Rahisi sana kuishi na mke akiwa na mimba, fuata masharti yote anayo kupa, tenga muda wa kutosha wa kuwa karibu naye, punguza marafiki wenye mtazamo tofauti, usijaribu kuwa na mchepuko kipindi hiki.
Siku ya kujifungua muombe daktari uwepo chumba cha kujifungulia. Utakapoona zile damu na maumivu anayopitia haki ya Mungu nakuapia kuanzia siku hiyo utaapa kwa miungu yako yote kuwa mke akitoka hapa salama hautamtenda kwa baya lolote. Hilo Agano linakuja automatikale na lina dumu sana. Pia mke anakuchukulia kama ni mtu mwenye upendo na unaye jali sana. Anajikuta anakupenda na kukuheshimu.
Kwanini uchepuke? Ile kitu kama haikuchanwa kuongeza njia ni siku tano tu na kama alichanwa ruhusu mwezi upite inakuwa tayari kwa matumizi halali ya nyumbani.
Muhimu:vaa condom kuepuka mimba na usinyonye maziwa maana utakuwa una dhurumu haki ya mtoto.