Wanaume acheni kudhalilisha miili ya wanawake

Wanaume acheni kudhalilisha miili ya wanawake

Akivaa nguo fupi hajastiri mwili wake? amstirie nani au anamuogopa nani na kwanini hadi avae migauni bululu bululu? Tena kwa taarifa yako hao wabakaji wanaongoza kwenye maeneo ya wanawake wanaovaa migauni na misketi mirefu
Haya sasa si haonei aibu mtu? Hayo ndio madhara anayokutana nayo
 
This is what we call internalized misogyny effects.

Somehow somewhere unaamini mwanamke akivaa vibaya inahalalisha kufanyiwa vitendo vya uzalilishaji, bado hamjafahamu tatizo ninini na tatizo linaanzia wapi, unadhani katika jamii wanazovaa stara hakuna ubakaji? Kama upo unauelezeaje?

Ukiachana na wanawake kuvaa hovyo, watoto wadogo wa kike na wakiume wanabakwa kwasababu zipi? Vikongwe je? wanabakwa kwanini na wanabakwa nani?

Naelewa unakotokea, sio mara moja mtu kureport kufanyiwa udhalilishaji, mwingine tena mwanamke anauliza kwani alivaaje 😏 Normalize kudeal na tatizo na sio kumlaumu victim. Wabakaji watatafuta justification za kubaka kila leo hata kama jamii nzima tutakuwa tunavaa majuba.
Upo sahihi mkuu, hili nililolisema sio justification ya moja kwa moja. Ni moja ya sababu tu, cases za ubakaji zinaweza kutokea kwasababu ya maadili mabovu ya baadhi ya wanaume, imani za kishirikina, changamoto ya afya ya akili, bila kusahau vileo..(Pombe na mibangi).

“Naelewa unakotokea” Hahaha! Unaweza usiwe sahihi mkuu, ni wapi huko? 😁😁
 
Guys, wallah leo nimechafukwa sana ukija hapa uje na akili timamu, nina kirungu changu ukileta uzwazwa nakubwenga cha utosi akili ikukae sawa,

Matukio ya ubakaji wanawake na watoto wa kike ni mengi hadi natetemeka lakini haya yote yanaletwa na wanaume wapumbavu wanaoangalia mwili wa mwanamke kama chombo cha starehe,

Hivi nyie wanaume miili ya wanawake ina tofauti gani na yenu? ile kujazia jazia hata nyie mmejazia, wembamba hata nyie kuna wembamba, manyonyo hata nyie kuna wenye nayo, nini shida jamani mbona mnatukosesha amani wanawake?

Mwanamke akivaa kiguo chake kifupi atembee kwa raha zake inakua gumzo lakini mwanaume akivaa kiguo kifupi husikii kabakwa au kadhalilishwa, miili mbona ni ile ile tu,

Mbona watu wa zamani walikua wanaishi uchi na hakukua na matukio ya ubakaji wala udhalilishwaji, hiki nini mnafanya nahisi hadi kichefu chefu,

Ifike mahala sasa tutaichukua heshima yetu kwa nguvu, haiwezekani kila siku nyinyi tu, kuna wengine humu humu hizo tabia chafu mnazo, unajisikiaje kushika titi la mwanamke bila ridhaa yake au kushika tako la mwanamke ambaye huna mahusiano nae?,

Hakuna mwili unaohalalisha ubakaji,
Hakuna vazi linalohalalisha ubakaji,
Hakuna tabia inayompa mtu haki ya kuvuka mipaka ya mwingine,

Tujenge jamii inayohehimu wanawake bila kufanya miili yao kua sababu ya lawama au udhalilishaji,

Nikisema hii gender ifutwe naitwa feminist.
gender ifutwe? gender ipi? si uifute unasubiri nini? kwanza wewe ndiyo nani? matako na matiti tutaendelea kushika na hakuna kitu utafanya... kwani tunakushika wewe? mbona tunaowashika hawalalamiki?

acha wivu au tukushike wewe nini? nyambafu mnuka shuzi la dona na kisamvu.
 
Jaribu kujichunguza vizuri kwenye uumbaji utakuja kugundua mwanamke alivyoumbwa nikama chombo cha starehe.
Pia Inasikitisha sana kuhusianisha namna mnavyo vaa na ubakaji mwanamke vaa unavyo vaa ukiwa mzuri lazima utavutia tu wanaume hata ujifunike kila mahali.

Mimi nadhani ubakaji ni tatizo kubwa zaidi ya uliyoandika hapo maana unaweza kuta mtu anamwanamke mzuri tu lakini kafumwa analawiti mtoto wa kindagaten. Au mzee wa miaka 78 amebaka mtoto wa miaka 7 .Au unakuta mtu kabaka mtoto wa miezi 2
 
Haha eti nakubwenga 😂

Dr. We ni mzanzibar au wa mtwara?

Ndani ya mada: Wanawake/wamama tunakosea katika malezi ya watoto wa kiume, Familia na jamii haijawahi kum-reward mtoto wa kiume kwa tabia njema, ila akifanya malice ndio utasikia huu ndio uanaume.

Sitegemei matokeo tofauti ya yale yote yaliyofanyika katika makuzi.

NB: katika kundi hili kuna watu wamejielea wenyewe, wamejilea mtaani.

Btw, kuitwa feminist katika dunia ya sasa ni kitu bora zaidi kuliko kuwa pickmisha (internalize misogynists)
Wanawake ndo mmekosa maadili ndo maana mnaishia kubakwa na kufanyia mambo ya ajabu.

Mwanamke anayejiheshimu hata wanaume huona haya kumwendea.. Ni nyie ndo mmekosa tabia nzuri, mnavaa nguo za uxhi mnategemea kuleta picha gani kwa jamii?
 
Haha eti nakubwenga 😂

Dr. We ni mzanzibar au wa mtwara?

Ndani ya mada: Wanawake/wamama tunakosea katika malezi ya watoto wa kiume, Familia na jamii haijawahi kum-reward mtoto wa kiume kwa tabia njema, ila akifanya malice ndio utasikia huu ndio uanaume.

Sitegemei matokeo tofauti ya yale yote yaliyofanyika katika makuzi.

NB: katika kundi hili kuna watu wamejielea wenyewe, wamejilea mtaani.

Btw, kuitwa feminist katika dunia ya sasa ni kitu bora zaidi kuliko kuwa pickmisha (internalize misogynists)

👏👏👏
 
Sasa jamani kwani mmezuiwa kutubaka?

Sisi tulishawapa ruksa kutubaka hata tukivaa kanzu haina shida kabisa tena mje wengi wengi.

Ni serikali tu ndo huwa ina kiherehere cha kuingilia mambo yasiyoihusu!
Unaona sasa, kwenye karne ya 21 tunaitafuta ya 22 bado unataka tuishi kama manyani, tubakane like seriously!!! yaani unatoka zako kwako ile unafunga mlango kundi la watu linakuja kukubaka, duh! Waafrika tunashida sana
 
Sikatai kuwa kuna wanaume wenye maadili 0, lakini hata sisi wanawake kuna muda tunavyojiweka ni chanzo kinachopelekea yote hayo.
Kama nini? kua mwanamke kamuita mwanaume njoo unibake?
Hivi nikuulize swali mbona jamii za wazungu wanavaa vichupi na vibikini ila hawabakani? ushajiuliza hilo swali?
Mimi nipo huku kanda ya ziwa ripoti za matukio ya ubakaji zinatishaa hawa wamama na vibinti wanavaa magauni na masketi marefu na bado wanabakwa,
Acha kuhalalisha ubakaji, haijalishi mwanamke kavaaje, kakaaje, mwili ni wake haimpi haki mtu mwingine kumuingilia bila ridhaa yake, ijue haki yako binti.
 
Back
Top Bottom