Dr. Mariposa
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 5,429
- 17,916
Ni ijumaa nyingine tulivu kabisa, nikiwa nafukiza udi nyumbani kwangu nikakumbuka kitu hiki, ukipishana na wanaume jamani ni aidha uzibe pua au ukubali kunukishwa harufu mbaya ya kwapa, inakuaje mwanaume umevaa vizuri tu ila unanuka kwapa na kuna vikata harufu vya kila aina kwa bajeti anayomudu mtanzania yoyote!!?
Juzi kati hapa nilikua sehemu nabarizi pembeni kulikua kuna wapendanao wanaogelea kwenye swimming pool, sijui ilikuaje yule mwanaume akanyanyua mikono juu yoh! nilihisi kutapika, makwapa yana manywele zimekua kama kapaka bleech yaani niliwaza sana yule mwanamke aliwezaje kukumbatiwa na mtu ana manywele yaliyochacha namna ile, nikawaza hiyo harufu ya kikwapa ikoje kwenye nguo zake na hata mwilini mwake, mmh wanawake wana huruma jamani ptuuuh!
Nimesikia kuna wengine wanavaa boxer mwezi mzima, seriously!!! unavaa nguo ya ndani mwezi mzima huo sio uchafu ni ukichaa kabisa hata humu mpoooo jirekebisheni, nyie ndio mnawapa wanawake zenu mafangasi ya uke,🤢
Hapo sijagusa wale mwenye uso mchafu pua imejaa vidude dude vyeupe, kidevuni ndio usiseme, hivi nyie wanawake mnawezaje kuwakiss watu wa hivyo mbona kinyaa jamani, scrub ya elfu 5 tu nayo mzozo!!
Ushauri wangu konky kwa wanawake kama mwanaume wako hajitunzi, hajipendi, ananuka makwapa, hataki kushave, tengenezeni kikundi chenu cha watu watano watano au kumi, mnakua mnasaidiana kukamkaba huyo mwanaume mchafu na kumfanyisha usafi kwa nguvu, eeh mbona mama zao walikua wanawakaba kunywa uji au wanawapiga bakora wakaoge, hebu anzeni hiyo kampeni mtokomeze harufu za vikwapa barabarani, mnatupa tabu sisi wengine yaani ukipishana na kundi la wanaume ni lazima uzibe pumzi ili tu ile harufu mbaya usiisikie,
Na nyie mnaoishi kwenye mikoa ya baridi habari zenu tunazo, mnakaa hata miezi mitatu hamuogi, mnanawa tu uso na kinywa, jamani uvundo lazima uwepo msijipe moyo ooh kuna baridi kwapa langu halitosikika harufu, tunasikia, wengine pua zetu nyembamba ndefu zinanusa hizo balaa,
Povu ruksaaaaaa😤😬