.hujakosea sehemu,labda niseme sina hisia na wewe ,siku nikiwa sawa nitakutafuta.📌

Maneno yale yaliniumiza moyo ,nikijiangalia wanawake wengi hunisifia Kuwa ni mmoja wa wanaume hodari,Kwa huyu nimefeli wapi?

Wanawake wengi huniita Mimi ni handsome,ina maana yeye haoni kama Mimi ni handsome,niliwaza kitoto.

Hakuna jambo baya kuwa na demu uliwaringishia washikaji,halafu penzi linakufa ,mbaya zaidi Wana na washikaji utawasikia vipi Yule shemu wetu mwingine hajambo?
Inakera.

Nikajikuta najipa kibarua cha kuanza kumchunguza kupitia marafiki zake, aiseee nilijuta kuyajua.

Kumbe mshikaji aliyekuwa Ng'ambo masomoni na alikuwa ana mawe,lakini ni alimuahidi demu ndoa,sema ubize wa mshikaji ukafanya demu anikubalie yaani nilikuwa backup.

Nilikuwa mtu wa Ziada,
Nilikuwa kipoza machungu,
Nilishikilia siti ya mtu Kwa muda sikuwa msafiri rasmi😂😂😂

Licha ya kujua yote niliumia kimyakimya,hata demu sikumwambia .Hadi siku moja aliponipigia simu na kuniamibia haya

👉Juzi Daniel nasikia ulipita pale ofisini,kama ulipita kuomba kazi sawa,kama ni kunifuata Mimi naomba tuheshimiane,sitaki mahusiano yeyote na wewe tena sawa?.📌

Mimi :salimia basi Kwani tuna ugomvi mpenzi wangu.

👉Mimi siyo mpenzi wako Dani nimejikuta tu niwe peke yangu ili niwe huru zaidi, kwahiyo fanya kama hukuwahi kunijua.

Mimi :Au Una mwanaume mwingine (niliuliza kama vile sijui)

👉 Sina,na hata kama ningekuwa naye wewe anakuhusu nini,Mimi ni nani wako Hadi utake kujua mambo yangu,unikome kaka,hii simu iwe ya mwisho usije kupiga labda kama unatafuta matatizo

Akakata simu,nilicheka kama vile masihara lakini niliumia,kumbe tangu mwanzo sikupendwq,nilikuwa najipendekeza tu kweli , mapenzi hayana formula nikiipenda familia yangu inatosha.

Ndugu msomaji,

Unadhani ni wangapi wamefanywa backup baada ya watu wao kuwa hawaeleweki,yaani anakukubalia kwakuwa mtu sahihi ,hayupo au ni maelewano?😂

Usifanye makosa kama mimi ukiona demu unatumia nguvu nyingi na siku kibao kutongoza ,na kufukuzia shtuka fanya mambo mengine kabla hujanasa kisha uje uachwe solemba.

Mchana mwema karibuni baadaye nitakuwa mabibo pale Ibungu tupate local beer 🍺
 
Umefanywa jiwe la kuvuka mto...siyo wewe tu; naamini wanaume wengi tumepitia mapito ya kufanana mpaka kumpata mwenza aliye sahihi.

Nilichojifunza kupitia kisa hiki; ukikataliwa kubali na usonge mbele. Mambo mengine ni ya kupita tu na kuweka historia
 
Nipo katika situation hiyo asa hivi ninajidanganya kuwa subira na uvumilivu kwa mtoto huyu wa kishua.

Ukweli ni kwamba sipendwi nafosi penzi unaenda mwezi wa Tisa .alooo ni kwele
Vumilia mkuu, siku akigombana na jamaa yake atakuja kukutunuku maana hasira zao mda mwingine ni kukigawa kipochi chao wamkomoe mwanaume. Labda kuna siku ataona kuna kitu atafaidika kwako ila akishakipata atakuacha solemba kama kawaida.Mvumilivu hula mbivu,.. Akija chapa na ukae kijanja😁
 
Umefanywa jiwe la kuvuka mto...siyo wewe tu; naamini wanaume wengi tumepitia mapito ya kufanana mpaka kumpata mwenza aliye sahihi.

Nilichojifunza kupitia kisa hiki; ukikataliwa kubali na usonge mbele. Mambo mengine ni ya kupita tu na kuweka historia
Ni sahihi kaka
 
Happy Sabbath wanajamvi.

Si rahisi kugundua ni Kwa kiwango gani unapendwa,ni ngumu mno,ila bahati mbaya wanaume Tunajikuta si wapembuzi wa mambo.mtu anajikuta anaingia kwenye mtego wa SUBIRA na UVUMILIVU.

Leo ni siku nzuri ya jumamosi,siku ya mapumziko Kwa wahangaikaji ,wengi.nitumie fursa hii kuongea na wadogo zangu wengi ambao,Tukikutana mtaani ni wababe,wakatili wanajua vitu vingi ila nyuma ya pazia mahusiano yanawatesa mno.

Wengi wapo kwenye ndoa nzuri na zinatambulika kwenye jamii, lakini hiyo ndoa wanaijua wao,mke na mume🤔

Kwa utafiti wangu mdogo,yaani mdogo tu ni kama 80%.
Wanaume wanalizwa na kuumizwa na mapenzi kuliko wanawake,ni vile tu mambo huenda vibaya.

Na hata mizani inaonesha mwanaume ndiye anayeifurahia zaidi ndoa kuliko mwanamke.hii mizani ni Kwa utafiti wangu siyo utafiti rasmi.

Kwanini mwanaume anahitaji zaidi ndoa?

👉Inaleta utulivu na heshima kwenye jamii.

👉 Uwezo wa kujiamini na maamuzi makini.

👉Utulivu kazini. (Ukiwa na stress za mapenzi ni rahisi Sana kuharibu kazi)

👉 Utulivu na utimamu kiakili na kimwili.

Haya yote humpata mwanaume mwenye mwenza sahihi.

Lakini je wote tunaishi na wenza wanaotupenda?😂

Jibu hapa huenda ni hakuna,lakini niseme tu wengi wanaishi na wanawake waliokosa watu wanaowataka kisha kuwa na watu wengine ili maisha yaende.

Kwa mfano Mimi Daniel.

1. Ukiachana na NDOA yangu kudumu Kwa miaka yote hadi leo,japo vitimbi,misukosuko vilitokea mara nyingi,ila najua mke wangu alinipenda sana,tena sana na ukipendwa unajua tu.
Kupendwa Raha.

STORI NZIMA IKO HAPA
👇

2. Niliwahi kuwa na mpenzi nje ya mke wangu,wengi mnaita mchepuko,
Yeah ni mtu nilimpenda Sana,tena sana ila ,nilichukua muda kidogo kumpata ,japo kulikuwa na mawasiliano mara nyingi ila hakuwa tayari kuwa na Mimi,japo tuliweza kupiga stori za kawaida mara kadhaa.

Joto la mapenzi lilikuwa juu ,(wanaume wengi tunajua haswa Kwa Yule mtu ambaye hamjakutana kimwili) hakika alinitesa na kunivuruga,siku za mwanzo hakuwa anapokea zawadi zangu hili lilinitesa zaidi. Unajua niwaambie ukweli,

Mwanamke akila hela zako kisha akakukimbia inauma,lakini pia yule ambaye unamtaka kindakindaki halafu hataki kupokea chochote inaumiza pia (wachache watanielewa)

Basi niliendelea kuwa king'ang'anizi huku nikijipa kitu kinaitwa SUBIRA nikiamini MVUMILIVU hula mbivu na lazima nitafaidi,kweli nilianza kuona mwanga mbele ,baada ya kuombwa kitu fulani ambacho nilikuwa nacho.
Kiukweli nilifurahi sana nilijikuta mwili unasisimka mithili ya mtu aliyepigwa electric shock.

Nilitoa mara 5 ya nilichoombwa,hadi ikawa kero Kwa muhusika.maana ni kama alinimaindi fulani Ila nilijitetea kwani nilifanya tu Kwa upendo.

Iko hivi nisifiche,mtu alitaka atengenezewe TV yake inayozima kila ikijisikia.mimi nikaamua kununua TV mpya brand ileile nikaipeleka,kiasi cha kumkwaza Kwa namna fulani.
Basi bwana ,tuliendelea hivyo hivyo ,kila nikiomba naambiwa nitapewa kwani Nina haraka gani,😂muda si upo? Nikawa MVUMILIVU huku nikipiga hesabu ya vitu vilivyonitoka ni vingi na sijawahi kuombwa automatically ni kujipendekeza na kufosi mapenzi.

Kumbuka Nina mke na kuna wanawake kibao nawakataa ila nipo na mtu ambaye naona ni hadhi yangu na nitaingia kwenye rekodi ya kupiga mtu wa maana kabisa😂.

Lakini nisichokijua Kwa wakati huo ni kwamba mwanamke alikuwa ana mtu wake ambaye alikuwa Abroad na walipanga akirudi waoane,hili sikujua,ningejuaje sasa?
Wakati Mimi mwenyewe nachepuka tu. Ila laiti ningejua ...............,..................

Siku moja ,nakumbuka nilikuwa nipo kijiweni tu napiga stori na washikaji,

Mwanamke nayempenda na kumkubali akanitext,

Hello Dani mzima!!
Ningependa tuonane kama upo free.tuongee jambo.

Moyo ulilipuka,nilikuwa na kaulimbukeni fulani,sikuaga mtu yeyote huku Ile meseji nikiichungulia kila nikipata muda wa kufanya hivyo.

Kweli nilifika home nikajimwagia maji maana kule si kuoga,nikachagua casual clothes nikaelekea sehemu husika huku nikiwa na bashasha,nikipanga kutumia fursa Ile kuzidi kukumbushia mambo yangu.

Kweli,tulikutana tukaongea huku tukianzisha rasmi mahusiano na kiukweli mwanamke wa watu alikuwa very romantic na mwenye mapenzi ya kweli,Hadi Mimi nikawa najisifu Kwa kuwa mwenye SUBIRA na UVUMILIVU.😋😋😋

Tuliweza kukutana kila nikimuhitaji hakukuwa na nyodo wala maringo nikawa najiona ndiye mwanaume mwenye mchepuko mzuri kuliko wote

Sasa siku moja bwana washikaji zangu walinialika sehemu tukapate kilaji,so kama ilivyo kawaida wanaume kuringishiana na kutambiana nikampigia yule demu haoo Hadi sehemu husika,halooo wanaume wenzangu wote walinipigia saluti
, Dani huwa hukosei,Dani wee ni mnoma vicheko vikatawala mambo yanaenda.
Na mchepuko wangu alikuwa very very very Educated kwahiyo ukikaa naye hakika unajivunia kuwa naye ,lakini pia Sura nzuri

Kigezo namba moja Kwangu Kwa mwanamke siyo figga,umbile au nini ni Sura kwanza.

Basi bwana tumeenda miezi ikapita demu akaanza kubadilika simu hapokei Kwa wakati,text hajisumbui kujibu lakini kubwa zaidi majibu ya mkato,na kusisitiza nijikite zaidi Kwa mke wangu Mimi nisimtegemee.

👉Sikia Dani Mimi si mkeo,kwahiyo usifanye kama Una wake wawili unagawa zamu,nikiwa Nina hamu na wewe nitakutafuta.📌

Mimi:Lakini my love unajua ni jinsi gani nimejitoa kwako ,naweza sema nimehamisha upendo wote nimeleta kwako,sihitaji sex. Nahitaji muda ,nahitaji kufurahi pamoja na wewe.tafadhali niambie kama kuna mahali nimekukwaza sema nirekebishe,Mimi pia ni binadamu.

👉 Daniel Acha ujinga, yaani uhamishe upendo Kwa mke aliyekuzalia,anakupikia,anakupa chochote Kwa muda sahihi,halafu uhamishie kwangu,Acha ushamba wewe.hujakosea sehemu,labda niseme sina hisia na wewe ,siku nikiwa sawa nitakutafuta.📌

Maneno yale yaliniumiza moyo ,nikijiangalia wanawake wengi hunisifia Kuwa ni mmoja wa wanaume hodari,Kwa huyu nimefeli wapi?

Wanawake wengi huniita Mimi ni handsome,ina maana yeye haoni kama Mimi ni handsome,niliwaza kitoto.

Hakuna jambo baya kuwa na demu uliwaringishia washikaji,halafu penzi linakufa ,mbaya zaidi Wana na washikaji utawasikia vipi Yule shemu wetu mwingine hajambo?
Inakera.

Nikajikuta najipa kibarua cha kuanza kumchunguza kupitia marafiki zake, aiseee nilijuta kuyajua.

Kumbe mshikaji aliyekuwa Ng'ambo masomoni na alikuwa ana mawe,lakini ni alimuahidi demu ndoa,sema ubize wa mshikaji ukafanya demu anikubalie yaani nilikuwa backup.

Nilikuwa mtu wa Ziada,
Nilikuwa kipoza machungu,
Nilishikilia siti ya mtu Kwa muda sikuwa msafiri rasmi😂😂😂

Licha ya kujua yote niliumia kimyakimya,hata demu sikumwambia .Hadi siku moja aliponipigia simu na kuniamibia haya

👉Juzi Daniel nasikia ulipita pale ofisini,kama ulipita kuomba kazi sawa,kama ni kunifuata Mimi naomba tuheshimiane,sitaki mahusiano yeyote na wewe tena sawa?.📌

Mimi :salimia basi Kwani tuna ugomvi mpenzi wangu.

👉Mimi siyo mpenzi wako Dani nimejikuta tu niwe peke yangu ili niwe huru zaidi, kwahiyo fanya kama hukuwahi kunijua.

Mimi :Au Una mwanaume mwingine (niliuliza kama vile sijui)

👉 Sina,na hata kama ningekuwa naye wewe anakuhusu nini,Mimi ni nani wako Hadi utake kujua mambo yangu,unikome kaka,hii simu iwe ya mwisho usije kupiga labda kama unatafuta matatizo

Akakata simu,nilicheka kama vile masihara lakini niliumia,kumbe tangu mwanzo sikupendwq,nilikuwa najipendekeza tu kweli , mapenzi hayana formula nikiipenda familia yangu inatosha.

Ndugu msomaji,

Unadhani ni wangapi wamefanywa backup baada ya watu wao kuwa hawaeleweki,yaani anakukubalia kwakuwa mtu sahihi ,hayupo au ni maelewano?😂

Usifanye makosa kama mimi ukiona demu unatumia nguvu nyingi na siku kibao kutongoza ,na kufukuzia shtuka fanya mambo mengine kabla hujanasa kisha uje uachwe solemba.

Mchana mwema karibuni baadaye nitakuwa mabibo pale Ibungu tupate local beer 🍺
UZURI WA MWANAMKE UPO MACHONI PA MTU
 
Mbona kila siku tunawaambia humu kuwa mwanamke akikupenda hutotumia hata wiki 2 kumfuatilia kabla akubali.

Kama mko kwenye same proximity na huwa mnaonana, anaweza kukubali hata siku ya kwanza umeenda kumtongoza, chances are… huwa anakuchunguza kimya kimya.

Kama mmeonana ghafla let’s say safarini, haichukui walau wiki 2 za kuongea na wewe na kutick viboksi (vigezo) alivyojiwekea.
 
Back
Top Bottom